Search

Kazania

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 6-1] Utangulizi katika Kitabu cha Warumi Sura ya 6

Yatupasa kujua siri ya ubatizo wa Yesu. 
 
Je, unaifahamu na kuiamini siri ya ubatizo wa Yesu alio upokea toka kwa Yohana? Ningependa kukueleza juu ya siri hiyo kupitia Warumi 6:1-4 “Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo kaitka mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzma.”
Ili kuelewa juu ya Andiko hili na kuchimbua ukweli wake, yatupasa kwanza kuielewa imani ya Paulo kama ilivyo onyeshwa katika Wagalatia 3:27 na kuwa na imani sawa naye. Anasema, “Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.” Andiko hili lina maana gani? Sasa tutaweza kuelewa maneno haya kwa kupitia Mathayo 3:13-17.
Paulo anauliza ikiwa tutaweza kuendelea kutenda dhambi kwakuwa tayari tumekwisha kupokea ondoleo la dhambi mara moja na kwa wakati wote kwa kuiamini haki ya Mungu. Jibu la Paulo ni hapana, na pia ni jibu la wale wote wenye kuiamini haki ya Mungu vyema, hii haina maana kwamba wenye haki kamwe hawatendi dhambi katika miili yao. Hivi sivyo kweli.
Pia haina maana kwamba, kwa sababu dhambi zetu zimekwisha samehewa, imetupasa kupanga jinsi ya kutenda tena dhambi. Wenye haki tayari wemekwisha batizwa katika mauti yake. Itawezakanaje wale walio na imani ya haki yake kuendelea kuwa ndani ya dhambi? Hii haiwezi kuwa kweli. Paulo anaelezea sababu ya Wagalatia 3:27 akisema “Maana ninyi nyote mliobotizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.”
Kwa maneno mengine, Yesu alibeba dhambi zetu zote kwa njia ya ubatizo wake na kufa msalabani ili kwamba wale wenye kuamini juu yake waweze kubatizwa katika Kristo kwa imani. Kwa hiyo yatupasa kuhodhi aina hii ya imani.
 

Yatupasa kuwa na imani ya kuungana na ubatizo wa Yesu.
 
Yatupasa kuwa na imani yenye kuungana na ubatizo wa Yesu na kifo chake. Inasema “Maana ninyi nyote mlio batizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.” Andiko hili maana yake ni kwamba Yesu alibatizwa na Yohana katika mto Yordani, alibeba dhambi zetu mara moja. Hii pia ina maanisha juu ya kifo cha Yesu msalabani kilikuwa ni upatanisho wa dhambi zetu zote kwa sababau alikuwa amekwisha beba dhambi zote za dunia kupitia ubatizo wake. Kuelewa na kuamini ukweli huu ni kuwa na imani inayo ungana na Bwana.
Tunatengwa na haki ya Mungu kwa sababau ya uovu wetu. Je, unajua kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu zote pamoja na makosa yetu pale alipo kubali kubatizwa na Yohana? Yesu alizichukua dhambi zetu zote mara moja kwa njia ya ubatizo na kufa msalabani ili kulipa mshahara wa dhambi. Sisi ni viumbe tusio weza kujizuia kutenda dhambi maishani mwetu pote. Kwa hiyo yatupasa tuwe na imani inayo ungana na Kristo kwa kuweka msingi wa imani yetu juu ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Tutaweza kuungana na Kristo ikiwa tu pale tutakapo amini kwamba Yesu aliitimiza haki ya Mungu kwa njia ya ubatizo wake.
Ni nani aliye tii mapenzi ya Baba, kutimiza haki yake? Alikuwa ni Yesu Kristo mwenyewe. Yesu alitimiza haki ya Mungu mara moja na kwa wakati wote. Yesu aliweza kulipa mshahara wa dhambi kwa kifo chake pale alipo beba dhambi zetu zote kwa kupitia ubatizo wake toka kwa Yohana. Ikiwa basi tunahitaji kuungana naye, yatupasa kuwa na imnai katika ubatizo wenye kubeba dhambi zetu zote mara moja na kwa wakati wote.
