Search

דרשות

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 8-2] Haki ya Mungu, Utimilifu wa Hitaji la Sheria Kwa Mwenye Haki (Warumi 8:1-4)

(Warumi 8:1-4)
“Sasa, basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya Roho.”
 

Warumi 8:1-4 inatueleza sisi juu ya aina ya imani ambayo wale walio katika Kristo wanayo. Siri ya kifungu hiki ni kwamba tunaweza kukutana na maagizo yote ya Sheria katika haki ya Mungu kwa imani yetu. 
Je, imani inayoamini katika haki ya Mungu ni ipi? Hii ni imani ambayo imepokea ondoleo la dhambi kwa kuamini katika ubatizo wa Yesu na damu yake ambayo kwa hiyo Bwana wetu alizichukulia mbali dhambi zote za ulimwengu. Kwa hiyo tunaweza kuishinda dhambi kwa kuamini katika Yesu ambaye ameitimiza haki yote kwa kuifuatilia haki ya Mungu kama Mwokozi wetu. Hii ni imani ambayo inaifuata haki ya Mungu na ushindi wetu katika imani. 
Kwanza kabisa, Warumi 8:1 inatueleza kuwa, “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.” Wale ambao wataishi katika Yesu Kristo kwa kuamini katika haki ya Mungu kwa hakika hawana dhambi. Imani ya jinsi hiyo imejengwa katika ubatizo wa Yesu na damu yake ambavyo vimelitimiza hitaji la Sheria kwa mwenye haki. Imani katika haki ya Mungu ndiyo imani ya msingi kwa watakatifu waliozaliwa tena upya. Inawezekanaje kwa viumbe wadhaifu kuwa hawana dhambi? Lakini bado kwa kuwa na imani yao isiyotikisika katika haki ya Mungu kwa kupitia Yesu Kristo dhambi zao zote zimetoweshwa. Hii ni kwa sababu Yesu alizichukua katika mwili wake dhambi zote za ulimwengu kwa kupitia ubatizo wake kwa ajili ya wale wote wanao amini katika haki ya Mungu. 
Warumi 8:3 inatueleza sisi kuwa Mungu alimtuma “Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi,” na kwamba “aliihukumu dhambi katika mwili.” Kwa maneno mengine, kule kusema kuihukumu dhambi katika “mwili” wa Yesu, maana yake ni kuwa Mungu Baba alizipitisha dhambi zote za ulimwengu juu ya Mwanawe pekee. Neno hili la kweli linafunuliwa katika Mathayo 3:13-17 (majadiliano zaidi ya kina katika somo hili yanaweza kupatikana katika kitabu changu kinachoitwa, “Je, Umezaliwa Upya Kweli Kwa Maji na Kwa Roho?”). Wale wanaoamini katika ukweli huu hawana dhambi kwa sababu Mungu amezisamehe dhambi zote za ulimwengu kwa haki yake.
 

“Ole wangu Maskini mimi mwenye dhambi!”
 
Kifungu cha maandiko toka Warumi 7:24 hadi 8:6 kina mambo makuu mawili ambayo yanakinzana. Moja kati ya mambo hayo ni majadiliano kuhusu tatizo la dhambi, kwa maneno mengine ni kuhusu kutomtii Mungu kwa sababu ya tamaa ya mwili wake, na jambo jingine ni majadiliano ya suluhisho la tatizo hili la dhambi ambalo amelipata katika Yesu Kristo. 
Warumi 7:24-25 inasema, “Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Namshukuru Mungu kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.” Paulo alilia kuwa yeye ni mtu maskini hasa pale alipouangalia mwili wake, lakini alimshukuru Mungu kwa sababu alikombolewa toka katika mwili wake kwa kupitia Yesu Kristo. Pia tunaweza kutambua kuwa hata Paulo aliitumikia sheria ya Mungu katika akili zake, lakini mwili wake aliitumikia sheria ya dhambi. 
