Search

Mahubiri

Somo la 8: Roho Mtakatifu

[8-12] Kuishi Maisha ya Ujazo wa Roho Mtakatifu (Tito 3:1-8)

(Tito 3:1-8)
“Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka na kutii na kuwa tayari kwa kila kazi njema, wasimtukane mtu yeyote wasiwe wagomvi, wawe wema, wakuonyesha upole wowoto kwa watu wote. Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili tulikuwa waasi tumedanganywa huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi tukiishi katika uovu na husuda tukichukiza na kuchukiana. Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu na upendo wake kwa wanadamu ulipofunuliwa alituokoa si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyotenda sisi bali kwa rehema yake kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu ambaye alitumwagia kwa wingi kwa njia ya Yesu Mwokozi wetu ili tukihesabiwa haki kwa neema yake tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu ni neno la kuaminiwa; na mambo hayo nataka uyanene kwa nguvu ili wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Hayo ni mazuri tena yana faida kwa wanadamu.”
 
 
Ni kwanamna gani twaweza
kuishi maisha ya ujazo wa
Roho Mtakatifu?
Imetupasa kuelewa mapenzi ya Mungu
Kuihubiri injili kwa
jinsi ilivyo.

Wale wote wenye kumwamini Yesu na kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao lazima waishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu. Kwa Wakristo maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu ndiyo mahitaji ya Mungu. Inatulazimu kufuata mpangilio wake. Hivyo basi, kwa vipi tutaweza kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu? Nilazima tuwe makini kwa lile Mtume Paulo aliloelezea.
 

Nini kinacho hitajika katika kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu?

Katika Tito 3:1 Paulo alisema “Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka na kutii na kuwa tayari kwa kila kazi njema.” Kwanza kabla ya yote alitueleza kuwa wanyenyekevu kwa wenye uwezo na mamlaka, kutii na kuwa tayari kwa kila kazi njema. Alichokuwa akimaanisha ni kwamba, hatutoweza kuishi maisha yaliyojaa uwepo wa Roho Mtakatifu ikiwa hatuto weza kutii sheria za dunia. Bila shaka ikiwa watawala wa dunia na sheria zinazo ongoza dunia zitaendana na ukweli, inatubidi kuzitii. Lakini ikiwa sheria hizo hazitokiuka imani zetu, ni lazima basi tuzitii ili tuweze kuitumikia Injili ya amani.
Sisi ndiyo tulio pokea uwepo wa Roho Mtakatifu. Tutawezaje kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu ikiwa tutazivunja sheria za duniani? Hivyo ili tuweze kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu imetupasa kuzifuata sheria za kidunia. Wale walio pokea uwepo wa Roho Mtakatifu imewapasa kutii taratibu za kijamii. Tutaweza kutembea na Mungu ikiwa tu, tutazifuata sheria za kidunia.
Kwa mfano mmoja wetu akitenda uhalifu akiwa njiani kuelekea kanisani, Je, ataweza kweli kumtumikia Bwana kwa amani? Ni kwa namna gani hapa ulimwenguni mtu huyo ataweza kuishi kulingana na mafundisho ya Bwana ikiwa ataishi nje ya sheria? Imetupasa kutovunja taratibu za kijamii huku tukitembea kiroho. Hakuna lililojema huja kwa kuvunja sheria. Lazima tuitunze amani kwa kuzifuata sheria, za jamii.
 

Imetupasa kuwa na unyenyekevu ndani ya mioyo yetu.

