Search

Preken

Somo la 8: Roho Mtakatifu

[8-5] Je, unataka kuwa na Ushirika na Roho Mtakatifu? (1 Yohana 1:1-10)

(1 Yohana 1:1-10)
“Lile lililoko tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, na mikono yetu ikalipapasa kwa habari ya Neno la uzima (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu) hilo tuliloliona na kulisikia twawahubiri na ninyi ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi, na ushirika wetu ni pamoja na Baba na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo. Na haya twayaandika ili furaha yetu itimizwe. Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu ya kwamba Mungu ni nuru wala giza lolote hamna ndani yake. Tukisema ya kwamba twashirikiana naye tena tukienda gizani twasema uongo wala hatuifanyi iliyo kweli bali tukienenda nuruni kama alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi na damu ya Yesu Mwana wake yatusafisha dhambi yote. Tukisema kwamba hatuna dhambi twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote. Tukisema kwamba hatukutenda dhambi twamfanya yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.”
 

Hitaji gani la awali muhimu 
kuweza kuwa na ufahamu wa usharika 
na Roho Mtakatifu?
Kwanza kabisa yatupasa kujua na kuaminiInjili 
ya maji na Roho na kujitakasa kwa 
dhambi zetu zot e kupitia 
imani hii.

Ikiwa unahitaji kuwa na usharika na Roho Mtakatifu kwanza kabisa lazima uelewe kwamba dhambi iliyo ndogo kabisa mbele ya Mungu inatosha kutokufanya usharika na Mungu. Unaweza kudhani “Sasa itawezekanaje mtu asiwe na dhambi hata kidogo mbele ya Mungu?” Lakini ikiwa kweli unatamani usharika na Bwana basi lazima pasiwepo na kiza moyoni mwako. Hivyo ili uwe na usharika na Bwana, unahitajika kujua kwamba lazima uamini Injili ya ukombozi na kujitakasa dhambi zako zote.
Ikiwa kweli unapenda kuwa na usharika na Roho Mtakatifu kwani itakupasa ujue na kuamini Injili ya maji na Roho na kujitakasa dhambi zako kupitia imani hiyo. Ikiwa Injili ya maji na Roho huichukulii moyoni, basi usifikiri hata kuwa na usharika na Bwana. Kuwa na usharika na Roho Mtakatifu kunawezekena ikiwa tu dhambi zako zote zimefutwa katika moyo wako kwa Injili ya maji.
Dhambi zote zitaweza kufutwa katika akili ya mtu kwa ukweli wa maji na Roho. Bwana anakubariki na Roho Mtakatifu pale unapoamini Injili njema ya maji na Roho. Je, kweli ungependa kuwa na usharika na Bwana na Roho Mtakatifu? Sasa basi tambua dhambi zako na uamini Injili njema ili ujitakase kwa dhambi hizo. Baada ya hapo ndipo utaweza kweli kuwa na usharika na Bwana.
Ikiwa unatamani kuwa na usharika na Bwana lazima uamini ubatizo wa Yesu, alioupokea kwa Yohana pale Yordani na pia amini damu ya Yesu msalabani. Ikiwa kweli watu wanatamani kuwa na usharika na Roho Mtakatifu ni lazima wamjue Roho Mtakataifu ni nani? Roho Mtakatifu ni mwenye utakatifu. Na hivyo ataweza kuweka makazi kwa wale tu wanaoamini Injili njema.
Hebu tuone ushuhuda wa mtu fulani ambaye dhambi zake zilitakaswa kwa kuamini ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake, ambaye sasa anausharika na Roho Mtakatifu.
“Wapo watu wa aina tofauti wengi ulimwenguni na kila mtu huishi kwa mawazo yake na njia zake. Nami nilikuwa moja kati ya hao. Nilikuwa na maisha ya kawaida toka utotoni huku nikimfuata mama yangu Kanisani na matokeo yake nikaanza kumwamini Mungu na mara kadhaa wenzangu walinipinga kwa imani yangu lakini familia aliyobaki sote tulikwenda Kanisani. Kwenda Kanisani kulikuwa ni sehemu kubwa katika maisha yangu. 
