Search

Sermões

Somo la 8: Roho Mtakatifu

[8-4] Wale walio na imani sawa na Mitume (Matendo 3:19)

(Matendo 3:19)
“Tubuni basi, mrejee ili dhambi zenu zifutwe zipate kuja nyaka za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana.”
 

Aina gani ya imani 
waliyokuwa nayo Mitume?
Waliamini katika mambo mawili ubatizo 
wa Yesu na damu yake 
msalabani.

Kwa kuangalia wafuasi wa Yesu Kristo kiwango cha imani zao walipokuwa na Roho Mtakatifu ndani yao ni tofauti kabisa na imani zao walipokuwa hawajawa na Roho huyo. Miili yao haikuonekana kuwa tofauti lakini baada ya kumpoke Roho Mtakatifu maisha yao yalibadilika kabisa kwa nuru ya Yesu Kristo.
Mji ninaoishi una milima na maziwa kwa mandhari nzuri. Kwa kuangalia mandhari hiyo nzuri naridhika na kuona sina la zaidi bali ni kumshukuru Bwana kwa uumbaji huu. Mng’ao wa maji yaliyo takasika huakisi jua na kuufanya moyo uridhike na hivyo ulimwengu unizungukao huonekana kama dhahabu.
Lakini zipo sehemu nyingine ambazo uzuri huu hujionyesha wenyewe. Zipo sehemu nyingine ambazo anga ni safi kabisa lakini maji chini ya jua huonekana kama dimbwi la tope. Hakuna nuru katika sehemu hiyo. Kwa kuangalia ziwa kama hili, namshukuru Mungu kwa Injili yake njema ambayo imetakasa dhambi zangu na kunipatia uwepo wa Roho Mtakatifu.
Kwa jinsi kina cha ziwa la tope kisivyoweza kuakisi mwanga hivyo ndivyo tulivyo mbali na nuru ya Mungu na kutokuwa werevu huku tukielekea tusiko kufahamu kutokana na asili yetu ya dhambi. Lakini Roho Mtakatifu akikaa ndani ya mioyo yetu tutaeleweka kuwa ni wana wa Mungu na hata kuongoza katika kufundisha watu Injili. Kwa kuwa tunaikubali nuru ya Yesu, basi tutang’ara bila shaka. 
Kwa jinsi hii pia baada ya kufufuka kwa Yesu, wafuasi wake walimpokea Roho Mtakatifu na kuwa watoto na Mitume wa nuru. Nuru ya Roho Mtakatifu ni baraka kuu kwa wale wote na hivyo watu wengi hutamani kumpokea Roho Mtakatifu.
 

