Search

Sermons

Somo la 11: Maskani

[11-7] Vifaa vya Ujenzi vya Hema Takatifu la Kukutania Vilivyoweka Msingi wa Imani (Kutoka 25:1-9)

Vifaa vya Ujenzi vya Hema Takatifu la Kukutania Vilivyoweka Msingi wa Imani
(Kutoka 25:1-9)
“BWANA akanena na Musa, akamwambia: ‘Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu. Sadaka utakayopokea mikononi mwao ni hii: dhahabu, na fedha, na shaba; na nyuzi za rangi ya bluu, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na kitani safi, na singa za mbuzi; na ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo, na miti ya mshita; na mafuta ya ile taa, na viungo vya manukato kwa yale mafuta ya kupaka, na kwa ule uvumba wenye harufu nzuri; na vito vya shohamu, na vito vingine vya kutiwa kwa ile naivera, na kwa kile kifuko cha kifuani. Nao wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao. Sawasawa na haya yote nikuonyeshayo, mfano wa maskani, na mfano wa vyombo vyake vyote, ndivyo mtakavyovifanya.’”
 

Maisha ya Kimaskini
 
Katika shairi linaloitwa ‘Zaburi ya Maisha,’ Henry Wadsworth Longfellow aliandika, “Usinieleze, kwa namba ya za majonzi, ‘Maisha ni Ndoto isiyo na kitu!’”
Hata hivyo, ukifikiri hasa kuhusu ushairi huo, kwa kweli maisha ya wanadamu ni ya kimaskini sana. Japokuwa maisha ya kila mtu yanaonekana yakiishia kuyarudia mavumbi baada ya kuishi maisha ya kisafari na upweke katika jangwa la ulimwengu, ndipo tunaona kuwa dunia si kituo chetu cha mwisho. Kwa sababu ya dhambi, mwisho wa kila maisha ya mtu utakuwa ni mateso ya kutisha ya milele huko kuzimu.
Hata hivyo, watu wako kinyume na kifo chao wenyewe na ulimwengu baada ya kaburi. Wakati wanaishi katika ulimwengu huu, watu wanaishi bila lengo lolote, wakielekea kuzimu, wakiwa hawawezi kukutana na Mungu aliyewaokoa. Haya ni maisha. Lakini kama kweli haya ndiyo yangekuwa maisha, je ni huzuni kiasi gani mbayo tungekuwa nayo?
Kwa maisha ya jinsi hiyo, Masihi anayangojea. Ikiwa watu wangekuwa wametupwa ovyoovyo katika ulimwengu huu ili wazunguke huku na huku bila lengo na mwisho kupotea katika giza, kwa kweli wangekuwa wakielekea maisha ya huzuni na ya kutisha. Sisi sote tunaweza kulitambua jambo hili kwa kuwaangalia wale wanaotuzunguka.
Siku moja nilipokuwa ndani ya gari, nilimuona mtu mmoja mzee mwenye miaka kama 60 hivi alikuwa akitembea barabarani. Hali akitembea mbele yangu akiwa amenipa mgongo alikuwa ameinamisha kichwa chake, na mabega yake yalikuwa yamelegea, alionekana kuwa ni mpweke sana. Nilipopiga honi aligeuka na niliona kuwa uso wake ulijawa na huzuni na simanzi. Nilipomuona mzee huyu jinsi alivyoonyesha, nilimtazama hali nikifikiria kwa kitambo. Mzee huyu bila shaka alikuwa akifikiria jinsi ambayo maisha yake yasivyo na kitu chochote. Huzuni ya anguko bila shaka imechangia sana kuongeza fikra hii ya utupu, ikimfanya kufikiri juu ya maisha yake yasiyo na maana. Kwa kweli si maisha ya mzee huyu tu ndiyo yenye huzuni, bali ni maisha ya kila mtu.
Wakati muda unapowapita, watu hawatambui kuwa wanaelekea kuwa wazee, mpaka pale wanapokuja kuona makunyanzi katika mwili mzima. Wengi wao wamekutana na shida nyingi katika maisha yao kiasi kwamba hawana hata nafasi ya kupumzika, kugeuka, na kuona mahali ambapo wamekuwa wakitembea. Japokuwa wazazi wote wameishi na kufanya kazi kwa juhudi sana kwa ajili ya watoto wao na familia zao, maneno hayawezi kuelezea huzuni yao, kwani wanapokaribiana na kuzama kwao kwa jua hakuna kitu kinachoweza kubakia katika maisha yao.
Hali wakiwa wametwaliwa na hisia zao wanajikuta wakishangazwa sana kwa machozi. Baada ya muda mwingi kupita, na baada ya miaka mingi kupita, ndipo mwishowe wanapata nafasi ya kuangalia nyuma walikotoka, na wanapofanya hivyo, wanachoweza kukiona ni mandhari ya ajabu ya upweke ya anguko la mwisho jinsi inavyoonekana katika mtazamao wao binafsi. Katika anguko, wakati majani yote yameanguka, wakati mmea ukikumbana na kipupwe kikali kinachoua, ndipo wanapotambua kuwa hata maisha yao yatatoweka kwa mtindo huo huo. Kwa hakika wanaweza kujuta kwamba imewachukua muda mrefu kulitambua jambo hili. Je, ni tumaini gani ambalo watu hawa wanalo, wakati wanapokaribia kufa hata pasipo kumuona Bwana? Watu wa jinsi hiyo ambao wanafikia mwisho wao bila kuonana na Masihi watakuwa na huzuni milele.
Kama si kukutana na Bwana, mimi binafsi ningekuwa nimeyaongoza maisha yangu katika huzuni. Je, vipi kuhusu wewe? Ikiwa hujakutana na Bwana unaelekea wapi sasa? Kuna watu wengi sana katika ulimwengu huu, ambao kwa sababu walikuwa hawawezi kukutana na Bwana, wamejihifadhia kutokuwa na furaha wao wenyewe.
Kwa kweli ninavunjika moyo sana ninapowafikiria watu hawa, kwamba kuna watu wengi sana ambao wamejihifadhia wao wenyewe kutokuwa na furaha. Kitu pekee ambacho Nguruwe wanafanya ni kujilisha wenyewe hadi pale watakapokutana na mwisho wao wenyewe, lakini maisha yetu ni tofauti kabisa na hawa Nguruwe, kwani ni lazima tutafakari na kuangalia zaidi ya wakati huu tulionao, yaani kwenye maisha yajayo ya milele. Watu wengi wanakutana na siku yao ya mwisho wakiwa wamejawa na majuto. Japokuwa wanafahamu kuwa kuna Ufalme wa Mbinguni wa milele, wanajitambua kuwa hawastahili na hawajitoshelezi kuuingia ufalme huo, kwa kuwa walibakia ni wenye dhambi. Ukweli kuwa kuna maisha mengi ya jinsi hiyo yaliyojaa majuto kunanifanya niomboleze na kulia kwa sababu ya bahati yao mbaya.
Tunapofikiria juu ya maisha haya, kwamba hayawezi kwenda mahali pazuri palipoandaliwa na Mungu, na kwamba yatatoweka toka katika ulimwengu huu hata kabla ya kutimisha lengo mahsusi kwa maisha yake, ndipo tunapoweza kuzionea huruma nafsi hizi na kuziombolezea kwa majaliwa yake. Hii ndiyo sababu maisha yanalinganishwa na safari katika bahari ngumu na iliyochafuka. Katika kuyaelezea maisha, watu wanasema kuwa ni kama kujaribu kuishi katika bahari iliyochafuka, ni kama kujaribu kuishi katika machungu ya dunia ya mwanadamu, mwanadamu ni lazima ateseke tangu kuzaliwa kwake hadi kufa kwake, akihangaika na kupiga makelele ili aweze kuishi.
Tunapojikumbusha sisi wenyewe kuwa hivi ndivyo maisha yalivyo, ndipo tunapotambua kwa hakika kuwa kazi ya kuuelezea ukweli wa Hema Takatifu la Kukutania kwa watu wote na kuwasaidia ili waweze kuonana na Bwana ni kazi muhimu na yenye maana sana. Ni Kwa nini? Kwa sababu kwa kupitia sadaka ya kuteketezwa, Mungu anawapatia watu hawa wenye dhambi wokovu toka katika dhambi kwa kukutana nao katika nyumba yake ya Mungu. Hema Takatifu la Kukutania ni Nyumba ya Mungu iliyoanzishwa na kuthibitishwa jangwani. Katika Nyumba hii ya Mungu, Hema Takatifu la Kukutania, Mungu anakutana na wenye dhambi kupitia neema ya ondoleo la dhambi iliyotimizwa kwa sadaka ya kuteketezwa. Mungu anatueleza kuwa, “Nitakufanya uijenge Nyumba yangu mahali nitakapoishi, na nitakutana nawe ndani ya Hema hili Takatifu la Kukutania, katika kiti chake cha rehema.” Ni katika Hema Takatifu la Kukutania tu, ambayo ni Nyumba ya Mungu, ndipo mtu yeyote amepewa nafasi ya kukutana na Mungu.
Imani hii ndiyo ukweli wa Hema Takatifu la Kukutania na haiwezi kubadilishwa kwa kitu chochote katika ulimwengu huu, na ni ya thamani sana isiyoweza kununuliwa kwa gharama yoyote ile. Ninaamini kwamba kwetu sisi ambao tunayo imani ya Kikristo inayomwamini Yesu Kristo kuwa ni Mwokozi wetu, kuwa na ufahamu sahihi na imani sahihi katika Hema Takatifu la Kukutania ndiyo njia ya kutupeleka katika barabara yenye baraka zaidi.
 

Tunaishi Maisha Yetu Yaliyobarikiwa
 
Moyo wangu umejazwa na mawazo ya furaha, nikishangaa ikiwa kuna mtu mwingine yeyote ambaye anaishi maisha yenye baraka kiasi hicho kama ambavyo sisi tunaishi. Japokuwa maisha ni uwepo wenye huzuni, watu wengi wanaendelea kuishi katika maisha yao hali wakiwa wamesahau mauti yao binafsi. Lakini Mungu anawataka watambue jinsi ambavyo maisha yao yamekuwa ni magumu mbele za Mungu, na anataka kuifanya mioyo yao iweze kutubu. Kwa upande mwingine, wao, wanajitahidi kuishi maisha yao bila kuisikiliza injili ambayo Mungu amewapatia bure na bila ya kufungua hata eneo dogo katika mioyo yao. 
Kutoka inatueleza juu ya mapigo kumi ambayo Mungu aliyaleta kwa Farao. Jumla ya mapigo kumi yaliletwa katika nchi ya Misri. Mungu alimwamuru Farao awaruhusu watu wake waliokuwa wakiishi Misri kuondoka. Alimwambia Farao kuwa ikiwa asingelitii, atayaleta mapigo kumi juu yake. Lakini Farao hakusikiliza yale ambayo Mungu alimwambia, akaipinga amri ya Mungu katika ukaidi, na akaishia kuyapata mapigo yote kumi ambayo Mungu aliahidi. Ukaidi wa Farao ulikuwa wa kimakosa. Pia, sababu iliyomfanya hatimaye awaruhusu watu wa Israeli baada ya kuzipokea adhabu zote za Mungu ni kuwa alikuwa ameshikiliwa na Shetani. Hii inatuonyesha pia juu ya ukaidi wetu wa kutotii unaopatikana ndani ya kila mmoja wetu.
Hata hivyo, watu wa jinsi hiyo bado wanaweza kupokea ondoleo la dhambi lililoandaliwa na Mungu katika Hema lake Takatifu la Kukutania, na wanaweza kuishi na Mungu katika imani. Lakini watu hawa bado ni wakaidi sana kiasi kuwa wanaendelea kukataa na kutouamini ukweli wa Mungu hali wakiwa na ugumu wa punda. Hii ndiyo sababu kuna watu wengi sana ambao wanashindwa kukutana na Mungu wa kweli, wakiendelea kuishi maisha yao kama wenye dhambi, na mwisho wake wanakutana na uharibifu. Jambo hili linanipa huzuni sana kupita majonzi ya kawaida. Watu wengi sana wanaelekea katika njia ya ugumu sana mbele za Mungu.
Kwa sababu watu wa jinsi hiyo wanajitoa kwa muda pale wanapokutana na magumu, lakini baadaye kidogo wanairudia ile hali waliyokuwa nayo ya kuyakataa mapenzi ya Mungu, kwa mara nyingine tena wanazirudia njia za ukaidi, watu hawa watakutana na pigo lao la pili. Kwa pigo hili la pili, wanaziacha njia zao kwa muda tu. Lakini hawadumu kwa muda mrefu kwani wataanza tena kutomtii Mungu na kumletea Mungu changamoto. Kwa hiyo wanajikuta wakiwa chini ya pigo la tatu, wakifuatiwa na mapigo mengine, la nne, la tano, la sita, la saba, la nane, na la tisa, ndipo mwisho wanatii baada ya pigo la mwisho na wanapokuwa tayari wameharibiwa.
Wakati pigo la mwisho linapokuja, kutakuwa na watu wengi ambao watayabeba mateso ya kuzimu kwa kutokuamini yale ambayo Masihi amefanya kwa ajili yao. Maisha ya watu hawa ni ya ujinga kiasi gani? Hii ndiyo sababu kuwa maisha ya kila mtu ni yenye huzuni sana.
Japokuwa maisha ya watu ni yenye huzuni tu mbele za Mungu, ni lazima utambue kuwa kukutana na Mungu katika Hema Takatifu la Kukutania ni baraka kuu kwako na ni vizuri uliishi Neno la Hema Takatifu la Kukutania ukiwa na uelewa huu.
 

Matoleo Ambayo Mungu Anayataka toka Kwetu
 
Mungu alimwamuru Musa kwenda juu katika Mlima Sinai na akampatia mtitiriko mzima wa Sheria yake. Kwanza kabisa, alimpatia Musa Amri Kumi: “Usiwe na miungu mingine ila Mimi; usijifanyizie sanamu kisha ukaziabudu; usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako; ikumbuke siku ya Sabato na kuifanya kuwa takatifu; waheshimu baba na mama yako, usiue, usizini; usiibe; usimshuhudie uongo jirani yako; na usitamani mali ya jirani yako wala chochote alichonacho.” Kwa nyongeza, Mungu aliwapatia sheria nyingine ambazo waisraeli walitakiwa kuzitunza na kuzifuata katika maisha yao ya kila siku: Hizo zilikuwa ni amri 613 na sheria za Mungu kwa jumla.
Amri hizi 613 zilihusisha mambo yote madogo madogo kwa mfano zilieleza ni kitu gani waisreali wafanye wanapokuwa wamepoteza ng’ombe zao, au mtu afanye nini ng’ombe wake anapokuwa ametumbukia katika shimo, kwamba wasifanye uasherati, kwamba ikiwa wana watumishi ni lazima wawaachilie huru katika mwaka wa saba, kwamba ikiwa walimruhusu mtumishi wao wa kike kuoana na mtumishi wa kiume na wakazaa mtoto, wamruhusu mtumishi wa kiume kwenda peke yake katika mwaka wa saba, n.k. Mungu alimwambia Musa kuhusiana na sheria hizo zote za kimaadili ambazo waisraeli walitakiwa kuzitunza na kuzifuata kwa imani mbele za Mungu katika maisha yao ya kila siku.
Kisha Mungu akamwambia Musa kushuka chini ya mlima na kuwakusanya wazee, na kuzitangaza amri za Mungu. Hali wakilisikia Neno la Mungu, watu wa Israeli walikubali na wakaapa kwa damu yao kuwa watatii amri zote za Mungu (Kutoka 24:1-4).
Kisha Mungu akamuita Musa kwenda mlimani kwa mara nyingine, wakati huu alimwita ili kumwamuru kulijenga Hema Takatifu la Kukutania.
Mungu akamwambia Musa, “Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu.” (Kutoka 25:2). Kisha Mungu akaziorodhesha sadaka zake: “Sadaka utakayopokea mikononi mwao ni hii: dhahabu, na fedha, na shaba; na nyuzi za rangi ya bluu, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na kitani safi, na singa za mbuzi; na ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo, na miti ya mshita; na mafuta ya ile taa, na viungo vya manukato kwa yale mafuta ya kupaka, na kwa ule uvumba wenye harufu nzuri; na vito vya shohamu, na vito vingine vya kutiwa kwa ile naivera, na kwa kile kifuko cha kifuani.” (Kutoka 25:3-7).
Kulikuwa na lengo mahususi ambalo kwa hilo Mungu alimwaambia kuzileta sadaka hizi. Lengo hilo lilikuwa ni kuijenga hapa duniani Nyumba ya Mungu yenye kung’aa, mahali ambapo hapana dhambi na ambapo Mungu atakaa, ili aweze kukutana na watu wa Israeli na kuzifanya dhambi zao kutoweka. Hata hivyo, hii haimaanishi kuwa Mungu aliwaeleza kuleta fedha ili kujenga jumba la kumbukumbu kama yalivyo makanisa ya leo. Manabii wa uongo wa Ukristo wa leo wanatumia kifungu hiki vibaya pale wanapotaka kuyajenga makanisa yao ili kuzitimiza tamaa zao binafsi.
Kinyume chake, Mungu aliwaambia waisraeli kumtolea sadaka hizo ili aweze kuzitumia kuijenga nyumba yake mwenyewe na kisha kuwabariki vya kutosha. Kwa kweli, sababu iliyomfanya Mungu apokee sadaka hizi ilikuwa ni kwa ajili ya kutukomboa sisi toka katika dhambi zetu na kutuokoa toka katika hukumu yetu. Pia ilikuwa ajili ya Mungu ili aweze kukutana nasi, sisi ambao tulikuwa tukiishi maisha yenye huzuni ya kutisha, ili aweze kuziosha dhambi zetu na kuzifanya zitoweke, na kutufanya sisi kuwa watu wake mwenyewe.
 

