Search

説教集

Somo la 10: Ufunuo (Ufafanuzi juu ya Ufunuo)

[20-2] Tutawezaje Kupita Toka Mautini Kwenda Uzimani? (Ufunuo 20:1-15)

(Ufunuo 20:1-15)
 
Mungu anatueleza kwamba wakati atakapoufanya ulimwengu huu kutoweka na kisha kutupatia Mbingu na Nchi Mpya, basi atamfufua kila mwenye dhambi aliyewahi kuishi hapa duniani na atakayekuwa amelala katika kaburi lake. Aya ya 13 inasema, “Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake.” Mwili wa mwanadamu unaozama katika maji mara huliwa na samaki, na mwili wa mwanadamu aliyeungua hadi kufa mwili wake mara nyingi utakuwa hauna umbile lolote la kuweza kutambuliwa na yeyote. Hata hivyo, Biblia inatueleza kwamba nyakati za mwisho zitakapowadia, Mungu atawafufua watu wote kurudi na kuwa hai na kisha atawahukumu ili kuwapeleka Mbinguni au kuzimu, hii haitajalisha ikiwa watakuwa wamemezwa na Shetani au la, au ikiwa watakuwa wameuawa na Jehanamu, au ikiwa watakuwa wameunguzwa na moto. 
Kabla Mungu hajakiweka Kitabu cha Uzima, ambamo majina ya wale watakaoingia katika Ufalme wa Mbinguni yameandikwa. Pia pale kuna Kitabu cha Matendo, ambacho kina majina na dhambi ya wale wote ambao watatupwa kuzimu. Dhambi zote ambazo mtu amezifanya alipokuwa anaishi hapa duniani zimeandikwa katika Vitabu vya Matendo. Mambo haya yote yamepangwa na Mungu kwa mujibu wa majaliwa yake.
 