Imani ya Mtume Paulo 

Ni imani ya namna gani Paulo alikuwa nayo? Paulo katika kukiri kwake kuwa alikuwa mwenye elimu na kufuzu chini ya Gamalieli aliyekuwa mmoja kati ya walimu mashuhuri wa sheria kwa nyakati hizo na pia kufundishwa kulingana na sheria za baba zake, bado hakuweza kuokolewa kwa dhambi zake na hivyo kuweza kuwa kati ya wanaomtuhumu Yesu, mwokozi wetu. Siku moja alikutana na Yesu akiwa njiani kuelekea Dameski na hatimaye kuwa Mwinjilisti wa Injili ya Yesu. Alikuwa na imani ya kuwa Yesu Kristo ndiye mwana wa Mungu, alikuja ulimwenguni na kutoa damu yake Msalabani ili kuibeba hukumu ya dhambi hizo. Kwa maneno mengine alikuwa na imani ya msamaha wa dhambi ndani ya moyo wake.
Wafuasi wa Yesu waliamini ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani ilikuwa ni kwaajili ya kuwasamehe dhambi zao zote. Paulo alishiriki imani hiyo na wafuasi hao na hivyo alivyokolewa kwa dhambi zote.
Paulo alisema katika Wagalatia 3:27 “Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo” na kukiri imani yake katika ubatizo wa Yesu kuwa ndio wokovu wake. Pia Petro alisema katika Petro 3:21 “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo unaowaokoa ninyi pia siku hizi (siyo kuweka mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu) kwa kufufuka kwa Yesu Kristo” na alielezea juu ya Injili njema ya ubatizo wa Yesu kwa kupitia kifungu hiki. Wafuasi wa Yesu waliamini kwamba ubatizo wa Yesu kwa Yohana ulitakasa dhambi zao zote ulimwenguni. Walisamehewa dhambi zao na hivyo hakuwa tena chini ya laana ya sheria kwa kuwa wameamini ukweli huu.
Waliamini yote mawili ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Ni ushahidi tosha kwamba imani hii ilikuwa ni muhimu kwa kuweza kuwa mtume bora. Katika Matendo 1:21–22 inasema “Basi katika watu waliofuatana nasi wakati wote Bwana Yesu alipokuwa akiingia na kutoka kwetu kuanzia tangu ubatizo wa Yohana hata siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu inapasa mmoja wao awe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi”. Ili uwe mfuasi wa Yesu kwanza lazima uamini ubatizo wa Yesu kwa Yohana. 
Ukweli tunaouhitaji ili tuweze kusamehewa dhambi zetu ni imani katika ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. “Maana ninyi nyote mlibatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo” (Wagalatia 3:27). Hivyo Paulo pia aliamini ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani.
Hebu tuone Tito 3:5 “Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi, bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu.” Hapa tafsiri ya “Kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili kwa kufanywa upya” maana yake ni kwamba dhambi zote za ulimwengu zilitakaswa pale Yohana alipombatiza Yesu. Kwa jinsi hiyo ikiwa unataka kusamehewa dhambi zako, basi unahitaji kuamini Injili njema ambayo inasema dhambi zako zilitwikwa kwake Yesu kwa kupitia ubatizo wake kwa Yohana. Sababu ya Yesu kusulubiwa na kumwaga damu yake hadi kufa ni kwakuwa alikuwa amekwisha beba dhambi zote kwa kupitia ubatizo alioupokea toka kwa Yohana. Kwa kuamini ukweli huu kunatosha kupokea moja kwa moja uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yako. Paulo pia alikiri kwamba aliamini ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani.
Hebu tuangalie Waebrania 10:21-22, inasema “na kuwa kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya tumeoshwa miili kwa maji yake safi”. Hapa “tumeoshwa miili kwa maji safi” maana yake ubatizo wa Yesu kwa Yohana ambao ulitakasa dhambi za wanadamu. 
Hivyo Agano la Kale na Jipya katika yote tutaweza kupata sehemu ya kiini cha Injili njema ambamo ni ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani. Nawe pia imekupasa kushiriki imani hii ya Paulo.
Leo hii, Wakristo walio wengi humwamini Yesu katika njia panda pasipo kujua kwamba wakati Yohana alipombatiza Yesu, dhambi zote za ulimwengu zilitakaswa. Baadhi ya Wanatheologia huwaasa watu wabatizwe ili wapate kusamehewa dhambi zao. Tamko hili hufanywa labda pasipo kujua ukweli na juu ya Injili ya maji na Roho kama ilivyoandikwa katika Biblia. Dhambi zetu kamwe hazitoweza kufutwa kwa namna ya ibada ya ubatizo wa maji, bali tu kwa imani katika ubatizo wa Yesu na damu yake hututakasa sisi sote kwa dhambi zetu zote. Ni wale tu wanaoamini Injili njema ndiyo wanaosamehewa dhambi zao. Na kwa kuamini damu ya Yesu pekee wamekwisha jiwekea hukumu yao. Ni wale tu wenye imani hii ndiyo watakaoweza kupewa kipawa cha Roho Mtakatifu. 
“Natukaribie wenye moyo wa kweli kwa utimiilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamira mbaya tumeoshwa miili kwa moyo safi” (Waebrania 10:22). Mwandishi wa Waebrania anatueleza kukaribia mbele ya Mungu na moyo wa kweli kwa ukamilifu wa imani ya Injili njema.
Nyakati hizi, Wakristo wanatumaini la kweli katika kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu huweka makazi kwa wale tu ambao dhambi zao zimekwisha samehewa. Wengi hakika hawaelewi hili hivyo hutamani kumpokea Roho Mtakatifu pasipo kuamini Injili njema ya ubatizo wa Yesu na damu yake. Wale wote wenye kumwamini Yesu huku hawaamini ubatizo wake, na damu yake msalabani kamwe hawatoweza kupokea karama ya Roho Mtakatifu. Sababu ni kwamba hawana mioyo safi.
Paulo aliamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani na hivyo alimpokea Roho Mtakatifu. Na zaidi ya yote, alieneza imani hii na hatimaye alishitakiwa kwa kuwa mzushi. Lakini kwa kuwa Roho Mtakatifu alikuwa ndani yake, aliweza kueneza Injili ya maji na Roho hadi mwisho wa maisha yake. “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu” (Wafilipi 4:13). Nashukuru kwa uwepo wa Roho Mtakaktifu ndani yake, kwani alimtumikia Mungu na kuishi chini ya ulinzi wa Roho Mtakatifu hadi alipokwenda mbele ya Mungu. Wale tu wenye imani sambamba sawa na ya Paulo ndiyo watakao mpokea Roho Mtakatifu.
Hebu tuangalie imani ya Paulo katika Wakolosia 2:12 inasema “mkazikwa pamoja naye katika ubatizo, na katika huo mkafufuliwa pamoja naye kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu”. Alisamehewa dhambi zake zote kwa kumwamini Yesu, aliyebatizwa na Yohana.
 