Paulo alikiri kuwa mwili wake ulikuwa unaifuata sheria ya dhambi ambayo haimpendezi Mungu badala ya kuishi maisha ambayo yanampendeza Mungu. Lakini bado Paulo alisema kuwa katika akili zake anaifuata sheria ya Roho wa Mungu. Hali akiwa kati ya sheria hizi mbili, Paulo alijihisi kuwa ni maskini na mpweke, lakini hata hivyo alitangaza ushindi wa imani kwa kumshukuru Mungu kwa kumkomboa toka katika dhambi zake kwa kupitia imani yake katika Yesu Kristo, ambaye ndiye utimilifu wa haki ya Mungu.
Paulo aliweza kutoa shukrani za jinsi hiyo kwa sababu aliamini kuwa Yesu Kristo alizipatanisha dhambi zake zote pamoja na dhambi za wanadamu wote. Ili kuzichukua dhambi hizi, Yesu alizibeba dhambi zote za wanadamu katika mwili wake kwa kubatizwa na Yohana. Yesu amewaokoa wote wanaomwamini toka katika dhambi zote za ulimwengu kwa kuhukumiwa kwa ajili ya dhambi hizo Msalabani. Hii ndiyo sababu Paulo alitangaza katika Warumi 8:1 kuwa, “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.” Kule kusema kuwa hakuna hukumu ya adhabu maana yake ni kuwa hakuna dhambi kabisa katika wale wanaoamini katika haki ya Mungu. Wale walio katika Kristo Yesu kwa kuamini katika haki ya Mungu hawawezi kuwa na dhambi katika mioyo yao. Wanaweza kuwa wadhaifu katika mwili lakini hata hivyo hawana dhambi. 
Kinyume chake, hukumu ya adhabu ina maanisha ni uwepo wa dhambi, hii ni sawa na kusema hali ya kuhukumiwa adhabu. Wakati mtu anapokuwa amefanya jambo fulani vibaya mara nyingi tunasema kuwa jambo hili ni dhambi. Lakini hii ni kwa sababu mtu huyo haamini katika haki ya Mungu kuwa yeye ni mwenye dhambi. Lakini kifungu hicho hapo juu bado kinatueleza sisi kuwa hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. 
Hata hivyo, tamko hili halijengwi juu ya Fundisho la Kiimani linaloitwa Kuhesabiwa Haki Kwa Imani ambalo dini nyingi za duniani zinadai kuwa zinasimama katika fundisho hilo. ‘Ukiri wa imani wa kuhesabiwa haki kwa imani’ una maanisha nadharia ya madai tete kwamba Mungu anamchukulia mtu kuwa mwenye haki hata pale ambapo si mwenye haki na ana dhambi katika moyo wake eti kwa kigezo cha imani yake tu katika Yesu. Kwa kweli hili ni kosa. Inawezekanaje Mungu akadanganya na kumuita mwenye dhambi kuwa hana dhambi? Mungu hawezi kufanya jambo hili. Badala yake Mungu atamwita mwenye dhambi huyo kwa kusema, “Unakabiliwa na uhakika wa kifo kwa sababu ya dhambi zako; amini katika haki yangu inayo onyeshwa katika injili ya maji na Roho!” 
Siku hizi watu wengi wanajaribu kuzifanya imani zao zenye makosa kuwa sahihi na kuipata haki ya Mungu hali waking’ang’ania katika mafundisho hayo ya kiimani. Lakini aina hii ya imani ni potofu na ya hatari. Kama Yesu asingekuwa Mungu wa ukweli basi pengine angelimwita mwenye dhambi kuwa mfuasi wake. Lakini ni lazima utambue kuwa Yesu, ambaye ni Kweli, hamwiti mwenye dhambi kuwa ni mwenye haki na asiye na dhambi. Kumwita mwenye dhambi kuwa ni mwenye haki na asiye na dhambi ni kitu ambacho hakiwezekani mbele za haki ya Mungu na mbele ya utakatifu wake. 
