Search

Khotbah-Khotbah

Somo la 3: Injili ya Maji na Roho

[3-7] Ukuhani Uliobadilika (Waebrania 7:1-28)

(Waebrania 7:1-28)
“Kwa maana Melkizedeki huyo mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapinga hao wafalme, akambariki ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena mfalme wa Selemu, maana yake mfalme wa amani, hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake bali amefananishwa na mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele. Basi angalieni jinsi mtu huyu alivyo kuwa mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara. Na katika wana wa Lawi nao wale waupatao ukuhani wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao yaani ndugu zao, kwa agizo la kisheria ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahimu. Bali yeye ambaye uzazi wake haukuhesabiwa kuwa umetoka kwa hao alitwaa sehemu ya kumi kwa Ibrahimu akambariki yeye aliye na ile ahadi. Wala haikanushi kabisa kwamba mdogo hubarikiwa na mkubwa. Na hapa wanadamu wapatikanao na kufa hutwaa sehemu ya kumi bali huko yeye ashuhudiwaye kwamba yu hai. Tena yaweza kusemwa ya kuwa kwa njia ya Ibrahimu hata Lawi apokeaye sehemu ya kumi alitoa sehemu ya kumi kwa maana alikuwa katika viuno vya baba yake hapo Melkizedeki alipokutana naye.
Basi kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi; (maana watu wale waliipata sheria kwa huo); kulikuwa na haja gani tena ya kuhani mwingine ainuke kwa mfano wa Melkzedeki na asihesabiwe kwa mfano wa Haruni? Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo ibadilike. Maana yeye aliyenenwa hayo alikuwa ni shiriki wa kabila nyingine, ambayo hapana mtu wa kabila hiyo aliyeihudumia madhabahu. Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lolote juu yake katika mambo ya ukuhani. Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine mithili ya Melkzedeki asiyekuwa kuhani kwa sheria yao amini iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na ukomo maana ameshuhudiwa kwamba wewe u kuhani milele kwa mfano wa Melkzedeki. Maana kuna kubatiliwa kwa ile amri iliyotangulia kwa sababu ya udhaifu wake na kutokufaa kwake; (Kwa maana ile sheria haikukamilisha neno) na pamoja na hayo kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi ambayo kwa hayo twamkaribia Mungu. Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo (maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye pamoja na kiapo kwa yeye aliyemwambia Bwana ameapa wala hataghairi, wewe u kuhani milele), basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na mauti wasikae bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usiondoka. Naye kwa sababu hii aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai siku zote ili awaombee.
Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji aliye juu kuliko mbingu ambaye hana haja kila siku, mfano wa wale makuhani wakuu wengine, kwanza kwa kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa ajili ya dhambi zao hao watu; maana yeye alifanya hivi mara moja, alipojitoa nafsi yake. Maana torati yawaweka wanadamu walio na unyonge kuwa makuhani wakuu; bali hilo neno la kiapo kilichokuja baada ya torati limemweka mwana aliyekamilika hata milele.”
 

YESU ANAHUDUMU UKUHANI WA MBINGUNI

Ni nani aliye mkuu
kuhani mkuu Melkzedeki au kuhani 
wa duniani atokanaye kwa 
mpangilio wa Haruni?
Kuhani Mkuu Melkzedeki.

Katika Agano la Kale, palikuwepo na kuhani mkuu aliyeitwa Melkzedeki. Wakati wa Ibrahimu, Kedorlaoma na wafalme walishirikiana naye na kutaka vitu vyote vya Sodoma na Gomora. Ibrahimu akawapa silaha watumishi wake waliofunzwa, wale waliozaliwa katika nyumba yake na kuwaongoza katika vita dhidi ya Kedorlaoma na washirika wake.
Hapo ndipo alipowashinda Kedorlaoma akiwa na Mfalme Elamu na wafalme walioshiriki naye na hatimaye kumrudisha nduguye Lutu na mali zake. Baada ya Ibrahimu kurudi katika vita na adui zake, Melkzedeki, Mfalme wa Salem na kuhani wa Mwenyezi Mungu, alileta mkate na divai na kumbariki Ibrahimu. Naye Ibrahimu akampa fungu la kumi la kila kitu (Mwanzo sura ya 14).
Katika Biblia ukuu wa kuhani mkuu Melkzedeki na makuhani wakuu kwa mtiririko wake umeelezewa kwa undani. Kuhani mkuu Melkzedeki alikuwa ni “mfalme wa amani”, “Mfalme wa haki” asiye na baba wala mama wala kizazi. Asiyekuwa na mwanzo wa siku wala mwisho wa uhai, lakini alifanywa kama Mwana wa Mungu, anabaki kuwa kuhani wa milele.
Biblia inatueleza kutilia maanani kwa unagalifu ukuu wa Yesu Kristo ambaye alikuwa ni kuhani mkuu kwa mtiririko wa Melkzedeki, kwa kuhusisha ukuhani wa Yesu katika Agano Jipya na ule wa kuhani mkuu Haruni katika Agano la Kale.
Kizazi cha Walawi ndicho kilichokuwa makuhani na kukusanya fungu la kumi toka kwa watu maana yeke hata kutoka kwa ndugu zao ingawa wote walitoka katika uzao wa Ibrahimu. Lakini Ibrahimu alipotoa fungu la kumi kwa kuhani mkuu Melkzedeki, Walawi walikuwa bado wakitoka viunoni mwa baba zao.
Je, makuhani katika Agano la Kale walikuwa ni wakuu kuliko Yesu? Imeelezwa katika Biblia. Je, Yesu ni mkuu kuliko makuhani wa duniani? Ni nani anayehitajika kumbariki mwingine? Mwandishi wa Waebrania alizungumzia juu ya hili toka awali. “Wala haikanushiki kabisa kwamba mdogo hubarikiwa na mkubwa” Ibrahimu alibarikiwa kupitia kuhani mkuu Melkzedeki.
Ni vipi basi inatupasa tuishi kwa imani? Je, imetupasa kutegemea amri za Mungu kupitia mpangilio wa dhabihu ya Hema takatifu katika Agano la Kale au yatupasa kumtegemea Yesu Kristo aliyekuja kwetu akiwa ni kuhani mkuu wa mbinguni kupitia sadaka yake katika maji na Roho?
Itategemea ni tafsiri gani tunachagua, ndivyo tutakavyobarikiwa au kuangamia. Je, tunaishi kulingana na neno la Mungu na kutoa dhabihu kila siku au tunachagua kuamini wokovu aliotupa Yesu kama sadaka yake kwa mara moja na kwa wakati wote kwa maji na damu? Imetupasa kuchagua moja kati ya haya mawili.
Katika nyakati za Agano la Kale, watu wa Israelii waliwategemea kizazi cha Haruni na Walawi. Nyakati hizi za Agano Jipya, ikiwa tutaulizwa yupi ni mkuu, Yesu au Makuhani walio katika mtiririko wa Haruni? Ndipo basi pasipo kusita, tutaweza kujibu kuwa Yesu ndiye mkuu. Lakini wakati watu wanafahamu ukweli huu bayana, ni wachache wenye kuufuata kwa imani.
Biblia inatupa jibu la uhakika kwa swali hili. Inatuambia kwamba Yesu, aliyekuwa wa kabila la tofauti ambako hakuna aliyewahi kutumikia madhabahu, alichukua nafasi ya ukuhani wa mbinguni. “Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo ibadilike.”
Mungu aliwapa watu wa Israeli amri na vipengele vya sheria 613 kupitia Musa. Musa aliwaeleza watu wazifuate sheria na amri zote nao walikubali kufanya hivyo.

Kwa nini Mungu alibatilisha 
agano la kwanza na kuweka 
agano jingine?
Kwa sababu watu walikuwa wadhaifu 
hata kushindwa kuishi katika 
agano la kwanza.

Katika Biblia watu wa Israeli walikula kiapo katika kuishi kwa kuzifuata amri za Mungu wakati wa Mwanzo, Kutoka, Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Torati. Mungu alitamka kila amri kwao na waliitika “Ndiyo” kwa kila amri bila kusita.
Ijapokuwa tunaweza kuona kwamba baada ya Kumbukumbu la Torati, tokea Yoshua hadi mwisho hawakuweza kamwe kuishi kulingana na sheria za Mungu. Kuanzia Waamuzi hadi wafalme wa kwanza na wa pili walianza kuwadharau viongozi wao, na kwa kiasi walicho haribika waliweza hata kubadilisha mpangilio wa utoaji dhabihu katika hema takatifu.
Mwishowe katika Malaki, walileta wanyama wasiofaa kutolewa tofauti na vile Mungu alivyoelekeza kutoa mnyama asiye na doa. Waliwaambia makuhani kwa kusema “Tafadhali, usijali hili. Naomba ukubali kupokea” Badala ya kutoa dhabihu kulingana na sheria ya Mungu, walibadilisha pasipo kujali.
Watu wa Israeli kamwe hawakuifuata sheria ya Mungu kabisa hata kidogo wakati huo wa Agano la Kale. Walisahau na hivyo kufikia kudharau wokovu uliomo katika mpangilio huo. Hivyo basi Mungu alisema “Nitafanya Agano jipya na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda.”
Hebu tuangalie katika Yeremia 31:31-34, “Angalia, siku zinakuja asema Bwana nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri, ambalo agano langu hilo walilivunja ingawa nalikuwa mume kwao asema Bwana. Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana. Nitatia sheria yangu ndani yao na katika mioyo yao nitaiandika, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake na kila mtu ndugu yake wakisema mjue Bwana; kwa maana watanijua wote tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao asema Bwana maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.”
Mungu alisema kuwa angeliweka agano jipya. Alikuwa amekwisha weka tayari agano la mwanzo na watu wa Israeli lakini walishindwa kufuata neno la Mungu. Hivyo aliamua kufanya agano jipya la wokovu kwa watu wake. 
Walikuwa wamekula kiapo mbele ya Mungu kuwa, “Tutakuabudu wewe tu na kufuata maneno na amri zako.” Mungu alikuwa amewaambia “Msiwe na miungu wengine zaidi yangu” na watu wa Israeli walijibu “hakika, hatutoabudu kamwe miungu wengine. Wewe ni Mungu wa pekee kwetu. Hatuna mwingine zaidi” Lakini walishindwa kusimamia kiapo chao.
Kiini cha sheria kilijumuisha Amri kumi; “Usiwe na miungu wengine zaidi yangu. Usijifanyie mfano wa kuchonga au kufanana na chochote na kukiabudu au kukitumikia. Ikumbuke siku ya Sabato na kuitakasa. Usilitaje jina la Bwana Mungu wako bure. Waheshimu baba na mama yako. Usiue. Usizini. Usiibe. Usishuhudie jirani yako kwa uongo. Usitamani mali ya jirani yako” (Kutoka sura ya 20).
Pia imegawanywa katika vipengere 613 za kina ambazo zilitunzwa katika maisha yao yote. Cha kufanya binti, na nini usifanye watoto wa kiume, nini cha kufanya kwa akina mama wa kambo .... Sheria ya Mungu iliwaamuru wafanye vitu vyote vizuri na wasifanye mambo mabaya. hizi ni Amri Kumi na vipengere 613 za kina.
Hata hivyo, kati ya wanadamu wote, hapajawahi kuwepo yeyote aliyeweza kufuata vipengele hivi vyote vya sheria ya Mungu. Hivyo Mungu aliweka mpango mwingine kwa njia ya kuokoa tokana na dhambi zote.
Lini ukuhani ulibadilika? Baada ya kuja kwa Yesu hapa duniani, ndipo ukuhani ulibadilika. Yesu alishika nafasi ya ukuhani kuanzia makuhani wote katika mlolongo wa Haruni. Aliweka kando dhabihu ya hema takatifu ambayo ilirithiwa na makuhani wa mlolongo wa Walawi. Yeye mwenyewe anahudumia ukuhani wa mbinguni.
Alikuja ulimwenguni, si kama kizazi cha Haruni bali kama uzao wa Yuda, nyumba ya ufalme. Alijitoa mwenyewe kama dhabihu kupitia ubatizo wake na damu yake msalabani na hivyo kuokoa wanadamu wote tokana na dhambi zao.
Kwa kujitoa yeye binafsi ametuwezesha kutatua tatizo la dhambi. Alitakasa dhambi zote za wandamu kupitia dhabihu ya ubatizo wake na damu yake. Alitoa sadaka ya milele kwa dhambi zote.
 

