Search

Sermoni

Somo la 8: Roho Mtakatifu

[8-11] Kutunza maisha yaliyo na ujazo wa Roho Mtakatifu ndani yako

(Waefeso 5:6-18)
“Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana kwa kuwa kwasababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasii. Basi msishirikiane nao kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza bali sasa mmekuwa nuru kwa kuwa tunda la uhuru ni katika wema wote na haki na kweli mkihakiki ni nini impendezayo Bwana. Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee kwa kuwa yanayo tendeka kwao kwa siri ni aibu hata kuyanena. Lakini yote yaliyo kemewa hudhihirishwa na nuru maana kila kilichodhihirika ni nuru. Hivyo husema amka wewe usinziaye, ufufuke katika wafu na Kristo atakuangaza. Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwasababu hiyo msiwe wajinga bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana, Tena msilewe kwa mvinyo ambamo mnaufisadi bali mjazwe Roho.”
 

Je inatupasa tufanye nini ili
tuyatunze maisha yetu yaliyo na
ujazo wa Roho Mtakatifu?
Yatupasa tuzikane nafsi zetu kubeba msalaba
na kuyakana mawazo ya uovu ndani 
yetu kujitolea katika 
kuihubiri injili.

Ili “kuyatunza maisha yaliyo na ujazo wa Roho Mtakatifu” ni lazima tujitolee katika kuihubiri injili. Ili kuishi maisha yaliyo na ujazo wa Roho Mtakatifu yatupasa kwanza kupokea baraka ambayo ndiyo huleta uwepo wa Roho Mtakatifu ndani ya mioyo yetu. Ili kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ni lazima tuwe na imani ambapo ni kuamini injili ya maji na Roho Mungu aliyotupatia na kwa kuwa na imani hii tutapokea baraka ambayo humfanya Roho Mtakatifu kuweka makazi ndani yetu.
Je, wale wote walio na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao wanahitaji ujazo wa Roho Mtakatifu maishani mwao? Bila shaka wanahitaji lakini kwanini sasa baadhi yao wanashindwa kuishi maisha hayo? Sababu ni kwamba shida zao huwekwa kipaumbele zaidi ya kazi za Mungu kwamaana hiyo hawawezi kutembea naye. Ili kutunza maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu yatupasa kujifunza na kuamini maneno ya Mungu. Kwanza ya yote hebu tuone katika Biblia ilitupate ni aina gani ya maisha na imani itupasayo kuwa nayo.
 

Ni kwasababu gani baadhi ya watu hawawezi kuishi maisha yaliyo na ujazo wa Roho Mtakatifu?

Kwanza tumeweza kusema kwamba ni kwasababu hawawezi kujikana. Biblia husema ni wale tu watakao jikana nafsi zao ndiyo pekee watakao tembea na Bwana kwa kuwa mafanikio ya maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu hayawezekani kwa njia ya nguvu binafsi. Basi kila mtu lazima awe na imani ya uwepo wa Roho Mtakatifu ili kujikana nafsi. Hata kwa wale wote walio na uwepo wa Roho Mtakatifu ni vigumu kwao hujikana nafsi zao pasipo kujihusisha na mambo ya Ufalme wa Mungu. Hivyo maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu yanatulazimu kuitumikia injili ya maji na Roho na ndipo tu hapo mtu atakapo ikana nafsi yake akiwa mtumishi wa haki.
Katika Mathayo 16:24-26 inasema “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake mtu yeyote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe ajitwike msalaba wake anifuate kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake ataipoteza na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona. Kwani atafaidi nini mtu akiupata ulimwengu wote na kupata hasara ya nafsi yake? Ama mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?”
Sababu ya baadhi ya watu walio zaliwa upya mara ya pili hawawezi kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu ni kwamba hushindwa kuzikana tamaa za miili yao. Hata wale walio na uwepo wa Roho Mtakatifu pia nao wataweza kuendelea kujazwa ikiwa tu watazikana tamaa za miili yao. Zipo nyanja nyingi za maisha ya kimwili ambazo ni lazima tuzikane ili kuweza kumfuata Bwana. Bwana alisema “Na ajikane mwenyewe ajitwike msalaba wake anifuate”.
Kufuata ya mwili ni mauti lakini kufuata ya rohoni ni uzima na amanini. Wale wenye kutamani kueneda katika roho imewapasa kuyakana maisha ya kimwili. Ni wale tu wanao thubutu kujitoa nafsi zao ndiyo watakao weza kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu. Huu ndiyo ukweli juu ya ujazo wa Roho Mtakatifu.
Kipi upendacho kufuata, kumfuata Bwana au dunia? Kulingana na uchanguzi wako maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu au maisha ya tamaa ni hiyari yako. Ikiwa kweli unataka kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu ni mapenzi yako. Mungu alituokoa toka dhambi zetu zote na kutupatia zawadi ya uwepo wa Roho Mtakatifu lakini hili ni hiyari yako kuchagua kati ya kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu au la! Kwa maneno mengine maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu Mungu hayaweki wala kuyachagua hatima yake mbeleni kwa ajili yako. Maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu hutegemea na utashi wetu sisi tunao iamini injili njema ya maji na Roho.
 