Maana ya Kiroho Iliyofichika ya Sadaka Ambazo Mungu Aliamuru Aletewe.
 
Kabla hatujaenda mbali, hebu tutumie muda kidogo kutafakari juu ya maana ya kiroho ya sadaka hizi ambazo Mungu aliamuru aletewe. Baada ya kutafakari tutaichunguza imani yetu kwa mtazamo wa sadaka hizo.
 

Dhahabu, Fedha, na Shaba
 
Kwanza ni lazima tuchunguze mahali ambapo dhahabu, fedha, na shaba vilitumika. Katika Hema Takatifu la Kukutania, dhahabu ilitumika kwa ajili ya Mahali Patakatifu, Patakatifu pa Patakatifu, na vifaa vilivyokuwamo ndani ya hizo sehemu takatifu ikiwemo kinara cha taa, meza ya mkate wa wonyesho, madhabahu ya uvumba, kiti cha rehema, na Sanduku la Ushuhuda. Dhahabu inamaanisha imani katika Neno la Mungu. Na fedha inamaanisha neema ya wokovu. Inatueleza kuwa ni lazima tuwe na imani inayoamini katika zawadi ya wokovu iliyotolewa bure na kwa ukamilifu na Masihi, na imani ambayo inaamini kuwa Bwana wetu amezichukua dhambi zetu zote na kwamba alihukumiwa kwa ajili yetu.
Kwa upande mwingine, Shaba, ilitumika katika vitanzi vya nguzo za Hema Takatifu la Kukutania, katika vigingi vyake, birika la kunawia, na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. Vifaa au vyombo vyote vya Shaba vilifukiwa au vilipigiliwa ardhini. Hii inamaanisha juu ya hukumu ya dhambi za watu, pia shaba inatueleza kuwa tunatahukumiwa adhabu na Mungu kwa kushindwa kuitunza na kuifuata Sheria kwa sababu ya dhambi zetu.
Je, ni maana ipi ya kiroho ya dhahabu, fedha, na shaba? Vitu hivi vinaunda misingi ya imani katika kupokea zawadi ya wokovu iliyotolewa na Mungu. Biblia inatueleza kuwa sisi sote ni wenye dhambi ambao hatuwezi kuifuata Sheria kikamilifu, na kwamba tunastahili kufa kwa sababu ya dhambi zetu, na kwamba badala ya kifo chetu Bwana alikuja hapa duniani na alihukumiwa kwa ajili ya dhambi zetu kwa kufanyika sadaka ya kuteketezwa ya sadaka ya dhambi ambayo ilitolewa katika Hema Takatifu la Kukutania.
Ili kutatua tatizo la dhambi zao, wenye dhambi walileta mnyama asiye na mawaa katika Hema Takatifu la Kukutania, na kwa mujibu wa utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa, walizipeleka dhambi zao katika mnyama huyo wa sadaka kwa kuiweka mikono yao juu ya kichwa chake; kisha sadaka ile ya kuteketezwa ambayo ilizipokea dhambi zao ilimwaga damu yake kwa kuuawa. Kwa kufanya hivyo, watu wa Israeli ambao walikuwa wamefungwa kuzimu (shaba), waliweza kupokea ondoleo la dhambi zao (fedha) na waliikwepa adhabu ya dhambi zao kwa imani (dhahabu).
 


Nyuzi za Bluu, Zambarau, na Nyekundu, na Kitani Safi ya Kusokotwa

 
Nyuzi za Bluu, Zambarau, na Nyekundu, na Kitani Safi ya KusokotwaHapa kuna vifaa vingine vilivyotumika mara kwa mara; nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa. Nyuzi hizi zilitumika katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania, lango la Mahali Patakatifu, na katika pazia lililotenganisha kati ya Mahali Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu. Nyuzi hizi nne zinatueleza juu ya ukweli kuwa kama ilivyotabiriwa katika Mwanzo 3:15, kwamba Bwana atakuja kama sehemu ya uzao wa mwanamke, ni kweli kuwa Bwana wetu atakuja hapa duniani na atawaokoa wenye dhambi toka katika dhambi zao kwa kubatizwa na kusulubiwa, na kwamba ni Mungu mwenyewe ndiye atakayetuokoa sisi.
Nyuzi nne hazikutumika tu kwa ajili ya malango ya Hema Takatifu la Kukutania, bali zilitumika pia katika mavazi ya Kuhani Mkuu na yalitumika kama kifuniko cha kwanza cha Hema Takatifu la Kukutania. Hili lilikuwa ni agano la Mungu kwamba Yesu Kristo atakuja hapa duniani na kutuokoa toka katika dhambi zetu kwa kuzitimiza kazi zake za nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Kwa kweli Bwana wetu aliitekeleza ahadi hii na kwa hakika ametuokoa toka katika dhambi za ulimwengu.
Sehemu ya msingi katika malango ya Hema Takatifu la Kukutania ni nyuzi za bluu. Kwa nini Yesu Kristo kama Masihi alikuja hapa duniani na kufa Msalabani? Ni kwa sababu Yesu alibatizwa. Nyuzi za bluu zinatuonyesha juu ya ubatizo wa Yesu, nyuzi za zambarau zinatueleza kuwa Yesu ni Mfalme, na nyuzi nyekundu zinatueleza juu ya kusulubiwa kwake na kumwaga damu yake. Nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ni vitu vya ujenzi ambavyo ni muhimu sana, ambavyo vinaifanya zawadi ya wokovu ambayo Yesu Kristo ametupatia kwa kuja hapa duniani kama Masihi na kuzichukua dhambi zetu zetu katika mwili wake.
Watu wengi katika ulimwengu huu wanasisitiza kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu tu, na kwamba kimsingi yeye ni Mungu mwenyewe. Lakini Mungu anatueleza wazi kupitia Hema Takatifu la Kukutania kwamba mafundisho ya jinsi hiyo hayawezi kuwa ndio ukweli kamili.
Mtume Petro katika 1 Petro 3:21, “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa nyinyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.”
Hii inatushuhudia sisi kuwa Yesu Kristo aliitimiza ahadi ya wokovu na akaweka msingi wa imani mkamilifu kwa kuupokea ubatizo wake, mfano unaotuokoa sisi. Masihi wetu ni nani? Masihi maana yake ni Mwokozi, neno hili linatueleza kuwa Yesu alikuja hapa duniani, alibatizwa ili kuzichukua dhambi zetu zote na dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake, na kwa kweli alizichukua dhambi zote katika mwili wake kwa ubatizo.
Mungu aliwaeleza waisraeli kulijenga lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania kwa kufuma nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Na dhumuni la Bwana wetu, ambaye ndiye Mfalme wa wafalme na Bwana wa Mbingu, kuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu ilikuwa ni kuutimiza ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safiya kusokotwa. Bwana wetu alikuja katika mwili wa mwanadamu na akaupokea ubatizo ambao ungeitimiza haki yote ya Mungu toka kwa Yohana Mbatizaji, ambaye ni mwakilishi wa wanadamu.
Hii inafanana na sadaka ya kuteketezwa ya Agano la Kale ambayo ilizipokea dhambi za waisraeli ambazo zilipitishwa katika sadaka hiyo kwa kuwekewa mikono na Kuhani Mkuu katika kichwa chake na kwamba mnyama huyu wa sadaka alihukumiwa kwa dhambi hizo akiwa mbadala kwa dhambi za waisraeli waliokosa. Kwa maneno mengine, kama ilivyokuwa kwa sadaka ya kuteketezwa ya Agano la Kale, Yesu alikuja katika Agano Jipya kama sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi za wenye dhambi wote, alibatizwa, alisulubiwa, na kwa hiyo alibeba adhabu yote ya dhambi za ulimwengu. Yesu aliutimiza ukweli wa nyuzi za bluu kwa kubatizwa na Yohana kama Mwanakondoo wa Mungu wa sadaka. Kwa ubatizo huu, Yesu alizichukua dhambi za mwanadamu katika mwili wake mara moja na kwa wote.
Sababu iliyowafanya wakristo wengi kugeuka na kuwa aina fulani ya watu ambao ni waovu hata kushinda watu wa dini nyingine za kidunia ni kwa sababu wamekuwa hawawezi kuufahamu na kuuamini ukweli huu wa nyuzi za bluu, yaani ubatizo wa Yesu, na kwa hiyo hawajapokea ondoleo la dhambi mara moja. Wakati Wakristo wanapokosa ufafanuzi sahihi wa ubatizo huu kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu katika mwili wake, ndipo misingi yao halisi ya imani inaposhindwa kujengeka vizuri tangu awali.
Kwa uhakika, nyuzi za bluu ni mbinu na ukweli ambao kwa huo Masihi alikuja hapa duniani na akazichukua dhambi zetu katika mwili wake. Na nyuzi nyekundu zinamaanisha damu ya Yesu. Sababu iliyomfanya Yesu Kristo akasulubiwa, akamwaga damu yake, na akafa Msalabani ni kwa sababu dhambi zetu zote zilikuwa zimepelekwa kwake kupitia ubatizo. Ni kwa sababu Yesu alizichukua dhambi zetu kwa ubatizo wake alioupokea toka kwa Yohana ndipo alipoweza kufa Msalabani, na ni kwa sababu ya ukweli huu kwamba sadaka yake pale Msalabani kwa ajili yetu haikuishia pasipo maana. Ni kwa sababu Yesu Kristo Masihi alibeba adhabu zetu zote za dhambi kikamilifu kwa ubatizo wake na kwa kusulubiwa ili kwamba aweze kuukamilisha wokovu wetu.
Nyuzi za zambarau zinamaanisha kuwa Yesu Kristo ni Mungu na Mfalme wa wafalme. Ingawa Yesu Kristo ni Mfalme wa wafalme (nyuzi za zambarau), lakini kama asingelibatizwa na Yohana Mbatizaji ambaye ni mwakilishi wa wanadamu, na kama asingelikuwa amezichukua dhambi zetu katika mwili wake (nyuzi za bluu), haijalishi ni kiwango gani cha mateso na maumivu aliyoyapata Msalabani (nyuzi nyekundu), kifo chake kingekuwa hakina maana. Kitani safi ya kusokotwa inatueleza sisi kuwa Neno la unabii ambalo Mungu aliliongea katika Agano la Kale limetimizwa lote katika Agano Jipya.
 


