Search

Perguntas Frequentes sobre a Fé Cristã

Assunto 2: O Espírito Santo

2-3. Wazazi wangu wawili walisisitiza ya kwamba wao ni wakristo walio zaliwa upya mara ya pili hata kabla hawaja funga ndoa, kwa nyongeza niliishi maisha ya kuifuata dini yetu toka nilipo zaliwa. Nilidhani ya kwamba Roho Mtakatifu amekuwa ndani yangu toka nilipo zaliwa kimwili. Hata hivyo nimechanganyikiwa kwa sababu sina ufahamu wa kibiblia juu ya Roho Mtakatifu kuweka makazi ndani ya mtu, Je, Roho Mtakatifu ni kweli huja na kuweka makazi ndani ya mtu aliye zaliwa upya kwa maji na kwa Roho?

Ndiyo ni kweli kila mtu huitaji dhambi zake zisamehewe kwa kuiamini Injili ya maji na Roho ili aweze kumpokea Roho Mtakatifu. Biblia inatueleza ya kwamba “maji” ni mfano wa wokovu (1 Petro 3:21). Hapa maji husimama badala ya ubatizo wa Yesu alio upokea kwa Yohana (Mathayo 3:15).
Kwanza kabisa kila mtu huitaji kusamehewa dhambi zake zote kwa kufahamu maana ya ubatizo wa Yesu ili kuweza kumpokea Roho Mtakatifu, Wagalathia 3:27 inasema “Maana ninyi nyote mliobatizwa katiak Kristo mmemvaa Kristo. Hapa neno “mliobatizwa katika Kriso” halimaanishi ubatizo wetu wa maji bali maana yake ni kupokea msamaha wa dhambi kwa kuelewa na kuamini sababu ya Yesu kubatizwa na Yohana.
Kila mtu amezaliwa akiwa na mwili wenye dhambi. Warumi 5:12 inasema “kwa hiyo kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni na kwa dhambi hiyo mauti na hivyo mauti ikawafikia” basi watu wote duniani wamezaliwa wakiwa ni wenye dhambi kwa kurithi toka kwa Adamu na Hawa.
Hivyo katika Zaburi 51:5 imeandikwa “Tazama mimi naliumbwa katika hali ya uovu Mama yangu alinichukua mimba hatiani”. Katika Isaya 1:14 “Ole wake taifa lenye dhambi watu wanaochukua mzigo wa uovu wazao wa watenda mabaya watoto wanao haribu”. Watu wana mbegu ya dhambi toka kuzaliwa waliyoirithi. Watu wote ulimwenguni wameirithi dhambi toka kwa wazazi wao na hivyo kuzaliwa duniani wakiwa wenye dhambi. Kwa maneno mengine miili yetu imefungwa kifungo cha dhambi na kubeba matunda ya dhambi wakati wote wa uhai wetu.
Kwa maana hiyo kwa kudhani kwamba wazazi wote wawili wa kimwili walio zaliwa upya mara ya pili wakiwa na mtoto basi naye atapeokea Roho Mtakatifu, ni jambo la kuchekesha na la kiuchawi kwa imani. Aliye na aina hii ya mawazo akidhani ataweza kumpokea Roho Mtakatifu na uwepo wake kwa njia binafsi kamwe haito wezekana kupitia aina hii ya imani.
Hivyo kila mtu imempasa kuamini Injili ya maji na Roho aliyo tupatia Yesu. Na hii ndiyo njia pekee ya kumpokea Roho Mtakatifu kwa kuwa ni zawadi ya Mungu. Yesu Kristo, mwana wa pekee wa Mungu alibeba dhambi zote za ulimwengu kwa kubatizwa na Yohana ndipo alihukumiwa msalabani na baadaye kutufanya sisi wote wenye kumwamini kuwa wenye haki kweli. Huu ni mpango wa Mungu na mapenzi yake kwa mwanadamu na amewapa uwepo wa Roho Mtakatifu kwa wale wote wenye imani kulingana na mapenzi yake.
Kila mmoja hapa ulimwenguni amezaliwa akiwa na dhambi zake. Kwa hivyo itawezekana kupokea karama ya Roho Mtakatifu pale tu mtu apatapo msamaha wa dhambi na kutakaswa kwa kuiamini Injili ya maji na Roho. Hivyo kila mtu imempasa kuweka akilini na kuamini kwamba Roho Mtakatifu huja juu yake pale anapo zaliwa upya mara ya pili kwa maji na Roho.
Haji kwa kutegemeana na aina fulani ya matakwa au juhudi tufanyazo bali kuweka kwake makazi kwa ujumla kunatokana na uaminifu wa Mungu aliyeweka ahadi. Kwa usemi mwinginie haji na kufanya makazi kutokana na mwanadamu au mafanikio ya kiroho, kuweka kwake makazi kutawezekana kwa imani kulingana na mapenzi ya Mungu.
Mapenzi ya Mungu yalikuwa ni kumtuma Yesu Kristo, Mwanawe wa pekee duniani ili awaokoe wanadamu wote kwa dhambi za ulimwengu kwa njia ya kubatizwa kwake na Yohana hatimaye akafanya afe msalabani kwa yote haya akaweza kuruhusu Roho Mtakatifu kuweka makazi ndani ya wale wote wenye kuamini, wenye haki walio kombolewa kutokana na dhambi zao zote kwa kutii mapenzi yake na kwa kuamini Injili ya maji na Roho Mtakatifu. 
Nasi kwa sababu tumezaliwa na wazazi walio okoka. Hii ni imani ya kishirikina na ya utii usio na sababu ya msingi. Hii ni sawa na kujaribu kumpokea Roho Mtakatifu kwa mapenzi binafsi kinyume na ya Mungu. Hakuna njia nyingine ya ziada bali ni kuamini Injili ya maji na Roho ikiwa mtu atahitaji kuona Roho Mtakatifu anaweka makazi ndani yake.