Nilazima uwe na utashi ili kuweza kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu. 

Ikiwa utakuwa na utashi wa kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu basi naye Mungu ataruhusu hilo. Atakusaidia na kukubariki lakini kama huna utashi, basi yakupasa kuachana na maisha hayo ya kujazwa na Rohoo Mtakatifu.
Utaweza kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ikiwa tu ni kwa imani katika injili ya maji na Roho na si kwa matakwa yako tu. Lakini kuishi na kutunza maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu kwa ujumla hutegemea utashi wa mtu mwenyewe.
Hivyo basi ikiwa unahitaji maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu ni lazima ujichunguze nafsi yako kwanza na kuomba msaada wa Mungu. Ikiwa kweli tunataka kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu basi Mungu atatubariki na kutimiza haja zetu. Lakini ili kufikia lengo letu ni lazima kukana tamaa za mwili.
Pili, ili kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu yatupasa kubeba misalaba yetu. Yatupasa kuishi na kuenenda kwa mapenzi ya Mungu hata katika hali ya taabu. Hii ndiyo maana halisi ya kuishi maisha ya haki yaliyo na ujazo wa Roho Mtakatifu.
Tatu, Bwana alisema “Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza na mtu atakaye iangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakaye isalimisha kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote kama akijiangamiza au kujipoteza mwenyewe?” Hii inamaana kwamba kumfuata Bwana ni muhimu zaidi kwa maisha yetu. Ukweli ni kwamba ikiwa tutamfuata yeye, roho na mwili uta sitawi kwa baraka zake lakini kinyume na hilo tusipomfuata na kuchagua kuishi maisha binafsi, roho zetu na miili yetu itaangamia.
Kwanini hatuwezi kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu? Sababu ni kwamba hatuyakani mawazo yetu ambayo ndiyo tamaa za mwili. Tunapomfuata Yesu Roho hututia nguvu ndani yetu na hivyo huweza kutuongoza kwa msukumo wa ajabu.
Katika Waefeso 5:11-13 inasema “Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza bali myakemee kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri ni aibu hata kuyanena lakini yote yaliyokemewa hudhihirishwa na nuru maana kila kilichodhihirika ni nuru”. Wakristo imewapsa wasiwe na usharika na matendo yasiyo zaa ya giza. Ikiwa tutajiingiza nafsi zetu katika matendo yasiyo zaa ya giza, Mungu anatuasa kuyaweka bayana. Yatupasa kukemewa kwa matendo yetu ya giza kwakuwa ni aibu hata kuyanenea kwa hayo yatendwayo sirini. Lakini mambo yote yanayo wekwa hadharani hutambulishwa kwa nuru.
Nani awezaye kuweka hadharani na kunena juu ya mambo yote haya ya aibu. Ikiwa wengine kaka au dada na watumishi wa Mungu hawatoweza kuyaweka bayana imekupasa wewe kufanya hivyo. Inasemekana kwamba mambo yote yanayo wekwa hadharani yanaonekana kwa nuru. Hivyo lazima tukiri matendo yetu maovu kuwa si mema na tuweze kuongozwa na Roho Mtakatifu katika kuyaweka wazi matendo yasiyo zaa ya giza kwa wenzetu au kwa kupitia viongozi wetu.
Katika ulimwengu huu vitu vyote vinavyo wekwa wazi huishia kuwa vilivyo hata baada ya kukemewa lakini katika ulimwengu wa Mungu yote yanayo wekwa hadharani huonekana kwa nuru kwa kuwa kila kinachowekwa hadharani ni kwasababu ya kuwepo nuru. Kwa kuwa tuko nje ya ukamilifu tunatenda dhambi nyingi bilakujitambua ulimwenguni. Hata hivyo, tunapo angaza kwa nuru ya maneno ya Mungu sisi wenyewe, tunakuwa makini nadhambi fulani na hivyo kuweza kuzikiri. Na hivyo basi tunaweza kumshukuru Mungu pasipo kikomo.
Kwasababu Yesu alizibeba dhambi zetu zote pamoja na uovu na hivyo haki yote ya Mungu ilitimizwa pale alipobatizwa Mto Yordani, sasa tunaweza kudhihirishwa kwa nuru kupitia haki ya Mungu. Mabilioni ya dhambi amabazo wanadamu hutenda zilihamishwa juu yake Yesu pale Yohana alipo mbatiza. Ni mwanakondoo wa Mungu aliyeichukua dhambi ya ulimwengu akafa msalabani kwa hukumu ya dhambi hizo na alifufuka. Yesu amesamehe dhambi zote za wanadamu na pale aliposema “imekiwsha” (Yohana 19:30) wanadamu wote waliokolewa. Tunatakaswa kwa njia ya imani yetu kwa kile Yesu alichofanya. Kwakuwa basi dhambi zetu zimekwisha kusamehewa tunaweza kurudi katika nuru tena na kumfuata Mungu kwa haki.
 