PAMOJA NA KUBADILIKA KWA UKUHANI PALIBADILIKA PIA NA SHERIA

Nini badiliko la 
sheria ya wokovu?
Sadaka ya milele kupitia 
Yesu Kristo.

Wapendwa Rafiki, ukuhani wa Agano la Kale ulibadilika katika Agano Jipya. Wakati wa agano la Kale, kuhani mkuu kati ya uzao wa Haruni, nyumba ya Walawi walitoa dhabihu ili kupatanisha Israeli kwa dhambi zao za mwaka mzima. Kuhani mkuu huyo aliingia sehemu ya Patakatifu. Alikwenda mbele ya kiti cha rehema akiwa na damu ya mnyama wa sadaka. Ni kuhani mkuu tu ndiye aliyeruhusiwa kwenda nyuma ya pazia ambamo ndimo Patakatifu pa patakatifu.
Lakini baada ya kuja kwake Yesu, ukuhani wa Haruni umewekwa juu ya Yesu. Yesu amerithi ukuhani wa milele. Anahudumia ukuhani wa milele kwa kujitoa mwenyewe, ili wanadamu wote waweze kuokolewa kwa dhambi zao zote.
Katika Agano la Kale kuhani mkuu pia ilimpasa ajipatanishe kwa dhambi zake kwa kuweka mikono juu ya kichwa cha ndama dume kabla ya kuhudumia kwa niaba ya watu wote. Alitwika dhambi zake kwa kuwekea mikono dhabihu, alisema “Mungu ninadhambi” Ndipo alimchinja koo mnyama huyo na kunyunyiza damu yake juu na mbele ya kiti cha rehema mara saba.
Ikiwa kuhani mkuu Haruni yeye binafsi hakuwa kamilifu basi unaweza kuona jinsi ile watu wasivyo wakamilifu. Watoto wa Walawi, kuhani mkuu Haruni mwenyewe wote walikuwa ni wenye dhambi, hivyo kwamba iliwapasa kuitoa dhabihu ya ng’ombe kwa upatanisho wa dhambi zao na zile za familia yao.
Bwana alisema katika Yeremia sura ya 31 “Nitalivunja agano. Nimefanya agano nawe, lakini hukulitunza. Hivyo nitaondoa agano amablo halikuweza kukutakasa na nitakupa agano jipya la wokovu. Sinto kuokoa tena kwa kupitia sheria zangu bali nitatoa sadaka ya wokovu kupitia injili ya maji na Roho.”
Mungu ametupatia agano jipya. Muda ulipowadia Yesu alikuja duniani kwa mfano wa mwanadamu, alijitoa nafsi yake ili kuchukua dhambi zote za ulimwengu na kumwaga damu yake msalabani kutuokoa sisi tunaomwamini. Alizichukua dhambi zote za wanadamu kupitia ubatizo wake.
Sheria ya Mungu ilibadilishwa. Watu wa Israeli wangeweza kuokolewa ikiwa wangelifuata sheria ya Mungu lakini walishindwa kuifuata. “Kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria” (Warumi 3:20).
Mungu alitaka Waisraeli kuelewa kwamba wao ni wenye dhambi hivyo sheria isingeweza kuwaokoa. Aliwaokoa kupitia sheria ya wokovu kupitia maji na Roho na siyo kupitia matendo. Kwa upendo wake wa milele, Mungu ametupa agano jipya ambalo ndilo lituokoalo kwa dhambi zetu zote ulimwenguni kupitia ubatizo na damu ya Yesu.
Ikiwa unamwamini Yesu pasipo kujua maana ya ubatizo na damu yake, imani yako yote ni bure. Unapokuwa namna hii hakika utajikuta katika taabu zaidi kuliko kumwamini Yesu kabisa.
Mungu alisema kwamba ilimpasa kuweka agano jipya ili kuokoa wanadamu kwa dhambi zao. Na kwa matokeo yake tumeokolewa si kwa matendo ya sheria bali kwa sheria ya haki ya wokovu kupitia maji na damu.
Hii ni ahadi yake ya milele na aliitimiza ahadi hii kwa ajili yetu wote tunaomwamini Yesu. Na ametufahamisha juu ya ukuu wa Yesu. Ametuelezea jinsi alivyo mkuu kwa kumlinganisha na makuhani wa uzao wa Haruni wakati wa Agano la Kale.
Tunakuwa maalumu kwa kuamini wokovu utokanao kwa maji na kwa damu ya Yesu. Tafadhali hebu chukulia jambo hili kwa uangalifu. Haijalishi ni kwa kiasi gani mchungaji wako alivyo msomi na mnenaji mzuri, lakini atawezaje kuwa mkuu kuliko Yesu? Hakuna kabisa! Tunaweza kuokolewa tu kwa kupitia injili ya maji na damu, kamwe si kwa kutii sheria za Mungu tu. Kwa sababu ukuhani ulibadilishwa, sheria ya wokovu nayo pia ilibadilishwa.
 

UKUU WA UPENDO WA MUNGU

Lipi ni kuu kushinda 
mwenzake upendo wa Mungu 
au sheria ya Mungu?
Upendo wa Mungu.

Tunaweza kuokolewa ikiwa tu tunamwamini Yesu kujua namna ile Yesu alivyotuokoa ukuu wa upendo wa Mungu ulivyokwetu. Nini basi tofauti kati ya imani katika amri na imani katika ukuu wa upendo wa Mungu?
Watu wa matendo ya sheria hushikilia kwa mkazo umuhimu wa mafundisho ya dhehebu lao na uzoefu binafsi badala ya Neno la Mungu. Hata hivyo imani ya kiroho iliyo kamili na kweli katika Yesu huja kwa kuamini ukuu wa wokovu uliotimizwa kwa maji na Roho.
Hata leo, watu wengi husema kuwa dhambi za asili ndizo husamehewa, hivyo inawapasa kutubu kila mara kwa dhambi za kila siku. Wengi huamini hivyo na hivyo kujaribu kuishi kwa kufuata amri za Agano la Kale. Watu hawa bado hawajafahamu ukuu wa wokovu wa Yesu aliyekuja kwa maji na kwa Roho.
Katika Agano la Kale, Waisraeli iliwapasa kuzifuata sheria za Mungu ili waweze kuokolewa kwa dhambi zao lakini hawakuweza kuokolewa. Kwa sababu Bwana anajua udhaifu wetu na ukweli kuwa hatuna ukamilifu, aliondoa amri zake. Kamwe hatutoweza kuokolewa kupitia matendo yetu pekee. Yesu alisema kuwa atatuokoa kupitiua injili ya maji na Rohoi. Alisena “nitawakomboa ninyi nyote kwa dhambi zenu mimi mwenyewe” Mungu alitabiri haya katika Mwanzo.
“Na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino” (Mwanzo 3:15). Baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi na kuanguka, walifanyiza mavazi ya majani ya aradali kwa nia ya kuficha uovu mbele ya Mungu. Lakini Mungu aliwaita na kuwatengenezea vazi la ngozi likiwa na maana ya wokovu. Mwanzo huzungumzia juu ya aina mbili za vazi la wokovu. Moja lilifanyizwa kwa majani ya aradali na lingine lilifanyizwa kwa ngozi ya mnyama. Lipi unadhani ni imara zaidi? Bila shaka vazi la ngozi ya mnyama ni imara zaidi kwa sababu uhai wa mnyama ulitolewa ili kumlinda mtu.
Vazi la majani ya aradali hunyauka haraka. Kama unavyojua jani la aradali hufanana na mkono wenye vidole vitano. Hivyo kuvaa vazi la majani haya maana yake ni kuficha dhambi kwa kuweka matendo mema mbele yake. Ikiwa unataka kuvaa vazi hili la jani utakapoketi chini majani hayo yatapukutika vipande. Hapo zamani nilikuwa na mchezo wa kutengeneza vazi la kivita kwa kutumia majani mapana ili kufanana na mwanajeshi. Lakini kila nilipojaribu kulivaa kwa uangalifu vazi hilo liliharibika kwa majani kupukutika mpaka ikifika jioni. Kwa njia hii hata wanadamu nao miili yao isiyo imara hufanya tendo la utakaso kuwa jambo lisilowezekana.
Lakini wokovu wa maji na damu, ubatizo wa Yesu na msalaba wake huokoa na zaidi humfanya mwenye dhambi kushuhudia ukuu wa upendo wa Mungu. Huu ndiyo ukuu wa upendo wa Mungu ulio katika sheria yake.
 

WALE AMBAO BADO WANA IMANI KATIKA SHERIA YA MUNGU

Kwa nini watu wale wa 
matendo ya sheria hufanyiza mavazi 
kwa matendo ya kila siku?
Kwa sababu hawajui kwamba matendo 
yao ya sheria kamwe hayawezi 
kuwafanya kuwa wenye haki.

