Search

Kazania

Somo la 8: Roho Mtakatifu

[8-1] Roho Mtakatifu Hufanya kazi kupitia ahadi ya Neno la Mungu (Matendo 1:4-8)

(Matendo 1:4-8)
“Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba ambayo mlisikia habari zake kwangu ya kwamba Yohana aliwabatiza kwa maji, basi ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada siku hizi chache. Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema Je? Bwana wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme? Akawaambia si kazi yenu kujua nyakati wala majira Baba aliyo weka katika mamlaka yake mwenyewe. Lakini mtapokea nguvu, akisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na katika Uyahudi yote, na Samaria na hata mwisho wa nchi.”
 

Je, uwepo wa Roho Mtakatifu 
ndani ya mtu ni kipawa cha Mungu 
au ni juhudi ya mtu binafsi?
Ni kipawa kitolewacho kwa mtu aliyepokea 
msamaha wa dhambi, na imejumuisha 
maana ya utimilifu wa 
ahadi ya Mungu.

Hapo mwanzo nilipatwa na tukio la kujiwa na miale ifananayo kama Roho Mtakatifu wakati wa maombi. Lakini miale hii haikudumu kwa muda, hivyo punde ilitoweka mbele ya kitita cha dhambi. Ingawa leo napenda kukuonyesha ukweli kuhusu Roho Mtakatifu ambaye atakaye kaa ndani yetu hata milele, si kwakupitia roho zidanganyazo ambazo hutambulika kwa dhambi, bali kupitia injili ya kweli. Roho Mtakatifu nitakaye mtambulisha kwako kwa kupitia ujumbe huu si kitu fulani unacho weza kupokea kwa maombi bali kupitia imani katika injili ya majina Roho tu.
Napenda kukuongoza katika kupokea 1uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yako kupitia kitabu hiki. Utagundua kwamba Roho Mtakatifu atakuhamasisha kwa ujumbe huu nitakao kupatia. Ni hamu kubwa ya Mungu kwetu kumpokea Roho Mtakatifu ndani yetu katika nyakati hizi. Utaweza kujifunza kuwa na Roho Mtakatifu ndani yako na kumpokea kupitia kitabu hiki. Ikiwa kama kitabu hiki hakitoweza kukidhi haja yako kikamilifu, nakushauri usome vitabu viwili vilivyo chapishwa nami hapo nyuma. Utaweza kupokea imani sahihi mbele ya Mungu kwa kupitia vitabu hivi.
 
1Roho Mtakatifu hukaa ndani ya mioyo ya walio zaliwa upya ambao dhambi zao zote zimesamehewa kwa kuiamini Injili ya maji na Roho. Punde, anapo kuja juu ya mtakatifu, hufanya makazi ndani yake milele na kamwe hatomwacha peke yake kadiri atakapo endelea kuamini Injili. Humpa ushawishi mtakatifu huyo, katika kumwongoza kuelekea mapenzi ya Mungu, kumwongoza katika Biblia, humpatia nguvu ili kushinda majaribu na taabu anazokutana nazo hapa ulimwenguni, na humfanya azae matunda ya Roho kwa wingi. Mungu huutukuza mwili wa mtakatifu ukiwa ni hekalu lake kupitia kuweka makazi ya Roho Mtakatifu (Matendo 2:38-39, Yohana 14:16, 16:8-10, 1 Korintho 3:16, 6:19, Wagalatia 5:22-23).