Ukristo wa Leo Umepoteza Maana ya Nyuzi za Bluu

 
Bado kuna mazoea yanayoonekana katika Ukristo wa leo kudharau nyuzi za bluu miongoni mwa zile nyuzi nne na kisha kulitafsiri Neno la Mungu kulingana na matamanio ya mtu mwenyewe—kwa hakika dhambi hii kuu itakuja kuhukumiwa.
Nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa zilizotumika katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania zinatueleza juu ya ukweli wa wokovu, kwamba ili kutuokoa sisi toka katika dhambi zetu, Yesu Kristo Masihi wetu alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, akabatizwa na kusulubiwa. Yesu alizichukua dhambi zetu zote katika mwili wake.
Yesu alizichukuaje dhambi zetu katika mwili wake? Alizichukua kupitia ubatizo alioupokea toka kwa Yohana. Ni kwa kule kuzichukua dhambi zetu katika mwili wake ndiko kulikomfanya Yesu kuwa Mwokozi wa kweli. Hii ndiyo sababu malango ya Hema Takatifu la Kukutania yalifumwa kwa nyuzi hizi nne, kwa kuwa zinatueleza kuwa Yesu, ambaye alikuja hapa duniani alibatizwa, akaimwaga damu yake Msalabani, na kisha akafufuka tena toka kwa wafu, yeye ni Mungu mwenyewe.
Kwa hiyo, lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania lilitengenezwa kwa nyuzi hizi za bluu, zambarau, nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Yesu ni mlango wa wokovu unaotuongoza katika Ufalme wa Mbinguni. Mlango huu ni mlango uliofumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Yesu ni Mwokozi wa wenye dhambi. Ubatizo wa Yesu na kusulubiwa kwake ni zawadi za wokovu ambazo zimewaokoa wenye dhambi toka katika dhambi zao.
Ni kwa sababu Ukristo wa leo umeshindwa kuelewa kiusahihi juu ya ubatizo wa Yesu ndio maana umekuwa hauwezi kukutana na Mungu halisi na badala yake umegeuka kuwa kama zilivyo dini nyingine za ulimwengu huu. Kwa kadri imani yetu inavyohusika, ni lazima tuweke msingi imara wa imani kuhusu ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Msingi huu wa imani ni ukweli kuwa Bwana wetu alikuja hapa duniani na ametuokoa mimi na wewe toka katika dhambi za ulimwengu kwa kupitia nyuzi zake za bluu, zambarau, nyekundu na kitani safi ya kusokotwa.
Yesu alikuja hapa duniani na ameitimiza ahadi ya wokovu ya kwamba ametuokoa sisi toka katika dhambi zetu kwa ubatizo wake na damu ya Msalaba. Kueleza kwa umakini zaidi, Yesu alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, akazichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake kwa kupitia ubatizo wake, alizitakasa dhambi zetu kwa damu yake ya Msalaba, na kwa hiyo alibeba adhabu ya dhambi zetu kwa kufa Msalabani. Huyu Yesu ambaye ametuokoa sisi kwa maji na kwa damu (1 Yohana 5:4-8) kimsingi ndiye Bwana wa uumbaji aliyetuumba sisi, na ndiye aliyetupatia zawadi ya wokovu iliyotuokoa sisi. Huyu Yesu aliyetuokoa toka katika dhambi zetu zote na adhabu amefanyika kuwa Mwokozi wa kweli. Hivi ndivyo ambavyo vifaa vya ujenzi vya Hema Takatifu la Kukutania vinavyotueleza sisi.
Kwa hiyo, ni lazima tuithibitishe imani yetu kikamilifu kwa kuviamini vifaa hivi. Katika kumwamini huyu Yesu ambaye alikuja kama Masihi wetu na Mwokozi wetu halisi, ni lazima tuamini kwa hakika na kwa mioyo yetu yote juu ya ubatizo ambao aliupokea, kwa adhabu zote ambazo alizibeba kwa ajili yetu Msalabani, na kwa ufufuko wake toka kwa wafu. Mwokozi ambaye ametupatia zawadi ya wokovu wetu toka katika dhambi zetu zote kwa kupitia ubatizo wake na damu yake ambayo ameimwaga Msalabani hakuwa ni mtu tu wa kawaida, bali alikuwa ndiye Muumba halisi aliyemuumba mwanadamu na ulimwengu wote. Ni lazima tuikiri imani yetu katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Bila ya ukiri huo wa imani ni jambo lisilothibitika kumwamini Yesu kuwa ni Mwokozi.
Je, umewahi kucheza mchezo wa maneno ya kimyakimya? Mchezo huu huanzia kwa mtu aliyepewa kadi ambayo imeandikwa sentensi fulani. Mtu anaisoma sentensi iliyoandikwa katika kadi kisirisiri, kisha anaielezea hiyo sentensi kimyakimya, ila kwa mgongano wa midomo tu. Kisha mtu anayefuata ambaye yeye hasomi ile kadi bali anaisoma midomo ya yule aliyekuwa anaisoma kadi anampasia mtu wa tatu sentensi hiyo kwa njia ya kuongea kwa kuchezesha midomo bila sauti. Mtu huyu wa tatu anaisoma midomo ya mtu wa pili, na kisha anampasia mtu wa nne kwa njia ile ile hadi mtu wa mwisho anapofikiwa. Kitu kinachozingatiwa katika mchezo huu ni kwa yule mtu wa mwisho kuiongea sentensi ya mwanzo waliyokuwa wakipasiana kwa ufasaha. Sababu inayoufanya mchezo huu kuwa wa kuchekesha ni kwamba mara nyingi ile sentensi ya kwanza huwa inapotoshwa kiurahisi. Kwa mfano, ikiwa mchezo ulianza na sentensi iliyokuwa ikisema, “Iwashe hiyo feni,” baada ya kuwa imepitia kwa watu wachache, basi inaanza kubadilishwa. Mwishowe, mtu wa mwisho anaweza kusema “Mfukuze huyo punda,” akimalizia kwa sentensi tofauti na ile iliyoandikwa na kusemwa hapo mwanzo.
Kama ambavyo mtu huyu wa mwisho anakuja na sentensi ambayo ni tofauti kabisa na ile ya awali, ndivyo Ukristo wa leo ulivyoipoteza imani, kana kwamba umekuwa ukicheza mchezo huu wa maneno wa kimyakimya. Kwa nini iko hivi? Ni kwa sababu Ukristo umeshindwa kuweka msingi wa imani katika imani ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Ukristo wa leo haujaiweka misingi yake katika imani hii ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Wakati msingi wa imani unapositasita, haijalishi kuwa tunamwamini Yesu kwa shauku kubwa, na haijalishi jinsi ambavyo tunayatumia mafundisho yake katika maisha yetu, kwa hakika hatuwezi kufanya mambo haya.
Wakati Bwana alipowaambia Waisraeli kumletea sadaka zao ili kulijenga Hema Takatifu la Kukutania, kwanza aliwaambia kuleta dhahabu, fedha, na shaba, na kisha akawaambia kuleta nyuzi za bluu, zambarau, nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Vifaa hivi vyote vya ujenzi vinatuonyesha kuwa Yesu ametuokoa kupitia ubatizo wake alioupokea toka kwa Yohana, damu yake aliyoimimina Msalabani, na ufufuko wake.
Nyuzi za bluu hazikutumika tu kwa ajili ya malango yote ya Hema Takatifu la Kukutania, pia zilitumika katika vazi ya Kuhani Mkuu na mapazia yaliyoifunika Hema Takatifu la Kukutania. Hii ni injili ambayo inatueleza sisi jinsi ambavyo Bwana wetu alikuja hapa duniani na jinsi ambavyo ametuokoa mimi na wewe kwa hakika toka katika dhambi zetu. Kwa hiyo, injili hii inatueleza jinsi ambavyo vitu hivi vinne vinavyoifanya imani—yaani, nyuzi za bluu, zambarau, nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa—kuwa ni muhimu kwa imani yetu. Hali tukiweka msingi katika Neno hili, sisi sote ni lazima tuuweke msingi wetu wa imani kikamilifu. Ni kwa kufanya hivyo tu ndipo tunapoweza kupokea ondoleo la dhambi, kufanyika watumishi wake ambao wanalieneza neno hili hapa na pale, na Bwana atakaporudi ndipo tutakapokuwa watu wa imani ambao tunaweza kusimama kwa ujasiri mbele za Mungu tukiwa na imani hii.
Ni kweli kuwa nchini Korea, bado kuna unafiki unaochukulia kuwa kila kitu kigeni ni kizuri. Tabia hii ipo miongoni mwa wanatheolojia wa nchi yangu pia, ambao wanaweka matumaini makubwa katika yale ambayo wanatheolojia wa nchi za Magharibi wameyasema, wanayaamini maneno yao kuliko hata Neno la Mungu. Ni lazima wawekwe huru toka katika ujinga huu, na ni lazima waliamini kwa kweli Neno la Mungu, hali wakimwamini na kumtegemea Mungu, kwa kuwa ukweli kuhusu ubatizo wa Bwana wetu, na ukweli kuhusu damu yake, na ukweli kuwa yeye ni Mungu mwenyewe, kimsingi umekuwa ndio mlango wa wokovu wetu.
Kama ambavyo Mtume Petro alikiri, “Wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu anayehai,” (Mathayo 16:16) ikiwa unamwamini Mungu, na ikiwa unaamini kuwa Bwana alikuja hapa duniani kutuokoa toka katika dhambi zetu, basi ni lazima ufahamu na uamini kuwa Bwana alifanyika Mungu wa kweli wa wokovu kwa kuzichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa ubatizo wake, kwa kufa Msalabani, na kwa kufufuka tena toka kwa wafu. Ubatizo wa Bwana wetu na damu ya Msalaba ni misingi ya imani ya kweli inayotuwezesha kupokea zawadi ya wokovu. Ikiwa hatuwezi hata kuiamini imani ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu kulingana na Neno la Mungu, je, tunawezaje kuiita imani hiyo kuwa ni imani ya kweli?
 

Sheria Ni Kivuli Cha Mambo Mazuri Yatakayokuja
 
Vifaa vya ujenzi vya Hema Takatifu la Kukutania vinatuonyesha sisi kuwa Bwana wetu alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, akazichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa ubatizo wake, akabeba adhabu ya dhambi zetu kwa kusulubiwa kwake, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo amefanyika kuwa Mwokozi wetu. Kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, Bwana wetu aliahidi katika Agano la Kale kuwa atatupatia sisi zawadi ya wokovu. Yeye aliyetupatia agano hili si mwingine bali ni Yesu Kristo, Mfalme wa wafalme ambaye alibatizwa na kusulubiwa kwa ajili ya wenye dhambi. Kwa maneno mengine, Mungu huyu, alikuja kwetu kama Mungu Masihi. Kwa hiyo, ni lazima tuuweke msingi wa imani yetu kwa kufahamu na kuamini katika ukweli huu kikamilifu. Kwa kuimini injili ya maji na Roho ni lazima sisi sote tupokee zawadi ya wokovu.
Dhahabu, fedha, na shaba vilikuwa ni vifaa vilivyotumika pia katika ujenzi wa Hema Takatifu la Kukutania. Vifaa hivi vinatueleza juu ya msingi wa imani yetu. Kwa hakika mbele za Mungu tusingeweza kujisaidia zaidi ya kutupwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zetu. Lakini kwa watu kama sisi, Bwana wetu ametupatia zawadi ya wokovu kwetu sisi tunaoamini. Yesu Kristo alibatizwa na Yohana na kusulubiwa kama sadaka ya kuteketezwa ya wanadamu wote, na kwa hiyo ametuokoa sote kikamilifu toka katika dhambi zetu. Hakukuwa na njia ya sisi kuikwepa kuzimu, kwa kuwa tulifahamu kuwa tulikuwa tumefungwa tayari kwa adhabu ya dhambi zetu, na hatukuwa tunafahamu jinsi ambavyo tunaweza kuwa na imani inayozifanya dhambi zetu zote kutoweka. Lakini ndani ya Mungu kulikuwa na zawadi ya wokovu. Kwamba Yesu alikuja hapa duniani, akazipokea dhambi zetu zote katika mwili wake kwa ubatizo wake, akafa Msalabani, na kwamba ametatua matatizo yote ya dhambi zetu na hukumu ya adhabu—hii ni zawadi ya wokovu.
Tunaokolewa toka katika dhambi zetu kwa kupitia imani yetu, kwa kuamini kuwa Mungu ameitimia kazi yake ya wokovu wetu na kuwa ametupatia zawadi ya wokovu. Hii ndiyo sababu Mungu alisema wamletee imani ya dhahabu, fedha, na shaba, kwa kuwa amewaokoa kikamilifu wale ambao wasingeweza kujisaidia bali walistahili kufungwa kuzimu kwa kuwapatia zawadi ya wokovu. Ni kwa sababu Bwana wetu kwa hakika ametuokoa kwa kuja hapa duniani, akizichukua dhambi zetu zote katika mwili wake, na akibeba hukumu yetu kwamba tumeokolewa kikamilifu mbele za Mungu kwa kuiamini zawadi hii ya wokovu.
Yesu Kristo sasa amefanyika kuwa Mwokozi mkamilifu. Hivyo ni lazima tusimame imara katika imani yetu katika zawadi yake ya wokovu, kwa kuwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ni zawadi za imani. Mungu hapendi sisi tuamini kiholela na kwa upofu bila kufahamu kitu chochote.
 

Singa za Mbuzi, Ngozi ya Kondoo Dume Iliyotiwa Rangi Nyekundu, na Ngozi ya Pomboo
Singa za Mbuzi, Ngozi ya Kondoo Dume Iliyotiwa Rangi Nyekundu, na Ngozi ya PombooHivi vilitumika katika kujenga mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania. Paa la kwanza lilifumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ambapo paa la pili la singa za mbuzi lililazwa. Kisha lilifunikwa kwa ngozi ya kondoo dume iliyotiwa rangi nyekundu, na mwisho ngozi pomboo ililazwa juu yake. Kwa njia hii aina nne tofauti za tabaka la paa zililifunika Hema Takatifu la Kukutania.
Paa la mwisho ambalo liliifunika Hema Takatifu la Kukutania lilikuwa la ngozi za pomboo. Kwa hiyo kilichoonekana katika uso wa paa la Hema Takatifu la Kukutania lilikuwa ni hizi ngozi nyeusi za pomboo. Pomboo ni mnyama anayepatikana baharini. Kipimo cha ngozi ya Pomboo ni kama kipimo cha mtu na pengine ni ndogo zaidi kuliko kipimo cha mtu, na aina hii ya ngozi ilikuwa haipitishi maji. Hii ndiyo sababu ngozi ya pomboo ilitumika kama paa kuezekea paa la Hema Takatifu la Kukutania. Kwa sababu ya hili, hali ya nje ya Hema Takatifu la Kukutania haikuwa ya kuvutia, na bila shaka halikuwa na mvuto wa kuangalia. Hii inatueleza sisi kuwa wakati Yesu alipokuwa hapa duniani kwa ajili yetu, kwa hakika alikuja katika hali ya chini kama ilivyokuwa hali ya nje ya Hema Takatifu la Kukutania, hakukuwa na kitu cha kutamanisha katika mwonekano wake.
Ngozi ya kondoo dume iliyotiwa rangi nyekundu inatueleza kuwa Yesu Kristo atakuja hapa duniani na atasulubiwa kwa ajili yetu, ilhali singa za mbuzi zinatueleza kuwa atatuokoa kwa kubatizwa kama sadaka yetu ya kuteketezwa na kwa hiyo atazipokea dhambi zetu katika mwili wake kwa kusulubiwa Msalabani.
Kwa maneno mengine, vifaa vya paa hili la Hema Takatifu la Kukutania, ni misingi ya imani yetu. Kweli hivi ni vifaa vya ujenzi vya imani ambavyo haviwezi kukosekana kamwe. Ili kutupatia zawadi ya wokovu, Yesu Kristo alikuja hapa duniani kama sadaka yetu ya kuteketezwa. Katika Agano la Kale, Mungu alianzisha utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa ili kuziondoa dhambi za waisraeli: Wanyama wa sadaka ya kuteketezwa wasio na mawaa (mbuzi, wanakondoo, na mafahali) walizipokea dhambi za waisraeli ambazo zilipitishwa kwao kwa kuiweka mikono yao juu ya vichwa vya wanyama hao, na wanyama hao waliuawa badala yao, walizimwaga damu zao na wakachomwa, na kwa jinsi hiyo waliwaokoa toka katika dhambi zao zote.
Yesu Kristo alikuja hapa duniani kama mwanakondoo wa sadaka na alizipokea dhambi zetu katika mwili wake kwa kupitia ubatizo wake, ambao ni ishara ya kuwekewa mikono. Kama ambavyo mwanasadaka wa kuteketezwa aliuawa kwa kuimwaga damu yake na kuchomwa katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa kuzipokea dhambi za waisraeli kwa kuwekewa mikono, vivyo hivyo, Yesu Kristo anabeba adhabu zote za dhambi zetu kwa kubatizwa na kufa Msalabani, na kwa hiyo ametuokoa toka katika dhambi za ulimwengu.
Kama ambavyo majina katika kitabu cha hukumu yalivyofutwa kwa kuiweka damu ya mwanasadaka wa kuteketezwa katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, ndivyo ambavyo Yesu alibatizwa na kuimwaga damu yake akautimiza upatanisho wetu wa milele kwa damu yake na kwa jinsi hiyo amezifuta dhambi zote za ulimwengu. Kama hivi, vifaa vyote vya Hema Takatifu la Kukutania vinatueleza juu ya Yesu Kristo na huduma zake, vinatueleza kuwa ametuokoa toka katika dhambi za ulimwengu. Toka katika Agano la Kale hadi katika Agano Jipya, Neno la kuwa Yesu ametuokoa toka katika dhambi zetu ndio ukweli kamili, lilikuwa halina makosa yoyote yale.
Wakristo wengi wa siku hizi hawaamini kuwa Yesu Kristo alikuja hapa duniani kama sadaka yetu ya kuteketezwa na kuwa alizichukua dhambi zetu katima mwili wake kwa ubatizo wake, bali wanaamini pasipo shida juu ya kifo chake Msalabani. Imani ya Kikristo ya jinsi hiyo ni ile isiyo na sheria ya ua wa lango la Hema Takatifu la Kukutania iliyofumwa kwa nyuzi nyekundu na za rangi ya zambarau tu hali nyuzi za bluu zikiwa zimeachwa. Wanayo imani yenye makosa ambayo haioni umuhimu wa paa lililoundwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, na kwamba badala yake wanaamini kuwa wanachohitaji ni paa la ngozi ya kondoo waume zenye rangi nyekundu na ngozi za Pomboo.
Tunapoiangalia michoro mingi ya Hema Takatifu la Kukutania inayochorwa katika dunia nzima, mingi kati ya hiyo ni ile ambayo inatuwia vigumu kuzipata nyuzi za bluu. Hii ni kwa sababu watu waliochora picha hizi ni wale ambao hawaifahamu injili ya maji na Roho; lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania katika michoro yao limefunikwa lote kwa rangi nyekundu na nyeupe. Lakini imani ya jinsi hiyo haiwezi kuwa imani sahihi mbele za Mungu.
Nyuzi ambazo zilitumika sana katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania zilikuwa ni nyuzi za bluu, zikifuatiwa na nyuzi za zambarau, kisha zikifuatiwa na nyuzi nyekundu na mwisho zikifuatiwa na nyuzi nyeupe. Kwa hiyo, unapoliangalia lango la ua, rangi hizo zote ni lazima zionekane mara moja. Lakini kwa sababu kuna watu wengi sana katika ulimwengu huu ambao imani yao haina ufahamu wowote kuhusu ubatizo wa Yesu, mara nyingi wamezidharau rangi nne za nyuzi zilizotumika katika Hema Takatifu la Kukutania na badala yake wameyajenga malango yao ya Hema Takatifu la Kukutania kwa nyuzi mbili tu.
Kwa kufanya hivyo wanawadanganya watu wengi, ambao tayari hawana uelewa wa kutosha kuhusu Mungu na ambao hawalijui kabisa Neno lake. Hawa wote ni manabii wa uongo. Yesu mwenyewe aliwahi kuwazungumzia watu wa jinsi hii kuwa ni magugu ambayo Shetani aliyapanda katikati ya ngano (Mathayo 13:25). Kwa maneno mengine, wamekuwa ni watu ambao wanaeneza uongo kwa kuacha nyuzi za bluu katika michoro yao ya ua wa Hema Takatifu la Kukutania. Hii ndiyo sababu watu wengi sana wanabakia ni wenye dhambi hata baada ya kuwa wanamwamini Yesu. Pamoja na imani yao katika Yesu bado wamefungwa katika uharibu kwa sababu ya dhambi zao.
Msingi wetu wa imani ni lazima uwe imara. Kuna uzuri gani kuishi kipindi kirefu cha maisha ya kidini katika nafsi yako ilhali maisha hayo yapo katika msingi usio wa sheria kiimani? Imani potofu inaweza na itavunjika mara moja baada ya tangazo. Haijalishi kuwa nyumba zetu ni nzuri kiasi gani, kutakuwa na uzuri gani ikiwa tunajenga nyumba hizi katika msingi dhaifu wa kiimani? Bila kujali jinsi ambavyo umemtumikia Mungu kwa juhudi, ikiwa msingi wako wa imani una dosari, basi utakuwa umeijenga nyumba yako katika mchanga; dhoruba itakapokuja na upepo kuvuma, na mafuriko yakaja, yataipiga nyumba yako nayo itaanguka chini mara moja.
Je, ni vipi kuhusu imani ya ambao msingi wao ni imara? Haitaanguka chini kamwe, hata ikitikiswa kiasi gani haitaanguka chini. Mungu alituambia sisi kuwa nyumba iliyojengwa katika mwamba wa ukweli uliofumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa haitaanguka chini kamwe. Na kwa kweli hivi ndivyo ilivyo. Je, imani ya mwamba ni nini? Ni imani inayoamini katika ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Imani ya watu waliojenga nyumba za jinsi hiyo za kiimani hazitaanguka kamwe. Na hii ndiyo sababu ni muhimu kwa imani yetu kuwa na msingi imara. Ikiwa hatuamini hata bila ya kufahamu vizuri yale ambayo Bwana ameyafanya kwa ajili yetu, basi imani ya jinsi hiyo itageuka kuwa imani ya dini za uongo isiyotakiwa na Mungu.
 