Hata hivyo, wakati wa ujana wangu kwa kumuona baba yangu aliye mahututi kitandani mawazo mengi kuhusiana na mambo kama uhai na kifo, mbinguni na motoni yalinijia. Watu wengi walisema kwamba ikiwa nitamwamini Mungu nitaweza kuingia mbinguni na kuwa mtoto wake, lakini sikuwa na uhakika na hilo. Kamwe sikuwa na uhakika kwamba nitaweza kuwa mtoto wa Mungu, nilikuwa nimejifunza kwamba ikiwa nitatenda mema hapa ulimwenguni basi nitaweza kuingia mbinguni na hivyo nikajitahidi sana kutenda mema kwa nia hiyo.
Lakini upande mwingine wa moyo, nilikwisha elewa kwamba nina dhambi. Ningeliweza kuonekana mtu mwema mbele ya wengine lakini sikuweza kujizuiya kuwa na hukumu ndani yangu kwaajili ya dhambi zangu muda huo. Ikawa ni mazoea yangu kwenda mara kwa mara kanisani kwa maombi, huku nikisali “Tafadhali Bwana naomba niwe Mwana wako daima. Tafadhali naomba niijue kweli” Wakati nikisali hivyo na vingine, nilianza kuwa na msukumo mpya moyoni. Kila niliposikia mafundisho ya maneno ya Mungu sikuweza kuelewa au hata kuona ugumu wa maneno. Hivyo nilichoka kwa utupu uliomo katika maisha yangu, dhambi, kifo na kadhalika.
Kwa mfano niliwaza “Ningependa kuzaliwa upya na kama ningezaliwa upya nisingekuwa hivi” Lakini licha ya mawazo haya yote niliendelea kwenda mara chache kanisani na hivyo umri wa Ujana ulipita na hivyo nilihitaji kutafuta kazi. Lakini ikawa hali ilizidi kuwa ngumu tofauti na nilivyodhani. Nilikata tamaa na hivyo kila nilivyo jibidiisha sikuweza kuwa na furaha yoyote. Nilipojiona mwenye moyo mtupu nilifikia hatua ya kuchanganyikiwa na katika muda huo ndipo nilipopata fursa ya kusikia Injili kamili kwa kaka yangu mkubwa.”
“Tubuni basi mrejee, ili dhambi zenu zifutwe zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana” (Matendo 3:19). Hii ilikuwa Injili ya maji na Roho kwa hakika. Yote niliyojifunza toka katika mikutano ya Kanisa la hapo awali ilikuwa ni kwamba Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Lakini Injili hii ya sasa imenieleza kwamba Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji ili kubeba dhambi zetu na kuhukumiwa na dhambi hizo msalabani.
Hapo awali nilikuwa nikienda Kanisani na kujifanya kuwa ni mtoto wa Mungu lakini hatimaye nilishindwa. Hata hivyo baada ya kusikia Injili kamili ya maji na Roho na kuiamini, dhambi zangu na yote yaliokuwa yakinitesa ndani yangu yalitoweka na moyo wangu kupata amani.
Nilidhani kwamba ikiwa nitamwamini Mungu kwa ushabiki na kwenda Kanisani bila kukosa ndipo nitakwenda mbinguni lakini Mungu aliniletea Injili ya maji na Roho hivyo dhambi zangu zilisamehewa. Akanipa kipawa cha Roho Mtakatifu. Kabla sijapokea ukombozi wa Mungu sikujua juu ya Roho Mtakatifu bali ni kunena kwa lugha tu. Nilikuwa nikienda kanisani na huku nikiamini kwamba ikiwa nitaishi maaisha yaliyo nyoofu na kutumika kanisani basi ndipo Mungu atanibariki. Lakini nilikuja kugundua kwamba ningeweza kumpokea Roho Mtakatifu ikiwa tu dhambi zangu zitasamehewa kupitia Injili njema ya maji na Roho.
Katika maisha yangu yaliyopita, nilikuwa bado na dhambi ingawa nilimwamini Mungu. Hivyo niliishi maisha ya uvuguvugu pasipo kujua umuhimu wa kumpokea Roho Mtakatifu ndani yangu. Lakini hatimaye kwa kupitia mtumishi wa Mungu aliyehubiri Injili njema kulingana na Biblia niliamini na kujua kwamba Roho Mtakatifu huweka makazi ndani yangu pia.