Ni lazima utambue kuwa ukombozi wako toka katika dhambi hauji kwa kumwamini Yesu tu, bali kwa kuamini katika haki ya Mungu ambayo baadaye inafanyika kuwa haki yako. Hata kama unamwamini Yesu, Mungu hawezi kukuita wewe kuwa ni mwenye haki ikiwa hauifahamu na hauiamini haki ya Mungu. Lakini ukweli wa siku hizi ni kuwa mafundisho ya kiimani kama Fundisho la Utakaso Unaozidi na Fundisho la Kuhesabiwa Haki kwa Imani yanakubaliwa na watu wengi kuwa ni mafundisho halisi ya Kikristo ya kiothodoksi. Lakini ni watu wachache tu wanaotambua kuwa kitu kinachoitwa mafundisho ya kiothodoksi kinaweza kumzuia mtu kuweza kuitambua na kuipata haki ya Mungu. Watu wengi wameshindwa kuipokea haki ya Mungu kwa sababu wanaamini katika mafundisho haya ambayo yapo kinyume na haki ya Mungu na kwa sababu hiyo mafundisho haya yamegeuka kuwa na mawe yanayowakwaza. 
Ikiwa unataka kuwa Mkristo wa kweli basi ni lazima ujipime wewe mwenyewe kwa Neno la Mungu ili kuona ikiwa kweli umo katika Kristo au la. Na ili kufanya hivyo ni lazima usikie, uone, na ulifahamu Neno la maji na Roho. Hebu jiulize mwenyewe, “Je, imani yangu katika Yesu ipo sahihi? Ninaposema kuwa ninamwamini Yesu, je mimi sifanyi mambo ya kidini? Je, ninababaika nikiwa nusunusu, sipo nje wala ndani ya Yesu?” Sasa ni wakati wako wa kuipokea haki ya Mungu kwa kuiamini na kukaa katika imani ya ukweli kuwa “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.”
Katika Waefeso tunaweza kukutana na kifungu hiki, “kwa kupitia ukombozi ulio katika Yesu.” Hii ina maanisha kuwa Mungu amekwisha tuchagua awali na kututeua sisi katika Kristo Yesu ili kutuokoa toka katika dhambi zetu zote. Wale waliopatanishwa na haki ya Mungu katika Yesu na wameingia ndani ya Kristo ndio wale ambao dhambi zao zimetoweshwa mbali kikamilifu. Kwa hiyo, wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho iliyotolewa na Bwana wetu hawakabiliwi na hukumu ya adhabu katika Yesu Kristo. Wakati mtu anapoamini katika injili ya maji na Roho, basi mtu huyo anafanyika kuwa mtu aliyeipokea haki ya Mungu katika Bwana ambaye anaihubiri injili hii. 
Wale wanaoamini katika haki ya Mungu katika Yesu Kristo na walioingia katika mikono yake iliyo wazi basi watu hao hawana dhambi. Huu ni ukweli na jibu sahihi. Hii ni kwa sababu ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani imezifanya dhambi zote kutoweka kwa wale walio katika Kristo kwa kuamini katika haki ya Mungu, na kwa sababu hiyo haiwezekani kwa wao kuwa na dhambi. Hivyo basi, wale walio katika Kristo hawana dhambi. Ukweli huu kuwa wale walio katika Kristo hawana dhambi ni jibu linalopatikana katika Neno la maji na Roho, na kwa sababu hiyo, hakuna kitu ambacho kinachochanganya kuhusiana na tatizo la dhambi. Unapoamini katika haki ya Mungu iliyofunuliwa katika injili ya maji na Roho, basi wewe pia unaweza kufanyika kuwa mwenye haki. Naomba ufahamu na uamini katika injili ya maji na Roho ambayo ina haki ya Mungu ndani yake. Hapo ndipo unapoweza wewe pia kufanyika mtakatifu mwenye haki anayeishi ndani ya Kristo. 
