Search

VITABU VILIVYOCHAPISHWA BURE,
VITABU NA VITABU VYA AUDIO

The New Life Mission ni huduma inayomtumikia Mungu kwa kueneza injili ya maji na Roho kwa watu duniani kote kupitia Huduma ya Fasihi katika lugha mbalimbali.

Lugha za tovuti: Lugha 27 Msaada wa lugha kwa vitabu-pepe: Zaidi ya lugha 130 Vitabu-pepe vya lugha moja: Zaidi ya vitabu 1,700 Vitabu-pepe vya lugha mbili: Zaidi ya vitabu 360 (Husasishwa mara kwa mara)
The New Life Mission inafanya Huduma ya Fasihi kupitia vitabu ili kufikisha ukweli wa Neno la Mungu kwa watu duniani kote, na inatoa mfululizo wa vitabu-pepe vya Kikristo na vitabu vya sauti vya Mchungaji Paul C. Jong bila malipo yoyote kwa wageni wote. Tembelea tovuti yetu kwa uhuru na upakue vitabu-pepe, vitabu vya lugha mbili na nyenzo za vitabu vya sauti bila malipo kwenye simu yako, kompyuta kibao au kompyuta ili kusoma na kusikiliza popote, wakati wowote.
  • Vitabu vilivyochapishwa vinapatikana kwa ununuzi binafsi kwenye Amazon. (Vitabu-pepe vya Kindle pia vinapatikana kupakua)
  • Ikiwa unataka kujiunga na huduma yetu kama msambazaji wa vitabu (kupokea na kusambaza vitabu vilivyochapishwa bila malipo) au kama mfasiri, tafadhali soma kwanza Kitabu 1 kutoka kwa mfululizo wa Mchungaji Paul C. Jong. Kisha jiandikishe kama mshirika kwenye tovuti na usubiri idhini ya msimamizi. Baada ya kupata idhini, utathibitishwa kama mshirika.
Lugha
Warning Chagua lugha yako

Vitabu vinavyopendekezwa zaidi

Roho Mtakatifu akaaye ndani yangu - Njia ya tahadhari kwako katika kumpokea Roho Mtakatifu

Kiswahili 3

Roho Mtakatifu akaaye ndani yangu - Njia ya tahadhari kwako katika kumpokea Roho Mtakatifu Rev. Paul C. Jong

Katika Ukristo nyakati hizi, mojawapo ya mambo yanayozungumziwa mara nyingi ni kuhusiana na habari za "wokovu toka dhambini" na "kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu". Hata hivyo ni watu wachache walio na ufahamu ulio sahihi wa mambo haya mawili, ingawa ukweli ni kwamba haya ni mabo mawili muhimu kuhusiana na maswala ya Ukristo. Mbaya ni nini, bado hatujaweza kupata maandiko yanayo tufunza kwa uwazi juu ya mambo haya yaliyo tajwa hapo juu. Wapo watunzi wa vitabu wa Kikristo walio wengi wakitukuza karama za Roho Mtakatifu au kuelezea maisha ya kujazwa na Roho. Lakini hakuna hata mmoja kati yao anaye thubutu kushughulika na swali la msingi,nalo ni "Kwa namna gani anaye amini ataweza kumpokea Roho Mtakatifu kwa uhakika?" Kwanini? Ukweli wa kushangaza ni kwamba hawajaweza kuandika kwa viwango vilivyo kamili kwa sababu hawakuweza kuwa na ufahamu ulio kamili juu ya hili. Kama vili Nabii Hosea alipo paza sauti na kusema "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa", kwa nyakati hizi si wakristo wachache wanao vutwa katika ushabiki wa kidini, wakitegemea kumpokea Roho Mtakatifu. Huamini kwamba wataweza kumpokea Kumpokea Roho Mtakatifu baada ya kufikia kiwango cha hisia kali na mashamusham. Lakini si swala la kutia chumnvi tukisema kwamba kinacho itwa imani na watu hawa ndicho kinacho fanya Ukristo udharaulike na hata kuonekana kama mojawapo tu ya dini mfano Shama (Shamanism), na ukereketwa wa aina hii unatoka na Shetani
Mtunzi, Mchungaji Paul C. Jong huthubutu siku zote kutangaza ukweli. Hujihusisha na maswala yaliyo muhimu kwa kiwango cha kutosha, ambacho wengi wa watunzi wa vitabu vya kiroho wamekwepa kwa muda mrefu. Kwanza amefafanua maana ya "kuzaliwa upya mara ya pili" na "kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu" na kuelezea uhusiano usio kwepeka kati ya mambo yaha mawili ya ngozo za msingi. Na ndipo basi akachukua maelezo ya kina kwa pamoja kuhusiana na Roho Mtakatifu, kuanzia "namna ya utambuzi war oho" kuelekea "namna ya kuishi maisha ya ujazo wa Roho". Kwa habari zaidi mwandishi anakushauri uchunguze yaliyomo katika kitabu hiki ambayo yamewekwa katika kurasa za tovuti hii.

Komentare na Mahubiri Juu ya Kitabu cha Ufunuo - JE, NYAKATI ZA MPINGA KRISTO, KUFIA-DINI, KUNYAKULIWA NA UFALME WA MILENIA ZINAKUJA? (Ⅰ)

Kiswahili 7

Komentare na Mahubiri Juu ya Kitabu cha Ufunuo - JE, NYAKATI ZA MPINGA KRISTO, KUFIA-DINI, KUNYAKULIWA NA UFALME WA MILENIA ZINAKUJA? (Ⅰ) Rev. Paul C. Jong

Baada ya mashambulio ya kigaidi ya tarehe 11 mwezi Septemba kulitokea msongamano katika tovuti hii "www.raptureready.com," ambayo ni tovuti inayotoa habari juu ya nyakati za mwisho, iliripotiwa kuwa watumiaji wa tovuti hiyo walizidi zaidi ya milioni 8. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa ushirikiano kati ya kituo cha CNN na kile cha TIME ulionyesha kuwa zaidi ya asilimia 59 ya Wamarekani wanaamini katika mafundisho ya siku za mwisho.
Akijibu masuala hayo ya nyakati, mwandishi anatoa ufafanuzi wa mada kuu za kitabu cha Ufunuo, zikiwemo mada za kuja kwa Mpinga-Kristo, Kufia-Dini, yaani kufa kwa watakatifu kwa ajili ya dini, Kunyakuliwa, Ufalme wa Milenia, na Mbingu na Nchi Mpya, zote zikitoka katika mazingira ya maandiko yote na chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu.
Kitabu hiki kinatoa maelezo katika mfumo wa komentare wa aya kwa aya toka katika Kitabu cha Ufunuo huku aya hizo zikiongezewa nguvu na mahubiri ya kina toka kwa mwandishi. Yeyote atakayesoma kitabu hiki atakuja kuifahamu mipango ambayo God anayo kwa ulimwengu huu.
Sasa ni wakati wako kutambua juu ya hitaji kamilifu la kuamini katika injili ya maji na Roho ili uweze kuipata hekima inayoweza kukukomboa toka katika majaribu na taabu zote za nyakati za mwisho. Kwa kupitia vitabu hivi viwili na kwa kuamini katika injili ya maji na Roho utaweza kuyashinda majaribu na taabu zote zilizotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo.

Vitabu Vipya

Vitabu vya kieletronic na Vitabu vya kusikiliza vya mwandishi Paul C. Jong

Panga
Jumla 23
The New Life Mission

Shiriki katika utafiti wetu

Ulitujuaje?