Search

คำสอน

Somo la 8: Roho Mtakatifu

[8-13] Kazi na vipawa vya Roho Mtakatifu (Yohana 16:5-11)

(Yohana 16:5-11)
“Lakini sasa mimi naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka, wala hakuna mmoja wenu aniulizaye unakwenda wapi? Ila kwa sababu nimewaambia hayo huzuni imejaa mioyoni mwenu. Lakini mimi nawaambia iliyo kweli, yawafaa ninyi mimi niondoke kwa maana mimi nisipoondoka huyo msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu nitampeleka kwenu. Naye akiishi kuja huyo atauhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi na haki na hukumu, kwa habari ya dhambi kwa sababu hawaniamini mimi, kwa habari ya haki kwa sababu mimi naenda zangu kwa baba wala hamnioni tena, kwa habari ya hukumu kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha hukumiwa.”
 
 
Ni zipi kazi za Roho 
Mtakatifu?
Kuuhakikishia ulimwengu kwa 
habari ya dhambi haki 
na hukumu.

Katika Mwanzo 1:2 imeandikwa, “Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu na giza lilikuwa juu ya uso wa maji”. Tunaweza kuona toka katika kifungu hiki kwamba Roho Mtakatifu hakai ndani ya mioyo iliyo jawa na vurugu na dhambi bali hukaa katika mioyo ya wale wenye kuiamini injili njema tu. Hata hivyo watu wengi kwa vurugu zao na utupu wa mioyo chini ya imani za matendo ya kimashamshamu, husema kwamba wanataka kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu huku wakiwa na dhambi mioyoni mwao. 
Roho atokanaye na hali ya kimashamshamu huyo si Roho. Kazi ya shetani hutegemea waumini waovu wenye tabia za kimashamshamu, na watu wa aina hii ni rahisi kwao kuishia katika mitego na nguvu za shetani. Lakini Roho Mtakatifu ni nafsi ya Mungu iliyo na ufahamu, hisia na inayo mapenzi kamili. Roho alitenda kazi na Mungu Baba na Mwana, Yesu Kristo, katika uumbaji wa dunia. Leo tutajifunza juu ya aina za kazi Roho Mtakatifu alizofanya hapa duniani.
 

Huuhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi.

Ni kazi gani ya kwanza kabisa Roho Mtakatifu hufanya? Huuwakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi. Watu wanaohakikishiwa naye ni wale wasio kubali injili njema ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani. Huakikishia wenye dhambi wote wasiyo amini injili ya maji na Roho.
 

Huuakikishia ulimwengu kwa habari ya haki.

Nini cha pili Roho Mtakatifu ufanyacho? Hubeba ushuhuda wa haki ya Mungu na juhudi za Yesu katika kuokoa wenye dhambi toka dhambini mwao. Yohana 16:10 inasema “kwa habari ya haki kwa sababu mimi naenda zangu kwababa wala hamnioni tena tena”. Yatupasa kufahamu nini maana ya haki ya Mungu katika Biblia. Hii maana yake ni ule ukweli kuwa Yesu alizichukua dhambi zetu zote ulimwenguni kwa njia ya ubatizo wa Yohana na hivyo kwa kila amwaminiye yeye ataweza kuwa mwenye haki kwa neema ya Mungu. Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji na kuzikubali dhambi zote za ulimwengu juu yake, kumwaga damu yake msalabani, akafufuka na kuwa mwokozi wa wote wenye dhambi. Hii ndiyo injili njema Mungu aliyetuapatia. Yesu alizibeba dhambi za ulimwengu kwa njia ya maji na damu kulingana na mapenzi ya Mungu na hivyo kuwa Bwana wa uzima wetu.
Roho Mtakatifu husaidia watu kuamini katika injili ya Ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani, na hivyo kuwasaidia kupata msamaha wa dhambi zao. Unapaswa kujua kuwa kazi za Mungu katika Utatu ni nyongeza. Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa injili nzuri, inawafanya watu waamini katika upendo wa Mungu. Ana hakikishia pia Injili ya maji na Roho kuwa ya kweli .
 

Kuuhakilishia ulimwengu kwa hukumu.