Baada ya kupokea ukombozi, mwanzoni sikuweza kuamini ikiwa nilikuwa na Roho Mtakatifu ndani yangu au la. Lakini nilipopendelea maneno ya Mungu na kuelewa kwamba ndani ya moyo wangu kuna imani mpya iliyochanua basi tayari nilikuwa nimekwisha kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu. Sasa ni kweli naamini kwamba Roho Mtakatifu ameweka makazi ndani yangu! Mungu aliposamehe dhambi zangu binafsi nilijua ya kwamba wale tu walio huru kwa dhambi ndiyo huwa ni watoto wa Mugnu na hata kumpokea Roho Mtakatifu.
Pia nilijua kwamba juhudi zangu binafsi kuonekana mkamilifu mbele za macho ya Mungu au kuishi kwa ukamilifu hakutoweza kunisaidia kumpokea Roho Mtakatifu. Mungu huja kwa wale wote wenye kufahamu kwamba ni wenye dhambi na hata hivyo hawajui wafanye nini juu yao. Mungu hukutana na wale wote wenye kumtafuta kwa dhati na kumhitaji.
Alinifanya nione kwamba kutenda mema na kumwamini Mungu kwa kujitolea mara kwa mara, hakutoniwezesha kufika mbinguni na hivyo Yesu Krsto alikuja ulimwenguni kuniokoa kutoka dhambini kupitia Injili njema ya maji na Roho. Alinipa Roho Mtakatifu ili akae ndani yangu daima.
Namshukuru Bwana kwa kunifanya kuwa mtoto wake na kunibariki kwa uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yangu. Kama isengelikuwa ni Bwana ningeliendelea kuwa na dhambi moyoni mwangu na ningelihukumiwa motoni maishani milele. 
Kwa jinsi hiyo pia, hapo awali niliamini damu ya msalabani pekee na sikuweza kumpokea Roho Mtakatifu hata nilipotamani. Katika muda huo nilimwamini Yesu lakini bado nilikuwa na dhambi moyoni iliyonizuia kumpokea Roho Mtakatifu. Wenye dhambi wengi kamwe hawatoza kumpokea Roho Mtakatifu moyoni mwao. Lakini leo hii wenye dhambi wengi hujaribu kumpokea Roho Mtakatifu huku wakiwa na dhambi nyingi mioyoni mwao.
Ikiwa kweli unatamani kumpokea Roho Mtakatifu na kuweza kuwa na usharika naye, unahitaji kuamini Injili njema ya maji na Roho na kupata ukombozi. Je, bado wewe unadhambi? Basi unayo nafasi ya kuisikia Injili ya kweli toka kwa wale wote waliokwisha kumpokea Roho Mtakatifu. Wale wote wenye kutamani kuwa na usharika na Roho Mtakatifu lazima wawe na kiu mioyoni mwao na kuiamini Injili njema ya maji na Roho. 
Wenye haki tu ndiyo watakaosikia maneno ya Roho Mtakatifu kupitia kanisa. Wataweza kuishi maisha ya uaminifu kwa kusikia Injili njema. Lakini wenye dhambi huishi maisha yao ya laana yenye hatima ya motoni pasipo hata kuisikiliza Injili.
Hivyo, ni lazima ujue juu ya Injili ya maji na Roho. Kwa nini unahitaji kuamini Injili hii? Ni muhimu kwako ili uepuke sheria za kidini na kujenga imani katika Injili njema iliyo na msingi wa maneno ya Mungu. Wafuasi wa Yesu waliifuata Injili hii njema ya maji na sasa ni kati ya wale wote waliompokea Roho Mtakatifu. Injili njema ya maji na Roho ndiyo iliyo pekee na halisi ambayo Mitume hapo mwanzo waliifuata wakati wa kanisa la mwanzo. Wakristo wote lazima wawe wamempokea Roho Mtakatifu ndipo watakapoweza kuwa wana wa Mungu.
Wale ambao bado hawajaamini Injili njema ya maji na Roho lazima wana dhambi mioyoni mwao. Ili waweze kuwa na usharika na Roho Mtakatifu lazima kwanza waamini Injili ya maji na Roho ambayo Mungu amewapa na hivyo watampokea Roho Mtakatifu.
 

