Search

Kazania

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 5-2] Kwa njia ya Mtu Mmoja (Warumi 5:14)

(Warumi 5:14)
“Walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo ili watawala hata wao wasio fanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja.”
 

Wenye dhambi lazima wawe na ufahamu wa juu ya dhambi zao kwanza.
 
Leo, napenda kuzungumzia juu ya asili ya dhambi. Je, unawaza moyoni huku ukisema, “Ah, huyu naye, kila siku anazungumzia mambo yale yale. Hebu nieleze mambo mengine mapya!” Basi napenda unisikilize kwa makini. Injili ni habari iliyo ya thamani kupitia chochote. Ikiwa mtakatifu ambaye dhambi zake zimefutwa asipo irudia mara kwa mara Injili, ili kujikumbusha kila siku atakufa. Itawezekanaje aweze kuishi pasipo kuisikia Injili ya maji na Roho? Njia pekee ya kuweza kuishi ni kwa kuisikiliza Injili. Hebu basi tufungue Biblia zetu na tushirikishane maana kamili zilizomo ndani yake.
Niliwaza “Ni kipi cha lazima kinachohitajika na mwenye dhambi ambaye haja pokea msamaha bado?” Ndipo ni kaja kuelewa kuwa wanahitaji ufahamu sahihi wa juu ya dhambi zao kulingana na neno la Mungu, kwa kuwa wanaweza kupokea msamaha ikiwa tu pale wanapojua juu dhambi. Naamini kwamba wenye dhambi wanahitaji ufahamu wa juu ya dhambi zao zaidi.
Mwanadamu hutenda dhambi nyingi tokea muda anao zaliwa ukiachilia mbali ikiwa ni kwa utashi au la. Yeye hafikiri juu ya dhambi zilizomo ndani yake ingawa ni mwenye dhambi mbele ya Mungu kwa sababu yeye hutenda dhambi mara nyingi mno kadiri anavyo zidi umri. Kutenda dhambi ni kawaida kama ilivyo mti wa mtufaa kukua kuchanua maua na kubeba tunda lake kwa msimu. Hata hivyo yatulazimu kufahamu kuwa mshara wa dhambi ni mauti kulingana na sheria ya Mungu.
Ikiwa mtu anawaza hivi na kuelewa vyema juu yamatokeo ya dhambi basi mtu huyo ndiye atakayeweza kukombolewa toka dhambini na hukumu ya Mungu hatimaye kupokea baraka za kiroho. Hivyo basi lipi muhimu linao hitajika kufahamu juu ya dhambi na matokeo yake, ni kujifunza ukweli wa ondoleo la dhambi ambalo Mungu ametupatia.
 

Dhambi iliingiaje duniani?
 
Kwa nini mwanadamu ana dhambi? Kwa nini ninatenda dhambi? Bibilia inazungumza juu ya hili katika Warumi 5:12 ikisema, “Kwa hivyo, kama vile dhambi iliingia ulimwenguni, na kifo kupitia dhambi, na hivyo kifo kilienea kwa watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi.” Ni nini kiliingia ulimwenguni kupitia dhambi? kifo. Watu huwa wanadhani kwamba kifo tu kinamaanisha mwili. Walakini, kifo hapa kinaweka maana ya kutengwa kiroho na Mungu. Vile vile inamaanisha kuzimu na hukumu ya Mungu, pamoja na kifo cha mwili. Warumi 5:12 inatuonyesha jinsi wanadamu wakawa wenye dhambi.
Biblia inasema “kwa hiyo kama kwa mtu mmoja dhambi ili ingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamafanya dhambi.” Neno la Mungu ni kweli na amini. Kupitia mtu mmoja dhambi iliingia duniani, na kifo kupitia dhambi.
Tulizaliwa kama uzao wa Adamu. Basi je! Sisi au hatuna dhambi kama uzao wa Adamu? -Ndio, tunayo dhambi. -Je! Tumezaliwa wenye dhambi? -Ndio, kwa sababu sisi ni kizazi cha Adamu, ambaye ni babu yetu.-
Adamu aliwazaa wanadamu wote ingawa, Adamu na hawa walitenda dhambi mbele ya Mungu kwa kwenda kinyume na neno lake chini ya ulaghai wa shetani walipo kuwa katika bustani ya Edeni. Mungu aliwaambia wasile tunda toka mti ule wa kujua mema na mabaya badala yake wawe na uzima wa milele kwa kula tunda toka mti ule wa uzima.
Lakini walidanganywa na shetani na kuyadharau maneno ya Mungu kwa kula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Adamu na hawa walitenda dhambi kwa kuyadharau maneno ya Mungu ambayo ni maneno ya uzima wa milele. Baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi akaja kukutana na Hawa kwa tendo la kimwili na ndipo wanadamu wote wakatokea kuzaliwa kizazi toka kizazi kupitia kwao. Sisi ni uzao wao. Hata kurithi maumbile yao tu, bali hata asili yao ya dhambi. 
Kwa hiyo, Biblia inasema kwamba wanadamu ni mbegu ya dhambi. Watu wote duniani tumerithi dhambi toka kwa Adamu na Hawa Biblia yatueleza kuwa “kwa hiyo, kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwengu na kwa dhambi hiyo mauti, na hivyo mauti ikwawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi.” Hivyo basi wanadamu wote wamezaliwa wakiwa na wingi wa dhambi.
Hata hivyo, watu hawajui kuwa wamezaliwa wakiwa na wingi wa dhambi ndani yao. Hawana ufahamu wa juu ya dhambi ingawa wamezaliwa wakiwa na wingi wa dhambi. Mti huanza kutoa tunda kutokana na mbegu kuota na hatimaye baada ya kunyauka kwa ua lake na ndipo tunda hutokea, lakini watu hudhani kuwa ni ajabu kutenda dhambi kwa sababu hawajui kwamba wao wamezaliwa wakiwa ni mbegu ya dhambi. Ndivyo ilivyo kwa kanuni ya tunda la tufaa amabalo laweza kuuliza “inanistaajabisha kwa jinsi gani imenipasa kuzaa tunda la mtufaa?”
Kwa jinsi hii, ni asili na ni kawaidia kwa mwanadamu kuwa mwenye dhambi. Wazo la mwanadamu kuweza kujizuia kutenda dhambi ni uongo mkubwa. Ni asili kwa mwana damu aliye rithi dhambi kuzaa matunda ya dhambi, lakini huku akishindwa kuelewa kuwa yeye ni mwingi wa dhambi. Sasa basi, Mungu anasema nini? “Kwa hiyo, kama kwa mtu dhambi iliingia ulimwengu na kwa dhambi hiyo mauti, ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi.”
Tunatenda dhambi maishani mwetu mwote kwa kuwa tunazaliwa tukiwa wenye dhambi, kwa hiyo basi tunastahili kupata hukumu ya Mungu. Unaweza kudhani “hii si haki kwa Mungu kutuhukumu sisi hali kama hatuna uchaguzi bali ni kutenda dhambi.” Hata hivyo baada ya kupokea ondoleo la dhambi utakuja kuelewa mpangao wa Mungu kwa nini alifanya hivyo ili aweza kutufanya kuwa watoto wake.
 

Sisi ni uzao wa mtu mmoja, Adamu.
 