 
Bwana Ana Vitabu vya Aina Mbili
 
Mungu amekwisha wapanga watu katika makundi mawili tofauti kulingana na vigezo vyake vya haki. Mungu amekwisha panga kwamba wafu wote watafufuliwa, na kisha watasimama mbele ya vitabu vyake viwili na kisha kuhukumiwa. Katika Kitabu cha Uzima yameandikwa majina ya wale to waliomwamini Yesu wakati walipokuwa hap aduniani, wakapokea ondoleo la dhambi zao, na kwa sababu hiyo wamepangiwa kuingia Mbinguni. Hivyo, hukumu ya Mungu ya mwisho itategemea mtu anaangukia katika kitabu gani, yaani jina lake limeandikwa katika kitabu gani. Kwa maneno mengine, Mungu amekwishapanga ni akina nani wataingia Mbinguni na akina nani watatupwa kuzimu. 
Hivyo, Mungu atawainua wafu wote ili waweze kuishi tena, atavifungua Vitabu vyake, na kisha ataangalia majina yao yameandikwa katika kitabu gani kati ya hivyo viwili. Kisha atawapeleka Mbinguni wale ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Uzima, lakini wale ambao majina yao hayataonekana katika Kitabu cha Uzima, atawatupa kuzimu. Ni lazima tuhakikishe kwamba tunaifahamu na kuuamini ukweli huu ulioanzishwa na Mungu. 
Mungu atawafufua wafu wote na kisha kuwahukumu ili kuamu ni akina nani watakwenda Mbinguni na akina nani watakwenda kuzimu. Imekwisha amuliwa kwamba Mungu atawahukumu watu kwa kuzingatia ikiwa majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Uzima au katika Vitabu vya Matendo (yaani Vitabu vya Hukumu). 
Kuna sehemu mbili ambazo Mungu amezitayarisha kwa ajili ya wale wote ambao watasimama mbele zake. Sehemu hizo si nyingine bali ni Mbinguni na kuzimu. Kuzimu ni ziwa la moto ambako moto na kibiriti vinawaka. Mungu ameazimia kwamba wale ambao majina yao hayajaandikwa katika Kitabu cha Uzima watatupwa katika ziwa la moto, wakati wale ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Uzima watakaribishwa Mbinguni. 
Huko Mbinguni, Mti wa Uzima upo pembeni mwa mto wa maji ya uzima, unazaa matunda kumi na mbili tofauti kulingana na kila muhula. Katika Mbingu hii nzuri, watakatifu hawataugua wala kuona maumivu, bali wataishi kwa furaha milele pamoja na Mungu. Tunapaswa kuuamini ukweli kwamba Mungu ameamua kuwapatia watakatifu hii Mbingu. 
Kwa upande mwingine, wale wasiomwamini Yesu, majina yao yameandikwa katika Vitabu vya Matendo. Kwa kuwa matendo yote ambayo wenye dhambi wameyatenda wakati wakiwa hapa duniani yameandikwa vitabu hivi, basi ndio maana Mungu anatueleza kwamba atawatupa wenye dhambi hao wote katika ziwa la moto, ili kuwaadhibu kwa ajili ya dhambi zao zilizoandikwa katika Vitabu hivi, pia atawaadhibu kwa sababu ya kutomwamini Yesu. Jambo la msingi hapa ni ule ukweli kwamba majina yenu yameandikwa katika Vitabu gani. 
Tunapoishi hapa ulimwenguni, tunapaswa kutambua kwamba maisha hapa duniani si kila kitu. Kama vile Zaburi ya 90:10 inavyotueleza, “Siku za miaka yetu ni miaka sabini, na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; na kiburi chake ni taabu na ubatili, maana chapita upesi tukatokomea mara.” Hata kama tutaishi katika dunia hii kwa miaka 70 au miaka 80, ukweli ni kwamba muda si mrefu tutasimama mbele ya Mungu. Na hatimaye tutakaposimama mbele za Bwana wetu, basi jambo la msingi hapo ni kwamba majina yetu yameandikwa katika Kitabu gani, ama katika Kitabu cha Uzima au katika Vitabu vya Matendo (Vitabu vya Hukumu), kwa kuwa hilo ndilo litakalo amua ikiwa tunakaribishwa Mbinguni au tunatupwa katika ziwa la moto. Tunapaswa kutambua kwamba maisha hapa dunini si kila kitu. 
 