Hebu fikiria kama vile tunakutana na tatizo kubwa sana. Ikiwa kweli tunataka kupata suluhisho kwa tatizo hili, basi ni lazima tuendelee kutafuta jibu bila kujalisha magumu na shida ambazo tunaweza kukutana nazo. Vivyo hivyo, wale wanaoamini katika Yesu na bado hawajaingia ndani yake basi ni lazima waitafute haki ya Mungu iliyofunuliwa katika injili ya maji na Roho. 
Baadhi ya watu wanaufikiria Ukristo kama moja ya dini nyingi za ulimwengu na wanajaribu kutafuta suluhisho la dhambi zao kwa kuamini katika mafundisho hayo mfano ni Fundisho la Utakatifu Unaozidi. Lakini ni hivi punde tu watatambua kuwa si mafundisho ya jinsi hiyo wala haki yao binafsi inayoweza kuzisafisha dhambi zao. Na badala yake watagundua kuwa tatizo lao la dhambi linaweza kutatuliwa kwa urahisi kwa kuamini katika injili ya maji na Roho. 
Ikiwa unapenda kuwa Mkristo wa kweli basi ni lazima uipokee haki ya Mungu kwa kuamini katika injli ya maji na Roho katika moyo wako. Lakini watu wa kidini wanajitahidi kuipata haki ya Mungu kwa kujipima katika mafundisho hayo ya kiimani kama vile Fundisho la Utakatifu Unaozidi na Fundisho la Kuhesabiwa Haki kwa Imani huku wakijitahidi kulitatua tatizo la dhambi zao kwa matendo yao binafsi. Imani za jinsi hiyo zinapelekea watu kutegemea sala za toba ambazo hatimaye haziwezi kuwakomboa toka maangamizo yao yaliyo dhahiri kwa sababu wanaendelea kuwa wenye dhambi zaidi na zaidi na mara wanapoziona dhambi zao basi wanarudi na kufanya sala za jinsi hiyo, yaani sala za toba. 
Lakini wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho, ijapokuwa wanaweza kuwa na madhaifu katika mwili, ukweli ni kuwa watu hao wamelitatua tatizo lote la dhambi kwa kuamini katika haki ya Mungu. Wale walioipokea haki ya Mungu kwa kuamini hivyo hawana dhambi katika akili zao na kwa sababu hiyo hakuna hukumu ya adhabu juu yao. 
 

Kwa Sababu Haki ya Mungu Ipo katika Yesu
 
Aya ya 2 inasema, “Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.” Mungu amempatia mwanadamu sheria mbili, sheria ya Roho wa uzima ulio katika Yesu na sheria ya dhambi na mauti. Kama Paulo anavyotueleza, sheria ya Roho wa uzima imetuweka huru mbali na sheria ya dhambi na mauti toka katika dhambi zetu zote. Ni lazima utambue na kuufahamu ukweli huu uliozungumzwa na Paulo ili uweze kupokea maisha mapya. Ukweli huu unamhusu kila mtu sawa katika ulimwengu huu. 
Sisi pia tumewekwa huru toka katika sheria ya dhambi na mauti kwa kuamini katika sheria ya Roho wa uzima; vinginevyo tungekuwa tumekutana na maangamizi chini ya sheria ya dhambi na mauti. Lakini kwa kuamini kwa mioyo yetu katika haki ya Mungu katika Yesu—ambayo ni ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani—basi sisi tumeipokea haki ya Mungu na tumewekwa chini ya sheria ya Roho wa uzima na kuupokea uzima wa milele uliokuwa umeandaliwa kwa ajili yetu. Ni wapi basi unapoweza kuipata injili ya maji na Roho inayoweza kuzisamehe dhambi zako zote? Huu ni ubatizo ambao Yesu aliupokea toka kwa Yohana na Msalaba ambao kwa huo aliimwaga damu yake. Kwa maneno mengine, haki ya Mungu inapatikana katika injili ya maji na Roho. 