Ukristo umebadilikaje tangu nyakati za kale?

Sasa, hebu tuone ushuhuda wa dada mmoja ambaye alikuwa mfuasi baada ya kumpokea Roho Mtakatifu katika Yesu Kristo. 
“Nilianza kuzeeka bila kuwa na mtoto, hivyo ili niweze kupokea baraka ya Mungu kwa kupitia maombi nilitangatanga katika Makanisa. Hata nilipokuwa mwenyewe nyumbani niliomba kupata mtoto kwa saa moja hadi tatu hivyo sehemu hii ya udini ikawa katika maisha yangu kila siku. 
Nilipoendelea na tabia hii ya kidini katika maisha yangu, nilikutana na mama mmoja wa makamo akaniambia, ikiwa nahitaji kumuomba Mungu mtoto itanipasa kuwekewa mikono naye. Hapo awali nilisikia juu ya mama huyo kuwa ni mtumishi wa Mungu na hivyo nilimkubalia kuniwekea mikono juu ya kichwa changu. Punde nilihisi jambo lisilokuwa la kawaida ndani yangu ulimi wangu ulianza kuchezacheza na kuanza kunena lugha ya ajabu na nilihisi jambo geni na joto lilinipanda. Nililichukulia jambo hili kuwa nimempokea Roho Mtakatifu na ndiyo jibu langu kwa Mungu. 
Mwanamke huyo aliyeniwekea mikono alionekeana kuwa na kipawa toka kwa Roho Mtakatifu, na aliweza kutoa Unabii na kuponya. Hakuwahi kupokea elimu ya neno la Mungu lakini aliweza kutumia nguvu ya Roho Mtakatifu na aliweza kuwasaidia Wachungaji wengi na Wasomi katika kumpokea Roho Mtakatifu kupitia tendo la kuwekea mikono. 
Tokea hapo na kuendelea nilianza kuhudhuria mikutano na mojawapo uliitwa 3 “Vuguvugu la Uamsho / Kufanyizwa upya” Wakati mojawapo ya maombi yangu katika mkutano huo, nilihisi kutetemeka mwili mzima na moyo wangu ukajawa na upendo kwa Mungu na jirani zangu. Hili lilitokea kwa watu siku hiyo na wote walianguka kwa kuzimia na kuanza kunena kwa lugha. Palikuwepo na watu wenye mapepo, na kiongozi wa mkutano alikemea pepo hawa. Dhumuni la vuguvugu la Uamsho/Kufanyizwa upya lilikuwa ni kuwafanya watu waamini kuwa Roho Mtakatifu ndiye aliye kuwa afanyaye mambo kama vile kutetemeka kutoa unabii kukemea pepo na kunena kwa lugha. Ingawa katika yote haya bado nilihisi kuwa na dhambi moyoni mwangu na hivyo zilinifanya niwe mwoga na aibu.
 