Mungu anatuasa kuukomboa Wakati.

Paulo alisema ikiwa tunataka kuishi maisha yaliyo na ujazo wa Roho Mtakatifu yatupasa kuukomboa wakati. Katika Waefeso 5:16-17 inasema, “Mkiukomboa wakati kwa maana zama hizi ni za uovu kwa sababu hiyo msiwe wajinga bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana”. Ikiwa tunataka kuishi maisha yaliyo ya ujazo wa Roho Mtakatifu yatupasa kuukomboa wakati na kutokuwa wajinga. Yatupasa kuelewa kwamba mapenzi ya Bwana ni yapi na kuyatenda. Lazima tuamue kipi ni cha thamani zaidi, maisha ya uaminifu kwa miili yetu au kujitolea kwa Mungu.
Baada ya kuzaliwa upya mara ya pili Roho Mtakatifu huweka makazi ndani yetu. Ikiwa tunapokea uwepo wa Roho Mtakafitu maana yake ni kwamba, Mkuu wetu ni Bwana na ndiye Mfalme. Yeye pekee ndiye Mwokozi wetu na yatupasa kumkiri yeye kwa hakika ndiye Mungu wetu. Yeye ndiye Mkuu pekee kwetu. Ni mkuu aliye niumba mimi aliye nisamehe dhambi zangu zote na kunibariki na ndiye Mfalme aliye na utawala juu ya maisha yangu na kifo changu baraka na laana. Yatupasa tukiri kwamba Bwana ndiye Mkuu pekee na ni Mungu hivyo imetupasa kumtii yeye maishani mwetu mwote.
Hebu tuone inasemaje katika Wafilipi 2:5-11 “Iweni na nia hiyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwemo pia ndani ya Kristo Yesu ambaye yeye mwanzo alikuwa yu namna ya Mungu naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa akawa ana mfano wa wanadamu tena alipoonekan ana umbo kama mwanadamu alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina ili kwa Jina la Yesu kila goti lipigwe, lavitu vya mbinguni na vya duniani na vya chini yanchi na kila ulimi ukiri kuwa YESU KRISTO NI BWANA kwa utukufu wa Mungu Baba”.
Paulo allisema “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu” Alisema huu ndiyo uliokuwa moyo wa Yesu Kristo. Kile Paulo alicho sema ni kwamba “nia iyo hiyo” ni ile ya Yesu aliyekuwa ndiye Mungu Muumba aliye kuja katika ulimwengu huu ili kuokoa watu wake tokana na dhambi zao tokana na mapenzi ya Baba yake. Bwana alikuja ulimwenguni na kubebe dhambi zote za dunia kwa njia ya ubatizo wake kwa Yohana, na alipokufa msalabani dhambi za duni zilifutwa naye ndipo alipo fufuka baada ya siku tatu na kuwa mwokozi wetu. 
Sababu kwanini Yesu Kristo Muumbaji kuja ulimwenguni ilikuwa ni kutuokoa. Alituonyesha upendo wake kwetu kwa njia ya ubatizo na damu yake pale msalabani viumbe wote imewapasa kupiga magoti mbele zake na kuthamini upendo wake aliotupatia, msamaha wa dhambi kwa kujishusha nafsi yake kama kiumbe ingawa yeye alikuwa ni Muumba na ndiyo maana viumbe wote imewapasa kukiri kwamba yeye ndiye Mwokozi wa kweli. Ametufanya tukiri kwamba yeye si Bwana tu wa viumbe vyote bali pia ni Bwana wa haki yote kwetu.
