(Mathayo 25:1-12)
“Ndipo ufalme wa Mbinguni utakapofanana na wanawali waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana harusi. Watano wao walikuwa wapumbavu na watano wenye busara. Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao na wasitwae na mafuta pamoja nao, bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. Hata bwana harusi alipokawia wote wakasinzia wakalala usingizi. Lakini usiku wa manane pakawa na kelele, haya bwana arusi tokeni mwende kumlaki. Mara wakaondoka wanawali wale wote wakazitengeneza taa zao. Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara tupatieni mafuta yenu kidogo maana taa zetu zinazimika. Lakini wale wenye busara wakawajibu wakisema hayatatutosha sisi na ninyi shikeni njia muende kwa wauzao mkajinunulie. Na hao walipokuwa wakienda kununua mafuta bwana harusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa. Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana Bwana tufungulie Akajibu akasema, Amin nawaambia siwajui ninyi. Basi kesheni kwa sababu hamwijui siku wala saa.”
Je, Roho Mtakatifu huja
juu ya watu gani?
Huja kwa wale wote walio samehewa dhambi
zao zote kwa kuamini ubatizo wa
Yesu na damu yake.
Ni watu gani walio mfano wa wanawali walio na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao?
Katika kifungu kilichopita hapo juu tumeona wanawali watano wenye busara na wapumbavu, wanawali wapumbavu waliwaomba wale wenyebusara kuwagawia kiasi cha mafuta ya taa lakini wenye busara wakawajibu wale wapumbavu “hayatatutosha sisi na ninyi shikeni njia muende kwa wauzao mkajinunulie”. Hivyo wakati wale walio wapumbavu wakienda nje kununua mafuta hayo, wale wenye busara walikuwa nayo katika taa zao na kuingia katika sherehe za harusi. Sasa basi ni kwa namna gani tunaweza kuyatayarisha mafuta kwa ajili ya Bwana? Kitu pekee tunachoweza kufanya ni kuusubiri msamaha wake wa dhambi katika mioyo yetu.
Katika ya watu tunaweza kupata aina mbili za imani. Moja ni imani ya injili ya msamaha wa dhambi. Hii ndiyo inayopelekea kumpokea Roho Mtakatifu. Nyingine ni ile ya kuwa mwaminifu wa kanuni za dini bila kujali mtu kusamehewa au kutosamehewa dhambi.
Kwa wale wote walio waaminifu kwa kanuni za dini, injili hubaki kuwa mzigo kwao kuichukulia. Kama walivyo wanawali wapumbavu waliokwenda nje kununua mafuta pale bwana harusi alipo ingia, wale wote wanaohama toka nyumba moja ya kuabudu kwenda nyingine kwa matumaini ya kumpookea Roho Mtakatifu ndani yao, hawamdanganyi yeyote bali nafsi zao. Watu wa aina hii ni wenye kiburi ambao kwa kweli ndiyo wanao hitaji kuwa na imani ya injili njema katika mioyo yao kabla ya siku ya hukumu. Watu hawa hutamani kuwa na Roho Mtakatifu kwa kumuonyesha Mungu ukereketwa wao. Tuone ushuhuda wa shemasi mmoja aliyefanya juhudi kubwa katika kumpokea Roho Mtakatifu. Ushuhuda huu kwa hakika utatusaidia sana.