Je, injili ya haki ya Mungu inayotuweka huru mbali na sheria ya dhambi na mauti ni ipi? Ni injili ambayo kwa hiyo Bwana wetu alizaliwa hapa duniani, akabatizwa na Yohana alipokuwa na umri wa miaka thelathini ili kuzichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake, alisulubiwa Msalabani na kisha akafufuka toka kwa wafu ili kutukomboa sisi toka katika dhambi zetu zote—hii ndiyo injili iliyoundwa kwa haki ya Mungu. 
Mungu, hali akijua kuwa mwanadamu alikuwa amefungwa ili kutenda dhambi amepanga kuwaokoa wenye dhambi wote toka katika dhambi zao kwa kupatia injili ya wokovu inayoweza kuwaweka huru toka katika sheria ya dhambi na mauti. Hii ndiyo injili sahihi ya upatanisho inayopatikana katika ubatizo wa Yesu alioupokea toka kwa Yohana na damu yake Msalabani. Watu wote wanaweza kuwekwa huru toka katika sheria ya kifo kutokana na dhambi zao kwa kuamini katika injili hii—hii haki ya Mungu ni sheria ya uzima ambayo imemkomboa mwanadamu toka katika dhambi zake zote. 
Mungu alimpatia mwanadamu Neno la Sheria na alipanga kuwa kushindwa kwa aina yoyote kule kuishi kwa kuifuata Sheria kutakuwa ni dhambi. Kwa wakati huo huo, Mungu ameiweka sheria ambayo inaweza kuwaokoa wenye dhambi toka katika dhambi zao. Sheria hii ya wokovu ni ukweli uliofichika katika haki ya Mungu, ni sheria ya neema inayotoa uzima wa milele kwa wale wanaoamini. Sheria ya upatanisho ambayo Mungu ameiweka kwa wanadamu ni sheria ya imani katika injili ya maji na Roho—ambayo ni ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani—na imani hii ndiyo sheria ya uzima ambayo inaweza kuwafunika wanadamu kwa haki ya Mungu. 
Ni nani basi anayeweza kuwa kinyume na sheria hii ya uzima? Yeyote anayeamini katika injili ya maji na Roho iliyotolewa na Mungu ataokombolewa toka katika dhambi zote za ulimwengu, na kwa imani hii, mtu huyo ataipokea haki ya Mungu. 
Mungu amekupatiaje sheria ya Roho wa uizma? Mungu amekupatia sheria ya Roho wa uzima kwa kumtuma Mwanawe Yesu kuja hapa duniani, na kuzaliwa kwa kupitia bikira, kwa kuziweka dhambi zote za ulimwengu juu yake kwa kupitia ubatizo wake alioupokea toka kwa Yohana, kwa kumfanya Yesu afe Msalabani kama mshahara wa dhambi, na kwa kumfufua toka kwa wafu—na hivyo kuziondosha dhambi zote za ulimwengu na kumfanya Yesu kuwa Mwokozi wa wenye dhambi. Mungu amewapatia msamaha na maisha mapya kwa wale wote wanaoamini katika ukweli huu, na hii ndiyo sheria ya Roho wa uzima ambayo Mungu ametupatia. 
Je, sheria ya dhambi na mauti ni kitu gani? Hii ni amri ambayo Mungu ameitoa kwa wanadamu. Sheria iliyowekwa na Mungu inatoa maelekezo yake katika msingi wa “fanya na usifanye,” na kosa lolote la kuzikiuka sheria hizi kutakuwa ni dhambi ambayo mshahara wake wa mauti utapaswa kulipwa adhabu huko kuzimu. 
