Search

Predigten

Somo la 8: Roho Mtakatifu

[8-19] Injili njema Iliyo pasua pazia la Hekalu (Mathayo 27:45-54)

(Mathayo 27:45-54)
“Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa. Na kama saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, eloi eloi, lama sabakitani? Yaani Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Na baadhi yao waliohudhuria waliposikia walisema huyu anamwita Eliya. Mara mmoja wao akaenda mbio akatwaa sifongo akaijaza siki akaitia juu ya mwanzi akamnywesha. Wale wengine wakasema, acha natuone kama Eliya atakuja kumwokoa. Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu akaitoa roho yake. Na tazama pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini, nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka makaburi yakafunuka ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala. Nao wakiisha kutoka makabuirini mwao baada ya kufufuka kwake waka ingia mji mtakatifu na kuwatokea wengi. Basi yule akida na hao walio kuwa nao pamoja naye wakimlinda Yesu walipoliona tetemeko la nchi na mambo yaliyofanyika wakaogopa sana wakisema, Hakika huyu alikuwa mwana wa Mungu.”
 

Kwa nini pazia la Hekalu la 
Mungu lilipasuka wakati Yesu alipotoa 
Roho yake pale msalabani?
Kwa sababu ufalme wa Mungu ulikuja kufunguliwa 
kwa wale wote wenye kuamini ubatizo 
wake na kusulubiwa kwake.

Ili kuelewa ukweli wa injili hii njema, imempasa mtu kwanza kujua na kuelewa juu ya mpangilio wa utoaji dhabihu ulivyokuwa ukifanywa katika kusamehe watu dhambi zao mbele ya Mungu nyakati zile za Agano la Kale. Yatupasa kujua na kuamini ukweli ufuatao.
Kulingana na dhabihu, upatanisho katika nyakati za mwanzo kama ilivyo andikwa katika Walawi sura ya 16 katika Agano la Kale, kuhani mkuu aliweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi aliye hai na kumtwika dhambi zote za watu kwa jumla katika mwaka mzima. Ndipo kwa niaba ya Waisraeli, mbuzi huyo ilichinjwa shingo, na kuhani mkuu alichukua kiasi cha damu yake na kunyunyizia juu ya kiti cha rehema. Huu ulikuwa ndiyo upatenisho kwa dhambi zao watu wote wa Israeli. Kwa jinsi hiyo pia wale tu wanao amini tendo la kuwekea mikono, damu na maneno ya Mungu ndiyo watakao weza kuingia Madhabahu Takatifu.
Makuhani kwa wakati wote huenda ndani katika sehemu ya kwanza ya chumba cha hema kwa ajili ya kuhudumu. Lakini kwa ile sehemu ya pili ya chumba, patakatifu pa patakatifu, ni mahali ambapo kuhani mkuu pekee ndiye aliye ruhusiwa kuingia mara moja kwa mwaka, akiwa na damu ambayo aliitoa kwa ajili yake na kwa ajili ya dhambi za watu wote walizotenda kwa kutojua (Waebrania 9:6-7). Kwa jinsi hiyo pia hata kuhani mkuuu asingeweza kuingia mahali patakatifu pa patakatifu pasipo damu ya sadaka iliyo tayarishwa kwa njia ya kuwekewa mikono kwa imani.
 

Kama ilivyo semwa katika Agano Jipya, Yesu Kristo alikuwa ni sadaka yetu.