“Nilifanya kila niwezalo ili kumpokea Roho Mtakatifu. Nilidhani kwamba, ikiwa nitajitolea nafsi yangu kwa imani yangu kwa uaminifu nitaweza kumpokea Roho Mtakatifu na matokeo yake nilijikuta kuhama kanisa moja hadi jingine, nyumba moja ya sala kwenda nyingine. Watu katika moja wapo ya nyumba hizi za sala walikuwa wakipiga kinanda cha umeme ikiwa ni sehemu ya ibada. Mchungaji aliyekuwa akiongoza mkutano huu aliwaita wale wote waliohitaji kumpokea Roho Mtakatifu moja baada ya mwingine na walipo wekewa mkono wa mchungaji katika mapaji ya nyuso zao, kila mtu baada ya tendo hilo alianza kunena kwa lugha. Mchungaji aliruka huku na kule akishikilia kipaza sauti na kupaza sauti “pokea moto, moto, moto!” na kuweka mkono wake juu vichwa vya watu na kusababisha baadhi yao kupagawa na kuanguka. Mwanzoni nilikuwa na wasiwasi ikiwa tendo hili linamaana ya kumpokea Roho Mtakatifu lakini tayari nilikuwa nimeathirika na mikutano ya aina hii. Licha ya haya yote kamwe sikuweza kupokea Roho Mtakatifu.
Baada ya tukio hili niliamua kwenda milimani nakujaribu kulia na kuomba usiku kucha nikiwa nimeegemea mti. Wakati mwingine nilijaribu kufanya maombi ndani ya pango lakini yote haikusaidia. Baada ya yote haya nilijaribu kufanya maombi usiku kucha kwa siku arobaini lakini kamwe sikuweza kumpokea Roho Mtakatifu. Semina hii ilikuwa ikifanyika kwa juma mara moja na kufululiza majuma saba.
Katika semina hii kulikuwa na mafundisho kuhusu upendo wa Mungu, msalaba na ufufuko wa Yesu, tendo la kuwekewa mikono, tunda la roho na kukua kiroho. Katika muda huo wakati ratiba ya semina ilipokuwa ikikaribia kuisha, mnenaji mkuu katika semina hiyo aliniwekea mikono juu ya kichwa changu na kuanza kuniombea ili niweze kumpokea Roho Mtakatifu huku nikimfuatisha maneno yake kama alivyonielekeza. Nilitulia na kunyanyua viganja vya mikono yangu na kuelekeza juu na kuanza kupiga kelele “la-la-la-la!” kwa kurudia rudia. Mara ghafla nilipokuwa nikipiga kelele “la-la-la-la!” nilianza kunena moja kwa moja lugha ya ajabu. Watu wengi walinipongeza baada ya hapo katika kumpokea Roho Mtakatifu. Lakini nilipokuwa mwenyewe nyumbani nilihofu. Hivyo nikaanza kujitolea kufanya kazi katika semina hiyo. Nilidhani kwamba ilinipasa kujitolea kwa kazi kama hii mapema sana. Hivyo nilisafiri nchi nzima katika kutoa huduma na nilipo wawekea mikono wagonjwa, magonjwa yao yalionekana kupona ingawa baadhi yaliwarudia baadaye. Na baadaye nikapata maono na nikagundua yakuwa naweza pia kutoa unabii. Chakushangaza unabii wangu mara nyingi ulikuwa wakweli. Tokea hapo nilialikwa sehemu za kila aina na kulakiwa kwa shangwe. Lakini bado nilikuwa na hofu ndani yangu ndipo nikasikia sauti ikisema “usitange tange toka sehemu moja kwenda nyingine namna hii badala yake nenda ukawasaidie jamaa zako nyumbani katika kupokea wokovu.” Hata hivyo sikuelewa maana halisi ya wokovu. Nilichokuwa nakielewa ni kile wengi walichokuwa wakisema kwamba, ikiwa nitaacha kuzitumia karama za Roho Mtakatifu basi atanipokonya. Kwa upande mwingine nilihofu kutumia uwezo wangu lakini sikuweza kujizuia hilo.
