Search

Sermões

Somo la 8: Roho Mtakatifu

[8-16] Mikakati ya wanao mpokea Roho Mtakatifu (Isaya 61:1-11)

(Isaya 61:1-11)
“Roho ya Bwana Mungu i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema, amenituma ili kuwaganga walio vunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao walio fungwa habari za kufunguliwa kwao. Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao; kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na Bwana ili atukuzwe. Nao watajenga mahali pa pale palipoharibiwa, watapainua mahali palipo kuwa ukiwa zamani, watatengeneza miji iliyoharibiwa mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi. Na wageni watasimama na kulisha makundi yenu na watu wa kabila nyingine watakuwa wakulima wenu, na watunzaji wa mizabibu yenu. Bali ninyi mtaitwa makuhani wa Bwana wetu watawaiteni wahudumu wa Mungu wetu; mtakula utajiri wa mataifa na kujisifia utukufu wao. Badala ya aibu yenu mtapata mara dufu, na badala ya fedheha wataifurahiya sehemu yao basi katika nchi yao watamiliki mara dufu; furaha yao itakuwa ya milele maana mimi Bwana naipenda hukumu ya haki nauchukia wivi na uovu, nami nitawalipa malipo katika kweli, nitaagana nao agano la milele. Nakizazi chao kitajulikana katika mataifa na uzao wao katika kabila za watu; wote wawaonao watakiri yakuwa wao ni kizazi kilichobarikiwa na Bwana. Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki kama bwana harusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu, maana kama nchi itoavyo machipuko yake na kama bustani ioteshavyo vitu vilivyopandwa ndani yake ndivyo kwangu Mungu atakavyo otesha haki na sifa mbele ya mataifa yote.”
 

Upi ni mkakati wa wa 
wale wote walio mpokea 
Roho Mtakatifu?
Ni kuihubiri injili ya maji na 
Roho kwa watu wote 
ulimwenguni.

Mtu aliye kwisha mpokea Roho Mtakatifu yampasa kufanya nini? Imempasa kuihubiri injili ya maji na Roho kwa watu wote. Mungu ameweka dhamana ya injili njema yakuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho mikononi mwa wale wote walio kwisha kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu.Wale wote walio kwisha pokea msamaha wa dhambi zao mbele ya Mungu hupokea Roho Mtakatifu. Sasa basi kwanini unadhani Mungu ametunuku karama ya Roho Mtakatifu kwao?
Kwa kuwapa uhakika wa mwisho ya kwamba alikwisha wafanya kuwa wana kwake. Mungu huwapa zawadi hiyo ya Roho Mtakatifu. Pia huwasaidia katika kumshinda shetani. Huwafanya wale wote walio kwisha samehewa dhambi zao na ambao wamekisha pokea uwepo wa Roho Mtakatifu kufanya yafuatayo.
 

Huwawezesha kuihubiri habari njema kwa maskini.

Ipi ni habari njema kwa maskini? Ni injili ya maji na Roho. Mungu anawapa maelekezo wale wote walio pokea uwepo wa Roho Mtakatifu kuihubiri injili njema kwa maskini. Wale wote walio mpokea Roho Mtakatifu kwa kuwa tayari wanatumaini la mbinguni, kamwe hawawezi kuridhika na mambo ya dunia hii.
Mungu huwatunukia injili ya maji na Roho maskini na kuwasamehe dhambi zao. Pia anawatunukia uwepo wa Roho Mtakatifu na kuwaruhusu katika kuingia, ufalme wa milele. Mungu aliwaamuru wenye haki kuihubiri injili ya maji na Roho kwa maskini. Pia huwashawishi kueneza imani ya Mungu na Yesu. Sababu ya Mungu kumleta Roho Mtakatifu ilikuwa ni kuihubiri injili njema kwa wingi katika ulimwengu wa maskini.
 

Hutumwa kuponya mioyo iliyovunjika.

