Aufgrund von COVID-19 und der Unterbrechung des internationalen
Postdienstes haben wir unseren "kostenlosen Druckbuch-Service" vorübergehend eingestellt.
Angesichts dieser Situation können wir Ihnen die Bücher derzeit nicht zusenden.
Beten Sie, dass diese Pandemie bald endet und der Postdienst wieder aufgenommen wird.
Mungu ni wa mipango, ndiye Mungu wa kweli na hakika ndiye aliye hai. Hivyo, aliweka sheria ulimwenguni kwa sababu zifuatazo: ① Aliwapa wenye dhambi Sheria na Amri ili waokolewe kwa dhambi zao “kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria” (Warumi 3:20). ② Sheria ya pili ni Sheria ya Imani iokoayo wenye dhambi. “Sheria ya Roho wa uzima” (Warumi 8:2) inayotoa njia ya wokovu kupitia imani katika Yesu Kristo mwokozi wetu (Warumi 5:1-2). Yesu alishuka ulimwenguni kuitimiza hii sheria. Alibatizwa akatoa damu yake Msalabani na akafufuka. Yesu aliweka sheria ya wokovu ili kuokoa wale wote wenye dhambi ulimwenguni. Mungu aliweka Sheria ya Imani kwa wale tu wenye kuamini wokovu utokanao kwa maji na Roho. Yeyote atakaye okolewa na kuwa mwana wa Mungu yampasa kwanza kuamini Sheria hii ya Imani ambayo Mungu ameitoa. Ndiyo pekee njia ya kuokoka. Kwa haya, ameruhusu njia ya kwenda mbinguni kwa wale wenye kuamini kuzaliwa kiroho katika kweli tokana na sheria hii.