Search

FAQ on the Christian Faith

Subject 1: Being born again of water and the Spirit

1-31. Kwa kuwa Mungu ni wa rehema na mwenye huruma je! asingeweza kutuchukulia kuwa wenye haki, ingawa tumetenda dhambi mioyoyoni mwetu ikiwa tumeamini katika Yesu tu?

Mungu ni Upendo na pia ni wa haki kwa hinyo, hutoa hukumu ya dhambi kwa haki hata iwe vipi. “Mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23) maana yake wenye dhambi mwisho wao ni motoni baada ya hukumu. Hutenga wenye haki toka kwa wenye dhambi kama alivyofanya mwanga toka kwenye giza. Mungu huwaita wale wasio na dhambi walio mwaamini Yesu kwa kutakaswa dhambi zao zote kupitia ubatizo wa Yesu na kusulubiwa kweke kuwa ndiyo wenye haki.
Kwa hivyo wale wote ambao bado wana dhambi ndani yao kwa kutoamini batizo wa Yesu, ni wenye dhambi mbele ya Mungu. Ndio wasio na imani katika maji kwa maneno mengine, ubatizo wa Yesu kama wakati ule wa watu wa Nuhu. Ikiwa Mungu atawachukulia wale wenye dhambi ambao bado dhambi umo ndani yao kuwa wenye haki na watakatifu, basi ni lazima kwake atakuwa ni mwongo na hivyo hatoweza kutoa hukumu ya haki au kutawala viumbe wake.
Mungu amesema “sinto wapa haki waovu” (Kutoka 23:7) waovu ni wale wafuatao na kutegemea zaidi taratibu za kibinadamu na kuacha injil ya maji na Roho ambayo Mungu alileta ukombozi wetu katika dhambi zetu zote katika haki na usawa kwa njia iliyo sahihi. Yesu alisema “kwa habari ya dhambi kwa sababu hawaniamini mimi” (Yohana 16:9). Dhambi iliyobaki duniani pekee sasa nikutoamini ukweli kwamba Yesu alizibeba dhambi zetu zote kwa ubatizo na msalaba na kuwa Mwokozi wetu.     Hii ni dhambi ya kufuru dhidi ya Roho Mtakatifu ambayo haitoweza samehewa. Hakuna njia nyingine tena kwa wale waliokufuru dhidi ya Roho Mtakatifu kuweza kuokolewa kwa sababu hawaamini kuwa Yesu alitaka dhambi zao zote.
Mtume yohana alisema “Kila atendaye dhambi afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. Nanyi mnajua ya kuwa alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi na dhmbi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila aatendaye dhambi hakumwona yeye wala hakumtambua” (1 Yohana 3:4-6). Ni kutenda uasi kwa kutoamini ukweli kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu zote kwa ubatizo na msalaba. Yeye atawakana wale wote waliotenda dhambi hii katika siku ya mwisho.
Wale wote wenye kumwamini hawana dhambi na wanaungana na Yesu kwa ubatizo wake. Wale ambao walio mwachia dhambi zao zote katika maisha yao juu yake kwa imani katika ubatizo hawana tena dhambi ingawa bado watendelea kutenda dhambi kutokana na udhaifu wa miili yao.
Mungu huwaita wale waliziweka dhambi zao juu ya Yesu na kutakaswa kwa sheria ya Roho ya Uzima kwa kuwa ndiyo wenye haki. Amewapa Roho Mtakatifu kama kipawa. Roho Mtakatifu kamwe haji juu ya wale na dhambi mioyoni mwao. Daudi alisema katika Zaburi “Maana huwi Mungu apendezwaye na ubaya. Mtu mwovu hatakaa kwako” (zaburi 5:4). Roho mtakatifu wa mungu kamwe hawezi kukaa mioyoni mwa wale wenye dhambi ndani yao. Hata mwenye dhambi asiye na Roho Mtakatifu ndani yake aweza kusema ameokoka toka dhambini kulingana na mafundisho na knuni za mawazo yake. 
Hata hivyo mtu hawezi kusema hana dhambi moyoni na ni mwenye haki mbele ya Mungu. Lakini Mungu hawezi kumwita mwenye dhambi kuwa ni mwenye haki. Mwenye dhambi ana wajibu kuhukumiwa na hivyo yampasa kuamini injili ya maji na Roho ili aweze kuokolewa.