" Gratis lo recibisteis, dadlo gratis" (Mateo 10:8)

CASA  |  MAPA DEL SITIO  |  CONTACTO  |  AYUDA    
Estudios Bíblicos Libros Cristianos
Gratuitos
Libros-e Cristianos
Gratuitos
Acerca de Nosotros
 



 Versión Gratuita Libro-E de la edición en Swahili 3

 


Njia ya tahadhari kwako katika kumpokea Roho Mtakatifu

 

Dokezo

Kitabu kamili cha kufundishia juu ya kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu.

Maelezo ya Kina

Katika Ukristo nyakati hizi, mojawapo ya mambo yanayozungumziwa mara nyingi ni kuhusiana na habari za "wokovu toka dhambini" na "kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu". Hata hivyo ni watu wachache walio na ufahamu ulio sahihi wa mambo haya mawili, ingawa ukweli ni kwamba haya ni mabo mawili muhimu kuhusiana na maswala ya Ukristo. Mbaya ni nini, bado hatujaweza kupata maandiko yanayo tufunza kwa uwazi juu ya mambo haya yaliyo tajwa hapo juu. Wapo watunzi wa vitabu wa Kikristo walio wengi wakitukuza karama za Roho Mtakatifu au kuelezea maisha ya kujazwa na Roho. Lakini hakuna hata mmoja kati yao anaye thubutu kushughulika na swali la msingi,nalo ni "Kwa namna gani anaye amini ataweza kumpokea Roho Mtakatifu kwa uhakika?" Kwanini? Ukweli wa kushangaza ni kwamba hawajaweza kuandika kwa viwango vilivyo kamili kwa sababu hawakuweza kuwa na ufahamu ulio kamili juu ya hili. Kama vili Nabii Hosea alipo paza sauti na kusema "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa", kwa nyakati hizi si wakristo wachache wanao vutwa katika ushabiki wa kidini, wakitegemea kumpokea Roho Mtakatifu. Huamini kwamba wataweza kumpokea Kumpokea Roho Mtakatifu baada ya kufikia kiwango cha hisia kali na mashamusham. Lakini si swala la kutia chumnvi tukisema kwamba kinacho itwa imani na watu hawa ndicho kinacho fanya Ukristo udharaulike na hata kuonekana kama mojawapo tu ya dini mfano Shama (Shamanism), na ukereketwa wa aina hii unatoka na Shetani
Mtunzi, Mchungaji Paul C. Jong huthubutu siku zote kutangaza ukweli. Hujihusisha na maswala yaliyo muhimu kwa kiwango cha kutosha, ambacho wengi wa watunzi wa vitabu vya kiroho wamekwepa kwa muda mrefu. Kwanza amefafanua maana ya "kuzaliwa upya mara ya pili" na "kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu" na kuelezea uhusiano usio kwepeka kati ya mambo yaha mawili ya ngozo za msingi. Na ndipo basi akachukua maelezo ya kina kwa pamoja kuhusiana na Roho Mtakatifu, kuanzia "namna ya utambuzi war oho" kuelekea "namna ya kuishi maisha ya ujazo wa Roho". Kwa habari zaidi mwandishi anakushauri uchunguze yaliyomo katika kitabu hiki ambayo yamewekwa katika kurasa za tovuti hii.


Kutoka kwa Mchapishaji

Utakapo amua kusoma kitabu kimoja tu, ukiachilia Biblia pekee, kwa mwaka mmoja kama Mkristo, basi nakushauri usome kitabu hiki. Nauhakika kitabu hiki kipo katika nafasi ya juu zaidi ya kitabu chochote kwa msomaji wa vitabu vya Kikristo. Kinamaelezo yaliyo shwari na ya uwazi kuhusiana na kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu kulingana na namna ya kibiblia. Baada ya kuchapisha vitabu vingi kwa miaka kadha vya Mchunagaji Jong chini ya jina la "Mtiririko wa Vitabu vya Kikristo vya Paul C. Jong", Nimeweza kubarikiwa zaidi ya yeyote kwa sababu nimekuwa msomaji wa kwanza kabisa wa hivi vitabu vyake kabla ya yeyote. Vichwa vya habari vya mahubiri yake ni vya wazi, sahihi, vya kuvuna roho, na vilivyo jaa imani. Ni mtumishi wa Mungu anaye thubutu kutangaza ukweli dhidi ya manabii waongo walio enea katikati ya Ukristo wa nyakati hizi. Tunajivunia juu ya vichwa hivi vyake vya habari na tupo tayari kuchapisha vitabu vingine vijavyo.


 
Free Christian eBooks
    Lista de Libros-E
    Edición en Swahili 3
  Sobre este libro
  Tabla de contenidos
    ¿Qué es un Libro-E?
  Acerca del Libro-E
  ¿La manera de leer un Libro-E?
  Preguntas frecuentes
  Ayuda descarga
    Lectores de Libro-E
  MS Reader 2.0
  Acrobat Reader 5.0
 

Bookmark
   
Copyright © 2001 - 2013 The New Life Mission. ALL RIGHTS reserved.