Search

Вопрсы о Христианской Вере

Тема 1: Рождение свыше от воды и Духа

1-22. Nimekuwa nikijisomea vitabu ulivyonitumia kwa wema wa kutosha na kukuta baadhi ya maswala yahusuyo ubatizo wa Yesu kuwa ni ya ajabu. Je, unaweza kunielezea juu ya mafundisho yako yahusuyo mahusiano kati ya ubatizo wetu na ubatizo, kifo na ufufuo wa Yesu Kristo?

Kwanza ya yote yatupasa kuwa makini juu ya “mafundisho ya ubatizo” kama ilivyo Waebrania 6:2. Kutokana na Biblia, ipo aina tatu za ubatizo; ubatizo wa Yesu alioupokea toka kwa Yohana Mbatizaji na ubatizo wa maji kwetu kama ibada.
Ubatizo tunaoupokea ni kukiri kwa imani yetu katika ubatizo wa Yesu. Hii ni kusema kwamba tunabatizwa ili tukiri imani yetu kwamba tunamwamini Yesu aliyebaitizwa ili kubeba dhambi zetu zote na kufa msalabani kutupatanisha. Sasa waweza kuelewa Mathayo 3:15 pale anaposema “kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.” Hapa neno “kwa kuwa ndivyo” lina maana kwamba Yesu mwenyewe alibeba dhambi za ulimwengu kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji, mwakilishi wa wanadamu wote.
Ulikuwa mpango mahususi wa Mungu kutuokoa toka mtego usioweza kuzuilika wa dhambi. Bwana Mungu “ameweka juu yake maovu yetu sisi sote” (Isaya 53:6) na kutupatia sisi haki. “Haki” hapa maana yake kwa Kigiriki “dikaisune” ambayo humaanisha “usawa na sheria.” Inatueleza kuwa Yesu alibeba uovu wa wanadamu katika namna ya usawa na sheria kwa kubatizwa katika kuwekewa mikono.
Tumeokolewa kwa umadhubuti wa imani ya ubatizo, kifo na msalaba na ufufuo wa Yesu. Nguvu ya tohara ya koroho (Warumi 2:29) katika ubatizo, ambayo ilikatia mbali dhambi zetu moyoni, imetutakasa mioyoni mwetu. Hivyo, Mtume Petro alisema mbele za watu “Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu” (Matendo 2:38) katika siku ya Pentekoste.
Wenye dhambi wote hupata msamaha katika mioyo yao kwa kumwamini Yesu. Nini maana ya jina la YESU? “Nawe utamwita jina lake YESU, maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao” (Mathayo 1:21). Jina la Yesu maana yake “Mwokozi” aokoaye watu wake kwa dhambi zao. Kwa namna gani aliokoa? Yesu alituokoa na dhambi zetu zote kwa kupitia ubatizo na kifo chake msalabani.
Mtume wa Yesu Kristo walipohubiri Injili walikuwa na uhakika wa kuelewa juu ya ubatizo wa Yesu na msalaba, hivyo walifundisha ile Injili ya kweli na kuwabatiza wale wote walio amini ubatizo huo. Kwa jinsi hiyo walibatizwa ili wakiri kwa nje kwamba wanaamini ubatizo na kifo cha Yesu kwa ndani ya mioyo yao. Tunapobatizwa, tunakiri “Na kushukuru Bwana ulibeba dhambi zangu zote kwa ubatizo wako, ukafa kwa ajili yangu na ukafufuka ili uniokoe mimi. Naamini Injili yako.” Tunabatizwa kwa maji na watumishi wa Mungu kama ishara ya imani katika ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani, kama alivyobatizwa na Yohana Mbatizaji. Kwa haya, watakatifu wa nyakati za Kanisa la kwanza walibatizwa ili kuthibitisha imani yao, baada ya kuikiri katika Injili na walikombolewa na kupata msamaha wa dhambi.
Ibada ya ubatizo si sharti muhimu la wokovu Ingawa ni jambo la maana katika kubainisha imani zetu maji ya ubatizo hayana cha kufanya katika wokovu wetu. Tutaweza kuokolewa pale tu tutakapo amini Injili ya maji na damu Biblia yatueleza kwamba tunabatizwa katika Yesu Kristo (Warumi 6:3, Wagalatia 3:27) pale tunapoamini ubatizo wake.
Sasa ni vipi tutaweza “kubatizwa naye.” Hii ni rahisi pale tu, tutakapo amini ubatizo ikiwa mwili, utu wetu wa kale utaweza kuungana na Yesu na kusulubiwa naye kwa imani yetu kwa ubatizo wake. Kwa matokeo haya ikiwa Yesu alibeba dhambi zetu zote kwa ubatizo wake, kifo chake kilikuwa ni hukumu ya udhalimu wetu. Hivyo basi, nasi pia tunakufa msalabani naye. Kwa maneno mengine, utu wetu au nafsi yetu, ambayo haina jinsi zaidi ya kuendelea kutenda dhambi hadi kufa, yenyewe hufa na tumeokolewa toka udhalimu wetu na kuungana na Yesu kwa ubatizo wake.
Wale walio ungana na Yesu kwa ubatizo na kifo wataweza pia kuungana naye katika ufufuo wake. Ufufuo huu si pekee kwake bali hata kwetu ambao hutuwezesha kuzaliwa upya kama wana wa Mungu na kututenga kuwa wake, walio safi na wasio na dhambi mbele yake.
Ikiwa hatuja mtwika dhambi Yesu kwa kutoamini ubatizo wake, kifo chake na ufufuko utaweza kuwa usio na maana, usio na la kufanya kwa wokovu wetu. Wale wote walio mtwika dhambi zao Yesu kwa imani wameungana na kifo chake, msalabani, kunako ruhusu kuzaliwa upya wakiwa wenye haki. Kwa jinsi hiyo, wale wasio mtwika dhambi zao yeye kwa kutoamini ubatizo, hawana usharika naye katika kifo na ufufuo wa jinsi hii.
Ubatizo wa wenye kuamini ni wakutegemewa kama tuwezavyo kukubaliana juu ya mke na mume kuwa washirika kisheria kwa kupitia maagano ya ndoa. Ubatizo wa watakatifu ni tamko la mwonekano wa nje au hadharani tokana na imani ya ndani mioyoni. Tunapo tamka imani yetu huwa yenye uimara isiyo futika kamwe.
Tusipoelewa vyema juu ya ukweli halisi wa maana ya ubatizo ambao Yesu aliupokea toka kwa Yohana Mbatizaji, yatupasa kutoamini ya kuwa tungeweza kuokolewa ikiwa hatutoamini juu ubatizo huo na umuhimu wake. Una maana ya mtego wa hadaa toka kwa shetani. Tutaweza kupokea ondoleo la dhambi na kukaribishwa Mbinguni kwa kuamini kwa dhati ubatizo wa Yesu moyoni badala kuamini ubatizo wa jinsi yetu.