Search

ЧЗВ за Християнската Вяра

Тема 2: Светият Дух

2-5. Nini Roho Mtakatifu anachofanya nyakati hizi?

Roho Mtakatifu katika nyakati hizi kwa uwazi hufanya kazi ya kutambulisha na kuweka bayana mafundisho ya uwongo kwa kupitia maneno ya Mungu.Yeye ndiye anaye hubiri injili ya maji na Roho, ambayo Bwana ametupatia kwa nafsi zinazokufa kutokana na uovu katika kipindi hiki cha mkanganyiko ili kuokoa.
Yatupasa kuelewa yakwamba wapo manabii wa uongo watendao kazi ndani ya Ukristo siku hizi ulimwenguni pote. Ingawa wanadhambi mioyoni mwao bado wanatenda dhambi, wakinena kwa lugha, wakitenda miujiza ya uongo, na kuona maono. Kwa nafsi zilizo changanyikiwa katika nyakati hizi Roho Mtakatifu aliye msaidizi ana uhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi, haki na hukumu (Yohana 16:8).
Kabla ya yote, Roho wa kweli huleta hukumu ya dhambi kwa wanadamu. Dhambi katika mtazamo wa Mungu ni kule kutoiamini injili ya maji na Roho aliyotupatia. Yeye huleta hukumu ndani ya mioyo ya wale wote wasio iamini injili njema ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana Mbatizaji na damu yake msalabani, huku akionya kwamba ni wenye dhambi na mwisho wao ni motoni.
Pia yeye hushuhudia juu ya haki ya Mungu alivyo mtuma Yesu kuja ulimwenguni akiwa mfano wa mwanadamu ili aweze kubeba dhambi zote za ulimwengu. Roho Mtakatifu husaidia watu wanao mwamini Yesu kupokea msamaha wa dhambi kwa kuamini injili ya maji na Roho, pia kuwaonya wale wote wasio tii injili ya kweli ingawa wanaelewa mapenzi ya Mungu wataweza kuhukumiwa kwa dhambi zao hapo baadaye.
Hapo mwanzo wakati Mungu alipoumba ulimwengu kwa neno lake, Roho Mtakatifu alishirikiana naye na baadaye kuleta nuru ya kweli katika mioyo iliyo na utupu na kuchanganyikiwa ya wanadamu ili aweze kung’arisha kwa injili ya maji na Roho (Mwanzo 1:2-3). Kwa haya yote Roho Mtakatifu ameweka nuru katika nafsi zilizochanganyikiwa kwa dhambi katika nyakati hizi kupitia haki ya Mungu na hukumu ya dhambi zao.