Sisi tunao mwamini Mungu na kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yetu imetupasa kuamini kwamba “Mungu ndiye pekee moyoni mwetu. Yatupasa kuwa na imani kwamba mkuu wetu si nafsi zetu bali ni Yesu Kristo aliye tuumba na kutuokoa tokana na dhambi zetu zote. Napia lazima tuwe na imani kwamba yeye ni Mkuu anayetuwezesha kuishi maisha mapya ya baraka na kutayarisha kila kitu kwetu na kutuwezesha.
Wapo watu wengi wasiotaka kumbadilisha mkuu wao baada ya kuzaliwa upya mara ya pili. Wapo wengi walio na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao lakini huendelea kuwa mkuu wa nafsi zao. Maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu ni maisha ya kumfuata Mungu. Maisha ya aina hii hayawezi kupatikana kwa siku moja bali yanawezekana pale tu tunapo amini kwamba Yesu ndiye Mkuu wa maisha yetu na ndiye pekee aliye tuumba sisi na viumbe wote ulimwenguni. Yatupasa tuwe na imani ili tuweze kumtumikia Yesu Bwana wetu Mkuu wetu na Mungu kwetu aliye tuokoa tokana na dhambi zetu na kutupa uzima wa milele katika ufalme wa Mbinguni.
Yatupasa kuwa na ukweli katika mawazo yetu. Watu wengi huishi maisha ya kuwa wakuu wa nafsi zao. Hulinda na kutunza utawala wa nafsi zao maishani. Lakini leo ndiyo wakati wa kumbadilisha mkuu. Sasa tumekuwa wale wamjuao Mungu na hivyo Mkuu wetu muhimu ndiye Bwana.
Sisi sote tuna dhambi mioyoni mwetu na imetupasa kuhukumiwa kwenda motoni kwa matendo yetu maovu. Lakini leo nimempata Mungu kwa njia ya imani katika injili ya maji na Roho. Mungu anatupenda sana hata kuja ulimwenguni na kubeba dhambi zetu zote kwa kubatizwa na Yohana na kufa msalabani ili kuweza kuwa mwokozi wetu na kwakupitia imani yetu kwa Mungu tulikombolewa tokana na dhambi zetu. Kwa maneno mengine, tulipokea uwepo wa Roho Mtakatifu.
Biblia husema “Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake” (Warumi 8:9). Tulipopokea ukombozi wake ambapo ni uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yetu, ndipo hapo tukawa watoto wa Mungu. Roho Mtakatifu ni Mungu kwetu na lazima tuenende katika haki ya Mungu kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu. Ili tuweze kuishi kwa namna hii yatupasa tuache kutawala nafsi zetu. Tulipo kutana na Yesu na kutukomboa yatupasa sasa kumfanya awe Mkuu kwetu.
 