Yatupasa kuungana na Bwana na kumwamini yeye kwa sababu yeye amekuwa ndiye Mwokozi wetu wa milele kupitia ubatizo wake. Uchaguzi pekee ulio baki kwako sasa ni ama kukubali ukweli huu au la. Ili kuwa mtoto wa Mungu kwa kuamini ubatizo wake na kumwaga kwake damu msalabani au kuangamia mauti ya milele katika jehanamu kwa kuwa umekataa ukweli, vyote hivi hutegemea uamuzi wako. Yesu alibatizwa ili kwamba dhambi zetu ziweze kuondolewa mbali (Mathoyo 3:13-15).
Tunapo angalia katika Mathayo 3:15 tunaweza kuona maneno “kwa kuwa ndivyo” ya kiwa na maana ya namna ya kuitimiza haki ya Mungu. Usemi huu kwa Kiyunani maana yake “hoo’-tos gar” maana yake “kwa njia hii”, “vile ipasavyo” au “hakuna njia nyingine zaidi ya hii” ikitamkwa kwamba ubatizo wa Yesu ilikuwa nidyo njia ya uhakika na sahihi katika kumtwika yeye dhambi zetu. Neno hili hudhihirisha kwamba Yesu alichukua dhambi za wanadamu juu yake kwa njia ya ubatizo alio upokea toka kwa Yohana badala yetu.
Alipo batizwa Yesu, dhambi zetu zilikabidhiwa kwake. Yatupasa kuuamini ukweli huu katika Warumi 6:5-11, ambapo Yesu alibatizwa ili kwamba dhambi zetu ziweze kufutiliwa mbali na baadaye afe msalabani ili kwa kufuta yote awaokoe wanadamu.
Ili uweze kurudisha kitu cha mtu, ni lazima ulipie gharama iliyo sawa na deni lako. Kwa njia hiyo pia yatupasa kujua ni kwa vipi na kwa kiasi gani Bwana wetu alilipa gharama ili kufuta dhambi zetu.
Yesu alipo batizwa, alibeba dhambi zetu zote tulizo tenda toka umri wa miaka 10, hata 20, 30, 40, 50, 70, 80, 90, na dhambi zile tuzitendazo hata mwisho wa pumzi ya mwisho. Alibeba dhambi zetu zote kupitia ubatizo na kulipa mshahara wa dhambi zetu. Yesu alibeba dhambi zote na uovu wetu mara moja, tulio tenda tukielewa au kutoelewa. Yesu alibatizwa ili kusafisha dhambi zetu na kulipa mshahara wa dhambi katika msalaba. Huu ndio ukweli ulio na Injili ya maji na Roho ambao Maandiko yanauzungumzia.
Twaweza kuona kwamba wa Kristo wengi wajaribu kwa dhati kumkubali Yesu kuwa Mwokozi wao kwa kuweka na kuunga mkono Fundisho la kanuni ya utakaso kwa sababu hawafahamu siri ya “ubatizo” Paulo aliyokuwa akizungumzia. Ikiwa Yesu asingeli kuja duniana na kupokea “ubatizo” toka kwa Yohana, dhambi za wanadamu zingebaki hata milele. Kwa hiyo yatupasa kuacha kabisa kuamini aina hii ya mafundisho ya uongo yenye kuelekeza kwamba mioyo na miili yaweza kutakaswa kwa kadiri muda unavyo kwenda.
Ukweli pekee na wa milele katika dunia hii ni ule wa Yesu kubatizwa na kubeba dhambi zetu zote duniani. Kuamini Injili ya maji na Roho hutusadia kuushinda uongo wote utokanao na mafundisho ya kanuni za ulaghai na hatimaye kutupa ushindi kwa wale waaminio. Hivyo yaputasa kuamini ukweli huu. Baadhi ya Wakristo huenda jehanamu huku wakiacha kuzaliwa upya mara ya pili kwa sababu hawaja ungana na ubatizo wa Yesu.
