Search

Sermões

Somo la 8: Roho Mtakatifu

[8-17] Yatupasa tuwe na imani na tumaini katika Roho Mtakatifu (Warumi 8:16-25)

(Warumi 8:16-25)
“Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu, na kama tu watoto basi tu warithi, warithi wa Mungu warithio pamoja na Kristo; naam tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwasi kitu kama utukufu ule utakao funuliwa kwetu. Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiyari yake ila kwa sababu yake yeye aliye vitiisha katika tumaini. Kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika ulimwengu wa uharifu hata viingie katika huru na utukufu wa watoto wa Mungu. Kwa maana twajua yakuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vinauchungu pamoja hata sasa. Wala si hivyo tu ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho sisi tunaugulia katika na fasi zetu, tukikukutazamia kufanywa wana yaani, ukombozi wa mwili wetu. Kwa maana tuliokolewa kwa taraja, lakini kitu kilicho tarajiwa kikionekana hatuna taraja tena. Kwa maana ni nani anayekitaraji kile akionacho? Bali tukitarajia kitu tusichokiona twakingojea kwa saburi.”
 
 
Kwanini wenye haki wanalo 
tumaini katika Roho Mtakatifu?
Kwa sababu sisi tulio zaliwa upya ndiyo tutakao 
miliki mbingu mpya na nchi mpya huku wale 
ambao bado hawajazaliwa upya mara 
ya pili wataangamia katika 
mwisho wa dunia hii.
 

Sasa ni wakati usio na tumaini.

Je, lipo tumaini la ulimwengu wa leo? Hapana Hakuna. Lipo kwa Yesu tu. Sasa ni wakati usio tabirika na kukosa matumaini. Kila kitu kinabadilika kila siku na kwa kasi watu wanajaribu kwa bidii kwenda sambamba na badiliko yaendayo kasi. Hawatafuti ukweli wa kiroho au hata kuhusika na faraja ya kiroho. Badala yake wanahangaikia kuzuia kushindwa na kuishia kuwa watumwa wa ulimwengu.
Nafasi za kazi zinaingia na kutoka. Kwa hali nyingine watu nao wanapitia mabadiliko makubwa. Hivyo kuishi wakiwa wanatingwa na kuwa na wawasi na maisha. Na hatua kwa hatua tumaini lao kwa dunia hii hutokomea. Sababu mojawapo ya hili ni kwakuwa wanaishi maisha yasiyo na uhakika wa mbeleni. Tunaishi katika ulimwengu wa aina hii usio na uhakika.
 

Yatupasa tuwe na tumaini la uzima wa milele katika Roho Mtakatifu.

Ni kwa namna gani tutaweza kupata tumaini la kweli? Tutaweza kulipata kwa kuiamini injili ya maji na Roho. Tumaini la wale walio kwisha mpokea Roho Mtakatifu si katika ulimwengu huu bali ni Mbinguni. Mtume Paulo alizungumzia juu ya tumaini la kweli Mbinguni. Sisi ambao tayari tumekwisha kupokea uwepo wa Rohao Mtakatifu huweka matumaini yetu katika mambo ya mbinguni. Tunafanya hivyo kwa sababu tunaamini ya kwamba, Yesu Kristo alikuja kuzichukua dhambi zetu zote duniani na hivyo kutuokoa sisi wenye dhambi kwa njia ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani. Mungu aliwatunukia tumaini la mbinguni wale wote wanao amini injili ya msamaha wa dhambi.
Warumi 8:19-21 inasema “kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake ila kwa sababu yake yeye aliye vitiisha katika tumaini kwa kuwa viumbe vyenye navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa na utukufu wa watoto wa Mungu.” Viumbe vyote vinatumaini kukombolewa toka kifungo cha uharibifu na kifo.
Viumbe vyote katika dunia hii si vikamilifu, hivyo vinaugulia na kusubiri kwa watoto wa Mungu kudhihirishwa, kwa nyongeza pia vinatamani kuwekwa huru toka kifungo cha uharibifu na kuishi milele. Viumbe vyote vinasubiri siku ambayo havitooza tena au kuchakaa bali kuishi milele. 
Siku moja viumbe vyote vilivyo umbwa na Mungu vitafanyizwa upya. Ingawa maua hunyauka na kuoza leo hii katika dunia, yatakuja chanua na kuishi milele katika dunia mpya. Sisi tulio na uwepo wa Roho Mtakatifu nasi pia tutakuja kuuona ulimwengu huo mpya.
Yesu Kristo alituahidi ya kwamba atarudi tena kuwafufua wale wote walio na uwepo wa Roho Mtakatifu, wakipewa miili mipya ambayo haitaharibika na ya milele kwa kila moja na hivyo kupewa uzima wa milele. Pia aliwaahidi kwamba wataishi milele mbinguni pamoja na Mungu. Viumbe vyote navyo vinasubiri kuishi nasi siku hiyo.
 