Hivyo kila mtu alikuwa amewekwa chini ya sheria ya kifo, lakini Yesu Kristo ametukomboa sisi toka katika sheria hii ya kifo kwa ubatizo na damu yake iliyomwagika Msalabani. Hakuna yeyote anayeweza kuwaokoa wenye dhambi toka katika dhambi zao, na hakuna njia nyingine ambayo kwa hiyo Yesu anaweza kutuokoa toka katika dhambi zetu zote zaidi ya injili ya maji na Roho iliyotolewa na Yesu. Hivyo ni lazima ufahamu na kuamini jinsi ambavyo Yesu alikuja hapa duniani kukuokoa na jinsi haki ya Mungu ilivyo. 
Hata hivyo, siku hizi kuna watu wengi ambao wanaitangaza imani yao katika Yesu na wanafahamu sana mambo yahusianayo na Sheria—ambayo ni sheria ya dhambi na mauti—lakini bado watu hao hawafahamu chochote kuhusiana na injili ya maji na Roho ambayo imewaokoa wao toka katika dhambi zote. Watu wengi wanaendelea kumwamini Yesu hali wakiwa na hali hii ya kutofahamu. Kutokana na hali hii tunaweza kuona jinsi ambavyo injili ya maji na Roho ilivyofichwa kwa muda mrefu. Injili hii ya maji na Roho ni tofauti kabisa na injili ambayo ina imani inayojengwa juu ya Msalaba tu. Watu wengi wanawekea umuhimu sana juu ya damu ya Yesu tu Msalabani, lakini maandiko yanatueleza kuwa Yesu aliimwaga damu yake Msalabani kwa kuwa alikuwa amezibeba dhyambi zote za ulimwengu katika mwili wake wakati alipobatizwa na Yohana na si wakati aliposulubiwa. 
Ni lazima utambue kuwa tofauti hizi katika ufahamu pia zinasababisha tofauti kati ya kwenda mbinguni na kwenda kuzimu. Tofauti hizi zinaweza kuonekana kama ni tofauti ndogo sana, lakini uelewa wa aina hizi mbili unatofautiana sana kati ya mmoja na mwingine na kimsingi zinajumuisha matokeo tofauti kabisa. Hii ndiyo sababu ikiwa unapenda kumwamini Yesu kuwa ni Mwokozi, basi ni lazima uiweke imani yako katika injili ya maji na Roho. Ni kwa kufanya hivyo tu ndipo unapoweza kukombolewa toka katika dhambi zako zote. Lakini bado na mara nyingi watu wengi wanaoendelea kuitangaza imani yao katika Yesu wanaendelea kubaki katika ujinga wa kutoifahamu haki ya Mungu. 
Watu wa jinsi hiyo wanajaribu kusimama mbele za Mungu kama walivyo hali wakijaribu kutenda dhambi chache kadri itakavyowezekana na kwa kujaribu kutakaswa kwa jitihada zao wenyewe. Lakini haki ya Mungu si kitu ambacho kinaweza kupatikana kwa fikra za mwanadamu mwenyewe, jitihada, au matendo. Ni kwa kuamini katika ukweli wa upatanisho uliofichika katika ukweli wa maji na Roho ndipo mtu anapoweza kuipata haki ya Mungu. Imani ya wale wanaojitahidi kujitakasa wenyewe kwa kuifuata Sheria ni imani ya kijinga. Hakuna hata mmoja anayeweza kuyafuata na kuyashika maagizo yote ya Sheria. 
 

Kwa Kuihukumu Dhambi Katika Mwili wa Yesu
 
Aya ya 3 inasema, “Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili.” Katika kifungu hiki tunaweza kuona jinsi Paulo anavyoishuhudia kwa kina sheria ya maji na Roho. Hapa, Paulo anatueleza kuwa Mungu Baba aliziweka dhambi zote za ulimwengu juu ya Yesu: “Kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili.”