Lipi jukumu la tatu la Roho Mtakatifu? Huaribu kazi za shetani. Shetani hunong’oneza katika fikra za watu kwa kusema “unaweza kumwamini Yesu lakini uchukulie Ukristo kama mojawapo ya dini za ulimwengu.” Shetani hujaribu kukwaza watu katika kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani hata ikiwa wanamwamini Yesu. Kwa kuwa shetani huushushia hadhi Ukristo hata kuwa dini ya “kawaida”, wengi huangukia katika udanganyifu huu wa shetani na kwasababu ya kumwamini kwao Yesu huwa ni namna ya kuwa watu wema. Hata hivyo sababu halisi ya kumwamini Yesu ni kuweza kuzaliwa upya mara ya pili na kuwa mtu mwenye haki.
Usiwe na imani potofu. Imani potofu, kamwe haitokuwezesha kutakaswa na haijalishi ni kwakiwango gani utakuwa unamwamini Yesu ikiwa unaimani potofu. Hautoweza kumjua au hata kumwona Yesu dhahiri kutokana ulaghai huo wa shetani. Roho Mtakatifu huja kuwa mhakiki wa wokovu kwa wote wale walio okolewa kwa kuiamini injili njema ya maji na Roho. Imani zote za wale wenye dhambi mioyoni ni bure tu.
Roho Mtakatifu huthibitisha ukweli wa injili njema isemayo, Yesu alibatizwa ili kubeba dhambi zote za ulimwengu na alisulubiwa ili kulipia mshahara wa dhambi. Roho Mtakatifu huthibitisha ukweli huu, Roho Mtakatifu huwapa maelekezo watu wote wa ulimwengu katika kusamehewa dhambi zao zote kwa kuiamini injili ya kweli. Hata hivyo imetupasa kukumbuka kwamba Roho Mtakatifu huwadhihirishia na kuwahukumu wale wote wasio ichukulia injili njema katika mioyo yao.
 

Kila mtu imempasa awe na baraka ya Imani.

Baraka ya Imani ni nini? Ni ile imani ituongozayo katika kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu kwa njia ya msamaha wa dhambi. Hata hivyo leo hii tunaweza kuwaona wakristo wengi ulimwenguni pote ambao bado wanadhambi mioyoni mwao, ingawa wanaendelea kumwamini Yesu kwa kipindi kirefu. Tatizo kubwa hapa linalo wakwaza kutokombolewa toka dhambini ni kwamba, wao hudhani kunena kwa lugha na kupata maono ndiyo uhakika ya kwamba tayari wamekwisha mpokea Roho Mtakatifu. Hawana ufahamu juu ya hukumu ya Mungu kuhusiana na dhambi zao.
Watu wengi ulimwenguni hawajaweza kuainisha kati ya kazi ya Roho Mtakatifu na zile za shetani. Kazi za shetani huwapelekea watu katika viwango vya hali ya kuchanganyikiwa kwa kuwapa imani potofu na hata kufikia hali ya kuangamia. Hivi ndivyo shetani anavyojaribu kwenda kinyume na Mungu. Shetani husababisha watu kuangukia katika mazingira ya imani za kichawi na hata kuwadhibiti kuwa watumwa wake. Shetani huwashinikiza ndani yao kutamani matendo ya miujiza na maajabu kwa kuwasababisha kudhani ya kwamba mambo kama haya ndiyo muhimu kuliko kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu kwa njia ya imani katika injili njema.
Hata hivyo Roho Mtakatifu huwawezesha watu kuutambua Ufalme wa Mungu kwa njia ya Neno. Kwa kupitia Roho Mtakatifu huja kufahamu na kuamini kwamba Mungu aliwaumba wanadamu na kwamba Mungu anawapenda na pia Mungu anataka kuwaokoa. Mpango wake kwa wenye dhambi ni kwa Yesu Kristo kuwaokoa kwa dhambi zao kwa njia ya injili ya maji na Roho na kuwaalika kuishi katika upendo wake kwa imani.
1 Petro 3:21 inaema “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo unaowaokoa ninyi pia siku hizi” napia 1 Petro 1:23 inaema “Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili si kwa mbegu iharibikayo bali kwa ile isiyo haribika kwa neno la Mungu lenye uzima lidumulo hata milele”. 
Kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwaangazia watu ukweli juu ya dhambi haki na hukumu na kuwawezesha kuamini ukweli. Roho Mtakatifu huwawezesha kujua juu ya hukumu ya Mungu na hivyo kuweza kukombolewa toka na dhambi zao kwa kuiamini injili njema ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Roho Mtakatifu huwapa ufahamu ya kwamba yeye yu pamoja nao pale wanapokuwa na imani ya injili ya maji na Roho.
Kwa kiasi tumekwisha ona matendo ya Roho Mtakatifu. Watu wote ulimwenguni hapa wataweza kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu na upendo wa Mungu pale watakapo pata msamaha wa dhambi kwa kuiamini injili njema ya maji na Roho.
 