Ulimwengu huu hutazamia kwa njia ya tumaini.

Ndoto hii itatimia lini kwa wale wenyehaki? Itatimia pale Bwana atakaporudi. Yatupasa kuwa na tumaini pale tunapotazama ulimwengu huu. Yesu anasema kwamba patatokea njaa, magonjwa na milipuko, matetemeko ya ardhi na vita pahala pote (Mathayo 24:7). Lakini mwisho bado haujawadia katika siku ya mwisho wa dunia. Bwana wetu atakuja tena akifanyiza upya mambo yote ya dunia na kutubadilishia miili ya kiroho isiyoharibika. Hii inamaana pia kwamba mimea na wanyama nayo pia itapokea miili isiyo haribika. Kwa kuamini hili yatupasa kuuangalia ulimwengu kwa tumaini jipya.
Katika ulimwengu hata wale walio na uwepo wa Roho Mtakatifu wanaugulia ndani yao pamoja na viumbe wengine wote kwa hamu wakisubiri utukufu wa ukombozi wa miili yetu tukiwa watoto wa Mungu. Tunauangalia ulimwengu kwa tumaini kwa sababu Bwana atatufanya kuwa wana kwake ambao hatutooza au kufa pale atakapo rudi.
Ingawa dunia itaharibiwa siku moja vitu vyote vitafanywa upya pale Bwana atakaporudi tena. Yatupasa kuishi kwa tuamaini kwa kuamini hili. Dunia hiyo mpya itakuwa yenye furaha na ya ajabu mfano wa dunia yoyote uliyowahi kuisikia katika simulizi. Hebu fikiri namna ya kuishi katika dunia hiyo kwa muda wa miaka elfu moja. Na pia tutakuwa na uzima wa milele tukiwa watoto wa Mungu pale tutakapo ingia katika Ufalme wa Mbinguni. Yatupasa kuishi kwa tumaini la aina hii.
Je, unaona tumaini lolote katika dunia hii? Hapana. Watu huishi maisha ya furaha ya muda mchache kwa sababu hawana tumaini la dunia hii. Lakini Bwana wetu amekwisha tupa tumaini la mbinguni kwa wale waliokwisha samehewa dhambi na kufanywa wenye haki. “Kwa maana tuliokolewa kwa taraja lakini kitu kilicho tarajiwa kikionekana hakuna taraja tena. Kwa maana ni nani anaye tarajia kile akionacho? Bali tukitarajia kitu tusichokiona twakingojea kwa saburi.” Hii maana yake imetupasa kuwa na subira katika ujio wa Yesu kwa mara ya pili kwa sababu tumeokolewa kwa kuyaamini maneno ya Mungu.
Tunauwepo wa Roho Mtakatifu ndani ya roho zetu kwa sababu tuliokolewa toka dhambini. Kwa maana hiyo wale waliokwisha samehewa na Yesu ndiyo wenye Roho Mtakatifu mioyoni mwao badala ya dhambi. Vipi kuhusu miili yetu? Miili yetu iliyo midhaifu nayo pia itafufuliwa kupokea uhai mpya wa miili isiyo haribika. Tutaishi milele pamoja na Mungu pale Yesu atakaporudi tena. Wale waliozaliwa upya kwa mara ya pili wanaupendeleo wa kufanyiwa hivyo kwa sababu wanatumaini hilo kwenye roho zao na miili yetu itakuwa kamilifu. Miili yetu itakuwa ya milele na kamwe haitaugua. Miili yetu ya duniani ni dhambi hivyo si rahisi kwetu kuishi maisha yaliyo makamilifu.