Paulo alisema “wasimtukane mtu yeyote wasiwe wagomvi wawe wema wakionyesha upole wote kwa watu wote”. Kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu imetupasa tusimtukane mtu yeyote, tuwe na amani, wapole na kuonyesha unyenyekevu kwa watu wote.
Katika mioyo ya wale wote walio zaliwa upya mara ya pili upo unyenyekevu kiasi na upole. Hili linawezakana kwa sababu Roho Mtakatifu kaweka makazi ndani yetu. Paulo alituambia kwamba haitupasi kuidhalilisha Injili kwa kugombana na kila mtu. Bila shaka inatulazimu kugombana ikiwa tu sheria za kijamii zitakwenda kinyume na Injili. Lakini ikiwa haziendi kinyume, basi nilazima tuishi kwa amani. Tusababishe wengine watuwazie kwa kusema, “Ingawa anaonekana mkali kama simba kwa wakati mwingine lakini ni mwenye amani kama hua. Imani yake katika Ukristo bila shaka ndiyo imfanyayo kuwa mpole na mtu mwenye hekima”.
Hakuna upole au unyeyekevu katika tamaa ya mwili. Lakini kwa njia ya uwepo wa Roho Mtakatifu na kwa kupitia Bwana aliyetuokoa dhambini ndipo tutaweza kuwa wa pole kwa wengine. Kusamehe mtu aliye kutendea kosa kubwa kwangu “msamaha” halisi na kumtendea unyenyekevu toka ndani ya kina huo ndiyo “unyenyekevu” wa kweli, unyenyekevu kwangu siyo kujifanya kuwa mtu mwenye wema kwa mwingine ikiwa bado ninachuki kubwa naye. Kuwa na moyo ulio jawa na unyenyekevu na msamaha ndiyo kina cha utu wa Mkristo aliye zaliwa upya mara ya pili.
Yatupasa pia kuwa na upole pale watu wanapo tukosea. Endapo hawatojaribu kuweka kikwazo katika Injili, imetupasa kuwa wapole kwa kila mtu. Lakini endapo wataweka kwazo, basi itatulazimu badala yake kuangaza nuru ya upole pamoja na nuru ya ukweli. Wenye kupinga kuingilia kati au kunenea uongo neno la Mungu hawana haki ya kutendewa upole zaidi ya ukali.
Mungu hawasamehi wale wote wanao mpinga yeye bali huwafanya walipe gharama. Mungu alimwambia Abrahamu “Nami nitawabariki wakubarikio naye akulaaniye nitamlaani” (Mwanzo 12:3). Watu wanao ipinga Injili ya kweli hawana njia ya kuokolea. Hawatoweza kuzuia janga litakalo waangamiza maisha yao tu bali pia hata kizazi chao.
Kwa nini imetupasa kuvumilia na kuwa wenyenyekevu? Kama ilivyo andikwa katika Tito 3:3 “Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili tulikuwa na anasa za namna nyingi tukiishi katika uovu na husuda tukichukizana na kuchukiana” sisi ni kama watu hawa kabla ya kuzaliwa upya mara ya pili. Hivyo inatulazimu kuvumilia na kusamehe watu kwa sababu nasi pia tulikuwa hivyo.
Katika Tito 3:4-8 inasema “Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu na upendo wake kwa wanadamu ulipofunuliwa alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyotenda sisi bali kwa rehema yake kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu ambaye alitumwagia kwa wingi kwa njia ya Yesu kristo Mwokozi wetu ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu. Ni neno la kuaminiwa; na mambo hayo nataka uyanene kwa nguvu ili wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Hayo ni mazuri tena yana faida kwa wanadamu”.
Kulingana na biblia Mungu hakutuokoa toka dhambini kwasababu tumetenda matendo mema. Ametupatia baraka ya kuzaliwa upya mara ya pili kwasababu alitupenda na kutuonea huruma. Kwa maneno mengine Yesu Kristo alikuja ulimwenguni, akabatizwa, akafa msalabani alifufuka na hivyo kutakasa dhambi zetu zote. Yesu alifufuka na sasa ameketi kuume kwa Mungu. Kwa kufufuka kwake kati ya wafu mambo yote yasiyokamilika ulimwenguni sasa yamekamilishwa.
Mungu alitubariki na Roho Mtakatifu kwanjia ya Yesu Kristo mwokozi wetu. Yesu Kristo alibatizwa na Yohana ili abebe dhambi zote za ulimwengu na kufa msalabani kwa ajili ya dhambi hizo zote ili tupate msamaha. Tumeokolewa na kuwa wenye haki.
Biblia pia inasema “tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu”. Maana yake ni kwamba, sisi kama warithi wa Mungu ndiyo tutakao urithi utajiri wote wa Mungu. Ili kuenenda katika aina hii ya baraka ya uzima, imetupasa kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu. Imetupasa kuamini injili ya maji na Roho, kusamehewa dhambi zako zote na kuihubiri injili hii kwa wengine. 
Hivyo, kwa kusamehewa dhambi zetu imetulazimu kuitenda kazi kwa manufaa ya wengine tuzifuate sheria za kidunia na kihubiri injili kwa wale wanao mtafuta Mungu. Na nilazima tuwasamehe watu wanao tutendea maovu na kuwatendea wema na upole ili wasiweze kuingilia kazi ya kuihubiri injili njema. “Hayo ni mazuri tena yanafaida kwa wanadamu.” Ikiwa unatamani ujazo wa Roho Mtakatifu itakubidi ukumbuke Paulo alicho sema. Hili laonekana halina maana lakini haya ni maneno muhimu kabisa. 
Kwa kuwa tunaendelea kuishi hapa ulimwenguni hatutoweza kujazwa na Roho Mtakatifu ikiwa bado tuna migogoro na wengine kwa kutotii kwetu kanuni na taratibu za ulimwengu. Hivyo inatubidi kuitii sheria. Ni vyema ikiwa tutachagua kuishi maisha yaliyo na ujazo wa Roho Mtakatifu. Kwetu kutenda matendo mema imetupasa kwanza kuzitii sheria za dunia na kushirikiana na majirani zetu.
 