Wale Ambao Majina Yao Yameandikwa Katika Kitabu cha Uzima
 
Hebu tuangalie Luka 16:19-26: “Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.”
Kwa kifungu hiki, Yesu anatufundisha kwamba ni kweli kuwa Mbingu na kuzimu vipo. Kama alivyo mtu tajiri katika kifungu hiki, vivyo hivyo watu wengi hawaamini juu ya uwepo wa Mbingu na kuzimu. Ibrahimu ni baba wa imani. Kifungu hiki kinaposema kwamba yule masikini Lazaro alipelekewa kifuani mwa Ibrahimu, maana yake ni kwamba kama vile Ibrahimu alivyoliamini Neno la Mungu, vivyo hivyo Lazaro pia alimwamini Yesu kuwa ni Mwokozi wake, akapokea ondoleo la dhambi zake, na hivyo akaenda Mbinguni. Tunapoishi hapa ulimwenguni, tunapaswa kutafakari juu ya hatma ya Lazaro na yule mtu tajiri. 
Mungu anatueleza kwamba kila mtu hapa ulimwenguni, anapaswa kufahamu kwamba maisha si kila kitu kabisa. Haijalishi kamba mtu anafanya kazi gani hapa duniani, ukweli ni kuwa mtu huyo hataweza kuishi zaidi ya miaka 70-80, lakini hatimaye kitakachobakia kwa mtu huyo ni kiburi na huzuni. 
Hivyo, tunapoishi maisha yetu ni lazima tujiandae kwa ajili ya yatakayojiri baada ya maisha haya. Pia tunapaswa kuirithisha imani yetu kwa watoto wetu, ili kwamba na wao waweze kwenda mahali pazuri. Je, halitakuwa jambo la kuhuzunisha kuona kuwa mtu ameishi hapa duniani hatimaye anasimama mbele za Mungu na kisha kuhukumiwa na kutupwa katika ziwa la moto? 
Hakuna mtu anayeweza kubadili kile ambacho Mungu amekiamua, yaani kwamba wale ambao majina yao yameandikwa katika Vitabu vya Matendo watatupwa katika ziwa la moto. Hivyo kuna njia moja ya tu kwetu sisi ili tuweze kulikwepa ziwa la moto, na njia hiyo ni kuhakikisha kwamba majina yetu yanaandikwa katika Kitabu cha Uzima. Hakuna njia nyingine ya kuweza kulikwepa ziwa la moto zaidi ya majina yetu kuandikwa katika Kitabu cha Uzima. 
Sasa, majina yetu yanawezaje kuandikwa katika Kitabu cha Uzima? Kama ambavyo Lazaro alivyochukuliwa hadi katika kifua cha Ibrahimu, vivyo hivyo sisi nasi ni lazima tupokee ondoleo la dhambi zetu kwa kulifahamu na kuliamini tendo la Mungu la haki (Warumi 5:18) kwa kupitia Neno lake. Ni hapo tu ndipo tunapoweza kuingia Mbinguni. Ili majina yetu yaweze kuandikwa katika Kitabu cha Uzima, ni lazima tumwamini Yesu. Yesu ni Mungu Mwenyewe na Masihi wetu. Masihi maana yake ni Yeye anayewaokoa wale walioanguka katika dhambi. Ni Yesu tu ndiye anayeweza kutuokoa sisi ambao kwa sababu ya dhambi tumefungwa ili kuhukumiwa na Mungu na kisha kutupwa katika ziwa la moto. 
Ni nani hapa duniani ambaye hawezi kutenda dhambi kabisa mbele za Mungu, na ni nani miongoni mwetu ambaye matendo yake kwa asilimia 100 ni matakatifu? Hakuna hata mmoja! Tunapaswa kutambua kwamba kwa kuwa sisi sote tuna mapungufu mengi, basi ni kweli kwamba hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kuanguka katika dhambi, na kwa sababu ya dhambi hizi tumefungwa ili kutupwa katika ziwa la moto. 
Lakini Mungu alimtuma Yesu kuja hapa duniani ili kutuokoa, sisi ambao hatukuweza kufanya lolote zaidi ya kutupwa katika ziwa la moto kwa sababu ya dhami zetu. Jina ‘Yesu’ maana yake ni ‘Yeye atakayewaokoa watu wake toka katika dhambi zao’ (Mathayo 1:21). Hivyo, tunaweza kuingia Mbinguni pale tu tunapoamini katika ukweli kwamba Yesu alikuja hapa duniani na akatuokoa toka katika dhambi zetu zote kwa tendo lake la haki. 
 

Ni Akina Nani Watakaotupwa Katika Ziwa la Moto? 
 
