Search

Sermoni

Somo la 3: Injili ya Maji na Roho

[3-8] Ubatizo wa Yesu ni moja wapo ya hatua ya Ukombozi isiyopaswa kuwekwa kando (Mathayo 3:13-17)

(Mathayo3:13-17)
“Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia akisema mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote. Basi akamkubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini na tazama mbingu zikamfunukia akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua akija juu yake na tazama sauti kutoka mbinguni ikisema Huyu ni Mwanangu mpendwa wangu ninayependezwa naye.”
 

UBATIZO WA YOHANA MBATIZAJI
 
Nini maana ya Toba?
Kugeuka toka maisha ya dhambi na
Kumwamini Yesu ili kutakaswa.
 
Watu wengi ulimwenguni hawafahamu ni kwa nini Yesu alikuja katika ulimwengu huu na kubatizwa na Yohana Mbatizaji. Hivyo hebu tuzungumzie juu ya sababu za ubatizo wa Yesu na juu ya Yohana Mbatizaji aliyembatiza Yesu. 
Kwanza, yatupasa kuwaza juu ya nini kilichomfanya Yohana Mbatizaji abatize watu katika mto Yordani. Inaelezewa katika Mathayo 3:1-12 kwamba Yohana Mbatizaji alibatiza watu ili kuwarejesha kwa Mungu tokana na dhambi kwa kutubu kwao.
“Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba” (msatri wa 11) na “sauti ya mtu aliyenyikani; itengenezeni njia ya Bwana yanyoosheni mapito yake” (mstari wa 3). Yohana Mbatizaji alivaa vazi la singa za ngamia na kubeba kifurushi cha mzigo na kupiga kelele jangwani, akihubiri ubatizo wa toba kwa msamaha wa dhambi.
Alipiga kelele kwa watu “Tubuni, mwokozi wa wanadamu anakuja, tayarisheni mapito kwake, nyoosheni njia ya wokovu. Acheni kuabudu miungu wa mataifa na mpokeeni Bwana mioyoni mwenu.”
Geukeni kutoka wapi? Kutoka katika kuabudu sanamu na matendo mengine yote ya uovu katika maisha yaliyojaa dhambi. Hivyo inatupasa kufanya nini? Yatupasa kubatizwa katika Yesu ili tuweze kutakaswa. Yohana Mbatizaji alipaza sauti nyikani Njooni niwabatize, mtakaswe dhambi zenu. Mwokozi Masiya wenu anakuja ulimwenguni. Atachukua dhambi zenu zote akiwa ni mwana kondoo wa sadaka katika Agano la Kale na kuzitakasa zote.
Katika Agano la Kale, dhambi za kila siku zilitwikwa juu ya sadaka ya dhambi ambaye ni mbuzi kwa kupitia kuwekewa mikono juu ya kichwa chake na mwenye dhambi, na kwazile dhambi za mwaka mzima za Waisraeli pia nazo zilitwikwa juu ya mbuzi na Kuhani Mkuu katika siku ya upatanisho ambayo ilikuwa tarehe ya kumi mwezi wa saba katika kila mwaka (Walawi 16:29-31).
Kimsingi umuhimu wa ubatizo uliofanywa na Yohana Mbatizaji ulikuwa kwa ajili ya toba ambayo iliwarudisha Waisraeli kwa Yesu ambaye angekuja baadaye. Toba maana yake kugeuka toka maisha ya dhambi na kumwamini Masiya ili kusamehewa dhambi zote.
Watu wa Israeli waliweza kukombolewa kwa kumtumaini Masiya amabye angelikuja baadaye kutakasa dhambi zao zote. Nasi pia tunakombolewa kwa kumwamini Yesu aliyeshuka toka mbinguni miaka 2000 iliyopita na kutakasa dhambi za ulimwengu. Lakini Waisraeli katika Agano la Kale waliitupilia mbali sheria ya Mungu kwa kutoa sadaka isiyo sahihi na kumsahau Masiya.
Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alihitaji kuwakumbusha juu ya sheria ya Mungu na ya Masiya atakayekuja punde, alianza kuwabatiza watu na ndipo alipombatiza Yesu pia katika Yordani.
Watu wengi walikuja kwa Yohana na walibatizwa wakitubu kwa kuabudu sanamu na kutupilia mbali sheria ya Mungu. Yapo mambo matatu yasiyowekwa kando katika sheria ya utoaji kafara (sadaka ya mnyama)—kwanza mnyama aliye hai, kuwekea mikono na damu. Watu wote wa ulimwengu wanaokolewa kwa kumwamini Yesu.
Pale ambapo Mafarisayo na Masadukayo walipokuja kubatizwa, Yohana aliwafokea, “enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? Basi zaeni matunda yapasayo toba, wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, tunaye Baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu mtoto” (Mathayo 3:7-9).
Mafarisayo na Masadukayo hawa ni kundi la wanasiasa na waabudu sanamu, walidhani kuwa wao ndiyo waliokuwa ni watu wa Mungu ingawa ukweli ni kwamba hawakuwa wakiamini neno la Mungu. Waliamini Miungu wengine na mawazo yao.
Walipokuja na Yohana Mbatizaji ili wabatizwe aliwaeleza kuwa “hampaswi kutoa sadaka isiyo sahihi bali kugeuka toka dhambini na kumwamini ipasavyo Masiya atakayekuja na kutakasa dhambi zenu. Inawapasa kuamini kwa moyo wenu wote.”
Kutubu ni kugeuka toka njia isiyo sahihi. Toba ya kweli ni kugeuka toka dhambini na imani isiyo ya kweli na kumrudia Yesu. Ni kuamini ukombozi wa ubatizo na hukumu ya Yesu pale msalabani.
Kwa jinsi hiyo, Yohana Mbatizaji alipaza sauti kwa watu wa Israeli ambao walikuwa tayari wamekwisha itupilia mbali sheria ya Mungu na mpangilio wa utoaji wa dhabihu, ili awashawishi kumrudia Mungu. Hili ndilo lilikuwa jukumu la Yohana Mbatizaji kuwarejesha watu kwa Yesu ili waweze kumwamini na hata kuokolewa kwa dhambi zao zote.
 

JE, UNAAMINI UKOMBOZI KUPITIA UBATIZO WA YESU?
 
Nini kinachopaswa kufanyika
Na watu wote mbele ya Yesu?
Wanapaswa kumwamini yeye ili waweze
Kuokolewa kwa dhambi zao zote.
 
