Search

FAQ on the Christian Faith

Subject 1: Being born again of water and the Spirit

1-7. Warumi 8:30 inasema “Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; hao akawatukuza.” Je, maandiko haya yanaunga mkono juu ya mafundisho ya utakaso wa hatua kwa hatua?

Kifungu cha maandiko haya, hakifundishi juu ya utakaso tunaoweza kuupata hatua kwa hatua. Wana theologia wengi na wale wahubiri walio waongo hufikiri hivyo kwa kufundisha “Wale wenye kuamini katika Kristo Yesu watabadilika hatua kwa hatua na kuweza kutakaswa kabisa katika mwili na Roho,” na wengi huamini hivyo!
Lakini kwa jambo la kweli Wakristo ambao bado hawajazaliwa upya hujikuta wakiwa wagumu siku hadi siku katika imani na kuelewa kwao. Dhambi iliyo mioyoni mwao hukua kadiri wanavyo kuwa. Itawezekanaje utakaso wetu kwenda na muda? Neno “Utakaso wa hatua kwa hatua” ndiyo maneno ambayo hakika Mungu huyachukia sana, na ndiyo shetani huyapenda na kuyatumia katika kuwapotosha watu wa Mungu.
Tutaweza tu kuwa wenye haki pale tunaposhindwa kwa dhambi zetu wenyewe. Kwa sababu Yesu alitakasa dhambi zetu zote kwa ubatizo na kujitoa kwake sadaka ili kulipia gharama zake yeye mwenyewe, tunadai haki yetu kupitia ubatizo na damu ya Yesu. Tunakuwa wenye haki kupitia imani kwamba Yesu alibeba dhambi zetu kwake yeye binafsi.
Neno “utakaso” maana yake “kuwa mtakatifu” Kwa kujaribu kutakaswa kwa juhudi zetu hii si kuamini katika kweli bali ni kuhamasishwa na miili yetu iliyo dhaifu.
Tumaini la hatua kwa hatua katika utakaso pia huja tokana na matamanio yetu ya koroho. Kila dini inalo neno lake la utakaso, lakini sisi sote tuaminiio katika Yesu hatupaswi kubadilisha umuhimu wa neno hili lenyewe.
Hatuwezi kutakaswa hatua kwa hatua kwa kuamini katika Yesu; tunakuwa wenye haki mara moja na kwa wakati wote kwa kuamini katika ubatizo na damu ya Yesu, Injili ya kutahiriwa kiroho. Wenye haki wa kweli ni wale tu walio zaliwa upya kwa imani ya Injili ya ubatizo na damu ya Yesu.