Lakini hapo baadaye tutakuwa na uwezo wa kuishi tukiwa wakamilifu. Hebu basi natutazamie mbeleni kwa kuja kwake Bwana. Ni kwa wale tu walio na uwepo wa Roho Mtakatifu ndiyo watakaoweza kuwa na aina hii ya tumaini la uzima. Tumaini la mwenye haki si mbinguni pekee bali hata pia huwa ni ukweli pekee katika dunia. Biblia inasema kwamba Bwana wetu atarudi mara ya pili pale dunia itakapo angamia katika tabu kuu. Hakika hapa ndipo atakaporudi. Alipo kuja kwa mara ya kwaza alibatizwa kwa ajili yetu wenye dhambi, akafa msalabani ili kutufanya wenye haki na hatimaye akapaa mbinguni. Sasa niwakati mwingine wa kutarajia kurudi kwake.
Katika siku hiyo atawafufua wale walio lala, yaani watakatifu walio mwamini Yesu na kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu na hivyo kuwaweka huru tokana na uharibifu. Atawapa miili mipya ya mbinguni ambayo kamwe haito oza au hata kuugua. Kwanyongeza, kwanza watakutana na Bwana mawinguni na hivyo kufanya vitu vyote upya. 
Baada ya hili sisi pamoja na Bwana wetu tutaishi milele na kutawala naye katika ulimwengu mpya kwa mileniamu (miaka elfu moja) na kufidia siku tulizo itumikia injili. Haya ni mazoezi na majaribio katika wale watakao kwenda mbinguni. Hili ni tumaini la mbingu na ukweli. Katika muda huo, vitu vyote visivyokamili vitarudia ukamilifu na vile viozavyo havitooza tena. Maneno “hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika” (1 Wakorintho 15:42) yatatimia katika wakati huo kwa njia ya Yesu Kristo.
Hebu sasa sisi tulio na uwepo wa Roho Mtakatifu tuwe na ukamilifu. Yakupasa ukumbuke kwamba vitu vyote vidhaifu hufa lakini huo sio mwisho wake. Yatupasa kuwa na imani ya tumaini ambalo Bwana ataufanya ulimwengu kuwa mpya tena. Tukiwa na tumaini hilo tutakuwa na uwezo kuihubiri injili. 
Tunauwepo wa Roho Mtakatifu kwa sababu tuliokolewa toka dhambini. Kwa upande mwingi Roho Mtakatifu ndani yetu naye anatazamia kurudi kwa Bwana. Hutuombea kwa Bwana Mungu kwa niaba yetu ili tuishi kwa tumaini na imani pasipo kuvunjika mioyo.
 

Yatupasa kuishi kwa matumaini katika Roho Mtakatifu.

