Search

Kazania

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 2-1] Utangulizi katika Kitabu cha Warumi Sura ya 2

Katika ulimwengu huu yapo makundi mawili, Wayahudi na Wakristo wamwaminio Mungu na kati ya watu hawa wapo wale wenye kumwamini Yesu na wale wasio mwamini Mungu huchulia imani ya wale wasio mwamini Yesu kuwa ni bure isiyofaa. Hata hivyo, tatizo kubwa linalowakabili Wakristo ni hili la kumwamini Yesu kwa njia yoyote huku wangali bado hawaja samehewa dhambi zao. Mtume Paulo alizungumzia hili katika Warumi Sura ya 2 si kwa Wayahudi na Wayunani pekee bali hata kwa Wakristo wa nyakati hizi.
 

Wayahudi huwahukumu wengine kirahisi.
 
Mtume Paulo huwakemea wote Wayahudi na Wakrsto walio na imani aina hii. Katika (Warumi 2:1) Paulo anasema “Kwa hiyo, wewe mtu uwaye yote uhukumuye huna udhuru” akiwakemea wale wote walio na upotofu kwa hisia za kuwa watu wa daraja ya juu kwa kuwa tu ni Wayahudi au Wakristo. Hata wale ambao bado hawajazaliwa upya mara ya pili kwa njia ya kumwamini Mungu, sasa wanaelewa kile kilicho uovu kwa msingi wa sheria ya dhamira za mioyo yao. Na ndiyo maana huwaambia wengine wasiibe ingawa wao hutenda uzinzi na kutofuata maneno ya Bwana, huku wakiongoza wengine kwa amri za Mungu nakutamka kwamba wanamwamini Mungu. Hivi ndivyo walivyo watu hawa walio Wayahudi na Wakristo ambao hawajazaliwa upya.
Wale wenye kumwamini Mungu huwaambia wengine wasiabudu sanamu au kutenda dhambi ya kuua, wakijigamba kwamba wao huzifuata sheria za Mungu. Hivyo basi huacha kumheshimu Mungu kwa kuzivunja sheria zake.
Watu wasio jua haki ya Mungu huku waki mwamini Yesu, nao husema kwamba Yesu ni Mwokozi kwao. Lakini imani zao hazipo katika msingi wa haki ya Mungu hivyo kwamba huipinga kweli ya haki ya Mungu ambayo tayari ilikwisha ondoa dhambi zao zote. Wao wenyewe hawajui kwamba wanawapinga kwa kutoamini kwao kweli ya Mungu. Twaweza kuona kwamba watu wengi hujuta kuwa Wakristo huku wakiikataa Injili iliyo na haki ya Mungu ndani yake pasipo kufahamu upendo wa Yesu, au hata tohara ya kiroho. Hudai kumfuata Mungu na mapenzi yake lakini ukweli ni kwamba bado hawaja mkubali Yesu na wamemsulubisha msalabani kwa kumshutumu kukufuru kwamba yeye alijitambulisha kuwa ni Mwana wa Mungu.
Mtume Paulo alisema kwamba Myahudi wa mwonekano wa nje si Myahudi halisi, bali yule wa mwonekano wa ndani ndiye hasa Myahudi halisi. Wao hudai kwamba ni watu wa Mungu na hivyo wataweza kumwamini Mungu kwakuwa wao ni sehemu ya taifa la Mungu. Lakini ni vipi Wayahudi wataweza kumwamini Mungu na hali walimkataa Yesu kuwa ni Mwokozi kwao?
Paulo husema “na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko” (Warumi 2:29). Wale wote wenye kuamini tohara ya roho ndiyo wenye kuamini kweli katika Mungu. Ni wenye haki kwa imani.
Ni kwa nani wenye kuamini wataweza kuipokea heshima na sifa? Yawapasa kuipokea toka kwa Mungu. Paulo alisema “Sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu” (Warumi 2:29). Ikiwa tunaamini haki ya Mungu, basi ndipo tutapata sifa yake na kupokea tuzo toka kwake. Ikiwa unamwamini Yesu kwa mwonekano wa nje huku ungali na dhambi moyoni, basi bado hujaiamini haki ya Mungu. Ukweli ni kwamba unamdhihaki yeye. Hivyo, utapokea hukumu ya wasio amini.
Ni watu gani wenye kuidharau kweli ya Mungu? Hawa ni wale wenye kufuata maneno ya wanadamu kwa dhati na kwa makini kuliko neno la Mungu. Hujitambulisha kwa dini zao mbali mbali katika Ukristo huku wakimpinga Mungu. Hukataa na kusimama kinyume dhidi ya haki ya Mungu katika wokovu wakiwa na nguvu ya muungano baina yao. Je, unaweza kudhani ni adhabu gani itakayo wakumba watu hawa?
 

Adhabu ya wale wote wenye kumpinga Mungu.
 
