" Freely you have received, freely give " (Matthew 10:8)

HOME  |  SITEMAP  |  CONTACT US  |  HELP    
  Free eBook Version of Swahili edition 13

 


TULIAMINI NINI ILI KUPOKEA ONDOLEO LA DHAMBI?

- MAHUBIRI KATIKA INJILI YA MATHAYO (II)

 • Electronic Book Format : MS Reader
 • Current Downloads : 11
 • About this book
 • Table of Contents
 

Dokezo

TULIAMINI NINI ILI KUPOKEA ONDOLEO LA DHAMBI?

Maelezo ya Kina

Mtume Mathayo anatueleza kuwa Neno la Yesu lilielezwa kwa kila mtu katika ulimwengu huu, hii ni kwa sababu Mathayo alimwona Yesu kuwa ni Mfalme wa wafalme. Kwa sasa, Wakristo katika ulimwengu mzima ambao wamezaliwa tena upya kwa kuamini katika injili ya maji na Roho wanatamani sana kuula mkate wa uzima. Lakini ni vigumu kwa wao kuwa na ushirikiano nasi katika injili ya kweli, kwa sababu wapo mbali sana na sisi. Kwa hiyo ili kutimiza mahitaji ya kiroho ya watu hawa wa Yesu Kristo, Mfalme wa wafalme, basi mahubiri katika kitabu hiki yameandaliwa kama mkate mpya wa uzima ili kuboresha ukuaji wao wa kiroho. Mwandishi anatangaza kuwa wale waliokwishapokea ondoleo la dhambi zao kwa kuamini katika Neno la Yesu Kristo, Mfalme wa wafalme, ni lazima wajilishe Neno lake halisi ili waweze kuilinda imani yao na kuyaimarisha maisha yao ya kiroho. Kitabu hiki kitawapatia mkate wa kweli wa uzima kwenu nyote ambao mmefanyika kuwa watu wa ufalme wa Mfalme kwa imani. Kwa kupitia Kanisa na watumishi wake, Mungu ataendelea kukupatia mkate huu wa uzima. Baraka za Mungu na ziwe juu yao wale wote waliozaliwa upya kwa maji na kwa Roho, na ambao wanatamani kuwa na ushirika wa kweli wa kiroho pamoja nasi katika Yesu Kristo.

Kutoka kwa Mchapishaji

Ni lazima tuwe na imani ambayo Mitume walikuwa nayo na kisha tuamini kama wao walivyoamini kwa kuwa imani yao ilitoka kwa Roho Mtakatifu. Mitume walimwamini Yesu Kristo, Baba yake, na Roho Mtakatifu kuwa ni Mungu wao. Mtume Paulo alikiri kuwa alikufa pamoja na Kristo na akaishi pamoja na Kristo. Paulo alifanyika kuwa chombo cha Mungu kwa kuamini kuwa alibatizwa katika Yesu Kristo (Wagalatia 3:27). Katika injili ya Mungu kunapatikana ubatizo ambao Yesu aliupokea, damu ambayo aliimwaga Msalabani, na karama ya Roho Mtakatifu ambayo ameitoa kwa mtu yeyote anayeamini katika injili hii. Tunaamini kuwa kila mtu katika ulimwengu huu anaamini katika injili hii ya asili, na anaishi maisha ya haki mbele za Mungu kwa kuwa mwenye haki ataishi kwa imani (Waebrania 10:38). Hii ndio sababu mwandishi ameamua kuuandika mfululizo huu wa Ukuaji wa kiroho. Tunahakika kuwa mfululizo huu utaiimarisha imani yako katika injili ya kweli na kisha itakuongoza kumfuata Bwana kama mfuasi wake.


 
Free Christian eBooks
    eBook List
    Swahili edition 13
 
 • About this book
 •  
 • Table of Contents
 •     What is eBook?
   
 • About eBook
 •  
 • How to read an eBook?
 •  
 • FAQ
 •  
 • Download Help
 •     eBook Readers
   
 • MS Reader 2.0
 •  
 • Acrobat Reader 4.0
 •  
  Partner's Zone

  register as a coworker
  Bookmark
     
  Copyright © 2001 - 2019 The New Life Mission. All Rights Reserved.