Wale wote wenyekujitengenezea mavazi kwa kutumia majani wanaishi maisha ya matendo ya sheria. Waumini hawa potofu inawabidi kubadilisha mavazi hayo kwa kila siku. Inawabidi kutengeneza mavazi mapya kila Jumapili kila wanapokwenda kanisani. “Mungu wangu, nimetenda dhambi nyingi juma lililopita. Lakini Bwana, naamini kuwa umeniokoa msalabani Bwana, tafadhali nitakase dhambi zangu kwa damu yako msalabani!” Ndivyo wanavyoshona viraka vya hapa na pale kwa vazi lao. “Oh, Bwana asifiwe. Haleluya!”
Lakini punde si punde inawapasa tena kutengeneza mavazi mengine wanapofika nyumbani. Kwa nini? Kwa sababu lile la kwanza limekwisha chakaa. “Bwana wangu, tayari nimekwisha kukosa tena majuma matatu yaliyopita. Tafdhali nisamehe” Wanatengeneza na kuvaa mavazi ya toba kila mara.
Mwanzo mavazi hayo yanaweza kukaa kwa siku kadhaa, lakini punde, huitaji mengine kila siku. Kwa jinsi ile wasivyoweza kamwe kuishi kwa kufuata sheria ya Mungu huishia kuona aibu wenyewe “Oh, hii ni aibu kwangu Bwana. Lo, Bwana nimeanguka dhambini tena!” Na inawabidi kutengeneza mavazi mengine ya toba, “Ah, Bwana ni vigumu kutengeneza mavazi haya kila siku” Hufanya bidii sana kutengeneza mengine.
Watu kama hawa wanapomwita Mungu, ni katika kuungama tu. Hung’ata midomo yao huku wakimwita Mungu “Muuu-ngu!” na kuendelea kutengeneza mavazi mapya kila siku. Ndipo basi, nini kitakachotokea pale wanapochoka kwa kufanya hivyo?
Mara moja au zaidi kwa mwka, hupanda milimani na kufunga kula. Hujaribu kutengeneza mavazi mengine yaliyoimara yasiyochakaa mapema. “Bwana tafadhali nitakase kwa dhambi zangu. Tafadhali nifanye upya. Nakuamini wewe Bwana.” Hudhani kuwa ni vizuri zaidi kuomba nyakati za usiku wa manane. Hivyo, hupumzika nyakati za mchana na kila giza linapoingia hupanda hata kwenye miti kwa nguvu zao zote au kuingia kwenye mapango yenye giza na kuanza kulia mbele ya Mungu. “Bwana, ninaimani nawe” huimba “Naungama na kuujaza moyo wangu kwa fikira za unyenyekevu” Husali kwa sauti kubwa na kwa kelele “Bwana ninaimani nawe” Kwa njia hii hutengeneza vazi jingine maalumu ambalo hutumaini kuwa litadumu muda mrefu lakini la hasha!
Ni kwa jinsi gani unavyojisikia mwenye nguvu za upako kila baada kutoka katika sala za mlimani! Kama upepo mwanana, au mvua ya matone madogo juu ya miti na maua, mioyo ya watu wa aina hii hudhani kuwa wamejawa na amani na neema ya mwenyezi. Hujisikia wametakasika roho zao kwa sala za mlimani kila wanaposhuka na kukutana na ulimwengu huku wakiwa na mavazi yao mapya maalumu.
Lakini punde tu baada ya kurudi nyumbani na kanisani na kuanza kuishi tena, mavazi hayo hupata madoa ya uchafu na hivyo kuanza taratibu kuchakaa. Rafiki zao huwauliza “Ulikuwa wapi ndugu?” “Ah unajua nilitoka kidogo” “Unaonekana umepungua kulikoni?”
“Ah wajua tena ni mambo ya kawaida.” 
Kamwe hawatoboi siri ya kuwa walifunga, bali huenda kanisani na kuendelea kuomba. “kamwe sitotamani wanawake tena. Sinto danganya. Sinto tamani nyumba ya jirani yangu. Nitawapenda watu wote.”
Lakini punde wanapoona maumbile ya wanawake warembo na miguu mizuri, utakatifu wa mioyo yao hubadilika mara moja na kuwaka tamaa ya mwili. “Hebu tazama ile sketi ilivyo fupi. Siku hizi bwana! Hizi sketi zinaendelea kuwa fupi na fupi! Hebu niangalie ile miguu tena! Oh! Hapana! Sasa Bwana nimesha anguka dhambini tena!”
Watu wa matendo ya sheria huonekana ni watakatifu lakini hufanya kazi ya ziada katika kutengeneza mavazi yao kila siku. Imani ya matendo ya sheria ni vazi la majani ya haradali, ambayo ni imani potofu. Wengi hujaribu kwa bidii kuishi kiutakatifu kwa kufuata sheria ya Mungu. Hupaza sauti katika vilele vya milima ili sauti zao ziweze kuonekana kuwa sasa ni watakatifu.
Watu wa matendo ya sheria huleta mvuto wanopoongoza mikutano ya sala na makanisani. “Baaba Mtakatifu wa Mbinguni! Tumekutenda dhambi juma hili. Tusamehe…..” Hutoka machozi ndipo usharika wote hufatisha. Wao hudhani “kwa kuwa ametumia muda mrefu katika maombi ya kufunga mlimani basi ni mtakatifu na mwaminifu” Lakini kwa kuwa imani yake ni ya matendo ya sheria, hata kabla ya kumaliza kuomba, mtu wa aina hii huanza kujawa na dhambi ya kiburi moyoni.
Wakati watu wanapojifanyizia mavazi maalumu ya majani, yanaweza kuchukua miezi miwili au mitatu hata kuchakaa. Lakini punde au baadaye, mavazi hayo huwa hayafai kabisa na inawalazimu kutengeneza upya na kuendelea na tabia yao ya unafiki. Haya ndiyo maisha ya watu wa matendo ya sheria wenye kujaribu kuishi kwa sheria ili waweze kuokoka. Inawabidi kuendelea kutengeneza mavazi ya majani siku zote za maisha yao.
Imani ya matendo ya sheria ni majani ya haradali. Watu wa matendo ya sheria huwaambia watu wengine “wewe ulitenda dhambi juma lililopita sawa? Sasa ungama!” Watakufokea kwa sauti “fanya sala ya toba!” 
Watu wa matendo ya sheria hujuta na kugeuza sauti zao kuwa za kitakatifu. “Ooh, Bwaaana! Nasikitika. Sikufuata sheria yako. Sikufuata amri zako. Unisamehe Bwaaaana, unisamehe tu leo kwa kweli.” 
Kamwe hawawezi kuishi kwa sheria ingawa hujaribu kufanya hivyo. Ukweli ni kwamba hushindana na sheria ya Mungu na Mungu mwenyewe. Ni wenye viburi mbele ya Mungu.
 

MFANO WA CHUDAL BAE

Kwa nini Mungu aliweka 
kando sheria?
Kwa sababu isingeweza kutumika 
kutuokoa katika dhambi zetu.

Palikuwepo na kijana mmoja kwa jina Chudal Bae. Katika mwaka 1950, kipindi cha vita ya Korea, askari wa Kikomunisti walikuja na kumpa amri kijana huyu kufagia uwanja siku ya Sabato ili waijaribu imani ya dini yake ili waweze kumfanya awe Mkomunisti. Lakini kijana huyu mshika dini alikataa kutii amri hiyo.
Mwishowe, askari wale wakamfunga kwenye mti na kumwelekezea mtutu wa bunduki wakimwambia “kipi unachochagua, kufagia uwanja au kuuawa?”
Walipokuwa wakimlazimisha kufanya uamuzi mwishowe akasema “Afadhali nife kuliko kufanya kazi siku ya Sabato!”
“Sawa umechagua mwenyewe, na inatubidi kutekeleza chaguo lako.”
Ndipo walipompiga risasi ya kichwa. Ndipo baada ya muda kupita viongozi wa kanisa walipomteua kuwa hayati shemasi ili kuikumbuka imani ya dini yake isiyotikisika.
Ingawa alikuwa na nguvu ya dhamira (uwezo wa kupania) bado imani yake ya kidini ilikuwa ni potofu. Kwa nini asingekubali kufagia huo uwanja na kwa wakati huo akapata fursa ya kuhubiri injili kwa askari hao? Kwa nini alihitaji kuwa mbishi na hivyo kukubali kufa? Je, Mungu atamsifu kwa kutofanya kazi siku ya Sabato? Hapana.
Yatupasa kuishi maisha ya kiroho zaidi. Si kwa matendo yetu ya sheria bali kwa imani ndiyo muhimu mbele ya Mungu. Viongozi wa kanisa hupenda kusherehekea kama ilivyo kuwa kwa Chudal Bae kwa sababu hupenda kujionyesha ukuu na uhalisi wa madhehebu yao. Hawa ni sawa na mafarisayo wanafiki walio mshutumu Yesu.
Hakuna tunachoweza kujifunza toka kwa watu wa matendo ya sheria. Hatuna budi kujifunza imani ya kiroho. Yatupasa kuwaza kwa undani kwa nini Yesu ilimpasa kubatizwa na kumwaga damu yake msalabani na pia kutafiti juu ya asili ya majibu kwa maswali haya yote kwanza na ndipo tujaribu kueneza injili kwa watu wote ulimwenguni, ili kwamba waweze kuzaliwa upya mara ya pili. Inatubidi kujitolea maisha yetu kwa kazi za kiroho zaidi.
Ikiwa mhubiri anakwambia “uwe kama kijana huyu Chudal Bae. Itunze Sabato takatifu” hapa anachojaribu kukuvuta ili uje kanisani siku za Jumapili.
Kuna hadithi nyingine tena ambayo inaweza kudhihirisha zaidi juu ya hili.
Palikuwepo na mwanamke mmoja ambaye alipitia majaribu mengi katika kuhudhuria kanisani siku za Jumapili. Wakwe zake hawakuwa wakristo, na walijaribu kumzuia kutokwenda kanisani. Walimwambia afanye kazi siku za Jumapili. Lakini badala yake yeye alikwenda siku za Jumamosi usiku na kufanya kazi shambani pakiwa na mbalamwezi ili familia isiwe na la kumzuia kutokwenda kanisani siku inayofuatia.
Bila shaka ni vyema na muhimu kwenda kanisani, lakini je, inatosha kuhudhuria ibada kila jumapili ili kuonyesha jinsi ulivyo mwaminifu? Waaminifu ni wale waliozaliwa kweli mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Imani ya kweli huanzia pale mtu anapozaliwa mara ya pili.
Je, utaweza kweli kuokolewa kwa dhambi zako kwa kuishi kulingana na sheria za Mungu? Hapana. Lakini hapa siwaambii kuwa muidharau sheria bali sote tunajua kwamba kibinadamu haiwezekani kufuata vipengele vyote vya sheria ya Mungu.
Yakobo 2:10 inasema “maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote ila akajikwaa katika neno moja amekosa juu ya yote.” Hivyo fikiri kabla ya kuamua kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Na ndipo uende kwenye kanisa lenye kuhubiri injili ya kweli. Utaweza kuishi maisha ya uaminifu ikiwa umezaliwa upya. Bwana atakapokuita kwake utaweza kwenda kwa furaha.
Usipoteze muda wako kwenda kwenye makanisa yenye upotofu, usipoteze fedha zako kwa kufanya matoleo potofu. Makuhani wa uongo hawawezi kamwe kukuongoza mbali na motoni. Kwanza sikiliza injili ya maji na Roho na uzaliwe upya mara ya pili.
Tafakari kwa nini Yesu alikuja ulimwenguni. Ikiwa tungeliweza kuingia katika Ufalme wa mbinguni kwa kuishi kulingana na sheria, Mungu asingehitaji kuja hapa duniani. Baada ya kuja kwake ukuhani ulibadilika. Matendo ya sheria yakawa ni jambo lililopitwa na wakati. Kabla ya kuokolewa, tulidhani tungeweza kuokoka kwa kuifuta sheria. Lakini hili silo tena alama ya imani ya kweli.
Yesu alituokoa tokana na dhambi zetu zote ulimwenguni kwa upendo wake, kwa maji ya ubatizo wake, kwa damu yake na kwa Roho. Aliukamilisha wokovu wetu kupitia ubatizo wake Yordani, damu yake msalabani na ufufuo wake.
Mungu aliweka kando taratibu za awali kwa kuwa zilikuwa dhaifu na zisizofaa. “Kwa maana ile sheria haikukamilisha neno; na pamoja na hayo kuliingizwa matumaini yaliyomazuri zaidi ambayo kwa hayo twamkaribia Mungu. Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo” (Waebrania 7:19-20). Yesu aliweka kiapo cha kutuokoa tokana na dhambi zetu zote kwa ubatizo na damu. Kufia imani kwa matendo ya sheria ni kazi bure na hivyo imani iliyo ya kweli ni kuiamini injili ya maji na Roho.
Yatupasa tuwe na imani yenye matunda mema. Kipi unachoona kuwa ni bora kwa roho yako? Je, ingekuwa ni vyema kuhudhuria kanisani kila mara na kuamini sheria au ingekuwa ni vyema kuhudhuria kanisani ambamo injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho huubiriwa ili uweze kuokoka? Kanisa gani na mhubiri yupi atakayekuwa muhimu zaidi kwa roho yako? Fikiri juu ya hili na uchague moja ambalo litakuwa jema kwa manufaa yako.
Mungu anaokoa roho yako kupitia muhubiri aliye na maneno ya injili ya maji na Roho. Kila mmoja imempasa kuchukua jukumu la roho yake. Muumini wa kweli mwenye hekima ni yule anayejitolea roho yake kwa neno la Mungu.
 