Je unataka kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu?

Waefeso 5:8-11 ina sema, “kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana enendeni kama watoto wa nuru kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki ya kweli mkihakiki ni nini impendezayo Bwana. Wala msishirikiane na matendo yasiyo zaa giza bali myakemee”. Kifungu hiki kinatueleza kutembea kama watoto wa nuru na kuzaa matunda ya Roho.
Pia Waefeso 5:12-13 inasema “kwakuwa yanayotendeka kwao kwa siri ni aibu hata kuyanena lakini yote yaliyokemewa hudhihirishwa na mtu maana kila kilichodhihirika ni nuru”. Paulo anasema hapa kwamba mambo yote yana yowekwa hadharani au kifichuliwa hutendeka kwa kupitia nuru. Ikiwa mtu mwenye haki hatoweza kuishi maisha ya haki basi atafichuliwa na Mungu au yeye mwenyewe. Nini kitakacho tokea ikiwa mtu atakutwa akitenda matendo ya giza na hivyo kufichuliwa na nuru? Baada ya kukiri makosa yake moyo wake utang’arishwa tena pale atakapo mgeukia Mungu. Lakini yote yaliyo kemewa hudhihirishwa na nuru maana kilicho dhihirisha ni nuru. Ni vyema kudhihirika kwa nuru. Ndipo basi tutakapo weza kuyakubali makosa yetu na kumgeukia Mungu.
Ikiwa hakika tunapenda kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu ni lazima tuwe wema mioyoni. Hata ikiwa mtu hana dhambi moyoni haina maana kwamba haimpasi kuwa mwema. Ni lazima kuishi kwa uzuri na wema mioyoni mwetu. Imetupasa kuhuribiri pamoja na hekima na kuwaombea wale wote wasiyo ifahamu injili ya maji na Roho ili waweze kuielewa na kuweza kusamehewa dhambi zao. Na tusiwadhuru wengine. Yatupasa tule, tulale na tuishi kwa injili na kuwatumikia wengine katika injili pia.
Kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu imetupasa kuwaza umuhimu wa muda na kuitumikia injili njema kama wenye hekima. Tunapo ipenda dunia nirahisi kwetu kuingia katika mitego ya giza na hata kupuuza kutenda kazi ya Mungu. Hivyo imetupasa kumtumaini Bwana na kufanya kile atakacho. Huku tukiamini wokovu aliotupatia Mungu, pia tuwe waangalifu nyakati zote. Mtu wa hekima ya rohoni imempasa kujitolea kuihubiri injili njema duniani kote kabla ya ulimwengu kukumbwa na giza.
 

Fahamu mapenzi ya Bwana.

Yatupasa kujaribu kutafuta namna ya kumridhisha Mungu. Yatupasa kujua yale yote ayatakayo sisi tutende kupitia kanisa lake na maneno yake. Yatupasa kujua nini linalohitajika kufanywa nasi ili tuweze kumpendezesha Mungu na kutathimini mapenzi yake kwetu. 
Watu waliokwisha samehewa dhambi zao ni wale walio zaliwa upya mara ya pili, na watu wa aina hii ni wale watu walio na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani. Wale walio na Roho Mtakatifu ndani yao hakika ndiyo watu watakatifu na watoto wa Mungu. Imewapasa kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu. Hili ndilo jukumu la watakatifu wote. Tusipoteze uwezo wetu na nguvu zetu kwa ajili ya nafsi zetu tofauti na mahitaji ya wengine. Hatupaswi kukwaza kazi za Mungu kwa kwenda sambamba na mtiririko wa nyakati. 
Kama umekwisha takaswa na kupokea uhuisho kwa njia ya upendo wa Mungu lazima tuwe watu wema ili tuweze kuendesha na kuifanya kazi ya Mungu. Kama tumekuwa watoto wa Mungu kwa kumuamini ni haki yetu kuwa watu wenye wema.
Miili ya watoto wa Mungu si mikamilifu lakini Mungu anapendezwa nayo ilimradi tunajihusisha na mapenzi ya Mungu na kutenda mema. Lakini hata hivyo wanaozaliwa upya mara ya pili wanaweza kujikuta wakitenda uovu kwa wengine ikiwa wataishi kwa ajili ya nafsi zao tu. “Tena msilewe kwa mvinyo ambamo mnaufisadi bali mjazwe roho” (Waefeso 5:18). Hii maanayake ni kwamba inatupasa tusilewe kwa tamaa za mwili bali kuzitenda kazi njema. 
Paulo alisema katika Waefeso 5:19-21, “Mkisemezena kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni huku mkiimba na kushangilia Bwana mioyoni mwenu na kumshukuru Mungu baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.” Tukitaka kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu ni lazima tuihubiri injili ya wokovu na kuweka bayana kile Mungu alichofanya kwetu. 
Mungu hutubariki kila tunapofanya maombi na ameweka kumbukumbu ya baraka zote katika Zaburi na tenzi pamoja na nyimbo za kiroho kwa ajili yetu katika kumsifu yeye katika sauti moja. Yatupasa kujisalimisha kumshukuru na kumsifu yeye. Tunauweza kuishi maisha yaliyo jawa na baraka za Roho Mtakatifu pale tunapowaombea wale wote ambao bado hawajaokoka na pia kujiombea sisi kwa sisi. Yatupasa kumshukuru Mungu toka kina cha mioyo yetu na kumtukuza Yesu Kristo aliye tuokoa. Kwa mawazo hayo ndani ya mioyo yetu nilazima kukiri makosa yetu kwa kueleza shukrani zetu kwa kuwa tumetakaswa dhambi na hivyo kumtii yeye. Hivi ndivyo maana ya kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu.
 