 
3 Uamsho/Kufanyizwa upya ni tendo la asili na ni sehemu muhimu katika maisha ya Mkristo, na huleta ukomavu wa kiroho, ni ushahidi juu ya tunda la Roho. Lakini kwa miaka ya karibuni baadhi ya vuguvugu zimetafsiri upya juu ya neno “Uamsho/kufanyizwa upya” hata kupelekea kutobeba tena maana kamili ya ukomavu wa Kiroho ambayo ni hatua iliyo ya kimaandiko. Uamsho/Kufanyizwa upya kwa tafsiri ya watu hawa kunako pelekea hisia isiyo tawalika, kunadhihirika kwa kila aina ya matukio yanayotia mashaka na kuandamana na mafundisho ya ziada nje ya Biblia au yasiyo ya Kibiblia kabisa zikiwa pamoja na tabia au matendo.
Haya ni baadhi ya mafundisho na matukio yenye utata yanayo sambazwa na vuguvugu za Uamsho/kufanyizwa upya: kusisitiza zaidi matukio ya karama kinyume na maandiko, matukio ya kimazingara, mafundisho ya ulaghai, unabii wa kilaghai, ishara na maajabu ya kiulaghai na kadhalika. Hata hivyo hatari kubwa zaidi ya vuguvugu za Uamsho/kufanyizwa upya ni kwamba, wamesababisha watu wengi kutoelewa ukweli juu ya kumpokea Roho Mtakatifu ndani yao na hivyo kutupilia mbali injili njema.
 