Ufunuo 21:8 inatueleza juu ya wale ambao watatupwa katika ziwa la moto: “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.” 
Kwanza kabisa, Biblia inapotumia neno “waoga” ina maanisha akina nani? Hii ina maanisha ni wale Wakristo wa mazoea ambao wameshindwa kupokea ondoleo la dhambi zao kwa kupitia injili ya maji na Roho, na kwa sababu hiyo wanaogopa wanapokuwa mbele za Mungu pamoja na kuwa wanamwamini Yesu kwa kiasi fulani. Mungu ameamua kwamba watu wa jinsi hiyo watatupwa katika ziwa la moto. Pia Mungu ameazimia kwamba wale wasioamini, wenye machukizo, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, na waongo wote hao watatupwa kuzimu. 
Kwa asili, kumekuwapo na waabudu sanamu wengi sana nchini Korea. Hata sasa, si ajabu kuona watu wakiabudu sanamu za vitu ambavyo ni uumbaji wa Mungu na kisha kutoa maombi kwa sanamu hivyo. Watu wanafanya hivyo kwa sababu ni wajinga na wapumbavu. Mungu anachukia kuona watu wakiabudu vitu visivyo na uhai kana kwamba ni Mungu. 
Mungu alimuumba mwanadamu kwa sura na mfano wake (Mwanzo 1:27). Mwanadamu pia ndiye msimamizi wa uumbaji wote. Hii ndio sababu ni lazima tumwamini Mungu. Kwa kuwa tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, basi sisi tunaishi milele, kama vile Mungu Mwenyewe anavyoishi milele. Upo ulimwengu wa milele kwa ajili yetu mara baada ya kifo. Hii ndio sababu Mungua ametueleza kumwabudu yeye, aliye Mungu wa milele. Nini kitatokea pale tunaposujudia vitu ambavyo ni uumbaji wa Mungu mwenyewe? Tutakuwa tunafanya dhambi kuu dhidi ya Mungu, kwa kuwa tutakuwa tunafanya kile ambacho Mungu anakichukia zaidi: yaani uabudu sanamu. Mwanadamu anaweza kuwa mjinga kiasi hicho na mpumbavu. Tunapaswa kutambua kwamba Mungu ameamua kwamba wale walio na imani hii iliyopotoshwa watatupwa wote katika ziwa la moto. 
Watu wanaotupwa kuzimu watakufa mara mbili. Hivi ndivyo Mungu alivyoazimia. Mauti ya kwanza inakuja mwishoni mwa maisha yao yenye shida hapa duniani, baada ya kutembea katika ulimwengu uliochoka. Mara nyingi husemwa kwamba wale wanaoishi na kutembea mwanzoni kwa kutumia miguu minne, kisha wakatumia miguu miwili, na hatimaye wakatumia miguu mitatu, na mwishowe kufa, si wengine bali ni wanadamu wenyewe. 
Baada ya kufa mara moja kwa njia hii ya kawaida, basi watu watakaposimama mbele ya Mungu kama wenye d hambi, basi watakabiliana na hukumu yao, na ni wakati huu ndipo watakapokutana na mauti ya pili, mauti ambayo haitakoma bali itadumu milele kwa wao kutupwa katika ziwa la moto. Kama wangelikufa katika hili ziwa la moto basi wangekuwa wamewekwa huru toka katika mateso ya hilo ziwa. Lakini wakiwa katika ziwa hili, basi hata kama watatamani kufa, kifo kitawakimbia. 
Kila mtu anatamani kuishi milele, ili asiweze kukutana na kifo kamwe. Ukweli ni kuwa uwepo wa mwanadamu ni wa milele kama vile watu wanavyotamani. Hii ndio maana wakati mtu anapokufa Biblia haisemi kuwa mtu huyo amekufa, bali inasema kuwa mtu huyo amelala. Hivi sisi sote ni lazima tuikwepe mauti ya pili ambayo itatutupa katika ziwa la moto. Sisi sote tunapaswa kufahamu tunachopaswa kukifanya ili majina yetu yaweze kuandikwa katika Kitabu cha Uzima. Na ili majina yetu yaweze kuandikwa katika Kitabu cha Uzima, basi tunapaswa kumwamini Yesu kiusahihi. 