Yatupasa kuitumikia injili njema kwa Maisha yetu yote.

Lazima tuweke mipango ya ratiba katika kazi njema na kuitekeleza kwa ajili ya utukufu mkubwa wa injili njema. Katika kujiunga na kanisa la Mungu imetupasa kufanya maombi kwa pamoja na kumwita Mungu ili aokoe roho za kila mmoja. Bado wapo watu wengi ambao hawajaweza kuzaliwa upya mara ya pili kwasababu hawaijui injili njema ingawa wamekuwa wakimtarajia Mungu. Yatupasa kuwaombea watu hawa tukisema, “Mungu tafadhali uwaokoe nao”, pia tusiwe wachoyo wa vitu bali tutoe mali zetu katika kuitumikia injili ili kuwaokoa waliopotea. Kuishi kwa ajili ya roho za wengine na kwa jili ya kuupanua Ufalme wa Mungu ni kufanya kazi njema.
Kwa kufaya aina hii ya kazi maana yake ni kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu. Kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu haina maana kuwa wa uwezo wa kunena kwa lugha na kufanya miujiza, bali ni kujifunza jinsia ya kumridhisha Mungu. Maana yake ni kuamini wokovu wa Mungu aliotupatia, kumsifu Mungu kwa mashairi na Zaburi. Kushukuru kusifu na kumtukuza Mungu kwa moyo wetu wote, na kumtumikia yeye kwa miili yetu ikiwa ni vyombo vya haki ndiyo mapenzi ya Mungu. Kufuata maelekezo yake maana yake ni kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu.
Ili kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu yatupasa tuweke utiii kati yetu na baina yetu. Ikiwa mtu fulani atatupa wazo yatupasa kusikiliza kwa kile anachosema. Kwa njia hiyo pia ikiwa tutatoa wazo kwake naye imemlazimu kusikiliza hata ikiwa hakubalini nasi kwa upande mwengine. Pia yatupasa kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu kwa kuweka utii baina yetu na kutenda kazi ya Mungu.
 

Kuishi maisha ya ujazo wa Roho maana yake ni kumtukuza Yesu Kristo.

Kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu maana yake kufuata amri za Yesu Kristo. Hebu tuone hii maana yake ni nini kwa kusoma katika Waefeso 6:10-13. “Hatimaye mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za shetani kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama: bali ni juu ya Falme na mamlaka za juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya. Vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kushinda siku ya uovu na mkiisha kuyatimiza yote kusimama.”
Nini maana ya kuishi maisha ya ujazo wa Roho? Maana yake ni kuwa imara katika Bwana na kuwa na imani katika nguvu yake. Maana yake ni kuishi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu aliye weka makazi ndani yetu na si kwa utashi wetu pekee. Zaidi ya yote maana yake ni kuishi maisha ya maombi. Kwa maombi twaweza kuishi maisha yenye nguvu kwa kupokea aina mbali mbali za uwezo na baraka Mungu azitoazo. Kwa kuishi maisha ya aina hii maana yake ni kuvaa silaa za Mungu. Sisi ni wadhaifu kiasi kwamba tuanapojaribu kuenenda na Mungu kumtumikia na kumtii yeye hatuwezi kuishi maisha ya ujazo wa Roho ikiwa hatutoshikamana na maneno yake.
Kuamini maneno Mungu ni muhimu katika kutia shime nguvu zetu za kiroho. Hata ikiwa tuna imani yatupasa kuvaa silaha zote za Mungu kwa kusema “na hakika itakuwa kama ilivyo andikwa katika maneno ya Mungu”. Hii ndiyo imani ituwezeshayo kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatiifu.
Je, yupo kati yenu mwenye matatizo katika aina hii ya maisha? Basi kumbuka maneno ya maandiko na uvae silaha zote za Mungu. Mungu ametuelekeza kuvaa silaha zake. Kwa kuyachukulia maneno ya Mungu ndani moyo wako ndipo utakapo jifunza nini maana ya kuvaa silaha zote za Mungu. Haijalishi mazingira na ni kwavipi watu wasemavyo, yatupasa kuyashikilia manaeno ya Mungu. Kwa njia hii tutaweza kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu.
Je, ni wapi tutaweza kuipata imani hii? Ufunuo 3:22 inasema “Yeye aliye na sikio na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”. Yatupasa kusikiliza kile Roho asemacho kwa kanisa. Kwa usemi mwingine hatukuweza kusikia maneno ya Mungu au hata kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu bali kwa njia ya watumishi wa Mungu. Ni kwa watu gani Roho Mtakatifu hunena? Mungu kanena kwa watakatifu na watu wote wa ulimwengu kwa kupitia watumishi wa kanisa lake.
Maana yake ni kusema, yatupasa kuamini mafundisho ya kanisa la Mungu kuwa ndiyo yatokanayo na maneno ya Mungu. Unahitajika kuyakubali mafundisho ya kanisa kwa imani hii katika fikra zako. Ikiwa Roho Mtakatifu hakukaa ndani ya mhubiri ni rahisi kwake kufundisha kwa mawazo yake binafsi. Mhubiri aliye na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yake huubiri maneno ya Mungu chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Ikiwa hafanyi hivyo na badala yake anahubiri maneno yasiyo na msingi wa biblia, Roho Mtakatifu humsimamisha kwa sababu yeye yu ndani ya moyo wake.
Roho Mtakatifu ni Mungu. Mamlaka ya mtumishi wa Mungu hupanda kwa kiwango cha juu zaidi kwasababu Mungu huweka makazi ndani yake. Katika Agano Jipya Yesu Kristo alimwambia Petro, “Nami nitakupa wewe funguo za ufame wa mbinguni” (Mathayo 16:19). Funguo za mbinguni ni injili ya maji na Roho. Kwa maneno mengine injili hii ni funguo wa kuingilia mbinguni. Mungu ametupa mamlaka ya kuhubiri neno lake. Si kwa Petro tu, bali pia kwa kila mtumishi wa Mungu na watakatifu wote endapo tu wamezaliwa upya mara ya pili na kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu.
Kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu yatupasa lazima tuvae silaha zote za Mungu. Ikiwa hatutokuwa na imani yatupasa kuyashikilia mafundisho ya kanisa akilini kila siku kwa kuamini mamlaka ya kanisa na watumishi wa Mungu. Hata ikiwa mahubiri utakayoyasikia siku hiyo hayatokuwa na maana kwako na moja kwa moja hayahusiki na maisha yako, bado amekulazimu kwa vyovyote uyasikilize na kuyachukulia moyoni. Tafuta maneno katika biblia yanayo husika na maisha yako ya kila siku na uyashikilie. Kwa njia hii utakuwa mtu wa imani, na ndipo utakapo weza kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu ukitembea na Mungu na kushinda vita dhidi ya mamlaka na watawala wa ulimwengu wa giza.
Unaweza kuwa umechanganyikiwa kwasababu ulikwisha ambiwa awali kuwa yakupasa uwatii watawala wa dunia, lakini hapa nasema kwamba, imekupasa kupingana dhidi ya watawala wa ulimwengu wa giza. Nyakati za utawala wa Warumi, mtawala wake alijiita kuwa yeye ndiye Mungu na hivyo sheria ilihitaji watu wote kumchukulia yeye kuwa ndiye Mungu. Lakini hili ndilo jambo ambalo Wakristo hawakuweza kulifanya kwasababu lilikuwa ni kinyumbe na Mungu hivyo hawakuwa na uchaguzi zaidi ya kupingana dhidi ya mtawala wa Warumi aliye kuwa akiwashurutisha watu kumsujudia yeye kama Mungu.
Ili uweze kushinda vita dhidi ya shetani, yakupasa kuamini na kushikilia neno la Mungu. Ikiwa tutaishi kulingana na neno la Mungu, tutajipatia baraka zake na kuweza kumshinda shetani. Ingawa tumeokolewa tutweza kushindwa vita dhidi ya shetani ikiwa hatutoshikilia neno la Mungu. Mungu ana tutahadharisha yakwamba, “Kwakuwa mshataki wenu ibilisi kama simba angurumaye, huzunguka zunguka akitafuta mtu ammeze” (1 Petro 5:8). Mtu asiye amini neno la Mungu ataweza kushambuliwa kiurahisi na shetani.
Hata Yesu mwenyewe asingeweza kushinda vita dhidi ya shetani ikiwa pasingelikuwapo neno la Mungu. “Imeandikwa, mtu hataishi kwa mkate tu ila kwa kila neneo litokalo katika kinywa cha Mungu” (Mathayo 4:4). Alimtimua shetani kwa imani ya maneno yaliyo andikwa. Nasi iweje? Tunaupungufu wa hekima na hatulingani na Yesu. Hivyo lazima tuamini na kushikilia zaidi neno la Mungu.
Tusiseme kirahisi, “Nadhani maneno ni ya kweli lakini si wezi kuyaamini yote” Yatupasa kuyashikilia maneno kama, “naamini kila jambo litakuwa ni kweli kama ilivyo andikwa.” Hii ndiyo imani iliyo sahihi itakayo kutuwezesha kuvaa silaha kamili ya Mungu. Wale wasemao, “kila jambo litakuwa kama vile Bwana alivyosema”, hawa ndiyo watakao barikiwa. Ikiwa mtu atashikilia maneno ya Mungu na kuyategemea mambo yatamnyookea kwa kutegeana na imani yake. Hata ikiwa shetani atajaribu kutushawishi bila shaka ataondoka ikiwa tutasema, “Naamini neno la Mungu, naamini neno lake ndilo jibu sahihi.” Hii ndiyo njia ya kuishinda vita dhidi ya shetani.
 