Hivyo kila nilipo fanya maombi, nilizama zaidi ili niweze kusuluhisha tatizo la dhambi hizi. Nilikiri kuwa mwenye dhambi lakini nje watu walinichukulia kama malaika. Nilidhani kuwa ni mwenye imani njema lakini nilikosea. Ikiwa nisingeweza kugundua makosa yangu nisengeweza kuwa na wasaa wa kumpokea Roho Mtakatifu.
Baada ya hapo nilikutana na wale waenezao Injili ya maji na Roho na hatimaye nilipokea msamaha wa dhambi zangu zote kwa kuamini neno la Mungu. Leo hii mimi ni mwenye furaha naamini Injili ya maji na Roho na nimepokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Namshukuru Mungu. Na natamani Wakristo wote ulimwenguni wangeliamini Injili njema na kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu. Namshukuru Bwana.”
Hapa tunajifunza kwamba ilituweze kumpokea Roho Mtakatifu tunahitaji Injili ya maji na Roho. Ikiwa unataka kusamehewa dhambi zako zote ni lazima uwe na imani katika ubatizo wa Yesu kwa Yohana hebu tuone katika Waefeso 4:5 “Bwana mmoja, imani moja ubatizo mmoja”. Hapa inasema kwamba yupo Bwana mmoja tu na ubatizo mmoja ambao tunauamini. Yatupasa kuamini ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani ili tupokee uwepo wa Roho Mtakatifu. Ikiwa sivyo, basi Roho huyo kamwe hawezi kuwepo ndani yetu.
Hapo awali paliondokea watu fulani waliofundisha na kuamini kwamba vuguvugu la utakaso na usafi lingeweza kuwasaidia kumpokea Roho Mtakatifu hata hivyo,je, unadhani Roho Mtakatifu hufanya makazi ndani yetu ikiwa tutajiunga katika mavuguvugu kama hayo? Je, wewe nawe umempokea Roho Mtakatifu kwa kuwa katika vuguvugu la utakaso na usafi? Ikiwa ingeliwezekana, basi ungelikuwa mwenye busara kuishikilia imani. Lakini ikiwa Roho Mtakatifu, alikuja juu yako kwa sababu hiyo, basi Yesu asingelihitaji kushuka ulimwenguni na kutuokoa na dhambi zetu na asingehitajika kubatizwa na Yohana wala kusulubuwa msalabani.
Kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ni karama itokanayo na imani katika Injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake, ambayo huleta msamaha wa dhambi zako. Kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani ni karama inayotunukiwa kwa wale wote wanaopata msamaha wa dhambi zao kwa kutakaswa kupitia Injili ya kweli.
Nyakati hizi kati ya wale wanaojitumbukiza katika vuguvugu za Uamsho/Kufanyizwa upya, wapo baadhi wanaoamini kwamba sala za toba kwa kujitoa zitaweza kuwasaidia kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu. Wao husema kwamba ingawa mtu ataweza kuwa na dhambi moyoni, basi ikiwa atafanya maombi ya toba, hatimaye ataweza kumpokea Roho Mtakatifu.
Vuguvugu la Karama za Pentekoste (Pentecostal Charismatic Movement) ambalo limesambaa ulimwenguni pote lilianza huko Marekani takribani miaka ya 1800. Vuguvugu hili lilikuja kati ya kipindi cha kabla ya Mapinduzi ya Viwanda (Industry Revolutaion) wakati maadili ya tabia za watu yalipotoka. Vuguvugu hili lilifika kilelele cha mafanikio pale mioyo ya watu ilipochoka kabisa kutokana na mfadhaiko mkuu wa maisha duniani. Tokea kipindi hicho imani itokanayo na neno la Mungu ilishuka na ndipo vuguvugu la madhehebu mapya lilianza kuchomoza. Mathalani vuguvugu la Karama la Kipentekoste (Pentecostal Charismatic Movement) ndilo lililolenga katika swala la kumtambua Roho Mtakatifu (Mungu) kwa hisia za kimwili - kushuhudia kazi za Mungu kwa macho na kushuhudia nguvu ya maneno ya Mungu kwa mwili na akili.