Kwa maana hiyo basi inakuaje wanadamu walio uzao wa mtu mmoja Adamu, wawe na aina za rangi ya ngozi tofatuti tofauti baina yao? Je, mbegu zao si tofauti? Kwa nini wawepo weupe, weusi na udhurungi? Baadhi hudhani kwamba Mungu alipomuumba mwanadamu kutokana na mavumbi ya ardhini na kuwa choma, baadhi aliwafanya wawe weupe kwa kuwa toa mapema katika tanuru, waliokuwa udharungi aliwatoa muda ulio mwafaka, na weusi alichelewa kuwatoa.
Unaweza pia kushanga kwa nini kuna watu weusi, weupe na udharungi ingawa wanadamu hawa walirithi dhambi kutoka mwanadamu mmoja. Biblia ina tamka wazi kwamba Mungu alimuumba Adamu mwazo, wakati alipo umba mbingu na dunia. “Adamu” maana yake mtu. Mungu alimuumba mtu. Kwanini kuna kabila mbalimbali tofauti duniani ikiwa kama Mungu alimuumba mtu, Adamu na kwa jinsi hiyo watu wote dunianai walizaliwa kupitia yeye? Tunaweza kuuliza kwa nini. Hivyo jibu ni kama ifuatavyo.
Wanasayansi husema kwamba vimelea vya rangi (pigment) katika ngozi viitwavyo melanini (melanin) hutoka nje ya ngozi ili kuikinga na miale ya jua. Dunia inapolizunguka jua katika njia yake (orbiti) wale wanao ishi katika ukanda wa jua kali hugeuka rangi na kuwa weusi, wale wenye kuishi katika ukanda wenye jua hafifu huwa weupe na wale wenye kuishi ukanda wenye jua la kiasi huwa na rangi za ngozi ya udhurungi. Hata hivyo mzazi wetu wa kwanza bado ni yule mtu mmoja, Adamu.
Wanasayansi walivyo tamka juu ya melanini kutokeza nje ya ngoazi na kuikinga kwa miale ya jua, nilikuwa naelewa tayari kwamba wanadamu ni uzao wa Adamu lakini sikua najua juu ya melanini. Hatukurithi mwili tu bali pia dhambi kwa sababu sisi ni uzao wa mtu mmoja, Adamu.
Je, unafahamu dhambi? Hebu futanye uchunguazi ikiwa wanadamu ni wenye dhambi au la, toka walipo zaliwa dunian.i “Vivyo hiyvo kila mti mwema huzaa matunda mazuri, na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri” (Mathayo 7:17-18). Mungu anasema kwamba manabii waongo huzaa matunda ya uongo na kamwe hawawezi kuzaa matunda mema. Sisi ni miti ya uovu kwa asili kwa sababu tumezaliwa tukiwa na dhambi, hivyo hatuwezi kujizuia kuzaa matunda ya uovu kwa sababu tumezaliwa kutokana na miti ya uovu.
Tumerithi dhambi kupita mtu mmoja. Sisi ni miti iliyo miovu ukitulinganisha na miti. Mwanadamu aliye zaliwa akiwa mwenye dhambi hawezi kujizuia kutenda dhambi hata ikiwa anataka kuishi kwa udilifu huku akijaribu kutotenda dhambi, kama ilivyo kwa mti wa uovu usio weza kuzaa tunda jema. Je, unaelewa hili? Wanadamu kwa hakika hutaka kuishi kwa upole, unyenyekevu na kw auadilifu. Hata hivyo, mtu asiye na ondoleo la dhambi na alizaliwa akiwa mwenye dhambi kamwe hawezi kuishi kwa haki. Hawezi kuwa mtu mzuri, hata kwa juhudi zisizo kikomo. Baadhi ya walevi hujaribu kuacha kunywa pombe, lakini hatimaye huiishia kupata madhara ya ulevi na hata kutengwa na jamii na kuacha mahospitalini kwa kushindwa kwao.
Siku moja, nilikua nikitazama kipindi katika runinga kiitwacho “Napenda kujua juu ya hili.” Mtu funalni alikuwa amelazwa hospitalini kwa miaka 13. Mtoa habari alipo muuliza juu ya familia yake, alisema kwamba hawakurudi kuja kumchukua aende nyumbani ingawa alikuwa tayari amekwisha kupona kwa ugonjwa wa ulevi, na hata daktari wake alithibitisha kupona kwake. Mgonjwa huyo wa ulevi hatimaye akaja kuelewa toka kwa yule mtoa habari kwamba familia yake ilimzuia asirudi nyumbani kwa kutoa hongo kwa daktari. Akachukia sana. Familia yake ilikwisha mchoka. Mtoa habari yule alisema kwamba wagonjwa katika hospitali wasingeweza kujizuia kutokunywa kwa mapenzi yao na hivyo kuwa walevi wa kupindukia mara nyingi hata kufikia kushindwa kuvumilika na yeyote.
Kwa nini Mtu asiweze kujizuia ulevi? Yeye anaelewa kuwa si vyema kwa afya yake na kujaribu kuacha, lakini hurudi na kuanza tena. Sababu ya hili ni kuwa yeye tayari ni mlevi, lakini sababu ya asili kwa hili ni kwa kuwa akili yake ni tupu. Hunywa na kuwa mlevi kwa sababu ndani ya moyo wake kuna utupu. Mtu wakatia wote huhisi maumivu na hawezi kuwa mwema kwa sababu ana dhambi moyoni. Hivyo anabaki kutaharuki na kuanza kurudi kuwa mlevi tena. Aweze kufikiri “Sijui kwa nini na ishia kufanya hivi, sikupasa kufanya haya” Kadiri anavyo hisi kupotoshwa na nafsi yake, ndiyvo kadiri anavyo zaidi kuwa mlevi zaidi hata kujitelekeza nafsi yake.
Mtu hawezi kuacha ulevi hata ikiwa atajaribu kuto kunywa kabisa. Hivyo, hisia zake humpotosha na kuendelea kunywa zaidi na hatimaye kuishia kutelekezwa hospitalini. Kauli na tabia za mwanadamu ni taswira ya uhalisi wa asili yake. Mwanadamu amezaliwa akiwa mwenye dhambi hivyo hawezi kujizuia kutenda dhambi, bila kujali hiyari yake au la kwa maisha yake yote kama ilivyo tunda la tufaa, kutoa ua na hatimaye tunda la tufaa kwa sababau limerithi mbegu za kizazi (gene) za tufaa. Watu hutamani kuwa wema lakini wale wanao taka kuwa hivyo pasipo ondoleo la dhambi hawatoweza, kwa sababu hawana uwezo ndani yao wa kuwa wema. Hudhani kuwa dhambi zao si kubwa sana, hivyo hujificha, na hatimaye hutokeza na kuwa tatizo kubwa zaidi pale zinapo fichuka.
Inakuwa ni asili, tabia na ni sawa kwa mwenye dhambi kutenda dhambi kwa sababu ya kuzaliwa akiwa na wingi wa dhambi na kurithi asili yake. Ni kawaidia kwa mwanadamu kutenda dhambi kwa sababau amezaliwa na asili ya maumbile ya dhambi, kama jinsi ilivyo hata kwa mmea wa pilipili nyekundu kuzaa pilipili na kwa mmea wa jujube kuzaa mjujube. Mtu kamwe hawezi kujizuia kutotenda dhambi kwa kuwa amezaliwa akiwa mwenye dhambi. Mwanadamu atawezaje kuishi pasipo kutenda dhambi hali amezaliwa akiwa na dhambi?
 

Mtu amezaliwa akiwa na aina kumi na mbili ya fikra zao uovu.
 