Mstari wa 8 na 9 unatamka “na wale wenye fitina wasiotii kweli bali wakubalio dhuluma, watapata hasira na ghadhabu, dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Myunani pia.”
Dhiki na shida itakuja kwa kila nafsi ya mwanadamu iliyo tenda uovu. Hapa neno “shida” ni adhabu itakayopokelewa jehanamu kwa wale watendao uovu. Ipo dhiki na shida jehanamu kwa watu hawa.
Ni aina gani ya laana kwa wale walio kataa kumpokea Mungu watapokea? Mungu ataleta hukumu ya ghadhabu juu yao wote walio ukataa upendo wake. Unategemea nini juu ya walio upinga ukweli wa Mungu ambao ulikuja kutokana na tohara ya kiroho, ili kuishi kwa amani katika mwili na akili? Baadhi ya watu huishi maisha ya upotofu kwa sasa hivyo baada ya kifo wanastahili ghadhabu ya Mungu. Wao ndiyo walio ipinga haki ya Mungu na hawawezi kuwa na hali ya kutosheka katika mioyo yao. Hawajui juu ya upendo ule utokanao na tohara ya kiroho, hata pale wanapo hudhuria kanisani huku wakitubu na kukiri kumwamini Yesu hivyo badae wanateseka kwa kuto ondolewa dhambi mioyoni mwao.
Hauto weza kujua juu ya siri hii kwanjia ya kumwamini Yesu kwa namna yoyote. Ni wale tu wanao iamini haki ya Mungu ndio watakao weza kuelewa. Kwa ushauri wangu, ninyi mnao amini visivyo katika Mungu ni kwamba, imewapasa kuelewa na kuiamini Injili ya maji na Roho ambayo hii ndiyo haki ya Mungu. Ndipo hapo basi mtaweza kuwa huru kwa mahangaiko ya laana.
Ikiwa mtu anasema kwamba ana dhambi moyoni mwake hata pale anapo mwamini Yesu, maana yake ni kuwa anaamini visivyo na inampasa aiamini Injili ya kweli yenye kuleta haki ya Mungu. Haijalishi watu wamo katika dhehebu gani lenye kumwamini Yesu, ikiwa wanadiriki kutamka kwamba wanamwamini kwa namna yoyote, huku wakiwa na dhambi mioyoni mwao basi wanatenda dhambi na kupuuzia haki ya Mungu. Matokeo yapi yaliyo mema katika kumwamini Mungu? Ikiwa unamwamini Yesu kama Mwokozi wa kweli hakika wewe utakuwa si mwenye dhambi tena. Hata hivyo ikiwa bado unadhambi moyoni hata baada ya kumwamini Yesu, maana yake ni kwamba wewe bado haujaelewa ipasavyo juu ya Haki ya Mungu.
Bwana anaye okoa wenye dhambi toka dhambini mwao tayari amekwisha kuja katika mwili, aliokoa wenye dhambi na kuwa Mwokozi kwa wale wote wanao mwamini. Sasa basi, je, mtu mwenye kuamini kwa hakika juu ya maji na Roho Mtakatifu anadhambi? Mtu haimpasi kuwa na dhambi ikiwa hakika anaamini haki ya Mungu tokea pale anapo mwamini Yesu kwa mara ya kwanza. Lakini ikiwa anadharau haki ya Mungu huku akimwamini Yesu vile atakavyo yeye na nafsi yake basi moyo wake haujawa na dhambi. 
Hivyo basi imekupasa uachane na ukaidi wako sasa hivi. Ukiri “Nilimwamini Yesu vile isivyo! Sasa ni njia ipi inipasayo kuelewa juu ya Yesu na kuamini? Hatimaye nimeelewa kwamba Msalaba ni muhimu katika kumwamini Yesu lakini pia hata ubatizo wake ni muhimu. Sasa nimekuja kuelewa kwamba Yesu alisulubiwa na kupokea hukumu kwa niaba yetu kwa sababu hapo awali alizibeba dhambi zetu zote ulimwenguni kwa njia ya ubatizo wake.” Yakupasa uelewe ukweli huu na pia kuuamini.
Wale wote watakao baki kuwa wakaidi dhidi ya Bwana watapokea adhabu ya Mungu. Matokeo yake ni kutupwa katika moto wa jehanamu. Na ndiyo maana Mathayo 7:22 inatamka kwamba “Wengi wataniambia siku ile Bwana, Bwana hatukufanya unabii kw ajina lako, na kwa jina lako kutoa pepo na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?” Bwana atakapo kuja tena wale wasio amini haki ya Mungu na kuwa na dhambi moyoni huku wakiwa mwonekano wa nje wakijisingizia kumwamini Yesu watahukumiwa mbele ya Mungu. Watasema mbele ya Bwana, “Je, sikukuamini vile ipasavyo Bwana? Je, sikukutumikia wewe Bwana?”
Hata hivyo Bwana atawajibu “Ondokeni kwangu, ninyi mtendao uovu! (hii inamaana kuwa hawa ni wale wote wasio iamini haki ya Mungu) Utaweza kusema kwamba unaniamini mimi hali huamini kwamba tayari nilikwisha zifuta dhambi zenu zote kwa kuupokea ubatizo na kufa msalabai? Ninyi ni waongo, mtakwenda jehanamu milele. Dhambi zenu ni zile za manabii wa uongo na zimewaongoza wengi wenu jehanamu.” Wale wasioamini haki yake na hata kutoacha ukaidi wao watapokea ghadhabu kuu ya Mungu.
Mfano mkuu wa aina hii ya imani ni ule wa Wayahudi ambao hadi sasa ni wenye mioyo migumu mbele ya Mungu. Hadi leo hii hawaamini kwamba haki ya Mungu ni kupitia Yesu Kristo. Hata kati ya Waprotestanti pia wamo Wakristo wakaidi wenye kusema kwamba dhambi zao za kila siku zitaweza kusamehewa kila wanapofanya sala za toba. Watu hawa wote imewapasa kuacha ukaidi huo wao wa kutoamini haki ya Mungu ili basi waweze kukwepa ghadhabu ya Mungu.
Je, Yesu husamehe wale wote kwa udhalimu wao binafsi pale wanapo tubu na kusali ili waweze kusamehewa kila siku? Sivyo. Yohana Mbatizaji aliye kuwa Kuhani Mkuu wa mwisho katika Agano la Kale na pia mwakilishi wa wanadamu, alimbatiza Yesu miaka 2000 iliyopita na kumwaga damu yake msalabani. Kwa kufanya yote haya aliitimiza haki ya Mungu na kufutilia mbali dhambi zote za dunia mara moja na kwa wakati wote.
Ni wapi Yesu alizibeba dhambi zetu zote? Yesu alijitwisha dhambi zote za wanadamu mara moja na kwa wakati wote pale alipo batizwa na Yohana katika Mto Yordani. Pia aliwaokoa wale wenye kumwamini milele kwa dhambi zao kwa kwenda kwake Goligotha ili kumwaga damu yake msalabani na hivyo kupokea hukumu badala yetu kwa ajili ya dhambi zote. Lakini Wakristo wote wenye dhambi mioyoni mwao bado ni wakaidi na hawataki kuiamini haki ya Mungu. Ikiwa mioyo yao imekwisha takaswa tayari kwa dhambi zao zote kwa njia ya damu ya msalaba pekee, sasa basi, ni kwa sababu gani inawapasa kuomba msamaha wa dhambi zao hadi kifo kinapo wakuta? Ni kutokana na ukaidi wao. Damu ya Yesu msalabani ni muhimu lakini pia ubatizo wake alio upokea toka kwa Yohana nao ni muhimu katika kuamini na hivyo dhambi za watu husamehewa mara moja ili kupata haki ya Mungu.
Ukweli ni kwamba kila mmoja wetu ni kaidi kwa namna fulani. Lakini mbele ya Mungu inatupasa kuacha ukaidi wetu wa kukataa ile iliyo haki yake. Wale wenye kumwamini Mungu imewapasa kutii na kuyaamini maneno yake. Nami pia bila kuficha ni mtu mkaidi lakini niliacha ukadi wangu mbele ya Mungu na hivyo kuwa mwenye haki kwa rehema yake.
Toba ya kweli ni kuacha ukaidi na kupokea msamaha wa dhambi kwa kukubali haki ya Mungu kwa moyo. Baada ya kusamehe yatupasa kuanza kubadilika nyendo zetu dhalimu na kuyakubali makosa yetu, huku tukijitahidi kuishi maisha mema kiroho mbele ya Mungu. La kwanza ni toba katika maisha ya kweli ya mtakatifu aliye zaliwa upya mara ya pili.
Wale wenye kumwamini Yesu huku hawaifahamu haki ya Mungu wataangamizwa. Watu hawa imewapasa kuachana na ukaidi katika njia zao, watubu na kuamini ubatizo na msalaba wa Yesu kwa ajili ya ondoleo la dhambi (Matendo 3:19). Bwana ametupatia amri hii ili tuweze kupata ondoleo la dhambi mara moja na kwa wakati wote kuamini haki yake. Yatupasa kumsikiliza Mungu ni kuyasikia maneno yake ili kwamba tuweze kuwa wakamilifu wenye haki na hata kusamehewa dhambi zetu zote mara moja kwa kuamini ukweli ambao Yesu alitupatanisha kwa dhambi zetu zote kwa njia ya ubatizo na kusulubiwa kwake. Mtu anapo amini haki ya Mungu basi atasamehewa dhambi zake zote na hatimaye kumpokea Roho Mtakatifu kwa zawadi au karama. Mitume wote na wafuasi wa Yesu waliamini haki ya Mungu na kupokea ondoleo la dhambi wakati huo huo. Nawe pia usiwe mkaidi mbele ya ukweli huu. Uwe na ukaidi kwa wakati unao faa. Ikiwa bado hujaelewa tohara ya kiroho vyema, yakupasa ujifunze na kuiamini. Haitosaidia kuendelea kuwa mkaidi. Yakupasa utubu na kuamini.
Watu huukataa ukweli “Hivi sivyo! Mtu atawezaje kuwa mwenye haki huku akiendelea kutenda dhambi kila siku? Unajua Mungu huwaita wale wanao mwamini Yesu kuwa ni wenye haki ijapokuwa bado ni wenye dhambi”. Hii ndiyo kanuni ya kuhesabiwa haki. Huitwi mwenye haki kwa sababu tu huna dhambi moyoni. Hata hivyo inakupasa uelewe kwamba hili ni fundisho potofu.
Katika Biblia, Mungu alisema kwamba kupitia Injili ya tohara ya roho ambayo ametupatia ondoleo la dhambi “nimekwisha futa dhambi zetu zote. Wewe huna tena dhambi. Kwa sababu nimekwisha beba dhambi zenu zote, ninyi ni wenye haki Je, mnaamini haki yangu? Ikiwa mnaanimi maneno yangu ya tohara ya kiroho, basi ninyi ni kati ya watu wangu na msio na dhambi” Hivi ndivyo Mungu azungumzavyo juu ya ukombozi wake ulio kamili. Lakini baadhi ya Wakristo wa majina hudhihaki na kuwazushia Wakristo walio okoka ambao huamini juu ya tohara ya kiroho. Husema “Mtu awezaje kuwa mwenye haki hali bado anaendelea kutenda dhambi pasipo kikomo? Mtu aweza kuitwa asiye na dhambi kwa Kanuni yafundisho la Kuhesabiwa haki tu. Utawezaje kudhani mtu hatendi dhambi kweli? Huwezi kujizuia kuacha kutenda dhambi.” Hudhihaki kwa maneno kama haya na hivyo kuendelea kuwa wakaidi kwa kuto amini haki ya Mungu.
Lakini Mungu ameleta uzima wa milele kwa wale wote wenye moyo wa subira katika kutenda mema. Wenye kutafuta utukufu, heshima na uzima wa milele kwa kuvumilia na kuendelea kufanya yote yaliyo mema na hivyo kuwa watoto wa Mungu. Bali wale wasio fuata haya watahukumiwa. Kila mtu anataka kuwa mwana wa Mungu na kuishi milele. Yesu ndiye atoaye uzima wa milele kwao wale wote wanao utafuta kwa dhati ili waishi milele huku wakiwa wasio na dhambi.
“Kile ninacho taka Bwana ni kuamini ondoleo la dhambi kwa njia ya tohara ya kiroho ili kwamba niishi pasipo aibu katika dhamira yangu. Nataka niwe mtoto wa Mungu. Nataka niamini haki yako na kukufanya uwe mwenye furaha. Napenda niwe mtu asiye na dhambi tafadhali niokoe na dhambi zote.” Kwa njia kama hii wale wote wenye kuitafuta haki ya Mungu katika wokovu na kutamani kusamehewa dhambi zao zote, Mungu huyasikiliza matamanio yao yote na hivyo basi kuwasamehe dhambi zao zote kwa kuwapatia Injili ya haki ya Mungu. Wale wote watakao kuishi milele basi Mungu huwapa uzima wa milele.
 