Mti wa Mshita, Mafuta, na Viungo
 
Nguzo za Hema Takatifu la Kukutania, madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na mbao na vifaa vingine vya Madhabahu vyote vilitengenezwa kwa mbao za mti wa Mshita. Kwa kawaida mti katika Biblia unamaanisha wanadamu (Waamuzi 9:8-15, Marko 8:24). Pia mti hapa unamaanisha kwetu juu ya asili ya mwanadamu; ile hali ya kuwa mti huu wa mshita ulitumika katika nguzo, katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na katika Hema Takatifu la Kukutania lenyewe inatueleza kuwa kama ambavyo mizizi ya mti wa mshita mara zote imefunikwa ardhini, basi asili yetu ni ile ambayo haiwezi kujisaidia bali kutenda dhambi wakati wote. Ni lazima watu wote wakiri kuwa hawawezi kujisaidia bali wataendelea kuwa wasio na haki na kutenda dhambi kila mara.
Kwa wakati huo huo, mti wa mshita pia unamaanisha juu ya ubinadamu wa Yesu Kristo. Masihi aliyekuja katika mwili wa mwanadamu alibeba dhambi zote za ulimwengu, na alihukumiwa kwa haki kwa ajili ya mwanadamu. Yeye ni Mungu mwenyewe, na kwa hiyo, sanduku la ushuhuda, meza ya mkate wa wonyesho, madhabahu ya uvumba, na mbao za Hema Takatifu la Kukutania vyote vilitengenezwa kwa mti wa mshita na vikafunikizwa kwa dhahabu safi.
Mafuta kwa ajili ya mwanga na manukato kwa ajili ya mafuta ya kupaka na kuwekea wakfu na kwa uvumba wa manukato vinamaanisha juu ya imani yetu ambayo tunaitoa kwa Yesu Kristo. Yesu Kristo ni Masihi aliyetuokoa mimi na wewe. Maana ya jina “Yesu” ni “yeye atakayewaokoa watu wake toka katika dhambi zao,” na jina “Kristo” lina maana ya “mtiwa mafuta,” hivyo, majina haya yanatueleza sisi kuwa Yesu Kristo ni Mungu mwenyewe na Kuhani Mkuu wa Mbinguni aliyetuokoa sisi. Ili kuheshimu mapenzi ya Mungu, Bwana wetu alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, alibatizwa, alisulubiwa Msalabani kwa ajili yetu, na kwa hiyo ametupatia zawadi ya wokovu. Kwa hakika jukumu la Kuhani Mkuu lililochukuliwa na Yesu aliyetupatia wokovu wetu lilikuwa ndio kazi nzuri sana.
 

Vito vya Shohamu, na Vito Vingine vya Kuwekwa Katika Naivera na Katika kile Kifuko cha Kifuani cha Kuhani Mkuu
 
Vito kumi na mbili vya aina tofauti vimetajwa hapa ambavyo vitawekwa katika naivera na katika kifuko cha kifuani cha Kuhani Mkuu. Kuhani Mkuu alivaa kwanza gwanda kama kanzu fupi, kisha akavaa joho la bluu, na kisha akavaa naivera juu ya joho. Kisha, kifuko cha kifuani kiliwekwa katika naivera ambayo ilivaliwa wakati wa sherehe maalum ya sadaka ya kuteketezwa, na katika kifuko hiki cha kifuani viliwekwa vito kumi na mbili vya thamani. Hii inatuonyesha sisi kuwa jukumu la Kuhani Mkuu lilikuwa ni kuwakumbatia na kuwajumuisha watu wa Israeli pamoja na watu wengine wa ulimwengu mzima katika kifua chake, kwenda mbele za Mungu, na kumtolea Mungu sadaka zao za kuteketezwa.
Yesu, ambaye ni Kuhani Mkuu wa milele wa Mbinguni pia aliyakumbatia mataifa yote ya ulimwengu katika kifua chake, akautoa mwili wake mwenyewe ili kuzichukua dhambi zetu kwa ubatizo wake na akasulubiwa kwa ajili yetu, na kwa hiyo amewaweka wakfu watu wake kwa Mungu Baba. Vito vya thamani kumi na mbili vilivyowekwa katika kifuko cha kifuani vinamaana ya mataifa yote ya ulimwengu huu, na Kuhani Mkuu aliyevivaa vito hivyo ni alama ya Yesu Kristo ambaye amewaokoa mataifa na kuyakumbatia mataifa yote ya ulimwengu katika kifua chake.
Hivyo, hizi zilikuwa ni sadaka ambazo Mungu wetu aliwaambia waisreli kumtolea ili kulijenga Hema Takatifu la Kukutania kwa ajili yake. Kuna maana ya kiroho katika ukweli kuwa Mungu aliwaambia waisraeli kumjengea Hema Takatifu la Kukutania, mahali ambapo Mungu angeishi, kwa sadaka zao. Mara nyingi watu wa Israeli walibakia ni wenye dhambi kwa sababu hawakuweza kuitunza na kuifuata Sheria ambayo Mungu aliwapatia. Hii ndiyo sababu Mungu aliwaeleza kupitia Musa kulijenga Hema Takatifu la Kukutania na akawapatia utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa, ambayo kwa hiyo ondoleo la dhambi lilitolewa kwa sadaka ya kuteketezwa iliyotolewa katika Hema Takatifu la Kukutania. Kwa maneno mengine, Mungu alizifuta dhambi zote za waisraeli kwa kuzipokea sadaka zao, kwa kutumia sadaka hizi kuijenga nyumba yake, na kwa kuwafanya kumtolea sadaka zao za kuteketezwa katika Hema Takatifu la Kukutania kwa mujibu wa kanuni za utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa. Hivyo ndivyo ambavyo Mungu angeliweza kuishi katika Hema Takatifu la Kukutania pamoja na watu wa Israeli.
Hata hivyo, kuna wakristo wengi mno katika dunia hii ambao hawaziamini nyuzi za bluu, zambarau, nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Wakati Mungu alipowaambia kumletea dhahabu, fedha, na shaba, kwa nini hawauamini ukweli unaonyeshwa katika sadaka hizi?
Je, sisi hatukuwa tumefungwa kwenda kuzimu kwa sababu ya dhambi zetu? Je, umeuamini Ukristo kana kwamba ni moja kati ya dini nyingi za ulimwengu huu kwa sababu hujakiri wewe mwenyewe kuwa ulistahili kufungwa kuzimu? Ikiwa hivi ndivyo ulivyokuwa ukiamini hadi sasa, basi ni lazima utubu na urudi katika imani ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Na ni lazima utambue kuwa mbele ya sheria kali za Mungu wewe ni lundo la dhambi, na kwamba umefungwa kuzimu kwa sababu ya dhambi hizi, na ni lazima uamini katika injili ya maji na Roho.
Sasa, ni lazima uiamini injili ya kweli kwamba hata pale ulipofungwa kuzimu, Bwana wetu bila kujali alikuja hapa duniani kama Masihi, akazipokea dhambi zako katika mwili wake kwa ubatizo wake, akazibeba dhambi hizi Msalabani, na akasulubiwa kwa kuimwaga damu yake Msalabani na kwa hiyo ametuokoa mimi na wewe toka katika dhambi zetu na adhabu. Bila kuiamini injili ya maji na Roho iliyodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, hatuwezi kuuweka msingi wetu wa imani kikamilifu.
 

Ni Lazima Tufikiri Juu ya Msingi Wetu wa Imani
 
Mungu anatueleza sisi tuwe na imani ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu; ni lazima tujiulize sisi wenyewe ikiwa kweli tunayo imani hii ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, au kama tunauamini ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za zambarau na nyekundu tu hali tukiziacha nyuzi za bluu.
Tunahitaji kujiangalia sisi wenyewe ikiwa tunampelekea Mungu imani potofu ambayo inatufaa sisi tu katika radha zetu binafsi. Wakati Mungu anatueleza kumletea nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, je tunampatia Mungu nyuzi hizo? Au tunampatia nyuzi nyeusi za nailoni? “Mungu, nyuzi ulizozihitaji zinaonekana kuwa hazifai kwa Hema Takatifu la Kukutania. Zitaoza na kuharibika na mvua. Na pia ni jambo la linalochosha kuzitafuta na kuzileta hadi hapa. Badala yake zijaribu nyuzi hizi za nailoni. Ninakuhakikishia kuwa nyuzi hizi za nailoni zitadumu kwa takribani miaka 50 na pengine hata miaka 100 ikiwa utazilinda vizuri. Pia hata kama utazizika ardhini, haziwezi kuoza kwa miaka zaidi ya 200. Je hili si jambo zuri la kushangaza?”
Je, hivi si ndivyo tunavyomwambia Mungu? Ni lazima pia tujiangalie sisi wenyewe vizuri ikiwa hatuichukui aina hii ya imani ya kujihusudu na ya kishirikina kwa Mungu. Na ikiwa tumewahi kuwa na imani kama hiyo ni lazima tutubu tangu sasa, kwa maneno mengine ni lazima tugeuke.
Kuna watu wengi miongoni mwetu wanajifikiria wao wenyewe kuwa ni Wakristo wazuri, lakini unapowachunguza kwa karibu, unaona kuwa ufahamu wao ni wa kimakosa na kwa hiyo imani yao pia ni yenye makosa.
 

Fumbo la Siri Lililomo Katika Ukristo wa Leo
 
Fumbo la siri ndilo ambalo kwa kawaida wakristo wanaliamini zaidi. Watu hawa hawafahamu jinsi ambavyo Neno la Mungu linasema kwa hakika. Kwa sababu hawalifahamu Neno la ukweli ambalo Masihi amewapatia, wanamwamini na kumfuata Bwana kulingana na misisimko na hisia zao binafsi. Na wanashawishika kwamba hisia za jinsi hiyo ni za kweli. Kwa sababu wanamuomba Mungu kwa juhudi, na kwa kuwa wanaifuata misisimko na hisia zao wanazozipata katika maombi kwa uaminifu wanashindwa kutofautisha juu ya ipi ni imani hasa ya kweli.
Kama hivyo, kumwamini Mungu kwa mujibu wa hisia na misisimko ya mtu binafsi ambayo inazunguka katika mawazo ya mtu ndiyo imani ya fumbo la siri. Watu wanaomwamini Mungu hali wakiongozwa na hisia wanazozipata wanapofunga, wanaposifu, wanapoamini, wanapotoa sala ya asubuhi na mapema, wanapopanda mlimani kusali, wanapofanya dhambi, wanapotoa maombi ya toba, na kadhalika—watu hawa wote ni wale wanaolifuata fumbo la siri. Kwa maneno mengine, kuishi maisha ya imani kwa kushikilia hisia za mtu fulani si imani ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu ambayo Masihi aliieleza.
Pengine karibu ya asilimia 99.9 ya wakristo wa leo waliwahi katika historia kuwa washiriki wa fumbo la siri. Kwa maneno mengine, itakuwa sio uvumishi tukisema kuwa karibu eneo zima la ukristo, ukiliacha Kanisa la Mwanzo, kuwa limekuwa likifuata imani hii ya fumbo la siri. Wale wasio na imani ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu wanadanganyika katika fikra kuwa, kwa sehemu, hisia zao binafsi ni sehemu ya imani yao. Wanadai kuwa wamemuona na kukutana na Mungu katika maombi yao, na wanatueleza sisi jinsi inavyopendeza na jinsi wanavyojisikia kila wakati wanaposifu.
Wanasema, “Tulikusanyika katika eneo la kusifu, na tukaiinua mikono yetu kwa pamoja na tukazitubia dhambi zetu. Tuliushikilia Msalaba na kisha tukafanya taratibu fulani za kiibada chini ya huo Msalaba, na kisha mioyo yetu iliwaka, na ndipo Kristo alipoonekana kwa upendo. Tulijisikia shukrani nyingi sana katika mioyo yetu kwa damu ambayo Kristo aliimwaga. Tuliamini kwa juhudi sana kwamba Bwana ameziosha dhambi zetu, na ndio maana twatambua kuwa aliimwaga damu yake. Kwa kweli tuliupenda uzoefu ule wote.” Lakini siku moja hisia zao zinaposhuka na kudidimia, wanasema, “Lakini hisia zile zote zimekauka, na bado tuna dhambi katika mioyo yetu.” Imani ya jinsi hii ndiyo imani ya fumbo la siri.
Bila kujali tofauti za dhehebu la mtu au kikundi chake cha kidini, kila Mkristo anahitaji imani inayoamini katika ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Imani ya hao wote ambao hawana imani hii ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu ambayo Mungu aliieleza ni wanamatambiko na washirikina. Watu hawa hawampatii Mungu imani ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, bali wanampatia Mungu imani ya nyuzi za nailoni. Kwa maneno mengine, wanamletea Mungu imani yao ya matambiko kitu ambacho kimeshindwa mbali kabisa, kitu ambacho Mungu haangalii kabisa.
Je, umewahi kuziona kamba nyembamba ambazo zinatumika kufungia boti katika nanga? Wanamatambiko watafurahia kumpatia Mungu aina hii ya kifaa. Wakati Bwana wetu ametueleza kumletea nyuzi za bluu, zambarau, nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, baadhi ya watu wengine wanamletea Mungu kamba hii nyembamba hali wakimwambia, “Bwana, pokea imani hii!” Na baadhi ya watu wanampelekea Mungu hata minyororo ya chuma inayotumika kufungia meli kubwa katika nanga kubwa za bandarini. Baada ya kuwa wameliviringisha burungutu kubwa la minyororo hii ya chuma, wanakwenda kumwekea Bwana miguuni pake hali wakimuomba alipokee burungutu hilo.
Lakini Mungu ametueleza sisi kumletea imani ya nyuzi za bluu, zambarau na nyekundu. Hajatueleza kumletea minyororo ya chuma. Lakini bado watu wengi wanampelekea Mungu kile kinachoonekana kuwa bora katika macho yao wenyewe au kile ambacho kinapatikana kwa urahisi. Ingawa kuna watu wanaomwendea Mungu wakiwa na minyororo ya chuma, kamba, nyuzi za nailoni, au hata aina ya mizizi ya chakula itokanayo na mizabibu, lakini kwa kweli Mungu anapokea nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu tu. Mungu ameshapanga kuwa imani pekee ambayo ataipokea ni imani ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Kwa hiyo, ni lazima tuichukue imani hii ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu kwenda mbele za Mungu.
 