Yesu alisema katika Marko sura ya 7 kwamba, mwana damu amezaliwa akiwa na aina 12 ya fikra za uovu ndani yake. Nazo ni uzinzi, uasherati, uuaji, wizi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho matukano, kiburi, na upumbavu. Fikra za wizi zimo ndani ya dhambi ya urithi. Je, unaiba? Kila mtu huiba. Ikiwa mtu haibi, ni kwa kuwa wapo watu wanao muona. Hata hivyo, pasipokuwepo mtu pembeni yake na kuna kitu cha kutamanisha karibu, dhambi ya wizi hujitokeza na kuleta ushawishi wa kuitenda.
Hivyo wanadamu waliweka maadili na kanuni ili zifuatwe. Wanadamu wanafanya sheia zao zenye kuonyesha kwamba si vyema kuwadhuru wengine. Sheria huitajika ikiwa pale watu huishi wengi kwa pamoja katika jamii. Yatupasa kuishi kwa vigezo vya maadili ya jamii. Hata hivyo tunaiba pale tunapo kuwa wenyewe huku tukikwepa macho ya wengine.
Ni nani asiye iba. Kila mtu huiba. Hapo kale niliwahi kuuliza mbele ya usharika katika mojawapo ya mikutano ya uamsho, watu wanyoshe mikono juu kama hakuna ambaye hajawahi kuiba maishani. Mwanamke mmoja mkongwe alinyanyua mkono wake na kusema, “sijawahi kuiba chochote”. Hivyo nikamuuliza ikiwa hakuwahi kuchukua chochote akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake. Ndipo akabaki akishangaa kwa swali ambalo hakutarajia na kujibu “siku moja niliona boga changa nilipokuwa naelekea yumbani, nikawaza kuwa lingeweza kuwa tamu sana, hivyo nikatazama pembeni na sikuona yeyote. Nilichuma boga hilo na kulificha ndani ya gagulo langu na baadaye nilipo lifikisha kwangu nikalikata vipande na kuliweka katika sufuria ya mbonga na kulipika hatimaye nikala.” Yeye hakufahamu kuwa alikuwa tayari amekwisha tenda dhambi ya wizi.
Hata hivyo Mungu anasema, dhambi ni kuchukua mali ya mwenzako pasipo ruksa yake. Mungu alitoa amri “Usiibe” katika sheria ya Mungu. Kila mtu amekwisha kuumbwa na tabia ya wizi wa mali. Mwanadamu ni mwepesi kuua na kuiba kila anapo pata mwanya. Huiba mifugo, mfano sungura na kuku toka kwa wengine. Hii ndiyo tabia ya wizi. Mwizi hana dhamira ya kutambua kuwa ni dhambi ingawa hupotoka na kuiba. Ni kawaida kufanya hivyo kwa sababu amerithi toka siku aliyo tungwa mimba hata kuzaliwa.
 

Mwanadamu amerithi dhambi.
 
Mwanadamu amerithi zambi ya uasherati toka kwa wazazi wake wa kwanza. Amezaliwa akiwa na tamaa ya kimwili katika kutenda uasherati. Ni rahisi kutenda uasherati pale inapokuwa hakuna watu wanao mzunguka. Watu hupenda sehemu kama vile migahawani na sehemu za kutengenezea nywele. Sehemu hizi ni maarufu kwa wenye dhambi. Kwa nini? Ni mahala rahisi kuonyesha urithi wa dhambi.
Hata wanaume hupenda sehemu kama hizi. Wao huwa ni baba wema wakiwa majumbani mwao na wanaume wenye hadhi. Lakini huenda sehemu za maficho zenye dhambi nyingi. Huenda sehemu ambako wanauhuru wa kuonyesha asili ya dhambi zao na hatimaye kugeuka kuwa tunda la adhambi. Hukutana, pamoja na punde hugeuka na kuwa kama marafiki wa kale hasa baada ya kunywa chupa kadhaa za pombe. Hujikuta kuwa karibu sana kimaongezi punde wanapo kuwa karibu wakinywa kwa kuwa wana asili moja ya tabia na hulka ya dhambi, “Je, wewe una hili pia?” “Ndiyo nina hili.” “Hata mimi pia. Basi wewe ni rafiki yangu. Una umri gani” “Ah umri haumati” “Nashukuru kukufahamu” Hayo ndiyo mfano wa mazungumzo yao.
Wanaume huonyeshana asili ya dhambi za urithi kila wanapo kutana kwa sababau wamezaliwa wakiwa na hulka ya dhambi duniani. Ni kawaida kwao kutenda dhambi. Kwa nini? Kwa sababu wana dhambi mioyoni mwao na wameumbwa kuwa namna hiyo kwa asili. Ni jambo la ajabu kwao kutotenda dhambi, ingawa hujizui kutoishi maisha ya dhambi wanapo ishi na jamii kwa sababau kila jamii ina maadili yake. Hivyo wanafanya mchezo wa kuwa wanafiki na kuvaa sura ya uungwana huku wakitenda kulingana na maadili ya jamii yaliyo wekwa. Watu hupenda namna hii na huwachukulia wengine kama wajinga na waovu kwao. Mwadamu hana jinsi zaidi ya kuzaliwa akiwa mwenye dhambi kama kama isemavyo Biblia “kwa mtu mmoja dhami iliingia ulimwenguni” (Warumi 5:12).
Ni kweli, Mtu anaweza kusema “Mimi sina tamaa mbaya sipendi wanawake kuvaa mavazi mafupi”. Je, mtu huyu kweli hapendi? Anaweza kuwa anajifanya hapendi pale anapozungukwa na watu wengi, lakini hawezi kwa undani kujizuia kutenda dhambi ya tamaa mbaya anapo kuwa peke yake.
Mti mbaya huzaa tunda la uovu kama ili vyo kwa mti mwema kutozaa tunda la uovu na kinyume chake. Mwanadamu imempasa kuelewa kwamba yeye ni mwenye dhambi. Ikiwa mtu anaelewa juu ya dhambi zake, basi ataweza kuokolewa kupitia Yesu. Hata hivyo ataweza kuhukumiwa na Mungu na hatimaye jehanamu ikiwa atajifanya kuwa hatendi dhambi. Wanadamu wamezaliwa wakiwa na dhambi. Kwa hiyo ni miti iliyo mibaya yenye kuzaa matunda ya uovu toka ilipo zaliwa.
Kwa hiyo, wale wenye kujitokeza asili zao za dhambi tokea utotoni ni wepesi kuendelea nazo maishani. Wale wenye kuchelewa kujionyesha huanza kuzaa matunda ya uovu wakati wa umri wao uzeeni. Palitokea mhudumu wa kiroho mwanamke katika mji wa Taegu, Korea. Alipo gueuka na kuwa mkristo wakati wa ujana wake, aliweka nadhiri ya kubaki bila ya kuolewa maishani ili kwamba amtumikie Bwana akiwa mwanamke aliye mhudumu wa kiroho. Hata hivyo aliivunja nadhiri hiyo na kuolewa na mwanaume aliye fiwa na mke baada ya kufikia umri wa miaka 60, alionyesha asili ya dhambi yake mapema mno. Alionyesha dhambi ya uzinzi mapema sana.
Watu wengi mara nyingi hujionyesha asili zao toka utotoni. Nyakati hizi, vijana hujionyesha asili zao tokea utotoni. Hujihisi kuna pengo la kizazi kati yao na kizazi cha wazee wao. Husemekana wao ndio kizazi kiitwacho X. Hivyo kwa njia hii tumegundua toka neno la Mungu kwamba tumezaliwa tukiwa na wingi wa dhambi na ni viumbe tusioweza kujizuia kutenda dhambi maishani pote, Je, una kubaliana na hili?
 

Sheria ya ukoma.
 