Siku moja nilisikia kuwa yupo mwanamke fulani ambaye ni wa dini ya Shama aliyehitaji kumwamini Yesu, hivyo mimi pamoja na rafiki yangu tulikwenda kumtembelea. Hatukumfahamisha juu ya ujio wetu kabla. Lakini mwanamke huyo alikuwa akitusubiria mlangoni nakuanza kutuambia “nilishajua kwamba mnakuja” mara ghafla alianza kutunyunyizia maji na kusema “hakuna tofauti kati ya ushama wa mashariki na ushama wa magharibi”. Alituita sisi kuwa ni “washama wa Yesu” na kutunyoshea kidole akisema “huyu ndugu ni muoga lakini huyu si muoga” Kile ambacho mwanamke huyu alichokua akisema kiligeuka kuwa kama pigo katika kichwa. Nikaanza kuwaza kwamba yote niliyokuwa nikiyatenda hayakuwa tofauti na yale ambayo dini ya shama wakitenda. Hakuna nilichokuwa nimekwisha tenda ili kumleta Roho Mtakatifu ndani yangu kwa sababu bado nilikwa na dhambi moyoni.”
Tokana na ushuhuda huu tunajifunza kwamba, swala la kumpokea Roho Mtakatifu lipo nje ya uwezo wetu. Kwasababu imani ya aina hii haihusiani na injili ya Mungu kwani wale wote wanaoishi katika aina hii ya udini ndiyo wasio kuwa na mafuta katika taa zao.
Taa katika biblia inamaana ya kanisa, na mafuta maana yake Roho Mtakatifu. Biblia inakusudia kwamba wale wote wanao hudhuria kanisani, iwe ni kanisa la Mungu au si la Mungu pasipo kumpokea Roho Mtakatifu, bado ni wapumbavu.
Wapumbavu wote hupandisha mori siku hata siku. Watu hawa hupandisha hisia zao kali na kujitolea kimwili mbele ya Mungu. Ikiwa tungelisema kuwa hisia zetu ziwe za kiwango cha sentimita 20 na hivyo kufanya kila siku 1 kupandisha sentimita 1, basi ingelichukua siku 20 kuweza kufikia kiwango cha juu katika hisia zetu zote. Hisia zao katika imani hupata nguvu mpya kwa kila maombi ya asubuhi, maombi ya usiku kucha, maombi ya kufunga na mikutano ya uamsho na pia katika maisha ya kila siku. Huathirika na tabia hii ya kudumu katika kuenenda kwa hisia.
Hisia zao hupanda katika jina la Yesu. Huudhuria kanisani ili kupandisha hisia zao, lakini mioyo yao bado imechanganyikiwa huku wakitafuta sababu nyingine. Sababu ya hili ni kwamba imani yao imetokana na kile kinachotokana na mwonekano wa nje kimwili na hivyo kuhitaji shinikizo la mara kwa mara ili kusukuma hisia zao ili moto wa hisia usizimike ndani yao. Hata hivyo bado hawato weza kumpokea Roho Mtakatifu kwa aina hii ya imani. Kwakupandisha hisia hizo kamwe hakutoweza kuwafanya kumpokea Roho Mtakatifu.
Sote imetupasa kuwa tayari na imani sahihi ili kuweza kumpokea Roho Mtakatifu katika uwepo kamili wa Mungu. Na ndipo pekee tutakapo kuwa na haki ya kumpokea Roho Mtakatifu. Ni kwanamna gani basi tunaweza kuwa na imani ambayo inatupa haki ya kuwa na Roho Mtakatifu? Ukweli upo katika injili njema ambayo ilikamilishwa kwa ubatizo wa Yesu Yordani na kumwaga damu yake Msalabani.
Mungu alituita kuwa sisi ni kama “wazao wa watenda mabaya, watoto wanaoharibu” (Isaya 1:4). Lazima tulikubali hili. Kwa asili wanadamu wamezaliwa wakiwa wanadhambi aina 12 (Marko 7:21-23). Wanadamu hawawezi kujizuia kutotenda dhambi tokea wanapozaliwa hadi kufa.