Yatubidi kulishikilia neno la Mungu.

“Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama basi simameni hali mmejifunga kweli kiunoni na kuvaa dirii ya haki kifuani na kufungiwa miguuni utayari tupatao anjili ya amani, zaidi ya yote mkitwaa ngao ya imani ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu” (Waefeso 6:13-17).
Katika mstari, “basi simameni hali mmejifunga kweli viunoni” hapa neno la Mungu linalinganishwa na mkanda uliofungwa kiunoni. Hii inamaana ya kwamba inatupasa kujifunga fikra zetu kwa maneno ya Mungu. Yeye anatuambia kuyafuata maneno ya kweli ili tuweze kuwa na fikra moja na Mungu. Kwa namna ile mkanda unavyotosha kufungwa kwa kuzungushwa kiunoni imetupasa pia kwa kujikaza tujishikilie na neno la Mungu. Tunapokuwa katika fikra mmoja na Mungu kwa asili tunapata uwezo wa kusema, “naamini kila jambo litakuwa sawia na salama. Na hakika kila jambo litawezekana kama Mungu aliivyo sema”. 
Jingine, inatupasa kuvaa dini ya haki kifuani. Yatupasa kuvaa dini ya injili ya maji na Roho kifuani ambayo inasema Mungu alitukoa. Yatuapasa kuvifunga viuno vyetu kwa ile kweli huku tukiwa tumevaa dirii ya haki. Nilazima iwe ya vito vya thamani. Yatupasa kuvaa katika ile imani kwamba Mungu alikwisha tusamehe dhambi zetu zote. Yatupasa kuliamini neno la Mungu kwa moyo wetu wote na kuhubiri injili ya wokovu unaotupa amani.
Baada ya kuyashika maneno haya yatupasa kuvaa viatu miguuni kwa utayari wa injili ya amani na kwenda kuihubiri injili ya wokovu inayoleta amani ya Mungu kwa watu wote. Ikiwa tumekwisha kuokolewa toka dhambini tunawajibu wa kukiri imani yetu kwa vinywa vyetu. Pia hasa pale dhambi zetu na uovu wetu unapodhihirika bayana kwa kujitokeza, basi imetupasa kusafisha kwa kurudia kuwaza kwa kina juu ya ukweli kuhusiana na ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Yatupasa kuishi maisha ya utakatifu kwa kumshukuru Mungu. Yatupasa kuihubiri injili ya maji na Roho yenye kuleta amani kwa kila yule ambaye bado hajakombolewa dhambini mwake.
Zaidi ya yote imetupasa kupigana vita dhidi ya uovu kwa ngao ya imani. Shetani anapotushambulia yatupasa kumfukuzia mbali kwa ngao ya imani mkono mmoja na neno la kweli kwa upande mwingine.
Pia imetulazimu kuvaa chapeo ya wokovu. Imetupasa kuyakubali maneno ya wokovu yasemayo, “niliokolewa kwa dhambi zangu zote kwa njia ya injili maji na Roho, Mungu alinisamehe dhambi zangu kwa njia hii”. Yakupasa kung’amua ukweli katika fikra zetu. Lazima tulifanye neno la Mungu, chepeo ya wokovu na upanga wa roho, kuwa ndiyo silaha dhidi ya shetani.
Ikiwa shetani atakushambulia, yakupasa kuuchomoa upanga na kumshambulia huku ukisema “Mungu amenena hivi! Na ninaamini hivyo!” Tunamfukuza shetani kwa imani ya neno la mungu. Ikiwa tutaamini maneno ya Mungu na kuuchomoa upanga wa kiroho, shetani atakimbia akipiga mayowe “oh! unanijeruhi!” Utaweza kushinda aina yoyote ya mashambulizi ikiwa unaamini neno la Mungu pekee.