Wakristo walio wengi hujaribu kumpokea Roho Mtakatifu kwa namna ile alivyo washukia wafuasi wa Yesu katika siku ile ya Pentekoste. Wapo baadhi ya watu wamepata vitita vya fedha kwa kutumia njia hii. Hujidai kwamba Roho Mtakatifu ni kitu fulani kinachoweza kupatikana kupitia juhudi ya mtu binafsi. Hutamani kuona maono, kutenda miujiza, kuisikia sauti ya Yesu, kunena kwa lugha, kuponya magonjwa na kukemea mapepo. Hata hivyo ndani yao huwa na dhambi mioyoni na wapo katika msukumo wa roho za shetani (Waefeso 2:1-2). Hata leo hii watu wengi bado wanaendelea kuishi pasipo kujua kwamba wapo chini ya nguvu za roho wa shetani. Hiki ndicho chombo na ulaghai wa shetani anao tumia dhidi ya watu kwa kutumia kila aina ya njia kama vile miujiza na maajabu ambayo hakika ni kiini macho tu. 
Yesu aliwatuma wafuasi wake wasitokeYerusalamu, bali waingoje ahadi ya Baba (Matendo1:4). Kupokewa kwa Roho Mtakatifu kunakofunuliwa katika Matendo si kwakupitia “mazoea”, “kujitoa” au “sala za toba” bali kupitia kungojea ahadi ya Baba kumleta Roho Mtakatifu kwao. Kile tunacho paswa kujifunza kutoka katika ujumbe huu ni kwamba, uwepo wa Roho Mtakatifu ndani ya mtu hautegemei kupitia maombi ya dhati afanyayo. Hii ni karama ya Mungu ambayo itaweza kupatikana pale tu kupitia imani kamili katika Injili njema ya maji na Roho ambayo Baba Mungu na Yesu Kristo aliyowapa wanadamu. Uwepo wa Roho Mtakatifu ndani ya mtu hutokea kupitia imani ya Injili ambayo Yesu kristo ametupatia. Mungu ametupa ukweli wa maji na Roho ili kwamba tuweze kumpokea Roho Mtakatifu ndani yetu (1 Yohana 3:3-5).
Neno “ahadi ya Roho Mtakatifu” hutokea mara nyingi katika Agano Jipya. Petro anaongelea katika mahubiri yake (Matendo 2:38-39) juu ya ubatizo wa Roho Mtakatifu katika siku ya Pentekoste. “Ni ahadi ya Mungu kutupatia Roho mtakatifu kwa wale walio pokea msamaha wa dhambi kutokana na kuamini injili njema.”
Roho Mtakatifu ni kipawa kilichomo ndani ya wale wote walio pokea msamaha wa dhambi zao na kujumuisha maana ya kutimia kwa ahadi ya Mungu. Roho Mtakatifu katika Agano Jipya si kitu kinachoweza kupatikana kupitia makubaliano kati ya Mungu na watu bali ni ahadi ya zawadi toka kwa Mungu. Hivyo Roho Mtakatifu ndani ya mtu kama ilivyoanishwa katika matendo sio kitu kinachoweza kupatikana kupitia maombi (Matendo 8:19-20).
Roho Mtakatifu huja juu ya wale wote wanaoamini Injili ya maji na Roho ambayo Yesu aliyotupatia. Yesu aliwaahidi Wanafunzi wake kumtuma Roho Mtakatifu ili kwamba waweze kuwa naye ndani yao. “Yohana aliwabatiza kwa maji bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache” (Matendo 1:5). Hivyo Mitume wake walisubiri kutimia kwa ahadi ya Mungu.
Kwa kuangalia imani za hawa walio katika Biblia ambao walipokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao, tunagundua kwamba haya yalitokea si kwa kupitia juhudi zao bali kwa mapenzi ya Mungu. Uwepo wa Roho Mtakatifu ndani ya wafuasi hao katika Matendo haukutokea kwa msingi wa juhudi za kibinamu au maendeleo ya kiroho.
Kuja kwa Roho Mtakatifu punde juu ya wafuasi wa Kristo kama ilivyoandikwa katika Matendo kulitokea kweli. Kulikuwa kama vile Yesu alivyosema “siyo siku chache kuanzia sasa”. Hii ndiyo iliyokuwa baraka ya kwanza katika kipindi cha Kanisa la kwanza. Kwa kuchunguza maandiko tunaweza kuona ahadi ya Mungu iliweza kutimia si kwa kupitia kufunga, maombi au kujitolea nafsi bali kupitia imani katika Kristo Yesu. Baada ya Yesu kupaa, waumini walimpokea Roho Mtakatifu kwa wakati mmoja.
 