Ni kwanamna gani Bwana huponya fikra zetu? Huponya mioyo iliyovunjika kwa injili ya maji na Roho. Wapo watu wengi walio vunjika mioyo. Kwao maisha hayana thamani, na haki zao binafsi zime haribika. Wana maisha ya unyonge na uchungu kwa sababu ya dhambi zao. Hivyo mara kadhaa huteswa kwa wasi wasi wa maisha. Watu wote hutamani kuishi maisha ya rehema na kutaka kufurahiya ustawi wa miili yao na roho zao, lakini hili halitokei kwa urahisi sawa na pale ambapo mtu anapoibiwa mali zake na majambazi.
Kwa upande mwingine pia wale walio na dhambi mioyoni mwao huendelea kuibiwa haki yao yote na hatimaye kwenda motoni kwa sababu ya dhambi zao. Na ndiyo maana Bwana huku akiwahurumia walio vunjika moyo, anatuamuru nasi kuhubiri injili njema kwao. Ni kwa maneno gani Mungu huwaponya? Huwaponya kwa injili njema ya maji na Roho. Huponya mioyo iliyo vunjika na pia kuwatunukia uzima wa milele.
 

Kuwa tangazia uhuru mateka wa dhambi.

Hutoa uhuru kwa mateka. Hii inamaana gani? Maana yake ni kwamba, Mungu amekwisha ziweka huru roho zote za watu tokana na dhambi zote za ulimwengu. Aliwapa jukumu hili wale wote ambao tayari wamekwisha kumpokea Roho Mtakatifu, na hivyo wataweza kusaidia kuwaweka huru wengine tokana na dhambi zao.
Mwanadamu ana mwili na Roho. Na mwili wake na roho yake huishi huku zikiwa zimefungwa na laana ya dhambi na sheria. Hawezi kufanya chochote bali ni kuishi akiwa mfungwa wa dhambi bila kujali kama anamwamini Mungu au hapana. Akiwa amezaliwa na dhambi hawezi kujizuia kutenda dhambi hizo. Kwa jinsi hii hatima yake ni kuendelea kuwa mtumwa wa dhambi wakati wote wa uhai wake. Maisha yake katika njia hii hatima yake ni kuangamia.
Na hii ndiyo maana huishi maisha haya bila kukwepa huku akiwa anajisikitikia kutokana na udhaifu wake ambao umempelekea kuwa katika hali hiyo. Mungu amewapa Roho Mtakatifu wale wote ambao hawawezi kujizuia kutenda dhambi ambao hatima yao ni kifo ili waweze kuihubiri injili njema kwa wale wenye dhambi na kuwaweka huru wafungwa tokana na dhambi zao zote.
 

Kuwafariji wote waliao.