Biblia mara kwa mara humataja Roho Mtakatifu.

Kuwa na Roho Mtakatifu ndani kulianza baada ya kufufuka kwa Yesu. Sasa ni siku ya wokovu na ni wakati wa rehema tele za Mungu. Lakini ukweli ni kwamba ni bahati mbaya ikiwa hatuto ipokea Injili ya maji na Roho na ikiwa tutaishi pasipo kuwa na usharika na Roho Mtakatifu.
Je, una usharika na Roho Mtakatifu? Je, umezuiliwa kuwa na usharika naye kwa sababu tu ya dhambi zako? Basi jifunze juu ya Injili ya maji na Roho ambayo Mungu amekupatia na hivyo uweze kuamini. Ikiwa utaiamini Injili ya maji na Roho ndipo basi Roho Mtakatifu ataweka makazi ndani ya moyo wako na kuwa rafiki kwako. Roho Mtakatifu huweka makazi ndani ya mioyo ya wale tu wenye kuamini Injili ya maji na Roho. Roho Mtakatifu hufunua mapenzi ya Mungu ndani ya mioyo ya wenye haki. Huduma ya Paulo akiwa na Roho Mtakatifu ilikuwa ni kueneza Injili njema.
Je, utaweza kumgundua mtu aliyempokea Roho Mtakatufu ndani yake? Nini kilicho kigezo? Kigezo cha mtu ni kwanza labda awe anaamini au kutoamini Injili njema ya maji na Roho ndiyo kikubwa. Ikiwa mtu anafahamu na kujua Injili njema ya maji na Roho basi ndiye aliye na Roho Mtakatifu ndani yake. 
Roho Mtakatifu haweki makazi ndani ya wale wasio amini Injili hii njema. Yeye hukaa ndani ya wale wote wenye kuamini msamaha wa dhambi utokanao na ubatizo wa Yesu alioupokea toka kwa Yohana na damu yake pale msalabani. Je, nawe ungependa kuwa na usharika na Roho Mtakatifu?
Je, unafahamu ni Injili ya aina gani unayo ihitaji kuielewa na uweze kumpokea Roho Mtakatifu na kuwa na usharika naye? Injili njema hupatikana katika kuamini ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani. Ikiwa huamini Injili ya maji na Roho dhambi zako kamwe hazitosamehewa na hivyo Roho Mtakatifu hatoweza kuweka makazi ndani yako. Roho Mtakatifu anahitaji watu waiamini Injili ya maji na Roho ili waweze kumpokea ndani yao.
Roho Mtakatifu kamwe hawezi kuweka makazi ndani ya mioyo ya wenye dhambi. Ikiwa unahitaji kumpokea ni lazima kwanza kuamini Injili njema ili uweze kutakaswa dhambi zako zote. Pia ikiwa unataka kuwa na usharika naye inakupasa kuwa mwaminifu na kuihubiri Injili njema, ikiwa unataka pia kuongozwa naye ni lazima wakati wote uipende Injili njema na kuihubiri kila uendapo. Roho Mtakatifu yu pamoja na wale wote wanaoihubiri Injili ya maji na Roho.
Uwepo wa Roho Mtakatifu ndani huwa ni kwa wale walio na haki, wale wenye kuamini Injili njema. Wenye haki tu wanoamini Injili njema ndiyo wataweza kuwa na usharika na Roho Mtakatifu. Injili njema ambayo Roho Mtakatifu huitambua ni ile Injili iliyokamilishwa na ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake (1 Yohana 5:3-7). 
Petro naye aliamini Injili njema na kusema, “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo unaowaokoa ninyi pia siku hizi (siyo kuweka mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu) kwa kufufuka kwa Yesu Kristo” (1 Petro 3:21). Katika Biblia neno “maji” mara nyingi husimama badala ya ubatizo wa Yesu alioupokea toka kwa Yohana Mbatizaji.
Wale wanao weza kumpokea Roho Mtakatifu ni waliokwisha pokea ukombozi kupitia Injili njema na wapo huru kwa dhambi zote. Wale wenye kuamini Injili njema ndiyo wanaoweza kumwabudu Baba katika roho na kweli kwa kuongozwa na Roho (Yohana 4:23). Roho Mtakatifu huwasaidia wenye haki kuishi maisha yao huku wakiwa wamejazwa na Roho Mtkatifu. Wale walio na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao wataweza kuishi wakimsifu Mungu milele. Roho Mtakatifu hututhibitishia sisi kuwa ni wana wa Mungu. Tunaweza kuishi milele tukiwa ndani ya Injili ya maji na Roho na ndani ya Roho Mtakatifu.
 

Roho Mtakatifu hawezi kuwa na usharika na wale wote wenye kudanganya nafsi zao.

