Search

FAQ on the Christian Faith

Subject 2: The Holy Spirit

2-9. Roho Mtakatifu alijidhihirisha vipi katika nyakati fotauti za Agano la Kale na Agano Jipya?

Roho Mtakatifu ni Mungu yule yule ukiachilia mbali vipindi vyake. Hivyo asili ya Uungu wake haibadiliki kamwe bila kujali ikiwa tunasoma juu yake wakati wa Agano la Kale au Jipya. Hata hivyo ni kweli kwamba alifanya kazi katika hali ya utofauti wakati wa Agano la Kale na Jipya kwa matakwa ya Mungu ili kuokoa wanadamu kwa dhambi zao.
Katika Agano la Kale Mungu alimwachilia Roho Mtakatifu kwa watu wake kwa njia ya aina yake ili kwamba waweze kunena maneno yake, kuonyesha mapenzi yake kwa njia ya miujiza na kutenda kazi yake. Mfano Roho wa Bwana alianza kuwa juu ya Samsoni aliye Mwamuzi kwa wakati huo alitenda kazi kuu kwa kupitia yeye, (Waamuzi 13:25, 14:19) kwa maneno mengine Roho Mtakatifu alikuja juu ya wale walio teuliwa halisi wakati wa Agano la Kale.
Hata hivyo wakati wa Agano Jipya kwa kuiweka wakfu siku ya Pentekoste kama mwazo wa kuja kwake Roho Mtakatifu, Mungu alimtuma Roho Mtakatifu kwa kila mtakatifu aliye kwisha pokea msamaha wa dhambi kwa njia ya imani ya injili ya maji na Roho na kuruhusu Roho huyo kuweka makazi ndani yao daima milele.
Hivyo baada ya kuja kwake Roho Mtakatifu katika siku ile ya Pentekoste wenye haki wote ambao dhambi zao zilisamehewa kwa kuamini kwao injili ya kweli wataweza kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao. (Matendo 2:38). Petro alikwenda nyumbani wa Kornelio aliyekuwa mtu wa mataifa akida wa kikosi kilichoitwa Kitalia na kumhubiria injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani, wakati Petro alipokuwa akiongelea juu ya injili hiyo kwao, ndipo Roho Mtakatifu akawashukia juu yao wale walio sikia neno (Matendo 10:34-45). Hii inatuthibitishia kwamba katika muda huo waliokuwa wakiisikiliza na kuamini injili ya ubatizo wa Yesu na msalaba wake ambaye Yesu aliikamilisha, waliweza kumpokea Roho Mtakatifu kama zawadi kwao.
Mungu alisababisha Roho Mtakatifu kuweka makazi ndani ya wale wote wenye haki ambao tayari wamekwisha pokea msamaha wa dhambi kwa kuiamini injili ya kweli. Roho Mtakatifu katika Agano la Kale amechukua nafasi ya juu katika kuwaongoza watu kwa Yesu Kristo. Roho Mtakatifu katika Agano Jipya anashuhudia haki ya Mungu na kusimama akiwa kama mthibitishaji kwa hilo. Haki ya Mungu maana yake ni Yesu kusamehe dhambi zote za ulimwengu kwa njia ya ubatizo wake na damu yake msalabani. Na Roho Mtakatifu husimama akiwa kama mthibitishaji wa injili ya wokovu na kusaidia kila aiaminiye.