Katika Yohana 1:6-7 imeandikwa, “palitokea mtu ametumwa kutoka kwa Mungu jina lake Yohana. Hivyo alikuja kwa ushuhuda ili aishuhudia ile nuru wote wapate kuamini kwa yeye”. Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu na kumtwika dhambi zote zaulimwegu akisema “tazaama mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya dunia” (Yohana 1:29). Tuliokolewa kwa dhambi zote nakuushukuru ubatizo wa Yesu Kristo. Kama Yohana asingeli mbatiza Yesu Kristo na nakutotangaza kwamba alikuwa ndiye mwana kondoo wa Mungu aichukuae dhambi ya ulimwengu, basi tusingeliweza kumjua Yesu kwamba ndiye aliye beba dhambi zetu zote kuelekea msalabani. Tusingeliweza kuifahamu njia ya kumpokea Roho Mtakatifu. Kwa hiyo basi tunamshukuru Yohana kwa ushuhuda kwani sasa tunaelewa yakwamba Yesu ndiye aliye beba dhambi zetu zote na hivyo tunaweza kumpokea Roho Mtakatifu kwa imani hiyo.
Kwaimani hii basi tumekuwa wanaharusi tuliotayarishwa kamili kumpokea Yesu Kristo, Bwana harusi. Sisi ni wanawali tulio mwamini Yesu na tumejitayarisha kamili kumpokea Roho Mtakatifu.
Je, unaamini injili ya maji na Roho kwa moyo wako wote? Je, unaanini kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu kwa ubatizo wake kwa Yohana? Biblia inasema “basi imani, chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:17). Nilazima tuamini yakwamba Yesu alibatizwa na Yohana na kufa msalabani ilituweze kumpokea Roho Mtakatifu. Yatupasa kuelawa kwamba kumpokea Roho Mtakatifu kutawezekana ikiwa tutaamini kwamba Yesu alikuja ulimwenguni akiwa kama mwanadamu na kubatizwa na Yohana hivyo alikufa msalabani na kufufuka.
Hata leo hii yapo makundi mawili ya wanaoamini kama ilivyo kwa wanawali kumi katika ile habari ya hapo mwanzo. Sasa basi wewe nawe uko upande upi? Yakupasa ujue ile njia ya kweli ambayo utaweza kumpokea Roho Mtakatifu kwa hakika.
Ni kwa imani gani utaweza kumpokea Roho Mtakatifu? Je utaweza kumpokea Roho Mtaktifu kwa kupitia shauku itokanayo na ukereketwa utokanao na dini kama Shama? Je utaweza kweli kumpokea Roho Mtakatifu katika hali ya kupoteza fahamu? Je utaweza kumpokea Roho Mtakatifu kwa kuamini ushabiki wa kidini? Biblia inasema kwamba Yesu alipobatizwa kwa kuzamishwa na kibuka toka kwenye maji Roho wa Mungu alitua kama hua juu yake. Alibatizwa ili kubeba dhambi zetu zote na hivyo kuweka bayana kwamba atakwenda kusulubiwa ili kulipia mshahara wa makosa yetu yote.
Yesu alibatizwa na Yohana ili kubeba dhambi za ulimwengu na hivyo kwenda msalabani ili tuweze kuokolewa na kupokea kipawa cha Roho Mtaktifu. Jambo hili ni kweli. Yesu alibatizwa na Yohana, akahukumiwa kwa dhambi zetu zote msalabani na kufufuka. Lazima tuamini ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani ili tupate msamaha wa dhambi zetu zote. Tunaweza kuona toka ubatizo wa Yesu (Mathayo 3:13-15) kwamba, Roho Mtaktifu huja kwa amani kama ashukavyo huwa kwa wale waliotakaswa kwa kuamini ubatizo wa Yesu.
Ili kumpokea Roho Mtakatifu ni muhimu kuamini ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani. Roho Mtakatifu huja juu ya mtu katika hali ya utulivu na amani kama vile hua pale mtu huyo anapo amini msamaha wa dhambi. Wale ambao tayari wamekwisha mpokea Roho Mtakatifu yawapasa kuelewa kwamba hili limewezekana kutokana na msamaha wa dhambi kwa imani. Roho Mtakatifu hutua juu ya wale wote wanao amini msamaha wa dhambi kwa mioyo yao yote.