Jambo la kwanza Yesu alilofanya katika huduma yake ya wazi ilikuwa ni kubatizwa na Yohana Mbatizaji. Dhambi zote za ulimwengu zilitwikwa juu yake kwa njia hii.
Hivyo ubatizo wa Yesu ulikuwa ndiyo mwanzo wa wokovu wa Mungu kwa wanadamu pamoja pia na tendo la haki kwa Yesu kuweza kutakasa dhambi zote za ulimwengu. Mungu hukomboa wale wote wenye kuamini kweli kwamba yesu alichukua dhambi zote za ulimwengu juu yake kwa njia ya ubatizo.
Yesu alipokuja ulimwenguni na kubatizwa na Yohana Mbatizaji, injili ya ufalme wa Mbinguni ndipo ilipoanza. Mbingu zilifunuka kwa ubatizo wake kama ilivyoelezwa katika Mathayo 3:15 ilikuwa sawa sawa kabisa na sadaka ya upatanisho ilivyoelezwa katika Walawi 1:1-5, 4:27-31 nyakati za Agano la Kale.
Kila kitu katika Agano la Kale kina mwenzake katika Agano Jipya, na pia Agano Jipya kwa Agano la Kale “Tafuteni katika kitabu cha Bwana mkasome hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo, hapana mmoja atakayemkosa mwenzake; kwa maana kinywa changu kimeamuru na roho yake imekusanya” (Isaya 34:16).
 

YOTE KATIKA AGANO LA KALE NA JIPYA HUZUNGUMZIA JUU YA UPATANISHO WA bDHAMBI ZA WATU WOTE
 
Je, imetupasa kutubu kwa
dhambi zetu kila siku?
Hapana. Toba ya kweli ni kukubali juu ya
dhambi zetu zote na kugeuka kwa mtu
kufikia kuelekea kuamini ubatizo wa
Yesu ili kupata ukombozi.
 
Katika agano la Kale, dhambi za kila siku zilitwikwa juu ya dhabihu ya dhambi kwa kuwekewa mikono. Dhabihu hiyo ilitoa damu yake na kuhukumiwa kifo kwa niaba ya mwenye dhambi. Na zile dhambi za jumla kwa mwaka mzima pia nazo zilisamehewa kwa njia hiyo ili watu waweze kusamehewa kwa dhambi za mwaka mzima.
Katika Agano Jipya, njia hiyo inafanana kabisa kwani Yesu Kristo alikuja na kubatizwa Yordani ili kubeba dhambi zote za ulimwengu. Kwa hivyo neno la Mungu lilihubiriwa katika Agano la Kale lilitimizwa katika Agano Jipya.
Yohana Mbatizaji aliyembatiza Yesu alikuwa ni mtumishi wa Mungu aliyekuja miezi 6 kabla ya Yesu. Alishuhudia kwamba Yesu alizibeba dhambi za ulimwengu kwa kusema katika Yohana 1:29 “Tazama Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.”
Yohana Mbatizaji alimtwika Yesu dhambi zote za wanadamu kwa njia ya ubatizo katika mto Yordani. Kwa njia hii, Bwana alifanya upatanisho wa dhambi zote za wanadamu. Kile tunacho paswa kufanya nikuamini tu.
Yohana Mbatizaji alitwisha dhambi za ulimwengu juu ya Yesu. Wanafunzi wa Yesu walisema katika Matendo 3:19 “Tubuni basi mrejee, ili dhambi zenu zifutwe zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana.”
Iliwapasa kuelewa kwa nini Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu, kwa nini aliwaambia watu wamfuate Yesu. Alisema, “Tubuni basi mrejee. Amini ukombozi wa ubatizo wa Yesu. Mtakaswe dhambi zenu.”
Masiya alikuja na kututakasa dhambi zetu zote kwa mara moja katika ubatizo wake. Dhambi za ulimwengu wote zilitwikwa kwake Yesu kwa njia hii. Hivyo Agano la Mungu lilitimia kwa ubatizo wa Yesu kama ilivyoandikwa katika Mathayo 3:13-17.
“Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, mimi nahitaji kubatizwa na wewe nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kitimiza haki yote. Basi akamkubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini na tazama mbingu zikamfunukia akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua akija juu yake na tazama sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu mpendwa wangu, ninayependezwa naye.”
Kwa kuutimiza wokovu wa Mungu, Yesu alikuja kwa Yohana Mbatizaji. Yohana Mbatizaji alikuwa mtumishi mahususi wa Mungu. Luka sura ya 1 inasema kwamba Yohana alikuwa ni uzao wa Haruni Kuhani Mkuu wa kwanza. Mungu alimchagua Yohana uzao wa Haruni, kwa sababu alitaka mwakilishi huyo wa wanadamu wote kuitimiza haki yote. 
Hivyo, Mungu aliwezesha Yohana kuzaliwa katika nyumba ya kuhani miezi 6 kabla ya kuzaliwa Yesu. Yohana Mbatizaji alitayarisha njia kwa ajili ya Yesu kwa kupaza sauti nyikani “Tubuni, enyi uzao wa nyoka! Tubuni basi mrejee. Masiya atakuja. Mrejee yeye au atawaangamiza na kuwatupa motoni. Amini ubatizo na damu yake msalabani. Tubuni mkabatizwe ndipo mtakapo kombolewa.”
Injili ya ukombozi imeelezwa wazi katika Matendo 3:19. Yohana Mbatizaji alipopaza sauti juu ya dhambi za wanadamu, wengi walirejea kwa Mungu.
Kwa kuwa Yohana alitwika dhambi za ulimwengu juu ya Yesu dhambi zote za wanadamu zilifutwa mara moja kwa wakati huo. Kwa sababu Yohana mbatizaji alishuhudia kwamba Yesu alibeba dhambi zetu zote, hivyo tunaelewa kuwa tutaweza kuokolewa kwa kuamini injili ya ukombozi, injili ya maji na Roho.
 

SABABU YA YOHANA MBATIZAJI KUJA MBELE YA YESU
 
Ni nini maana ya neno
“kwa kuwa ndivyo?”
(1) stahili (2) tosheleza
(3) Muhimu kwa namna hii tu
(hakuna njia nyingine tena).
 
Wale wote ambao dhambi zao zimetakaswa kwa kumuamini Yesu Mwokozi, wataweza kuthibitisha wokovu wao kupitia ushuhuda wa Mathayo katika injili ya Yesu katika Mathayo 3:15-16, Yesu alikuja kwa Yohana na kusema “Nibatize” naye Yohana akajibu “mimi nahitaji kubatizwa na wewe nawe waja kwangu?”
Yohana Mbatizaji ndiye aliyembatiza Yesu baada ya kugundua kuwa Yesu alikuwa ni nani. Yohana alikuwa ni mtumishi wa Mungu aliyetumwa kumbebesha Yesu dhambi za wanadamu. Kwa kuwa Yesu alikuja akiwa ni mwokozi ili kuitimiza ahadi ya unabii wa Agano la Kale ilimbidi amwamuru Yohana Mbatizaji ambatize ili aweze kubeba dhambi za ulimwengu juu yake.
Kwa nini? Kwa sababu Yesu ni Mwana wa Mungu Mwnyezi, Muumba na Mwokozi. Alikuja kwetu ili kututakasa na dhambi zetu. Hivyo ili aweze kuokoa watu wote ilimbidi abatizwe.
“Kwa kuwa ndivyo” Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji na kutakasa dhambi zetu zote. Alihukumiwa kwa niaba yetu masalabani. Ubatizo wa Yesu ulikuwa ni ushuhuda wa wokovu wetu. Jinsi ile Mungu alivyoahidi katika Agano la Kale kwamba atatwika dhambi zote juu ya mwana kondoo wa sadaka ndivyo hivyo basi Mwana wa Mungu alivyokuwa Mwana Kondoo na kubeba dhambi zote juu yake.
Hivyo vyote, kuwekea mikono katika Agano la Kale na ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya ni kutwika dhambi na wokovu pamoja na uzima wa milele utolewao kwao wale wenye kuamini injili ya maji na Roho.
 