Mungu amewapa nini wale wote waliao? Amewapa injili ya msamaha wa dhambi. Mungu huwatuliza watu wote wa dunia hii wanao lia. Amemleta Yesu Kristo ulimwenguni ili kuwasamehe wanadamu kwa dhambi zao na kumtwika dhambi zote za ulimwenguni juu yake, alibatibwa na Yohana na kufa msalabani. Hivi ndivyo Mungu alivyo tutakasa kwa dhambi zetu. Kwa jinsi hii Mungu alituokoa tokana na dhambi zote za ulimwengu.
Bwana wetu huwafariji wale wote waliao kwa kuwajulisha juu ya injili njema ya maji na Roho. Kwa kufanya hivyo, huwabariki wale wote wanao teseka kutokana na imani isiyo kamilika. Huwaongoza wale tu walio na Roho Mtakatifu katika kuihubiri injili njema, kuponya mioyo iliyo vunjika na kuwaweka huru wafungwa wa dhambi.
Dhumuni la kuwepo kwetu hapa duniani ni kuweza kusamehewa na Bwana na ndipo tuihubiri injili njema kwa wale walio fungwa na dhambi na kuihitaji faraja ya kuwekwa huru na dhambi. Mungu anatuambia ya kwamba ingawa maisha yetu ni mafupi bado niyathamani. Kwa Mungu kutayarisha msamaha wa dhambi na baraka ya ajabu kwa wanadamu, ni ushahidi tosha wa ukweli huu.
Bwana wetu pia amewatunukia taji la utukufu wale wote wenye huzuni waliao. Maana yake ni kwamba, wenye dhambi wamesamehewa dhambi zao kwa shukrani ya ubatizo wa Yesu na kwa njia hiyo wataweza kuingia Ufalme wa Mbinguni. Ikiwa mtu atasamehewa dhambi zake hufanywa upya mawazo yake na kufikia kuikubali baraka hii ya ajabu. Bwana wetu humvika taji ya utukufu. Amewapaa wenye dhambi injili ya maji na Roho na kuwafanya wale waiaminio inijili hiyo kuwa wana kwake. Wale waiamini injili hii njema hufanywa wajisikie wenye furaha badala ya huzuni.
Kama ilivyo watu wote wanao zaliwa na kufa wakiwa na kilio, furaha kwao ni ya kipindi maalumu hivyo fikra zao mara zote zimejaa huzuni. Hata hivyo Mungu hukutana nao na kuwawezesha kuzaliwa upya kwa tumaini na furaha. Kwa upande mwingie, wale walio zaliwa upya mara ya pili kwa kuiamini injili njema huishi maisha mapya na kuwa na mikakati mipya. Kwanyongeza, wanauwezo wa kufanya kile Mungu anachokihitaji ambacho ni kuihubiri injili ya maji na Roho kwa wenye dhambi wote ulimwenguni, wakiondoshea mbali huzuni zilizomo katika mioyo ya watu na badala yake kuwawezesha kufarijika katika aina zote za furaha na fanaka.
Wale wote walio kwisha samehewa dhambi zao humrudishia Mungu utukufu. Huwaelekeza wenye haki kuihubiri injili njema. Huwaambia kuhubiri kwamba yeye ni nani, ni injili gani aliyotupatia na jinsi utukufu wa Ufalme wa Mbinguni ulivyotayarishwa kwa ajili yetu. Tunaweza kuuona utukufu wa Mungu katika wale wote waliokwisha samehewa dhambi. Wale walio na huzuni katika maisha yao kabla ya kujazwa na Roho Mtakatifu, sasa wataweza kuwa na baraka ya furaha. Wale walio fungwa na dhambi, sasa watajisikia faraja ya uhuru, na wale walio ishi maisha ya siyo na thamani wataweza kuishi maisha ya haki. Hayo yote huonyesha utukufu wa Mungu. Mungu huwachukulia wenye haki kuwa ndiyo watakao jenga upya magofu, kujenga upya makazi yaliyoachwa na kurekebisha miji iliyo haribiwa.
Ukweli ni kwamba, injili hii njema ya maji na Roho ndiyo iliyokuwa ikihubiriwa na mitume katika nyakati zile za kanisa la mwanzo. Yesu alitumwa ulimwenguni takribani miaka elfu mbili iliyopita. Injili hii njema ya maji na Roho ilihubiriwa ulimwenguni hadi kufikia miaka 300 BK. Injili inayo hubiriwa na wenye haki leo hii ni sawa na injili ile ya Roho Mtakatifu, ambayo Mitume waliihubiri nyakati zao. Hata hivyo katika nyakati za karne ya 4 dola ya Kirumi ilipofanya ukristo kuwa dini ya kitaifa na hivyo kuwafanya raia wake wawe na uhuru wa kidini, ndipo hapo injili ya ubatizo wa Yesu ilipo fifishwa hatua baada ya hatua na kupotea. Ilikuwa katika kipindi hiki baadaye ukristo ukawa dini iliyoanzishwa ikiwa na ustawi na hivyo wale watu wote walio ihubiri injili ya kweli walitoweka.