 
Yatupasa kusalimisha madhabahu ya mioyo yetu kwa Yesu

Hatutoweza kumfuata Bwana ikiwa hatutojichukulia nafsi zetu kuwa ndiyo bwana wa maisha yetu. Mungu anapotuamuru kumtumikia tutaitika tukisema “Ndiyo” pasipo kusita. Ikiwa tunatawaliwa na nafsi zetu kwa namna nyingine tutaweza kusema “kwanini nikubali?” Mtu anaye tawaliwa na nafsi yake atakataa kufanya kile Mungu atakacho mwagiza kufanya akidhani “Imempasa Mungu kuomba msaada kufanya atakalo”. Kwa mtu wa aina hii maelekezo ya Mungu si kitu bali ni upuuzi na maneno ya kuchosha.
Hata hivyo ili kujazwa Roho Mtakatifu imetupasa kutii maelekezo yake. Hatutaweza kuwa kama ng’ombe wanao swagwa kwenda machinjioni bali nilazima tujitolee kumfuata Mungu. Yatupasa kumfuata Mungu Mwokozi wetu ambaye hutuongoza katika njia ya haki. Mungu ni Bwana anayetubariki kwa wokovu tunapo mtumikia akiwa ni Mkuu kwetu. Na kwa kufuata kanuni zake, ndipo tutakapo weza kujazwa na Roho Mtakatifu ikiwa wewe na watu wa familia yako mtakapo mfanya Yesu kuwa mfalme na kumweka juu ya vitu vyote. Hivyo mtakuwa na neema na baraka katika maisha yenu.
Inawezekana umekwisha wahi kuona picha kama ya mtu anaye safiri kwa chombo baharini huku akipata upinzani wa dhambi huku Yesu akiwa amesimama karibu naye. Inapoonekana kwamba tunayamudu matatizo katika maisha yetu nikwakuwa tumemfanya Kristo ndiye atuongozaye na kutushika mkono. Ni Mwenyezi Mungu ndiye aongozaye maisha yetu. Alituokoa, hutukinga na shetani, kutuongoza na ndiye aliye na mamlaka katika maisha yetu. 
Kwakuwa amekuwa Mkuu kwetu anayo mamlaka ya kutuongoza na kutubariki. Lakini tusipo mtambua kwamba yeye kuwa ni Mwokozi wetu, hatoweza kufanya jukumu lake. Ni Mungu mwenye utashi, asiye tulazimisha kutenda mapenzi yake. Ingawa yeye ni Mungu Mwenye enzi hafanyi mambo kwa niaba yetu hadi pale tutakapo jitolea kumtumikia akiwa ni Mkuu na kuomba msaada.
 