Pili, Mungu anasema “kwa hiyo kama kwa mtu dhambi iliingia ulimwengu na kwa dhambi hiyo mauti, na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi” (Warumi 5:12). Dhambi imemsababishia mwanadamu kuhukumiwa na Mungu, hivyo mwenye dhambi yampasa kujielewa nafsi yake ili awe na ondoleo la dhambi. Atawezaje kujielewa? Itawezekanaje kwa dhambi zake zote kusamehewa?
Mungu alimfundisha Musa na Haruni namba ya kuchunguza ukoma katika Walawi sura ya 13. Katika Agano la Kale nyakati zake, palikuwemo wakoma wengi. Sijui mengi kuhusianana na ugonjwa wa ukoma, lakini nimekwisha ona vilema wengi nilipo kuwa kijana. Mmoja wa rafiki zangu naye pia aliwahi kuathirika na ukoma.
Mungu alimwambia Mungu na Haruni kuwachunguza wakoma na kuwatenga toka hemani pa Israeli. Mungu aliwafundisha namna ya kuwachunguza. “Mtu atakapo kuwa na kivimbe katika ngozi ya mwili wake, au kikoko, au kipaku king’aacho nalo likawa pigo la ukoma katika ngozi ya mwili wake ndipo atakapoletwa kwa Haruni kuhani, au kwa wanawe, makuhani mmoja wapo” (Walawi 13:2). Kuhani alipoona ana ugonjwa wa ngozi baada ya kumchunguza naye humtenga mtu huyo siku saba, Ndipo tena kuchunguza ngozi yake baada ya siku saba. Ikiwa uvimbe hauta sambaa kwenye ngozi ndipo atakapo tamka kuwa mtu huyo ni safi akisema “usafi na waweza kuishi katika hema.”
Ikiwa uvimbe katika ngozi utakuwa mweupe, na kufanya nywele kuwa nyeupe, na kuonekana nyama katika uvimbe, basi huo uli kuwa ni ukoma ndipo hapo Kuhani atakapo tamka kuwa ni najisi. “Pigo la ukoma litakapokuwa katika mtu, ndipo ataletwa kwa Kuhani naye ataangalia, na tazama ikiwa pana kivimbe cheupe katika ngozi yake, na malaika yamegeuzwa kuwa meupe tena ikiwa pana nyama mbichi iliyomea katika kile kivimbe ni ukoma wa zamani ulio katika ngozi ya mwili wake na kuhani atasema kuwa yu najisi, hatamweka mahali kwa kuwa yeye yuna unajisi” (Walawi 13:9-11). Kuhani alimtenga na hema ya Israeli.
Mfano huu unafanana katika nchi yetu. Vipo vijiji vilivyotengwa katika Korea mfano kijiji cha Maua au kisiwa cha Sorok. Siku moja nilipokuwa na rudi nyumbani nikiendesha gari langu mke wangu aliniambia niangalie kando ya barabara akinitania “tazama kijiji cha Maua” alipoona kibao cha tangazo pembezoni mwa barabara kuu. Ndipo nilipowaza “hujui nini maana ya jina hili la Maua” nikamwambia “Mpenzi je, unataka kutembea katika mji huu?” Akajibu kwa shauku “Ndiyo!” Ingawa alikuwa akishangaa kusikia jina “kijiji cha Maua” ambapo palikuwa ni mahali ambamo wakoma huishi. Baadaye na tokea hapo aliacha moja kwa moja kutania juu ya kijiji hicho cha Maua. Watu wenye ukoma walitengwa katika kijiji hicho mbali na jamii.
Hapa kuna swala tunalo paswa kuwa makini, nalo ni lile la kuhani kutamka juu ya mtu fulani kuwa ni safi hali ukoma umesambaa na kufunika ngozi yake yote. Je, unadhani hili ni jambo la busara? Kuhani alimtenga mtu pale ukoma ulipo sambaa kwa kiasi kidogo tu, na alimwambia aondoke katika hema pale ugonjwa huo ulipo sambaa katika ngozi, toka kichwa hata vidole.
Mungu alimwelekeza Kuhani namna ya kuainisha ukoma “Tena kwamba huo ukoma ukitokea katika ngozi yake, na ukoma ukamwenea ngozi yote, tangu kichwa hata miguu kama aonavyo kuahani” (Walawi 13:12) hivi ndiyvo ilivyo kuwa njia ambayo Mungu alimwelekeza Kuhani namna ya kuainisha ukoma.
 

Sheria ya ukoma inatuaelezaje....
 
Inatueleza hivi, watu huzaliwa wakiwa wenye dhambi ndani yake na tabia au hulka za dhambi maishani mwao mwote, lakini baadhi ya watu hudhihirisha dhambi chache tu. Hutenda dhambi kwa mikono yao mara moja na kwa miguu yao hufuata na kwa akili zao wakati mwingine baada ya muda wa kipindi kirefu. Hivyo basi kwa utu wa nje hushindwa kung’amua dhambi zao. Ni nani angeweza kutamka wazi pale ukoma unapo jitokeza kwa doa au baka moja hapoa na pale kwa uchache? Hakuna ajuaye dalili za ukoma.
Mwanadamu amezaliwa akiwa na dhambi ya kurithi lakini yeye binafsi hafahamu kuwa ni mwenye dhambi hadi pale atakapo tenda dhambi zisiozo na idadi ingawa Mungu alikwisha kumtamkia kuwa ni mwenye dhambi, hatimaye hujua yeye ni mwenye dhambi duniani.
Ni nani awezaye kuingia Ufalme wa Mbinguni? Ni wale tu ambao dhambi imetapakaa mwilini pote na kugundua kwamba wao ni wenye dhambi pasipo hiyari au kujizuia ndio watakao ingia Ufalme wa Mbinguni. Dhambi zao zote zimesamehewa kwa kumwambini Yesu, na wataingia katika Ufalme wa Mungu na kutawala na Mungu.
Biblia inasema kwamba, Mungu hutamka mtu mwenye dhambi zilizo chache kuwa ni najisi. Mungu humwita mtu mwenye kurudia kutenda dhambi, ingawa hana dhamira na kukiri kuwa yeye ni mwenye dahambi kwa jumla. Yesu alisemea “Kwa maana sikuja kuwaita wenye haki bali wenye dhambi” (Mathayo 9:13). Mungu huwaita wenye dhambi na kuwasafisha dhambi zao zote. Mungu alikwisha wasamehe dhambi zao zote. Mungu tayari amekwisha safisha dhambi zao mara moja na kwa wakati wote. Yesu alibeba dhambi zao zote kupitia ubatizo wake, na alihukumiwa msalabani kwa ajili yao na kuwafanya wawe wenye haki kupitia ufufuko wake na hatimaye atawachukua kwenda katika Ufalme wa Mungu.
 

Yutupasa kujielewa nafsi zetu.
 
Yatupasa kuelewa ikiwa sisi ni wenye dhambi kwa jumla au kwa kiasi. Mungu anatamka mtu kuwa najisi pake ukoma unapo sambaa katika ngozi yote mwilini. Mungu aliweka sheria ya ukoma kama hivi. Mtu anaye fahamu kwamba yeye amejaa dhambi hana la zaidi ya kuamini Injili ya maji na Roho na kupokea ondoleo la dhambi pale Yesu anapokuja kwake akisema kwamba, yeye tayari amekwisha takasa dhambi zake zote kupitia ubatizo na msalaba. Hata hivyo anaye dhani kuwa anadhambi kiasi hudhihaki Injili.
Je, ikiwa Yesu tayari amekwisha takasa dhambi zote, patakuwepo tena na dhambi? Hapana, twaweza kupokea ondoleo la dhambi mara moja na kwa wakati wote. Hivyo, mwenye dhambi imempasa kujielewa nafsini. Watu wanapendelea zaidi kuleta mbele za Mungu dhambi zao chache tu, huku wakisema “Bwana nimetenda dhambi si kwa hiyari, bali ni kwa sababu ya huyu, tafadhali nisamehe kwa hili na sintorudia kutenda dhambi tena” Ndiyo waletavyo dhambi chache mbele ya Mungu. Ndipo Mungu humjibu mtu kama huyu “Wewe ni najisi tu.”
Mwanadamu hana haki mbele ya Mungu. Waweza kusema, “Mungu vile nitakavyo kuwa au kutokuwa kunategemea wewe. Mimi ni mwenye dhambi na hatima yangu ni jehanamu. Tafadhali fanya utakavyo, lakini Mungu unirehemu na uniokoe. Tafadhali ikiwa wewe ndiwe Mungu kwangu uniokoe, ndipo nitakapo kuamini na nitaishi kwa kufuata mapenzi yako.” Mungu humwokoa mtu anaye kiri kwamba yeye ni mwingi wa dhambi.
 

Mwanadamu hurithi dhambi aina 12 zenye mawazo ya uovu.
 