Roho Mtakatifu huwaambia wenye dhambi wote katika 1 Yohana1:8 “Tukisema kwamba hatuna dhambi tunajidanganya wenyewe wala kweli haimo mwetu.” Roho Mtakatifu hawezi kuweka makazi ndani ya wale wenye kudanganya nafsi zao. Roho Mtakatifu huzihukumu nafsi za wenye dhambi kwa kusema “Kwa nini huamini Injili njema iliyokamilishwa kwa ubatizo wa Yesu na damu yake?” 
Tutaangalia juu ya Mkristo fulani aliyezaliwa upya mara ya pili hapo mwanzo kama aliweza kumpokea Roho Mtakatifu pasipo ushuhuda wa ubatizo wa Yesu na damu yake. Mtu huyu sasa anaamini Injili ya maji na damu na amempokea Roho Mtakatifu. Hapa ni lazima tutaje barabara ni mtu gani ambaye Roho Mtakatifu huweka makazi ndani yake.
“Mungu alianza kuishi ndani ya moyo wangu pale nilipogundua sababu ya kuwepo kwangu hapa ulimwenguni. Kwa kuangalia niliwaza juu ya uhai wangu kuishi peke yangu katika dunia iliyojaa ukatili hivyo kulinifanya kuwa na hamu ya kumtafuta Mungu. Lakini sikumtafuta Mungu kwa jinsi nyingine zaidi ya kukubali kuwepo kwake, si kwa kuwa hakuonekana bali kwa uwepo wake. Hata hivyo nilijiuliza Je, ni kweli yupo? Lakini mawazo juu ya hili yalinitisha kwa kuwa kwa dhati niliamini kwamba yeye ndiye muumba wa yote. 
Wale wampingao Mungu huwa ni wajinga lakini kwa njia nyingine huwa ni wenye nguvu zaidi yangu. Huonekana kuwa wataweza kupitia mambo mengi peke yao na badala yake kwa upande wangu mimi nilijiona kuwa dhaifu na mjinga dhidi yao. Lakini kwa kuwa nilikuwa na tumaini la uzima baada ya kifo nilimtumaini Mungu kwa heshima kuu zaidi. Nilishindwa kuelewa ikiwa mbinguni palikuwa ni mahali pa watu kama mimi wenye kujisikia wakati wote wenye upungufu. Na swali hilo lilinifanya niwe natamani mbingu ya paradiso.
Wazazi wangu waliwadharau watu walio na udini na hivyo ndugu zangu wote nyumbani walikwenda kanisani pasipo na msukumo ndani yao wa kujitoa. Walidhani msukumo ndani yangu ungetoweka punde hivyo hawakunizuia kutokwenda hadi nilipo fika elimu ya kidato cha pili. Hivyo nilikwenda kanisa moja hadi jingine na mwishowe nikaanza kwenda katika kanisa moja dogo karibu na nyumba yetu hadi nilipofikia elimu ya chuo. 
Sababu ya kuchagua kuhudhuria kanisa hili ilikua ni kwamba waliwekea mkazo zaidi katika injili. Mchungaji wa kanisa hilo alikua ni Mwinjilisti mhamasishaji ambaye hakufanya lolote baya katika kwenda kinyume na maneno ya Biblia. Nikawa na sababu ya kuishi maisha ya udini kwa dhati ingawa nilichoka na kugandamizwa na masomo yangu.
Sababu ni kwamba pale watu walipowaita waumini wenzengu kuwa ni wazushi niliamini kwamba kanisa langu ni la kweli na bila shaka ningelikwenda mbinguni. Uhakika huu ulitokana na injili. Ilisemekana kwamba wenye dhambi kamwe hawawezi kuingia mbinguni lakini hata hivyo watu hao husema kwamba mioyo yao imejaa dhambi. Nami pia niliamini juu ya hili. Kabla sijaanza kuhudhuria kanisa hilo, sikuwahi kuwaza juu ya changamoto hii sana.
Lakini wale wanaoitwa Wainjilisti wa uamsho walikua ni tofauti na wale nilio wazoea hapo awali. Wao husema kwamba ikiwa tutamwamini Yesu kwa namna iliyo sahihi basi tutakuwa wasio na dhambi bali wenye haki. Mwanzo sikuweza kuamini hili lakini nilipowaza juu ya hili niliona ni la kweli. Nilikua bado ni kijana na nilidhani kwamba ikiwa nahitaji kwenda mbinguni basi Mungu angeliweza kuniruhusu ikiwa tu sitokua mwenye dhambi, kwani Mungu hapendi dhambi.
Kanisa hili lilikuwa na imani tofauti dhidi ya vile nilivyozoea na ibada ya kuabudu ilikua ni tofauti kidogo pia, lakini kwa kuwa mbinguni ni mahala ambapo wachache wataingia ilionekana kwamba watu katika kanisa hili walikua na imani iliyo sahii. Kwa kuwa kanisa lilitilia mkazo sakramenti ya mwili wa Yesu na damu yake kila Jumapili, hivyo tulikula mkate na kunywa divai. Kwa kuwa karamu hii ilikua katika msingi wa Biblia nilikubaliana na hili. Nikagundua baadae kwamba watu walishiriki ibada hii pasipo kuelewa maana iliyo ya kweli.
Niliamini kwamba roho Mtakatifu huweka makazi ndani yangu. Nilikua na uhakika kwamba Mungu alikua pamoja nami na sikua na shaka na injili iliyo ya amani. Nilipopitia magumu nilizungumza na Mungu kama vile yupo pembeni yangu kimwili. Niliamini kwamba alinisikiliza nilipomweleza vitu ambavyo nisingemweleza yeyote. Hivyo nilimtumaini na kumtegemea yeye tu.
Sikuweza kuwaelewa wale wanaokwenda katika mikutano ya uamsho ili kunena kwa lugha na niliwacheka wale wote wenye kufanya maombi ya kufunga kula. Kwa kuangalia juhudi hizo niliwaza kwanini wanapitia mambo haya yote yasiyo na maana kwa juhudi ya kumpokea Roho mtakatifu? Roho Mtakatifu huja kwa wale tu wasio na dhambi na kukaa ndani yao daima. Hawezi kuja kwao hata wakijibidisha kwa dhati. Niliwaonea huruma. Niliwaona kuwa ni wapumbavu na kwa kuwaza hivyo nilikuja kufikiri kwamba imani yangu katika injili ilikuawa ni bora na hivyo kwa wengine walikua ni waongo.