Nafsi ya Roho Mtakatifu.

Roho Mtakatifu ni Mwenyezi Mungu. Anahodhi tabia muhimu za nafsi ziitwazo ufahamu, hisia na matakwa. Kwa kuwa Roho Mtakatifu anahodhi ufahamu huweza hata kuchunguza yote hata mafumbo ya Mungu (1 Wakoritho 2:10) na hata mioyoni mwa wanadamu.
Kwa kuwa Roho Mtakatifu anahodhi hisia, hufurahishwa na wale wote wano amini neno la Mungu lakini huuzunishwa na wasio amini. Pia wenye haki huweza kuhisi upendo wa Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu pia huitwa “mtulizaji”. Hii inamana kwamba yeye huwasaidia wenye haki katika taabu na kuwaletea ushindi, kuwapigania dhidi ya maadui wao. Yeye ana ufahamu hisiya na mapenzi ndani ya wale wenye kuamini injili njema ya maji na Roho.
 

Kazi za Roho Mtakatifu ni kama zifuatazo.

Roho Mtakatifu huwawezesha watu kugundua ukweli wa msamaha wa dhambi na kuweka makazi ndani ya mioyo ya wanaoamini. Kazi yake ni kushuhudia ukweli kwamba Yesu alizibeba dhambi zote za wanadamu kwa njia ya ubatizo wake na damu yake (1 Yohana 5:6-8). Pia huwatuliza watumishi na watakatifu katika taabu na kuwatia nguvu katika kusimama imara upya. Yeye binafsi huomba kwa niaba yao pale wasiojua nini cha kuomba (Warumi 8:26). Na huwatuliza wenye haki katika kanisa la Mungu na kuwaongoza katika utele wa neno lake (Zaburi 23).
 

Kazi ya Roho Mtakatifu inahusika moja kwa moja na Biblia.

Roho Mtakatifu huwaongoza wenye haki kugundua na kuamini ukweli mioyoni mwao na hivyo kuhubiri ukweli huo kwa wengine. “Kila andiko lenye punzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho na kuwaonya watu makosa yao na kwa kuwaongoza kwa kuwaadabisha katika haki” (2 Timotheo 3:16). 
“Tafuteni katika kitabu cha Bwana mkasome, hapana katika hao wote atakaye kosa kuwapo hapa na moja atakayemkosa mwenzake kwa maana kinywa changu kimeamini na roho yake imewakusanya” (Isaya 34:16).
“Mkijua neno hili kwanza ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu: bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu” (2 Petro 1:20-21).
Roho Mtakatifu aliwatia hamasa watumishi wa Mungu kuandika maneno ya Mungu ili kwamba tuweze kuyasoma. Huwajulisha watu juu ya injili ya maji na Roho na kuwaongoza katika kuihubiri duniani. Hivyo, ingawa wanye haki huweza kuteseka kwa majarihu mengi katika maisha yao huweza kuyashinda kwa shukrani ya nguvu za Roho Mtakatifu.
 

Karama na Tunda la Roho Mtakatifu.