Mtwike mambo yako yote kwake

Mtwike mambo yako yote kwake ili aweze kutimiza miujiza. Mtumikie na ukiri kwamba ni mkuu. Kwakuwa sisi si wakamilifu, imetupasa kumtwika Mungu mambo yetu yote na kumkabidhi jukumu lote kwake. Tunapo mwachia familia zetu maisha ya kila siku na kila kitu juu yake tutapokea hekima toka kwa Mungu na kuweza kuishi kama atakavyo kwa kumudu shida zote kwa imani na nguvu ambayo Mungu alizotupatia.
Matatizo yetu ndipo huwa ni ya Mkuu wetu ambapo ikiwa tunamfuata Yesu mwenyeenzi Mungu atachukua jukumu kwa niaba yetu. Hapa ndipo tutakapoweza kuishi maisha yaliyo jaa uwepo wa Roho Mtakatifu na kufurahiya amani inayotoka kwake. Kama Mkristo mwaminifu imetupasa kunyenyekea kwa magoti mbele ya Mungu kukiri na kumtumikia yeye kama Mkuu wetu.
Hebu tuone nini Wafilipo 3:3 inasema juu ya aina ya imani inayotupasa kuwa nayo ili kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifi “Maana sisi tu tohara tumwabuduo Mungu kwa Roho na kuona fahari juu ya Kristo Yesu wala hatuutumaini mwili”. Maana ya “tohara” hapa ni yule anayemwabudu Mungu katika Roho kuona fahari juu ya Kristo Yesu na kutouamini mwili.
Kuishi kama aliyetahiriwa maana yake ni kuondolea mbali dhambi zote za moyoni na kumtwika Yesu Kristo aliyebatizwa na Yohana. Wale waongozwao na roho maisha yao huwa juu ya roho, humtumikia Mungu na kumfurahiya Kristo Yesu kwa kusema “Yesu ameniongoza kuishi maisha haya ya utukufu, alinifanya mwenye haki na kunibariki, alinipa neema zote ninazozihitaji katika kumtumikia yeye”. Imetupasa kuishi kwa namna hii. Haya ndio maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu. Paulo alisema “basi mlapo au mnywapo au mtendapo neno lolote fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu” (1 Wakorintho 10:31). 
Katika Wafilipi 3:13-14 inasema “Ndugu sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika ila natenda neno moja tu nikiyasahau yaliyo nyuma nikiyachuchumilia yaliyo mbele nakaza mwendo niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu”. Mungu alituambia tusahau yale mambo ambayo ni yanyuma yakiwa yamepita na kuyafikia yale ya mbeleni. Yatupasa kuchuchumilia malengo yetu. Ukiachilia mbali matendo yetu ya haki au maovu imetupasa kusahau mambo yale ya nyuma na kujaribu kuyafikia yale ya mbeleni na kuchuchumilia malengo yetu. Malengo hayo ni kuyatumikia mapenzi yake kwa kujishika na Yesu Kristo kwa njia ya kumwamini.
Sisi si wakamilifu hivyo ni rahisi kwetu kuanguka tunapo hisi kitanzi cha mwili. Hata hivyo kwa kumtumaini Mungu na kuwa na imani tutaweza kumbwagia udhaifu wetu wote na uovu wetu. Yesu alipo batizwa na Yohana na kufa msalabani, dhambi zetu zote zilitwikwa juu yake ndipo tulipo pokea uzima mpya kwa shukrani kwake. Hivyo imetupasa kumwachia mambo yetu yote ya nyuma kufikia ya mbeleni kwa kuchuchumilia lengo letu.
 
 
Kutunza maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu. 

Lazima tuyafikie mambo yale ya mbeleni na kukazia lengo la juu. Natumaini utaweza kusahau ya nyuma haraka iwezekanavyo ikiwa yamekuelemea. Yapo mambo mengi ambayo hayawezi kufanyika kwa sababu ya udhaifu lakini hayana maana kwasababu kilicho muhumu kutegemea zaidi yaliyo mbeleni. Kwajinsi mbeleni yalivyo muhimu imetupasa basi kumwachia ukanda Yesu Kristo kwa imani na hivyo kuongozwa naye. Imetupasa kumwachia yeye uamuzi wa namna tutakavyo ishi katika majaliwa yetu na hivyo kufanya atakayo.
 