Masihi Hapokei Kila Sadaka Yoyote
 
Pia waisraeli walitakiwa kumpelekea Mungu dhahabu, fedha, shaba, na vito kumi na mbili vya thamani kwa ajili ya kuwekwa katika naivera na kile kifuko cha kifuani. Hata hivyo kuna baadhi ya watu ambao wanampelekea Mungu chuma. Je, Yesu anafanya kazi ya kukarabati vitu vilivyotumika, kana kwamba atapokea kila aina ya vitu? Kwa kweli sio kweli!
Yesu si kama mtu anayepokea kila aina ya uchafu. Yeye hajihusishi na kazi ya kukarabati vitu vichakavu, akichukua kila kitu kisicho na maana ambacho unamletea. Yesu ni Masihi ambaye anapenda kuturithisha sisi rehema yake ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu inayotusamehe dhambi zetu, naye anapenda kutupatia upendo wake wa kweli. Hii ndiyo maana Yesu anaitwa kuwa ni Mfalme wa upendo. Kwa kweli Mchungaji wetu ni Mfalme wa upendo. Kwa kweli Yesu ni Masihi wa kweli. Masihi huyu ameiratibu imani ambayo anaitaka kutoka kwetu sisi hali akielezea baadhi ya tabia ambazo zinahitajika. Ni pale tu tunapomwendea Mungu kwa imani hii, ndipo atakapotupatia kile alichotuahidi.
Lakini bado tunaona kuwa miongoni mwa wale ambao imani yao katika Masihi imejengwa katika ufahamu wao potofu, wapo baadhi ambao ugumu wao mioyo hauwezi hata kuelezewa. Kwa kweli ni waovu na wenye dhambi kama vile Farao ambaye alisisitiza njia zake za ukaidi mbele za Mungu. Wakati Musa alipomwambia, “Yehova amejifunua yeye mwenyewe; waruhusu watu wake waende,” Farao alimaka, “Huyu Yehova ni nani?”
Wakati uwepo wa Mungu ulipoelezwa kwake bila shaka ingekuwa vizuri kwake kujisalimisha na kujinyenyekeza mbele za Mungu baada ya kutafakari faida na hasara ya ukaidi wake. Ikiwa angeendelea kabisa kutoamini na akaendelea na ugumu wake wa moyo, angejaribu kushikilia msimamo wake kwa muda, lakini baada ya mapigo kadhaa alipaswa kuacha ukaidi wake. Ni upambavu kiasi gani ambao Farao aliufanya kwa kung’ang’ania ugumu na ukaidi na kutotii Neno la Mungu hata pale alipopata pigo la vyura kulifunika taifa lake lote?
Sio vyura tu, bali hata chawa waliipiga Kasri ya Farao. Kulia na kushoto, mahali popote alipogeukia mtu, kila mahali katika nchi ya Misri ilijazwa na chawa, hata hivyo Farao hakusalimu amri. Je, inawezekanaje kwa mtu kuishi ikiwa kila mahali pamejaa chawa? Katika hali hii, alipaswa kutambua, “Kwa kuwa sijamtii Mungu, sasa ananionyesha jinsi alivyo Mfalme. Ninaweza kuwa mfalme wa dola yangu katika ulimwengu huu lakini siwezi kulinganishwa naye. Ingawa mimi ni mfalme wa taifa kubwa kuliko yote katika uso wa dunia hii, na japokuwa nina nguvu juu ya ulimwengu wote, Mungu ana nguvu zaidi kuliko mimi nilivyo, na ananiletea mapigo haya kwa sababu ya kutotii kwangu.” Hivi ndivyo alivyopaswa kusalimu amri.
Jambo la busara ambalo Farao angelifanya lilikuwa ni kusalimu amri baada ya kuona gharama ya kupinga kwake. Bila kujali jinsi ambavyo Farao alikuwa na nguvu, kama alifikia hitimisho kuwa hakukuwa na nguvu ya yeye kumpinga Mungu, jambo kubwa ambalo angelifanya lilikuwa ni kusalimu amri mbele za Mungu, na kusema, “Sawa, Mungu, Unastahili kuchukua nafasi ya kwanza; na mimi nitachukua nafasi ya pili” Lakini kwa sababu Farao alikataa kukiri hivyo, taifa lake lote na watu wake wote walipatwa na pigo la chawa.
Kwa sababu ya hili, hakuna Mmisri aliyeweza kufanya jambo lolote. Wakati kila mmoja alipokuwa akiteswa na chawa, ingeliwezekanaje kwa mtu kufanya jambo lolote zaidi ya kuwakwepa chawa? Sisi sote tunaweza kuwafikiria hawa wamisri maskini wakikimbia huku na huko wakijaribu kuwakwepa chawa, bila shaka baadhi yao wanaweza kuwa walizichoma hata nyumba zao katika harakati ya kuwapiga vita chawa, na bila shaka harufu ya chawa walioungua ilienea katika vijiji vyote.
Kuna vitu ambavyo mwanadamu anaweza kufanya, na kuna vitu ambavyo mwanadamu hawezi kuvifanya. Kwa sababu Mungu ni Bwana wa Majeshi, ni Mungu anayetawala juu ya maisha na kifo, furaha na huzuni, na baraka na laana. Hali inapokuwa kama hii, badala ya kujiamini sisi wenyewe kusimama kinyume na Mungu, ni lazima sisi sote tufikirie kwa akili na tufikie hitimisho lenye maana la kuundoa ugumu na ukaidi wetu. Miongoni mwetu sisi wenyewe, tunaweza kusisitiza katika njia ya mtu mmoja na kujaribu kuwa juu ya wengine, lakini tunaposhughulika na Masihi, hatustahili kufanya hivyo.
Ni lazima tufikiri kuwa sisi ni aina gani ya watu mbele za Mungu. Ni lazima tutafakari kwa makini ikiwa tutasimama kinyume na Mungu au ikiwa mioyo yetu itakuwa ni ya upole na unyenyekevu. Na ni lazima tufikie hitimisho kamili kwamba ni lazima sisi sote tuwe wanyenyekevu mbele za Mungu. Mbele za watu, tunaweza kushikilia ugumu na ukaidi wetu na kisha tukakutana na matokeo yake, lakini mbele za Mungu, mioyo yetu ni lazima iwe na unyenyekevu.
“Mungu nimefanya makosa”—wale wanaokiri kama hivi ndio waliochagua njia sahihi. Hawa ni watu ambao wanaweza kuokolewa toka katika maisha yao yenye tuhuma. Kwa wale ambao wamemwacha Mungu kwa sababu ya dhambi zao, njia itakayowafanya wakumbatiwe katika mikono ya Mungu na kuyanywa maji yake ya uzima ni kwa kuzaliwa upya kwa maji na kwa Roho. Je, tunaweza kutarajia nini toka katika miili yetu, wakati maisha yetu yametumika vibaya bila matunda katika jangwa la dunia hii, miili inayoelea ikiizungusha ardhi kavu isiyo na kitu pasipo lengo lolote, miili hii ambayo itairudia mavumbi?
Njia pekee kwetu ili tuweze kuokolewa, sisi ambao tutarudi mavumbini na ambao tumefungwa tayari kutupwa katika ziwa la moto, ni kwa kuiamini injili ya maji na Roho na kwa hiyo tutapokea ondoleo la dhambi zetu. Hii ni kwa ajili ya watu wenye maisha yaliyokata tamaa na yasiyo na matumaini ambao walikwisha pangiwa uharibifu wa milele kwa sababu ya kusimama kinyume na Mungu; na kwa ajili ya dhambi zao ili ziweze kufufuliwa kimiujiza mbele za Mungu kwa kupitia upendo wake wa rehema, upendo wa wokovu. Kwa hiyo, ni lazima sisi sote tujivike wokovu.
Je, inawezekanaje kwa mtu yeyote ambaye ana mwili wa kuharibika akadiriki kumpa changamoto Mungu? Wakati Mungu anapotueleza kuleta sadaka kama hizo, ni lazima sisi sote tulitii Neno lake. Tukikiangalia kifungu kikuu hapo juu, ambapo Mungu anatueleza aina ya sadaka ambazo tunapaswa kumletea, ni lazima sisi sote tutambue kuwa, “Aha, kwa hiyo hii ndiyo imani ambayo Mungu anataka tumletee.”
Katika kile kifuko cha kifuani cha Kuhani Mkuu, kuliwekwa vito kumi na mbili vya thamani. Na chini ya kifuko hicho cha kifuani cha hukumu, kuliwekwa Urim na Thumim, maneno ambayo yana maanisha Mwanga na Ukamilifu, Urim na Thumim viliwekwa ili Kuhani Mkuu aweze kubeba hukumu sahihi juu ya wana wa Israeli.
Hii inaonyesha kuwa ni watumishi wa Mungu tu ndio ambao wanaweza kupitisha hukumu ya haki kwa watoto wao wa kiroho wa imani kwa kuwamulikia mwanga wa Roho Mtakatifu anayeishi ndani yao na Neno la Mungu.
Ni lazima tutambue sasa kuwa mbele za Mungu, ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu ni ukweli halisi na wokovu halisi. Ukweli huu wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu ni wokovu wa kweli unaotuletea uzima, na nje ya ukweli huu hakuna kitu kingine chochote kinachounda wokovu wetu. Haya yote yamejikita katika Neno la Mungu la wazi na la kweli.
 


Vifaa Vyote vya Hema Takatifu la Kukutania Vinahusianishwa na Wokovu wa Mwanadamu Toka Katika Dhambi

ubatizo wa YesuMsalaba
Lakini katika hali ya ujinga, bado watu wanakataa kwa ukaidi. Je, ni kitu gani kitatokea kwao? Hawataweza kamwe kuokolewa. Ni lazima tuundoe ujinga wetu mbele za Mungu. Pia ni lazima tuisafishe mioyo yetu. Ni lazima tuziache mbali fikra zetu binafsi na ukaidi mbele za Mungu, na badala yake tulitii Neno lake na tumpatie Mungu mioyo yetu. Ni lazima tusisimame kinyume na Mungu hali tukisisitiza njia zetu binafsi za ukaidi. Tunaweza kufanya hivyo mbele ya watu wengine, lakini kama Wakristo, hatuwezi kufanya hivi hasa mbele za Mungu. Lakini bado watu wajinga wanasimama kinyume na Mungu na wanakuwa wanyenyekevu mbele za watu wengine. Hili ndilo kosa walilonalo. Ni lazima tuziinamishe nyuso zetu chini mbele za Mungu na tukiri kwamba yale ambayo Mungu ametueleza ni sahihi.
Na ni lazima tuliamini Neno la nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Imani ni kuliamini Neno la Mungu. Tunapojiangusha chini ya miguu ya Mungu, tukatubu shida zetu zote mbele zake, na tukamng’ang’ania tukiomba msaada, kwa hakika Mungu atatujibu. Kisha ni lazima tupokee lile ambalo amelifanya kwa ajili yetu kwa shukrani. Hii ndiyo imani jinsi ilivyo. Ni kwa upuuzi na wazimu gani, kwamba tunaweza kumwonyesha Mungu kitu kingine zaidi ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, yaani tukimletea Mungu kamba za kuvulia samaki na minyororo ya chuma? Kuleta nyuzi zingine zisizo na maana mbele za Mungu na kusema, “Hii ni imani yangu binafsi. Hivi ndivyo nilivyoamini kwa nguvu sana. Hii ni imani imara ambayo nimeihifadhi kipekee,”—kwa kweli hii si imani bali ni kufanya ujinga binafsi mbele za Mungu.
Mtu ni lazima aache ugumu na ukaidi wake mbele ya Masihi. Kwa maneno mengine, mtu ni lazima ainamishe matakwa yake mbele za Mungu. Ni lazima sisi sote tujitambue mbele za Mungu. Ni lazima tutambue kwa kadri ambavyo Mungu anasema nasi na kutuamulia. Hakuna imani nyingine kwa wakristo iliyosahihi zaidi ya hii. Kutii na kuamini kulingana na Neno la Mungu ndiyo msimamo sahihi na moyo wa mtu mwaminifu. Hili ndilo tunapaswa kulitunza katika fikra zetu mbele za Mungu.
Kwa kweli miongoni mwetu tunaweza kujisifu kwa mafanikio ya mtu binafsi, tunaweza kujilinganisha, kushindana, na kupeana changamoto. Japokuwa jambo hili ni tendo lisilo na maana mbele za Mungu, jambo hili ni kitu ambacho tunajikuta tukikifanya mara zote.
Hata mbwa na paka wanawafahamu mabwana zao, na wanawatii na kuwanyenyekea. Kwa maneno mengine, hata mbwa wanawatii wamiliki wao, wanazitambua sauti zao, na wanawafuata mabwana zao tu. Wakati mbwa wanapokaripiwa na mabwana zao mara zote wanayatambua makosa yao, wanaviinamisha vichwa vyao kwa unyenyekevu, na wanajitahidi kurudia hali nzuri ya nidhamu wakifanya mambo mazuri madogomadogo. Wakati hata wanyama wanafanya hivi, inashangaza kuona watu wanaendelea kumpa Mungu changamoto kwa kumpelekea imani inayotokana na mawazo yao binafsi. Kwa maneno mengine, wanaendelea kumng’ang’ania Mungu hata pale wanapoendelea kusisitiza juu ya njia zao binafsi na mawazo yao binafsi.
Kwa nyuzi zake za bluu, zambarau na nyekundu, Mungu amezifanya dhambi zote za mwanadamu kutoweka, na alichotuambia sisi ni kuwa na imani inayoziamini kazi za Bwana wetu. Lakini bado watu wanaendelea kukaidi na kumpa Mungu changamoto.
Bwana ametueleza sisi kumpelekea dhambi zetu zote, na kwa kule kuzifanya dhambi kutoweka kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, Mungu ametupatia ondoleo la dhambi. Wakati Mungu ametueleza kumletea imani ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, bado watu hawaliamini jambo hili, na kwa hiyo wanadharau na kumchafua Bwana wao. Watu hawa watalaaniwa.
Wanapomletea Masihi imani ambayo haitaki na haitarajii toka kwao, Masihi anaweza kukasirika. Wanaendelea kuuleta ugumu na ukaidi wao mbele za Mungu na kusema, “Nimeitunza imani yangu kiasi hiki na kwa ubora huu. Nipe alama ya safi sana kwa kazi!” Je, Mungu atawapatia alama nzuri kwa sababu ya kuitunza imani yao binafsi ilhali imani hiyo imekuwa haina maana kwa kipindi hicho chote?
Inawezekana kukawa na nyakati ambapo ugumu na ukaidi ukawa unahitajika katika maisha yetu. Lakini ukaidi wa imani potofu ni kitu kisichofaa kabisa mbele za Mungu. Mungu alitumia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu ili kuzifanya dhambi zetu kutoweka. Biblia haisemi kuwa alitumia nyuzi za zambarau pekee au kwamba alitumia nyuzi nyekundu tu, au hata kuwa alitumia minyororo ya chuma au nyuzi za nailoni. Ndani ya nyumba ya Mungu, na ndani ya sheria yake ya wokovu tuliyopewa sisi, Masihi anahitaji toka kwetu imani ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu.
Wakristo wanachukuliwa kuwa ni wale wanaomwamini na kumfuata Yesu Kristo. Hivyo, sisi nasi ni Wakristo. Hata hivyo, kuna watu wengi sana ambao pamoja na kuwa wanamwamini Yesu kuwa ni mwokozi wao, bado hawajazaliwa upya, hawajapokea ondoleo la dhambi, na hawana imani ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu—hawa ni wakristo wa mazoea tu ambao sehemu yao ni kuzimu kwa sababu wanaamini kwa mujibu wa njia zao wenyewe. Mungu atawakataa watu hawa kwa sababu wao ni watu wa dini tu na si wakristo wa kweli.
Walau mbele za Mungu sisi sote tunatakiwa kuwa wakweli na kujitambua sisi wenyewe jinsi tulivyo. Kila wakati, kila dakika na kila sekunde ni lazima tukiri kuwa tulifungwa kwenda kuzimu kwa sababu ya dhambi zetu. Ni lazima sisi sote tuwe na imani ya nyuzi za bluu, zambarau na nyekundu mbele ya Masihi. Kuamini kwa jinsi hiyo ni jambo sahihi kulifanya. Na kila tunapotubu, ni lazima tujikumbushe sisi wenyewe juu ya yale ambayo Masihi ameyafanya kwa ajili yetu, kwamba alibatizwa ili kutukomboa sisi toka katika dhambi na alihukumiwa kwa ajili ya dhambi zetu kwa kusulubiwa kwake, na anautambua wokovu wetu kila wakati. Hii ni imani ambayo Mungu anaihitaji toka kwetu.
Hatuwezi kumpendeza Mungu ama sivyo tufanye yale ambayo Masihi anataka tuyafanye. Kwa nini? Kwa sababu amefanyika kuwa Mwokozi wetu wa milele kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, tunatakiwa kuamini kila mara kwa yale ambayo Mungu ameyatenda kwa ajili yetu. Kama ambavyo imani ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu ni ya kweli, tunaihitaji zaidi kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu tunazozifanya kila siku.
 


