Kwa sababu ya Changamoto ya COVID-19 na usumbufu kwa huduma ya utumaji barua kimataifa, tumesimamisha kwa muda huduma yetu ya 'Utumaji wa Vitabu vya Bure viyilivyo chapishwa.
Kwa kuzingatia hali hii hatuwezi kukutumia vitabu hivi kwa wakati huu.
Omba kwamba janga hili litamalizika hivi karibuni na kuanza tena kwa huduma ya posta.
Ikiwa wewe ni mfanyakazi mwenzangu na ungependa kutuma ujumbe na picha kwa "Ujumbe kutoka kwa Wenzako", bonyeza kitufe cha "Tuma ujumbe", na uingie. Chapisho lako litaonekana tu baada ya kuidhinisha
Ubatizo ni zana muhimu katika maisha ya mwanadamu inayojulikana kama tendo la ondoleo dhambi kwa maana ya kwamba dhambi zinatoweka kabisa. Tunaweza kupata wokovu kutoka katika maisha ya dhambi na hivyo kutakaswa dhambi zote mara moja tu kwa njia ya Injili ya maji na Roho. Imani katika Injili ya Maji na Roho ni kuamini katika kuwepo kwa Yesu kama mwana wa Mungu kuja kwake katika ulimwengu huu katika mwili wa mwanadamu, ubatizo wake na kusurubishwa kwake pale msalabani ni kwaajili ya wokovu wetu sisi sote. Ukombozi ambao Yesu alimpa mwanadamu ni kupitia njia ya imani katika ubatizo na damu yake kama ilivyo andikwa katika Agano Jipya (Mathayo 1:21-23) kwamba Yesu mwenyewe angewaokoa watu wote kutoka katika dhambi zao kwa maana ya kwamba ukombozi katika Biblia unaeleza kwenye kuoshwa kwa dhambi kwa njia ya Imani, katika ubatizo wa Yesu na damu yake. Dhambi zilipitishwa kwa Yesu, hivyo hakuna dhambi mioyoni mwa wanadamu tunaweza kujiita waliokombolewa na wenye haki tu baada ya kupitia ubatizo wake na kifo chake msarabani.
Ninaweza kusema kwamba, mimi pamoja na wanadamu wenzangu kwa ujumla kabla ya kumwamini Bwana Yesu Kristo nilikuwa mwenye dhambi na hii nikwa mujibu wa maandiko matakatifu (warumi 3 :23-24) inasema kwa sababu wote wametenda dhambi nakupungukiwa na utukufu wa Mungu … wanahesabiwa haki kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Yesu Kristo. Hivyo baada ya kumwamini Yesu na kukubali Injili ya Maji na Roho kupitia ubatizo wake dhambi zangu zimepitishwa kwa Yesu kupitia Imani katika Maji na Roho kupitia ubatizo wake dhambi zangu zote zimetakaswa. Ufahamu wangu juu ya ubatizo wa Yesu Kristo ni kama ifuatavyo:- Mtu ili aweze kuingia ufalme wa Mungu inampasa azaliwe mara ya pili kwa maji na Roho kwa maana ya kwamba ni ile hali ya kupata kibali cha kutufikisha katika ufalme wa milele mbinguni. Tunapo tamka habali ya maji kibibilia tunamaanisha ubatizo wa Yesu, jambo linalo onyesha umuhimu wa fundisho hili kuhusu ubatizo Yesu mwenyewe kama kielelezo cha wokovu wetu alibatizwa na Yohana Mbatizaji katika Mto wa Yordani kwa njia ya kuwekewa mikono kama tunavyosoma katika (Walawi 16 :21) kwamba, lilikuwa ni tendo moja la haki linganisha Agano Jipya (Rumi 5 :18) lilitoa picha ya kuchukua dhambi zote za wanadamu. Hivyo kwa mantiki hii Yesu alipokuwa anapokea ubatizo wa katika Mto wa Yordani kupitia Yohana Mbatizaji alise, kubali hivi sasa kwakuwa "ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote" (Mathayo 3 :15).Jambo la mwisho linalo nipa msukumo juu ya ubatizo wa Yesu kupitia Maji na Roho ni ule ushuhuda wa Yohana kupitia ubatizo "Alisema Tazama mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu (Yohana 1 : 29). Kwa hiyo ubatizo wa Yesu twaweza kusema kwamba, ni mfano wa wokovu bila kuwa na imani katika ubatizo wa Yesu hatuwezi kuokolewa Petro alitangaza maji ya ubatizo ni mfano unaotuokoa sasa (1 petro 3 :21). (Dibaji 8,9) Kifo cha Yesu Kristo pale msalabani kinatoa picha ya ukombozi kwani Yesu Kristo kupitia ubatizo amefanywa watakatifu kwa toleo la mwili wa yesu mara moja pale msalabani tumestahilishwa kwa kufanywa watakatifu kwa maana ya kwamba tumetakaswa. Hivyo yeye alituokoa sisi sote tuliokuwa tukiteseka kutokana na dhambi na hayo yote yalikuwa ni mapenzi ya Mungu. Kwaajili ya kutuokoa Yesu alijitoa mwenyewe mara moja kwa wote ili sisi tuwe watakatifu tumetakaswa. Yesu alijitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zetu zote akafa badala yetu ili sisi tusihukumiwe dhabihu za Agano la Kale ilitolewa siku kwa sababu dhambi zote zilihitaji toleo lingine kuoshwa. Kwa mujibu wa ukweli unaotokana na Neno la Mungu (Warumi 3 :23) inasema kwa sababu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu wana hesabiwa haki bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo, Yesu kutokana na swali hili la pili ninakubali kwamba niko na dhambi kwa maana ya kwamba sisi sote ni wenye dhambi mbele za Mungu tunapaswa kuendelea kumwamini Yesu ambaye alitumwa kwetu kutoka kwa Mungu kwa sababu ya upendo wake. Pia Mungu alitupa Torati na kutufanya tutambue dhambi zetu na adhabu ya dhambi hizo ili kutuokoa roho zetu kutoka dhambi kupitia ubatizo wake na tunaweza kuokolewa kwa kumwamini. Nilazima tutambue kwamba sisi ni wenye dhambi wasio na tumaini tutambue kwamba sisi ni wenye dhambi wasio na tumaini na tunapaswa kumwamini Yesu ili tuweze kuwekwa huru kutoka kwa dhambi na kuwa watoto wake na kurudisha utukufu kwa Mungu.
Nicodemo Philipo Budodi, Tanzania
Nicodemo Philipo Budodi
Tanzania, United Republic of
11/11/20241
Nambari 1
INJILI YA MAJI NA ROHO IMEFUNGUA MACHO YANGU YA KIROHO;
Nimekuwa nikitamani sana kujua ukweli wa wokovu wa mwanadamu,na uhakika kuurithi ufalme wa Mungu.Kama ilivyokawaida ya Mkristo yeyote anayemwabudu na kumtumikia Mungu,Nilijitahidi sana kwa juhudi nyingi na maarifa ya kibinadamu ili angalau kumfanya Mungu wangu anione nikiwa safi mbele zake.Lakini kila nilipojaribu hayo yote,nilijikuta bado ninamapungufu mengi sana,Na hata kufikia kukata tamaa na kuona hakuna haja ya kusali,Kweli nilijiona mimi sifai kabisa kila mara.Mwaka wa 2007 nikiwa katika kibanda cha huduma za kimtandao nikituma barua pepe kwa rafiki yangu,Nilikutana na tovuti hii ya www.bjnewlife.org na baada ya kuifungua niliona nuru ya ajabu sana,macho yangu yalifunguliwa na kugundua kuwa kumbe Tayari Yesu alikwisha beba dhambi zangu zote kupitia Ubatizo alioupokea katika mto Yordani kupitia kwa Yohana Mbatizaji,na kisha kufa msalabani,Hakika hili ni Pendo kuu mno.Ninamshuku Mungu kwa baraka hizi ambazo ametupatia,Ahsante pia kwa Mchungaji Paul C.Jong kwa mafundisho mazuri ambayo yamenifanya huru kweli kweli.Mungu awabariki nyote na awatunze siku zote mbawani mwake.Ndimi katika Shamba la BwanaEllys Mpanilehi, Tanzania( Sema Biblia Ministries)