Mara nyingi watu wanafikiri na kusema kwamba Yesu, Budha, Konfusiasi, na Muhamad wote hao ni watu wa kawaida, na kwamba kinachotakiwa ni kuishi ukiwa mtu mwema. Hii ndio sababu hawawezi kuelewa ni kwanini tunakazia kwamba wanapaswa kumwamini Yesu peke yake. Lakini mawazo haya ni potofu. Wewe na mimi, pamoja na vitu vingine vyote hapa ulimwenguni, si chochote zaidi ya uumbaji na wanadamu mbele za Mungu. Lakini tunapoangalia kuzaliwa kwa Yesu na yale ambayo ameyakamilisha alipokuwa hapa duniani, basi sisi sote tunaweza kutambua kwamba Yeye si mwanadamu wa kawaida kama walivyo hawa wanadamu wenye Hekima. Yeye ni Mungu Mwenyewe, ambaye ili kuwaokoa wanadamu alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, akazichukua dhambi zetu zote kwa kupitia ubatizo wake, akaipokea adhabu yote ya dhambi zetu kwa niaba yetu, na hivyo akaitimiza kazi yake ya kuwakomboa wanadamu toka katika dhambi. 
Kuzaliwa kwa Kristo kulikuwa tofauti kabisa na kuzaliwa kwa wanadamu wa kawaida. Watoto wanazaliwa kwa muungano wa mwanamume na mwanamke. Hivi ndivyo kila mtu anavyozaliwa hapa duniani. Lakini Yesu alizaliwa kwa bikira ambaye hakuwa amemjua mwanamume. Yesu, ambaye ni Mungu Mwenyewe alizaliwa hapa duniani katika mwili wa mwanadamu kwa kupitia mwili wa bikira ili kutuokoa wanadamu, na ili kulitimiza Neno la unabii lililokuwa limenenwa zaidi ya miaka 700 iliyopita kwa kupitia Nabii Isaya (Isaya 7:14). Na alipokuwa hapa duniani sio tu kwamba aliwafufua wafu na kuwaponya wagonjwa na waliokuwa walemavu, bali alizifanya dhambi zote za ulimwengu kutoweka. 
Mungu, Bwana wa uumbaji aliyeuumba ulimwengu wote, alikuja hapa duniani na akafanyika kuwa mwanadamu kwa kitambo kifupi, alifanya hayo yote ili kuwaokoa wanadamu toka katika dhambi zao zote. Sababu inayotufanya tumwamini Yesu ni ule ukweli kwamba Yesu ni Mbungu Mwenyewe. Pili, ni kwa sababu Yesu alizichukulia mbali dhambi zetu zote, ili kwamba majina yetu yaweze kuandikwa katika Kitabu cha Uzima, na akatufanya sisi kuwa watoto wa Mungu tusio na dhambi. Tunapozaliwa hapa duniani, sisi sote ni lazima tufe mara moja, na baada ya kifo chetu sisi sote ni lazima tuhukumiwe. 
Lakini Yesu alikuja hapa duniani, akazichukua dhambi zetu zote katika mwili wake kwa ubatizo alioupokea toka kwa Yohana, alihukumiwa Msalabani kwa niaba yetu, na kwa sababu hiyo ametuwezesha sisi tunaomwamini kuishi pamoja naye milele katika Ufalme wake wa Mbinguni na wa milele. Kwa maneno mengine, ili aweze kutukomboa toka katika hukumu yetu ya dhambi, Mungu Mwenyewe alitusafisha dhambi zetu zote. Hii ndio sababu tunapaswa kumwamini Yesu, Yeye aliyefanyika kuwa Mwokozi. 
Yesu si mwanadamu wa kawaida. Kwa kuwa Mungu aliwaahidi wanadamu kwamba atawaokoa, na kwa kuwa ili kuitimiza ahadi hii alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu kwa kupitia mwili wa bikira, na kwa kuwa ni kweli kwamba aliwaokoa wote toka katika dhambi zao, basi sisi sote ni lazima tumwamini Yesu, ambaye ni Mungu Mwenyewe. Tunapomwamini Yesu kiusahihi, majina yetu yanaandikwa katika Kitabu cha Uzima. Mungu alitueleza kwamba mtu anaweza kuuona na kuingia katika Ufalme wa Mbinguni ikiwa atakuwa amezaliwa tena upya kwa maji na Roho. Sisi sote ni lazima tumwamini Yesu. 
 