Je, Mungu Atapendezwa Ikiwa Tutampatia Matoleo ya Jitihada Zetu Binafsi?

 
Ikiwa tungempatia Mungu vitu vya duniani, tusingekuwa tunajikusanyia hasira ya Mungu tu, bali tungekuwa tunatenda dhambi kuu kwa kutoa changamoto kinyume na Mungu. Imani ya jinsi hiyo ni uhaini mkubwa, kwa kuwa inasimama kinyume na Mungu. Hakuna kitu katika ulimwengu huu, hata kikiwa cha thamani kubwa na bei ya juu, kinachoweza kumpendeza Mungu. Kumletea Mungu vifaa vya ulimwengu huu si imani sahihi inayoweza kukubaliwa na Mungu. Haijalishi vitu hivyo ni vizuri kiasi gani kwa mitazamo ya kibinadamu, Mungu hapokei vifaa vya jinsi hiyo. Ni lazima tuwe na imani ile ambayo Mungu anaitaka toka kwetu na tumpatie imani hiyo.
Imani yetu ni lazima iwe inayoliamini Neno la Mungu kama lilivyo, imani ile inayompelekea Mungu sadaka kamili ambayo Mungu anaihitaji toka kwetu. Kila wakati, na kila muda unaopita, ni lazima pia tutambue yale ambayo Mungu amefanya kwa ajili yetu, na ni lazima tukiri udhaifu wetu pia na mapungufu yetu. Ni lazima tuzikumbuke baraka nyingi ambazo Mungu ametupatia, na ni lazima tufahamu kikamilifu na kuamini yale ambayo Mungu ameyatenda kwa ajili yetu, kwamba kwa hiari yake amekutana nasi.
Ni lazima tuziache kabisa imani zote za matambiko, na ni lazima tuwe na imani inayoliamini Neno lililozungumzwa na Mungu. Sadaka ya imani hii ndiyo ambayo tunapaswa kumtolea Mungu. Ni pale tu tunapomtolea Mungu sadaka ya imani sahihi ndipo atakapopendezwa, atakutana nasi, na kisha ataikubali imani yetu. Na ni pale tunapofanya hivyo ndipo Mungu anapotupatia baraka zote ambazo ameziandaa kwa ajili yetu.
Tunapokaa katika Neno, ni lazima tutafakari, “Ni imani ipi ambayo Mungu anaihitaji toka kwetu? Je, ni aina ipi ya maombi ambayo Mungu anaitaka?” Ndipo tunatambua kuwa maombi ambayo Mungu anataka si mengine bali ni maombi katika imani. Bwana wetu anataka tumpatie maombi ambayo yanatolewa katika imani ya wokovu ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, yaani ndani ya imani ambayo imeyapokea yale ambayo Mungu ametupatia. Hivyo Mungu anachokihitaji toka kwetu ni maombi ya shukrani ndani ya imani; Mungu hataweza kupokea kitu chochote tunachojitengenezea tunapojaribu kumpatia au kukiweka miguuni pake. Ni lazima sisi sote tutambue kuwa hatupaswi kufanya hivi.
Mungu anatuambia sisi, “Hapana, hapana, hiyo si imani ninayoihitaji toka kwako. Nilibatizwa na kusulubiwa kwa ajili yako. Niliupokea ubatizo ili kuzifanya dhambi zako zote kutoweka. Ni kwa sababu nilitakiwa kuzichukua dhambi zako katika mwili wangu kabla ya kuhukumiwa kwa ajili ya dhambi hizi na kufa Msalabani. Mimi ni Mwokozi wako, lakini kimsingi mimi pia ni Mungu wako. Mimi ni Mfalme wa wafalme, lakini kwa sababu pia mimi ni Mungu wako, nilikuja hapa duniani na nikatimiza kila kitu. Ninakuhitaji wewe uniamini mimi kwa kweli, utambue mamlaka yangu katika moyo wako, na ukiri kwa moyo wako wote kuwa mimi ni Mungu wako wa kweli.” Ni kwa madhumuni haya kwamba Mungu ametupatia nyuzi za bluu, zambarau, nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Hii ni imani ambayo Mungu anaihitaji toka kwetu.
Kwa kweli ni lazima tuwe na imani hii ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Unaweza kujifikira wewe mwenyewe, “Sawa, bado nina nafasi ya kuishi. Bado ninafanya vizuri, na mambo yanaenda vizuri sana. Kama kitu hakijavunjika kwa nini nikitengeneze? Kwa nini ni lazima niamini kwa namna hii? Ikiwa ninaamini kwa njia hii au kwa njia nyingine, je njia hizi si zote ziko sawa?” Hapana, haziko sawa! Ikiwa unayo imani nyingine tofauti na hii katika moyo wako, basi kwa hakika haujaokolewa. Kwa sababu katika moyo wa jinsi hiyo bado dhambi inapatikana, ni lazima uugeuze moyo wako na urudi katika imani inayoamini kwa kweli katika injili ya maji na Roho.
Kimsingi, mioyo ya wale wanaoamini katika injili ya kweli na mioyo ya wale ambao hawaamini iko tofauti. Mungu analifahamu hili, na hata sisi pia ambao tumezaliwa upya. Unapokuja kujifahamu wewe mweyewe, ni lazima ugeuke. “Mungu, kwa kweli nina dhambi. Tafadhali niokoe.” Hivyo pale utakapougeuza moyo wako na kuutafuta wokovu wako, Mungu atakutana nawe kwa ukweli wake.
 

Bwana Wetu Ametuokoa Sisi Toka Katika Dhambi Zetu Zote.
 
Bwana wetu alibatizwa na kusulubiwa kwa ajili yetu. Kama ilivyoandikwa katika Mathayo 3, hivi ndivyo ambavyo Bwana wetu ametenda kwa ajili yetu. Tunaliamini hilo. Tunamshukuru Mungu kwa hilo. Wakati Yesu alipobatizwa, dhambi zetu zote zilipelekwa kwake. Wakati aliposulubiwa ni kwa sababu alikuwa amezichukua dhambi zetu katika mwili wake ili aweze kuzipeleka dhambi hizi Msalabani. Alihukumiwa si tu kwa ajili ya dhambi zetu tu, bali kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote.
Wakati Bwana wetu anapotueleza kumletea sadaka za vifaa vya ujenzi wa Hema Takatifu la Kukutania, au wakati anapotuambia kitu chochote, kwa kawaida anatueleza kwa mfuatano. Kwa kawaida anatueleza kuwa, “Niletee nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu.” Nyuzi za bluu mara nyingi zinakuwa ndio za kwanza. Na anaendelea kwa kutaja kitani safi ya kusokotwa inayotueleza juu ya kuliamini Neno la Mungu. Kuamini kwanza katika damu ya Msalaba na kisha kuuamini ubatizo wa Yesu inaweza kuonekana kuwa ni sawa katika mtazamo wa kwanza, lakini kwa kweli hii si sawa. Hii ni kwa sababu Yesu alibatizwa kwanza ili aweze kuimwaga damu yake katika Msalaba. Ninakueleza tena kwamba si vizuri kuiamini kwanza damu ya Yesu Msalabani na kisha ndipo kuuamini ubatizo wake. Mungu haruhusu imani ya jinsi hiyo.
Bwana wetu alipokuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu alibatizwa alipokuwa na umri wa miaka 30, kwanza alibatizwa ili kuzichukua dhambi zetu zote katika mwili wake. Baada ya kufanya hivyo, ndipo akazichukua dhambi hizi za ulimwengu Msalabani, alihukumiwa kwa kusulubiwa kwake, na kisha akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo akafanyika kuwa Mwokozi wetu. Kwa hiyo, ni lazima tuyaamini yale ambayo Mwokozi wetu ametenda kwa ajili yetu kwa mujibu wa mfuatano na utaratibu ambao kwa huo amezitimiza kazi zake. Hivi ndivyo inavyotupasa kuamini. Hapo ndipo imani yetu inapoweza kusimama kikamilifu, haiwezi kuvurugwa wala haiwezi kutikiswa. Na pale tunapoitangaza injili kwa wengine, ni lazima tufanye kama hivyo. Kwa maneno mengine, ni lazima tuamini kwa namna ambayo itampendeza Mungu kwa kadri alivyotupangia.
Ni sadaka zipi za imani ambazo Mungu anataka umletee? Je, Mungu hakuelezi kumletea imani ya nyuzi za bluu, zambarau, nyekundu na kitani safi ya kusokotwa? Je, unayo imani hii? Je, bado huna imani ya jinsi hii na kwamba unaamini kinyume chake? “Hata kama ninaamini katika njia hii au katika njia ile haijalishi. Bado ninaamini, na ni hivyo tu. Kwanza ninaziamini nyuzi nyekundu, na kisha ninafuatia kuziamini nyuzi za bluu, na kisha nyuzi za zambarau.” Ikiwa hivi ndivyo unavyoamini, basi inakupasa uamini tena. Mungu hawezi kuikubali imani yako hii iliyogeuzwa.
Bwana wetu ni Mungu wa haki na Mungu wa kweli. Kwa hiyo, hazikubali imani potofu. Kwa sababu imani haiwezi kusimama vizuri wakati mpangilio wake umevurugika, Mungu hawezi kuithibitisha imani ya jinsi hii hata kama anataka hivyo. Kama ambavyo hatuwezi kuuweka msingi baada ya kuwa tumekwisha maliza kuijenga nyumba, na hii ni kwa sababu Yesu amezichukua dhambi zetu zote katika ubatizo wake na ndipo akaweza kusulubiwa.
Hivyo, ni lazima tuamini kwa mujibu ambao Bwana ametueleza. Huku ndiko kuliweka jiwe la msingi kwa imani sahihi. Kwa sababu Mungu ametuokoa kikamilifu, na kwa haki, sisi hatuwezi kuubadili mtiririko wake. Ikiwa tunaiamini kwanza damu ya Msalaba na kisha katika ubatizo wa Yesu, basi imani ya jinsi hii ni potofu. Na dhambi bado inapatikana kwa watu wanaoamini hivyo, kwa sababu dhambi zao hazikuoshwa kwa sababu ya namna walivyoigeuza imani yao. Kwa kweli hii ina shangaza na kufurahisha. Hakuna imani zaidi ya hii inayoshangaza kwa kufurahisha.
Kabla ya Masihi, wengi wetu tulikuwa tukiiamini damu ya Yesu tu Msalabani. Tuliamini kuwa, “Yesu alizichukua dhambi zangu zote na akabeba hukumu zangu zote kwa kuimwaga damu yake Msalabani. Kwa hiyo sisi tumeokolewa kikamilifu. Wokovu wetu ulikuja toka kwa Kristo ambaye alikufa kwa ajili yetu Msalabani. Yeyote anayeamini hivi sasa ameokolewa.” Ndipo tukatambua maana ya asili ya ubatizo wa Yesu. Kwa hiyo ukiongezea ile imani yetu ya awali ambayo ilikuwa potofu, ndipo tukaiongeza imani ya kweli. Nini kilitokea baadaye? Dhambi zetu hazikutoweka kiukweli. Kwa sababu aina hii ya imani ni ile ya kiufahamu na kimafundisho tu, haikuweza kuwa imani halisi na ya kweli ya mioyo yetu.
Ikiwa imani yako ni kama hii, ni lazima ugeuke mara moja na kuibadili. Kwanza kabisa, ni lazima uamini kwa wazi kuwa imani yako haikuwa sahihi. Na kisha ni lazima uujenge upya msingi wako wa imani mara moja. Unachotakiwa kufanya hapo ni kubadili ule mfuatano au utaratibu. “Baada ya kuja hapa duniani, wakati Bwana alipobatizwa na Yohana Mbatizaji katika Mto Yordani, alizichukua dhambi zangu zote katika mwili wake. Ni kwa sababu Yesu alibatizwa ili kwamba dhambi zote za ulimwengu zipelekwe kwake, na kwa sababu dhambi zote za ulimwengu zilipelekwa kwake, basi dhambi zangu zote pia zilipelekwa kwa Yesu. Na kisha, akaimwaga damu yake Msalabani ili kulipa mshahara wa dhambi zangu zote.” Hivyo ndivyo inavyokupasa uamini.
“Ni nani anayejali ikiwa ninaamini namna hii au namna ile? Jambo kuu ni kuwa ninaamini katika huduma zote nne za Bwana. Kwa nini uwe mkaidi na kuusisitiza mfuatano huu?” Je, kwa bahati unaamini na kuung’ang’ania mtazamo huu? Basi ni lazima uuchukue ukweli huu katika moyo wako: Yesu alikufa Msalabani baada ya kubatizwa. Na huu ndio ukweli ambao unapaswa kuuamini.
Roho Mtakatifu hathibitishi kamwe mambo yasiyo ya haki. Mungu Roho Mtakatifu anaikubali imani yetu pale tu tunapoyaamini yale ambayo Masihi ameyafanya kwa ajili yetu katika ulimwengu huu kama yalivyo. Roho Mtakatifu hasemi, “Kwa hiyo unaziamini hizi kazi zote nne za Yesu. Amin. Haijalishi kuwa unaamini kiusahihi au unaamini kinyume chake, haijalishi kuwa unaamini kwa njia hii au kwa njia ile, hiyo ni sawa tu hata ukiamini vyovyote vile. Amin. Safi, kwa hiyo ninyi basi ni wana wangu.”
Yesu Masihi alikuja hapa duniani kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu Baba na akafanya kwa kadri ya Baba alivyotaka. Hivi ndivyo alivyoyaishi maisha yake ya miaka 33 duniani, aliikamilisha kazi yake ya wokovu wetu kwa kubatizwa, alisulubiwa, na akafufuka, na kisha akapaa mbinguni. Na ametutumia Roho Mtakatifu. 
Mungu Roho Mtakatifu anakaa ndani ya mioyo ya sisi tuliolipokea ondoleo la dhambi, na anaithibitisha imani ya wale wanaoyaamini yale ambayo Bwana ameyatenda kwa ajili yao kama walivyo. Hii ndiyo sababu hatuwezi kuamini kulingana na mawazo yetu binafsi. Ingawa wewe na mimi tunamwamini Yesu kiukweli, je yamkini kwa bahati mbaya unaamini kinyume chake? Kama ndivyo, ni lazima uamini tena kiusahihi.
Unapofanya hivyo, Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani ya moyo wako. Japokuwa tuna mapungufu mengi, Roho Mtakatifu anaishikilia mioyo yetu kikamilifu kwa neema yake pale tunapopungukiwa mbele zake. Roho Mtakatifu anatupatia sisi nguvu. Anatupatia sisi uimara. Anatufariji. Anatubariki. Anatuahidi wakati ujao ulio mzuri. Na kwetu sisi tunaoamini, anatuongoza toka imani hata imani ili tusipoteze sifa za kuingia katika Ufalme wake wa milele.
Hiki ndicho tunachokihitaji wakati tunapoyaamini yale ambayo Bwana ameyafanya kwa ajili yetu, au wakati anapotueleza kumletea sadaka zetu—kwamba, ni lazima tuamini kuwa ametuokoa kwa maji na kwa Roho. Vifaa vyote ndani ya Hema Takatifu la Kukutania ni vya muhimu sana kwa sababu vyote vinatueleza kwa usahihi juu ya siri ya kuzaliwa upya kwa maji na kwa Roho. Kwa maneno mengine, kwa kupitia vitu vingi vya Hema Takatifu la Kukutania, Mungu anataka kutueleza sisi juu ya kitu kimoja—ambacho ni injili ya maji na Roho.
 