UBATIZO WA YESU UMETAKASA KABISA DHAMBI ZETU
 
Tutaweza vipi kumvaa Kristo?
Kwa ubatizo katika Kristo.
 
Yesu alipotaka abatizwe, Yohana Mbatizaji alijaribu kumzuia akisema “mimi nahitaji kubatizwa na wewe nawe waja kwangu?”
Lakini Yesu alimjibu akisema “kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote” kubali hivi sasa. Kubali. Alimwambia Yohana “Ni lazima unibebeshe dhambi zote za wanadamu ili niweze kuwarejesha wale wote watakaoamini injili ya ukombozi wa maji. Ndipo nitakapohukumiwa kwa dhambi hizo zote ili wale watakao amini ubatizo wangu watakombolewa kwa dhambi zao zote. Nitwike dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo ili wale wote watakao kuja baadaye waweze kukombolewa dhambi zao zote mara moja na kwa wakati wote. Sasa basi, kubali hivi sasa.”
Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji na ubatizo wa Yesu ulikuwa ni kulingana na sheria ya haki ya ukombozi wa Mungu. Kwa kuwa dhambi zote zilitwikwa kwake Yesu alipobatizwa, leo tunaweza kukombolewa mara moja kwa wakati wote pale tu tutakapo mwamini Yesu. Kwa kuwa alichukua dhambi zetu zote kwa kuwekewa mikono na kufa msalabani kwa niaba yetu, hivyo leo ameketi kuume kwa Mungu tutaweza kuokolewa kwa kuamini ukombozi wa maji na Roho.
Ndiye Yesu aliyetuokoa toka dhambi za ulimwengu. Tutaweza kuokolewa kwa kumwamini Yesu aliyechukua dhambi zetu zote na kulipia mshahara wa dhambi mslabani. Ubatizo wa yesu ulikuwa ndiyo mwanzo wa injili ya ukombozi. Ubatizo wa ukombozi umetajwa mara nyingi katika Biblia na mtume Paulo pia alisema katika Wagalatia kwamba alisulubiwa na Kristo kwa kuwa alibatizwa katika Kristo na kumvaa Kristo. Mtume Paulo anazungumzia juu ya imani yake katika ukombozi kupitia ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani.
 

“KUBALI HIVI SASA”
 
Yohana Mbatizaji alikuwa
na jukumu gani?
Jukumu lake lilikuwa kutwika dhambi
zote za ulimwengu juu ya Yesu
akiwa ni Kuhani Mkuu wa
wanadamu wote.
 
Yesu alisema “kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote.” Haki yote maana yake kufutilia mbali dhambi zote kwa ubatizo wa Yesu na kuwaweka watu huru pasipo dhambi ndani ya mioyo yao. “Basi akamkubali” Yesu alibatizwa katika mto Yordani.
Kama jinsi ile Kuhani Mkuu alivyoweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi, ndivyo Yohana Mbatizaji pia aliweka miono yake juu ya Yesu na kumtwika dhambi zote za ulimwengu. Yohana Mbatizaji alikuwa ni kuhani mkuu aliyetenda kazi ya kutwika dhambi zote za ulimwengu juu ya Yesu akiwa ni mwakilishi wa wanadamu. “Mungu natwika dhambi zote za ulimwengu juu ya Mwana kondoo Yesu” Hivi ndivyo dhambi zote za wanadamu zilitwikwa juu ya Yesu.
Yohana Mbatizaji aliweka mikono yake juu ya kichwa cha Yesu akamzamisha katika maji, na akaondoa mikono yake pale Yesu alipoibuka toka kwenye maji. Ubatizo wa Yesu ulileta wokovu wa haki. Hivyo Yesu aliokoa wanadamu wote watakaoamini ubatizo wake.
 

MBINGU ZIKAMFUNUKIA NA SAUTI IKATOKA MBINGUNI
 
Kuanzia lini ufalme wa
Mbinguni ulikuwa wazi?
Kuanzia siku zile za Yohana
Mbatizaji (Mathayo 11:12).
 
 “Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua akija juu yake na tazama sauti kutoka mbinguni ikisema, huyu ni Mwanangu mpendwa wangu ninayependezwa naye” (Mathayo 3:16-17).
Yesu alipobeba dhambi zetu za ulimwengu kwa ubatizo wake, mbingu zilimfunukia. Hivyo Agano la Mungu ambalo alikuwa ameliweka miaka zaidi ya elfu moja hapo nyuma liliweza kutimia kwa ubatizo wa Yesu katika mto Yordani.
Hivyo basi Yesu, akiwa ni Mwana Kondoo wa Mungu aliokoa watu wote ulimwenguni kwa dhambi zao. Dhambi zote za ulimwengu zilitwikwa juu ya Yesu na kutimiza mapenzi ya Mungu.
Inashuhudiwa katika Yohana 1:29 “Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu” Kwa kuwa dhambi zote za ulimwengu ziliwekwa juu ya Yesu, Mwana Kondoo wa Mungu, alikwenda nazo msalabani Golgota baada ya miaka mitatu akiwa na mzigo huo mabegani mwake. Baada ya kubeba dhambi zote kwa ubatizo wake, kila mahala alipokwenda aliwaambia wale waliompokea kwa imani kwamba dhambi zao zote zimesamehewa. 
Katika Yohana 8:11, alimwambia yule mwanamke aliyeshikwa ugoni “Nami pia sikuhukumu”. Hakuweza kumhukumu kwa kuwa aliyepaswa kuhukumu ni Yesu pekee, aliyebeba dhambi zake zote. Hivyo aliwaambia watu wote kuwa yeye ndiye Mwokozi wa wenye dhambi.
Kwa kuwa Yesu, Mwana wa Mungu alibeba dhambi zetu zote kila amwaminiye hapa ulimwenguni ataweza bila shaka kutakaswa. Mbingu zilimfunukia alipobatizwa. Lango la ufalme wa mbinguni lilikuwa wazi na kwa yeyote atakayeamini ubatizo wa Yesu ataweza kuingia bure.
 

YESU ALISULUBIWA BAADA YA KUBEBA DHAMBI ZOTE ZA ULIMWENGU KUPITIA UBATIZO WAKE
 
Kwa namna gani Yesu alikanyaga
kichwa cha shetani?
Kwa kufufuka kwake toka kifoni baada ya
kukubali hukumu ya dhambi zote.
 