Yesu Kristo alikuja kwa mkate na divai ya uzima wa milele (Mathayo 26:26-28, Yohana 6:53-56) Yesu alipoibuka toka majini baada ya kubatizwa, palitokea sauti mbinguni ikisema “Huyu ni mwanangu mpendwa wangu ninaye pendezwa naye” (Mathayo 3:17).
Nirahisi kuamini katika Mungu kwa Utatu. Mungu ni Baba wa Yesu na Yesu ni Mwana wa Mungu. Roho Mtakatifu pia ni Mungu. Utatu huu ni Mungu mmoja kwetu.
Yakupasa kujua kwamba, kamwe hautoweza kumpokea Roho Mtakatifu kwa kuamini msalaba pekee au kujaribu kujitakasa binafsi kwa matendo ya haki. Utaweza kumpokea Roho Mtakatifu pale unapoamini ubatizo wa Yesu na hivyo kumtwika dhambi zote juu yake, na kuamini kusulubiwa kwake ili kutupatanisha kwa dhambi zetu zote. Hakika hivi ndivyo ilivyo rahasi na wazi ju ukweli huu! Si vigumu kupokea msamaha wa dhambi na Roho Mtakatifu.
Mungu huzungumza nasi kwa namna iliyo rahisi. Kiwango cha akili ya mtu wa kawaida ni kati ya 110 na 120 (yaani IQ - intelligence quotient). Injili ya Mungu ni rahisi kumtosheleza mtu wa kawaida kuielewa. Hata kwa watoto wa umri kati ya miaka 4 na 5 injili hii njema kamwe haijawa ngumu kueleweka kwao. Lakini Mungu anapo zungumza nasi juu ya kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani kwa njia iliyo rahisi zaidi, je, tusingeliweza kweli kumwelewa? Mungu husamehe dhambi zetu zote na kutupa Roho Mtakatifu kama zawadi kwa wale wote waaminio injili hii.
Mungu anatuambia kwamba hatutoweza kumpokea Roho Mtakatifu kwa kupitia tendo la kuwekewa mikono au sala ya toba. Roho Mtakatifu haji kwa namna ambavyo tutakapo funga au kujitolea au hata kuomba usiku kucha milimani. Ni aina gani basi ya imani itakayo sababisha kumpokea Roho Mtakatifu ndani yetu? Ni imani ya kweli ya kwamba Yesu alikuja hapa ulimwenguni alibatizwa ilikubeba dhambi zetu zote, akafa msalabani na alifufuka.
Je, ni kweli imetupasa kuamani hivi?
Kwanini imetupasa kuamani msamaha wa dhambi na hivyo tuweze kumpokea Roho Mtakatifu? Ili tuweze kuwa raia wa Ufalme wa Mungu, tunamhitaji Roho Mtakatifu tunahitajika kumwanamini Yesu kuwa ni mwokozi, kuamini ubatizo wake na damu yake, na hatimaye kusamehewa dhambi zetu zote.
Kwanini Mungu huwatunukia Roho Mtakatifu wale wote ambao dhambi zao zimekwisahamewa? Ni kwa ajili ya kuwapiga mhuri wa kuthibitisha kuwa ni watu wake. Katika kuwapiga mhuri wale wote wenyekumwamini Yesu, hunategemea neno la Mungu, hivyo huwapa Roho Mtakaktifu kama kinga ya uthibitisho.
Baadhi ya watu hushikilia aina za imani potofu. Nirahisi kuamaini ubatizo wa Yesu na kumpokea Roho Mtakatifu. Nirahisi kwetu sisi tuliokwisha kumpokea Roho Mtakatifu lakini ni vigumu kwa wale wote ambao bado hawajapata msamaha wa dhambi. Hawaijui kweli na badala yake kutafuta namna nyingine ili kumpokea Roho Mtakatifu kama vile kuzama katika mawazo potofu ya kidini tokana na mashamshamu. Hupumbazwa na hivyo kuchanganyikiwa kutokana na mbegu ya shetani aliyo pandikiza ndani yao hatimaye kuangukia katika mkumbo wa mazingaombwe ya kidini.