Lakini pigo la kuangukia katika vuguvugu hili ni kwamba huwavutia wanaoamini na kuwapeleka mbali na maneno ya Mungu na hata kuwafanya kuwa katika dini yenye kuhangaikia baraka za kimwili tu. Matokeo yake, wafuasi katika vuguvugu hili jipya huanza kueneza imani za kishirikina (Shamanism). Hata leo, wale wote waliojizamisha katika vuguvugu la karama za Kipentekoste huamini kuwa ikiwa mtu atamwamini Yesu atatajirika kifedha na kimali magonjwa yake yataponywa atafanikiwa katika kila jambo, atampokea Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha na hata kuwa na nguvu ya kuwaponya wengine. Vuguvugu hili, limesambaa ulimwenguni pote na limekuwa ni kikwazo kwa imani za watu kuelekea Injili njema na uwezo wa kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani.
Ukristo wa leo umechipuka tokana na imani za Luther na Calvin takribani miaka 500 iliyopita. Lakini ndani ya mipaka ya Ukristo somo la Kibiblia linalohusu uwepo kwa Roho Mtakatifu halikuweza kusimikwa kwa umadhubuti. Tatizo ni kwamba, tokea mwanzo wa Ukristo wa kisasa, Wakristo wengi walimwamini Yesu pasipo kugundua umuhimu wa ubatizo wake na kifo chake msalabani. Mbaya zaidi watu walianza kusisitizia mafundisho potofu ya Kikristo na hata kutilia mkazo matukio ya kimwili peke yake. Wakristo wote imewapasa kuamini Injili njema ambayo inasema kwamba Yesu alibatizwa na Yohana ili kubeba dhambi hizo. Hakika imani hii itawawezesha kumpokea Roho Mtakatifu.
Leo hii sababu ambayo Imeufanya Ukristo kuwa duni ni kwamba watu wamejaribu kuupuzia ukweli juu ya ubatizo wa Yesu toka kwa Yohana na damu yake msalabani. Maana yake ni kuamini Injili ya maji na Roho. Ikiwa unahitaji kumpokea Roho Mtakaktifu basi amini kwamba Yohana alimbatiza Yesu, dhambi zako alimtwika Yesu na hivyo damu yake alikuwa ni hukumu na msamaha wa dhambi zako zote. Ndipo utakapo mpokea Roho Mtakatifu.
Wakristo huamini damu ya Yesu tu kama ndiyo Injili ya ukombozi. Lakini je, kati yenu mnao amini damu ya Yesu tu mtaweza kuwa huru kwa dhambi? Je, mtaweza? Ikiwa unadhani utaweza, labda unaufahamu usio sahihi juu ya ukweli wa ubatizo wa Yesu. Katika hilo bado utakuwa na dhambi moyoni mwako. Ni pale tu utakapounganisha ubatizo wa Yesu na damu yake kwa pamoja kuwa na imani moja ndipo atakapoweza kuokolewa kwa dhambi zako zote na hatimaye kumpokea Roho Mtakatifu. Biblia inasema kwamba hii ndiyo Injili pekee ya kweli inayotuwezesha kuushindwa ulimwengu. “Kwa maana wako watatu washuhudiao duniani, Roho na maji na damu na watatu hawa hupatana kwa habari moja” (1 Yohana 5:9). Hivyo tuelewe kwamba, nia ya Mungu katika kutuokoa kwa dhambi zetu zote, aliwezesha Yohana ambatize Yesu na baadaye kumfanya asulubiwe.
Sababu kwa nini Wakristo wengi hawana msamaha wa dhambi ingawa wanamwamini Yesu? Ni kwamba hawaiamini Injili njema iliyo kamilishwa kwa ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Wale wote wenye kuamini mambo haya mawili watasamehewa dhambi zao na kumpokea Roho Mtakatifu.
Wakati watu wanapogundua kuwa dhambi zao zimetakaswa mioyo yao huwa na amani na kufurika kama maji yaliyo tuama. Wakati Roho Mtakatifu anapoweka makazi ndani ya moyo wa mtu, amani huwa kama mto utiririkao ndani toka nje ya moyo wake. Tunakutana na Bwana wetu kwa kuamini katika ukweli huu na kutembea na Roho huku tukieneza Injili ya kumpokea Roho Mtakatifu. Toka tulipo amini Injili ya maji na Roho, maisha yetu yamekuwa na amani na mioyo yetu imekuwa na furaha halisi. Hatutaweza kamwe kuiacha Injili hii njema. Roho Mtakatifu siku zote yumo ndani ya mioyo yetu, kutuwezesha kueneza neno lake na kuwezesha watu wanoamini neno hilo kumpokea Roho Mtakatifu.
Kwa kuwa tuliamini Injili njema ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani, tulipokea baraka ya Roho Mtakatifu. Ni muhimu watu ulimwenguni waanze hatua ya kuamini neno la Mungu lisemalo kwamba Yesu alibatizwa na Yohana ilikubeba dhambi zote za ulimwengu na hivyo alikufa msalabani ili kuhukumiwa kwa dhambi zao. Wanapofanya hivyo, hatimaye humpokea Roho Mtakatifu.