Kwa kuwa dhambi zote zilitwikwa juu ya kichwa cha Yesu ilmpasa ahukumiwe msalabani. Alihuzunika sana na kuumia moyoni alipowaza juu ya mateso atakayopata msalabani. Aliomba hadi kutoka jasho la matone ya damu. Alipokwenda na Mitume wake sehemu iitwayo Gethsemane, alipasa sauti na kusema “Baba yangu ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi” (Mathayo 26:39). “Nilibatizwa na kubeba dhambi zote za ulimwengu, lakini naomba nisife kwa ajili ya hizo dhambi” Lakini Mungu hakujibu.
Katika siku ya upatanisho nyakati za Agano la Kale, sadaka ya dhambi ilipaswa kuuawa kwa kuchinjwa koo ili damu yake iweze kunyunyizwa mbele ya kiti cha Rehema na Kuhani Mkuu. Kwa njia hiyo pia Yesu alipaswa kusulubiwa na Mungu alikwisha amua lazima iwe hivyo.
Madhabahu ni hukumu ya Mungu na sadaka ya dhambi ni uzima. Kunyunyiza damu mara saba mbele na nyuma ya kiti cha rehema maana yake ni kwamba hukumu imefutwa (Walawi 16:1-22).
Yesu aliomba kwa Mungu ili akiepushe kikombe. Lakini Baba yake hakumruhusu na ndipo hatimaye akasema “walakini si kama nitakavyo mimi, bali kwa mapenzi yako” (Mathayo 26:39). Aliomba kwa Mungu ili afanye atakavyo. Alipomaliza kuomba alifuata mapenzi ya Baba yake.
Yesu aliacha mapenzi yake na kumtii Baba yake. Kwa nini? Kwa sababu ikiwa kama asingehukumiwa baada ya kubeba dhambi zote za ulimwengu, wokovu usingekamilika. Alisulubiwa kwa sababu alibeba dhambi zote za wanadamu kwa ubatizo wake. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23).
Mungu alitimiza Agano ambalo alisema atamtuma mwokozi na kuokoa wanadamu kupitia kuwekewa mikono ubatizo wa Yesu. Yesu alitii mapenzi ya Mungu na kukubali hukumu kwa niaba yetu.
Ilikuwa pia ni utimilifu wa unabii katika Mwanzo 3:15 “nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino.” Mungu alimpa ahadi Adamu ya kumtuma Masihi, uzao wa Hawa naye ataishinda nguvu ya shetani iliyo mfanya mwanadamu kuwa mwenye dhambi na kwenda motoni.
Tunapojua na kuamini ubatizo wa Yesu pamoja na kifo chake msalabani, dhambi zetu zote hutakaswa na kuokolewa kwa hukumu.
Yatupasa tuwe na imani iliyosahihi katika mioyo yetu tunapotilia maanani ubatizo wa Yesu na damu yake pale msalabani. Amini kwa moyo wako wote na ndipo utaokolewa.
 

UBATIZO WA YESU NI MWANZO WA INJILI YA MBINGUNI
 
Yesu aliamuru nini mara
ya mwisho kabla ya kupaa
kwenda mbinguni?
Aliamuru mitume wake kuwafanya mataifa
yote kuwa wanafunzi wake kuwabatiza
kwa jina la Baba na Mwana
na Roho Mtakatifu.
 
Ubatizo wa Yesu ulikuwa ndiyo mwanzo wa Injili, naye aliokoa wenye dhambi wote kwa ubatizo wake na damu yake. Katika Mathayo 28:19 imeandikwa “Enendeni ulimwenguni pote mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu”. Yesu aliwaambia wanafunzi wake wakashuhudie kwamba Baba na Mwana na Roho Mtakatifu wote hawa walikwisha waokoa wanadamu wote toka dhambini mwao na kuwasafisha wote kwa njia ya ubatizo na damu yake.
Yesu aliwapa nguvu ya kuwafanya wanafunzi mataifa yote; kuwafundisha juu ya ubatizo wa Yesu, ubatizo wa ukombozi, ubatizo ambao ulisafisha dhambi zote za ulimwengu.
Takribani miaka 2000, Yesu alikuja duniani katika mwili na alibatizwa na Yohana Mbatizaji. Kwa ubatizo wa Yesu dhambi zote za dunia, zikijumuishwa na zetu zote zilitwikwa juu yake.
Dhambi ngapi zilitwikwa juu ya Yesu? Je, ni pamoja na zile za kesho? Anatuambia kwamba hata na zile za kesho nazo zilitwikwa juu yake. Dhambi za watoto, wale wote wa kizazi cha kale, sasa na kijacho hata zile za Adamu zilitwikwa juu ya Yesu.
Je, itawezekanaje kuwa hakuna tena dhambi? Je, itawezekanaje kuwa sisi hatuna dhambi? Kwa sababu Yesu alibeba dhambi zetu zote duniani kwa ubatizo wake ili wale wote wamwaminio waweze kuwa huru kwa dhambi na tena kuwa na uwezo wa kuingia Ufalme wa Mbinguni.
“Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu” (Yohana 3:21).
Yesu alitakasa dhambi zetu zote kwa ubatizo wake, damu yake msalabani, kifo chake na ufufuo wake. Hivyo kwa kuamini ubatizo wake na kifo chake msalabani ni kuokolewa kwa dhambi zako zote. Hii ndiyo imani ya ukombozi. 
Tunapoamini ubatizo wa Yesu na damu yake Kristo tunaokolewa tunapomwamini katika njia iliyosahihi, je, tunakuwa wenye haki au wenye dhambi? Tunakuwa wenye haki. Je, hatuna dhambi tena ingawa si wakamilifu? Ndiyo hatuna dhambi. Kuamini ubatizo wa Yesu na hukumu yake msalabani ni kuwa na imani sahihi iliyo kamilika.
 

KUBATIZA NA KUBATIZWA KATIKA JINA LA YESU
 
Ni lini ulikuwa ni mwanzo
wa injili ya mbinguni?
Katika Ubatizo wa Yesu.
 
Kwa kuwa watu si viumbe wakamilifu, watumishi huwabatiza wale wanaoamini ubatizo wa Yesu na damu yake ili kuwafanya waweze kukiri imani hiyo. Waliozaliwa upya mara ya pili wahakikishe wameokolewa kwa kubatizwa kwa jinsi hiyo ya ubatizo wa Yesu ili kuhakikisha wazi imani yao.
Kwanza Mtumishi husali akiweka mikono yake juu ya kichwa cha mtu aliyeokoka huku akiomba baraka za Mungu ili mtu huyo aweze kumwabudu Mungu hadi siku zote maishani. Ndipo humbatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.
Tumebatizwa kwa msingi wa imani yetu katika ubatizo wa Yesu na damu yake. Ubatizo huu ni kuonyesha kwamba dhambi zetu zote zilitwikwa juu yake Yesu hivyo kwamba mtu aliyebatizwa hufa pamoja na Yesu na akafufuka naye. 
Kubatizwa ni kutoa tamko la imani katika kumtwika Yesu dhambi kupitia ubatizo wake, hukumu yake kwa ajili ya dhambi na kufufuka naye. Ni tamko la imani mbele ya Baba, Mwana na Roho Mtakatifu na mbele ya ndugu katika imani. Ni kukiri katika kuzaliwa upya mara ya pili katika maji na Roho. 
Wale wanomwamini Yesu, wakijua ukweli wa maana ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani hakika huokolewa kwa dhambi zao zote duniani. Hivyo wamebatizwa katika jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. “Yakale yamepita tazama! Yamekuwa mapya” (2 Wakorintho 5:17). Mambo yetu ya kale yamepita na tumezaliwa upya mara ya pili tukiwa watu wa imani. Ili kuhakikisha mioyoni mwetu tunabatizwa. Tunabatizwa katika Yesu kwa kuamini ubatizo wa Yesu.
 