Hebu tuangalie katika Marko 7:20-23 “Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya usherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.” Ndani ya moyo wa mwanadamu hutoka mawazo ya uovu. Mwanadamu hurithi dhambi kwa asili. Je, unaelewa? Mtu ana mawazo ya uovu kwa maisha yake yote. Hakuna namna kwa mtu kukombolewa dhambi zake zote ikiwa hatosamehewa dhambi hizo mara moja.
Mwanadamu huzaliwa akiwa na dhambi hizi aina 12 katika mawazo yake. Uasherati, uzinzi, uuaji, wizi, tamaa mbaya ulafi, ukorofi na ufisadi, Hivyo hawezi kujizuia kutotenda dhambi maishani pote. Yule ambaye dhambi zake hazijasamehewa huishi akiwa mwenye dhambi ingawa hana hiyari. Vitu vyote katika mwanadamu kama vile mawazo na tabia ni dhambi mbele ya Mungu.
Ni unafiki kwa mwenye dhambi kuwa mwema. Anachofanya ni kujikosha kwa kuwa mstaarabu. Ni sawa na kumdanganya Mungu. Mwanadamu aliyezaliwa akiwa na dhambi yampasa kujielewa nafsi yake ili aweze kuokolewa. Hata hivyo ikiwa mtu hatojielewa kuwa ni mwenye dhambi basi mara kadha atajisikia hovyo na kukata tamaa pale anapo anguka dhambini, na hivyo kusema “Ah! kwa nini ninafanya hivi?” Hudanganywa na nafsi yake.
Mwanadamu ana mawazo ya uovu. Mtu anaweza kuwaza “Kwani ni nina mawazo ya uovu hivi? Hapana, imenipasa kuwaza hivi kwa nini ninawaza unajisi? Mwalimu wangu aliniambia niwe mwadilifu. Hufikiri hivi kwa sababu hajui kwa nini hufanya mambo fulani. Huhisi kuchoka na kuchanganyikiwa kwa sababu ya dhambi azitendazo za wizi na uzinzi kwa kutofahamu kuwa amerithi uuwaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kiburi, upumbavu, matukano, kijicho, mawazo mabaya na uuaji hutoka ndani yake pasipo kikomo. Hivyo hujikasirikia na hatimaye kuona haya pasipo kujua ni kwa sababu gani.
Sisi ni wenye wingi wa dhambi na kuwa na aina 12 ya matunda ya uovu maishani mwetu pote kwa sababau tumezaliwa tukiwa na dhambi tulizo rithi toka kwa Adamu. Heri yao wale wenye kufahamu kuwa wao ni wenye dhambi.
Mwanadamu humtafuta Yesu, Mwokozi amwokaoye kwa dhambi zake zote, pale anapotambua kuwa yeye ni mwenye dhambi asiye na cha kutegemea. Ndiyo njia pekee ya kubarikiwa na Mungu. Hata hivyo mwanadamu hawezi kumtafuta Mwokozi ikiwa bado hajafahamu nafsi yake vile ilivyo. Mtu mwenye kufahamu nafsi yake vile ilivyo kufikia kujikana akiacha juhudi zake, kuacha kutegemea wanadamu. Humtafuta Yesu Kristo ambaye ni Mungu, Mwokozi na Mtume hatimaye kusamehewa kwa rehama za Yesu Kristo.
Wenye dhambi imewapasa kujua nafsi zao kwa sababu wale wenye kujitambua wataweza kubarikiwa mbele ya Mungu, na yule asiye jitambua kamwe hawezi kubariwa. Je unaelewa? Je, umekwisha wahi kutenda uovu kabla ya kupokea ondoleo la dhambi? Ikiwa ndiyvo, je, unajua ni kwa nini? Ulitenda hivyo kwa sababau si hiyari yako, bali ni kwasababu ya kurithi dhambi kwako.
 

Kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni na kwa dhambi hiyo mauti.
 
Kifo hakizuiliki kwa wanadamu kwa sababu wanadhambi. Mwanadamu imempasa kumtafuta Yesu na kukutana naye ili aweze kukombolewa tokana na dhambi zake ili zifutwe. Ndipo ataweza kuwa na uzima wa milele. Je, ungependa kukombolewa toka dhambini?
“Walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Mungu naye iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu aliye mfano wake yeye atakaye kuja. Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa. Kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi, wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyefanya dhambi si kadiri ya kile kipawa kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu, bali karama ya neema ilikuja kwa ajili ya makosa mengi ikaleta kuhesabiwa haki, kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana uzima kwa yule mmoja Yesu Kristo. Basi tena kama kwa kukosa mmoja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima. Kwa sababau kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki. Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana, na dhambi ilipo zaidi neema ilikuwa nyingi zaidi, ili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu” (Warumi 5:14-21).
“Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni na kwa dhambi hiyo mauti, na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababau wote wamefanya dahmbi” (Warumi 5:12). Hapa neno “mtu” ni nani? Ni Adamu. Hawa naye alitokana na mtu, Adamu. Hivyo Biblia inasema “kwa mtu mmoja.” Mungu alimuumba mtu mmoja hapo mwanzo na kwa kupitia mtu mmoja dhambi iliingia duniani. Palikuwepo na watu wawili katika bustani ya Edeni kwa mtazamo wetu, lakini ukweli mbele ya Mungu palikuwepo mtu mmoja. Jamii zote za wanadamu zimetokana na mtu mmoja, Adamu.
Maneno yasemayo “kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni” yana maana ya uzao wa Adamu uligeuka na kuwa na dhambi kwa sababu ya Adamu mwenyewe. Mauti ilipita kwa wanadamu wote kwa sababu wote wametenda dhambi. Mauti ni hukumu ya wanadamu wote kwa sababu ya dhambi. Mungu kamwe hatoweza kumvumilia mtu mwenye dhambi.
Mungu ni mweza wa yote lakini hawezi kufanya mambo mawili, hawezi kusema uongo au hata kumwacha mtu mwenye dhambi kuingia Ufalme wa Mbinguni. Yeye hutekeleza sheria zake kama alivyo ahidi. Bila shaka yeye humhukumu mtu mwenye dhambi kwa sababu Mungu hawezi kusema uongo au kuidharau sheria yake mwenyewe aliyo iweka. Wanadamu wote wamekuwa ni wenye dhambi kupitia mtu mmoja, Adamu, aliyeanguaka na kutenda dhambi mbele ya Mungu. Hukumu ya Mungu na mauti yalisambaa kwa wote wanadamu kwa sababu walifanywa kuwa wenye dhambi na kuzaliwa wakiwa ni uzao wa mtu mmoja, Adamu. Mauti ilikuja kusambaa kwa wote namna hiyo.
Mungu alipo muumba mtu hapo mwanzo hapakuwepo mauti. Hapakuwepo na mti wa ujuzi wa mema na mabaya tu bali pia mti wa uzima. Mungu alimwamuru Adamu kula tunda toka mti wa uzima wa milele. Hata hivyo Adamu alidanganywa na shetani na hatimaye kula tunda toka mti wa ujuzi wa mema na mabaya, ambao Mungu alimwamru kuto kula na hatimaye kumkaidi Mungu kwa kuliacha neno lake, hivyo mauti ikaweza kuenea kwa watu wote duniani. Kutokana na dhambi hiyo Mauti iliingia duniani kupitia mtu mmoja, Adamu.
 

Kwa nini Mungu alimpa mtu sheria?
 