Roho Mtakatifu huweka makazi ndani ya wale wote wanao amini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani na wale wote wanao upokea msamaha wa dhambi. Wale tu wanao amini wokovu wa Mungu ndiyo watakao weza kukiri “nimekwisha samehewa dhambi”. Ikiwa mtu hatoamini injili ya maji na Roho basi hawezi kusema kwamba hana dhambi. Kwa upande mwingine Mungu ametupatia Roho Mtakatifu kama ahadi kwa watoto wake wote wanao amini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani na kupokea msamaha wa dhambi.
Ni nani anaye shuhudia kwamba ubatizo wa Yesu na damu yake uliondolea mbali dhambi zetu? Yesu, wafuasi wake pamoja na Roho Mtakatifu ndiyo washuhudiao. Ni nani aliyepanga kuokoa watu wote kwa dhambi zao? Baba aliye Mtakatifu ndiye aliye panga. Nani aliye leta uthibitisho kwamba mpango huu ulitekelezwa? Roho Matakatifu ndiye anayethibitisha.
Mungu anataka kutufanya kuwa watu wake na hivyo amedhamiria kutuokoa tokana na dhambi zetu zote kupitaia ubatizo wa Yesu na damu yake. Hivyo utatu wa Mungu huthibitisha wokovu pekee na kutuhakikishia msamaha wa dhambi zetu zote.
Katika Mathayo 3:17 imeandikwa “huyu ni mwanangu mpendwa wangu ninaye pendezwa naye”. Yesu ni Mungu halisi. Mungu Baba anatuambia, “ikiwa mnataka kupokea msamaha wa dhambi zenu basi amini kwamba, dhambi zote za wanadamu ziliondolewa mbali milele na Yesu mwana wangu wa pekee, hivyo pokeeni Roho Mtakatifu na muwe watoto wangu” Wale wote wenye kuamini hivi watapokea msamaha wa dhambi na hatimaye kuwa watoto wa kiume na wa kike wa Mungu. Hawa huwapa kipawa cha Roho Mtakatifu ili kuwatia mhuri kama watoto wake. Tunapokea msamaha wa dhambi zetu pale tunapo amini ubatizo wa Yesu na damu yake kwa pamoja.
Watu wasio safisha mioyo yao kwa kuamini injili ya msamaha wa dhambi, hudhani kuwa dhambi zao za asili zimeondolewa lakini imewapasa kuomba sala za toba pasipo kikomo ili kupokea msamaha wa dhambi wazitendazo kila siku. Kwa kuangukia katika mawazo ya aina haya, biblia huwa kwao ni kitu kisicho eleweka na chakuchanganya akili. Hivyo hujikuta wakiwa na imani iliyo tofauti na ile ya wafuasi wa Yesu.
Baadhi hudiriki kusema kwamba Roho Mtakatifu huja kwa kupitia maombi. Lakini hii si kweli kulingana na mtazamo wa kibiblia. Inaweza kuonekana ni kweli lakini biblia inasema kwamba Yesu alipoibuka katika maji baada yakubatizwa na Yohana, Roho Mtaakatifu alitua juu yake kama huwa. Hii inatuthibitishia kwamba, ikiwa tunatamani kumpokea Roho Mtakatifu, tunahitaji kuamini kwamba Yesu alikuja ulimwengui na kubatizwa na Yohana ili kubeba dhambi zetu.
Mungu anasema nini kwetu sisi tunaomini ukweli huu na kumpokea Roho Mtakatifu? Husema, “Wewe ni mwanangu. Huyu ni mwanangu mpendwa, ninaye pendezwa naye” Mungu alisema namna hii pia hata kwa wale watakao mwamini na kusamehewa dhambi zao hapo baadaye. Ahadi hii ni ukweli kwa Mungu kutufanya kuwa watoto wake.