MAISHA BAADA YA KUZALIWA UPYA MARA YA PILI KWA UBATIZO WA YESU NA DAMU YAKE MSALABANI
 
Waliozaliwa upya huishi
kwa ajili ya nini?
Huishi kwa ajili ya Ufalme wa Mungu
na haki yake, wakihubiri injili
ulimwenguni pote.
 
Maisha baada ya kukombolewa na kuzaliwa upya mara ya pili lazima yajumuishe imani ya Neno la Mungu. Haipaswi kuwa ni maisha ya hisia ambayo mtu inampasa kutubu dhambi za kila siku. Bali, inapaswa yawe ni maisha ya uaminifu ambao tunauhakika wa kila siku kwamba Yesu alibeba dhambi zetu kwa ubatizo wake.
Dhambi zetu zote zilitwikwa kwake Yesu pale alipobatizwa. Na baadaye aliishi miaka mitatu akiwa na mzigo huo hadi pale alipokubali hukumu ya dhambi hizo zote na kusulubiwa.
Hivyo sisi tunaoamini yatupasa kuwa na imani ya maandiko ya Neno, na si kwa hisia hata kidogo. Ikiwa tutashindwa, ndipo tutakapokuwa na wasiwasi juu ya dhambi zetu za kila siku baada ya kukombolewa na kuzaliwa upya. 
Tuachane na swala juu ya tuonavyo kuhusu dhambi na kuamini injili ya maji na damu tu. Haya ndiyo maisha ya mtu aliyekombolewa anavyopaswa kuishi.
Yohana Mbatizaji alisema nini juu ya Yesu? Alisema “Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu” (Yohana 1:29). Alishuhudia kwamba Yesu alibeba dhambi za leo, kesho na kesho kutwa, kuanzia ile ya asili. 
Je, hakuchukua dhambi zote? Je, dhambi zote hazikutwikwa kwa Yesu? Dhambi za ulimwengu ni pamoja na zote za kale, sasa na wakati ujao. Yatupasa kuhakiki injili ya ukombozi kwa kupitia ubatizo wa Yesu.
Wale wote wanaoamini ukweli wa ubatizo wa Yesu na damu yake wataokolewa. Yeyote aaminiye ubatizo wa Yesu hana tena dhambi moyoni.
Ingawa watu wengi hudhani kwamba bado wana dhambi kwa sababu hawaelewi kwamba dhambi zao zote zilikwisha twikwa juu ya Yesu tayari kwa ubatizo wake. Hudanganywa na shetani. Shetani huwaongoza kwa kupitia mawazo yao ya kimwili… “wewe unatenda dhambi kila siku. Utawezaje kutokuwa na dhambi?”
Wanapaswa kumwamini Mungu tu ili wasiwe na dhambi. Lakini shetani huwashambulia ili wajione kuwa ni wenye dhambi kwa kuwa wanaendelea kutenda dhambi. Hakuna yeyote awezaye kuwa na dhambi ikiwa ataamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani.
Kwa kuwa tunaishi hapa duniani tukiwa ni viumbe tusio wakamilifu na dhaifu, kamwe hatuwezi kusema tunakuwa wenye haki kupitia matendo yetu pekee. Lakini tunaweza kusema kwa imani kwamba tumeokolewa kwa ukweli wa ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Pale tunapoelewa kwamba kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu, mioyo yetu hutakaswa, tunajua kwa uhakika kuwa hatuna tena dhambi. 
Wimbo: “♬ Nimekombolewa. Umekombolewa. Wote tumekombolewa” Ni furaha iliyoje kuishi na matamanio ya kuhubiri injili kwa wote na kuelewa kuwa tunaongozwa na Roho.
Bila shaka sisi wenye kuamini hutenda dhambi kila siku lakini hatuna dhambi. Tuna ubatizo wa Yesu na damu yake mioyoni mwetu. Mioyo yetu hapo awali ilijaa dhambi lakini sasa tunaamini ubatizo wa Yesu sasa tutaweza vipi kuwa wenye dhambi.
“Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile anena Bwana. Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, na katika nia zao nitaziandika ndipo anenapo” (Waebrania 10:16).
Mioyo yetu iko huru kwa dhambi. Yesu amewezasha tuwe huru kamili kwa ubatizo wake na kifo chake msalabani. Wokovu toka dhambini hutokana na imani katika neno la Mungu.
 

YEYOTE ANAYEAMINI UBATIO WA YESU NA DAMU YAKE MSALABANI HAKIKA KAMWE HATOKUWA TENA MWENYE DHAMBI
 
Je, tunakuwa
wenye dhambi tena pale
tunapotenda dhambi?
Hapana. Hatuwezi tena kuwa
wenye dhambi.
 
Tusipoamini ubatizo wa yesu na damu yake, haijalishi ni kwa mara ngapi unafanya sala ya toba, bado utakuwa nadhambi moyoni. Lakini pale tunapokuja kuamini ukweli wa injili dhambi zetu zote hutakaswa.“Vipi! Imekuwaje siku hizi unaonekana mwenye furaha na mchangamfu?”
“Unaona sina dhambi tena moyoni.”
“Kweli? Nadhani sasa utaweza kutenda dhambi kadiri upendavyo?”
“Unajua, mwanadamu hawezi kujizuia kutenda dhambi. Hivyo ndivyo alivyo. Lakini Yesu alibeba dhambi zote kwa ubatizo na kukubali hukumu ya msalaba. Kwa sababu hiyo basi mimi nami najitolea kuitumikia injili hii katika kanisa. Warumi sura ya 6 inasema kwamba yatupasa sisi sote tuishi kwa namna hii. Kwa kuwa sina tena dhambi moyoni, napenda kufanya jambo la haki. Yatupasa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani na kuhubiri injili duniani pote! Tunapomwamini Yesu, Bwana wa ukombozi, hatutoweza kamwe kuwa wenye dhambi tena. Yatubidi kuamini wokovu wa milele katika ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Hakika nimejawa na shukrani nyingi!”
 

NANI APOKEAYE ROHO?
 
Yohana Mbatizaji alishuhudia
nini kuhusu Yesu?
Alishuhudia kwamba Yesu ndiye Mwana
Kondoo wa Mungu aliyebeba dhambi ya
ulimwengu zikiwemo dhambi zilizopita,
zilizopo na zijazo hata
dhambi ile ya asili.
 