Ikiwa dhambi isinge ingia duniani kupitia Adamu mauti isingeweza kuenea kwa wanadamu. Kwa nini mwanadamu afe? Wnadamu hufa kwa sababu ya dhambi. Dhambi iliingia duniani kupitia mtu mmoja, na hivyo dhambi ikaenea kwa watu wote. Kabla ya sheria kuja, dhambi ilikwisha kuwepo duniani, lakini wanadamu hawakujua juu ya dhambi mpaka pale ilipo wekwa.
Sheria ya Mungu ililetwa kwa watu wote kupitia Musa. Hata wakati wa Adamu na Nuhu palikuwepo dhambi, lakini Mungu hakuwa amekwisha weka sheria, hadi pale kipindi cha Musa. Hata hivyo Biblia inasema palikuwepo dhambi katika mioyo ya watu wote walio ishi wakati huo.
Hebu tuangalie katika Warumi 5:13 “Maana kabla ya sheria dhambi ilikuwemo ulimwenguni lakini dhambi haihesabiwi isipokuwa sheria.” Palikuwemo dhambi wakati hapakuwemo sheria duniani. Hivyo watu wote iliwapasa kufa kwa kuwa wametenda dhambi mbele ya Mungu. Mungu iliwapa sheria iliyo jumuisha aina 613 za vipengele vya sheria, ambavyo vilipaswa kufuatwa mbele zake na watu ili kwamba waweze kuelewa juu ya dhambi. Watu walikuja kuelewa nini kupitia sheria ya Mungu? Walijua ya kwamba wao walikuwa na wingi wa dhambi mbele zake na hivyo kujua makosa yao. Watu waligundua kwamba wasingeweza kamwe kuifuata sheria ya Mungu.
Hivyo huja kuelewa dhambi zao. Uzao wa Adamu na Hawa ulifahamu kuwa ni wenye dhambi na hivyo Mungu ndiye pekee atakaye wasamehe dhambi zao. Lakini walisahau, kadiri muda ulivyo kwenda kwamba wao ni wenye dhambi na walikuwa wamerithi dhambi kutoka kwa wazazi, kabla ya kipindi hicho walielewa kuwa wao ni wenye dhambi pale walipo tenda dhambi, lakini hawakujua kuwa ni wenye asili ya dhambi pale ambapo hawakutenda dhambi. Lakini walikuwa si sahihi. Nyakati hizi, watu wengi bado hudhani kwamba wao huwa ni wenye dhambi ikiwa kama watatenda dhambi, na kwa upande mwingine si wenye dhambi ikiwa hawato tenda dhambi. Ukweli ni kuwa watu wote ni wenye dhambi haijalishi labda hutenda dhambi au la, kwa kuwa walikwisha rithi dhambi toka tumboni hata kuzaliwa.
Wanadamu ni wenye dhambi bila hiyari kabla ya kukombolewa toka dhambini. Hivyo Mungu amewapa sheria yake ili wafahamu hali yao ya dhambi miyoni mwao. Mtu anaye mjua Mungu kupitia sheria na hukiri sheria ambayo inaonyesha kuwa yeye ni mwenye dhambi. Mwanadamu hugeuka na kuwa mwenye dhambi zaidi hasa baada ya kuijua sheria ya Mungu.
 

Kifo kilienea kwa watu wote kuipitia mtu mmoja.
 
Warumi 5:13-14 inatamka “Maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwengu, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwa sheria, walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata woa wasiofanya dhambi, ifananayo na kosa la Adamu aliye mfano wake yeye atakayekuja.”
Mungu anasema kwamba watu wote wanakua wenye dhambi kwa kupita mtu mmoja na kifo kuenea kwa kupita mtu huyo mmoja. Kifo kilienea kwao wote kupita dhambi. Ilikuwa ni kwa sababau ya mtu mmoja. Mtu huyo mmoja ni nani? Adamu. Kwa pamoja twajua hili. Lakini watu wengi hawaelewi hili. Hata Wakristo walio wengi nao hawafahamu vyema. Wao hutenganisha kati ya dhambi ya asili na dhambi za kila siku na kudhani kwamba dhambi zao za kila siku zaweza kusamehewa kila siku kupitia sala za toba. Hawajui kwa hakika kwamba sababu yao kuhukumiwa na hatimaye kwenda jehanamu ni kwa sababu ya Adamu.
Uzao wa Adamu hauna uhusiano na Mungu kwa sababu ya dhambi zao haijalishi kwa vipi wanaweza kuwa wema. Mungu huwahukumu wote kwa sababu wao ni uzao wa Adamu, ingawa wanaweza kujaribu kutia juhudi ya kuwa wema watatupwa jehanamu milele kwa sababu ya mzazi wao wa pamoja, Adamu.
 

Adamu aliye mfano wake yeye atakaye kuja.
 
Imeandikwa kwamba Adamu ni mfano wake yeye atakaye kuja. Watu wote walikuwa ni wenye dhambi na mauti ilikuja kwao kupitia mtu mmoja. Hata hivyo mwanadamu alifanywa kuwa mwenye haki kupitia mtu mmoja, Yesu Kristo yaani kwa jinsi ile watu walivyo fanywa kuwa wenye dhambi kupitia mtu mmoja Adamu. Hii ndiyo sheria ya Mungu.
Kutenda matendo mema ili waokolewe wanapomwamini Yesu. Inaenea vipi ulimwenguni na mara ngapi wanasema uwongo! wao hufundisha watu, wakisema, “Unapaswa kuwa mzuri kama wakristo.” Dhambi zetu hazijafutwa kamwe na matendo.
“Adamu aliye mfano wake yeye atakaye kuja.” Mtu huyo atakaye kuja kwa ajili ya wokovu wa wenye dhambi ni nani? Ni Yesu Kristo. Yesu alitumwa kuja duniani na kwa uhalali alibeba dhambi za dunia kwa utabizo wake mara moja na kwa hiyo kutufanya sote kuwa wenye haki na hatimaye alisulubiwa ili kutuokoa na hukumu.
Dhambi iliingia duniani kwa sababau shetani alimlaghai kiumbe Adamu. Dhambi ili ingia kupitia Adamu. Hata hivyo Yesu Kristo, Mwokozi, Muumba na Mfalme wa wafalme aliye mwenye enzi, alitumwa akiwa mfano wa mtu ili kuwaokoa wanadamu toka dhambini mara moja na kwa wakati wote. Alibeba dhambi za dunia juu yake kupitia ubatizo wake mara moja na kwa ajili ya wote alilipa mshahara wa dhambi kwa kusulubiwa.
Mwanadamu hupokea uzima mpya na kupata ukombozi ikiwa ataamini kwamba Yesu alitumwa ili kufuta dhambi zote, bila kujali ukubwa wa dhambi zake. Mungu alipanga na kuamua kuumba mbingu na nchi ili aweze kutufanya kuwa wana kwake. Alikuja duniani na kwa ukamilifu akatimiza ahadi yake. Hivyo bila shaka hatuna dhambi tena. Mungu kamwe hajawahi kufanya kosa. Adamu alikuwa ni mfano wa Mtu atakaye kuja. Sijui ni kwa sababu gani watu hutegemea zaidi matendo yao ya kimwili. Wokovu wetu kwa jumla hutegemea Yesu. Wanadamu huja kuwa wenye dhambi kupitia mtu mmoja, Adamu na walikombelewa kupita Mtu mmoja Yesu.
Kitu pekee tunachopaswa kuamini ni wokovu uletao ondoleo la dhambi. Ni kitu pekee tupaswacho kukifanya. Hatuna chochote cha kutenda zaidi ya kufurahia ukweli kuwa Yesu alifuta dhambi zetu zote. Kwa njia hiyo, kwa nini basi unawahamasisha wengine kuwa watu wakareketwa wa kutenda mambo mema kwa ajili ya wakovu wao? Je, watu wataweza kukombolewa toka dhambini mwao kwa njia ya matendo? Hapana wokovu hutegemea imani tu ya ondoleo la dhambi.
 

Dhambi si kadiri ya kile kipawa.
 