Ni sehemu gani wenye haki wataishi? Itakuwa katika 5  mileniam5 ambapo Bwana atafanya upya dunia hii pale atakapo kuja pia katika Ufalme wa Mbinguni. Hivyo yatupasa tuwe na subira ya kutosha katika siku hiyo itakayo kuja. Yatupasa kumwamini Bwana wetu kuwa ataifanya miili yetu kuwa kamili pale dunia hii itakapo angamia. Yatupasa kuwa na tumaini la utukufu ujao.
5 Pale Bwana wetu Yesu atakapo shuka dunianini kwa mara ya pili kulingana na ahadi yake, atashuka toka mbinguni na kuwafufua wafu waliokufa katika Kristo kwanza. Kitakacho fuata baada ya hili atawabadilisha watakatifu wote walio hai na walio fufuliwa na kuwapa miili ya milele isiyoharibika na baadaye kukutana na watakatifu hao mawinguni. (1 Wathesalonike 4:16-17, 1 Wakorintho 15:51-53) Ndipo atafanya vitu vyote upya baada ya kumwaga mapigo saba ya hasira yake kwa wenye dhambi walio baki. Baadaye ataweka ufalme wake katika dunia mpya na kutawala miaka elfu moja na wale walioshiriki ufufuo wa kwanza. (Ufunuo 20:4-15) Baada ya mileniamu atawahukumu wafu wote walio baki na kuwatupa motoni. (Ufunuo 20:11-15) Ndipo atakapo waongoza watu wake katika mji wa mbinguni, Jerusalemu mpya na ataweka makazi milele huko. (Ufunuo 21:1-4)
Akiwa na upeo wa Roho Mtakatifu, Paulo alikuwa na tumaini sawa tulilo nalo sisi. Tunaishi na tumaini hilo pia katika fikra zetu tukisubiri mileniam na Ufalme wa Mbinguni. Wale ambao bado hawajazaliwa upya wataangamia mwisho wa dunia hii, lakini wale waliozaliwa upya mara ya pili watamiliki dunia na mbingu mpya. Tumaini hili bila shaka litatimia. Miili yetu itakuwa kamili na tutaishi na kutawala na Yesu kwa miaka elfu moja katika dunia mpya. Tukiitazamia siku hiyo tutaweza kutumaini na kuishi pasipo kuogopa ulimwengu.
Hebu na tuwe wenye subira na kutulia. Ingawa maisha yetu yamechoka, tumaini letu litatimia na kuwa la kweli kwa sababu tunamwamini Mungu. Wale wasio na tumaini hawana thamani bali ni wafu tayari. Tafadhali uwe na tumaini na kuendelea na ndoto yako kwa kuyaamini maneno ya Mungu.
Kama vile msamaha wetu ulivyo wa kweli, badiliko la mili yetu litakuwa ni la kweli na hakika kila kiumbe kitapata uzima wa milele. Tumaini letu pia ni kweli. Uwe na imani na kile unacho amini. Wale walio na tumaini ndio watakao weza kuwa werevu na wenye furaha. Watu hukosa furaha ikiwa hawana tumaini. Wale wasio na ndoto hawana furaha. Tutaweza kuishi maisha yenye furaha kwa sababu tunatumaini la mileniamu na Ufalme wa Mbinguni katika dunia mpya na mbingu mpya.
Wale walio na tumaini ni waaminifu katika kazi ya kuhubiri injili njema. Yatupasa kuwa na tumaini ili tuweze kuihubiri injili katika kipindi hiki cha kukatisha tamaa. Yatupasa kuihubiri injili kwa waliochoka, wasio na tumaini, maskini, na wanyenyekevu. Yatupasa tuwakomboe kwa kuhubiri tumaini juu ya Ufalme wa Mbinguni, ambapo kwa wale waliokwisha samehewa dhambi zao kwa kuamini injili ya maji na Roho wataweza kuingia. Yatupasa kuwahamasisha kuwa na tumaini la ulimwengu wa Mungu utakao kuja ghafla kama mwizi baada ya kipindi hiki cha taabu kuu. 
Enyi watumishi na watakatifu mliozaliwa upya, tafadhalini ihubirini injili hii hadi mwisho wa dunia. Tunzeni kwa dhati tumaini lenu la mbinguni. Haijalishi ni kwa jinsi gani dunia inavyokwenda kwa kasi katika kuangamia, wale walio na tumaini kamwe hawato angamia, kwa sababu wana ahadi ya milele baada ya maisha ya duniani. Hakika wanayo maisha ya pili waliyopewa na Bwana.