Je, umekwisha wahi kuona picha ya moyo ulio pasuka kwa upanga? Huonyesha sadaka ya upendo wa Mungu. Mungu anatupenda sana hata kutuokoa kwa dhambi zetu zote kwa njia ya Injili ya maji na Roho, “kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).
Yakupasa ukubali upendo wa Yesu aliotupatia kwa kubatizwa na kumwaga damu yake yote pale msalabani. Mioyo yetu inapaswa kuungana na haki ya Mungu. Yatupasa kuishi tukiwa tumeungana na Yesu. Maisha ya uaminifu katika umoja na haki ya Kristo ni mazuri sana. Paulo anasema kwa uwazi na kwa kusisitiza katika Warumi sura ya 6 kwamba, yatupasa kuishi kwa imani ya umoja na haki ya Mungu.
Kama Paulo asemvyo, katika Warumi 7:25. Je, tunaitumikia au la? Na ndiyo maana sisi kama Paulo wakati wote tuna mioyo yenye kuungana na haki ya Mungu. Itatokea nini kama hauto ungana moyo wako na haki ya Bwana? Uharibifu utatokea moja kwa moja.
Wale wenye kuungana na haki ya Mungu huishi maisha ya umoja na kanisa lake. Ukiiamini haki ya Mungu basi ni lazima uungane na kanisa lake pamoja na watumishi wake. Mwili mara zote hujaribu kuitumikia sheria ya dhambi hivyo basi yatupasa kuishi kwa imani, mara kwa mara tukitafakari juu ya haki ya Mungu kila siku na ndipo tutakakapo ungana na Bwana. Ndiyo maana Biblia inasema kwamba mnyama anaye cheua na kutafuna ndiye safi asiye najisi (Walawi 11:2-3).
Ungana na haki ya Mungu. Je una hisi nguvu mpya ikikujia au la? Jaribu kuungana na haki ya Mungu sasa! Hebu kwa mfano umekwisha ungana moyo wako na ubatizo wa Yesu. Sasa basi je, bado unadhambi au la? —Ndiyo, sina.— Basi nasi tumefufuka pia. Tunapo ungana na Kristo, dhambi zetu husafishwa tunakuwa tumekufa msalabani naye na kufufuka toka kifoni naye pia.
Hata hivyo, nini kitokeacho pale tusipo ungana na Kristo? “Unazungumiza nini? Oh sawa, una zungumzia juu ya ubatizo wa Yesu, ina maana katika Agano la Kale ilikuwa ni lile tendo la kuwekea mikono juu ya sadaka ya dhambi na sasa katika Agano Jipya ni ubatizo wa Yesu kwa Yohana, na ndivyo ilivyo sasa! Lakini sasa ni lipi la muhimu katika hili kiasi kila mtu hulitilia mkazo?”
Wale wote wenye kuamini ubatizo wa Yesu kwa nadharia tu, hawana imani ya kweli, hivyo hatimaye kuachana na Ukristo mwishoni. Imani ya kinadharia kama ilivyo taarifa anayo jifunza mwanafunzi katika shule toka kwa mwalimu haitoshi kupokea haki ya Mungu. Lakini wapo wanafunzi ambao kwa kweli huwaheshimu walimu wao na kujaribu kuiga tabia na uongozi wa mwalimu. Tusikubali maneno ya Mungu kama sehemu ya elimu na ufahamu, bali tuyaweke mioyoni mwetu pamoja na tabia ya Kristo, upendo, neema na neno lake la haki. Yatupasa kuachana na hamu ya kujifunza juu ya elimu au namna ya ufahamu pale tunapo fundishwa neno la Mungu.
Fikra za wale ambao tayari wamekwisha jiunga kwa kina na neno la Mungu hudhamiria kumtumikia Bwana na hata kuwa na usharika mzuri naye, pia hawawezi kuyumbishwa kirahisi na mazingira! Hawaenendi na mazingira ili waweze kufanikisha Amri kuu. Lakini mambo madogo huwaathiri wale ambao bado hawajaunganisha mioyo yao na Yesu.