Kwa Kuwa Imani Yetu, Msingi Wake ni Muhimu Sana
 
Ikiwa tunajenga nyumba ya imani bila ya kuuweka kwanza msingi wa imani yetu kikamilifu, basi kadri tunavyoendelea kumwamini Yesu ndivyo tunavyozidi kuziongeza dhambi zetu, na ndivyo tunavyozidi kutoa maombi ya toba, na ndivyo tunavyozidi kuwa wanafiki wenye dhambi. Lakini tunaiamini zawadi ya wokovu, kwamba Bwana wetu ametuokoa kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, basi ndipo tunapoweza wote kuwa watoto wakamilifu wa Mungu. Kwa hiyo, ni lazima sisi sote tuuamini ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, na hivyo ni lazima sisi sote tufanyike wana wa Mungu.
Wale ambao msingi wao wa imani ni mkamilifu wanaweza wakati wote kubeba ukuhani wao katika mwanga unaong’aa, hata pale ambapo wao wenyewe wana mapungufu. Kwa maneno mengine, wanaweza kuyatimiza majukumu yote ya ukuhani kwa ukweli pale wanapowakumbatia watu wote wa ulimwengu huu katika vifua vyao, hali wakiwaombea ondoleo la dhambi zao na kuitumikia injili hii mbele za Mungu.
Tofauti na hivyo, wale ambao msingi wao wa imani hauko sahihi, kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo wanavyozidi kuwa wanafiki. Wanakuwa waovu. Wanakuwa ni wanadini waovu. Kama Bwana wetu alivyotueleza kwamba tutautambua mti kwa matunda yake, matunda yanayozaliwa na watu wa jinsi hiyo ni yale yenye maudhi na karaha, yenye uchafu, na unafiki. Hata hivyo, sisi ambao tumezaliwa upya sio wanafiki kabisa. Wote ni wakweli. Ingawa wana mapungufu yao, lakini ni watu wakweli. Wanatambua udhaifu wao na makosa yao, na wanaishi katikati ya mwanga unaong’aa. Kwa sababu Bwana wetu alibatizwa na kusulubiwa ili kuziondosha dhambi zetu zote, na kwa sababu kwa hakika amezitowesha dhambi zetu zote, basi kwa kuuamini ukweli huu sisi tumepokea ondoleo la dhambi zetu. Kwa sababu msingi wa imani yetu ni imara, japokuwa tuna mapungufu, ingawa tunatenda dhambi, na japokuwa sisi ni dhaifu, lakini bado maisha yetu yanang’aa kwa kuwa mioyo yetu haina dhambi wakati wote. Kwa sababu ya mapungufu yetu tunaweza tukajikuta tunakwenda kinyume katika nyakati fulani, lakini kwa sababu sisi hatuna dhambi, hatufanyi hivyo ili kuwapoteza wengine na sisi wenyewe kuelekea uharibifu. Ingawa tuna mapungufu, bado tunatembea katika njia ambayo inampendeza Mungu, tukisonga mbele hatua kwa hatua hali tukiitumikia injili zaidi na zaidi. Hii imewezekana kwa sababu Yesu ametuokoa sisi kikamilifu.
Ikiwa Yesu Kristo, Masihi wetu, na Mwokozi wetu angekuwa hajatuokoa sisi kikamilifu kwa nyuzi nne, tusingekuwa tumeokolewa kamwe. Ni kwa sababu Yesu ametuokoa ndio maana tumeokolewa, na ni kwa sababu ya hili ndio maana tunaamini, tunaieneza injili, na tunamtukuza Mungu kwa imani yetu. Ni kwa imani yetu kwamba tunamshukuru Mungu, ni kwa imani yetu kwamba tunamtumikia, na ni kwa imani yetu kwamba tunamfuata. Hivi ndivyo tulivyofanyika sasa. Kwa maneno mengine, tumefanyika wale tunaompendeza Mungu kwa imani yetu. Tumefanyika wale ambao msingi wao wa imani unasimama imara.
Wale ambao msingi wao wa imani haujawekwa vizuri ni lazima wauweke tena vizuri. Hii ndio maana Waebrania 6:1-2 inasema, “Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na imani kwa Mungu, na wa mafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele.”
Kifungu hiki cha maandiko kinatueleza nini? Kinatueleza kufahamu na kuthibitisha kwa wazi, na kuuweka msingi imara juu ya maswali kama: “Kwa nini Yesu alibatizwa?”; “Je, huu ubatizo ni dhana inayowiana na kitendo cha kuweka mikono juu ya wanasadaka katika Agano la Kale?”; “Je, sisi tutaishi tena?”; na, “hukumu ya milele ni ipi?” Kifungu hiki kinatueleza kuwa na imani kamilifu na kuuweka msingi wake imara tangu awali, ili kwamba tusiweze kutikiswa wala kulazimishwa kuuweka msingi wetu tena kwa vitu hivi. Imani inayoamini katika nyuzi za bluu, zambarau, nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ndiyo imani kamili inayoamini kuwa Bwana wetu ameukamilisha wokovu wetu kiusahihi. Ni lazima tusimame imara katika msingi huu, na ni lazima tukimbie tukianzia toka katika msingi huu. Ni lazima tuzikimbie mbio za imani.
Baadhi ya watu wanakitafsiri kifungu hicho toka kwa Waebrania kuwa kinasema hatuwezi tena kuwa na dhambi zetu kwa kuwa zilipelekwa kwa Yesu kwa kupitia ubatizo wake, na kwamba hatuhitajiki kuujenga msingi wa imani tena. Lakini, Mungu angetueleza kuujenga upya msingi wa imani ikiwa ungelikuwa umejengwa vizuri mara ya kwanza? Kifungu hiki kinatueleza kuwa wale ambao hawana msingi sahihi wa imani ni lazima waujenge msingi huu, na kwa wale wenye msingi sahihi wa imani ni lazima wauimarishe zaidi na wasonge mbele.
Ili kutuokoa, Mungu alimwamuru Musa kulijenga Hema Takatifu la Kukutania na kuzipokea sadaka toka kwa watu wake. Mungu aliwaamuru watu wa Israeli kumletea dhahabu, fedha, na shaba; nyuzi za bluu, zambarau, nyekundu, na kitani safi, na singa za mbuzi; ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, ngozi ya pomboo, na mbao za mshita. Kama ilivyoonyeshwa katika vifaa hivi, kwa kweli Bwana wetu ametupatia zawadi ya wokovu kwa kutukomboa mimi na wewe toka katika dhambi za ulimwengu. Kwa njia hii, kwa kweli Mungu aliwaeleza waisraeli kumletea sadaka hizi, kulijenga Hema Takatifu la Kukutania, kuuweka utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa, na akazisamehe dhambi za waisraeli waliomtolea sadaka zao za kuteketezwa kwa mujibu wa kanuni za utaratibu huu wa sadaka ya kuteketezwa.
 

Imani Yetu Imefanywa Kamilifu Kwa Kuziamini Nyuzi za Bluu, Zambarau, na Nyekundu na Kitani Safi ya Kusokotwa Ambavyo Vilitueleza Kabla Juu ya Utimilifu Kamili wa Wokovu Wetu Kwa Yesu Kristo.
 
Ikiwa sisi tutashindwa kuuamini ukweli kamili uliotimizwa na Yesu Kristo, ikiwa hatutauweka msingi imara wa imani yetu mara moja, kwa kweli imani yetu itaendelea kutikiswa mara kwa mara. Pasipo ufahamu, utambuzi, na imani juu ya ukweli kuwa Bwana wetu ametuokoa sisi kiukamilifu, sisi sote tutajikuta tunaishia kujaribu kuufikia wokovu wetu kwa jitihada zetu wenyewe. Imani ya jinsi hiyo si kamilifu na imepotoshwa.
Hebu tuangalie Waebrania 10:26-31: “Maana kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao. Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashihidi wawili au watatu. Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema? Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake. Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai.”
Kifungu hiki kinatueleza sisi kuwa ikiwa tunatenda dhambi kwa makusudi baada ya kuwa tumeshaupokea ufahamu wa kweli, basi haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi, bali ni hukumu ya kutisha tu. Hapa, wale wanaotenda dhambi kwa makusudi baada ya kuwa wameshaupokea ufahamu wa kweli inamaanisha ni wale wasioamini katika injili ya maji na Roho pamoja na kuwa wanaifahamu. Ni lazima tuamini katika ukweli kuwa Mungu ametuokoa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, na kuwa ametuokoa kwa dhahabu, fedha, na shaba, na kwamba alilitengeneza paa la Hema Takatifu la Kukutania kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, kwa singa za mbuzi, kwa ngozi za kondoo dume zilizonakshiwa rangi nyekundu, na kwa ngozi ya pomboo. Ni lazima sisi sote tuvifahamu vitu hivi kwa wazi na kuuweka msingi wa imani yetu imara.
Bwana wetu aliahidi kuwa atatuokoa sisi kikamilifu, na wakati ulipowadia, alibatizwa ili aweze kuzichukua dhambi zetu katika mwili wake, akafa Msalabani, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo ametuokoa sisi kikamilifu. Kwa hiyo tumeokolewa kikamilifu kwa kumwamini huyu Yesu Kristo aliyeweka msingi wa imani yetu kikamilifu.
Lakini wale wanaoufahamu ukweli huu lakini bado wanakataa kuuamini kwa hakika watakutana na hukumu ya Mungu ya kutisha itapofika siku yao ya mwisho ya hukumu.. Miili yao haitakufa bali itateseka milele. Biblia inatueleza sisi kuwa kutakuwa na uchungu wa kutisha kwa ajili yao, na mateso yao ya kuzimu yatakuwa makubwa sana kiasi kuwa inaelezewa kuwa wataishi na kuteseka nyakati zote kwa moto (Marko 9:49). Biblia inatueleza kuwa kutakuwa na kiasi cha matumaini ya kutisha ya hukumu, na uchungu wa kutisha utawateketeza maadui.
Ikiwa kule kushindwa kuitunza na kuifuata Sheria kunawapeleka watu katika hukumu hii ya kutisha, je, ni kiasi gani cha mateso kitakuwa kwa wale wasiouamini wokovu wao uliotolewa na Mwana wa Mungu? Hii ndiyo sababu sisi sote inatupasa kuamini katika Yesu Kristo kuwa ni Mwokozi wetu, katika Bwana aliyekuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, aliyezichukua dhambi zetu zote katika mwili wake kwa ubatizo wake, aliyezibeba dhambi za ulimwengu kwenda Msalabani na aliyebeba adhabu zote za dhambi kwa kusulubiwa kwake, aliyefufuka tena toka kwa wafu, na ambaye sasa anaishi.
 

Kwa Hiyo Msingi wa Imani Yetu Ni Lazima Uwekwe Kikamilifu.
 
Kwa nini Mungu alimwambia Musa kulijenga Hema Takatifu la Kukutania? Tunapokitazama kila kitu na kila kifaa kilichotumika katika Hema Takatifu la Kukutania, tunaweza kuona kwamba vyote vinadhihirisha ukweli kwamba Yesu Kristo alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, alizichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa ubatizo alioupokea toka kwa Yohana Mbatizaji, alizibeba dhambi hizi za ulimwengu Msalabani na akafa kwa ajili hiyo, akafufuka tena toka kwa wafu, akapaa mbinguni, na anakaa katika upande wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu Baba, na kwa sasa amefanyika kuwa Mungu wetu wa milele. Toka katika lango lake hadi katika nguzo yake na vitasa vya shaba, vifaa vyote vya Hema Takatifu la Kukutania vinatueleza ukweli wa injili. Kwa maneno mengine, Agano la Kale lote linatueleza juu ya ubatizo wa Yesu Kristo, kusulubiwa kwake, utambulisho wake, na kazi zake za wokovu.
Kutoka katika Agano la Kale hadi Agano Jipya, kwa sababu Yesu Kristo anazungumza nasi kuhusu injili ya maji na Roho—ambayo ni, injili ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa—wale wanaouamini ukweli huu mara nyingi wanaongelea juu ya ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa kila wanapopata nafasi. Kwa sababu ukweli huu umehubiriwa na umesikika mara kwa mara, wakati mwingine tunaweza hata kusahau jinsi ukweli huu ulivyo wa thamani. Lakini ukweli huu ni muhimu kiasi gani? Kana kwamba tulikuwa tunaishi katika kipindi cha utawala wa Mfalme Sulemani wakati ambapo dhahabu ya thamani na fedha vilikuwa vingi sana kiasi kuwa vilichukuliwa ni kama mawe, kwa sababu tunausikia ukweli huu kila siku katika Makanisa ya Mungu, kuna nyakati tunaweza kuuchukulia wokovu huu kiurahisi-rahisi. Lakini ukumbuke jambo hili: ukweli huu hauwezi kusikika kila mahali zaidi ya kusikika katika Kanisa la Mungu, na pasipo wokovu huu hakuna hata mmoja anayeweza kuokolewa wala kuuweka msingi wa imani ukawa imara.
Imani ambayo kwa hiyo mimi na wewe tumeokolewa ni imani katika ukweli kuwa Bwana wetu ametuokoa sisi kikamilifu na aliuweka msingi imara wa imani yetu kwa nyuzi nne za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Ngoja nirudie tena kuwa ni lazima sisi sote tuuamini ukweli huu katika mioyo yetu. Mungu alituahidi sisi, na kama alivyotuahidi, alikuja hapa duniani kama Uzao wa Mwanamke (Mwanzo 3:15), alizichukua dhambi zetu zote katika mwili wake kwa ubatizo wake, akabeba adhabu yote ya dhambi zetu zote Msalabani, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo ametuokoa sisi kiusahihi. Kwa sababu huu ni ukweli rahisi ambao ni rahisi sana kuuelezea na kuuelewa, basi tunaweza kuihubiri injili hii katika ulimwengu mzima kila siku. Kwa kweli, bado kuna watu wengine wenye kusikitisha ambao hawaufahamu ukweli huu. Hata hivyo, wapo wanaosikitisha zaidi, yaani wale ambao hawaamini pamoja na kuwa wamo katika Kanisa la Mungu.
Pamoja na kuwa umepokea kikweli ondoleo la dhambi zako, mawazo yako yanaweza bado kuwa mabaya, lakini walau moyo wako umekuwa ni mnyenyekevu. Lakini wanafiki hawako hivyo, ingawa wanaweza kujaribu kujionyesha kwa nje kuwa ni wanyenyekevu, lakini ndani ya mioyo yao ni wenye dhambi sana kiasi kuwa wanaendelea kumdanganya Mungu na watu wengi kila siku. Mimi na wewe ni lazima tuweke msingi wa imani kikamilifu. Ni lazima tusimame mbele za Mungu tukiamini hali tukiwa juu ya wokovu ambao Bwana wetu ameuanzisha na kuuthibitisha.
 