Kiburi cha moyo wangu kilifikia kileleni na kwa takribani miaka kumi nilikuwa nimekwisha jiingiza katika maisha ya udini. Kadiri muda ulipozidi kwenda nikaanza kujiuliza maswali ndani ya mawazo yangu na moyoni. Nilidhani mimi si mwenye dhambi kutokana na injili ya damu ya msalaba wa Yesu, lakini je, wote wanaoamini nao hawana dhambi pia? Je, nao wanaamini injili hii pia? Sikujua kwa nini nilianza kujiuliza maswali haya. Yote haya yalikuja akilini na sikuthubutu kumuuliza yeyote. Hili lilikua swala la imani binafsi lisiloingiliwa, na si uungwana kumuuliza mtu mwingine namna hii.
Lakini niliendelea kujiuliza maswali haya binafsi. Nilipokua chuoni nilianza kutenda mambo niliyozoea nikitawaliwa na mitazamo ya kidini. Hivyo moyo wangu ukaanza kuwa na doa jeusi ambapo imani yangu ikaanza kutoweka. Sikuwa tena na uhakika na imani yangu. Je nitaweza kujiita kweli ni mwenye haki? Je Yesu alitakasa dhambi zangu zote? Katikati ya mtafaruku huu wa mawazo nilijilazimisha kuiwaza injili ya msalaba na kujiliwaza nayo. Lakini nilipozidi kujilazimisha nilizidi kupotoka na nikaacha kuhudhuria kanisani katika ibada. Nikaanza kutumia shughuli za taaluma yangu kuwa ni sababu ya kushindwa kuhudhuria.
Mwishowe baada ya mtafaruku huu na kuchanganyikiwa kwangu nilikutana na ukweli. Nilipata kusikia juu ya habari ya injili ya maji na Roho na ikawa kwangu kama mwanga wa radi. Mlipuko huu ukawa mkubwa kunifanya hata nikataka kulia.
Lakini kwa kuisikia injili hii nilikubali kwamba nilichokuwa nikikiamini hapo mwanzo ni uongo. Sikuwahi kumtwika Yesu dhambi bali nilikuwa namwamini kwa hisia tu kwamba amekwisha beba dhambi zangu na hivyo si mwenye dhambi na hatimaye kushindwa kuwa na suluhusho. Kwa nini Yesu amekuja hapa ulimwenguni na kubatizwa? Je ni kwa sababu alipenda kutuonyesha unyenyekevu wake kama kondoo? au kutabiri kuwa kifo hakimshindi? Sikuwahi kamwe kuota kwamba hisia za kuelewa juu ya ubatizo nilizokua nazo zilikuwa simuhimu kiasi hicho. Ukweli ni kwamba Yesu alibatizwa na Yohana aliyekua mwakilishi wa wanadamu wote na kwa ubatizo huo dhambi zetu zote zilitwikwa juu yake.
Oh…na ndio maana Yesu alikua ni Mwanakondoo wa Mungu aliyebeba dhambi zetu zote pale msalabani. Ndio maana mimi si mwenye dhambi tena katika moyo wangu. Pale tu nilipo fahamu juu ya injili ya maji (ubatizo wa Yesu), damu (msalabani) na Roho Mtakatifu (Uungu wa Yesu) ndipo basi dhambi zangu zilizo moyoni zilifutika.
Sasa hakika mimi si mwenye dhambi tena bali ni mwenye haki, na Roho Mtakatifu ameweka makazi ndani yangu. Imani niliyowahi kuwa nayo ya msalaba haikuwa imetosheleza kutakasa dhambi nilizokuwa nazo moyoni mwangu. Ikiwa hufahamu namna ile dhambi zako zilivyotwikwa juu ya Yesu, basi hakika dhambi hizo hazitoweza kusamehewa na hivyo Roho Mtakatifu kamwe hatoweza kuweka makazi ndani yako. Namshukuru Mungu kwa hili. Niliweza kumpokea Roho Mtakatifu kwa kupitia Injili iliyo njema.
Pasipo juhudi yoyote binafsi, nilisamehewa kwa kupitia Injili ya maji na hivyo Roho Mtakatifu ameweka makazi ndani yangu sasa na hata milele. Sasa naweza kujivunia kwa kujiita nisiye na dhambi na kwamba Ufalme wa Mbingu ni mali yangu. Nachukua fursa hii kumshukuru Bwana kwa kunipa aina hii ya baraka pasipo gharama. Haleluya!”
Wale wote wanaompokea Roho Mtakatifu wanaweza kusema hivi, kwamba hawana dhambi mbele ya Mungu na haijalishi ni kwa muda gani umemwamini Yesu, ikiwa huamini Injili njema ya Mungu aliyotupatia hakika bado wewe unadhambi moyoni. Watu wa aina hii hujidanganya nafsi zao pia humdanganya Mungu. Watu hawa bado hawajakutana na Bwana. Ikiwa mwenye dhambi anatamani kuwa na usharika na Roho Mtakatifu, ni lazima kwanza akome kudanganya nafsi yake na kukiri kuwa yeye ni mwenye dhambi. Ndipo basi atawza kuhitimu katika kuamini Injili ya maji na Roho. Wale wote wanaoamini Injili njema wanahakika ya kumpokea Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu anasema nini kuhusu wenye dhambi? Anawashauri kupokea kwanza msamaha wa dhambi zao kwa kuamini Injili njema ambayo ilidhihirishwa kwa ubatizo wa Yesu na damu yake. Ikiwa unasema kwamba wewe si mwenye dhambi huku ukiwa na dhambi moyoni basi hakika huwezi kumpokea Roho Mtakatifu. Wale wote wasioamini Injili njema huku wakisema kwamba hawana dhambi hujidanganya nafsi zao na pia Mungu. Wenye dhambi ni lazima waelewe Injili njema ya maji na Roho na kumpokea Roho Mtakatifu. Ndipo watakapokombolewa tokana na hukumu ya Mungu iliyo kali ya kutisha.
 