Yeyote anaye amini ubatizo wa Yesu na damu yake pale msalabani hupokea wokovu. Sasa tunapokeaje Roho? Matendo 2:38-39 inatupa jibu “Petro akawaambia tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu na kwa watoto wenu na kwa watu wote walio mbali na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.”
Kubatizwa katika jina la Yesu Kristo maana yake ni kuamini ubatizo wa Yesu na kukombolewa. Ndipo Roho huyo huja akiwa ni kipawa toka kwa Mungu. 
Kubatizwa katika jina la Yesu Kristo pia maana yake ni kutakaswa kwa kuamini ubatizo wa Kristo na damu yake. Tunapo ikumbatia imani hii, tunapata ukombozi na kuweza kuwa wenye haki. Wanao amini hili hutakaswa na kuwa kama theluji kupitia huo ubatizo wa Yesu na hiyo damu yake msalabani.
“Nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu” Tunapoamini kwa dhati kwamba dhambi zetu zote zilitwikwa juu ya Yesu kupitia ubatizo wake na alipokea hukumu yake kwa kifo cha msalabani, mioyo yetu hutakaswa na kuwa safi. Imani yetu mpya huanzia pale tunapoamini ubatizo wa Yesu na damu yake na kupokea zawadi au kipawa cha Roho Mtakatifu na kuweza kuwa wana wa Mungu.
“Tena mtafahamu kweli, na hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32). Yatupasa kuelewa maana halisi ya hukumu ya Bwana pale msalabani. Ukweli ni huu, Yesu alifuta dhambi zetu zote kwa ubatizo wake na kifo chake juu ya msalaba. Ukombozi umeletwa kwetu pale tu tunapoamini ukweli huu.
 

UBATIZO WA YESU UMETUKOMBOA
 
Nani apokeaye Roho?
Yule ambaye aliyekombolewa kwa
dhambi zake zote kupitia imani katika
ubatizo na damu ya msalaba.

Upatanisho wa dhambi kupitia ule mpangilio wa dhabihu katika Agano la Kale unawakilisha ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya. Ubatizo wa Yesu ni kiini kikuu katika kila unabii wa Agano la Kale. Upande wa pili katika kuwekea mikono wakati wa Agano la Kale utaweza kupatikana katika tendo la ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya.
Dhambi zote za ulimwengu zilitwikwa juu yake Yesu kupitia ubatizo kwa namna ile ambayo dhambi zote za Waisraeli zilivyotwikwa juu ya mnyama wa kafara kwa kuwekewa mikono.
Je, ni kweli yatupasa kuamini ubatizo wa Yesu ili tuweze kuokolewa kwa dhambi zetu zote? Ndiyo! Yatupasa hakika! Lazima tukubali ukweli juu ya Yesu kubeba dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo wake. Tusipoamini ubatizo wa Yesu, dhambi zetu kamwe hazitoweza kuwa juu ya Yesu. Lazima tuamini hilo ili wokovu wetu ukamilike. Bila hivyo hatutoweza kuwa wenye haki.
Yesu ameokoa wale wote wenye dhambi duniani kwa njia iliyosahihi na ya haki kupitia ubatizo wake. Hapakuweza kuwepo na njia nyingine yeyote ile zaidi ya hii. Kwa sababu ubatizo wa Yesu ulikuwa ni mlolongo wa kutwika dhambi juu yake, lazima tuamini kwa moyo wetu wote utakaso ambao ni wa kudumu milele.
Lazima pia tuamini damu ya Yesu kuwa ndiyo hukumu ya dhambi zetu zote. Kwa hivyo vyote, yule anayeamini ubatizo na damu ya msalabani ameokolewa.
Yatupasa kuamini ubatizo wa Yesu ili tuweze kuingia ufalme wa mbinguni. Hii ndiyo njia pekee ya kuweza kukombolewa kwa dhambi zetu zote na hata kukwepa hukumu ya haki.
Ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya na kuwekea mikono katika Agano la Kale ni vitu vinavyoshabihiana moja kwa moja. Ni viunganishi kwa kila kimoja katika Agano la Kale na Jipya.
Katika Agano Jipya, Yohana Mbatizaji alikuja duniani miezi sita kabla ya Yesu. Yesu alipobatizwa huo ndiyo “mwanzo wa injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu” (Marko 1:1). Injili ilianza pale kipindi Yesu alipobeba dhambi ya ulimwengu kwa ubatizo wake.
Huduma ya wokovu kwa wanadamu ilifanyika kwa kupitia matukio ya kuandamana: kuzaliwa kwa Yesu, Ubatizo wake, kifo chake msalabani, ufufuko wake, na kupaa kwake mbinguni. Tunapofahamu haya na kuelewa pamoja na kuamini mlolongo huu kuelekea wokovu wetu basi tunakuwa moja kwa moja tumeokoka kwa dhambi zetu zote. Ubatizo wa Yesu ndiyo mwanzo wa injili bali damu yake msalabani ilikuwa ni hitimisho la wokovu wetu.
“Mwanzo wa injili ya Yesu Kristo mwana wa Mungu” (Marko 1:1). Kamwe si rahisi kuondoa moja kati ya matendo ya haki—Ubatizo wake, damu yake msalabani, kufufuka kwake, kupaa kwake na kuja kwake mara ya pili—katika injili ya mwana wa Mungu.
Yesu alikuja ulimwenguni akiwa katika mwili wa mwanadamu na kusafisha dhambi zetu zote sisi wanadamu kwa ubatizo wake, na huo ndiyo mwanzo wa injili ya mbinguni. Ikiwa hata moja ya haya yatakosekana katika injili, hakika injili hiyo haitokamilika kabisa. 
Hivyo ikiwa mtu ameokoka yaani kuzaliwa upya mara ya pili ni lazima awe ameamini ubatizo wa Kristo na damu yake. Nyakati hizi watu wengi hawaamini ukweli huu wa ubatizo wa Yesu na damu yake. Wao hudhani kuwa ubatizo wa Yesu ulikuwa ni ibada tu. Hili ni jambo hatari sana kushindwa kuelewa. Yeyote anaye mwamini Yesu ni lazima aamini ubatizo na damu yake
Dhambi zetu zitaweza kufutwa vipi kirahisi kwa kuomba sala ya toba? Dhambi zetu alitwikwa Yesu pale alipobatizwa na Yohana Mbatizaji. Hapana kabisa njia nyingine ambayo Yesu angeweza kubeba dhambi za wanadamu juu yake.
Yatupasa kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho ili tuweze kuingia ufalme wa mbinguni. Hakuna ukombozi pasipo maji ya ubatizo, damu ya msalaba na Roho. Ni kwa yule tu aliyezaliwa upya mara ya pili ndiye atakayemwona Mungu kama Yesu alivyomwambia Nikodemo katika Yohana 3:5 “Wokovu wa kweli huja kwetu ikiwa tu tutaamini ubatizo wa Yesu na damu yake pale msalabani.”
 

JE TUTAWEZA KUOKOLEWA PASIPO UBATIZO WA YESU?
 
Kwa njia gani amekuwa
mwokozi wetu?
Kwa kubeba dhambi zetu zote
kupitia ubatizo wake.
 