Tohara ya roho ni nini?
 
Maana yake ni ondoleo la dhambi lililokamilishwa kwa njia ya ubatizo wa Yesu na damu yake pale msalabani. Damu ya mwanakondo ni kafara la hukumu na ule ubatizo wa Yesu kwa Yohana maana yake ni dhambi za dunia kutwikwa juu yake Yesu. Hata hivi leo, Ukristo kamwe hautoweza kudharau Agano la Kale kwa sababu kwa njia hiyo itakuwa ni vigumu kuamini Agano Jipya. Katika maandiki twaweza kuona kwamba tohara ya roho na damu ya mwanakondoo wa Pasaka ni mambo yaliyo shabihiana.
Katika 1 Yohana 5:6 inasema kwamba Yesu alikuja “Si katika maji tu bali katika maji na katika damu.” Yesu hakuja kwa maji au damu, bali kwa yote mawili. Yakupasa uamaini tohara ya kiroho iliyo na maneno ya maji damu na Roho ili kwamba uweze kukombolewa kwa dhambi zako zote.
Ukisoma katika sura ya 12, niliwahi kuwa na maswali juu ya hii tohara ya rohoni. Nini sura hii inamaanisha? Nilipitia kwa uangalifu mkubwa sura yote, mwanzo hadi mwisho na vifungu vingine nje ya hapo vyenye kuhusiana na sura hiyo katika Biblia kwa kurudia rudia. Na nikaja kugundua kwamba Waisraeli waliweza kushiriki katika sikukuu ya Pasaka kwa sababu tu walikuwa tayari wamekwisha tahiriwa. Na katika Agano Jipya inasema kwamba Yesu hakumwaga damu pale msalabani bure, bali kwa sababau alikuwa tayari amekwisha batizwa na Yohana.
Mungu aliwaagiza Waisraeli ibada mbili kisheria kwa ajili ya siku ya Pasaka, kwanza kutahiriwa na ndipo kuila nyama ya mwanakondoo wa Pasaka. Hii ilikuwa ndiyo tohara ya rohoni katika Agano Kale! Katika Agano Jipya inasemekana kwamba dhambi zetu zilitikwa juu ya Yesu kwa kupitia ubatizo wa Yesu kwa Yohana Mbatizaji na hivyo kumwaga damu yake msalabani. Niligundua kwamba kwa kuukubali ukweli huu hupelekea katika ukweli wa kupokea tohara ya kiroho. Yesu Kristo alibatizwa na Yohana pale Yordani, na hivi ndivyo alivyo beba dhambi zote za dunia hivyo kwamba kupelekea kifo chake msalabani katika hatua ya kupokea hukumu kwa niaba yetu.
Unaweza kushuhudia wokovu kwa dhambi zote na uovu wote kwa kuukubali ukweli huu moyoni mwako. Kwa mtu kuweza kupokea wokovu wa dhambi zake zote anahitaji kuamini haki ya Mungu, ambayo inaweza  kutupatia ile iliyo tohara ya rohoni. Imewapasa watu kuelewa ukweli huu. Ninyi wasomaji wangu mnapaswa kuelewa juu ya ukweli wa tohara ya kiroho katika Agano la Kale na ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya ambavyo ni muungano pacha pale inapo husu ondoleo la dhambi. Yesu hakupokea hukumu kwa sababu ya kutenda dhambi, bali alikufa msalabani kwa ajili ya wanadamu kwa kuwa alibatatizwa na kubeba dhambi za dunia juu ya mwili wake. Hii ndiyo imani ya wale wote walio kwisha kupokea tohara ya rohoni.
Wale wote, wenye kuamini haki ya Mungu kwa kupitia tohara ya kiroho hawana dhambi tena kwa kuwa wamemwamini Yesu vile inavyo stahili. Nawasikitikia wale wanao mwamini Yesu kwa namna yoyote, huku wangali bado kupokea tohara ya Rohoni itokayo kwa Mungu. Imewapasa kuamini ukweli kwamba Yesu alizibeba dhambi zote za ulimwengu pale Yohana alipombatiza.
Kwa bahati mbaya, wakristo wengi, huamini juu ya msalaba pekee na si ubatizo Yesu, kwa jinsi hii hawana imani katika haki ya Mungu. Yatupasa kujua kwamba imani katika haki ya Mungu. 
Yatupasa kujua kwamba imetulazimu kuamini kile Mungu alicho tueleza katika Maandiko.Yatupasa kuzirarulia mbali bila kujali kanuni zote au mafundisho yote ya kitheologia na hatimaye kuamini maneno ya Mungu. Hii ni kwa sababu pasipo haki yake hakuna kweli ya Mungu. Injili isiyo na tohara ya roho haijakamilika. Na ndiyo maana katika Biblia, Mungu ananena mara kwa mara juu ya tohara katika Agano la Kale na ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya. Kwa maneno mengine inazungumziwa juu ya tohara na damu ya mwana kondoo wa Pasaka katika Agano la Kale ikiwianishwa na ubatizo wa Yesu na damu yake katika Agano Jipya. Yatupasa kuamini ukweli huu ili kuweza kupokea tohara ya rohoni. Hata hivyo ikiwa hatutaamini ukweli huu, basi tutatupwa kando katika Ufalme wa Mungu.
Je, haki ya Mungu imetimia kwa damu ya Yesu msalabani pekee? Hivi sivyo. Haki ya Mungu ilitimia kwa yote mawili, yaani ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Hivyo twapokea tohara ya kiroho mioyoni mwetu si kwa kumwaga kwake damu msalabani tu, bali pia kwa ubatizo alio upokea toka kwa Yohana. Tohara ya kiroho itawezekana kwetu ikiwa Yesu alikwisha zifuta dhambi zetu zote kwa njia ya ubatizo na upatanishao wa kifo chake msalabani.
 

