Search

Preguntas Frecuentes sobre la Fe Cristiana

Tema 3 : Apocalipsis

3-12. Je, “mkutano mkubwa ambao hakuna anayeweza kuuhesabu (Ufunuo 7:9)” una maanisha ni watakatifu walionyakuliwa?

Ndiyo, hiyo ni sahihi kabisa. Ufunuo 7:9 inaeleza, “Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao,” hapa tunaweza kuona kwamba kwa imani yao katika injili ya maji na Roho, idadi kubwa ya makutano miongoni mwa Wamataifa watapambana na kumshinda Mpinga Kristo, halafu wauawa na kuwa wafia-dini, kisha watashiriki katika ufufuo wa kwanza na kunyakuliwa. 
Ingawa katika siku hizi za mwisho Mpinga Kristo atacharuka pasipo kuhofia adhabu, basi tunaweza kuona kwamba katika nyakati hizo kutainuka idadi kubwa ya watu wanaoamini katika injili ya maji na Roho iliyotolewa na Mungu. Kwa hiyo, mkutano mkuu utatokea miongoni mwa Wamataifa, mkutano ambao ni mkubwa kiasi kuwa hakuna hata mmoja anayeweza kuuhesabu, huo utakuwa ni mkutano wa watu ambao wameokolewa toka katika dhambi kwa kuamini katika injili ya maji na Roho na kisha kupokea vifo vya kuwa wafia-dini kwa imani. 
Ufunuo 7:14 inasema, “Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.” Wakati Dhiki Kuu ilipokuja hapa duniani, watu hawa waliokolewa toka katika dhambi kwa kuamini kwa mioyo yao yote katika injili ya maji na Roho iliyokuwa ikihubiriwa na Kanisa la Mungu. Hivyo waliuawa na kuwa wafia-dini, kwa kuwa hawakumwabudu Mpinga Kristo wala kuipokea alama ya Mnyama katika mikono yao ya kulia au katika vipaji vya nyuso zao, hivyo wakajiunga katika ufufuo wa watakatifu na unyakuo. Hii ndio maana wanasimama mbele ya kiti cha enzi na mbele ya Mwana-kondoo huku wakisifu; “Wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo!”
Hivyo, Mungu, si Mungu wa Wayahudi, bali ni Mungu pia wa Wamataifa. Kwa hiyo, Mungu atahakikisha kwamba wakati siku za Dhiki Kuu zitakapowadia, idadi kubwa ya Wamataifa toka mataifa mbalimbali, makabila, watu, na lugha mbalimbali wataiamini injili ya maji na Roho, watapokea ondoleo la dhambi, kisha watasimama miongoni mwa orodha ya wafia-dini.