Ikiwa tungeliondoa huduma ya kwanza ya Bwana ambapo Yesu alikuja hapa ulimwenguni na kubeba dhambi zetu zote kupitia ubatizo wake, au hata kudharau utakatifu wa Yesu aliyezaliwa na Bikira Mariamu au kupuuza kuami msalaba wa Yesu, Ukristo basi ungelikuwa ni dini ya mazingaombwe au uchawi ambayo inawaongoza watu kwa kiitikio “nisamehe dhambi zangu, nisamehe dhambi zangu….” Kama wafanyavyo watu wa imani ya Budha katika mahekalu yao.
Kuondoa ubatizo wa Yesu utakuwa na maana kwamba dhambi zetu hazikutwikwa juu yake. Hapo imani yetu itakuwa haina thamani na kutufanya tusiwe tofauti na mdaiwa anayedai kulipa deni lake lote hali hajalipa chochote. Itatufanya tuwe waongo. Ikiwa mdaiwa atasema kwamba amekwisha lipa deni lake lote wakati ukweli ni kuwa haja lipa chochote, bado ataendelea kuwa mdaiwa kweli na kwa hisia.
Yesu alitakasa wanaoamini kwa maji ya ubatizo na kuwafanya kuwa watoto wa Mungu. Yesu alibeba dhambi zote za ulimwengu kupitia Yohana Mbatizaji ili wale wote wanaoamini waweze kutakaswa. Tunapoelewa na kuamini juu ya hili, mioyo yetu hutakasika milele.
Namshukuru Mungu kwa neema hii. Luka 2:14 inasema “atukuzwe Mungu juu mbinguni na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia” Imani yetu katika maji na damu ya Yesu hutuletea wokovu kamili na kutufanya kuwa watoto wa Mungu. Ubatizo wa Yesu na damu yake imetuokoa sisi na wale wote wanaoamini mambo haya mawili huokolewa.
Hapana chochote kinachoweza kutolewa katika kazi hii ya Yesu. Wengine huamini damu ya Yesu tu, wakisema Mtume Paulo hakujivunia kingine ila msalaba. 
Lakini ubatizo wa Yesu ulijumuishwa katika msalaba. Tunaweza kuona katika Warumi sura ya 6 kwamba Paulo alibatizwa katika Kristo na kufa na Kristo. Na pia katika Wagalatia 2:20 “Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilionao sasa katika imani ya Mwana wa Mungu ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.”
Na katika Galatia 3:27-29 “Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. Na kama ninyi ni wa Kristo basi mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawa sawa na ahadi.”
Kubatizwa katika Kristo maana yake ni kuamini yale yote aliyofanya hapa ulimwenguni, ubatizo wake na damu yake msalabani. Kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake ni kuamini ukweli kwamba Yesu tayari amekwisha futa dhambi zetu zote takriban miaka 2000 iliyopita. Hakuna njia nyingine ya kutuletea wokovu.
 

TUMEOKOLEWA NA MUNGU PALE TUNAPOAMINI UBATIZO WA YESU NA DAMU YAKE MSALABANI
 
Je dhambi zetu zitaweza
kutakaswa kwa sala ya toba?
Hapana. Msamaha wa dhambi unawezekana
ikiwa tu kupitia imani yetu katika kumtwika
dhambi zetu zote Yesu kupitia ubatizo
wake kwa Yohana Mbatizaji.
 
 “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata wokovu” (Warumi 10:10).
“Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo” (Wagalatia 3:27). Imani yetu hutuongoza katika ubatizo ndani ya Kristo, kumvaa Kristo na kuwa watoto wa Mungu. Yesu alipokuja ulimwenguni na kubatizwa, dhambi zetu zote na zile za ulimwengu zilitwikwa juu yake.
Imani yetu imetuongoza kuwa kitu kimoja na Kristo. Tunakufa pale alipokufa. Tulifufuliwa pale alipofufuka. Sasa kwa kuwa tunaamini ubatizo wa Yesu, damu na ufufuo wake, kupaa kwake na kuja kwake tena basi tutaweza kuingia ufalme wa mbinguni na kuishi milele.
Watu wanapoamini damu ya Yesu pekee, kamwe hawawezi kuzuia kupata tabu ya dhambi zinazobaki mioyoni. Kwa nini? Kwa sababu hawajui wala kukubali maana ya ubatizo wa Yesu, ambao huchukua dhambi zote na kutakasa mioyo ya dhambi, na kuwafanya weupe kama theluji milele.
Je, unaamini ubatizo wa Yesu na damu yake kuwa ndivyo vitu viokoavyo toka dhambini? Tafadhali amini ukweli huu usiobadilika. Pasipo kuamini ubatizo wa Yesu imani yako ni bure. Pasipo imani ya ubatizo wa Yesu hakika hutoweza kukombolewa dhambi zako na utakuwa umejiingiza katika upendo usiokuwa na matunda.
Wale wenye kuamini msalaba pekee husema “Yesu ni Bwana kwangu, Mwokozi aliyenifia msalabani, alifufuka toka kuzimu na kushuhudia ufufuo wake kwa siku 40 kabla ya kupaa mbinguni na sasa ameketi kuume kwa Mungu. Naamini kwamba atakuja mara ya pili kutuhukumu na naomba Yesu anibadilishe kabisa ili niweze kukutana naye Oh, mpendwa Yesu, Bwana wangu.”
Huomba msamaha kwa dhambi zao wakitumaini kutokuwa na dhambi mara, lakini bado wanabaki na dhambi zao mioyoni. “Namwamini Yesu lakini bado ninadhambi moyoni. Nampenda Yesu lakini bado ninadhambi moyoni, siwezi kusema, Tafadhali njoo kwangu Bwana harusi, kwa sababu nina dhambi na siwezi kuwa na uhakika wa wokovu wangu. Hivyo natumaini Yesu atakuja pale tu nitakapokuwa safi na kujitayarisha na pale tu nitakapo sali sala ya toba kwa dhati. Nampenda Yesu kwa moyo wangu wote lakini sikuthubutu kuwa mbele ya uso wake kwa sababu ya dhambi zangu katika moyo.”
Ikiwa Yesu angewauliza watu wa aina hii “kwa nini unadhani wewe si mkamilifu?”
Wangeweza kujibu “Bwana najua mimi si mwenye haki kwa sababu bado nandelea kutenda dhambi kila siku. Hivyo tafadhali niite utakapowaita wenye dhambi.”
Hawana uhakika kwamba Mungu muumba na Hakimu ataweza kuwakubali kuwa ni wenye dhambi au kuwafanya kuwa watoto kwake. Bwana harusi alikuja na kumaliza matatizo ya dhambi za bibi harusi, lakini kwa sababu bibi harusi hakuwa makini katika ukweli huu, anaendelea kuteseka. Tunapodhani kuwa ni wenye dhambi kwa sababu tu, tunatenda dhambi kwa miili yetu, hapo hatuna imani na Mungu. Tusipo fahamu au kutoelewa ukweli wa neno la Mungu, dhambi zilizomo ndani ya mioyo yetu huendelea kuzidi.
 