Matunda ya Roho Mtakatifu maana yake ni uwezo anao wapa watakatifu katika kuieneza injili ya Mungu kwa wengine. Kwajinsi hiyo Watakatifu huweza kujitolea nafsi zao kwa kazi ya Mungu kwa karama zote Mungu awapazo na hivyo Roho Mtakatifu huwasaidia katika kumpa utukufu Bwana. “Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana” (1 Wakorintho 12:7). 
Dhumuni la vipawa vya Roho Mtakatifu ilikuwa ni kuwezesha watakatifu kwa imani na kuwasaida kupiga mbio zilizo mbele yao (Waefeso 4:11-12). Roho Mtakatifu huwapa uwezo kuwa watumishi wa Mungu na watakatifu katika kuieneza injili. Kanisa la Mungu ni mkusanyiko wa watakatifu walio takaswa katika Kristo Yesu (1 Wakorinto 1:2). 
Kila Mkristo aliye kwisha mpokea Roho Mtakatifu imempasa kushika tabia inayo endana na nafasi aliyo kabidhiwa na kazi zake, kwa kuwa Yesu Kristo ndiye kiongozi wa kanisa. Roho Mtakatifu hutoa malengo ya kiroho na uwezo kwa watakatifu ili waweze kufanya kazi katika Ufalme wa Mungu. Hufanya kila jambo ili kudhihirisha wazi utukufu wa injili Mungu aliyo tupatia. Husema “Basi mlapo au mnywapo au mtendapo neno lolote fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu” (1 Wakorinto 10:31).
 

Aina za karama za Roho.

Zipo aina 12 za karama za Roho Mtakatifu. Tunaweza kuziona katika Biblia kwamba karama hizi huwa katika aina mbali mbali kwa watu tofauti. Mlolongo wa karama hizi huonekana katika Warumi 12:6-8, 1Wakkoritho 12:8-10 na Waefeso 4:11. Zifuatazo ni karama tisa za Roho zilizo ongelewa katika 1Wakoritho sura ya 12.
1. Neno la maarifa: Hili hutupa uelewa wa kiroho katika kuielewa injili ya majina ya Roho na hivyo kutuwezesha kuihubiri injili hii njema.
2. Neno la Hekima: Huu ni uwezo wa kutatua aina mbali mbali za matatizo yajitokezayo katika maisha ya mwenye haki kwa njia ya maandiko ya Mungu.
3. Imani: Roho Mtakatifu huleta imani madhubuti na uhakika kwa watakatifu ili waweza kufanya miujiza ya kuziokoa roho tokana na dhambi na shetani. Watu wenye haki wataweza kusamehewa dhambi zao na kuponywa matatizo yao ya kiroho kwa njia ya nguvu ya imani.
4. Uponyaji: Roho Mtakatifu huwapa uwezo wenye haki kuponya kwa kupitia imani ya neno la Mungu.
5. Matendo ya miujiza: Hii ni karama ya ajabu inayo mwezesha mtakatifu kutenda kazi ya Mungu kwa kuamini neno la Mungu. Miujiza ni kitu kitokeacho kwa njia ya kinyume na utaratibu wa kawaida, kwa njia ya imani au kinyume na uwezo wa ufahamu wa mwanadamu na utaratibu wa asili.
6. Unabii: ni kwa wale tu wenye kuamini na kutii neno la Mungu kwa sasa ndiyo watakao toa unabii kwa kilicho andikwa. Maneno ya mtu asiye na imani isiyo na msingi wa maandiko ya neno la Biblia hayatoweza kuwa unabii wa kweli. Watumishi wa Mungu walio na upeo wa Roho Mtakatifu huubiri neno la Mungu na kupelekea nasaha na kufundisha kwa kufanya kazi ya Mungu kwa njia ya kanisa ambalo ndiyo mwili wa Yesu. Roho Mtakatifu huwapa uwezo watumishi wa Mungu na watakatifu.
7. Kupambambanua Roho: Huu niuwezo wa kupima ikiwa mtu fulani anao msamaha wa dhambi. Inawezekana kwetu kuongozwa vibaya na shetani ikiwa hatutokuwa na karama hii, kwa kuwa ulimwengu umetawaliwa na shetani, tunaweza kuwa na karama hii. Mwenye haki hupokea karama hii kwa kuamini ukubwa wa injili. Kwa jinsi hiyo ataweza kuelezea ikiwa mtu fulani bado anadhambi moyoni.
8. Kunena kwa lugha: Biblia hutuambia juu ya kunena kwa lugha, “Napenda kunena maneno matano kwa akili zangu nipate kuwafundisha wengine zaidi ya kunena maneno kumielfu kwa lugha” (1 Wakorintho 14:19). Watakatifu imewapasa kuelewa ya kwamba ni muhimu zaidi kuelewa neno la Mungu la kweli kuliko kunena kwa lugha ambako yeye binafsi hawezi kujielewa. Imempasa aachane na kunena kwa lugha.
9. Tafsiri za lugha: Karama hii walipewa wafuasi ili kuwawezesha kuishudia injili katika kanisa la mwanzo. Nyakati hizi Roho Mtakatifu anaihubiri injili kwa njia ya huduma ya kutafsiri na kuainisha ujumbe katika aina mbalimbali za lugha. Hatuna haja ya mkalimani ikiwa yupo awezaye kuhubiri kwa kuongea lugha mbalimbali hata hivyo tunapokumbuna na mipaka ya lugha, Mungu siku zote hutuwezesha katika kutafsiri ili kuitimiza kazi yake. Mungu hatendi kazi kwa machafuko au katika hali ya mchanganyiko. Roho Mtakatifu hutenda kazi katika injili njema na pia kutuongoza sisi watakatifu katika kutafsiri injili katika aini mbalimbali za lugha.
 