Imani Ambayo Inasimama Imara Kama Sehemu ya Vifaa Vya Hema Takatifu la Kukutania.
 
Mungu alitueleza kumletea sadaka hizo na kulijenga Hema lake Takatifu la Kukutania. Wewe na mimi ni lazima sote tufanyike watu wa imani ambao tunaamini kuwa Yesu Kristo alikuja hapa duniani na kwamba ametuokoa kiroho. Ni lazima tusimame imara mbele za Mungu kwa kuwa na aina ya imani ambayo ni kama vifaa vya ujenzi vilivyotumika katika Hema Takatifu la Kukutania. Je, unaamini? Je, una imani ya jinsi hii? Kwa kupitia Kanisa la Mungu, injili ya maji na Roho bado inaendelea kuhubiriwa. Kwa sababu injili hii ni msingi halisi wa imani ya kweli kiasi kuwa ninashindwa hata kusisitiza vya kutosha.
Makanisa na madhehebu mengi ya ulimwengu huu yanabaki hayafahamu juu ya ukweli kwamba Yesu alizipokea dhambi zote katika mwili wake kwa ubatizo wake, na badala yake wanaiamini damu ya Msalaba tu. Hata katika mazingira kama haya, bado Bwana wetu ameturuhusu kuutafuta ukweli. Sababu iliyomfanya Yesu akapigiliwa misumari na kuangikwa Msalabani ni kwa sababu alikuwa amebatizwa na Yohana Mbatizaji katika Mto Yordani. Ni kwa sababu alikuwa amezipokea dhambi zote za ulimwengu zilizopitishwa kwake kwa ubatizo wake ndio maana alisulubiwa na kuangikwa Msalabani.
Kwa hiyo, imani ya wale wanaoamini kuwa wamepokea ondoleo la dhambi kwa kuiamini damu ya Msalaba tu ni imani potofu ambayo itawaangusha chini bila kujali jinsi wanavyojitoa. Bila kujali jinsi wanavyohubiri bila kuchoka katika makutano ya watu kwa sauti kali juu ya kumwamini Yesu, juu ya imani yao inayoamaini juu ya damu ya Msalaba tu, juu kusali sala za toba pamoja na kuwa sala hizo zimeshindwa kutatua tatizo lao la dhambi, ukweli ni kuwa imani ya jinsi hiyo imejengwa katika msingi mlegevu ambao utavunjika mara mvua zitakapomwagika, upendo utakapovuma, na mafuriko yatakapokuja.
Mimi mwenyewe sikuwa nimesikia juu ya ubatizo wa Yesu kwa habari zozote za undani kwa zaidi ya takribani miaka 10 tangu nilipoanza kumwamini Yesu. Hata hivyo, Yesu alikutana nami kwa Neno lake la kweli, ndipo nilipozaliwa upya kwa maji na kwa Roho. Sasa, ninafahamu kuwa kuna watu wengi katika ulimwengu mzima ambao wanautafuta ukweli lakini bado hawajaufikia. Ninataka kuwaambia wote ili waweze kuusikia ukweli wa maji na Roho ili kwamba waweze kupokea ondoleo la dhambi zao kwa kuamini katika mioyo yao.
Kabla hujazaliwa upya, wewe pia, bila shaka uliishi maisha yako ya kidini. Bila shaka kwa wakati huo ulikuwa hujasikia juu ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Sio hilo tu, bila shaka ulikuwa haujaisikia injili ya maji na Roho, pia pengine ulikuwa hujasikia kuwa dhambi zetu zote zilipelekwa kwa Yesu pale alipobatizwa.
Ni muhimu sana kwa Wakristo kuufahamu na kuuamini ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa kama zilivyo. Ni pale tu msingi wa imani unapokuwa umewekwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa ndipo tunapoweza sote kusimama imara katika imani yetu. Ikiwa ulikuwa haujaamini hivi hadi sasa, bado hujachelewa—unachotakiwa kufanya ni kuamini hata sasa. Nia pale tu utakapo amini ndipo unapoweza kuokolewa kikamilifu, kuuweka msingi imara wa imani yako, na kuianzisha na kuithibitisha imani yako katika msingi huu.
 

Wale Waliomo Katika Kanisa la Mungu Ni Lazima Pia Waiweke Misingi yao ya Imani Kikamilifu.
 
Mathayo 24:40 inasema, “Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.” Wakati wote tumekuwa tukikiri kuwa tunauamini ukweli mmoja na kuitumikia injili moja kwa pamoja katika Kanisa la Mungu, itakuwaje basi baadhi miongoni mwetu wakaachwa?
Kwa sababu Neno la Mungu ni lenye akili na heshima, basi imani haiwezi kulazimishwa kwa mtu kwa lazima. Basi pale unapolisikia Neno la Mungu likihubiriwa kwako kwa heshima, ni lazima uliamini kwa fikra za haki, hali ukiziweka fikra zako katika ukweli kuwa unalisikia Neno la Mungu. Wakati watu waisraeli walipomsikia Mungu alivyowaambia, waliyachukulia maneno ya Musa kuwa si maneno yake binafsi bali kuwa ni Neno halisi la Mungu. Vivyo hivyo, unapokuwa umeelezwa juu ya kile ambacho Neno la Mungu linasema, unahitaji kuangalia kuona ikiwa unaamini au huamini kwa mujibu wa Neno hili la Mungu. Ni lazima ulitakafakari Neno kwa kichwa kilichotulia, na kisha uamini kwa yale ambayo Neno la Mungu linakueleza.
Biblia iliwapongeza watu wa Beroya kwa moyo wa uungwana katika mtazamo wao mzuri juu ya Neno la Mungu. Waamini katika Beroya “walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba hayo ndivyo yalivyo” (Matendo 17:11). Kwa kifupi, waliamini kwa akili katika Neno la Mungu kadri walivyofundishwa.
Imani ya kweli inatoka katika akili na moyo wenye fikra za kiungwana unaolitafakari Neno. Je, inaweza kuleta maana yoyote kwa mtu kulazimishwa kuamini kinyume na matakwa yake? Hata kama mtu anaweza kumlazimisha mtu fulani kuamini, kwa kweli jambo kama hili litakuwa ni jambo lisilo na maana, kwa kuwa yule anayelazimishwa hataweza kuamini kile anachoambiwa kukiamini. Mbele za Mungu, kila kitu kinategemea jinsi mtu husika anavyoamini katika uhuru wake. Ikiwa mtu fulani haamini wakati anapokuwa ameambiwa habari ile ile mara kwa mara, basi kunakuwa hakuna njia nyingine zaidi ya mtu huyu kuishia kuzimu. 
Kwa hiyo, kila mwenye dhambi katika ulimwengu huu anahitaji huruma zetu, lakini ikiwa baadhi yetu hatuliamini Neno la Mungu kama lilivyo hata pale ambapo tupo sote chini ya dari moja ya Kanisa la Mungu, basi wenye dhambi hao wamo kwenye shida zaidi. Je, haitishi sana kwa baadhi yao ambao wanaishia kuzimu hata baada ya kuwa wamebakia kimwili katika Kanisa la Mungu hilohilo ambalo na sisi tumekuwapo?
Yesu alikuwa na wanafunzi kumi na mbili, na miongoni mwao ni Yuda tu ambaye hakuamini kuwa Yesu alikuwa ni Masihi na Mwokozi. Kwa hiyo Yuda alimwita Yesu kuwa ni mwalimu mara kwa mara. Vivyo hivyo Petro, alizoea kumwita Yesu mwalimu katika nyakati hizo, lakini hatimaye alikuja kuamini kinyume chake na akakiri, “Bwana, Wewe ni Kristo Mwana wa Mungu. Wewe ni Mwana wa Mungu, Mwokozi uliyekuja kuzifanya dhambi zangu kutoweka. Wewe ni Mungu wa wokovu.”
Kwa maneno mengine, imani ya Petro ilikuwa tofauti na ile ya Yuda. Baada ya Yuda kumsaliti Yesu na kumuuza, alijinyonga na kujiua mwenyewe. Ingawa Yuda alikuwa pamoja na wanafunzi wengine kumi na moja, mwishoni, alishindwa kutambua kuwa Yesu Kristo alikuwa ni nani hasa, na hivyo akaishia kuzimu. Kwa upande mwingine, japokuwa Petro alikuwa si mvumilivu na mwenye mapungufu mengi, aliokolewa kwa kumtambua Yesu Kristo na kumwamini kuwa ni Mwokozi.
Vivyo hivyo, wokovu unategemea juu ya hakika kuwa mtu anaufahamu na kuuamini katika moyo wake. Mtu hawezi kuuamini ukweli wakati haufahamu. Hata hivyo, ikiwa watu hawauamini ukweli hata pale wanapoufahamu, kwa hakika watakutana na adhabu kuu (Luka 12:48). Hii ndiyo sababu Mungu anatueleza sisi kuwa msingi wa imani yetu ni lazima uwe imara na ulio sahihi.
 

Imani Yetu Ikoje?
 
Je, msingi wetu wa imani umeimarishwa sasa? Je, uko imara? Je, unaamini kuwa Bwana amekuokoa kwa hakika? Kwa kupitia maji na Roho, kwa hakika Bwana wetu ametuokoa sisi. Hiki si kitu cha pekee ambacho dhehebu letu linakifundisha, bali ni kitu ambacho Mungu alikiahidi katika Agano la Kale na ambacho Yesu amekitimiza katika Agano Jipya—hivi ndivyo ambavyo Kristo ametuokoa sisi kwa hakika.
Yesu ni Mfalme wa wafalme (nyuzi za zambarau) aliyekuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, alizichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake kwa ubatizo wake (nyuzi za bluu), akazibeba na kuzipeleka dhambi hizi Msalabani na akasulubiwa (nyuzi nyekundu), akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo ametuokoa sisi. Mungu aliahidi kuwa atafanya hivyo katika Agano la Kale, na sasa ametuokoa kwa kuitimiza ahadi hii katika Agano Jipya. Je, unaamini? Hakuna imani zaidi ya hii ambayo inajenga msingi imara wa imani.
Kuna mamia ya mamilioni ya Wakristo katika ulimwengu wote, lakini kwa wengi wao, msingi wao wa imani bado ni mlegevu. Tunaweza kuona na kutambua ikiwa watu wana au hawana imani sahihi kwa kuviangalia vitabu vingi vya Kikristo ambavyo vinapatikana sasa. Waandishi wa vitabu hivi mara nyingi wanakuwa ndio viongozi wa jumuiya za Kikristo, na kwa kuvisoma vitabu vyao ndipo tunapoweza kufahamu ikiwa wanao au hawana ufahamu sahihi wa kweli. Ikiwa mmoja wa viongozi hawa hajui au hauamini ukweli hata pale ambapo anaufahamu, basi kila anayemfuata kiongozi wa jinsi hiyo wote wataishia kuzimu. Ukweli wa kuhuzunisha ni kuwa kuna watu wachache sana wanaoufahamu ukweli huu takribani watu milioni moja tu. Hii ndio sababu wachache wetu tunaoufahamu ukweli huu tumeieneza injili kwa uaminifu katika ulimwengu mzima.
Mungu anafanya kazi kupitia kwetu. Mimi na wewe hatuwezi kukwepa bali kuihubiri injili, kwa kuwa kutoihubiri injili hii ya maji na Roho katika ulimwengu mzima ni sawasawa na kufanya dhambi kuu mbele za Mungu. Kwa kweli, ikiwa hatufuati kwa kweli na kuitumikia kazi hii kwa imani, basi kwa hakika tutakuwa tukifanya dhambi kuu mbele za Mungu. Hii ni dhambi ya kuwapeleka watu kuzimu hata pale tunapofahamu kuwa tunaweza kuizuia; kwa kweli ni dhambi isiyosameheka kwamba watu wataishia kuzimu katika ujinga wao ati kwa sababu sisi tunaoufahamu ukweli tumeifunga midomo yetu.
Ikiwa hatutalikamilisha jukumu tulilopewa, watu hawa watatulalamikia, kwa kuwa ni jukumu letu la msingi. Biblia inatuonya sisi, ikisema, “Bali mlinzi akiona upanga unakuja, kama hapigi tarumbeta, wala watu hawakuonywa, na upanga ukaja ukamwondoa mtu awaye yote miongoni mwao; ameondolewa huyo katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwa mlinzi huyo” (Ezekieli 33:6). Sisi ambao tumefahamu kwanza na tumeamini kwanza ni lazima tulibebe jukumu hili la mlinzi.
Ninamshukuru Bwana kwa kutupatia sisi injili hii na kwa kutuwezesha kuufahamu ukweli huu. Ninamshukuru sana pale ninapotambua kuwa sisi tumechaguliwa wachache katika ulimwengu huu ambao tunaufahamu ukweli huu na kuiamini injili hii. Tumeihubiri injili ya maji na Roho kwa wachungaji wengi na waamini wa kawaida katika ulimwengu mzima, lakini kila siku tumethibitisha ukweli kuwa hakukuwa na hata mmoja aliyefahamu na kuamini katika injili hii hapo kabla. Kwa kupitia sisi, wahubiri wa injili ya maji na Roho wamekuwa wakitokea katika dunia nzima. Kama ilivyo kwetu, wao nao, wana msingi imara wa imani na wanaieneza imani hii imara.
Ikiwa kuna watu wengi wa jinsi hiyo wanaoieneza injili, basi pengine tunaweza kupumua kwa unafuu na kupumzika kidogo katika kazi ya kuhubiri injili, lakini, ni jambo la kuhuzunisha kuwa hadi sasa hakuna watu wengi katika ulimwengu huu wanaoufahamu na kuuamini ukweli huu. Wengi walikadiria vibaya mafanikio ya Matengenezo ya Kanisa katika historia ya ulimwengu. Tunapoyaangalia matengenezo hayo kwa undani, tunaweza kuona kuwa wana matengenezo walipoteza kishikizo cha kwanza cha imani ya kibiblia katika kipindi cha matengenezo, na kwamba kila kitu kilichofuata pia kiliwekwa pasipo pake. Hata kama makosa yaliyofuatia yatasahihishwa, ikiwa kishikizo cha kwanza kikiwa bado kimepotea, bado mafundisho yote yatabakia kuwa ni uchafu; kwa hiyo, historia ya Ukristo ni lazima iandikwe upya.
Ninatumaini na kuomba kuwa ninyi nyote mtasimama mbele za Mungu katika msingi imara wa imani yetu, na kwamba katika msingi huu wa imani, mtayaishi maisha yetu kwa nia ya kuitumikia injili ya kweli. Unapoiishi injili, kwa kawaida moyo wako utajazwa furaha. Wakati mtu anaiishi injili, moyo wake unageuzwa kuwa katika moyo wa kiroho. Na kwa kadri Roho Mtakatifu anavyoijaza mioyo yenu na kufanya kazi ndani yake, mioyo hiyo yote itafurika furaha.
Lakini ikiwa hauiishi injili bali unayafuata matamanio ya mwili wako hata pale unapokuwa umepokea ondoleo la dhambi na umeifahamu injili ya maji na Roho, basi utaishia kuishi maisha yasiyo na maana na yasiyo na kitu.
Ninamshukuru Mungu kwa kutupatia injili hii ya thamani na kwa kutupatia wokovu wake bure. Ni maombi na matumaini yangu kuwa nyote mtazifakari imani zetu kwa mara nyingine, na kupokea zawadi ya wokovu kamili kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa.