Search

ΣΥΧΝΕΣ ΕΡΩΤΗΣΕΙΣ για την Χριστιανική Πίστη

Θέμα 1: Αναγέννηση εξ ύδατος και Πνεύματος

1-26. Je unaweza kunipa maelezo juu ya Injili ya maji na Roho?

Ikiwa tumepoteza sindano mahala Fulani nje tungetafuta mahala pale ilipopotelea bila shaka. Kwa jinsi hii, haitoleta maana hata kidogo ikiwa tutajaribu kuitafutia ndani ya nyumba si kwa sababu nje ni penye mwanga zaidi. Nimekutana na watu wasio na maana kwa namna hii nyakati hizi Makanisani. Wanapo jihusisha na mambo ya utata katika biblia juu ubatizo wa waumini, hawajiulizi wenyewe nafsini umuhimu wa swali “sababu gani Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji?” Kutokana na tabia za aina hii, kumekuwepo na madhehebu na vitengo vingi leo hii katikati ya jamii ya Wakristo wa leo.
Ili kuweka mwisho wa utata huo uendeleao siku hadi siku, yatupasa kujitoa katika kijiji hiki chenye ghasia na kurudi nyuma pale tulipo potezea sindano yetu. Ikiwa tutakuwa waaminifu kutafuta kweli yatupasa kuachana kabisa mawazo potofu juu ya kile tushindwacho kukipata katika kijiji cha udini. Kwa nini Mitume waliweka mkazo juu ya ubatizo wa Yesu Kristo? Siri ya ukweli wa Injili ya maji na Roho waliyo ipokea toka kwa Yesu ilihubiriwa ulimwenguni pote kwa uwazi.
Yesu alisema “Amin, amin nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu” (Yohana 3:5). Biblia yatuambia kwamba Yesu alikuja kwa maji na damu ili atuokoe toka dhambini mwetu (1 Yohana 5:6). Maana ya damu ni kifo chake msalabani. Hivyo una maana gani juu ya “maji”? Kwa nini Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu? Kwa nini alitangaza “kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote” (Mathayo 3:15) punde kabla ya kubatizwa?
Tumaini langu nafikiri unaelewa na kuamini juu ya Injili ya maji na Roho, hasa katika ubatizo wa Yesu. Huo hapo juu ni muhtasari wa maelezo juu ya Injili ya maji na Roho ambao Yesu aliwapa wafuasi wake. Mitume walitilia mkazo mkubwa juu ya ubatizo wa Yesu pindi walipohubiri Injili. Mtume Paulo alisema “Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kama yanenavyo maandiko na ya kuwa alizikwa; na yakuwa alifufuka siku ya tatu kama yanenavyo maandiko” (1 Wakorintho 15:3-4).
Nini maana ya “Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko” Maana yake ni kwamba, kifo cha Yesu kimetupatanisha kwa dhambi zetu zote kulingana na mpango uliowekwa na Mungu katika Agano la Kale. Alikufa kwa ajili yetu kulingana na ufunuo na agano katika Agano la Kale. Waebrania 10:1 inasema, “Basi torati, kwakuwa ni kivuli cha mema yatakayo kuja” Hebu tuone namna ile halisi ya utoaji wa sadaka katika Walawi 1:3-5. Mwenye dhambi ilimpasa kutimiza mambo matatu kama sharti la sadaka ya kuteketezwa kwa upatanisho wa dhambi zake.
1) Kumleta mnyama wa sadaka asiye na doa (Walawi 1:3).
2) Ilimpasa kumwekea mikono juu ya kichwa chake yule mnyama wa sadaka (Walawi 1:4). Hapa, yatupasa kuweka wazi sheria ya Mungu; kuwekea mikono juu ya kichwa cha sadaka ilikuwa ni sheria ya Mungu kuwezesha kutwika dhambi juu yake.
3) Ilimpasa kumchinja kwa upatanisho wa dhambi (Walawi 1:5).
Katika siku ya upatanisho, Haruni aliweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha mbuzi aliye hai, kutubu juu yake udhalimu na makosa ya wana wa Israeli, juu ya dhambi zao zote na kumwekea juu yake, kichwani, mbuzi huyo (Walawi 16:21). Katika muda huo, Haruni alikuwa ni mwakilishi wa Israeli. Binafsi aliweka mikono yake juu ya mbuzi, lakini madhambi yote ya mwaka ya watu wa Israeli (kati ya milioni 2-3) yalitwikwa juu yake. Matoleo ya sadaka katika Agano la Kale ni kivuli cha mambo mema yajayo. Yesu alikijitoa nafsi yake kwa mapenzi ya Mungu ili atutakase kulingana na maandiko.
Kwanza ya yote, alikuja katika mwili wa mwanadamu na kuwa mwana kondoo asiye na doa yeye pia ni mwana wa pekee wa Mungu asiye na doa ”ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake” (Waebrania 1:3). Kwa yote haya imempasa kuwa sadaka ya dhambi kwa wanadamu.
Pili, Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu katika Yordani. Ubatizo uliotolewa kwa namna ya “kuwekea mikono” na Yohana Mbatizaji ni mzao wa Haruni na mwakilishi wa wanadamu wakati Yohana alipoweka mikono yake juu ya kichwa, cha Yesu Kristo, dhambi zote za dunia zilibebeshwa juu ya Yesu kulingana na sheria ya Mungu aliyoweka. Yesu alimwambia Yohana kabla “kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote,” na akambatiza Dhambi zetu zote mwishowe alibeba yeye. Siku iliyofuatia, Yohana akasema “Tazama! Mwana Kondoo wa Mungu azibebaye dhambi za ulimwengu“ (Yohana 1:29).
Tatu, Yesu alipokaribia kufa pale msalabani kwa ondoleo la dhambi zetu zote alisema “Imekwisha” (Yohana 19:30). Alifufuka tena toka kifoni ili kutufanya kuwa wenye haki mbele ya Mungu kumbuka kwamba sadaka ya dhambi ilitolewa kwa ajili ya msamaha wa dhambi. Mwenye dhambi ilipasa kuweka mikono juu ya sadaka yake kabla ya kuchinjwa. Kama angesahau hatua mojawapo, kwa maneno mengine, ikiwa ataondoa kuweka mikono juu ya kichwa cha mnyama wa sadaka asingeweza kukombolewa takana na kutenda kinyume cha sheria. Ikiwa Mkristo hana ufahamu nini maana ya ubatizo, mtu huyo lazima ataendelea kuwa na dhambi moyoni mwake na hatoweza kuokolewa kwa sababu tu ya imani yake.
Wakristo wengi hujua nusu ya haki ya Yesu tu! Mtume Yohana ameweka wazi katika waraka wake “Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo si katika maji tu bali katika maji na katika damu, naye Roho ndiye ashuhudiaye kwa sababu Roho ndiye kweli” (1 Yohana 5:6) vipo vifungu vingi ndani ya Biblia vinavyo unga mkono juu ya umuhimu wa ubatizo wa Yesu kati ka kukamilisha haki zote za wokovu wetu. Wakristo wote yatupasa kurudi katika Injili ya maji na Roho.