Yatupasa kuwa na imani iliyo ungana na haki ya Mungu. Tusiachilie mioyo yetu kuyumbishwa na mambo madogo madogo ya dunia. Wale wenye kuunganisha mioyo yao na Kristo walibatizwa katika Yesu, wakafa naye msalabani na kufufuka tena naye ili waokolewe kwa dhambi zao zote. Sisi si watu wa dunia hivyo yatupasa kuamini. Yatupasa kuungana na haki yake ili kumridhisha yeye aliye tuita kuwa watumishi wa haki yake.
Ikiwa tutaungana na haki ya Mungu mioyo yetu wakati wote itakuwa na amani na kujawa na furaha kwakuwa nguvu ya Bwana ita kuwa yetu. Twaweza kuishi kwa baraka kuu kimaisha kwa sababa Mungu hutujaza baraka zake tele pamoja na nguvu za uungu wake.
Uruhusu moyo wako uungane na haki ya Mungu, ndipo utakapo weza kuungana na watumishi wake kama mimi na kuwa na imani thabiti katika neno lake kupitia ushirika wa hiyari na kuitumikia kazi yake kwa bidii. Bwana amekwisha takasa dhambi zote ingawa imani yako yaweza kuwa ndogo kama punje ya aradali. Endelea kuungana naye, hasa kwa ubatizo wake ingawa haujitoshelezi.
Namshukuru Mungu kwa kutupatia imani ya kuunganika na Bwana kupitia ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani. Yatupasa kuungana mioyo yetu na Bwana tokea sasa hadi pale tutakapo kutana naye. Binafsi sisi ni dhaifu hivyo yatupasa kuungana. Je amegundua imani ya kuunganisha moyo wako na haki ya Yesu ilitimizwa? Je, unayo imani yenye kuungana na ubatizo wa Yesu? Yakupasa sasa kuwa na imani yenye kuungana na ubatizo wa Yesu na damu yake iliyo mwagika. Wale wasio na imani hii watashindwa kuokolewa hatimaye kuishi maisha yasiyo ya imani. Hivyo haki ya Mungu ni muhimu kwa maisha yako.
Kuungana na Bwana huleta baraka ya ondoleo la dhambi na hatimaye kuishi ukiwa mtoto wa Mungu kupitia imani ya haki ya Mungu. Ni hamu yangu kuona haki ya Mungu inakuwa haki yako leo. Amini! Na upate haki ya Mungu, ndipo baraka za Mungu zitakapo kuwa na wewe.
 

Tusijaribu kumpa Mungu sadaka ya matendo yetu ya kujitoa.
 
Baadhi ya Wakristo hawaamini haki ya Mungu na humsifu Bwana wakiimba “♫Oh, Mungu chukua kilicho changu na ufanye kuwa chako, ♪matendo yangu ya kujitolea mbele yako”. Kwanjia hii Mungu hana nafasi yoyote ya kufanya chochote kwao.
Wanadamu humchosha Mungu kwa kujifanya wao ni wakujitolea matendo yao zaidi. Mungu amechoshwa na upofu huu wa kujitolea kwa sadaka ya matendo. Wao humsihi Mungu apokee haki zao za kibinadamu. Hudumu waki mlilia Bwana “O, Mungu! Pokea kujitoa kwetu sadaka” huku wakitenda kazi za kanisa kama vile kufagia, kuosha sakafu, kufanya maombi, kuimba mapambio na hatakula chakula. Hii inatia dosari kwa Wakristo wengi. Siku hizi Wakristo wengi humsihi Yesu kuyajali matendo yao ya kujitolea kimwili huku hawaijui haki ya Mungu au hata kuiamini. Yatupasa kuachana na kujitolea huku kimwili na kuanza kuikubali na kuielewa haki ya Mungu ambayo ndani yake umo ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani.