Wenye haki ndiyo watako weza kuwa na usharika na Roho Mtakatifu kwa kukiri dhambi zao.

Hapa nazungumza na wale ambao tayari wamekwisha amini Injili ya maji na Roho na hivyo kumpokea Roho Mtakatifu. Hebu na tuangalie nini Mungu alichowaeleza wenye haki. Katika Yohana 1:9 inasema. “Tukiziungama dhambi zetu yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolea dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote.” Mstari huu una maana kwamba tutaweza kusafisha dhambi zetu tuzitendazo tokana na mioyo iliyochafuliwa kwa kujikumbusha nafsi zetu na kuamini Injili njema ambayo inatangaza kuwa Yesu alibeba dhambi zetu zote pale alipobatizwa na kuleta upatanisho kwa kusulubiwa kwake. Wenye haki ndiyo inawapasa kukiri dhambi watendazo na kuendelea kuamini Injili njema.
Hapo kale, Injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake ilikwisha takasa dhambi zetu zote na hivyo leo hii wenye haki imetupasa kuiamini injili hii na kuwa huru kwa dhambi zetu. Bwana tayari alikwisha tusamehe dhambi zetu zote kupitia Injili ya maji na Roho. Wenyehaki lazima waamini Injili hii njema ili wawekwe huru tokana na dhambi zao. Wenye haki wataweza kutakaswa mioyo yao kwa kuamini Injili njema ya maji na Roho pale wanapochafuliwa kwa dhambi wazitendazo kila mara.
Bwana wetu alitakasa dhambi zote za wenye haki siku nyingi kwa ubatizo na damu yake. Hivyo wale wote wanaoamini ukweli hakika ni huru toka dhambini. Hata hivyo wenye haki ni lazima wakiri na kukubali kuwa wametenda dhambi mbele ya Mungu. Na ndipo basi waweze kuirudia imani ya ubatizo wa Yesu na damu yake ambayo imejenga Injili hiyo njema ili kuweza kuwa huru kwa dhambi zao zote. Hivyo kwa wakati wote wataweza kuanza kuishi upya maisha ya kwenda sambamba na Roho Mtakatifu. Wale wote wanaomtumaini Bwana pasipo kuangalia udhaifu wao ndiyo watakoweza kuwa na usharika na Mungu kwa kuishukuru Injili njema ya maji na Roho.
 

Tutawezaje kupata tathimini ya ukweli katika usharika na Roho Mtakatifu?

Wapo watu wengi wanotamani kuwa na usharika na Roho Mtakatifu. Lakini hawajui namna ya kufanikisha hili ingawa wanamwamini Yesu. Watu wote humpokea Roho Mtakatifu kwa kuiamini Injili ya maji na Roho na moja kwa moja kuanza kuwa na usharika naye muda huo.
Kwa upande mwingine, njia pekee ya mwenye haki itakayo mwezesha kuwa na ushirika na Roho Mtakatifu ni kwa kuifahamu vyema na kuiamini Injili ya maji na Roho iliyo ya kweli. Usharika kati ya mwenye haki na Roho Mtakatifu haupatikani pasipo Injili ya kweli. Nini maana juu ya usharika na Roho Mtakatifu? Huu unawezekana ikiwa tu utaamini injili njema.
 

Mungu anasema kwamba, mwanadamu ataendelea kutenda thambi maishani pote.