Yesu Aliyefanyika Kuwa Njia ya Mbinguni
 
Sasa, ni lazima tufahamu jinsi Yesu alivyozifanya dhambi zetu zote kutoweka. Baada ya kuja hapa duniani, Yesu alibatizwa na Yohana katika Mto Yordani (Mathayo 3:13-17). Yesu aliupokea ubatizo wake toka kwa Yohana ili aweze kuzichukua katika mwili wake dhambi zote za mwanadamu (zikiwemo dhambi zako na zangu). Kwa kupitia mikono ya Yohana Mbatizaji, ambaye ni mwakilishi wa wanadamu, basi kila dhambi ya mwanadamu ilipitishwa kwenda kwa Yesu. Hivyo, baada ya kuzichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake kwa kupitia Yohaha, Yesu aliimwaga damu yake Msalabani na kufa juu yake. Kisha siku ya tatu alifufuka toka kwa wafu. 
Bwana wetu ameahidi kwamba yeyote anayemwamini atapokea uzima wa milele. Mungu ameazimia kwamba yeyote anayeamini katika ukweli kwamba Yesu alizichukua dhambi zake zote katika mwili wake na kisha akapokea adhabu kwa ajili ya dhambi hizi Msalabani, basi mtu huyo hawezi kutupwa katika ziwa la moto, na badala yake jina lake litaandikwa katika Kitabu cha Uzima. 
Katika Yohana 14:6 Yesu anasema, “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi.” Wanadamu ni lazima wamwamini Yesu ambaye amefanyika kuwa njia ya kwenda Mbinguni. Yesu ni Mwokozi wetu. Yesu ni Mungu wetu. Yesu ndiye ukweli halisi hapa ulimwenguni. Na Yesu ndiye Bwana wa uzima. Sisi sote ni lazima tumwamini Yesu ili kuhakikisha kwamba majina yetu yanaandikwa katika Kitabu cha Uzima na kwamba tutakaribishwa kuingia katika Ufalme wa Mbinguni. 
Kwa kuwa Yesu alizichukua katika mwili wake dhambi zote katika mwili wake kwa kuupokea ubatizo toka kwa Yohana Mbatizaji katika Mto Yordani, basi tunapaswa kumwamini Yesu, Yeye aliyefanyika kuwa Mwokozi wa upatanisho. Mimi na wewe tunaweza sasa kuingia Mbinguni kwa kuwa Yesu ameukamilisha wokovu wetu wote kwa kusulubiwa na kwa kuimwaga damu yake Msalabani kama adhabu kwa ajili ya dhambi zetu. 
Yesu amekwisha amua ni nani atakayetupwa katika ziwa la moto. Wale wasioamini na waoga watatupwa wote katika ziwa la moto. Wale wasioamini sio tu kwamba watatupwa katika ziwa la moto kwa sababu ya kutokuamini kwao, ukweli ni kuwa hata watoto wao na ukoo wao utakaofuata utatupwa pia katika ziwa la moto. Ili mtu aweze kufikia hali njema ya kiroho na kimwili, mtu huyo anapaswa kumwamini Yesu. 
 

Vipi Kama Yesu Asingeliupokea Ubatizo Wake? 
 