Kujitoa kwetu kimwili hakuna mguso wowote mbele ya Mungu. Lakini wanadamu huendelea kuhitaji Mungu apokee kujitoa kwao kimwili na kuwasamehe dhambi zao kwa kupande mwingine. Ni sawa na upumbavu wa mtu masikini na omba omba kumpa tajiri bilionea kila alicho nacho na kuomba akae katika makazi ya kifahari kwa fidia ya kile alichoa toa. Mungu haitaji kwetu kujitia sifa ya haki zetu binafsi. Mungu anahitaji tuwe na imani kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani.
Ukristo si aina ya dini iliyo letwa na watu hapa duniani. Ukristo si sawa na dini nyingine za dunia hii kama vile Ubudha, ambapo huitaji kusali kila mara, kuinama na kujitakasa binafsi. Tusiwe na imani za aina hii, kuinama na kusali ilikupata baraka toka kwa mwanzilishi wa dini hiyo ya kidunia. Tusijitolea kwa matendo yetu na kuomba baraka ya Mungu kama malipo, badala yake tumjue na kuikubali haki ya Mungu kwa kuwa anahitaji kutupatia haki hiyo.
Tutapokea ondoleo la dhambi ikiwa pale tutakapo amini ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani. Yesu alibatizwa ili kubeba dhambi zote za dunia na kufa ili kuzifuta dhambi hizo mara moja na kwa wakati wote.
Waebrania 10:18 inatamka “Basi ondoleo la hayo likiwapo hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.” Yesu alichukua dhambi zetu zote kwa kubatizo wake na kufa mara moja, kuitimiza haki yote ya Mungu. Hivyo imani zetu katika ubatizo na damu ya Kristo imerudisha mahusiano yetu na Mungu.
Paulo anazungumzia juu ya “Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti hata mkazi tii tamaa zake” (Warumi 6:12). Tutatawala na Yesu Kristo aliye Bwana wetu na Mfalme wa milele. Dhambi haitoweza kuwa na mamlaka juu yako. Muda ambao dhambi inatula unakaribia kwisha. Tusifuate tamaa mbaya au matakwa ya miili yetu. Twaweza kushinda vyote moja kwa moja kwa sababu Mungu ametupatia haki yake iliyo kamili
 

Toeni mioyo yenu na miili yenu kama sadaka ya haki ya Mungu.
 
“Wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi, bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki” (Warumi 6:13).
Paulo anatueleza kanuni muhimu tatu za kuzuia dhambi. Kwanza, tusitii tamaa za miili yetu. Yatupasa kukataa kile ambacho ule utu wa nje unachotaka katika tamaa zake. Pili tusi vitoe viungo vyetu kama silaha kwa dhambi. Tuvikomeshe viungo vyetu ambapo ni uwezo wetu, ili visitumike kama silaha ya dhuluma. Tatu, yatupasa kujitolea wenyewe kwa Mungu kama silaha ya haki ya Mungu.
Kabla ya kumwamini Yesu tuliitoa mikono yetu, miguu, midomo na macho yetu kwa dhambi. Tukawa silaha ya dhambi na kufata kila ilipo ongoza. Lakini sasa imetupasa kuamua kuacha kuvitumia viungo hivyo kama silaha ya dhuluma katika dhambi. Tusiiache dhambi itutawale pasipo kujizuia. Jaribu la dhambi linapo kuja yatupasa kutamka, “dhambi ulikwisha kufa na Kristo.” Na imetupasa kukiri kwamba Mungu ni Bwana wa uhai wetu wote.
Katika maisha ya imani, yatupasa kuelewa yote mawili ambayo yatupasayo kufanya na kutofanya. Tusi vitii viugo vyetu vya mwili kwa ajili ya dhambi bali tuvitoe kwa Mungu. Kile kinacho paswa kufanyika ni muhimu sana kama vile tusivyo paswa kufanya. Tusipo toa chochote kwa Mungu, kwa upande mwingine maana yake tunajitolea kwa dhambi. Mfano ikiwa tutajitolea muda wetu kwa Mungu hatuto weza kuwa na muda kwenye dhambi. Yatupasa kuwa adui wa dhambi na kujiunga na familia moja ya Mungu.