Katika 1 Yohana1:10 inasema “tukisema kwamba hatukutenda dhambi twamfanya yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu”. Hapajatokea yeyote ambaye hajatenda dhambi mbele ya Mungu. Hata biblia inasema “bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani ambaye afanyaye mema asifanye dhambi” (Mhubiri 7:20). Watu wote hutenda dhambi mbele ya Mungu. Ikiwa mtu yeyote atasema kwamba hajatenda dhambi basi ni muongo. Watu hutenda dhambi maishani mwao mwote hadi saa ya mwishoni kabla ya kufa, na hii ndiyo maana Yesu alibatizwa na Yohana ili kubeba dhambi hizo zote. Ikiwa hatujawahi kutenda dhambi basi tusingelihitaji kumwamini Mungu kuwa ni mwokozi.
Bwana anasema “neno langu si neno lako” kwa wale wenye fikra wakidhani kuwa hawajatenda dhambi. Ikiwa mtu hana imani katika injili njema ya maji na Roho basi anastahili kuangamia. Ikiwa mtu mwenye haki au mwenyedhambi atasema kwamba hajatenda dhambi mbele za Mungu, basi huyo hatastahili kuiamini injili njema.
Bwana amempa kila mmoja zawadi nzuri ya injili njema. Tulikiri dhambi zetu zote na kutubu ilikupokea msamaha kwa injili njema. Tunaweza kuirudia injili hii ambayo Mungu aliyo tupatia kama msamaha wa dhambi zetu na kuiamini ili kuweza kuwa na usharika wa Roho Mtakatifu. Maana ya kweli ya usharika wa Roho mtakatifu ipo katika injili ya maji na Roho, na pia kwa wale tu walio na injili hii ndiyo watakao weza kuwa na ushirika na Mungu.
Wanadamu walikuwa mbali na Mungu kwa sababu ya dhambi walizorithi kwa Adamu na Hawa. Lakini leo hii sisi tuliokuwa tumerithi mbegu ya uovu tunaweza kutarajia kuwa na usharika na Mungu kwa mara nyingine tena. Ili kuweza kufanikisha hayo yote ni lazima tuwe na imani ya injili ya maji na Roho toka kwa Yesu Kristo, na hivyo kuwa na msamaha wa dhambi ambazo zilituweka mbali na Mungu. 
Wale wote wenyekuamini injili njema ndiyo watakao okolewa kutokana na dhambi zote, na hapo basi Mungu atawajaza Roho Mtakatifu. Wenye haki wataweza kuwa na ushirika na Mungu kwa kuwa wamempokea Roho Mtakatifu. Kwa wale wote waliowekwa mbali na Mungu kutokana na dhambi zao lazima wairudie injili njema ya maji na Roho na kuiamini na hapo ndipo watakapoweza kuanza kuwa na ushirika na Mungu.
Kuwa na Roho Mtakatifu ndani huja kutokana na imani katika injili njema. Lazima tujue kwamba kuwa na Roho Mtakatifu ndani yetu huja pale tunapoamini injili ya maji na Roho tu. Kuiamini injili njema ndiko kunako jenga njia mpya kumuelekea Mungu. Bwana amevunja ukuta wa kati ulio kuwa ukitutenganisha naye kwa sababu ya dhambi zote mbili, yaani dhambi tuzitendazo maishani na ile dhambi ya asili, na hivyo tutaruhusiwa kuwa na ushirika na Mungu kwa kupitia imani yetu katika injili njema ya maji na Roho. 
Yatupasa kuanzisha upya ushirika na Roho Mtakatifu kwa mara nyingine tena. Usharika wa kweli na Roho Mtakatifu hufanikishwa kwa kupita kuelewa injili ya maji na Roho kwa kutii imani. Ushirika wa Roho Mtakatifu huja pale tunapokuwa na imani ya kweli na msamaha wa dhambi ambao unatokana na injili njema. Wale wote ambao hawajapokea msamaha wa dhambi kamwe hatoweza kuwa na ushirika wa Roho Mtakatifu. Kwa maneno mengine hakuna yeyote atakaye weza kuwa na ushirika wa Roho Mtakatifu pasipo kuiamini injili ya maji na Roho. 
Ikiwa bado ni vigumu kwako kuwa na ushirika wa Roho Mtakatifu basi ni lazima kwanza akubali kwamba bado hajaamini injili ya maji na Roho na hivyo dhambi zako hazijasafishwa. Je, unatamani kuwa na uhusiano na Roho Mtakatifu? Sasa basi amini injili iliyokamilishwa kwa ubatizo wa Yesu na damu yake. Ndipo hapo tu utaweza kusamehewa dhambi zako zote na thawabu yako itakuwa ni kumpokea Roho Mtakatifu ndani ya moyo wako. Injili hii njema kwa hakika ndiyo inayotuletea ushirika na Roho Mtakatifu.