YESU ALIKUWA KUHANI KWA KIAPO

Je, kizazi cha ukoo 
wa Walawi walifanywa kuwa 
makuhani kwa kiapo?
Hapana. Ni Yesu pekee alifanywa 
kuhani kwa kiapo.

Waebrania 7:20-21 inasema “na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye pamoja na kiapo kwa yeye aliyemwambia Bwana ameapa na wala hataghairi, wewe u kuhani milele.”
Na Zaburi 110:4 inasema “Bwana ameapa wala hata ghairi, ndiwe kuhani milele kwa mfano wa Melkzedeki.” Bwana aliapa. Aliweka agano nasi na kutuonyesha kupitia maandiko ya Neno lake. “Nitakuwa Kuhani Mkuu wa milele kwa mfano wa Melkzedeki.” Melkzedeki ni mfalme wa haki, mfalme wa amani na kuhani wa milele. Nitakuwa Kuhani Mkuu wa milele kwa mfano wa Melkzedeki kwa ajili ya wokovu wenu.
Yesu alikuja duniani na kuwa kuhani wa uhakika wa agano bora (Waebrania 7:22). Badala ya damu ya ng’ombe na mbuzi alijitoa yeye mwenyewe akiwa dhabihu kwa kubatizwa na kumwaga damu msalabani kusafisha dhambi zetu zote.
Wakati wa Agano la Kale, kuhani mkuu alipofariki, watoto wake wa kiume walirithi ukuhani pale walipotimiza umri wa miaka 30. Naye alipozeeka na mtoto wake kufikisha umri wa miaka 30 alimrithisha ukuhani mtoto wake.
Palikuwapo na vizazi vingi vya makuhani. Hivyo Daudi akapanga mpango ambao uliwezesha hawa wote kuchukua majukumu kwa zamu. Wakati kizazi cha Haruni kilipoteuliwa kuwa makuhani, ndipo walipokuwa na jukumu la kuhudumu katika nafasi hiyo. Luka inasema “Zakaria wa zamu ya Abiya... Basi ikawa alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele za Mungu...”
Yesu alikuja ulimwenguni na kuchukua nafasi ya kuhudumu ukuhani milele. Alikuja akiwa kuhani wa mambo mema yatarajiwayo. Aliyatimiza kupitia wokovu wa kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
Kizazi cha Haruni walikuwa dhaifu na wenye kasoro katika miili yao. Nini kilichotokea wakati kuhani akifa? Watoto wake wa kiume walimrithi, lakini utoaji wa sadaka katika namna hii kamwe kusingeweza kutosha kuleta uhakika wa wokovu wa mwanadamu. Imani kupitia mwanadamu kamwe haikuweza kuwa imani kamili.
Katika kipindi cha agano Jipya, Yesu alikuja ulimwenguni. Lakini hakuhitaji kutoa dhabihu mara kwa mara kwani yeye huishi milele. Alizichukua dhambi zetu milele kwa ubatizo wake. Alijitoa yeye mwenyewe na alisulubiwa ili kuwafanya wale wote wenye kumwamini kuwa huru kwa dhambi.
Sasa, yeye huishi daima na anaketi mkono wa kuume kwa Mungu kushuhudia kwa ajili yetu. “Baba, wanaweza kuwa si wakamilifu lakini wananiamini mimi, Je, Baba si mimi niliyezichukua dhambi zao zote kitambo kilichopita?” Yesu ni kuhani Mkuu wa milele kwa wokovu wetu.
Makuhani wa duniani hawakuwa wakamilifu. Walipofariki watoto wao wa kiume walirithi ukuhani wao. Bwana wetu anaishi milele. Alitimiza wokovu wa milele kwa ajili yetu kwa kuja ulimwenguni, kubatizwa na Yohana Mbatizaji na kutoa damu yake msalabani kwa ajili ya dhambi zetu zote.
“Basi ondoleo la hayo likiwapo hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi” (Waebrania 10:18) Yesu anashuhudia katika wokovu hadi siku ya mwisho. Je, wewe umekwisha zaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho?
“Maana ilikupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiye kuwa na uovu asiyetengwa na wakosaji, aliye kuwa juu kuliko mbingu” (Waebrania 7:26). “Maana torati yawaweka wanadamu walio na unyonge kuwa makuhani wakuu; bali hilo neno la kiapo kilichokuja baada ya torati limemweka mwana aliyekamilika hata milele” (Waebrania 7:28).
Ninachotaka kukwambia ni kwamba, Yesu Kristo asiye na doa, alitakasa dhambi zetu mara moja na kwa wakati wote kupitia maji na ubatizo na damu yake msalabani. Ametuokoa sisi wote kwa dhambi zetu zote si kwa matendo ya sheria bali kwa kuchukua dhambi zetu zote na kupokea hukumu milele.
Je, unaamini kwamba yeye alikuokoa kwa maji na kwa Roho kupitia wokovu wa milele? Ikiwa unaamini, basi umeokolewa. Lakini ikiwa huamini, basi una mengi ya kujifunza juu ya wokovu wa milele kupitia Yesu.
Imani ya kweli huja kwa injili ya maji na Roho ambayo kwa umakini inatokana na maandiko. Yesu Kristo Kuhani Mkuu wa milele mbinguni, alikuwa Mwokozi wetu milele kupitia ubatizo wake na damu yake msalabani.
 

YATUPASA KUIFAHAMU IMANI YETU KIKAMILIFU

Nini maana ya “kumwamini Yesu?”
Ni kuwa na imani katika ubatizo wa Yesu 
na kifo chake pale msalabani.