Tohara maana yake ni kukatilia mbali.
 
Isaya alitoa unabii kwamba Masia, Yesu Kristo atapokea hukumu ya dhambi kwa niaba yetu kwa kujeruhiwa na kuchubuliwa. Hivyo lipo jambo tunalo paswa kufahamu kabla ya kuendelea. Kwa nini Kristo ilimpasa asulubiwe msalabani?
Katika Agano la kale mwenye dhambi ilimpasa aweke mikono juu ya sadaka ya mwana kondoo ili kumtwika dhambi zake na ndipo kumchinja shingo. Ndipo kuhani kwa vidole vyake, aliweka katika pembe za wanyama zizungukazo pande nne za madhabuhu ya kuteketeza kwa moto na kuimwaga damu iliyo baki chini ya madhabahu hiyo (Walawi 4:27-30). Mwenye dhambi katika Agano la Kale aliweza kuondoleea dhambi zake zote kwa njia hii pekee. Je, Yesu Kristo aliyekuja akiwa mfano wa Mwanakondoo wa Mungu (Yohana1:29) angeweza vipi kutuokoa sisi sote kwa dhambi zetu ikiwa kama asingewekewa mikono juu ya kichwa chake mfano wa Agano la Kale ili aweze kubeba dhambi za wanadamu?
Sasa basi, ni lini na kwa namna gani Bwana alizibeba dhambi za ulimwengu? Je, si hili lionekanalo katika Mathayo 3:13-17 ambapo Yohana alimbatiza Yesu katika Yordani?. Hivi ndivyo ilivyo kwa jinsi ya Walawi katika Agano la Kale pale inapo endelea ikisema mwenye dhambi “Kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa” (Walawi 1:4, 3:8, 4:29) ili kwamba aweze kumtwika dhambi zake. Kuhani Mkuu katika Agano la Kale ilimpasa weke mikono yake juu yakichwa cha kondoo wa sadaka na kumtwika dhambi zake binafsi na zile za Waisraeli wote (Walawi 16:21). Ndipo alipo ichukua damu ya mnyama huyo kiasi na kuiweka katika pembe zizungukazo kingo nne za madhabahu ya kuteketeza na kumwaga iliyo baki chini ya madhabahu hivyo ndivyo walivyo pokea ondoleo la dhambi kwa njia hii.
Kwa njia kama hii, dhambi zetu ziliwezekana kuondolewa kwa njia ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani. Hii ndiyo haki ya Mungu na tohara ya kiroho ambayo Mungu alipenda kutupa sisi ndani ya Biblia. Hivyo kwa sasa sisi wenye kuamini haki ya Mungu, dhambi zetu zote zilifutiliwa mbali kwa ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani. Tunapoelewa maana ya ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya, basi tunaweza kuiamini haki ya Mungu na hatimaye kuweza kupokea tohara ya kiroho miyoni mwetu.
 

Tohara ya kweli ya kiroho katika Agano la Kale.
 
