" I har fået det for intet, giv det for intet " (Matt 10:8)

HJEM  |  OVERSIGT  |  KONTAKT  |  HJÆLP    
Bibelstudier Gratis Kristne Bøger Gratis Kristne e-Bøger Om Os
 Helt GRATIS Trykte Bøger
- Swahili udgave # 9

 


HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA: Taswira ya Wazi na ya Kina ya Yesu Kristo( I )

 

Dokezo

Taswira ya Wazi na ya Kina ya Yesu Kristo

Maelezo ya Kina

Je, tunawezaje kuupata ukweli uliofichika katika Hema Takatifu la Kukutania? Ni kwa kuifahamu injili ya Maji na ya Roho Mtakatifu tu, ambayo ni kiini cha kweli cha Hema Takatifu la Kukutania, ndipo tunapoweza kufahamu kwa usahihi jibu la swali hili.
Kwa kweli, rangi za bluu, Zambarau, na nyuzi nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa kama zilivyodhihirishwa katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania zinatuonyesha kazi za Yesu Kristo katika kipindi cha Agano Jipya ambazo zimemuokoa mwanadamu. Kwa njia hii, Neno la Agano la Kale la Hema Takatifu la Kukutania na Neno la Agano Jipya yanahusiana kwa karibu sana kama vile ilivyo kwa nyuzi za kitani safi ya kusokotwa. Lakini, kwa bahati mbaya ukweli huu umefichwa kwa muda mrefu kwa kila mtafuta ukweli katika Ukristo.
Alipokuja hapa duniani, Yesu Kristo alibatizwa na Yohana Mbatizaji na akamwaga damu yake katika Msalaba. Bila ya kuifahamu na kuiamini injili ya maji na Roho Mtakatifu, hakuna kati yetu anayeweza kamwe kupata ukweli uliofunuliwa katika Hema Takatifu la Kukutania. Hivyo ni lazima tujifunze na kuuamini ukweli huu wa Hema Takatifu la Kukutania. Sisi sote tunahitaji kutambua na kuamini juu ya ukweli uliodhihirishwa katika rangi za bluu, zambarau, na nyuzi nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa za lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania.


Kutoka kwa Mchapishaji

Wakristo wengi katika zama hizi hudai kuwa wamekutana na injili inayoweza kusafisha kabisa dhambi zao, wakati hawaujui ukweli wa nyuzi za bluu unaodhihirishwa katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania. Ni wazi kuwa wakristo wa jinsi hiyo ambao bado wana dhambi katika mioyo yao wanaamini katika Yesu kwa upofu bila kuufahamu ukweli uliofunuliwa katika rangi za bluu, zambarau, na nyuzi nyekundu zilizotumika katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania.
Kwa hiyo mwandishi anahitaji kuutangaza ukweli uliodhihirishwa katika rangi za bluu, zambarau, na nyuzi nyekundu na kitani safi ya kusokotwa iliyotumika katika lango hili. Ukweli huu wa bluu, zambarau, na nyuzi nyekundu zilizotumika katika Hema Takatifu la Kukutania ni kivuli cha injili ya maji na Roho iliyofunuliwa kwetu katika Agano Jipya, na ni udhihirisho halisi wa injili ya kweli.
Kupitia kitabu hiki, utaugundua ukweli unaofunuliwa katika rangi hizi za bluu, zambarau, na nyuzi nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, na kwa hiyo utaweza kuonana na Bwana kwa imani. Ninakusihi uamini katika injili kama inavyofunuliwa katika rangi za blue, zambarau, na nyuzi nyekundu zilizotumika katika Hema Takatifu la Kukutania ili uweze kuwa na imani itakayoweza kukuokoa kutokana na dhambi zako zote.


 

 
Free Christian Books
    Trykt Bogliste
    Swahili udgave 9
 
 • Om denne bog
 •  
 • Indholdsfortegnelse
 •     Om gratisbøger service
      Hvordan bestiller man gratis bøger
      FAQs
  Se
  Kurv
   

     
  Copyright © 2001 - 2019 New Life Mission. Alle rettigheder er forbeholdt.