Yatupasa kuwaza juu ya namna tutakayomwamini Yesu kwa njia iliyosahihi na kuweka imani yetu sawa. Ni kwa namna gani basi tutaweza kumwamini Yesu katika njia iliyosahihi? Tutaweza kufanya hivyo kwa kuamini injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani.
Imani iliyo sahihi ni kuamini ile kazi Yesu aliyoifanya, ubatizo na damu yake, pasipo kuongezea mafundisho yetu mapotofu. Je, unaamini hili kuwa ni kweli? Hali yako ya kiroho ipoje? Je, unategemea sana matendo yako ya sheria na juhudi binafsi?
Si muda mrefu sasa upite tangu nilipoanza kumwamini Yesu, lakini hapo awali niliteseka kwa takribani miaka 10 kwa sababu ya kuwa mtu wa matendo ya sheria. Hatimaye nilichoka kwa aina hii ya maisha. Sipendi hata kukumbuka nyakati hizo. Mke wngu ameketi hapa nami. Yeye anajua vyema namna ilivyokuwa taabu kwetu.
Siku za Jumapili, ningeliweza kusema “mpenzi hebu tustarehe leo.”
“Lakini leo ni Jumapili.”
Hakutaka hata kufua nguo siku za Jumapili. Siku moja nguo zangu za ndani zilichanika. Lakini aliniambia kuwa inabidi nisubiri hadi Jumatatu. Ukweli wa mambo ni kwamba, tulikuwa tunajihimiza hata kuifuata Sabato kwa usahihi. Lakini ilikuwa vigumu kwetu. Hatukuweza kupumzika siku za Jumapili kwa sababu ilikuwa ni vigumu kuifuata Sabato kwa usahihi. Nakumbuka sana nyakati hizo.
Marafiki wapendwa, ili kumuamini Yesu kwa usahihi, yatupasa kuamini upatanisho wa dhambi zetu kupitia ubatizo wake na damu yake pale msalabani. Imani ya kweli ni kuamini Uungu na uanadamu wa Yesu na mambo yote Yesu aliyoyafanya hapa ulimwenguni. Imani ya kweli huamini maneno yake takribani yote kabisa.
Nini maana ya “kumwamini Yesu?” Ni kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake. Kwa hili ni jambo la maana lililorahisi. Kile itupasachokufanya ni kutafuta katika biblia na kuamini injili. Yatupasa sisi sote kuamini katika njia iliyo sahihi.
“Nakushukuru Bwana. Naona sasa haikufanyika kwa juhudi zangu! Kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria (Warumi 3:20). Nimekwisha elewa juu ya hili sasa. Nilidhani kwamba kwa kuwa sheria ni njema nilipaswa kuifuata, hivyo ninakosea ninapodhani ningeweza kuifuata. Sasa ninatambua ya kwamba kamwe sintoweza kufuata amri zako Mungu! Hivyo kwa kupitia sheria ya Mungu nimegundua moyo wangu umefurika mawazo ya uovu na matendo yake. Naelewa sasa kwamba sheria imeletwa ili kuingiza ndani yetu ufahamu wa dhambi. Oh, nashukuru Bwana. Sikuelewa mapenzi yako hivyo kujaribu kwa juhudi kubwa kuifuata sheria. Hiki ni kiburi ambaocho nisingejaribu kutenda. Nakiri. Naelewa sasa kuwa Yesu alibatizwa na kumwaga damu kwa ajili ya wokovu wangu! Naamini!”
Yakupasa uamini kwa moyo mweupe na kwauaminifu. Yakupasa uamini maneno yaliyomo katika Biblia tu. Ndiyo njia pekee utakayoweza kuzaliwa upya mara ya pili. 
Kumwamini Yesu ni nini? Je, ni kitu ambacho tunachopaswa kukamilisha kwa muda fulani? Je, imani yetu ni dini ambayo inakubidi uitafute? Watu wamejiundia miungu na kuwa na dini zao kulingana na miungu yao. Dini ni njia ambayo watu huifuata kufikia malengo; kuvutia uzuri wa mwanadamu.
Hivyo, imani ni nini? Maana yake ni kumwamini Mungu na kumtegemea. Tunautegemea wokovu wa Yesu na kumshukuru yeye kwa baraka hivyo. Hii ndiyo imani ya kweli. Hii ndiyo tofauti kati ya imani na dini. Wakati utakapoweza kutofautisha kati ya haya mawili, basi utapata alama 100 kwa kuelewa vyema imani.
Wanatheolojia ambao hawajazaliwa upya mara ya pili hutuambia ya kwamba inatupasa kumwamini Yesu na kuishi maisha matakatifu. Je, itawezekana mtu kuwa mwaminifu kwa namna ya utakatifu tu? Bila shaka inatupasa tuwe wema. Lakini ni yupi anayeishi maisha hasa matakatifu zaidi yetu sisi tuliozaliwa mara ya pili?
Lakini jambo kuu hapa ni kuwa wanawaeleza watu walio na dhambi. Zipo aina 12 za dhambi ndani ya kila mwana damu. Sasa itawezekana vipi kuishi maisha matakatifu? Labda akili yake inaweza kukubali nini cha kufanya lakini moyo usitende. Mwenye dhambi anapoliacha kanisa swala la kuishi maisha ya uongofu hubaki kuwa katika kanuni, na hivyo tabia yake humwongoza dhambini.
Hivyo yatupasa kuamua moyoni ama tutaishi kwa kuifuata sheria au kuokolewa kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani, kwa kuwa na imani na Kuhani Mkuu wa milele katika ufalme wa Mbinguni.
Kumbuka kuwa Yesu ndiye Kuhani Mkuu wa kweli kwa wale wote wenye kuamini. Hebu sasa sisi sote tuokoke kwa kujua na kuamini wokovu wa kweli kupitia ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani.
 

WALIOZALIWA UPYA HAWAOGOPI MWISHO WA DUNIA

Kwa nini waliozaliwa 
upya mara ya pili hawaogopi 
mwisho wa dunia?
Kwa sababu imani yao katika injili ya 
maji na Roho huwafanya wawe 
huru mbali na dhambi.

Ikiwa kweli umezaliwa upya mara ya pili haupaswi kuogopa dunia itakapofika mwisho wake. Wakristo walio wengi katika Korea walidai kwamba dunia ingelifika kikomo tarehe 28 Oktoba 1992. Hakika ingekuwa siku ya utisho na hofu kuu kwa jinsi walivyosema. Lakini madai haya yote yaligeuka kuwa ni uongo mtupu. Waliozaliwa upya huishi maisha matakatifu kwa kuhubiri injili mpaka siku ya mwisho. Ikiwa dunia hii itafika mwisho, kile tunachopaswa kufanya ni kuhubiri injili ya maji na Roho.
Bwana harusi atakapo kuja, bibi harusi waliozaliwa upya mara ya pili kweli kwa maji na kwa Roho watakutana naye kwa furaha kuu wakisema “Oh, hatimaye umekuja! Mwili wangu si kamilifu, lakini ulinipenda na kuniokoa kwa dhambi zangu zote. Hivyo sina dhambi tena moyoni. Nashukuru, Bwana. Wewe ni Mwokozi wangu!”
Yesu ni Bwana harusi wa kiroho kwa wale wote wenye haki. Ndoa inafanyika kwa sababu bwana harusi anampenda bibi harusi, si bibi harusi. Najua wakati mwingine huwa namna hii duniani, lakini mbinguni ni bwana harusi ndiye anayeamua juu ya ndoa kufanyika. Ni bwana harusi Yesu ndiye huchagua juu ya ndoa kutokana na upendo wake na zawadi ya wokovu na siyo bibi harusi.
Bwana harusi anaelewa vyote juu ya bibi harusi. Kwa sababu bibi harusi mpendwa wake alikuwa ni mwenye dhambi, alimwonea huruma na hivyo kumuokoa kwa dhambi zake kwa kubatizwa na kumwaga damu yake msalabani.
Bwana wetu Yesu hakuja duniani akiwa kama uzao wa Haruni. Hakuja ulimwenguni kutoa dhabihu ya kidunia. Palikuwepo Walawi wengi uzao wa Haruni kufanya kazi hiyo.
Ukweli nikuwa, mhusika mkuu wa dhabihu katika Agano la Kale si mwingine ila ni Yesu mwenyewe. Hivyo kile kilichohalisi kilipokuja duniani, nini kilichotokea kwa kile cha kivuli? Kivuli kiliwekwa kando.
Yesu alipokuja duniani, kamwe hakutoa sadaka kwa mfano wa Haruni. Alijitoa yeye mwenyewe kwa ajili ya wanadamu kwa kubatizwa na kutoa damu yake kwa wokovu wa wenye dhambi. Alikamilisha kazi ya wokovu pale msalabani.
Kwa wale wenye kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani, wokovu huja kwao kwa njia isiyo ya wasiwasi. Yesu hakutupatanisha kwa dhambi kupitia njia isiyoeleweka. Alifanya kwa njia bayana kabisa. “Mimi ndimi njia na kweli na uzima; mtu haji kwa Baba ila kwa kwa njia ya mimi” (Yohana 14:6) Yesu alikuja duniani na alituokoa kwa ubatizo wake kwa kifo chake na ufufuo wake.
 

AGANO LA KALE NI MFANO WA YESU

Ni kwa sababu gani kuwepo 
kwa agano jingine?
Kwa sababu agano la kwanza halikuwa 
imara na kutohitajika.

Agano la Kale ni kivuli cha Agano Jipya. Ingawa Yesu kamwe hakutoa dhabihu kwa jinsi ile ya Kuhani Mkuu katika Agano la Kale bali yeye alihudumu ukuhani uliobora zaidi, ukuhani wa milele mbinguni. Kwa sababu watu katika ulimwengu huu ni wenye dhambi toka kuzaliwa wanakuwa ni wenye dhambi na kamwe hawatoweza kuwa wenye haki toka kuzaliwa kupitia sheria ya Mungu. Hivyo Mungu alianzisha agano jingine.
Baba yetu wa mbinguni alimtuma mwana wake wa pekee kuja ulimwenguni na kutuhitaji kurudi kwa kuwa na imani kwa ubatizo wa Yesu, damu yake na ufufuko wake. Hili ni agano la pili. Agano hili hutuhitaji kuamini injili ya maji na Roho.
Bwana haitaji tena matendo mema. Hatuelezi tena namna ya kuishi ili tuweze kuokolewa. Anacho tuhitaji kufanya ni kuamini wokovu kupitia Mwana wake. Anatuhitaji kuamini ubatizo wake na damu yake msalabani kuliko vyote. Natuseme ndiyo.
Katika biblia, nyumba ya Yuda ilitunza mamlaka ya kifalme. Wafalme wote wa Israeli walizaliwa katika nyumba ya Yuda hadi kufikia mfalme Sulemani. Hata baada ya kugawanyika kwa dola hii, nyumba ya Yuda ilibaki na dola ya Kusini hadi ilipoanguka katika mwaka 586 kabla ya Kristo. Kwa njia hii watu wa Yuda waliwatetea Waisraeli. Kabila la Walawi ndilo liliokuwa moja ya makuhani. Kila kabila la Israeli lilikuwa na jukumu lake. Mungu aliahidi kabila la Yuda kwamba Yesu atatokea katika kabila zao.
Kwa nini aliweka agano hili kwa kabila la Yuda? Kwa kuweka agano hili lilikuwa ni sawa na kuweka agano hili na watu wote ulimwenguni kwa sababu Waisraeli husimama badala ya watu wa ulimwengu. Yesu alitimiza agano jipya ambalo ndilo wokovu wa wanadamu wote kupitia ubatizo wake, kifo chake msalabani na ufufuko wake.
 

DHAMBI ZA WANADAMU HAZIWEZEKANI KUTAKASWA KWA TOBA.

Je, dhambi za watu zinaweza 
kutakaswa kwa sala ya toba?
Hapana.

Yeremia 17:1 imeandikwa kwamba dhambi za kila mtu zimeandikwa kwa kumbukumbu katika sehemu mbili “Dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma, na kwa ncha ya almasi, imechorwa katika kibao cha moyo wao na katika pembe za madhabahu zenu.”
Dhambi zetu zimeandikwa ndani ya mioyo yetu. Hivi ndivyo tunavyoelewa kuwa sisi ni wenye dhambi. Kabla ya mtu kumwamini Yesu haelewi kuwa ni mwenye dhambi. Kwa nini? Kwa sababu sheria ya Mungu haimo moyoni. Hivyo, mara mtu huyo anapomwamini Yesu, anagundua kuwa ni mwenye dhambi mbele ya Mungu.
Wengine hugundua hili baada ya miaka 10 baada ya kumwamini Yesu. “Oh! Mimi ni mwenye dhambi! Nilidhani nimeokolewa, lakini kwa kiasi bado ni mwenye dhambi!” Kujitambua huku huja siku moja pale baada ya kujiona vile alivyo. Watu wa aina hii wanaweza kuwa na furaha mathalani kwa miaka 10 lakini ghafla wanaona ukweli. Unaelewa ni kwa nini? Utambuzi huu huja kwa sababu ya hatima ya kujua dhambi zake halisi na makosa yaliyowazi mwishoni kupitia sheria ya Mungu. Watu wa aina hii pia wanaweza kuwa wamemwamini Yesu kwa miaka 10 iliyopita pasipo kuzaliwa upya.
Kwa kuwa mwenye dhambi hana uwezo wa kutakasa dhambi zake moyoni, hubaki nazo mbele ya Mungu. Wengine huchukua miaka 5 na wengine miaka 10 kila mmoja hufikia mahala akagundua. Wengine hugundua baada ya miaka 30 na wengine 50 na zaidi wengine kwamwe hawagundui ukweli huo hadi mwisho. “Mungu wangu, nilikuwa mwema hapo awali nilipoishika amri yako akilini. Nilikuwa na uhakika kwa kufuta sheria vyema, lakini sasa nagundua kwamba ninatenda dhambi kila leo, kama vile Mtume Paulo alivyosema, “nami nilikuwa hai hapo kwanza bila sheria ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihurika nami nikafa” (Warumi 7:9). Mimi ni mwenye dhambi ingawa namwamini Kristo.”
Ni dhambi zako ndio zenye kukuzuia kwako kutokufuata neno la Mungu. Dhambi zako zimeandikwa katika moyo. Kwa kuwa Mungu ameweka kumbukumbu ya dhambi zako, unapoinamisha kichwa na kusali, dhambi hizo huibuka. “Unashangaa! Mimi ndiye dhambi uliyotenda.”
“Lakini mbona nilipatanishwa miaka 2 iliyopita kwa nini unajitokeza tena ghafla? Kwa nini hukufutika?”
“Oh, usiwe mjinga! Nimo katika kumbukumbu ya moyo wako. Hata ikiwa vipi, wewe ni mwenye dhambi.”
“Hapana! Hapana!”
Hivyo, mwenye dhambi anatubu tena kwa dhambi alizotenda miaka 2 iliyopita. “Tafadhali Bwana nisamehe. Bado nateseka kwa dhambi nilizotenda siku za nyuma. Nimetubu lakini bado zimo ndani yangu. Tafahali nisamehe kwa kuwa nimekosa.”
Lakini je, dhambi hizi kweli hufutika kwa sala za toba? Kwa kuwa zimeandikwa katika mioyo ya watu, kamwe hazitoweza kufutika pasipo injili ya maji na Roho. Ni kwa njia ya injili ya maji na Roho ndipo upatanisho wa kweli utaweza kupatikana. Tunaweza kuokolewa kupitia imani yetu katika injili ya Yesu tu.
 

NITAKUWA MWOKOZI WAKO

Kwa namna gani tunapaswa 
kuitika wito wa agano jipya?
Kwa kuamini agano hilo kwa moyo wetu 
wote na kulihubiri ulimwenguni.

Bwana wetu wa Mbinguni aliweka agano jipya nasi. “Nitakuwa mwokozi wenu. Nitawaweka huru kwa dhambi zote za ulimwengu kupitia maji na damu. Hakika nitawabariki wale wote wenye kuniamini mimi.”
Je, unaamini agano hili jipya la Mungu? Tutaweza kuokolewa kwa dhambi zetu zote na kuzaliwa upya mara ya pili ikiwa tutaamini ukweli wa gano lake na wokovu wake kupitia maji na damu.
Hatuwezi kumtumaini tabibu ikiwa hafanyi uchunguzi wa mgonjwa kwa usahihi. Tabibu kwanza inampasa kufanya uchunguzi wa ugonjwa na ndipo atoe utaratibu wa tiba kwa dawa zilizosahihi. Zipo aina mbalimbali za madawa, lakini tabibu inampasa kujua ni ipi kati ya hizo zitakazotumika. Punde tabibu anapofanya uchunguzi wa ugonjwa kwa ushahihi, zipo dawa nyingi za kumtibu mgonjwa wake. Lakini uchunguzi ukifanyika visivyo, dawa zozote zilizo nzuri zitaweza kumfanya mgonjwa awe kwenye hali mbaya zaidi.
Kama ilivyo pia, unapomwamini Yesu unapaswa ufanye uchunguzi wa hali ya roho yako kwa msingi wa Neno la Mungu. Unapofanya uchunguzi wa roho yako kwa neno la Mungu, ndipo utakapoweza kuona bayana hali ya roho yako ilivyo. Tabibu wa roho anaweza kuponya wagonjwa wake wote pasipo kubagua. Wote wataweza kuzaliwa upya mara ya pili.
Ikiwa unasema “sijui kama nimekwisha kukombolewa” hii maana yake hujaokolewa. Ikiwa mchungaji ni mfuasi kweli wa Yesu, inampasa awe na uwezo wa kutatua tatizo la dhambi kwa wafuasi wake. Ndipo ataweza kutatua matatizo mengine ya imani zao hivyo kuwaongoza kiroho. Inampasa awe na uwezo wa kuona vyema hali za kiroho za washirika wake.
Yesu alikuja katika ulimwengu huu kuchukua dhambi zote za ulimwengu. Alikuja na alibatizwa na kufa msalabani. Alipotupatanisha kwa dhambi zetu zote, je, alizisahau dhambi zako? Neno la maji na Roho limefuta kabisa dhambi za wale wote wanaomwamini.
Injili ni mfano wa baruti. Hulipua kila kitu toka magorofa hata milima. Kazi ya Yesu ni kama baruti. Hufuta dhambi za wale wote wanaomwamini yeye na injili yake ya maji na Roho. Hebu tuone injili ya maji na Roho inavyofafanuliwa katika Biblia.
 
 
INJILI YA KUWEKEA MIKONO KATIKA AGANO LA KALE

Sababu gani kulikuwepo 
na tendo la kuwekea mikono 
katika Agano la Kale?
Sababu yake ilikuwa ni kutwika dhambi 
juu ya sadaka ya dhambi (kafara).

Hebu na tuangalie ukweli wa injili ya ukombozi katika Walawi 1:3-4 “matoleo yake kwamba ni sadaka ya kuteketezwa ya ng’ombe, atatoa ng’ombe mume mkamilifu, ataleta mlangoni pa hema ya kukutania ili akubaliwe mbele ya Bwana. Kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa, nayo itakubaliwa kwa ajili yake ili kufanya upatanisho kwa ajili yake.”
Kifungu hiki kinatueleza kwamba dhabihu ya kuteketezwa ilipaswa kutolewa mbele ya mlango wa hema ya kukutania mbele ya Bwana kwa kuwekwa mikono juu ya kichwa cha mnyama wa sadaka na sadaka hiyo ilipaswa kuwa hai na isiyo na doa.
Katika nyakati za Agano la Kale, mwenye dhambi aliweka mikono juu ya dhabihu atakayotoa kwa upatanisho wa dhambi za siku. Atamchinja koo sadaka ya mnyama mbele ya Mungu na kuhani atachukua kiasi cha damu na kuweka katika pembe zilizopo katika madhabahu ya sadaka za kuteketeza. Damu iliyosalia ataimwaga chini ya madhabahu hiyo na ndipo mwenye dhambi husamehewa kwa dhambi zake za kila siku.
Kwa dahmbi zile za mwaka mzima kwa watu wote katika Walawi 16:6-10 inatueleza kuwa “na Haruni atamtoa yule ng’ombe wa sadaka ya dhambi aliye kwa ajili ya nafsi yake na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe na kwa ajili ya nyumba yake. Kisha atatwaa wale mbuzi wawili na kuwaweka mbele za Bwana mlangoni pa hema ya kuutania. Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili, kura moja kwa ajili ya Bwana na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli. Na Haruni atamleta yule mbuzi aliyeangukia na kura kwa ajili ya Bwana na kumtoa awe sadaka ya dhambi. Bali yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Azazeli, atawekwa hai mbele za Bwana ili kumfanyia upatanisho, ili kumpeleka jangwani kwa ajili ya Azazeli.” Kama ilivyoelezwa katika Biblia kafara maana yake “kitolewacho kwa niaba” Hivyo dhambi za mwaka zilifutwa katika siku ya kumi ya mwezi wa saba.
Katika Walawi 16:29-30 imeandikwa “amini hii itakuwa amri ya milele kwenu; katika mwezi wa saba, siku ya kumi ya mwezi, mtajitaabisha roho zenu msifanye kazi ya namna yoyote mzalia na mgeni akaaye kati yenu. Kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa kwa ajili yenu ili kuwatakasa nanyi mtatakaswa na dhambi zenu zote mbele za Bwana”.
Hii ilikuwa ni siku ya Israeli kupatanishwa kwa dhambi zao za mwaka mzima. Hili lilifanyikaje? Kwanza Kuhani Mkuu Haruni ndiye aliyepaswa kuwepo katika utoaji wa sadaka. Ni nani aliye wawakilisha watu wa Israeli? Haruni. Mungu alimteua Haruni na kizazi chake kuwa makuhani. 
Haruni alitoa ndama wa kiume kwa upatanisho wake binafsi na familia yake. Alimchinja ndama huyo na kunyunyuzia damu yake juu na mbele ya kiti cha rehema mara saba. Ilimlazimu kufanya upatanisho wake kwanza kabla ya yote.
Upatanisho hapa maana yake kutwika dhambi za mtu juu ya sadaka ya dhambi na hivyo kufanya sadaka hiyo ambayo ni mnyama ife kwa kuchinjwa koo badala ya mwenye dhambi. Mwenye dhambi ndiye aliyepaswa kufa, lakini upatanisho wa dhambi zake kwa kuzitwika juu ya mnyama na kumchinja badala yake ndiyo ulifanyika.
Baada ya dhambi zake na watu wa nyumba yake kufutwa, alimtoa mbuzi mwingine kwa Mungu na mbuzi mwingine alimwachia jangwani kama kafara mbele ya watu wa Israeli.
Mbuzi mmoja alitolewa kama sadaka ya dhambi. Haruni aliweka mikono juu ya kichwa cha sadaka hiyo na kutubu, “Oo Mungu, watu wa Israeli wamevunja amri zote kumi na vipengele vyake 613 katika sheria yako. Waisraeli wamekuwa wenye dhambi, naweka mikono juu ya mbuzi huyu kumtwika dhambi hizi zote juu yake.”
Ndipo humchinja koo na baadaye kuingia hemani sehemu takatifu akiwa na damu. Hunyunyiza kiasi mbele na juu ya kiti cha rehema mara saba.
Ndani ya patakatifu pa patakatifu palikuwepo sanduku la agano. Ganda la nje liliitwa kiti cha rehema na ndani yake paliwekwa vipande vya mawe ya agano, bakuli la dhahabu likiwa na mana na fimbo ya Haruni.
Fimbo hiyo ya Haruni humaanisha ufufuo, vipande vya mawe ya agano ni hukumu ya Mungu na bakuli la dhahabu lenye mana ni neno la Mungu la Uzima.
Palikuwepo na pazia katika sanduku la agano. Damu ilinyunyuziwa katika kiti cha rehama mara saba wakati kengele za dhahabu zilizoning’inizwa katika vazi la kuhani zikilia ndipo damu ilikuwa ikinyunyizwa.
Katika Walawi 16:14-15 imeandikwa “kisha atatwaa baadhi ya damu ya yule ng’ombe na kunyunyiza kwa kidole chake juu ya kiti cha Rehema upande wa mashariki na mbele ya kiti cha Rehema atanyunyizia ile damu kwa kidole chake mara saba. Kisha atamchinja yule mbuzi wa sadaka ya dhambi aliye kwa ajili ya watu na kuleta damu yake ndani ya pazia na kwa damu hiyo atafanya vile vile alivyofanya kwa damu ya ng’ombe na kuinyunyizia juu ya kiti cha rehema na mbele ya kiti cha rehema.”
Kila kengele ilipolia mara kadhaa kuhani aliponyunyuzia damu ya mbuzi, Waisraeli walio kusanyika nje waliweza kusikia sauti. Kwa kuwa upatanisho huo ulifanyika kwa kupitia Kuhani Mkuu, sauti za kengele zilipolia ilimaanisha kuwa dhambi zao zilikuwa zimesamehewa. Zilikuwa ni sauti za baraka kwa watu wote wa Israeli.
Kengele zilipolia mara saba walisema, sasa tumepata nafuu, “tumekuwa tukiwa na hofu kwa muda wa mwaka mzima juu ya dhambi zetu na sasa tunajisikia tuko huru.” Ndipo watu wanapoendelea na maisha yao, kuwa huru na hukumu. Sauti ya kengele katika nyakati hizo huwa ni sawa na habari njema za kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho katika nyakati hizi.
Tunaposikia injili ya ukombozi kupitia maji na Roho na kuamini kwa moyo wetu wote na kukiri kwa midomo yetu; hii ndiyo injili ya maji na Roho inayoongelewa. Kengele ilipolia mara saba, dhambi zote za watu wa Israeli zilisafishwa mbele ya Mungu.
Baada ya kutolewa kwa mbuzi wa sadaka kwa Waisraeli, Kuhani Mkuu alimchukua yule mbuzi wa pili na kwenda mbele za watu waliokuwa wakisubiri nje ya hema. Huku wakitazama Kuhani Mkuu akimwekea mikono juu ya kichwa chake.
Katika Walawi 16:21-22 “Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israelii, na makosa yao, naam, dhambi zao zote, naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliyetayari. Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote mpaka nchi isiyo watu; naye atamwacha mbuzi jangwani.”
Kuhani Mkuu Haruni aliweka mikono yake juu ya kichwa cha yule mbuzi (kafara) na kuungama dhambi zote za mwaka mzima za wana wa Israelii mbele ya Mungu akisema “oo Mungu, Waisraeli wametenda dhambi mbele yako. Tumevunja amri zote kumi na vipengele 613 katika sheria yako. Oo Mungu, namtwika dhambi hizi zote za kipindi cha mwaka za wana wa Israelii juu ya kichwa cha mbuzi huyu.”
Kutokana na Yeremia 17:1, dhambi zimeandikwa sehemu mbili kwa kumbukumbu. Moja zimo katika kitabu cha matendo na nyingine katika mbao za mioyo.
Hivyo watu hupatanishwa kwa dhambi zao kwa kuzifuta toka kitabu cha matendo na katika mbao za mioyo yao. Katika siku ya upatanisho, mbuzi alikuwepo kwa ajili ya dhambi zilizoandikwa katika kitabu cha hukumu na nyingine zilizoandikwa katika mbao za mioyo.

Mungu alitaka kuwaonyesha 
nini wana wa Israeli kupitia 
mpangilio wa utoaji wa sadaka 
katika agano la Kale?
Alitaka kuwaonyesha jinsi ile mwokozi 
atakapokuja na kufuta dhambi zote 
mara moja na kwa wakati wote 
katika njia iliyostahili.

Kwa kuwekea mikono juu ya kichwa chake mbuzi, Kuhani Mkuu alionyesha watu kwamba dhambi za mwaka zilihamishwa juu ya mbuzi. Dhambi hizo zilipowekwa juu ya kichwa cha mbuzi mtu aliye tayari alimkokota mbuzi huyo kwenda naye jangwani.
Nchi ya Palestina ni jangwa. Mbuzi aliyebeba dhambi zote za mwaka za Waisraeli aliongozwa na mtu aliyechaguliwa kwa shughuli hiyo kwenda jangwani pasipo maji wala nyasi. Watu walisimama na kuangalia kafara hiyo ya mbuzi ikitokomea jangwani.
Walisema “ilinipasa nife lakini mbuzi amekufa kwa ajili ya dhambi zangu. Mshahara wa dhambi ni mauti lakini mbuzi huyo amekufa badala yangu. Nakushukuru mbuzi kifo chako kimeniletea uhai” mbuzi alitokomea mbali katika jangwa na Waisraeli waliweza kusamehewa dhambi zao za mwaka. 
Dhambi za moyoni mwako zinapotwikwa juu ya sadaka ya dhambi, unakuwa umetakaswa. Hivi ndivyo ilivyo rahisi. Ukweli siku zote huwa rahisi ikiwa tu tutaelewa.
Mbuzi alitokomea katika upeo. Ndipo yule mtu aliporudi peke yake baada ya kumuacha huko. Dhambi zote za mwaka za Waisraeli zilipokwisha mbuzi huyo alitangatanga jangwani pasipo maji na nyasi, hatimaye alikufa kwa dhambi za mwaka za Israelii.
Mshahara wa dhambi ni mauti, sheria ya Mungu ilitimizwa. Mungu alimtoa sadaka yule mbuzi ili Waisraeli waweze kuwa na uhai. Makosa yote ya Waisraeli katika mwaka mzima yalitakaswa.
Wakati dhambi za siku na zile za mwaka ziliposamehewa katika nyakati za Agano la Kale lilikuwa ni agano la Mungu kwamba dhambi zetu pia kwa mfano huu zitasamehewa mara moja na kwa wakti wote. Hili ni agano la Mungu ya kwamba atamtuma Masihi na kutukomboa kwa dhambi zetu zote maishani. Agano lilifanyika kupitia ubatizo wa Yesu.
 

KUZALIWA UPYA MARA YA PILI KWA MAJI NA KWA ROHO KATIKA AGANO JIPYA

Kwa nini Yesu alibatizwa 
na Yohana Mbatizaji?
Kuitimiza haki yote kwa kubeba dhambi 
zote za ulimwengu. Ubatizo wa Yesu 
katika Agano Jipya ulikuwa ni 
sawa na kuwekea mikono 
katika Agano la Kale.

Hebu na tusome Mathayo 3:13-15 “wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote. Basi akamkubali.”
Yesu alikwenda Yordani na kubatizwa na Yohana Mbatizaji na kwa kufanya hivyo, alitimiza haki yote. Alibatizwa na Yohana Mbatizaji aliye mkuu kuliko wote walio zaliwa na wanawake.
Mathayo 11:11-12 “amini nawaambieni, hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji, wa lakini aliyemdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye. Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatika kwa nguvu nao wenye nguvu wauteka.”
Yohana Mbatizaji aliteuliwa na Mungu kuwa mwakilishi wa wanadamu na alitumwa miezi 6 kabla ya Kristo. Alikuwa ni uzao wa Haruni na kuhani wa mwisho.
Yohana Mbatizaji alimwambia Yesu alipomwona akimjia “mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?”
“Kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote” Dhumuni lake lilikuwa ni kuwaweka wanadamu wote huru toka dhambini ili waweze kuwa wana wa Mungu. Yesu alimwambia Yohana “yatupasa kuikamilisha injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Hivyo inakupasa unibatize.”
Yohana alimbatiza Yesu. Ilimpasa Yesu abatizwe ili kubeba dhambi zote za ulimwengu. Kwa kuwa alibatizwa kwa njia iliyopaswa, hivyo nasi tumeokolewa kwa njia iliyo stahili kwa dhambi zetu zote. Yesu alibatizwa ili dhambi zetu zote ziweze kutwikwa juu yake.
Yesu alikuja ulimwenguni na kubatizwa alipofikisha umri wa miaka 30. hii ndiyo huduma yake ya awali. Yesu alitimiza haki yote kwa kufuta dhambi zote za ulimwengu hivyo kuweza kuwatakasa watu wote.
Yesu alikuja ulimwenguni na kubatizwa kwa njia iliyostahili ili kutukomboa kwa dhambi zetu zote. “Hivi ndivyo” haki yote ilivyotimizwa.
Mungu alisema “huyu ni Mwanangu Mpendwa wangu ninayependezwa naye” (Mathayo 3:17). Yesu Kristo alijua ya kuwa atabeba dhambi zote za wanadamu na kumwaga damu kwa kifo chake msalabani, lakini alitii mapenzi ya baba yake, kwa kusema “walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe” (Mathayo 26:39).
Mapenzi ya Mungu yalikuwa ni kutakasa dhambi za wanadamu na hivyo kuwapa wokovu watu wa ulimwengu. Hivyo Yesu mwana mtiifu alitii mapenzi ya Baba yake na kubatizwa na Yohana Mbatizaji.
Katika Yohana 1:29 “siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake akasema, tazama Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” Yesu alichukua dhambi zote na kumwaga damu msalabani Golgota. “Tazama Mwana Kondoo aichukuaye dhambi ya ulimwengu” ndivyo Yohana Mbatizaji alivyoshuhudia.
Je, unadhambi au hapana? Je, ni mwenye haki au mwenye dhambi? Ukweli ni kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu zote ulimwenguni na kusulubiwa msalabani kwa ajili yetu sote.

Ni lini dhambi zote 
za waovu wa ulimwengu 
ziliwekwa juu ya Yesu?
Yesu alibeba dhambi zetu zote wakati 
pale alipobatizwa na Yohana 
Mbatizaji katika mto Yordani.