Kwanini imani ya wale walio amini na kuhubiri ukristo wa kweli katika injili ya kweli ilibadilika? Baada ya ukristo kuwa dini ya kitaifa katika utawala wa Kirumi, wakristo wakawa huru tokana na aina zote za maonyo na mipaka na hivyo kuweza kufurahia nafasi na fursa sawa na wakazi wengine katika utawala wa Kirumi. Wakristo walipata kibali hata cha kuoa katika koo za watawala wa Kirumi. Napia waliweza kuingia katika huduma za kiserekali. Kwasababu ya nafasi hizi, imani zao zilipungua toka imani ya ufufuko hata kufikia kuwa udini mtupu. Tokea hapo injili njema ya maji na Roho ili anza kutoweka kabisa na kutokomea katika ina ya Ukristo wa maadili ya kidunia ulioshamiri sana.
Sasa Mungu anatuamuru sisi Wakristo wa leo katika kipindi chake cha kurudi mara ya pili, kuweza kuihubiri injili hii njema ya maji na Roho ambayo ilitupiliwa mbali kwa muda wote huo mrefu, na kwa jinsi hiyo kuweza kuokoa wanadamu wote kwa dhambi zao. Mungu ameileta upya tena injili hii njema ya maji na Roho ambayo ilihubiriwa nyakati za mitume. Injili ya nyakati za mitume ilikuwa ni injili njema ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Anatuita sisi ili tujenge upya magofu ya miji. Anatufanya tuelewe nakuiamini injili hii njema ya maji na Roho na hivyo katufanya kuwa wakulima katika shamba la mizabibu. 
Mungu ametupatia jukumu sawa kama alilowapa mitume wa kwanza. Amekufanya wewe na mimi kuihubiri injili halisi ya maji an Roho. “Roho ya Bwana i juu yangu kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema.” Mungu amewafanya wale waliokwisha kumpokea Roho Mtakatifu kuihubiri injili na kutupa Roho Mtakatifu.
Mungu ametuvika shada la maua, akiondoa huzuni zote na kutuvika vazi la shangwe kwa kutupa fanaka juu yetu. Wale walio na Roho Mtakatifu moyoni mwao hupanda mbegu za injili njema kwa wengine ili waweze kumpokea. Nandipo pia nao wataweza kuikubali injili iliyoletwa na Bwana huku wakisamehewa na hatimaye humpokea Roho Mtakatifu. 
Tumekuwa watenda kazi wa Mungu. Mimi na wewe tumebarikiwa na utukufu wa Ufalme wa Mbinguni. Hata hivyo Mungu amewafanya wale wasio na Roho Mtakatifu kuwa vipofu ili wasijue, kuona au kuelewa injili hii njema. Hawa wanachoweza ni kuwafanya wengine kumwamini Yesu kwa jina tu lakini kamwe hawatoweza kuwaongoza kumpokea Roho Mtakatifu. 
Bwana amekwisha fanya mambo yafuatayo kwa kupitia wale walio na Roho Mtakatifu. Amewafanya waihubiri habari njema kwa maskini na hivyo kuwaponya walio vunjika mioyo kwa injili ya maji na Roho. Pia amewatangazia mateka wa dhambi uhuru wa kweli katika wokovu, na kuwafariji wale wote wenye huzuni kwa injili njema ya maji na Roho. Amewaweka huru wale waliofungwa kwa dhambi kwa sababu ya udhaifu wao huku akiwatangazia furaha na tumaini lishukalo mbinguni.
Kwa kuyafuata haya, Roho Mtakatifu aliyeweka makazi ndani yetu hutufanya tuihubiri habari njema ya maji na Roho kwa watu wote. Yesu Kristo aliwaeleza wale wote waliokwisha samehewa dhambi zao na kumpokea Roho Mtakatifu ndani yao kwamba, watumike katika kuwaokoa wenye dhambi toka na dhambi zao. Mungu huwapa mamlaka wale walio na uwepo wa Roho Mtakatifu kuwa wasimamizi wa mipango atakayo kutekeleza. Huwafanya wenye haki kutenda kazi yake. Sisi ni watenda kazi wake tulioteuliwa tukiwa waangalizi katika shamba lake la mizabibu, kanisa la Mungu. Sisi ni watumwa kwake. Mungu ametupatia baraka hii ya ajabu.
Tunagundua udhaifu wetu pale tuanapoangalia miili yetu. Lakini kwakuwa Mungu hutenda kazi nasi basi tunamtumaini yeye na hata kuendelea kuwa watumishi wake kwa amani. Tunatumaini kuwa Mungu atatenda mambo makuu kwa kupitia sisi na kusambaza utawala wake kwetu.
Mungu ameamua kujenga upya ngome ya injili katika miji iliyo na magofu. Alituahidi ya kwamba atajenga upya mabaki na kurudishia miji iliyobomolewa. Naamini kwa dhati patatokea uamsho wa injili kwa mara nyingine tena duniani pote.
Kwa hili, hata hivyo si kwa mapenzi yangu. Naamini hivyo kwa sababu ni lazima itatokea. Bwana wetu amewafanya wale wote walio na Roho Mtakatifu kuihubiri injili njema ulimwenguni pote. Amemtuma mwana wake kuja duniani na kuitimiza injili, hivyo naamini mapenzi yamefanikiwa kwa kupitia sisi tulio na Roho Mtakatifu. Wale wanaoiamini injili hii njema ndiyo watakao uona utukufu wa Mungu. Haleluya!