Ni yapi matunda ya Roho Mtakatifu?

Kuhusiana na matunda ya Roho Mtakatifu, biblia inatuambia “lakini tunda la roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utuwema, fadhila, uaminifu, upole, kiasi juu mambo kama hayo hakunasheria” (Wagalatia 5:22-23).
1. Upendo: upendo wa kweli ni kwa wenye haki kushiriki katika kuokoa wale wote wenye dhambi kwa njia ya kuwahubiria injili njema ya maji na Roho. Kwa kuwa watu wenye haki ndiyo wenye injili njema ambayo ndiyo upendo wa Yesu, basi wao ndiyo wenye upendo wa kweli kwa roho nyingine. 
2. Furaha: hii ni furaha yenye utukufu isiyo elezeka inayobubujika toka kwenye kina cha mioyo pale tunapo zaliwa upya mara ya pili. Mtu mwenye haki aliyesamehewa dhambi zake zote anayofuraha moyoni mwake (Wafilipo 4:4). Kwa kuwa ipo furaha mioyoni mwa wenye haki basi wao ndiyo wenye uwezo wa kushiriki furaha hiyo na watu wengine.
3.Amani: huu ni moyo uliyo tulia ambao mtu mwenye haki hupatiwa kwa kusamehewa dhambi zake zote kwa kuwa na imani ya injili ya maji na Roho. Roho Mtakatifu ndiye asababishaye mwenye haki kuihubiri injili njema ya amani. Watu walio isikia injili njema ya amani wana uwezo wa kuongoza wengine kuzishinda zambi za ulimwengu na kuweza kuwa na ufahamu wa imani wenye nguvu na kuwa kifua mbele kwa karama ya wokovu. Watu wenye haki wanaoleta amani kati ya Mungu na wanadamu huitwa wana wamungu (Mathayo 5:9) na kuwaongoza wengine kupata msamaha wa dhambi (Mithali 12:20). Roho mtakatifu husababisha wenye haki kuishi maisha yenye haki na kuwabariki wengine kwa amani kwa kuieneza injili njema.
4. Uvumilivu: Tunda la uvumilivu limo ndani ya mioyo ya wenye haki ambao walio kwisha kombolewa tokana na dhambi zao kwa kuamini injili ya kweli. Tunaweza kuwa na tunda hili kwa kuchochea bila kikomo hisia za ushindi na Roho Mtakatifu. Katika moyo wa mwenye haki upo uvumilivu na subira.
5. Wema: Mungu aliturehemu pale tulipokuwa wenye dhambi na hivyo kutukomboa kwa dhambi zetu zote kwa injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Nasi pia tutaweza kuwapenda na kuwarehemu wengine kwa sababu Yesu aliturehemu na kutufutia dhambi zetu zote. Na kwa kuwa tunamwamini yeye na kupokea rehema yake mioyo ya wenye haki imefurika wema na matunda ya injili njema.
6. Fadhili: Hapa maana yake “matendo mema” watu wenye haki wana fadhili katika Bwana ndani ya kinywa na ndani ya kina cha mioyo yao.
7. Uaminifu: Hapa maana yake ni ule moyo uliojawa na imani katika Mungu. Uaminifu wa mtakatifu huja kutokana na kutunza amana ya Yesu. 
8. Upole: Maana yake ni kuwa na uwezo wa kuwaelewa wengine kwa ukamilifu na kuwachukulia kwa upole na taratibu mioyoni mwetu. Wenye haki wanamioyo ya kuwapenda maadui zao na kuwaombea kwa ajili ya ukombozi wao.
9. Kiasi: Huu ni uwezo wa kujitawala nafsini, kujizuia katika kuishi maisha yasiyo ya uadilifu kwa kuwa na kiasi.
 