Imetupasa kuishi namna ile wafuasi walivyo ishi

Tunaweza kuenenda maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu ikiwa tutaweza kuwa madhubuti katika imani ya ondoleo la dhambi. Hili ndilo muhimu. Hebu tuone (2 Timotheo 2:1-10) “Basi wewe mwanangu uwehodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu na mambo yale uliyo yasikia kwangu mbele ya mashaidi wengi hayo uwakabidhi watu waaminfu watakaofaa kuwafundisha na wengine. Ushiriki taabu pamoja nami kama askari mwema wa Kristo Yesu. Hakuna apigae vita ajitiaye katika shughuli za dunia ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari. Hata mtu akishindana katika michezo hapewi taji asiposhindana kwa halali. Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza wa kupata fungu la matunda. Yafahamu sana hayo nisemayo kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote. Mkumbuke Yesu Kristo aliye fufuka katika wafu wa uzao wa Daudi kama inenavyo injili yangu. Nami katika hiyo nimeteswa hata kufungwa kama mtenda mabaya, lakini neno la Mungu halifungwi kwa ajili ya hilo na stahilimili mambo yote kwa ajili ya wateule ili wao nao waupate wokovu ule ulio katika Kristo Yesu pamoja na utukufu wa milele”.
Kama Paulo alivyosema kwa Timotheo, Roho Mtakatifu anasema kwetu pia “Uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu na mambo yale uliyo yasikia kwangu milele ya mashaidi wengi hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine”.
“Uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu”. Kuwa hodari katika neema maana yake imekupasa kujitia nguvu imani katika injili ya maji na Roho kwa kumwamini yeye na kumshikilia Yesu Kristo aliyekuja hapa ulimwenguni kuzikubali dhambi zote kwa njia ya ubatizo, kufa msalabani na alifufuka na kuwa mwokozi wetu. Hii ina maana kwamba imetupasa kuwa hodari katika neema ya Mungu na kumshukuru yeye Mungu aliyetuokoa na hivyo imetupasa kuukimbilia wokovu huo kwa njia ya imani kama ni zawadi au karama ya Mungu. Huu ndiyo wokovu wa msamaha wa dhambi. Haihusishwi na swala la kufanya maombi kila asubuhi na mapema au kutoa mchango wa ujenzi wa jengo la kanisa, yote haya ni mambo yaletayo hasara zaidi kuliko faida kwa nia ya kupata wokovu.
Wokovu wetu kwa njia ya kupokea msamaha wa dhambi maana yake ni Yesu Kristo, ukiachilia mbali matendo yetu, aliweza kubatizwa ili kubeba dhambi zetu zote ndipo akafa msalabani ili kufuta makosa yetu yote. Alifufuka ili kutuokoa sisi tokana na dhambi zetu zote. Wachungaji husamehe watu dhambi zao nao kwa kuamini injili ya kweli kama ilivyo waumini wengine wa kawaida. Yeyote anaye mwamini Yesu Kristo kwa njia hii kwa moyo wake wote hupokea msamaha wa dhambi. Tunaweza hata hivyo kuwa na uhakika na neema hii ya wokovu na hata kutia imani yetu nguvu.
Ikiwa tunataka maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu imetupasa kuwa hodari katika imani yetu ya injili ya maji na Roho. Yapo maeneo katika maisha yetu ambapo tunashindwa kujipima na hivyo kuwa ni sehemu ya udhaifu wetu. Na ndiyo maana imetupasa kuwa hodari katika neema ya wokovu. Kila wakati mawazo yetu yanapojitokeza imetupasa kuwaza kwa kina juu ya imani yetu kwa kusema “Mungu aliniokoa kwa kupitia injili ya maji na Roho” “Yesu alinisamehe dhami zangu zote kwa njia ya maji na Roho”. Tunakuwa wenye haki kwa kuamini injili na kuwa hodari kwa kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yetu. Tuliokolewa kwa dhambi zetu zote na kuwa hodari kwa kuamini injili ya maji na Roho. Tunakuwa watu tulio barikiwa kwa imani zetu.
Paulo alisema “Basi mlapo au mnywapo, au mtendapo neno lolote fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu” (1 Wakorintho 10:31). Hili ni muhimu sana maana yake ni kwamba lazima tuamue maisha ya kujitolea kwa Mungu. “Basi Mlapo au mnywapo” Imetupasa kula, kunywa nakuwa hodari kwa Mungu ili tuweze kuzifanya kazi zake. Imetupasa tule vitu bora kwa ajili ya afya zetu ili tuweze kuihubiri injili.