Roho Mtakatifu aliwashukia Wafuasi wa Yesu ghafla toka Mbinguni!

“Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja” (Matendo 2:1). Wafuasi wa Yesu walikusanyika wakisubiri kutimia kwa ahadi ya Mungu kumtuma Roho Mtakatifu. Ndipo Roho Mtakatifu alipokuja juu yao.
“Kukaja ghafla kutoka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kwa kasi ukaijaza nyumba yote waliokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi za moto uliwakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu wakaanza kusema kwa lugha nyingi kama Roho alivyowajalia kutamka” (Matendo 2:2-4). 
Roho Mtakatifu alishuka “ghafla kutoka mbinguni” hapo neno “ghafla” maana yake kulifanyika si kwa kupitia mapenzi ya Mwanadamu. Kwa nyongeza tafsiri ya “toka Mbinguni” inaweza kuelezwa mahali Roho Mtakatifu alipotoka, na pia kuondoa mawazo kwamba ujazo wa Roho Mtakatifu ndani ya mtu hutoka na mapenzi yake au juhudi. Tafsiri “Toka mbinguni” inatuonyesha kwamba, kusema Roho Mtakatifu anaweza kupatikana kwa kupitia maombi ni hoja za kitapeli.
Kwa maneno mengine, kusema kwamba Roho Mtakatifu alishuka ghafla toka mbinguni maana yake kuwa na Roho Mtakatifu ndani hakutokei kwa kupitia namna za kidunia kama vile kunena kwa lugha au kujitoa nafsi. Wafuasi wa Yesu walinena kwa lugha hapo awali katika kuhubiri Injili njema kwa watu wa mataifa yote. Sababu ya hili ni kuwa aliwawezesha kuhubiri Injili kwa lugha za kigeni toka ile ya Kiyahudi kwa msaada wake. Watu toka Mataifa yote waliweza kusikia wafuasi hao wakinena kwa lugha zao ingawa wengi wa wafuasi hawa walitokea Galilaya.
“Kukawatokea ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu wakaanza kusema kwa lugha nyingine kama Roho alivyowajalia kutamka…” (Matendo 2:3-4). Hapa ni lazima kuwa makini zaidi tunapoona tafsiri, Roho Mtakatifu “kuwakalia kila mmoja wao”. Wafuasi walisubiri kuja kwa Roho Mtakatifu mahali pamoja wakiwa tayari wamekwisha kuamini Injili ya kuzaliwa upya mara ya pili katika maji na Roho.
Wakristo wengi nyakati hizi huelewa vibaya sehemu hii ya kifungu, wakiamini ya kwamba ujio wa Roho Mtakatifu hutokea kwa sauti kama ya upepo uvumao wanapokuwa kwenye maombi. Hata hivyo hili ni jambo potofu kuhusiana na Roho Mtakatifu litokanalo na upumbavu na kuchanganyikiwa. Je, Roho Mtakatifu hufanya sauti pindi anaposhuka juu ya watu? Hapana, hakika hafanyi. 
Kile watu wanachosikia ni sauti ya shetani afanyayo pale anaposhambulia roho za watu. Hufanya sauti hizi pale anapofanya mazingaombwe, sauti za kunongoneza na miujiza ya uongo katika juhudi za kuwaingiza watu katika kuchanganyikiwa kwa kusingizia kuwa ni Roho Mtakatifu. Watu wengi hupokea kwa kudhani mambo haya yote ni ishara na ushuhuda wa kushuka kwa Roho Mtakatifu. Pia hudhani kwamba Roho Mtakatifu huja kwa sauti kama ya “Shwuihhh….” Kama ya upepo mkuu. Wanadanganyika na mapepo. Kuja kwa Roho Mtakatifu kama ilivyoandikwa katika Matendo kuliwezeshwa kwa kupitia imani katika Injili njema tu.
 