Kujazwa na Roho Mtakatifu. 

Nini matokeo ya kujazwa na Roho Mtakatifu? Kwa kupokea baraka hii kunawezesha watakatifu kuishi wakiwa wafuasi wa Yesu Kristo huku wakijiunga na kanisa la Mungu. Roho Mtakatifu huwezesha wenye haki kuwa vyombo vya haki na kujitolea kutimiza mapenzi ya Kristo. Mapenzi ya wenye haki huongozwa na mapenzi ya Bwana na kwa hiyari hujitolea mali zao zote na vipaji vyao kwake. Roho Mtakatifu huwawezesha wenye haki kuishi maisha ya kujitolea ili kuzishinda dhambi za ulimwengu wakiwa na fikra za ushindi, furaha na kifua mbele, na si ufukara wa kiroho kushindwa na kuchanganyikiwa (Warumi sura ya 7).
“Lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu nanyi mtakuwa mashaidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi yote na Samaria na hata mwisho wa nchi” (Matendo 1:8). Ujazo wa Roho Mtakatifu huwaongoza wenye haki katika kuihubili injili.
Bwana aliwapa hisiya ya imani yenye nguvu kwa wale ambao Roho Mtakatifu ameweka makazi ndani yao. Na Mungu amewapa haki watoto wake wale ambao wamekwisha samehewa dhambi zao kwa imani ya injili ya Yesu (Yohana 1:12). Watu wenye haki walio wana wa Mungu kwa njia ya imani ndiyo wenye kuweza kuihubiri injili njema ulimwenguni.
Watu wenye haki wanauwezo wa kumshinda shetani kupitia injili ya msamaha wa dhambi. Pia wanayo nguvu ya kuponya magonjwa ya kiroho, (Marko 16:18) kukanyaga nguvu za shetani, (Luka 10:19) na kuingia katika Ufalme wa Mbinguni (Ufunuo 22:14) Watu wenye haki huishi na mamlaka sawa na wafalme kwa kuyaamini maneno ya ahadi za Mungu (Wakorintho 6:17-18).
Roho Mtakatifu huwewazesha watu wenye haki kukabili tamaa zao za dunia. Pia hutuongoza katika kuhubiri injili ya kweli (Wagalatia 5:6).
Roho Mtakatifu husababisha wenye haki kusoma na kuamini injili nzuri na kuifundisha kwa wengine (1 Timotheo 4:13) .
Roho Mtakatifu huwakutanisha wenye haki katika kanisa la Mungu (Waebrania 10:25).
Roho Mtakatifu huwawezesha wenye haki kukiri dhambi zao (1 Yohana 1:9) ili kufanya mioyo yao iangaze nuru ya kweli (Waefeso 5:13).
Roho Mtakatifu huwaongoza wenye haki kuelekea njia ya kweli katika maisha yao (Zaburi 23). 
Roho Mtakatifu huwaambia wenye haki wasizimishe karama zake ndani yao (1 Wathesalonike 5:19).
Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa njia ya injili njema (Marko 16:17-18).
Roho Mtakatifu huongoza wenye haki katika kuishi wakiwa wafuasi wa Bwana kwa kujiunga katika kanisa la Mungu. Huwaongoza wenye haki kuishi maisha ya kiroho ya kuihubiri injili njema na kujazwa na Roho Mtakatifu. Hii ndiyo kazi ya Roho Mtakatifu kupitia njia ya injili njema (1 Petro 2:9).
Hufanya kazi ndani ya mioyo ya watakatifu hata katika muda huu. Haleluya!