Baada ya kuzaliwa hapa duniani tunaanza kutenda dhambi hata kati ya umri wa mwaka 1 na miaka 10. Yesu alichukua dhambi hizi zote. Pia tunatenda dhambi kati ya umri wa miaka 11 na 20. Dhambi tuzitendazo mioyoni mwetu na kwa matendo ya nje hizi nazo pia alizibeba zote.
Pia tunatenda dhambi tukiwa na umri kati ya miaka 21 na 45. hizi nazo alizibeba pia. alizichukua dhambi hizo zote za ulimwengu na kusulubiwa msalabani. Tunaanza kutenda dhambi tokea kuzaliwa hadi tunapokufa. Lakini hizi zote Yesu alizibeba.
“Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya dunia!” Dhambi zote, kuanzia za yule mtu wa kwanza, Adamu hadi yule wa mwisho kuzaliwa hapa duniani—awaye yote—Yesu alibeba. Hakuchagua kuangalia ni za nani azichukue.
Hakuamua kuwapenda baadhi yetu. Alikuja katika mwili na kubeba dhambi zetu zote ulimwenguni na hivyo kusulubiwa msalabani. Alipokea hukumu kwa ajili ya wote na kufuta dhambi za ulimwengu huu milele.
Hapana yeyote aliyetengwa kwa wokovu wake. “Dhambi ya ulimwengu” inajumuishwa dhambi zetu zote. Yesu alizibeba zote.
Kwa ubatizo na damu yake, ametakasa dhambi zote za ulimwengu. Alizibeba zote kwa ubatizo wake na hivyo kuhukumiwa kwa ajili yetu msalabani. Kabla ya Yesu kufa pale msalabani, alisema “imekwisha” (Yohana 19:30) maana yake wokovu wa wanadamu ulikamilika.
Kwa nini Yesu alisulubiwa msalabani? Kwa sababu uhai wa mwili u ndani ya damu, na damu hufanya upatanisho kwa uhai wa mtu (Walawi 17:11). Kwa nini Yesu ilimpasa kubatizwa? Kwa sababu alitaka kubeba dhambi zote za ulimwengu.
“Baada ya hayo, Yesu hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema “naona kiu”” (Yohana 19:28). Yesu alikufa hali akijua maagano yote ya Mungu katika Agano la Kale yalitimizwa kwa ubatizo wake katika Yordani na kwa kifo chake msalabani.
Yesu alijua kwamba ukombozi ungeliweza kutimizwa kupitia kwake na hivyo kusema “imekwisha”. Alifia msalabani. Alitutakasa, alifufuka toka wafu baada ya siku 3 na kupaa mbinguni, alipo sasa kuume kwa Mungu.
Kusafisha dhambi zote kupitia ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani ni baraka ya injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Amini nawe utasamehewa dhambi zako zote.
Kamwe hatutoweza kupatanishwa kwa dhambi zetu zote kwa kusali sala ya toba kila siku. Ukombozi uliletwa mara moja na kwa wakati wote kupitia ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani pekee. “Basi ondoleo la hayo likiwapo hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi” (Waebrania 10:18).
Sasa basi tunachopaswa kufanya ni kuamini ukombozi kupitia ubatizo wa Yesu na kusulubiwa kwake. Amini na utaokolewa.
Warumi 5:1-2 inasema “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani na niwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kufikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.”
Hakuna njia nyingine ya kuweza kuhesabiwa haki bali kuamini baraka ya injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
 

DHUMUNI LA SHERIA YA MUNGU

Je, tutaweza kutakaswa 
kwa sheria?
Kamwe hatutoweza kutakaswa kwa 
sheria bali kupitia sheria tutazifahamu
dhambi zetu.

Katika Waebrania 10:9 imeandikwa “ndipo aliposema tazama nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza ili kusudi alisimamishe la pili.” Hatuwezi kutakaswa kwa kupitia sheria. Sheria inachoweza ni kutufanya tuwe wenye dhambi zaidi. Mungu hakuwa na maana kwetu sisi kutii sheria.
Warumi 3:20 “kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria” Mungu aliwapa Waisraeli sheria kupitia Musa baada ya mwaka 430 iliyopita tangu Ibrahimu alipopokea Agano. Aliwapa sheria ili kwamba waweze kung’ahamu nini maana ya kutenda dhambi mbele ya Mungu. Pasipokuwepo na sheria ya Mungu, wanadamu wasingekuwa na ufahamu juu ya dhambi. Mungu ametupatia sheria ili tuwe na ufahamu wa juu ya dhambi.
Hivyo basi sababu pekee ya sheria ni kutufanya kuelewa kuwa sisi ni wenye dhambi mbele ya Mungu. Kwa kupitia ufahamu huo tunatarajiwa sasa kumrudia Yesu kwa kuamini baraka ya injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Hili ndilo dhumuni hasa la sheria ya Mungu kwetu.
 

BWANA AMEKUJA KUFANYA MAPENZI YA MUNGU

Yatupasa kufanya nini 
mbele ya Mungu?
Yatupasa kuamini ukombozi wa 
Mungu kupitia kwa Yesu.

“Tazama nimekuja nifanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza ili kusudi alisimamishe la pili” (Waebrania 10:9). Kwa kuwa hatuwezi kutakaswa kwa sheria, Mungu hakutukomboa kwa sheria yake, bali kwa ukombozi ulio kamili. Mungu ametupa kwa upendo na haki yake.
“Katika mapenzi hayo mmepata utakaso kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu. Na kila kuhani husimama kila siku na kufanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi, ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi. Lakini huyu alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele aliketi mkono wa kuume wa Mungu” (Waebrania 10:10-12).
Aliketi mkono wa kuume wa Mungu kwa kuwa kazi yake ya ukombozi ilikamilika na hapakuwepo na chochote tena cha ziada kwake kutenda. Hatobatizwa tena wala kujitoa sadaka mwenyewe tena katika kutuokoa.
Sasa basi dhambi zote ulimwenguni zimetakaswa, anachohitaji ni kutoa uzima wa milele kwa wale tu watakao mwamini. Hivyo leo huwatia mhuri wale wote wanaouamini wokovu wa maji na Roho kwa kuwapa kipawa cha Roho.
Yesu alishuka ulimwenguni na kubeba dhambi zote za ulimwengu na kufa msalabani, kwa hivyo alikamilisha kazi yake. Leo hii kazi ya Bwana imekwisha, ameketi kuume kwa Mungu.
Yatupasa kumwamini Bwana Yesu kuwa ametuokoa kwa dhambi zetu zote milele. Ametufanya kuwa wakamilifu milele kwa ubatizo na damu yake.
 

WALE WALIO ADUI WA MUNGU

Ni nani aliye adui wa Mungu?
Ni wale wote wanaomwamini Yesu huku 
wakiwa na dhambi mioyoni mwao.

Katika Waebrania 10:12-14 Bwana anasema “Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele aliketi mkono wa kuume wa Mungu tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake” Anasema anasubiri hadi hapo siku ya mwisho ya hukumu kuamua mwisho wao.
Adui zake bado wanasema “Bwana tafadhali nisamehe dhambi zangu” shetani na wafuasi wake hawaamini injili ya maji na Roho hivyo wanaemdelea kuomba msamaha kwake. 
Bwana wetu hatowahukumu sasa. Lakini siku ya kuja kwake Yesu mara ya pili, watahukumiwa na kutupwa motoni milele. Mungu anawavumilia hadi hapo siku ya mwisho akitumaini kwamba wapo watakaotubu na kuwa wenye haki kupitia ukombozi wake. 
Bwana wetu Yesu alichukua dhambi zetu zote na kufa kwa ajili yetu sisi tunaomwamini. Yesu atarudi tena siku moja kwa mara ya pili ili kuwachukua wale wote waliomwamini. “Oo tafadhali Bwana uje haraka”, atakuja mara ya pili kuwachukua wasiokuwa na dhambi ili kuishi nao milele katika Ufalme wa Mbinguni.
Wale wote wenye kusisitiza kuwa ni wenye dhambi Bwana atakaporudi hawatokuwa na nafasi mbinguni, katika siku ya mwisho watahukumiwa na kutupwa moto wa milele. Adhabu hii inawasubiri wale wote wanaokataa kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
Bwana wetu Yesu huwachukulia wale wote wenye kuamini uongo kuwa ni adui kwake. Na ndiyo maana yatupasa kupigana na uongo huu. Na ndiyo maana pia yatupasa kuamini baraka ya injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
 

YATUPASA KUAMINI INJILI YA MAJI NA ROHO

Je, inahitajika tena kupatanishwa 
kwa dhambi zetu sasa ambazo zilikwisha 
lipiwa zote kwa pamoja?
Hapana, hata kidogo.

Waebrania 10:15-16 inasema “na Roho Mtakatifu naye amshuhudia kwa maana baada ya kusema. Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile anena Bwana. Nitatia sheria zangu mioyoni mwao. Na katika nia zao nitaziandika ndipo anenapo.”
Baada ya kufuta dhambi zetu zote, alisema “hili ni agano nitakalo agana nao” Agano hili ni lipi? “Nitatia sheria zangu mioyoni mwao na katika nia zao nitaziandika ndipo anenapo” Mwanzoni tulijaribu kuishi maisha ya kufuata sheria kulingana na sheria ya Mungu lakini hatukuweza kuokolewa hakika kwa sheria hiyo.
Baadaye tukaja kuelewa kwamba Yesu alikwisha tuokoa tayari wale tunaoamini kwa moyo wetu wote ile baraka ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Yeyote anayeamini ubatizo na damu ya Yesu amekombolewa.
Yesu ni Bwana wa wokovu. “kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo 4:12), Yesu alikuja ulimwenguni akiwa ni mwokozi. Kwa kuwa hatutoweza kuokolewa kwa matendo yetu, Yesu alituokoa na kuandika katika vibao vya mioyo yetu kwamba ametuokoa kwa sheria ya upendo na wokovu.
“Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa. Basi ondoleo la hayo likiwapo hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi” (Waebrania 10:17-18).
Sasa Mungu hakumbuki tena uovu wetu. Alikwisha beba yote tunaamini hatuna tena dhambi zitakazohitajika kusamehewa. Deni letu limekwisha lipwa lote na hakuna kilichobaki kulipiwa upya. Watu huokolewa kwa imani kupitia huduma ya Yesu, aliyetuokoa kwa ubatizo na damu yake msalabani. 
Hivyo kinachotupasa kufanya ni kuamini maji na damu ya Yesu. “Tena mtaifahamu kweli nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32) Amini wokovu katika Yesu. Kupata wokovu ni jambo rahisi kuliko hata kupumua. Unachopaswa kufanya ni kuamini vile mambo yalivyo. Wokovu ni kuamini tu neno la Mungu.
Amini kwamba Yesu ni mwokozi wetu (katika ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani) na uwe na imani ya wokovu kuwa ni kwa ajili yako. Achana na fikra zako na amini wokovu wa Yesu tu. Naomba kwamba hakika umwamini Yesu na uwe tayari kuelekea katika uzima wa milele naye.