Kule kusema Mungu aliihukumu dhambi katika mwili kuna maanisha nini? Kuna maanisha kuwa Mungu Baba alimtuma Mwanawe pekee kuja hapa duniani, akamfanya abatizwe na Yohana ili kuziweka dhambi zote za ulimwengu juu ya mwili wake, na hivyo kuzifisha dhambi zote za waamini milele. Hii ndiyo sababu maandiko yanasema kuwa “yale yasiyowezekana kwa sheria… Mungu alifanya.” Mungu alizitoweshea mbali dhambi zote za ulimwengu kwa kuziweka juu ya Mwanawe. Kitendo cha Mungu kumfanya Yesu afe Msalabani na kisha kufufuka toka kwa wafu kimesababisha dhambi zote kutoweshwa. 
Hii ndiyo injili ya ukweli inayokuokoa, na injili hii ni injili ya maji na Roho. Kile ambacho Bwana wetu alikisema kwa Nikodemo katika Yohana 3:5, “Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuungia ufalme wa Mungu,” kwa uhakika ndiyo injili hii. Injili hii ambayo inaidhihirisha haki ya Mungu ilifunuliwa wakati Yesu alipobatizwa na Yohana, alipoimwaga damu yake Msalabani, na alipofufuka toka kwa wafu. 
Mathayo 3:15 inasema, “Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali.” Kifungu hiki kinatoa ushahidi kwa haki ya Mungu na udhihirisho wake katika Yesu. Wakati Yesu alipokuja katika Mto wa Yordani toka Galilaya na kujaribu kubatizwa na Yohana Mbatizaji, Yohana alikataa kwanza kufanya hivyo hali akidai, “Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, na wewe waja kwangu?” Lakini Yesu alimwamuru Yohana kwa sauti kwa kifungu hiki, “Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.” 
Sasa, kule kusema “kuitimiza haki yote” kuna maanisha nini? Kuna maanisha kuwa Yesu alizichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake kwa kupitia ubatizo alioupokea toka kwa Yohana. Wakati Yesu alipokuwa akitoka toka katika maji baada ya kuwa amebatizwa, mbingu zilimfunukia na Roho wa Mungu alishuka kama hua. Kisha “sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye” Mungu alipendezwa na ubatizo wa Yesu ambao kwa huo alizichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake. Hapa tunaziona nafsi zote tatu za Utatu wa Mungu zikiwa pamoja, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ambao waliamua kumwokoa mwanadamu toka katika dhambi zake na kuitimiza ahadi hii. 
Maandiko yanatueleza kuwa mbingu zilimfunukia Yesu wakati alipobatizwa, na kwamba sauti kutoka mbinguni ikatangaza, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.” Hii ni kusema kuwa, Mungu Baba alipendezwa na ukweli kuwa Mwanawe alizichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake mara moja kwa kubatizwa na Yohana. Hivyo, kwa kuwa Yesu alibatizwa, na kwa kuwa kwa ubatizo wake dhambi zote za ulimwengu ziliwekwa katika mwili wake, basi Yesu aliitimiza haki yote kwa kusulubiwa Msalabani na kufufuka tena toka kwa wafu. 
Kwa maneno mengine, Yesu alibatizwa na Yohana ili kuitimiza haki yote ya Mungu. Kisha alikufa Msalabani. Ubatizo huu na kifo hiki zilikuwa vimelengwa ili kuitimiza haki yote ya Mungu. Yesu alizichukua katika mwili wake dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo wake na hii ndiyo sababu aliweza kuimwaga damu yake Msalabani. Yesu aliyatimiza mapenzi yote ya Mungu kwa kufufuka kwake toka kwa wafu. 
“Haki yote ya Mungu” ina maanisha ni tendo la kumkomboa mwanadamu toka katika dhambi zake zote. Ili kulitimiza tendo hili la haki, Yesu alizichukua dhambi zote za watu kwa ubatizo wake na kisha akaimwaga damu yake Msalabani. Haki yote ya Mungu ilitimizwa kwa njia sahihi na ya haki. Ubatizo, damu, na ufufuo wa Yesu ndivyo vilivyoitimiza haki ya Mungu, na haki hii ya Mungu imetufanya sisi kuwa tusio na dhambi hali ikiiweka juu yetu ile haki ya Mungu. Mungu wa Utatu alipanga jambo hili, Yesu alilitimiza jambo hili, na Roho Mtakatifu anatoa ushuhuda juu ya haki hiyo hata sasa. Ni lazima uliamini Neno ambalo Mungu alilituma kwa kupitia “Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili.”
