Search

FAQ on the Christian Faith

Subject 2: The Holy Spirit

2-1. Ninamwamini Yesu na nadhani nilikwisha pokea ondoleo la dhambi. Pia naamini kwamba Roho Mtakatifu ameweka makazi ndani yangu. Nafahamu yakwamba mtu aliyeokolewa ni hekalu la Mungu. Kila ninapo anguka na kutenda dhambi, Roho Mtakatifu hunirejesha katika mahusiano na Mungu upya kwa kunihukumu na kunisaidia ili niweze kutubu dhambi zangu ili niweze kupokea msamaha wa dhambi. Nimegundua ya kwamba nisipofanya hivyo, Mungu ataniadhibu. Je ni kweli kwamba Roho Mtakatifu hakai ndani yetu kwa nyakati fulani ikiwa hatuto tubu dhambi zetu na kusamehewa?

Hakika hivi sivyo ilivyo, Roho Mtakatifu kuweka makazi hakutegemei vile ilivyo juhudi zetu, au hata tukitenda jambo jema au la. Kwa maneno mengine haitegemei mapenzi yetu au matamanio yetu. Sasa basi kunategemea kitu gani? Roho Mtakatifu hakai ndani ya mtu kwa sababu eti ametubu dhambi na kusamehewa, badala yake Roho Mtakatifu huweka makazi ndani ya mtu nyakati zote ikiwa pale mtu huyo amepokea msamaha wa dhambi kwa kuiamini Injili ya maji na Roho. Roho Mtakatifu kamwe hatoweza kuweka makazi ndani ya mtu aliye na hata dhambi kiasi kidogo.
Hata hivyo watu wengi hudhani ya kwamba Roho Mtakatifu huweka makazi ndani yao ikiwa pale watakapo tubu dhambi na kuomba msamaha, na ikiwa kinyume basi hatoweka makazi ndani yao. Hakika huu ni upotofu, Biblia inasema Roho Mtakatifu aliwafikia Mitume siku ile ya Pentekoste. Lakini imetupasa kuelewa akilini kwamba waliweza kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao si kwa sababu ya sala za toba, bali kwa sababu walikwisha samehewa dhambi zao zote baada ya kuiamini Injili ya maji na Roho.
Roho Mtakatifu ni Roho wa Mungu na huja juu ya wale wote wenye haki walio takaswa kwa dhambi zao kwa kupokea msamaha wa dhambi zao zote. Kile biblia inachomaanisha kwa neo “Utakatifu” ni “kutengwa toka dhambini”. Kuondoa dhambi kwa kutubu na kusali sala ya toba pale dhambi inapotendeka si msamaha ulio sahihi mbele za Mungu. Je, mtu anaweza kutubu dhambi zote pasipo kusahau nyingine mbele za Mungu?
Ni wale tu wanao amini juu ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake iliyo mwagika msalabani kulingana na mpango wa Mungu kwa wokovu wao, ndiyo watakao weza kupokea msamaha wa dhambi pamoja na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao ikiwa ni kipawa cha Mungu. Hata hivyo sababu ya baadhi ya watu wanao jaribu kumpokea Roho Mtakatifu kwa kupitia juhudi zao nikunatokana na wao kushindwa kupokea msamaha halisi wa dhambi ndani ya mioyo yao.
Roho wa kweli wa Mungu haji na kufanya makazi ndani ya watu kwa kupitia toba. Huja moja kwa moja ndani ya pale wanapopokea msamaha wa dhambi kwa kuamini Injili ya maji na Roho. Jambo hili ni muhimu sana kwa imani ili uweze kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu mbele ya Mungu.
Roho Mtakatifu haji kwa kupitia aina zozote za juhudi na matendo kwa upande wetu. Huja juu ya yule anaye amini Injili ya maji na Roho. Tulisamehewa dhambi zetu zote kwa kuamini ya kwamba, Yesu alibeba dhambi zetu zote ulimwenguni kwa kupitia ubatizo wake kwa Yohana pale Yordani takribani miaka 2000 iliyo pita. Roho Mtakatifu ataweza kuweka makazi ndani ya yule atakaye hifadhi aina hii ya imani.
Kamwe hatoweza kuweka makazi ndani ya moyo wa yule aliye na dhambi. Jambo hili ni hakika na kweli ikiwa mtu ataomba uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yake kwa kupitia sala za toba kila mara anapo anguka katika dhambi badala ya kuwa na imani ya Injili ya kweli, kamwe hatoweza kupokea Roho Mtakatifu. Hii inadhihirisha ya kwamba bado anadhambi moyoni mwake ingawa anamwanini Yesu.
Shetani ndiye anaye tuhukumu, katika Watumi 8:1 imeandikwa “sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu”.
Ingawa wapo wanaothubutu kudai kuwa wamekwisha kupokea msamaha wa dhambi na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao. Ikiwa yeyote bado kusamehewa dhambi zake zote kwa kuamini Injili ya maji na Roho, basi bado dhambi zitaendelea kuwe ndani ya moyo wake. Na hii ndiyo maana imekupasa kuwa na ufahamu ulio sahihi juu ya Injili ya maji na Roho ili kwa hakika uweze kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yako. Ikiwa ungependa kujifunza juu ya Injili ya maji na Roho kwa undani zaidi tungependa kukuelekeza usome mlolongo wa vitabu vya Pauli C Jong kuanzia kile cha kwanza kiitwacho “Je umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa Roho?”