 
Imani ya Petro (1 Petro 3:21) ilikuwa ni sahihi kumwezesha kupokea Roho Mtakatifu ndani yake.

Kwa kuweka bayana tukio la kwanza la Pentekoste katika Matendo 2, Mungu anataka kuweka msisitizo wa ukweli kuwa Roho Mtakatifu alishuka juu yao kwa sababu walikuwa tayari wamekwisha amini Injili ya maji na Roho. Lakini watu mara nyingi hudhani Pentekoste ni wakati ule Roho Mtakatifu anaposhuka toka mbinguni kwa ishara zisizo za kawaida na tafrani za makelele.
Na ndiyo maana nyakati hizi katika mikutano ya uamsho inaaminika kwamba mtu aweza kupokea Roho Mtakatifu kupitia sala za kurudia rudia, kufunga kula au kuwekewa mikono. Matukio yasiyo ya kawaida kama vile kuwa na mapepo, kuanguka bila fahamu, kukosa fahamu kwa siku kadhaa au kutetemeka bila kujizuia hizi si kazi za Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu ni nafsi iliyo na utashi kamili na kamwe haidharau utu wa mwanadamu. Roho Mtakatifu hana tabia ya kumdhalilisha mtu kwa sababu yeye ni nafsi ya Mungu aliye na utashi akili na hisia. Huja juu ya watu pale tu wanapoamini maneno ya Injili ya maji na Roho (Matendo 2:38).
Petro alishuhudia kwamba Roho Mtakatifu alikuja juu ya wafuasi kama ilivyo tabiriwa na Nabii Joeli. Ilikuwa ni kutimizwa kwa ahadi ya Mungu iliyo sema kwamba Roho Mtakatifu atawashukia wale wote watakao pokea ondoleo la dhambi. Kwa maneno mengine kuwa na Roho Mtakatifu ndani huja kwa wale wanaoamini ukweli kuwa Yesu alibatizwa na Yohana na kusulubiwa ili kuwaokoa wanadamu na dhambi zao. Hotuba ya Petro ukijumuisha na unabii wa Yoeli, hutuonyesha kwamba yatupasa kujua kwanini Yesu alibatizwa, na kwa nini imetulazimu kuamini hili. Kwa kujua ukweli huu ndipo kunako pelekea Wakristo kumpokea Roho Mtakatifu.
Je, unaamini Injili hii njema ambayo Petro anayoshuhudia? (1 Petro 3:21) au bado wewe unaamini upuuzi na mazingaombwe ya imani zisizo na umuhimu kinyume na Injili njema? Je, unajaribu kumpokea Roho Mtakatifu kwa kupitia juhudi zako kwa kuweka kando mpangilio wa Mungu? Hata ikiwa mtu atamwamini Mungu na kufanya maombi ya toba kwa matumaini ya kutakaswa dhambi zake hakuna njia nyingine ya kuweza kumpokea Roho Mtakatifu zaidi ya kuamini injili ya majina Roho.
Je, bado unasubiri kumpata Roho Mtakatifu ndani yako huku ukiwa huna ufahamu wa injili ya maji na Roho? Je, wajua maana halisi ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani ambayo hupelekea Roho Mtakatifu kuja ndani ya moyo wako? Ni lazima ujue kwamba Roho Mtakatifu kuweza kuwa ndani yako inawezakana ikiwa tu unapoamini injili ya maji na Roho. Ukweli wa Roho Mtakatifu kuwa ndani yako unawezekana kwa wote wale watakaoamini Injili ya maji na Roho. Tunamshukuru Mungu kwa kutupatia Injili yake ya maji na Roho ambayo ndiyo pekee ituwezeshayo kumpokea Roho Mtakatifu ndani yetu.