Warumi 5:14-16 inatamka “Walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wo wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu aliyemfano wake yeye atakaye kuja. Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa, kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yele mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi. Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyefanya dhambi si kadiri ya kile kipawa kwa maana hukumu ilikuja kwa ajili njia ya mtu mmoja ikataleta adhabu. Bali karama ya neema ilikuja kwa ajili ya makosa mengi ikaleta kuhesabiwa haki.”
Kifungu hiki kina maana gani? Biblia inasema “dhambi si kadiri ya kile kipawa.” Kipawa hapa kina maanisha wokovu wa Mungu. Inamaana kwamba watu wote waliorithi dhambi kupitia Adamu walikuwa na hatima ya jehanamu lakini dhambi zao ziliweza kusamehewa pasipo kuchagua kupitia imani katika Yesu, aliye futa dhambi zote. Ina maana pia Yesu alikwisha futilia mbali dhambi zote za kipindi kijacho mbeleni.
Mwanadamu aliyezaliwa akiwa ni uzao wa Adamu ni mwenye dhambi hata ikiwa hatotenda dhambi. Hivyo basi hawezi kujizuia kwenda jehanamu hata ikiwa hatotenda dhambi. Yesu alikuja ulimwenguni na kuwa Mwokozi wetu. Kipawa ni kile Yesu alicho tupatia cha ziada katika ukombozi ili kutusamehe dhambi zetu ambazo sisi wanadamu tunaendelea kuzitenda hata mwisho wa dunia.
Kwa hiyo kipawa cha Mtu mmoja ni zaidi ya dhambi ya mtu mmoja. Ikiwa mtu atatenda dhambi ya kumpinga Mungu dhambi hiyo peke yake inatosha kuhukumiwa na Mungu hatimaye kwenda jehanamu. Hata hivyo, kipawa cha Bwana ambaye tayari amekwisha futa dhambi zetu zote na makosa ni zaidi ya dhambi ile ya mtu mmoja.
Ina maana kwamba, upendo wa Yesu na kipawa cha ondoleo la dhambi ni zaidi ya makosa yote ya wanadamu wote. Bwana amefuta ipasavyo dhambi zote za dunia. Upendo wa Yesu, aliyetuokoa, na kipawa cha wokovu vimejaa na ni vikubwa zaidi ya dhambi aliyotenda mtu mmoja, Admu. Bwana tayari amekwisha futa dhambi ya kumpinga Mungu ingawa bado tuko kinyume naye kimwili. Sasa Bwana anatuhitaji kuamini ya kwamba tayari amekwisha futilia mabali dhambi za dunia mara moja na kwa wakati wote. Na ndiyo maana aliokoa wenye dhambi kutokana na dhakmbi zao zote akiwa Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya dunia.
Nadharia isemayo kwamba, dhambi zetu hufutwa pale tunapo mwamini Mungu na kutofutwa tusipo mwamini, si kweli. Mungu amekwisha futa hata zile dhambi za wasio mwamini kwa sababau aliwapenda walimwengu ingawa bado hawapendi kupokea upendo wa Mungu. Hukuna hata mmoja aliye wekwa kando ya wokovu wa Mungu. Wokovu wa Mungu huja kwa wale wote wenye kuamini ukweli wa Injili utamkao kwamba Yesu alikwisha futa dhambi zetu zote.
Sisi ni viumbe dhaifu. Mungu huwachukuliwa wale wote wenye kuamini kwamba Yesu alifuata dhambi zote kuwa ndiyo wasio na dhambi. Bado tuna madhaifu mengi katika miili yetu hata baada ya dhambi zetu zote kusamehewa. Mara kwa mara, tunampinga Mungu na hata kujaribu kutupilia mbali haki yake pale tunapo ya pinga mapenzi yake. Lakini Mungu anasema “Ninawapenda na nimekwisha kuwaokoa. Nimekwisha futa dhambi zenu ambazo mlizo tenda hata sasa.” “Haa! Ni kweli Bwana?” “Ndiyo, nimekwisha futilia mbali dhambi zoate.” “Nakushukuru Bwana. Nakusifu. Siwezi kujizuia kukusifu kwa sababu unanipenda sana hata kufuta dhambi ya kukupinga wewe.”
Wale walio kuwa na dhambi walifanywa kuwa wenye haki na hatimaye kuwa watumwa wa pendo. Hujitoa nafsi zao kwa pendo lake. Hawawezi kujizuia kumwamini Yesu kwa sababu Bwana alifuta dhambi ya kumpinga yeye ingawa walimkataa kwa sababu ya udhaifu wao, kama ilivyo mfano wa Petro. Hi huwafanya wamsifu Bwana. Hivyo Mtume Paulo anasema kwamba wokovu wa Mungu ni mkuuu zaidi ya makosa ya mwanadamu.
Yesu alichukua dhambi zote ya asili zilizo rithiwa na zile za kila siku zitendwazo kutokana na udhaifu hata mwisho wa dunia. Hivyo ni kwa jinsi gani upendo wa Mungu ulivyo mkuu! Hivyo basi, Biblia inasema “Tazama! Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya dunia!” (Yohana 1:29)
 

Wenye haki watatawala uzimani kupitia Mtu mmoja, Yesu Kristo.
 
Dhambi za dunia haziwezi kusamehewa kupitia sala za toba. Waumini hufikia kutokuwa na dhambi na kupokea wokovu wa dhambi zao zote kwa sababu Bwana amekwisha ondolea mbali hata dhambi ambazo watakazo tenda mbeleni Warumi 5:17 inamtamka “kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa.”
Tunabarikiwa kwa rehema. Ni watu gani hao wapokeao wingi wa rehema na kipawa cha haki? Ni wale wote wenye kumwamini Bwana na walio kwisha samehewa dhambi zao kwa kumwamini Mungu. Tunamsifu Bwana kwa sababu tulipokea wingi wa rehema ya ondoleo la dhambi zetu zote. “Wao wapokeao wingi wa neema na kile kipawa cha haki watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.” Sisi ni wafalme tutawalao uzimani.
Ni wafalme tu ndio watawalao. Sisi tunatawala sasa. Ni nani awezaye kuwapinga wafalme? Sisi tulio pokea neema tele na kipawa cha haki, hutawala daima. Tunatawala kila leo na tutatawala hata kesho. Yeyoye atakaye tukirimu atakuwa na heri na hatimaye kutawala nasi. Asiye amini Injili ya kweli ambayo wafalme wanayoihubiri wata ishia jehanamu.
Pamekwisha kuwepo wafalme wengi walio tumikia duniani na pamekuwepo na watu wengi walioishia jehanamu kwa sababu waliwapinga wafalme. Wangeliweza nao kuwa wafalme kama wangeliuona ukweli kwa macho yao na mioyo yao.
Je, wewe nawe unatawala? Tunajivunia na kuwa na uhakika kwa kuwa ni wafalme wa dunia. Tunajivunia na kuwa na uhakikaa kwa kuwa ni wafalme wa dunia. Tunatangaza kwamba wasioamini wata kwenda jehanamu pale watakapo pingana nasi. Ni wafalme tu ndiyo wawezao haya. Hakisha sisi ndiyo wafalme Je, yupo asiye tawala kati ya wenye haki? Ni aibu kwao kutotawala kama wafame. “Unafikra potofu? utakwenda jehanamu ikiwa hauto ukubali ukweli.” Mfalme imempasa awe mwenye hulka ya kifalme. Mfalme lazima aheshimike na kutoa amri kwa wenye dhambi kuamini.
Mfalme aweza na imempasa kuhukumu kuamrisha na kutoa karipio kwa wasio amini kuwa wata kwenda jehanamu kwa kuwa kinyume na haki ya Mungu, hata ikiwa mfalme huyo ni mdogo kiumri. Ana nguvu na mamlaka huukumu wasio amini kwenda jehanamu mbele ya Mungu, lakini haina maana kwamba mfalme huyo ana uhuru wa kutumia vibaya mamlaka yake atakavyo. Bwana hutuelekeza kutawala dunia. Hivyo hebu basi sasa tutawale na kuingia Ufalme wa Mbinguni.
Hata hivyo baadhi ya wenye haki ni wadhaifu mno hata kushindwa kutumia mamlaka zao. Bwana atawakemea atakapo rudi “Uliiacha imani yako, kwa nini ulishikilia tabia ya utumwa? Nilikufanya uwe Mfalem.” Wapo baadhi hushika tabia ya kitumwa kwa dunia. Je, inafaa kwa mfalme kuwaita “Bwana” kwa walio chini yake? Hata hivyo, baadhi ya wenye haki huongea kwa namna hii ingawa haina maana. Huomba msamaha wakupiga magoti kwa dunia hata baada ya Mungu kuwakomboa dhambini. Mfalme imempasa awe na tabia ya kifalme.
Nilijitangazia ufalme huru dhidi ya dunia baada ya kuwa mfalme. Ni liamini kuwa nimekuwa mfalme na kuwa na hulka ya kifalme ingawa nilikuwa mdogo kiumri.
 