Natuangalie Mathayo 3:13-15 “Yesu akijibu akawaambia, kubali hivi sasa, kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali.”
Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu katika mto Yordani Alimwekea mikono kichwa Yesu na kumbatiza. (Ubatizo kwa lugha ya Kiyunani ni “baptizo” ambapo inamaana ya kutumbukiza, kuzamisha majini).
Ili Yesu afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, kwanza ili mpasa abebe dhambi zetu zote kwa njia ya ubatizo. Hivyo alibatizwa na Yohana kwanza kwa kuzamishwa kwenye maji ya mto Yordani. Kwa nini basi alibatizwa? Jibu ni ili aweze kuitimiza haki yote ya Mungu. Ilikuwa ni haki na inavyofaa au kustahili ili aweza kuzibeba dhambi za wanadamu kwa njia ya ubatizo na hivyo kuweza kuwa Mungu wetu na Mwokozi. Ilikuwa ni sahihi kwa Yesu kufa msalabani akiwa amezibeba dhambi zetu zote katika mwili wake kwa njia ya ubatizo.
Kile Yesu alichoweza kufanya awali katika maisha yake ya hadharani ilikuwa ni kupokea ubatizo kwanza. Ubatizo kwa lugha ya Kiyunani, “baptizo” unamaanisha “kusafisha, kutakasa, kuzika, kuhamisha, na kutwika.” Katika Agano la Kale siku ya 10 katika mwezi wa 7 ilikuwa ni siku ya Upatanisho kwa Waisraeli, na Haruni aliweka, mikono juu ya mbuzi wa sadaka ili kumtwika dhambi zote za Waisraeli. Kati ya mbuzi wale wawili, mmoja alitolewa kwa Mungu na mwingine alifanywa sadaka kwa ajili ya upatanisho mbele ya Waisraeli (Walawi 16). Katika Agano Jipya Yesu alizibeba dhambi zetu zote kwa kubatizwa na Yohana.
Siku iliyo fuata baada ya ubatizo Yohana alikutana na Yesu na kumnyooshe kidole akisema “Tazama Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” (Yohana 1:29).
Yakupasa ukubali kwamba tohara ya kiroho haitowezekana kwa kuamini damu ya Yesu pekee.
Tuangalie kwa kuanzia 1 Yohana 5:4 “Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huishinda ulimwengu, ni nani isipo kuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu? Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu. Yesu Kristo, si katika maji tu, katika maji na katika damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli. Kwa maana wako watatu washuhudiao (mbinguni, Baba, Neno na Roho Mtakatifu na watatu hawa ni umoja. Kisha wako watatu washuhudiao duniani) Roho na maji na damu na watatu hawa hupatana kwa habari moja” (1 Yohana 5:4-12).
Je! Ni nini dhibitisho la kutahiriwa kwa roho? ni imani ya kuamini katika Ubatizo wa Yesu na damu yake kama wokovu wetu. Ushindi ambao umeshinda ulimwengu ni maji na damu. “Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si kwa maji tu, bali pia kwa damu. naye ndiye Roho anayeshuhudia kwa sababu Roho ni kweli. Na kuna watatu wanaoshuhudia duniani: Roho, maji, na damu.” Shuhuda hizi zenye kuonyesha Mungu kuwa ni Mungu kwetu na Mwokozi, zinadhihirisha kwamba alishuka duniani akiwa na mwili wa mwanadamu, akibeba dhambi zetu zote juu ya mwili wake kwa niaba yetu, kwa njia huyo alitukomboa kutokana na dhambi zetu zote.
Katika Agano Jipya, Injili ya tohara ya kiroho imejumuisha maji na damu. Katika Agano hilo Jipya, maji ya ubatizo wa Yesu alioupokea kwa Yohana na damu yake, una maanisha kifo cha msalabani. Ubatizo wa Yesu ni upande mwingine unaofanana katika Agano la Kale ambao ni tohara. Ubatizo wa Yesu kwa Yohana ni uthibitisho kwamba dhambi zetu zilitwikwa juu yake. Wale wote wenye kuamini ukweli huu wataweza kusimama mbele ya Mungu huku wakisema “Mungu wewe ndiwe Mwaokozi wangu. Naiamini haki yako hivyo hakika sina dhambi. Mimi ni mtoto wako nisiye na lawama na wewe ndiye Mungu wangu.” Msingi gani wa Maandiko ambao unakupelekea kuwa na uhakika wa kupaza sauti yako ukisema hivyo? Ni imani katika ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani, ambavyo vyote vimejenga haki ya Mungu. Kuikubali haki ya Mungu kama ndiyo haki yangu haitowezekana kwa damu ya Yesu pekee. Yote mawili yaani ubatizo na damu ndivyo viletavyo hili.
Hebu tuangalie kifungu kinacho zungumzia juu ya kutowekwa kando kwa ubatizo wa Yesu kwa wokovu wetu. 1 Petro 3:21 ni uthibitisho wa Ukweli huu “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamira safi mbele za Mungu kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.”
Mtume Petro hapa anazungumzia juu ya ushuhuda ulio dhahiri wa wokovu wetu. Vile Waisraeli walivyo kata magovi yao katika tohara nyakati za Agano la Kale, katika Agano Jipya Yesu alibatizwa na Yohana na kubeba dhambi zote za ulimwengu, akituwezesha kupokea tohara ya rohoni. Ubatizo na damu ya msalabani umeunda haki ya Mungu. Tohara ya kiroho na ubatizo una maana moja. Yakupasa uelewe kwamba ubatizo wa Yesu unamaanisha tohara ya roho kwetu sote.
“Mfano wa mambo haya ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi.” Tunapokeaje haki ya Mungu? Kwa kuamini kwamba Yesu alibatizwa na kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Mathayo 3:15 inatamka “hivi ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote” Kwa kuwa dhambi zote za wanadamu zilitwikwa juu ya kichwa cha Yesu, dhambi zote za watu wote zilifutwa kabisa. Kila mwenye dhambi akawa mwenye haki kwa kuamini ubatizo na damu ya Yesu Kristo. Alimwaga damu kwa kuhukumiwa msalabani baada ya kubeba dhambi zote za dunia. Dhambi zote za wanadamu zilipatanishwa kwa njia hii. Kwa kuamini kwamba Yesu alibeba dhambi zote za dunia kwa kubatizwa kwake na hatimaye kupokea hukumu kwa niaba yetu, ndiyo kuwa na imani ya kweli ambayo itakayoleta haki ya Mungu kwa kila muumini. Amini ukweli huu.
Yohana 1:29 inatamka “Tazama! Mwanakondo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Yesu ni mwana wa Mungu na ni Muumba wetu, aliye timiza agano lake la tohara kwa kubeba dhambi zote za wanadamu. Hii ni imani ya kweli ambayo ndiyo iletayo tohara ndani ya mioyo yetu, ambayo ndiyo haki ya Mungu. Yesu ndiye haki kwetu. Yatupasa kumshukuru. Tumshukuru kwa ubatizo na damu yake ambayo ndiyo imetuwezesha kupokea tohara ya kiroho.
1 Petro 3:21 inaendelea kusema “Siyo kuwekea mbali uchafu wa mwilini bali jibu la dhamira safi mbele za Mungu.” Uchafu wa mtu mwilini hauondolewi kwa kuwa tu anamwamini Yesu kuwa ndiye Mwokozi. Utaweza kupokea ondoleo la dhambi kwa kuamini kwamba dhambi zako zote zimetwikwa juu ya Yesu kwa njia ya ubatizo na damu yake aliyo mwaga msalabani. Kupokea ondoleo la dhambi kwa kukiri Yesu kuwa ni mwokozi kutokea moyoni. Hii hutokea ndani ya moyo wa mwenye kuamini. Ikiwa unamwamini Mwokozi kwa moyo wako wote, basi utaondolewa dhambi zako zote, hali mwili wako utaendelea kuwa mchafu na kuendelea kutenda uovu kila siku, lakini si mwenye dhambi tena. Unapokea haki ya Mungu kwa kuamini kwamba, pale Yesu alipo batizwa dhambi zako zote zilitwikwa juu yake na hivyo hakuna tena dhambi moyoni.
 

Yakupasa uamini ukweli ili uweze kuwa wako.
 
Katika Yohana 1:12 inasema “Bali wate waliompokea aliwapa uwezo za kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake”.
Maneno gani uliyopokea na kuyakubali? Yakupasa upokee yale ambayo mwana wa Mungu aliyo tenda. Mambo gani hayo? Mwana wa Mungu alikuja duniani akiwa na umbile la mwili wa dhambi na alipotimiza umri wa miaka 30, alibatizwa ili kubeba dhambi zote za wanadamu na hivyo kuwapa tohara ya kiroho ili dhambi zetu zote zifutwe. Ndipo akafa msalabani akiwa ni mwanakondoo wa Mungu na kuleta upatanisho kwa ajili yetu. Bwana amekuwa sadaka ya dhambi ya milele kwa wote wenye dhambi na kutuokoa milele. Hii ndiyo imani ya kweli. Tunaweza kuwa wenye haki kwa kuamini ukweli huu.
Je, tunaweza kupokea tohara ya kiroho kwa damu ya Yesu, pekee? Hapana hatutoweza. Ubatizo wa Yesu huondolea mbali dhambi zetu, na hukumu aliyo ipokea msalabani kwa kumwaga damu yake kwa ajili ya dhambi za watu ni hukumu kwa niaba yetu wewe na mimi. Tuliokolewa kwa dhambi zetu na tumeepushwa na hukumu kwa sababu tunaamini Injili ya haki ya Mungu. Kumpokea Yesu kuwa ni Mwokozi ndiko kuwezako kufuta dhambi zote za watu moyoni. Pokea tohara ya kiroho ndani ya moyo wako ndipo basi haki ya Mungu itaweza kuwa yako.
 