Twaweza kusema kwa nadra, “sina ujasiri wakushinda dhambi.” Hata hivyo Paulo anatuambia katika Warumi 6:14 kwamba tusiwe na fikra hizi “kwa maana dhambi haita watawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria bali chini ya neema.” Ikiwa bado tuko chini ya utawala wa dhambi basi bila shaka tuta endelea kutenda dhambi. Lakini ikiwa bado tuko chini ya neema, basi itatushikilia na kutupa ushindi. Mwandishi wa Zaburi alisali akiema “Uzielekeze hatua zangu kwa neno lako, uovu usije ukanimiliki” (Zaburi 119:133).
Kwa kadiri tutakapo endelea kuishi hapa dunianai bado dhambi itaendelea kutufuata hata baada ya kukiri kuwa tumekwisha kufa katika Kristo, dhambi bado itaendelea kutuangusha na kututawala. Ikiwa tutajaribu kuwa wenye haki kwa juhudi zetu binafsi chini ya sheria, hatutoweza kuwa huru na mamlaka ya dhambi. Lakini imetupasa kuelewa kuwa tuna imani yenye haki ya Mungu. Hivyo dhambi haitoweza kututawala. Yatupasa kujua hili na kulitamka hadharani kwa sauti.
Wote imewapasa kuiamini haki ya Mungu na kuikiri kwa vinywa, “kwa moyo mtu huamini haki, na kwa kinywa kukiri na kupokea wokovu” (Warumi 10:10). Hakika ni muhimu kwako kuiamini haki ya Mungu kwa moyo wako wote na kuikiri kwa kinywa.
Kwa hiyo, dhambi inapotutawala kila wakati ndipo hasira inapo jaribu kutawala akili zetu, kila wakati uzinzi na tamaa mbaya vinapo tugandamizia, ulafi unapo tujaribu kutudanganya ili kukidhi maisha yetu, chuki na taharuki inapo kuja juu, au wivu unaapotufunga moyo yatupasa tupaze sauti na kusema “Yesu alikwisha yachukua yote haya!” Yatupasa tupaze sauti kwa imani “Wewe dhambi! Huwezi kunitawala. Mungu pamoja na haki yake aliniokoa vyema kutokana na dhambi zangu zote na uharibufu, laana kutoka kwa shetani.”
Msemo wa “tunaishi kwa Mungu” maana yake tunaishi kwa haki kwa sababu ya imani zetu katika haki yake. Haki ya Mungu ilitufanya sisi tunao amini ubatizo na damu ya Yesu kuwa kamili. Na ndiyo maana tumekufa kwa dhambi na kuishi kwa Mungu kwa njia ya imani ya haki yake. Hakuna lililo muhimu kama kujua na kukiri kuwa sisi tumefufuka kiroho kwa kuamini haki ya Mungu.
Paulo alisema kwamba, “dhambi ilipo zidi neema ikawa nyingi” (Warumi 5:20). Ndipo watu hawakumwelewa na kusema kwamba mtu imempasa kutenda dhambi zaidi ili neema iongezeke. Lakini Paulo aliwasahihisha. Mambo bado hayatokwisha baada ya kuamini ubatizo na damu. Dhambi za kidunia zitakuzunguka na kujaribu kukuanguasha moyo wako.
Hata hivyo, kila inapotokea, twaweza kuitegemea haki ya Mungu na kuushinda udhaifu wetu au kutoiamini haki yetu. Twaweza kuishi tukiwa watoto wa Mungu anao pendezwa nao. Kwa imani hiyo, tumeweza kufa kwa dhambi na kuishi kwa Mungu. Twaweza kuishi maisha yetu yote katika kuitafuta haki ya Mungu na kuifuata, na hatimaye kuishi milele katika Ufalme wa Mungu tutakapo fika huko.
Warumi 6:23 “Kwa maana msharaha wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.” Wale wote waliomkiri Kristo kama Mwokozi wao huamini nguvu ya ubatizo wake na matokeo ya hukumu ya msalaba. Amina.
Haleluya! Bwana Asifiwe!