Hebu jiulize mwenyewe. Hebu jiulize wewe mwenyewe kama unafikiri kuwa unaweza kikwelikweli kuzifuata amri zote za Sheria kikamilifu katika kipindi chote cha maisha yako kilichosalia. Kwa kweli unaweza kujitahidi sana kuzifuata amri hizo, lakini ukweli ni kuwa hutaweza kamwe kuishi kwa kuzifuata na kuzitunza amri zote kikamilifu. Unapoivunja amri ndogo katika Sheria, basi unakuwa umeivunja na kuiharifu Sheria nzima (Yakobo 2:10), na hii ndiyo sababu kuwa kila mtu anajikuta akiishia kuwa ni mwenye dhambi mkamilifu anapokuwa akiishi chini ya Sheria. 
Unaweza kuwa ni mkweli na mwaminifu hali ukitamani kuifuata na kuitunza Sheria hali ukifanya kila uwezalo, lakini haki ya Mungu ambayo Mungu anaihitaji toka kwetu haipatikani kamwe kwa kuifuata Sheria. Ni lazima utambue kuwa sababu pekee ambayo ilimfanya Mungu kutupatia sisi Sheria yake ilikuwa ni kwa nia ya kutufanya sisi tuweze kuzitambua dhambi zetu. Hii ni kwa sababu miili yetu ni ya udhaifu na kwamba hakuna hata mmoja anayeweza kuifuata Sheria ya Mungu katika ukamilifu wake. 
Hii ndiyo sababu ili kutukomboa sisi toka katika dhambi zetu, Mungu alimtuma Mwanawe kuja hapa duniani na akamfanya abatizwe na Yohana ili aweze kuzichukua dhambi za kila mtu. Kwa maneno mengine, dhambi zote za ulimwengu ziliwekwa juu ya mwili wa Yesu mara baada ya kuubatiza mwili wa Yesu. Hii ndiyo sababu Maandiko yanatueleza kuwa Mungu “aliihukumu dhambi katika mwili” wa Yesu, hivi ndivyo Mungu alivyotufanya sisi kuwa tusio na dhambi. 
Ni lazima tufahamu na kuamini jinsi ambavyo Mungu amezifanya dhambi zetu kutoweshwa. Mungu aliziweka dhambi zetu zote juu ya Yesu kwa kumfanya abatizwe na Yohana ambaye ni mwakilishi wa wanadamu. Kisha Mungu alimfanya Yesu kuzibeba dhambi zote za ulimwengu Msalabani na kisha kulipa mshahara wa dhambi badala yetu kwa kuimwaga damu na kufa juu yake. Yesu aliifungua njia ya ukombozi kwa wote wanaoamini kwa ufufuo wake toka kwa wafu. Hivyo, Mungu alipanga na akautimiza wokovu wetu toka kwa wafu. 
Hivyo, ni lazima tuamini katika mioyo yetu kuwa ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani vilifanyika kwa ajili ya upatanisho wetu. Wale wanaoamini katika haki ya Mungu ni lazima waamini kwa hakika katika ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani. 
Wewe pia ni lazima uamini vivyo hivyo ili uweze kupokea ondoleo la dhambi zako na ili uweze kuhesabiwa haki kikamilifu na kuwa usiye na dhambi. Ni lazima ufahamu kiusahihi jinsi ambavyo Mungu amezifanya dhambi zako kutoweka na kisha ufuate mapenzi yake na kuyaamini mbele za Mungu badala ya kuziamini juhudi zako binafsi.