Kwa nini baadhi ya watu
huendelea kuteseka kwa dhambi
zinazobaki mioyoni mwao?
Kwa sababu hawajui au hawakubali moyoni
mwao maana ya ubatizo wa Yesu
ambao ulibeba dhambi zao zote.
 
Bwana harusi alibeba dhambi zote za ulimwengu. Wapi? Katika mto Yordani pale alipobatizwa. Wale wasioamini hili bado ni wenye dhambi. Wanabaki kuwa bibi harusi najisi. 
Bwana harusi anamuuliza bibi harusi “utawezaje kunipenda wakati wewe si bibi harusi kwangu? Kabla ya kuniita kuwa bwana harusi, dhambi zako zote ziwe zimetakasika.”
Tutaweza kukombolewa pasipo ubatizo wa Yesu? Hapana! Tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, hivyo tunatafuta haki mioyoni mwetu, na dhamira zetu hujaribu kujifanyia haki binafsi. Lakini haitowezekana kwetu kudhani kuwa hatuna dhambi mioyoni mwetu ikiwa hatujatakaswa. Ni pale tu tunapokubali na kuamini ubatizo wa Yesu ndipo hakika tutaweza kuwa watu wasio na dhambi na wenye haki.
Dhamira zetu hazitoweza kamwe kutakaswa ikiwa tunajichukulia kuwa si wenye dhambi hali huku ni wenye dhambi mioyoni. Hata Mungu hatoweza kamwe kutukubali katika mazingira ya aina hii. Mungu si mwongo.
Mungu alimwambia Musa achukue idadi ya Waisraeli kwa kuhesabu na walipe fidia ya uhai wao. Aliye tajiri alipaswa kulipa zaidi ya nusu shekeli na yule aliye masikini si chini ya hapo. Kila mtu ilimpasa kulipa fidia hiyo.
Hivyo, inawezaje mtu kutakaswa ikiwa hamwamini Yesu aliye mlipia fidia kwa uhai wake? Mtu wa aina hii huendelea kuwa na dhambi moyoni.
Pale tunapoamini damu ya Yesu pekee tunaendelea kuwa na dhambi moyoni mwetu na hata kukiri kuwa sisi ni wenye dhambi. Lakini tunapoamini injili ya ubatizo na msalaba kwa pamoja tutaweza kutamka kweli kuwa hatuna dhambi, wokovu na uzima ni wetu.
 

KUMKUFURU ROHO
 
Dhambi gani inayomhukumu
mtu kwenda motoni?
Kumtenda dhambi Roho au kwa maneno
mengine kutoamini ubatizo wa Yesu.
 
Warumi 1:17 inasema “kwa maana haki ya Mungu inadhihiriswa ndani yake toka imani hata imani.” Haki ya Mungu imedhihiriswa katika injili. Yesu alikuja katika ulimwengu huu na kutakasa dhambi zetu zote kwa ubatizo na kifo chake msalabani. Ubatizo wa Yesu na damu yake ndiyo nguvu ya injili. Hivyo alisafisha dhambi zetu mara moja na kwa wakati wote.
Kuamini maana yake ni wokovu na kutoamini maana yake ni motoni. Baba yetu aliyembinguni alimtuma mwana wake wa pekee Yesu Kristo hapa ulimwenguni na kumfanya abatizwe kwa ajili ya upatanisho wa dhambi zetu. Kwa jinsi hiyo yeyote anaye mwamini ataweza kutakaswa na uovu wake wote.
Dhambi pekee iliyobaki hapa ulimwenguni ni ile ya kutoamini ubatizo wake na damu yake. Kutoamini ni kumkufuru Roho na ni dhambi itakayohukumiwa na Mungu hivyo kumpeleka asiyeamini motoni milele.
Je, wewe nawe umeokolewa kwa ushuhuda wa ukombozi kupitia ubatizo wa Yesu na damu yake? Je, umepokea ushuhuda wa Yohana kama ilivyoandikwa katika Yohana 1:29 “tazama! Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu” Je, unaamini ubatizo wa Yesu na damu yake kama ilivyoandikwa katika Waebrania 10:18 “Basi ondoleo la hayo likiwapo hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.”
Mungu amewatunuku wale wote wenye kuamini ubatizo wa Yesu na damu kwa moyo wao wote. Mungu amewafanya kuwa wana kwake wale wote wanaoamini ubatizo wa Yesu na damu yake kukombolewa kwa upendo wa haki ya Yesu.
Aliyetumwa na Mungu hunena ya Mungu, lakini wale wa duniani, ambao hawakutumwa na Mungu, huubiri kulingana na mawazo yao. Wapo wengi leo hapa duniani wanao hubiri neno la Mungu na wale waliotumwa na Mungu hunena juu ya ubatizo wa Yesu na damu yake.
Lakini wale wahubirio maneno yao huelezea juu ya hisia zao tu. Watu hawa husema “tumekombolewa dhambi zetu za asili, lakini kila mmoja wetu yampasa kutubu kila siku dhambi azitendazo” Husema imewapasa kujitakasa kila mara na hatua kwa hatua.
Lakini ni kweli mtu ataweza kujitakasa mwenyewe? Tutaweza kweli kutakaswa kwa uwezo wa viwango vyetu na kwa kupitia juhudi zetu? Je, tunatakaswa kwa kuwa Mungu alikwisha safisha dhambi zote au kwa kuwa tunajaribu kutafuta ukombozi kwa njia zetu binafsi?
Kinachotutakasa si kingine ila imani ya kweli. Je, itawezekana kweli kufanya kaa jeusi kuwa jeupe kwa kusafisha sana hata mara elfu? Tutaweza kufanya ngozi nyeusi kuwa nyeupe kwa kuchovya? Hakuna kiasi chochote cha sabani au rangi ya kuchovya kitakachoweza kutakasa dhambi zetu, na haki yetu ni kama tambara bovu. Je, tunakuwa ni wenye haki kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake au kwa kuamini damu yake msalabani tu?
Imani ya kweli hutokana na maji ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Wokovu hauji kutokana na matokeo ya juhudi zetu. Ni imani yetu tu katika ubatizo wa Yesu na damu yake ndiyo itakayotuweka huru kwa dhambi zetu na kutufanya wenye haki.
Baba amewapa watu wote kupitia mkono wa Yesu, na wale wanaomwamini yeye uzima wa milele. Kumwamini Mwana maana yake ni ukombozi kupitia ubatizo na damu yake. Wale wote wenye kuamini watapata uzima wa milele wakiwa ni wana wa Mungu. Wale wote walio okolewa wataishi milele mkono wa kuume wa Mungu. Imani katika ubatizo wa Yesu na umoja wake katika Mungu pia ni imani katika Roho. Neno la ukweli huruhusu sisi kuweza kuzaliwa upya. Tumeokolewa kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake.
Uwe na imani. Kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake ni kupokea ukombozi. Uwe na imani ya injili ya kweli na upate msamaha wa dhambi.