Katika Agano Jipya tumeambiwa kwamba mtu aliweza kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa njia ya imani katika ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Ni wakati gani pazia la hekalu la Mungu lilipo pasuka vipande viwili toka juu hadi chini? Ilikuwa ni wakati Yesu alipo sulubiwa baada ya kuja ulimwenguni nakubatizwa na Yohana.
Sababu gani kulipelekea kwa hili kutokea? Yesu alikuja ulimwenguni akiwa ni sadaka iliyojulikana kama mwanakondoo wa Mungu aliye beba dhambi zote za wanadamu aliposulubiwa. Kuchanika kwa pazia la hekalu ni alama ambayo dhambi zote a wanadamu zilizokuwa zikiwatenga na Mungu zilifutwa kwa njia ya ubatizo wake na damu ya msalaba.
Binafsi Yesu alivunja kizuizi kwa kulipa mshahara wa dhambi ambao ni mauti. Yesu alibatizwa na kusulubiwa ili kuondolea mbali dhambi za ulimwengu. Hii ndiyo sababu ya kupasuka kwa pazia la hekalu la Mungu na kuwa vipande viwili. Kama ilivyo kwa makuhani walipoweza kuingia hemani wakiwa na imani ya kuwekea mikono, leo hii nasi tunaweza kuingaia Ufalme wa Mbinguni kwa shukrani ya imani ya ubatizo wa Yesu na damu yake.
Wakati Yesu aliposulubiwa alipaza sauti kubwa akisema, “Eloi, Eloi, Lama sabakitani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?” (Mathayo 27:46). Mwishoni alipotoa roho yake alisema “Imekwisha” (Yohana 19:30). Yesu aliachwa na Baba yake pale msalabani kwa muda kwa sababu ya dhambi za ulimwengu alizobeba kwanjia ya ubatizo wake kwa Yohana katika mto Yordani.
Alikufa kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Matokeo ya ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani yamewezesha wale wote walio na imani kwake waokolewa. Kwa kuwa tumezaliwa tukiwa wenye dhambi na hatima yetu ni hukumu, Yesu alibatizwa ili kubeba dhambi zetu.
Mlango wa Ufalme wa Mbinguni ulikuwa umefungwa kabisa hadi pale Yesu alipofuta dhambi zetu zote. Yesu alipobatizwa na Yohana na kufa msalabani pazia la hekalu la Mungu lilipasuka vipande viwili kutoka juu hadi chini ili kila atakaye amini injili njema aweze kuingia hekalu la Mungu.
Ninashukrani kwa Bwana kwasababu nina imani katika injili ya maji na Roho. Sasa nitaweza kuingia Ufalme wa Mbinguni kwa njia ya kuamini injili njema ambayo Yesu aliikamilisha kwa njia ya ubatizo na damu. Nisingeweza kufanikiwa katika wokovu kwa uwezo wangu binafsi, mafanikio na juhudi zangu. 
Baraka inayo tuwezesha kuingia Ufalme wa Mbinguni haipatikani kwa njia ya maombi, mchango, au kujitolea. Mtu ataweza kuokolewa toka dhambini ikiwa tu ataamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Mtu ataweza kuingia Ufalme wa Mbinguni kwa kuwa na imani katika injili njema tu. Hakuna imani nyingine iliyo muhimu kwa wale wanao mwamini Yesu. Kiingilio cha mbinguni hakitolewi kwa mchango wa kujitolea, juhudi za kidunia au matendo mema. Jambo la kweli ambalo ni muhimu kwa anaye tazamia kuingia mbinguni ni imani ya injili ya ubatizo wa Yesu pale Yordani na damu yake msalabani.
Kwakuamini maji (ubatizo wa Yesu katika mto Yordani) na damu yake (msalabani) kutakuwezesha kuingia katika Ufalme wa Mbinguni. Mwenye dhambi moyoni huku akimwamini Yesu, anahitaji kuamini jambo moja; injili ya maji na Roho. “Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32).
Kamwe hatujui muda sahihi wa vifo vyetu laki Yesu hujua yote. Kwakuwa yeye anajua asili yetu ya dhambi vyema, alitakasa dhambi zetu kwa njia ya ubatizo na damu ya msalaba kwa takribani miaka elfu mbili iliyo pita.
 

Yatubidi kuiamini Injili njema ambayo ilipasua pazia la Hekalu la Mungu.

Mwokozi alizaliwa na mwanamwali bikira ili kuokoa wanadamu kwa dhambi zao. Ilikuwa ni kwanjia ya ubatizo akiwa na umri wa miaka 30 pale Yordani, ndipo Yesu alibeba dhambi zetu zote ulimwenguni. Dhambi zote za ulimwenguni zilizosababisha udhaifu na makosa zilisamehewa kwa wema wa Yesu. Ubatizo na damu ni ufunguo wa milele kwa wokovu wa wanadamu wote. Yesu alibatizwa na kumwaga damu yake msalabani na sasa wale wote walio na imani katika injili hii wataweza kuingia Ufalme wa Mbinguni.
Pazia la Hekalu la Mungu lilipasuka pale Yesu alipo ikabidhi roho yake msalabani. Ni kwasababu gani pazia la Hekalu la Mungu lilipasuka vipabde viwili pale alipo kufa msalabani? Ni kwasababu wokovu wa wanadamu ulipatikana kwa kupitia injili njema.
Katika Agano la Kale tunajifunza juu ya hema ya kukutania ya Israeli. Hapa ndimo ilimo kuwemo madhabau ya sadaka ya kuteketezwa kwa moto na bakuli la shaba. Ukipita bakuli hili kwa mbele utakuta hema nyingine na ndani yake baada ya pazia ya hema hii palikuwemo sanduku, hapo ndipo uwepo na Utukufu wa Mungu ulikuwemo. Pazia hilo lilifumwa kwa umadhubuti wa nyuzi kiasi kwamba farasi wanne wakifungwa pande zake nne na kuvuta kila mmoja upande wake wasingeweza kulichana nyuzi zake. Ingawa Mfalme Suleimani alibadilisha hema hiyo kwa kujenga hekalu, lakini mambo ya msingi hakuyabadilisha na pazia liliendelea kuwepo huku likikinga sehemu kuelekea Patakatifu pa patakatifu. Hata hivyo siku hiyo lilichanika vipande viwili toka juu hadi chini pale Yesu alipo kata roho huku akimwaga damu msalabani. Hii ina shuhudia namna gani ilivyo ukweli wa injili njema na hakika iliyo kamilishwa kwa ubatizo wa Yesu na damu yake.
Mungu aliwabariki wanadamu wote kwa msamaha wa dhambi na uzima wa milele, huku akiwatunukiwa injili njema. Yesu akiwa ni dhabihu, alilipa mshahara wa dhambi pale alipo batizwa na Yohana na kufa msalabani. Biblia inasema “mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23). Kama ilivyo wakati wa Agano la Kale mtu angeliruhusiwa kuingia hekaluni pa Mungu akiwa na damu ya dhabihu na kupokea upatanisho kwa dhambi zake, hivyo ndivyo hata leo hii tunaweza kuja mbele ya Mungu tukiwa na dhabihu ambayo ni Yesu, hivyo kuweza kusamehewa makosa yetu. Huu ni ukweli. Na maneno “mshahara wa dhambi ni mauti” yanatuonyesha jinsi ile injili njema ilivyo sahihi.
Njia ya kwenda mbinguni ni kuamini injili njema. Kuchanika kwa pazia la hekalu vipande viwili kunaashiria kufunguliwa kwa Ufalme wa Mungu. Tunapokuja kufahamu na kuamini injili hii kwa kusema, “Oh, Yesu alizichukua dhambi zanguzote. Oh, Yesu alilipa mshahara wote wa dhambi pale msalabani!”, basi hapa ndipo mlango wa Mbinguni utakapo funguliwa kwa ajili yetu. Mbingu sasa ipo wazi kwa wale wote walio kwisha kupokea ukombozi kwa njia ya imani ya ubatizo wa Yesu na damu yake. Damu ya Yesu iliokoa wenye dhambi toka mautini na ubatizo wake ulikuwa ni namna ya kubeba dhambi za wanadamu wote.
Dunia ilitetemeka na miamba kupasuka pale roho ya Bwana ilipowekwa mikononi mwa Mungu akiwa msalabani. Hapo ndipo damu yake ilipo mwagika duniani na kuanza kutiririka kuelekea uwanda wa chini. Pale Yesu alipokufa msalabani, dhambi zote za wanadamu zilifutwa na kufanya injili njema kukamilishwa hivyo kuwezesha wote wale wenye kuamini, kuhesabiwa haki kwa sheria hii ya kuingia Ufalme wa Mbinguni. Huu ndiyo ukweli halisi katika kuzaliwa upya mara ya pili.
Wapo wakufunzi wengi ambao wamefanya uchunguzi wakitafuta kupinga juu ya Yesu Kristo kuwa mwanadamu kamili. Lakini hawakuweza kudumu katika ulaghai dhidi ya vithibitisho mbalimbali vya kuwepo kwa Yesu. Kati yao wengi walishidwa na hivyo kuacha kupinga kwa kuamini injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake. Walikuja kugundua kwamaba, uthibitisho wa Yesu ulikuwa ni dhahiri kiasi cha kushindikana kubisha uwepo wake. Walimkubali Yesu kuwa Mwokozi wao pale walipo jua na kuamini injili njema inayoeleweka kwa tendo la kuzaliwa kwake, ubatizo wake, kifo chake na ufufuo wake, kupaa na kuja kwake mara ya pili.
Hatukushuhudia ubatizo wa Yesu kwa macho yetu. Hatukuona kile kilicho tokea takribani miaka 2,000 iliyo pita. Hata hivyo, kwa njia ya kile kilicho andikwa, yeyote aweza kukutana na injili njema. Yesu alivunjilia mbali kikwazo cha dhambi kati ya Mungu na wanadamu kwa njia ya ubatizo na damu yake na hivyo pazia la Ufalme wa Mungu lilipasuka vipande viwili toka juu hadi chini.
Sasa basi, yeyote anaye amini injili njema, ambayo ilikamilishwa na ubatizo wa Yesu na damu yake ataweza kuingia katika Ufalme wa Mbinguni. Je, unayo imani ambayo ubatizo wa Yesu na damu yake ndiyo injili njema, ufunguo wa kuingia Ufalme wa Mbinguni?
Hata mimi hapo awali nilikuwa ni mwenye dhambi ambaye nilimtumaini Yesu kuwa Mwokozi lakini sikuwa najua juu ya injili njema. Hata hivyo siku moja nilikuja kusoma juu ya upendo wake usio na masharti kwangu katika Biblia. Nilikuja kuelewa kwamba alibatizwa kwa ajili yangu, alikufa msalabani kwa ajili yangu na kufufuka kwa ajili yangu pia. Yesu alituokoa kwa kubatizwa kwake mto Yordani na kusulubiwa ili kulipa mshahara wa dhambi kwasababu ya upendo wake kwetu. Tunaweza kuingia katika ufalme wa Mbinguni kwa kuamini injili hii njema.
Hii ndiyo haki ya Mungu kwa wanadamu na ni tukio la ukurasa mpya wa historia. Huduma yake yote – kuzaliwa kwake, ubatizo wake katika mto Yordani, kifo chake msalabani na ufufuko wake – vyoye hivi ni katika kutuokoa sisi sote na dhambi zetu. Hatima yetu ilikuwa ni motoni baada ya kifo, lakini Yesu alituokoa na moto wa milele na kutupatia injili njema ikiwa ndiyo njia ya kuingia Ufalme wa Mbinguni.
Ndugu wapendwa, wakati Yesu alipokufa msalabani, askari mmoja alimchoma ubavu kwa mkuki na mara damu na maji vikamiminika. Hivi ndivyo ilivyo andikwa katika biblia. Hii inakushuhudia juu ya ukweli wa injili njema ya ubatizo wa Yesu na damu yake. 
Je, umekua ukichukulia kwa uzito wa juu imani yako katika damu ya Yesu msalabani ndiyo inayo tosha kukuweka huru na dhambi zako zote? Je, ubatizo wa Yesu hauna umuhimu sana kwako au ni moja kati ya matukio katika wokovu wako? Ikiwa unaamini hivyo nakusihi utubu katika hilo. Imetupasa sasa tuamini injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake kwa kukubali kuwa huo ndio ukweli wa Mungu.
 

Je ungependa kutakaswa dhambi zako zote? 
 
Kama ilivyo jinsi ile itupasavyo kulipa deni ili tusiwe wadaiwa, pia imetupasa tuwe na imani katika injili njema ya ubatizo wa Yesu na damu yake ili tuweze kutakaswa kwa dhambi zetu zote. Tusitende dhambi tena ya kutoamini injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake. Ingawa sisi binafsi hatukumtwika Yesu dhambi zetu, lakini mwakilishi aitwaye Yohana Mbatizaji alitekeleza jukumu hili kwa niaba yetu sote.
Wakati Yesu alipokufa msalabani, baadhi ya makaburi ya watakatifu katika Yerusalemu yalifunuka na siku tatu baadaye alifufuka na kwenda Galilaya. Tukio hili la ajabu hakika kweli lilitokea, lakini watu wengi bado hawakuamini.
Bwana wetu ametutunuku Ufalme wa Mbinguni, sisi wenye haki ambao tulio kwisha pokea ondoleo la dhambi. Tuliokolewa na kuzaliwa upya mara ya pili, si kwa nguvu ya miili yetu au juhudi za kidini, bali kwa njia ya imani katika injili njema. Injili hii si hadithi ya kufikirika. Dhambi zote za ulimwengu zilitwikwa juu yake Yesu pale alipobatizwa. Yeye binafsi hakuwa na dhambi, lakini ilimpasa afe msalabani ili kutupatinisha kwa dhambi zile alizo beba katika ubatizo wake.
Wakati Yesu alipotoa roho yake, dunia ilitetemeka na miamba kupasuka. Wakati huo, Akida na wale waliokuwa naye ambao walikuwa wakiuchunga mwili wa Yesu, walisikia tetemeko na matukio mengine hivyo walihofu sana hata kukiri kwamba, “Hakika huyu alikuwa ni Mwana wa Mungu” (Mathayo 27:54).
Yusufu aliyekuwa mtu tajiri toka Armathea aliuchukua mwili wa Yesu, akaufunga kwa kitambaa safi cha kufumwa na kumlaza katika kaburi alilolimiliki yeye. Kuhani Mkuu na Mafarisayo walitoa amri kulinda kaburi hilo hadi siku ya tatu.
Hata hivyo, Yesu alifufuka kuleta uzima mpya kwa wale wote wenye kuamini injili njema. Alikwenda Galilaya alikoahidi kukutana na wafuasi wake hapo kabla ya kusulubiwa. Mambo yote haya – kuzaliwa kwake, ubatizo, kusulubiwa kufufuka, kupaa na kuja kwake mara ya pili – yalilengwa kwa wale wote wenye kuaimini injili njema. Nami pia nimekua mshuhudiaji ya kwamba Yesu ni mwana wa Mungu na Mwokozi.
 

Ni kwawatu gani injili ya kweli ilihubiriwa?

Wenye kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake hushuhudia injili njema ya kweli. Injili njema inasambaa kwa kupitia ushuhuda wa watu hawa walio okolewa toka dhambini mwao. Mtu anapo wekwa huru tokana na dhambi zake kwa kuamini injili njema, Roho wa Mungu huanza kumjenga hatua kwa hatua na kumpa hata imani madhubuti. Hatimaye mtu huyo hugeuka na kumsifu Bwana. Neno la Mungu hukaa ndani yake na hatimaye hukumbana na kuhuishwa kwa utu wake wa ndani siku hadi siku. Kwa kuona yote haya, ndipo watu hushuhudia wakisema, “Hakika mtu huyu amekombolewa. Amekuwa mkristo wa kweli na mwana wa Mungu”.
Hata shetani mwenyewe hukubali na kusalimu amri kwa injili hii njema akisema, “nimefedheheshwa! Lakini ni kweli kwamba hakuna tena dhambi duniani. Hakuna mwenye dhambi moyoni”. Hivyo shetani kutenda kazi katika fikra za watu wa Mungu, akiingilia maisha yao ya uaminifu. Kazi za shetani ni kuwazuia wasiweze kupokea baraka za kiroho toka injili.
Shetani alikwisha shindwa vita na Yesu kwa hakika. Alifanikiwa kumsulubisha Yesu kwa kuyateka mawazo ya watu na kuyaongoza. Hata hivyo Yesu tayari alikwisha zichukua dhambi za ulimwengu pale alipobatizwa na kufa msalabani na hivyo kulipia mshahara wa dhambi hizo. Kwa sababu hiyo basi, alikamilisha wokovu kwa wote wanao amini injili njema. 
Hivyo sasa hakuna tena dhambi duniani. Yesu alizichukua dhambi zote kwa njia ya ubatizo na kuweka hitimisho kwa dhambi zote kwa njia ya ubatizo na kifo chake msalabani akisema, “imekwisha!” (Yohana 19:30). Shetani alidhohofishwa nguvu ya kuwashitaki wale wote walio na imani katika injili njema. Yesu alimshinda shetani kwa njia ya kuzaliwa kwake, ubatizo wake, kusulubiwa kwake na kufufuka.
Je, bado wewe unadhambi moyoni? Hapana. Wakristo wataweza kuwa na ushupavu huku wakisema, “sina tena dhambi moyoni” kwa msingi wa imani zao katika injili ya kweli. Mtu anaye amini injili njema ya ubatizo wa Yesu na damu yake hakika hana tena dhambi moyoni.
Sasa basi injili njema imekwisha andikwa mioyoni mwetu. Leo hii tunasimama huru kinyume na dhamira mbaya mbele ya Mungu. Je, ninyi nyote mnamwamnini Yesu kuwa ndiye aliye zichukua dhambi zenu kwa ubatizo wake pale mto Yordani? Ikiwa ndivyo basi shukrani zako kwa Mungu na furaha yako vyote vitakamilika. Kuwa na imani katika injili njema ndiko kutakako tutakasa na kutuweka huru toka dhambi za ulimwengu. Tunamshukuru Mungu.
“Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake ambaye katika yeye tunaukombozi yaani msamaha wa dhambi” (Wakolosai 1:13-14). Haleluya Bwana Asifiwe!
Yesu alifungua lango la wokovu kwa njia ya injili njema. Wewe nawe pia yakupasa uondoe kizuizi cha moyo wako mara moja kwa nguvu ya injili njema, kama ilivyo kuwa kwa pazia la Hekalu la Mungu kupasuka vipande viwili ndivyo injili njema ifanyavyo kwa ajili yako na yangu. Tuataweza kuingia katika ufalme wa Mbinguni kwa kuamini injili hii na ndiyo ukweli pekee ambao utakao tuwezesha kufanikisha uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yetu.