" Freely you have received, freely give " (Matthew 10:8)

HOME  |  SITEMAP  |  CONTACT US  |  HELP    
  Free eBook Version of Swahili edition 35

 


HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA (III): Ubainisho wa Injili ya Maji na Roho

 • Electronic Book Format : MS Reader
 • Current Downloads : 42
 • About this book
 • Table of Contents
 

Dokezo

Ubainisho wa Injili ya Maji na Roho

Maelezo ya Kina

Je, tunawezaje kuupata ukweli uliofichika katika Hema Takatifu la Kukutania? Ni kwa kuifahamu injili ya Maji na Roho tu, ambayo ni kiini cha kweli cha Hema Takatifu la Kukutania, ndipo tunapoweza kufahamu kwa usahihi jibu la swali hili.
Kwa kweli, nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa kama zilivyodhihirishwa katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania zinatuonyesha kazi za Yesu Kristo katika kipindi cha Agano Jipya ambazo zimemuokoa mwanadamu. Kwa njia hii, Neno la Agano la Kale la Hema Takatifu la Kukutania na Neno la Agano Jipya yanahusiana kwa karibu sana kama vile ilivyo kwa nyuzi za kitani safi ya kusokotwa. Lakini, kwa bahati mbaya ukweli huu umefichwa kwa muda mrefu kwa kila mtafuta ukweli katika Ukristo.

Alipokuja hapa duniani, Yesu Kristo alibatizwa na Yohana Mbatizaji na akamwaga damu yake katika Msalaba. Bila ya kuifahamu na kuiamini injili ya maji na Roho, hakuna kati yetu anayeweza kamwe kupata ukweli uliofunuliwa katika Hema Takatifu la Kukutania. Hivyo ni lazima tujifunze na kuuamini ukweli huu wa Hema Takatifu la Kukutania. Sisi sote tunahitaji kutambua na kuamini juu ya ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa za lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania.


Kutoka kwa Mchapishaji

Wakristo wengi katika zama hizi hudai kuwa wamekutana na injili inayoweza kusafisha kabisa dhambi zao, wakati hawaujui ukweli wa nyuzi za bluu unaodhihirishwa katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania. Ni wazi kuwa wakristo wa jinsi hiyo ambao bado wana dhambi katika mioyo yao wanaamini katika Yesu kwa upofu bila kuufahamu ukweli uliofunuliwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu zilizotumika katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania.
Kwa hiyo mwandishi anahitaji kuutangaza ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa zilizotumika katika lango hili. Ukweli huu wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu zilizotumika katika Hema Takatifu la Kukutania ni kivuli cha injili ya maji na Roho iliyofunuliwa kwetu katika Agano Jipya, na ni udhihirisho halisi wa injili ya kweli.
Kupitia kitabu hiki, utaugundua ukweli unaofunuliwa katika nyuzi hizi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, na kwa hiyo utaweza kuonana na Bwana kwa imani. Ninakusihi uamini katika injili kama inavyofunuliwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyuzi nyekundu zilizotumika katika Hema Takatifu la Kukutania ili uweze kuwa na imani itakayoweza kukuokoa kutokana na dhambi zako zote.


 
Free Christian eBooks
    eBook List
    Swahili edition 35
 
 • About this book
 •  
 • Table of Contents
 •     What is eBook?
   
 • About eBook
 •  
 • How to read an eBook?
 •  
 • FAQ
 •  
 • Download Help
 •     eBook Readers
   
 • MS Reader 2.0
 •  
 • Acrobat Reader 4.0
 •  
  Partner's Zone

  register as a coworker
  Bookmark
     
  Copyright © 2001 - 2019 The New Life Mission. All Rights Reserved.