Ni Mungu pekee anayetoa baraka au laana kwa kila mwanadamu. Hii ndio sababu tunapaswa kumwamini Mungu. Unafahamu ni maisha mangapi ya watu ambayo ni ya kuhuzunisha na taabu, na kwamba ni kwanini mataifa ya dunia hii yanaanguka? Hii ni kwa sababu Mungu alisema kwamba atawalaani wale wanaomchukia na kuabudu sanamu kwa vizazi vitatu hadi vinne vitakavyofuata. Lakini pia alisema kwamba atawabariki kwa vizazi elfu wale wanaomtumikia na kumpenda Mungu na kuzishika amri zake (Kutoka 20:5-6).
Hii haimaanishi kwamba ikiwa mtu anamwamini Yesu kwa kiasi fulani basi atabarikiwa bila masharti. Mtu anapaswa kumwamini Yesu hali akiwa na ufahamu sahihi kumhusu Yesu. Kwa maneno mengine, ikiwa watu wanaamini kwamba Yesu ni Mungu Mwenyewe aliyekuja hapa duniani, na kwamba alizisafishilia mbali dhambi zao zote kwa kuzichukua dhambi hizo katika mwili wake kwa ubatizo wake, na kwamba amefanyika kuwa Mwokozi wao wa kweli kwa kusulubiwa kwa niaba yao—yaani kwa kifupi, kama wanaamini kwamba Yesu ni Mungu wao na Mwokozi wao—basi Mungu alisema kwamba atawabariki watu wanaoamini hivi kwa vizazi elfu vitakavyofuata. 
Lakini kwa wakati huo huo, pia Mungu ameahidi kwamba atawalaani kwa vizazi vitatu hadi vinne wale wasiomwamini Yesu. Hii ndio sababu kila mtu bila kujalisha yeye ni nani, anapaswa kumwamni Yesu, na hii ndio sababu kwamba kila mtu anapaswa kuufahamu na kuuamini ukweli wa kuzaliwa tena upya kwa maji na Roho. Wale walio na imani kama hiyo watasamehewa dhambi zao zote, watapokea uzima wa milele, wataingia Mbinguni, kisha wakiwa hapa duniani watapokea baraka baraka ambazo Mungu alimpatia Ibrahimu hapo zamani. 
Sisi sote ni lazima tuishi katika ulimwengu huu ambao Mungu ametuamlia kwa ajili yetu, na imani yetu ni lazima iwe kwa mujibu wa Neno lililoandikwa. Tunapswa kutambua na kuamini katika ukweli kwamba wale wasiomwamini Mungu watatupwa katika ziwa la moto, na kwamba wale wanaoamini majina yao yataandikwa katika Kitabu cha Uzima na kisha kukaribishwa katika Mbingu na Nchi Mpya. Pia ni lazima tuamini kwamba sisi tunaoamini tutaishi tena. Na kule kusema kwamba tumezaliwa tena upya kumewezekana kwa sababu ya injili ya maji na Roho. 
Kama ambavyo hakuna anayeweza kuishi pasipo maji, basi injili ya maji, pamoja na injili ya damu, ni muhimu sana kwa ajili ya wokovu wetu. Wakati Yesu alipobatizwa, alizichukua dhambi zetu zote katika mwili wake. Naye alizamishwa katika maji na kisha akachomoza toka katika maji. Hii ilimaanisha kifo chake Msalabani na ufufuo wake. Kwa maneno mengine, Bwana wetu alihukumiwa kwa ajili ya dhambi zetu zote kwa niaba yetu. Na kile kitendo cha Bwana kutokeza kwenye maji kuna maanisha ufufuo wake. Hii pia ina maanisha ni ufufuo wote, yaani kwetu sisi tunaoamini. 