Kwa kutii kwake mmoja, Yesu Kristo.
 
Warumi 5:18-19 inatamka “Basi tena kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima. Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.”
“Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi.” Hapa maneno “waliingizwa katika hali ya wenye dhambi” maana yake ni hukumu. Mtu aliye zaliwa akiwa uzao wa Adamu, na ambaye hakuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho, ingawa anamwamini Yesu atahukumiwa “kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.”
Watu wote wamefanywa kuwa haki kwa ajili ya tendo moja la haki ya Yesu, aliyezaliwa toka kwa Bikira Mariamu, na alibatizwa mto Yordani ili kubeba dhambi zote za duniani. Aliyejitolea maisha yake kwa kusulubiwa kwa niaba yao ili kuwafanya wawe wenye haki. Kwa utii wa mtu mmoja kwa mapenzi ya Mungu Baba wengi wamefanywa haki.
Kwa kusema bayana, je, watu wote duniani ni wenye dhambi, au wenye haki, ikiwa tutachunguza katika msimamo wa imani? Wote ni wenye haki. Baadhi ya watu hukasirika na kugombana na mimi ninapo sema hivyo kwa imani. Ukweli ni kwamba, hakuna mwenye dhambi kulingana na mtazamo wa Mungu. Mungu alimtuma Mwana wake wa pekee duniani na humtwika dhambi zote za dunia juu yake na kumfanya ahukumiwe akiwa mwakilishi wa watu wote.
 

Watu huingia Ufalme wa Mbinguni au jehanamu kulingana na imani zao.
 
Mungu haukumu ulimwenge tena kwa sababu alimhukumu Yesu kwa niaba ya watu wote. Hata hivyo, baadhi ya watu huamini hili na wengine hawaamini, ingawa Mwana wa Mungu alikwisha chukua dhambi zote na kufuta kwa utii wa mapenzi ya Mungu. Wenye kuamini huingia ufame wa Mbinguni kwa kuamini haki ya Mungu. Mungu huwa hesabia kuwa wenye haki na kusema “Ninyi ni wenye haki. Mliamini kwamba nilifuta dhambi zenu zote. Njooni, nimewatayarishia Ufalme wa Mbinguni kwa ajili yenu.” Wataingia Ufalme wa Mbinguni wakiwa wamejitosholeza.
Lakini baadhi ya watu hawamwamini Mungu na kukataa Injili, wakisema, “Mungu hii ni kweli? Siwezi kuamini hili. Ni kweli? Kwa kweli sielewi vizuri?” Ndipo Mungu atakapo sema, “Kwa nini unanikasirisha? Niamini ikiwa unataka kuniamini, lakini kama hutaki usiniamini” “Hivi Bwana, Injili ya maji na Roho ni kweli?” Atajibu Bwana, “Nilikuokoa.” “Hapana, siwezi kuiamini. Labda naweza kuamini kwa 90% tu lakini 10% ninamashaka.”
Ndipo Mungu atakapo sema “Huamini ingawa tayari nilikwisha kukuokoa. Sasa amua kulingana na imani yako. Nilighairi kuwatupa wale wenye dhambi walio uzao wa Adamu kwenda jehanamu. Niliumba Ufalme wa Mbinguni pia. Ukipenda ingia katika Ufalme wa Mbinguni au uende jehanamu ili ukatupwe motoni milele.” Hutegemea imani ikiwa wataingia Ufalme wa Mbinguni au jehanamu.
Je, unaamini kwamba Yesu alikuokoa kutokana na dhambi zako zote kwa ubatizo wake na damu yake ambayo ilimwagika pale msalabani? Yote hutegemea imani yako. Hakuna semehu ya kati kati kuelekea Mbinguni na jehanamu. Hakuna kitu kama “Hapana” mbele ya Mungu. Ipo “Ndiyo” tu. Pia Mungu kamwe hatutamkii “Hapana.” Mungu ameahidi yote na kuyatimiza yote. Alikwisha futa dhambi zote za wakosaji.
 

Dhambi ilipozidi neema ilikuwa nyingi zaidi.
 
Hebu tuangalie katika Warumi 5:20-21 “Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana, na dhambi ilipozidi neema ilikuwa nyingi zaidi ili kwamba, kama vile dhambi ilivyo tawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo. Bwana wetu.” Kwa nini sheria iliingia? Ili kufanya kosa liwe kubwa. Wanadamu wana dhambi pasipo hiyari wakiwa ni uzao wa Adamu kwa asili. Lakini hawakuwa wakifahamu juu ya asili yao ya dhambi, na hivyo Mungu kuwapa wanadamu hao sheria ili wapate kualewa juu ya hali zao za dhambi kwa sababu sheria huwaamrisha kile cha kufanya na chakutofanya, na inakuwa ni dhambi kuto tii sheria hiyo kwa mawazo na kwa vitendo.
Sheria iliingia ili makosa yawe makubwa. Mungu alitupa sheria ili tuweze kujua kwamba sisi ni wenye dhambi sana na ni mzigo wa dhambi. Hata hivyo, pale dhambi ilipo zidi, neema nayo ilizidi na kuzidi. Maana yake ni kwamba, mtu aliyezaliwa akiwa na dhambi kizazi cha Adamu, akidhani kuwa yeye anadhambi kidogo tu basi hana la kufanya dhidi ya ukweli wa Yesu kumwokoa.
Hata hivyo, yule anaye dhani kuwa ana mapungufu na udhaifu mwingi na kamwe hawezi kuishi kwa kufata neno la Mungu kwa mwili wake, hurejea na kumshukuru Mungu aliye mwokoa. Injili isemayo kwamba, Bwana alizichukua dhambi zote za dunia mara moja na kwa wakati wote ni zawadi kuu kwa mtu wa aina hii. “Na dhambi ilipozidi neema ilikuwa nyingi zaidi.” Karama ili zidi zaidi, hivyo wale wenye dhambi nyingi walifanywa kuwa wenye haki. Wenye dhambi kidogo, wale wenye kudhani kwamba wao si wenye dhambi sana ndio watakao kwenda jehanamu. Ni wale tu wenye dhambi nyingi ndio watakao fanywa wenye dhaki kamili.
Hivyo basi, mtu anaye fahamu kwamba yeye ni mwenye dhambi sana, kwa furaha kusifia wokovu wa Yesu. Wapo wahubiri wachache walio stawi kati ya wahubiri wa dunia hii. “Dhambi ilipo zidi neema ilikuwa nyingi.” Hii haina maana kwamba tunaweza kutenda dhambi kwa makusudi ili kwamba neema iwe nyingi zaidi.
Mtume Paulo anasema katika Warumi 6:1 “Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?” Paulo ana maana kuwa “tumeokolewa ikiwa tutaiamini haki ya Mungu. Bwana tayari amekwisha okoa wenye dhambi kwa makosa yao. Tumefanywa haki kwa kuamini kwa mioyo yetu yote. Tutaweza kuokolewa ikiwa tutaamini kile Bwana alicho fanya. Haijalishi ni kwa kiwango gani tu wadhaifu kimwili au ni mara ngapi tunaweza kuanguka dhambini, bado tumefanywa haki pasipo matendo kwa kuamini ukweli tu.”
Tumekuwa wenye dhaki kwa imani. Ni kwa jinsi gani matendo yetu yalivyo maovu? Ni mara ngapi tuna tenda dhambi? Tuna mapungufu mangapi kwa idadi ikiwa Mungu aliye mtakatifu ataangalia matendo yetu? Siwezi kujizuia kumshukuru Bwana. Warumi 5:20-21 inatamka kuwa “Dhambi ilipo zidi neema ilikuwa nyingi zaidi ili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.”
Mungu alitupatia uzima wa milele kupitia Yesu Kristo. Haki ya Bwana wetu hutawala naye. Namsifu Bwana, aliye tuokoa kwa wingi sisi tuliokuwa wenye dhambi kutokana na makosa yetu. Nakushukuru Bwana.