Lakini bado watu wanadhani zipo njia nyingine katika kumpokea Roho Mtakatifu. Je, unadhani kwamba Roho Mtakatifu atakushukia kwa kupitia kupiga kelele na kulia pamoja na juhudi binafsi? Kazi za Mungu zinaweza kugundulika kwa mapenzi yake na kuwapa Roho Mtakatifu kwa wale tu waliopata masamaha wa dhambi. Yeye husema “nimemfanya mwana wangu abatizwe ili aweze kubeba dhambi zenu zote, kumsulubisha ili ahukumiwe kwa dhambi hizo. Nimemteua mwana wangu kuwa mwokozi wenu. Ikiwa mtaukubali msamaha wa dhambi ambao mwana wangu aliukamilisha basi nitamtuma kwenu Roho Mtakatifu.”
Baba yetu hutenda atakalo. Hata ikiwa mtu atapiga magoti usiku kucha na kumlilia kwa sauti kuu, Mungu hatoona umuhimu wowote wa kumtumia Roho Mtakatifu juu yake zaidi atamkemea na kumwambia “bado haujakubali ufahamu wa kweli kwani unaendelea kukubali imani potofu. Roho Mtakatifu ataendelea kuzuiwa asije kwako endapo utakataa imani ya kweli”.
Katika ulimwengu huu maamuzi ya mwanadamu huweza kubadilika kutokana na mazingira, lakini sheria ya Mungu iliyowekwa katika kusamehe dhambi na kutunuku Roho Mtakatifu hubaki pale pale pasipo kubadilishwa. Ikiwa umeangukia katika dimbwi la imani potofu ni vigumu kuiona njia iliyo sahihi kwa mara nyingine. Biblia inasema kwamba Yesu nikikwazo kwa wale wote wasio watiifu (1 Petro 2:8).
Watu wanaomwamini Yesu huku wangali bado hawajui kwanini alibatizwa, huamini injili iliyo nusu ya ukombozi na bila shaka wataangukia motoni. Hivyo mwanzo unapomwamini Yesu ni lazima ujue juu ya ubatizo wake na damu yake ambamo ipo ndani ya injili ya msamaha wa dhambi. Na ukiwa umepokea msamaha wa dhambi ndipo basi moja kwa moja utampokea Roho Mtakatifu.
Hebu na tufikiri juu ya maisha ya Yesu hapa duniani yalikuaje. Yeye alikuja akiwa na umbile la mwanadamu na kubeba dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo wake. Alikufa msalabani na kuhukumiwa kwa ajili ya dhambi hizo ili kutuokoa tusiende motoni. Wale wote wanao mwamini yeye humpotoka Roho Mtakatifu akiwa ni zawadi kwao.
Hivyo basi sote ni lazima kufuate njia ya kweli ili tuweze kumpokea Roho Mtakatifu ndani yetu. Kinachohitajika ni kuwa na mtazamo unaolingana na maneno ya kweli. Tunapofanya hivi Yesu atatutunza na kutubariki. Wale wote wenye kuweka mioyo yao wazi na kuamini maneno ya Yesu wataweza kuishi katika kweli kwa kupokea msamaha wa dhambi na kuongozwa na Roho Mtakatifu. Zaidi ya yote wataweza kuwaongoza wengine kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
Amini ukombozi uliokamilishwa kwa ubatizo wa Yesu na damu yake. Kwa njia hii utaweza kumfuata yeye kwa imani na kupokea baraka ya msamaha wa dhambi, uzima wa milele na uwepo wa Roho Mtakatifu. Yesu ni Bwana wa msamaha aliyebeba dhambi zetu zote ulimwenguni kwa njia ya ubatizo wake na kifo chake msalabani. Yesu ametakasa dhambi zetu zote na kutupatia Roho Mtakatifu kwetu sisi tunaoamini injili ya kweli na hivyo kuishi na amani ya kweli.