Tunaamini kwa undani kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa ubatizo wake. Kama Yesu asingeliupokea ubatizo wake, ni nini kingetokea kwetu? Kusingelikuwa na njia ya sisi kulikwepa ziwa la moto. Kama ambavyo pasipo mvua hakuna mtu yeyote anayeweza kuishi katika ulimwengu huu, basi vivyo hivyo sayari hii ya dunia ipo kwa sababu ya uwepo wa maji. Vivyo hivyo, ubatizo wa Yesu ni wa muhimu sana kwetu sisi. Pia kifo chake Msalabani ni cha muhimu sana, kwa kuwa hii ina maanisha kwamba Yesu alihukumiwa kwa ajili ya dhambi zetu. Ikiwa tunataka kukombolewa toka katika laana ya Mungu na hukumu, basi tunapaswa kumwamini Yesu kikamilifu. Na ikiwa tunataka kusafishwa dhambi zetu, basi tunapaswa kuamini kwamba dhambi zetu zote zilipitishwa kwenda kwa Yesu wakati alipobatizwa. 
Imani ya Kikristo si aina ya dini inayowafanya watu kutetemeka kwa hofu. Kila mtu ni lazima amwamini Yesu. Wale waliozaliwa tena upya ni lazima waje katika Kanisa lililozaliwa tena upya ili waweze kulisikia Neno na kujengwa katika imani. 
Baadhi ya watu wanaamini kwamba mtu anapaswa kumwamini Yesu na kisha kutenda matendo mema ili aweze kuokolewa na kupokea baraka, lakini haya ni madai ya kitapeli ya waongo. Ni kweli kwamba tunapaswa kuishi kama Wakristo wema hali tukitenda matendo mema, lakini kwa mujibu wa tatizo letu la msingi kuhusu wokovu, asili yetu ni yenye uovu sana kiasi kuwa hakuna hata mmoja wetu anayeweza kuishi kwa asilimia 100 akiwa mkamilifu. Hii ndio sababu wale wanaodai kamba mtu anapaswa kuokolewa kwa kupitia matendo mema ni waongo na hawaifahamu injili ya maji na Roho na kwa sababu hiyo wanawadanganya watu. 
Tunatambua kwamba kimsingi tumefungwa ili kutenda dhambi, na tunapoutafakari ubatizo ambao Yesu Kristo aliupokea pamoja na Msalaba alioubeba kwa ajili yetu toka katika Neno la Mungu lililoandikwa, na tunapoyapokea mambo haya yote, basi ni hapo tu ndipo tunapoweza kuwa wenye haki, ambao mioyo yao haina dhambi, na kisha kustahilishwa kuingia Mbinguni. Kabla ya Roho Mtakatifu kukaa ndani yetu na kutuongoza, ukweli ni kuwa hakuna hata mmoja wetu anayeweza kuwa mwema hata kama atajaribu kiasi gani. 
Mungu alituokoa kwa kuzifanya dhambi zetu zote kutoweka. Badala ya kututupa katika ziwa la moto linalowaka milele, Mungu ameyaandika majina yetu katika Kitabu cha Uzima, ametupatia Mbingu na Nchi Mpya, na kama vile bibi harusi alivyojipanga kwa ajili ya Bwana harusi, Mungu ametupatia nasi nyumba nzuri zaidi, bustani, na maua mazuri. Pia Mungu atayaondoa magonjwa yote toka kwetu, naye ataishi pamoja nasi milele katika Ufalme wake. Tunapaswa kumwamini Yesu kwa ajili ya maisha yetu baada ya kufa, lakini tunapaswa pia kumwamini Yesu kwa ajili ya maisha yetu ya sasa. Pia tunapaswa kuamini kwa ajili ya watoto wetu pia. 
Je, unapenda kukaribishwa Mbinguni, au unapenda kutupwa katika ziwa la moto? Ni aina gani ya urithi utawarithisha watoto wako mwenyewe? Hata kama unakabiliana na baadhi ya shida na mateso kwa ajili ya imani yako katika Yesu, ukweli ni kuwa bado unatakiwa kuendelea kumwamini, maana kwa kufanya hivyo baraka kuu zitakujia wewe pamoja na watoto wako. 
Watakatifu wenzangu wapendwa, Mungu, kwa kupitia Neno lake ametueleza ni kwa nini tunapaswa kuihubiri injili ya maji na Roho, na kwamba ni kwa nini familia zetu pia zinapaswa kuokolewa. Ninampatia Mungu shukrani zangu.