Rev. Paul C. Jong
YALIYOMO
Dibaji
1. Wokovu wa Wenye Dhambi Unafunuliwa Katika Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 27:9-21)
2. Nguzo za Ua wa Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 27:9-19)
3. Madhabahu ya Sadaka ya Kuteketezwa Iliyotengenezwa Kwa Mti wa Mshita na Kufunikwa Kwa Shaba (Kutoka 38:1-7)
4. Madhabahu ya Uvumba Ni Mahali Ambapo Mungu Anaitoa Neema Yake (Kutoka 30:1-10)
5. Maana ya Kiroho ya Vikuku vya Fedha Vilivyotumika Katika Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 26:15-30)
6. Kiti cha Rehema (Kutoka 25:10-22)
7. Vikombe Vya Mapambo Kwa Injili ya Maji na Roho (Kutoka 25:31-40)
8. Maana za Kiroho Zilizofichika Katika Mavazi ya Kuhani Mkuu (Kutoka 28:1-43)
9. Utakatifu Kwa Bwana (Kutoka 28:36-43)
10. Kifuko cha Kifuani cha Hukumu (Kutoka 28:15-30)
11. Sadaka ya Dhambi Ili Kumsimika Kuhani Mkuu (Kutoka 29:1-14)
12. Kuhani Mkuu Aliyetoa Sadaka Siku ya Upatanisho (Mambo ya Walawi 16:1-34)
13. Vifaa Vilivyotumika Katika Mavazi ya Kuhani Mkuu (Kutoka 28:1-14)
(Swahili)
Je, tunawezaje kuupata ukweli uliofichika katika Hema Takatifu la Kukutania? Ni kwa kuifahamu injili ya Maji na Roho tu, ambayo ni kiini cha kweli cha Hema Takatifu la Kukutania, ndipo tunapoweza kufahamu kwa usahihi jibu la swali hili.
Kwa kweli, nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa kama zilivyodhihirishwa katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania zinatuonyesha kazi za Yesu Kristo katika kipindi cha Agano Jipya ambazo zimemuokoa mwanadamu. Kwa njia hii, Neno la Agano la Kale la Hema Takatifu la Kukutania na Neno la Agano Jipya yanahusiana kwa karibu sana kama vile ilivyo kwa nyuzi za kitani safi ya kusokotwa. Lakini, kwa bahati mbaya ukweli huu umefichwa kwa muda mrefu kwa kila mtafuta ukweli katika Ukristo.
Alipokuja hapa duniani, Yesu Kristo alibatizwa na Yohana Mbatizaji na akamwaga damu yake katika Msalaba. Bila ya kuifahamu na kuiamini injili ya maji na Roho, hakuna kati yetu anayeweza kamwe kupata ukweli uliofunuliwa katika Hema Takatifu la Kukutania. Hivyo ni lazima tujifunze na kuuamini ukweli huu wa Hema Takatifu la Kukutania. Sisi sote tunahitaji kutambua na kuamini juu ya ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa za lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania.
(English)
How can we find out the truth hidden in the Tabernacle? Only by knowing the gospel of the water and the Spirit, the real substance of the Tabernacle, can we correctly understand and know the answer to this question. In fact, the blue, purple, and scarlet thread and the fine woven linen manifested in the gate of the Tabernacle`s court show us the works of Jesus Christ in the New Testament`s time that have saved the mankind. In this way, the Old Testament`s Word of the Tabernacle and the Word of the New Testament are closely and definitely related to each other, like fine woven linen. But, unfortunately, this truth has been hidden for a long time to every truth seeker in Christianity. Coming to this earth, Jesus Christ was baptized by John and shed His blood on the Cross. Without understanding and believing in the gospel of the water and the Spirit, none of us can ever find out the truth revealed in the Tabernacle. We must now learn this truth of the Tabernacle and believe in it. We all need to realize and believe in the truth manifested in the blue, purple, and scarlet thread and the fine woven linen of the gate of the Tabernacle`s court.
Next
English 36: Sermons on the Gospel of John (Ⅳ) - HAVE YOU MET JESUS WITH THE GOSPEL OF THE WATER AND THE SPIRIT?