Yakupasa uishi katika aina hii ya imani kwa kukiri “mwili wangu si mkamilifu lakini mimi ni mtu wa Mungu aliyekwisha kupokea ukombozi. Naishi kwa imani huku nikishikilia maneno ya Mungu aliyokwisha niambia”. Ikiwa tutakuwa na imani ya aina hii, ndipo tutaweza kumfukuza shetani kwa upanga wa kweli kila wakati anapokuja kutusumbua na kutukwaza katika maisha yetu ya imani. Shetani hatoweza kuchelewa kufumba na kufumbua ikiwa tutamshambulia kwa maneneo ya kidunia tu. Hivyo yatulazimu kumshambulia kwa kusema, “hivi ndivyo Mungu asemavyo” ndipo shetani atakapojisalimisha mbele ya mamlaka ya neno la Mungu. 
Ikiwa tutataka kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu, yatupasa kuomba kwa Mungu ya kwamba kanisa, watakatifu wote na watumishi wa Mungu wajitolee nafsi zao katika kuihubiri injili. Kwa kufanya maombi kama vile “kwa ujasiri hebu nikufunulie siri ya injili” tutaweza kuishi maisha ya kuitumikia injili. Haya ndiyo maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu. Kuishi maisha haya ni muhimu kwa watakatifu wote kama ilivyo ondoleo la dhambi umuhimu wake kwa roho zote. Huu ndiyo mpangilio wa Mungu.
Kwa wale wote ambao wamekwisha kuokolewa toka dhambini lakini hawajui namna ya kuishi maisha ya uaminifu ni lazima sasa kuwa na maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu. Hivi ndivyo Mungu anavyo tuitaji tuishi. Imewapasa watakatifu kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu ambayo ndiyo mapenzi ya Mungu. Maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu huwawezesha watakatifu katika kuihubiri injili kwa kutenda matendo mema. Huwezeshwa kupenda kuihubiri injili na kuiamini, kumwomba Mungu pia na kuyashika manaeno ya Mungu. Yatupasa kuvaa chepeo ya wokovu na dirii ya haki ili kumtimulia mbali shetani kwa kusema “mimi ni mwenye haki muda wote”.
Kwakuwa watakatifu wanauwepo wa Roho Mtakatifu, hutembea kwa roho na kuweza kupokea nguvu ya Roho Mtakatifu. Hufanya kazi ya Mungu kwa baraka ya Mungu ipatikanayo kwa maombi ya imani. Na imewapasa kuenenda kwa roho hadi pale watakapo mshinda shetani na kusimama mbele ya Mungu. Wale wote wanaoweza kuvaa silaha yote ya Mungu ni wale tu walio zaliwa upya mara ya pili katika Kristo, na wataweza kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu.
“Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama bali ni juu ya ufalme wa mamlaka, juu ya wakuu wa giza, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho” (Waefeso 6:12). Vita ya wale walio zaliwa upya mara ya pili si vita ya mwili na damu. Hata hivyo, vita ya wale walio na uwepo wa Roho Mtakatifu ni dhidi ya majeshi ya roho za uovu na dhidi ya wale wote wenye kukwaza maisha yetu ya uaminifu, wasiyo itumikia injili na hivyo kututaabisha.
Tunapojitokeza kupigana vita ya kiroho kwa ajili ya injili ya Bwana, nilazima tuvae chapeo na silaha ya Roho. Ikiwa tutavaa mavazi ya kawaida tu katika vita hii tutajeruhiwa. Hivyo basi yatupasa kuvaa vazi la kivita. Tunahitaji upanga, ngao na chapeo kushinda vita. Inatupasa tuwe wakamilifu katika matayarisho kabla ya vita. Yatupasa kuvaa dirii, tukijifunga kifuani na kuvaa viatu miguu yote miwili. Pia upanga pamoja na ngao. Ndipo hapa lazima maadui zetu watashindwa. Haya ndiyo maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu.
 

Yatupasa kuishika injili njema

Paulo alituambia, “Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu” (2 Timotheo 1:14). Ni ipi iliyo amana nzuri? Ni injili ya maji na Roho ambayo ilituokoa kwa dhambi zetu. Katika Tito 3:5 inasema, “Kwa kwoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu”. Bwana wetu amekwisha takasa dhambi zetu zote tuzitendazo hapa ulimwenguni, akafa msalabani na kufufuka. Yatupasa kuishika injili hii njema. Yatupasa kuvaa chepeo ya wokovu na dirii ya haki na kujifunga viunoni mwetu ukweli. Yatupasa kuiamini injili ya maji na Roho. 
Baada ya kuvaa silaha kwa njia hii lazima tuishinde vita dhidi ya shetani. Ndipo tutakapoweza kuupata ushindi na pia kushiriki na wengine. Yatupasa kupigana vita dhidi ya shetani na kuchukua ushindi kwake hadi siku ile Ufalme wa Bwana utakapokuja, ambao ndiyo urithi wetu. Kiasi cha vita tutakachoshinda dhidi ya adui wetu, ndivyo urahisi wa pambano linalofuata itakavyo kuwa. Yatupasa sote tuombe ufalme wake ustawi na kumea. Ndipo tutakapopata maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu.
Tusiridhike tu na msamaha wa dhambi zetu bali ni lazima tuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu kwa injili na matendo yetu mema. Yatupasa kuamini neno la Mungu, kuongozwa na Roho Mtakatifu na kuishi kwa kushika neno la Mungu na kuliamini ili tusishindwe vita dhidi ya shetani na kuangamizwa.
Je, unanielewa? Hapa ndipo mwanzo wa kuweza kuwa na maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu. Natumaini utaweza pia kuitumikia injili ya maji na Roho na kutegemea zaidi kuyafuata maneno ya Mungu. Hebu sasa natufanye kazi ya Mungu kwa kutumika kuziokoa roho toka kwa shetani. Tutaweza kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu hadi pale Bwana atakapokuja tena. Kupokea ujazo wa Roho Mtakatifu ni amri ya pili ya Mungu aliyotupatia. Nashukuru leo hii tunaweza kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu kutokana na msamaha wa dhambi mioyoni mwetu. Na kama si uwepo wa Roho Mtakatifu nisinge weza kuanza kuishi katika utele huo! Namshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuishi maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu.
Je unaamini kwamba utaweza kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu? Kwetu sisi tulio kwisha samehewa dhambi zetu tunao uwepo wa Roho Mtakatifu. Lakini wote ambao dhambi zao hazijafutwa, bado hawajaweza kupokea uwepo wa Rohoo Mtakatifu. Wale wasio ijua au kuiamini injili ya maji na Roho, hawana uwepo wa Roho Mtakatifu. Watu wote ulimwenguni watatupwa motoni ikiwa hawatokuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu.
Kwakuwa hatuna dhambi mioyoni mwetu, basi tunaouwepo wa Roho Mtakatifu na kwasababu Roho Mtakatifu ameweka makazi mioyoni mwetu, basi twaweza kuishi maisha ya ujazo wake. Sisi tulio na uwepo huo yatupasa kufuta matakwa ya Roho ili tuweze kujazwa naye, kiasi tunacho tii ndicho kiasi tunacho kuwa madhubuti katika imani hata kuwa mashujaa wenye mwelekeo mmoja. Lakini ikiwa tutashindwa kumtii Roho kwetu ni sawa sawa na kuzivua silaha au vazi la kivita. 
Hebu natukue kwa kupitia maneneo ya Roho Mtakatifu hadi kufikia kiwango cha watu wa imani. Tunapo sikia maneno ya Roho Mtakatifu imani zetu hukua kwa sababu Mungu husema “Basi imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:17). Hivyo hata ikiwa shetani atatushambulia sisi, tumekingwa na imani zetu katika maneno haya. Shetani hatoweza kitushambulia sisi tulio kwisha jilinda na ngao ya imani kwa kuamini injili ya naji na Roho. Watu waaminifu huwa na nguvu ya kuyadhibiti mashambulizi ya shetani kwa imani zao. 
Hebu natuishi maisha yaliyo na ujazo wa Roho Mtakatifu kwa imani. Maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu humaanisha kuihubiri injili ya maji wa Roho kwa uaminifu ulimwenguni pote. Hivyo ndivyo maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu yalivyo.