Tohara ya kweli ya Kiroho inapaswa kufanyika ndani ya moyo.
 
Katika Warumi Sura ya 2 Mtume Paulo anasema “tohara ni ya moyo.” Je, una jitahiri vipi moyoni? Hii inawezekana kwa kuamini kwamba Yesu Kristo alikuja ulimwenguni akiwa katika mwili wa mwanadamu, na hivyo kubatizwa ili kubeba dhambi zote za dunia, akafa kwa kumwaga damu yake msalabani na hatimaye alifufuka tena ili aweze kuwa Mwokozi wetu wa milele. Mtume Paulo alisema kwamba tohara inapaswa kufanyika moyoni. Na utaweza kutahiriwa ndani ya moyo wako kwa kuamini ubatizo wa Yesu. Ikiwa unahitaji kupokea tohara ya kiroho moyoni mwako amini ubatizo wa Yesu.Ndipo kwa njia hii mtaweza kuwa wana wa Mungu. Mtu mwenye haki ni yule anaye amini ubatizo wa Yesu na damu ambavyo ndivyo vilivyo mkombao kwa dhambi zake zote. Amen.
Hata alipokua na umri wa miaka 29, bado Yesu aliishi maisha binafsi ya kawaida kama wengine huku akisaidia familia yake. Lakini alipo fikisha umri wa miaka 30 alianza kuishi maisha ya hadharani nje ya familia yake. Katika kipindi hicho cha kutoka nje ya familia ndipo hapo alipo zifuta dhambi zote za wanadamu na kuwakomboa wenye dhambi wote kwa dhambi zao. Cha kwanza alicho kifanya ilikuwa ni kupokea ubatizo ili aweze kuwakomboa wenye dhambi wote na kuwafanya wenye haki “Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe” (Mathoyo 3:13). Kwa nini Yesu alikuja ili abatizwe? Yatupasa kutambua kwamba alifanya hili ili kwamba aweze kubeba dhambi zote za watu. Tusishindwe kuelewa maana kamili ya ubatizo wake. Ubatizo ni kusafisha dhambi kwa njia ya kutwika au kuzihamisha. Na ndiyo maana Yesu aliweza kubeba dhambi za wanadamu akimtaka Yohana ambatize.
Yohana huyu aliye mbatiza Yesu ni nani? Yohana ni mwakilishi wa wanadamu wote. Hili limeelezewa vyema katika Mathayo 11:11-14 “Amini nawaambieni, Haijaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji, walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye. Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa Ufalme wa Mbinguni hutapatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. Kwa maana manabii wote na torati walitabiriwa mpaka wakati wa Yohana. Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakaye kuja.”
Tangu kuanza kwa siku za Yohana Mbatizaji kipindi cha Agano la Mungu kili hitimishwa. Hii ni kwa sababu Yesu, mtu aliye itimiza ahadi yake aliwasili. Sasa basi ni watu gani walio zitimiza ahadi za Mungu katika Agano la Kale?. Sasa basi ni watu gani walio zitimiza ahadi za Mungu katika Agano la Kale? Walikua ni Yesu na Yohana Mbatizaji. Yohana Mbatizaji alimtwika Yesu dhambi akiwa ni kuhani wa mwisho katika Agano la Kale aliye tumwa ili amtwike Mwana kondoo wa Mungu dhambi zote ambaye aliyekuja katika Agano Jipya. Yohana alitekeleza jukumu hili kwa kuweka mikono yake juu ya kichwa cha Yesu kulingana na utaratibu wa kisheria uliowekwa katika utoaji wa sadaka za kafara wakati wa Agano la Kale. Dhambi zote za ulimwengu ziliondolewa mbali na kuhamishwa juu yake Yesu pale alipo batizwa. “Hivi ndivyo” Mungu alivyo toa tohara ya kiroho kwa kila mioyo ya wanadamu.
Ushikilie kwa dhati ubatizo wa Yesu na damu yake kama upatanisho wako. Yesu alikwisha zichua dhambi zote za ulimwengu na pia kubeba hukumu ya wote. Injili ya haki ya Mungu ni ukweli ambao Yesu alibatizwa nakumwaga damu yake katika upatanisho wa dhambi zote. Sasa hivi twaweza kupokea ondoleo la dhambi kwa kuikubali haki ya Mungu mioyoni mwetu tu. Ikiwa utaipokea basi utaweza kuingia katika “Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu” (Mathoyo 1:1). Wapo wale wenye kuifahamu haki hii ya Mungu na pia wapo wasio ifahamu ambao bado wamo nje ya Yesu Kristo. Jua lina kuchwa. Amini ubatizo wa Yesu na damu yake pia na uingie kwake. Imani inayo wekwa katika ubatizo ndiyo itakayo kuwa mafuta ya taa yatarishwayo katika tafrija ya harusi. Natumaini unaijua siri hii ili uweze sasa kutayarisha mafuta ya taa kwa ajili ya taa ili uweze kukutana na Bwana mara ya pili ajapo kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani.
Yesu alipokea ubatizo ili aweze kufutilia mbali dhambi za kila mtu, Yesu ni mwana wa Mungu na ni Mungu pia. Yeye ndiye Muumbaji. Alikuja duniani kwa mapenzi ya Baba yake ili aweze kuturithi kuwa watoto wa Mungu Je, unabii wote katika Agano la Kale unamzungumzia nani? Unatoa unabii juu ya Yesu. Ulikuwa ukitolewa kuhusiana na vile Yesu atakavyo kuja duniani na kubeba dhambi zote na hatimaye kuziendolea mbali milele. Kwa jinsi hii unabii katika Agano la Kale ulisema, Yesu alikuja duniani takribani miaka 2000 iliyo pita na kubeba dhambi zetu zote kwa kubatizwa. Alibeba dhambi zote za wanadamu kuanzia Adamu na Hawa hadi mtu wa mwisho ajaye.
Pokea tohara ya kiroho ndani ya moyo wako “Tohara ni moyo, katika roho” (Warumi 2:29). Unapoa amini ubatizo wa Yesu, moja kwa moja unapokea tohara ya moyo. Tohara ya moyo maana yake ni kuondolea mbali dhambi za moyoni pale tunapo kiri kwamba dhambi zetu zote zilitwikwa juu ya Yesu kwa ubatizo wake. Je, wewe umekwisha pokea tohara hiyo ya moyo? Kwa kuamini tohara ya moyo “dhambi zote zitatakaswa kwa imani.”
 

Je, hakika unaukubali ukweli wa tohara ya kiroho ndani ya moyo wako?
 
Imekwisha pita miaka takribani 2000 tangu Yesu alipokuja ulimwenguni, kubatizwa na kufa msalabani. Yatupasa kuukubali ukweli huu na kuupokea mioyoni mwetu leo. “Tohara ni ya moyo katika roho” Twaweza kupokea tohara katika akili zetu na mioyo yetu kwa imani ya kweli. Sisi sote tumekwisha kupata ukombozi kwa kuamini haki ya Mungu. Ingawa hukumu ya Mungu itakuja ulimwenguni, kamwe hatuto hofu. Wale wote wenye kuiamini haki ya Mungu hawatopokea hukumu yake. Hukumu ya Mungu itawaangukia wote wale ambo hawaja ipokea haki ya Mungu mioyoni mwao.
Kwanini hadi leo Wakristo wanaamini damu ya Yesu pekee kwa ajili ya Wokovu wao? Sasa yakupasa ukiri kwamba ulimuudhi Mungu kwa ukaidi wako na hivyo urudie ukweli ambo Yesu alibeba dhambi zetu zote kwa kubatizwa kwake Yordani, ndipo tohara ya kiroho itafanyika moyoni mwako.
Ikiwa unaamini vyote ubatizo wa Yesu na damu yake, tohara ya kiroho itafanyika ndani ya moyo wako na hautopokea hukumu ya Mungu bali kuwa kati ya watoto wake. Mungu atakuwa ni Mungu wako nawe utakuwa moja ya watu wake. Ikiwa wamo kati yenu ambao wana mwamini Yesu lakini bado wanaitegemea damu yake tu, napenda niwaulize swali, Je, tohara zetu za kiroho na haki ya Mungu ni kwa damu ya msalabani pekee? Ama kwa hakika wokovu umehitimishwa si kwa damu tu bali kwa ubatizo wa Yesu, damu na Roho.
 

Haki ya Mungu hupatikana kwa kushikamana na Kristo.
 
Hebu natujifunze katika Warumi 6:3-8 “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama mlivyo unganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake, mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena kwa kuwa yeye aliyekufa anahesabiwa haki mabali na dhambi. Lakini ikiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye.”
Mstari wa 5 unatamka “Kwa maana kama mlivyo unganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwamfano kufufuka kwake.” Biblia inasema kwamba mshahara wa dhambi ni mauti, maana yake, yeyote aliyo na dhambi ataangamia jehanamu. Je, ninyi nyote hamkutenda dhambi kabla ya kuamini ukweli kamili wa Yesu Kristo? —Ndiyo.— hata kama unadhambi kiasi kidogo bado utakwenda jehanamu na kupokea hukumu ya “lile ziwa liwakalo moto na kiberiti” (Ufunuo 21:8). Ikiwa ingetupasa kulipa mshahara wa dhambi zetu, ambao ni mauti, basi tusinge weza kuokolewa kwa dhambi zetu zote na kumhukumu yeye badala yetu.
Mungu ametuokoa sisi sote kwa sababu alitupenda sana. Mungu Baba alimtuma mwana wake ulimwenguni, akamtwika dhambi zote za ulimwengu juu yake kwa njia ya ubatizo na kumsulubisha kwa kumgongelea misumari ili kwamba amwage damu kwa upatanisho wa dhambi zote. Kuamini hili ni kuungana na Yesu. Mshahara wa dhambi ni mauti. Sisi sote tumekwisha kuwa na dhambi mioyoni mwetu na tulipaswa kwenda jehanamu kwa sababu ya dhambi hizo. Lakini kwaniaba yetu, sisi tuliokuwa tutupwe jehanamu, Yesu alizichukua dhambi hizo pale Yordani kwa kubatizwa na kuhukumiwa kama sadaka msalabani. Hivyo, kifo chake kikawa ni kifo chetu kwa sababu ya kubatizwa kwake ambako ndiko kuliko beba dhambi zetu zote. Hii ndiyo imani yakushikamana na Kristo.
Watu wengi bado wanamwamini Yesu kwa njia ya “kidini.” Wao huudhuria makanisani na kububujikwa machozi huku wakitubu dhambi zao, wakiomba msamaha. Acheni kufanya hivyo mara moja na muanze kuamini haki ya Mungu na mtapokea tena amani toka kwa Mungu ndani ya mioyo yenu. Yesu alibatizwa na kufa msalabani ili kwamba aweze kutuokoa sote, hivyo natumaini mataiamini Injii hii.
Mungu alitufundisha kwa kupitia Musa juu ya ondoleo la dhambi. Musa alilikubali agizo la Mungu kwa kwenda Misri ili kuwakomboa Waisraeli huku akipanda punda, yeye, mkewe na mtoto wao kuelekia huko. Katika usiku huo, mjumbe wa Munga akamtokea nakutaka kumuua Musa. Ndipo mkewe Sipora, kwa haraka alichukua jiwe lenye makali na moja kwa moja kukata govi la uume wa mtoto wake, na kumtupia miguuni Musa, huku akiseam “hakika wewe u Bwana arusi wa damu kwangu mimi” (Kutoka 4:25).
Ukweli wa kifungu hicho ni kwamba. Hata mtoto wa Musa asingeliweza kuchukuliwa kama sehemu ya watu wa Mungu ikiwa kama asingelipokea tohara, hivyo Mungu ilikuwa amuue. Mungu alisema kwamba, Waisraeli wasinge weza kuhesabiwa kuwa ni watu wake ikiwa kama wasinge tahiriwa. Tohara katika Agano la Kale ilikuwa ni alama ya kujumuishwa katika watu wa Mungu. Mungu alitaka kumfanya Musa aelewe hili. Hivyo mkewe kwa haraka alishika jiwe gumu lenye makali na kuikata govu ya zunga la mwanawe na kuibwaga miguuni pake akisema “Hakika wewe ni bwana arusi wa damu kwangu mimi.” Mungu alitaka kumuua Musa kwa sababu ya mtoto wake asiye tahiriwa.
Hata ikiwa mtu ni wa uzao wa Abrahamu ataondolewa mbali ya Waisraeli ikiwa hatokuwa ametahiriwa. Ni yule aliye tahiriwa tu ndiye atakaye weza kula Pasaka ya mwana kondoo. Kwa mfano huu wale tu walio tahiriwa kiroho ndio watakao shiriki Meza ya Bwana. (Mkate na divai) Wasio na imani hii kamwe hawato weza kuungana na haki ya Mungu na hivyo hawato weza kushiriki utukufu wa Mungu.
Mtume Paulo alikuwa ni Myahudi. Alitahiriwa alipo fikia siku nane baada yakuzaliwa na alilelewa chini ya Gemalieli ambaye alikuwa maarufa sana wakati huo wa Agano la Kale. Hivyo Paulo alielewa fika kwa nini Yesu Kristo alibatizwa katika mto Yordani na ni kwa nini ilimpasa afe msalabani. Hivyo aliweza kuihubiri Injili ya maji na Roho akiwa na uhakika zaidi. Na ndiyo maana alisema “tohara ni ya moyo katika roho” (Warumi 2:29).
Bila shaka Mtume Paulo alizungumzia zaidi mara kwa mara juu ya kifo cha Yesu msalabani kwa nini? Kwa sababu ingawa Yesu alifanya tohara yetu ya rohoni kwa kuzichukua dhambi zetu zote, ikiwa kama asingelitolewa sadaka pale msalabani, kwa maneno mengine, ikiwa asingelipokea hukumu basi tusinge weza kuokolewa. Na ndiyo maana Paulo alizungumzia juu ya msalaba mara kwa mara. Yakupasa uelewe zaidi kwamba msalaba ni hitimisho na mjumuisho wa tohara ya kiroho. Hata hivyo wakristo wengi nyakati hizi hawana hata wazo kidogo juu ya uwiano uliopo kati ya ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani, na hivyo wataangamia jehanamu. Ikiwa nguvu ya imani katika tohara ya kiroho ingeliweza kurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine, basi ukristo wa leo usingeliweza kufikia hatua hii iliyopo.
Baadhi ya watu wanajawa na shukrani pale wanapo kutana na Yesu mara ya kwanza lakini baadaye wanakata tamaaa kutonana na udhaifu wao usio kwisha na hivyo kuishia kuwa watenda dhambi zaidi siku hadi siku. Miaka kumi ya weza kupita baada ya kumwamini Yesu kwa mara ya kwanza lakini wanaishia kuwa watenda dhambi wakuu. Je, wataweza kuwa wenye dhambi baada ya kumwamini Yesu kweli? Huimba tezi zenye maneno kama haya. 
“♪Kulia hakuto nisaidia! ♫Ingawa uso wangu umetapakaa machozi, ambayo bado hayatoweza kuondosha hofu yangu. ♫Hayatoweza kutakasa dhambi za miaka yote. ♫Kulia hakutoweza kuniokoa! ♫Imani katika Kriso ndiyo itakayo niokoa! ♫Hebu basi acha nimwamini Mwokozi aliye niokoa, ♫Niamini kazi aliyoitenda kwa mkono wake, ♫Bwana anisaidie kupiga mbio. ♪Imani katika Kristo ndiyo itakayo niokoa.”
Huimba “Kulia hakuto niokoa. Imani katika Kristo ndiyo itakayo niokoa.” Lakini haya ni maneno tu. Husali huku waki bubujikwa machozi, ila mara wanapo tenda dhambi husema, “Mungu tafadhali unisamehe. Ulikwisha nisamehe,sasa mara hii naahidi nitakuwa mwema toka sasa.” Mkristo anapo tenda dhambi huanza kutubu, akilia na kuomba msamaha na baadaye huisi kuwa vyema. Lakini mtu huu anayerudia jambo hili miaka hadi miaka huanguka na kuwa mwenye dhambi moyoni mwake kuliko mwanzo wakati alipomwamini Yesu miaka kumi iliyo pita. Mtu aina hii huanza kujiuliza kwa hasira “Kwa nini nilimwamini Yesu mapema namna hii? Ningelimwamini pale nifikapo umri wa miaka 80 au punde tu kabla ya pumzi yangu ya mwisho. Nimemwamini mapema sana.” Hii yote ni kwa sababu alipenda kuishi sawa na mapenzi ya Mungu lakini ameshindwa.
Kwa kila dhambi ya mtu, ni lazima iwepo hukumu. Na ndiyo maana Yesu alibatizwa na kuhukumiwa msalabani kwa kumwaga damu yake yenye thamani ili kwamba aweze kutuokoa toka dhambini. Alifufuka tena toka kifoni siku ya tatu. Mungu Baba alimfufua Yesu. Mtu anaye amini tohara ya kiroho ataweza pamoja na uzima kuineza Injili. Tohora ya kiroho ni ushuhuda wa kuwa tumefanyika watoto wa haki ya Mungu. Ubatizo wa Yesu ni ushuhuda wa dhambi zetu kutwikwa juu yake, na damu yake yenye thamani pale msalabani ni ushuhuda pia kwamba alikwisha lipa mshahara wote wa dhambi zetu zote kwa kupokea hukumu kwa niamba yetu.
Je unamwamini Yesu, hali bado ni mwenye dhambi moyoni? Basi hiyo ni imani ya mzushi (Tito 3:10-11) inayo tamka kwamba “mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae ukijua yakuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi maana amejihukumu kuwa hatia yeye mwenyewe.” Wale wenye imani za uzushi ni wenye kujihukumu nafsi zao. Wao husisitiza ya kuwa ni wenye dhambi hata pale wanapo tishwa kwa kifo. Ni wenye mioyo migumu kubadilika katika upotofu wao. Mungu anawaambia wenye dhambi hawa “Ninyi ni wazushi Ni wenye dhambi; si watoto wangu na mtakwenda jehanamu kwenye moto wa milele.”
Wale wenye kumwamini Yesu, huku bado hawajaikubali haki ya Mungu, au ile tohara ya kiroho itokanayo na ubatizo wa Yesu na damu yake, ni Wakristo wazushi na wenye dhambi wakubwa wasio jizuia kusema kwamba wao ni wenye dhambi mbele za Mungu. Wenye dhambi wasio amini haki ya Yesu hawato weza kuingia Ufalme wa Mungu.
Wale waliokwisha kuwa wenye haki baada ya kumwamini Yesu wana ushuhuda wa kuipokea tohara ya kiroho katika mioyo yao. Vifuatavyo ni vithibitisho: Yesu ni Mungu alikuja katika mwili wa mwandamu, alibatizwa na kumwaga damu yake msalabani. Yesu alikuja duniani na kubatizwa na Yohana Mbatizaji ili awezekubeba dhambi za dunia. Alipokea hukumu hiyo msalabani ili kuweka imani bora kwa wale wenye kuamini tohara ya kiroho. Alifufuka kifoni siku ya tatu na kuweza kuwa mwokozi wetu aliye hai. Huu ndiyo wokovu sahihi katika haki ya Mungu ambao hautokani na damu yake tu, bali kwa maji, damu na Roho Mtakatifu. Yote haya ni uthibitisho wa ushuhuda wa tohara ya kiroho wenye kuonyesha wazi wokovu kamili kwetu.
Wapendwa Wakristo, kubali miyoni mwenu kwamba wokuvu haukuwezeshwa kwa damu ya Yesu pekee, bali kwa maji damu, na Roho Mtakatifu. Mungu alikwisha kuondolea mbali dhambi za dunia na kufuta kabaisa hukumu yetu. Si kuondolea mbali dhambi zangu tu bali hata dhambi za duni. Alizibeba zote kwa njia ya ubatizo wake na damu yake. Kwa kupokea tohara ya kiroho kutamsaidia yeyote anaye amini haki ya Mungu ambayo ilikamilishwa na Yesu aliyekuja kwa maji na damu.
Dhambi zote za dunia zimekwisha ondolewa mbali kwa ubatizo wa Yesu kwa Yohana. Sasa wale wote wenye kuamini tohara ya kiroho hawatowezea tena kuwa na dhambi moyoni mwao. Yesu alifufuka tena katika wafu na kuziinua nafsi zetu zilizo kuwa zimekwisha potea kwa dhambi kwa haki yake. Mungu anatutazamia tuwe na Injili ya ubatizo wa Yesu, damu yake na Roho ili tuweze kuokolewa kwa tohara ya kiroho. Tohara hii ya kiroho ni mpango wa Mungu katika Yesu hata kabla ya uumbaji, kwa wale wote waaminio. Hivyo basi ninyi nyote mnaoamini haki ya Mungu nimekwisha kupokea pia tohara ya kiroho.