“Hakuna apiganaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari” (2 Timotheo 2:4). Imetupasa kuishi maisha yaliyo jaa Roho Mtakatifu ili kuweza kuihuiri injili. Tutaweza kuishi maisha ya kweli pale tu tutakapo ishi kwania ya kuihubiri injili. Wale wote wanao ishi maisha ya uaminifu ndiyo walio jazwa na Roho Mtakatifu. Imetupasa kuyachuchumilia maisha ya kujazwa Roho Mtakatifu. Hata swala la kutoa sadaka ambayo ni matunda ya kazi yako inapaswa kutumika kwa ajili ya injili.
Ikiwa unataka kudumisha maisha kamili ya Roho Mtakatifu, lazima ujitoe kwa Bwana, uwe katika huduma Yake, tumia pesa zako kwa injili na ushiriki furaha yako na huzuni zako na Mungu. ikiwa tunataka kuishi maisha ya aina hii, lazima tuishi kwa imani na nia thabiti ya kuitumikia injili
Watu wengi wamekuwa wakiishi maisha ya ubinafsi hata sasa. Wamejiwekea wigo na hata kujikusanyia mali kwa ajili ya nafsi zao ambazo ndizo kiongozi wao. Hata hivyo leo hii imetupasa kuishi kwa ajili ya Mungu. Imetupasa kumweka Mungu kuwa ndiye pekee na Mkuuu pekee. Bwana anasema “Hakuna apiganaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia ila ampendeze yeye aliye mwandika awe askari”. Kuishi maisha ya askari hodari maana yake ni kufuata kanuni. Bwana hutatua matatizo yetu, kutukinga na kutuongoza ikiwa tutaishi kwa ajili yake tukiwa askari waaminifu. Anatuambia tutafute kwanza ufalme wa Mungu na haki yake (Mathayo 6:33).
Hakuna ulaghai katika neno la Mungu. Ikiwa tutamfuata yeye tutaona ukweli wa neno lake, lakini kumbuka kwamba kwanza imekupasa uwe na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani ya moyo wako. Mtu asiye na uwepo wa Roho Mtakatifu kamwe hatoweza kumkabidhi Mungu nafsi yake. Kwa upande mwingine yule aliye na uwepo wa Roho Mtakatifu ataweza kumkabidhi Mungu nafsi na moyo wake na hivyo kushuhudia ujazo wa Roho Mtakatifu na kuwa na furaha na amani moyoni mwake.
Uwepo wa Roho Mtakatifu ndani huja kwa hakika ndani mwako ikiwa tu utaelewa na kuamini Injili njema ya maji na Roho. Ikiwa unataka kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu na hata kuishi maisha yenye baraka imekupasa kumtumikia Mungu akiwa Mfalme na kuishi maisha yako kwa ajili ya ufalme wake. Ndipo basi utakapo jazwa na Roho Mtakatifu na moyo wako kuweza kuwa na utele na baraka ya maisha itaendelea kwa jinsi utakavyo kuwa katika baraka ile ya kuwa mwana wa Ufalme wa Mungu.
Nimekwisha leta ujumbe ambao watu walio pokea wokovu wa dhambi na uwepo wa Roho Mtakatifu kwa kuamini Bwana imewapasa kuenenda katika maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu. Tayari nimekwisha eleza juu ya maisha ya kujazwa Roho Mtakatifu na pia ni kwa jinsi gani aina hii ya maisha yanaweza kutunzwa. Pia nimekwisha elezea kwamba kwa imani imekupasa kumkabidhi nafsi yako Bwana na kwa imani ni lazima umtumike yeye na kutunza maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu.
Kwa mara nyingine tena kwa yule aliye na ujazo wa Roho Mtakatifu swala la kuzaliwa upya mara ya pili si kikomo. Imempasa kujua na kuamini kwamba Roho zetu na miili yetu itaweza kubarikiwa ikiwa tu tutaishi maisha ya aina hii.
Aina hii ya maisha hayatokei kwa ghafla. Hutokea pale tu tunapo mwamini Bwana akiwa Mkuu na kumweka nafasi ya mbele katika mioyo yetu. Mungu alituokoa na tayari amekwisha tupatia uzima ulio jaa uwepo wa Roho Mtakatifu, maisha ya kuitumikia Injili. Pia ametupatia maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu.
Imekupasa kuitoa nafsi yako kwake na kuishi maisha kwa ajili yake. Kumtumikia kwa kuihubiri Injili njema. Ndipo basi moyo wako utakapo jawa na uwepo wa Roho Mtakatifu na furaha na neema itatiririka ndani mwako. Katika siku ya kurudi kwake utabarikiwa, ukisimama kifua mbele za Mungu na kuipata thawabu yake. Mimi na wewe imetupasa kuyatamani maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu. Imetupasa kuyahangaikia katika kuishi maisha ya aina hii kwa njia ya imani. Hivi ndivyo maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu yanavyoweza kutunzwa.
Je umekwisha kabidhi nafsi yako moyoni ili iweze kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu? Natumaini utamwachilia Mungu ashikilie sehemu kubwa ya moyo wako. Yakupasa uwe na utashi wa kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu.