Search

Mahubiri

Somo la 8: Roho Mtakatifu

[8-18] Ukweli uongozao wanao amini kujazwa Roho Mtakatifu (Yoshua 4:23)

(Yoshua 4:23)
“Kwa sababu Bwana Mungu wenu aliyakausha maji ya Yordani mbele yenu hata milipokwisha kuvuka, kama Bwana Mungu wenu alivyoitenda bahari ya Shamu aliyoikausha mbele yetu hata tulipokwisha kuvuka.”
 

Tukio la mto wa Yordani 
linatufundisha nini?
Linatufundisha kwamba Yesu Kristo aliondoa 
kabisa kifo kitokanacho na dhambi 
na hatimaye hukumu ya 
wanadamu.

Ningependa sasa nizungumzie injili njema ya kweli inayotuwezesha kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu. Baada ya kifo cha Musa, Mungu katuletea Yoshua kuiongoza Israeli. Musa alikuwa ni mwakilishi wa sheria katika Agano la Kale. Ikiwa Musa angelivuka mto wa Yordani akiwa na wana wa Israel na kuingia Kanani pasingelikuwepo na umuhimu wa Yoshua kuwa kiongozi wa watu. Hata hivyo Mungu alimwezesha Musa kufika eneo lile karibu na ardhi ya Kanani na kumzuia asiingie.
 

Bwana wetu ametupatia Musa na Yoshua

Musa mwakilishi wa sheria katika Agano la Kale asingeliweza kuwachukua watu na Israeli kuingia Kanani. Kama angelifanya hivyo huku akiwa kiongozi wa sheria angelikwenda kinyume na mpango wa Mungu kwa ajili ya wokovu wetu. Hakuna yeyote awezaye kuwekwa huru kwa dhambi mbele ya sheria ya Mungu kwasababu hakuna yeyote awezaye kufuata sheria kwakuwa sheria ipo kwaajili ya kujua au kufahamu dhambi (Warumi 3:20).
Sababu ya Mungu kumpa mwanadamu sheria ni katika kumpa ufahamu wa dhambi, kuifanya sheria kuwa mwongozo kuelekea kwa Kristo ili aweze kufanywa mwenye haki kwa imani (Wagalatia 3:24). Kwa kuwa sheria haikuwa na jingine zaidi ya mwongozo kumwelekea Yesu Kristo, hivyo watu wanamhitaji Yesu na ndiyo maana ilimpasa kuja ulimwenguni. Kile Mungu alichomwagiza Yoshua ni kuwaamrisha Waisraeli kuvuka mto Yordani na kuingia nchi ya Kanani.
Mungu aliwawezesha kuingia nchi ya Kanani wakiwa na kiongozi wao mpya baada ya kifo cha Musa. Yoshua aliamrisha viongozi wa makundi akisema, “piteni katika ya matuo, mkawamuru hao watu mkisema, fanyeni tayari vyakula kwa maana baada ya siku tatu mtavuka mto huu wa Yordani ili kuingia na kumiliki nchi awapayo Bwana Mungu wenu mpatekumiliki” (Yoshua 1:11).
Mungu alimwamuru Yoshua aingie Kanani baada ya kuthibitika kwamba isingewezekana kwa kupitia Musa. Mungu alimwamuru Yoshua akisema, “Nawe uwaamuru hao makuhani walichukuao sanduku la agano, ukawaambie, mtakapofika ukingo wa maji ya Yordani, simameni katika Yordani. Basi Yoshua akawaambia wana wa Israeli njooni huku mkayasikie maneno ya Bwana Mungu wenu. Yoshua akasema kwa jambo hili mtajua kuwa Mungu aliyehai yu kati yenu na yakuwa hatakosa kuwatoa mbeleyenu na mbele ya Mkaanani, Mhiti na Mhivi na Mperizi na Mgirgashi na Mwamoni na Myebusi” (Yoshua 3:8-10). 
Baada ya kifo cha Musa Mungu alimteua Yoshua kuwa kiongozi wa Israeli na kumwamuru aingie nchi ya Kanani na watu wote Israeli. Jina Yoshua maana yake “mwokozi”. Kwa tafsiri nyingine “Yesu” au “Hosea”. Mtumishi huyu wa Mungu Yoshua aliwaamuru makuhani kubeba sanduku la Agano na kuvuka mto Yorudani huku akiwaongoza watu. Pale makuhani hawa waliobeba sanduku walipo tumbukiza miguu yao ndani ya maji (kwa kua mto Yordani humwanga maji yake pwani nyakati wa mavuno) basi maji yale yatokayo juu ya vijito yali simama na kujaa mbali na Adamu mji ulio kando ya Zarelani. Hivyo maji yaliyokuwa ya kimiminika baharini yalikatwa na kuweza kufanya watu wavuke upande wa pili wa Jeriko (Yohana 3:15-16). 
Kwa tukio hili Mungu hutufundisha sisi kwamba, alikwisha kutuondolea mbali kifo moja kwa moja kile kitokanacho na dhambi na kufuta hukumu ya mwanadamu. Kwa maneno mengine Yesu Kristo mwokozi wetu alizichukua dhambi zote za wanadamu pale alipo batizwa na Yohana Mbatizaji na kusulubiwa. Kwa njia hii basi, aliokoa wanadamu tokana na dhambi zao kwa kuwaongoza katika nchi ya Kanani amabayo inasimama badala ya Ufalme wa Mungu.
 

Mto Yordani ni mahala mwanadamu alipo takasawa.

Matukio ya kihistoria yanayo husishwa na kuvuka mto Yordani kama ilivyo andikwa katika Agano la Kale na Agono Jipya, ni mojawapo ya matukio ambayo yana umuhimu mkubwa ambako ndiko kuliko pelekea tukio la wokovu tokana na laana na hukumu zitokanazo na dhambi za wanadamu.
Mto Yordani kwetu unamaana ya mto wa mauti, na mwisho wa mto huu ni bahari ya Chumvi (hii ni bahari isiyo na uhai wowote ndani yake kwa sababu ya kiwango kikubwa cha chumvi zaidi ya kile cha bahari ya kawaida.) Neno Yordani maana yake “mto pekee ambao hutiririkao, kuelekea kifoni” au “kuzama, kudidimia, kugandamizwa chini, kushuka”. Kwa uwazi hili linatuthibitishia juu ya historia ya dhambi za wanadamu. Katika mto huu, Yesu kwa kupitia ubatizo wake, alimiminiwa dhambi zote zitokanazo na wandamu, na baadaye kufa msalabani na hivyo kupokea hukumu badala yao hao wanadamu.
N wapi tulipokuwa tukielekea sisi ambao ni uzao wa Adamu na Hawa? Kwakuwa viumbe wote huzaliwa na dhambi, hutenda dhambi, na kwa jinsi ya mshahara wa dhambi hizo hujikuta wakielekea mautini. Kwa kipindi chote cha historia ya wanadamu, viumbe wote wamekuwa wakielekea katika kuangamia toka kuzaliwa kwao. Ingawa hujaribu kwa uwezo wote kutawala asili yao ya dhambi, bado hushindwa na ndiyo maana huzidi kuijongea hukumu ya mwisho kwa dhambi zao.
Hata hivyo Mungu alikata mtiririko wa dhambi na hukumu. Mungu alimpa Yoshua mwongozo wa kuwapeleka watu wa Israeli katika nchi ya Kanani kwa kuvuka mto Yordani. Haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa Yoshua. Habari hii inamaanisha kwamba, ili kuweza kuwa huru kwa dhambi, yatupasa kulipa mshahara wa dhambi, ambao ni mauti, na hivyo kwamba kwa njia ya gharama hii ndipo basi tunatakaswa kwa dhambi zetu zote na kuingia mbinguni.
Katika Agano la Kale, mtiririko wa mto ulisimamishwa na ukabadilishwa na kuwa ardhi kavu pale makuhani walipo tumbukiza miguu yao katika mto. Hili ndilo ondoleo la dhambi ambalo lililotolewa kwa wale tu walio amini injili njema. Hii ndiyo iliyo kuwa injili ya maji na Roho iliyo lipia mshahara wa dhambi za wanadamu na hivyo kuwezesha kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu kwa imani.
 

Jemadari Naamani.

Naamani anaye simuliwa katika 2Wafalme 5, alikuwa ndiye jemadari mkuu wa majeshi na kamanda wa jeshi la Shamu mwenye kueshimiwa na aliye okoa nchi yake kutoka kwa maadui. Pia alikuwa nikiwete aliye na hatima yakupoteza kila kitu kwa sababu ya laana. Lakini hapo baadaye aliweza kuisikia habari njema ambayo ingemwezesha kumwokoa tokana na laana hii. Ilisemekana kwamba angeliweza kuponywa endapo angefunga safari na kwenda kumwona mtumishi na Mungu aliyeishi Israeli. Alikuwa ni msichana mdogo kijakazi ndiyo aliye leta habari hizi. Alimwambia “Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule na bii aliyeko Samaria maana angemponya ukoma wake” (2 Wafalme 5:3).
Ndipo alipo amini habari hizi na kwenda na Israeli. Alipowasili mbele ya nyumba ya Elisha, naye Elisha akamtuma mjumbe kwake “Enenda ukaoge katika Yordani mara saba na nyama ya mwili wako itakurudia, nawe utakuwa safi” (2 Wfalme 5:10). Akitarajia muujiza wa uponyaji, Naamani alighadhabika na kuamua kurudi nchini kwake. Hata hivyo kwa sababu ya watumishi wake kumsihi, alikubali kumtii Elisha na kushuka katiaka maji na hivyo kuzamisha mwili wake wote mara saba katika mto Yordani. Ndipo mwili wake uliporudi upya mara moja na kuwa kama mwili wa mtoto mchanga. 
Kwa njia hiyo pia nasi tumekuja kujua kwamba, ili tuweze kusamehewa dhambi zetu zote, yatupasa kuachana na fikra zetu na kukubali kile kilicho andikwa katika biblia. Ndipo tutakapo weza kupokea baraka njema. Yeyote atakaye kuokolewa yampasa kutii maneno ya Mungu na kuyaamini yote.
Biblia inasema kwamba dhambi zote za ulimwengu zilisafisha kwa njia ya injili ya ubatizo wa Yesu Kristo na damu yake. Tusiwe na fikra sawa na zile za Naamani. Kamwe hatutoweza kutakaswa kwa dhambi zetu pasipo kwa njia ya injili ya maji na Roho. Hivyo ili tuweze kusamehewa dhambi zetu zote, inatupasa kuiamini injili njema ya maji na Roho. Kama vile Naamani ilivyo weza kutakasa kwa kuzamisha mwili wake mara saba katika maji, nasi tunaamini kwamba tutaweza kutakaswa dhambi zetu kwa kuamini injili njema ya ubatizo wa Yesu, kusulubishwa kwake msalabani na kufufuka kwa kweli. Yatupasa kuihubiri injili njema kama ilivyo.
Muujiza huu katika mto Yordani, unawakilisha kizazi chote cha Adamu kwa baraka ambayo inaondelea mbali mtiririko wa dhambi zote na kuhitimisha hukumu. Wanadamu wote walifukuzwa toka bustani ya Edeni kwa sababu ya Adamu na Hawa kutenda dhambi kwa kushawishiwa na shetani. Hata hivyo tukio la Yordani ilikuwa ni injili njema ambayo iliwaongoza wanadamu kurudi katika bustani ya Edeni tena.
 

Tukio la mto Yordani.

Biblia imeandika juu ya habari njema kwamba Yesu alijitwika dhambi zote pale Yordani. “Kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo ipasavyo kuitimiza haki yote” (Mathayo 3:15). Biblia inatangaza kwamba dhambi zetu zilitwikwa kwake Yesu pale alipobatizwa katika mto Yordani. Kwa maneno mengine, ubatizo wa Yesu ni tukio lililo katilia mbali mnyororo wa dhambi uliowafunga wanadamu wote. Hivi ndivyo Yesu alivyoweka kikomo cha dhambi na hatimaye kutoa wokovu kwa malipo ya damu yake msalabani. 
Yordani ni mto wa ubatizo ambao husafisha dhambi zetu zote. Tuliweza kutimiza sheria ya Mungu isemayo, “Mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23) kwa sababu Yesu amelipa mshahara kwa kubatizwa katika mto Yordani na kufa msalabani. Hii ndiyo injili njema ambayo Bwana wetu ametupatia sisi wanadamu.
Dhambi zote za wanadamu zilianzia kwa Adamu lakini zikakomea katika ubatizo wa Yesu katika mto wa Yordani na damu yake msalabani. Hakuna dhambi iliyobaki kwa shukrani ya ubatizo wa Yesu. Hakika hii ndiyo baraka njema na habari njema. Nasi kwa kuiamini injili hii njema, tumeokolewa na mtiririko wa dhoruba ya dhambi, kutakaswa kwa dhambi zetu na kuweza kusafishwa katika sheria ya ukombozi ya Mungu. Kwa jinsi hiyo, ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani ndiyo injili inayo waokoa wanadamu wote. Yatupasa tuamini hili kwa hakika. “Nakila tendo lisilo tokana katika imani ni dhambi” (Warumi 14:23) asema Bwana Kwa jinsi hiyo pia, tunabarikiwa ikiwa tu tutaamini injili hii njema.
Je, ungali na dhambi moyoni, ikiwa ukweli unadhihirisha kuwa dhambi zote zilitwikwa juu yake Yesu pale alipo batizwa na Yohana? Yesu alizichukua dhambi zote za ulimwengu. Yakupasa ukubaliane na kile kilicho andikwa katika Biblia. Hii ndiyo injili ya ubatizo wake na damu yake msalabani ambayo ndiyo pekee itakayo weza kufuta dhambi yako na kukukinga na kifo pamoja na laana zote. Ubatizo maana yake “kusafishwa, kuzikwa, kutwikwa au kuhamishia”.
Wanadamu wote wataweza kusamehewa dhambi kwa kuamini injili njema iliyoletwa na Yesu. Na ndiyo maana Yesu amejiita yeye kuwa ni “njia ya kwenda mbinguni” Tutaweza kuingia mbinguni na kuweza kuwa na uzima wa milele kwa kumwamini yeye kuwa ni Bwana aliyetupatia uwepo wa Roho Mtakatifu. Tumetengwa na hukumu zote za dhambi kwa kuamini ubatizo wa damu yake.
Laana imeisha na mto umegeuka kuwa ardhi kavu kwa sababu makuhani walio beba sanduku la agano walitumbukiza miguu yao ndani ya maji kwa imani. Hivi ndivyo Mungu alivyopanga kwa ubatizo wa Yesu na damu yake yote haya yakiwa ndiyo injili njema. Hii ilikuwa ndiyo sheria ya wokovu na pasipo hivyo basi, hakuna wokovu. Wale waminio injili hii njema kwa sasa wataweza kuvuka mto Yordani na kuingia nchi ya Kanani. Maji yalikauka kabisa, kwa jinsi hiyo dhambi zetu zote ulimwenguni ziliwekwa juu yake Yesu na hivyo kupelekea kuhukumiwa kwa niaba yetu. Hii ndiyo injili inayo tupatia uwepo wa Roho Mtakatifu. 
Mungu aliyeumba wanadamu hujua kwamba kiwango cha kawaida cha ufahamu wa mtu (IQ) ni kati ya kipimo cha 110 hadi 130. Hivyo hawezi kufanya ukweli huu kuwa mgumu kueleweka ili kumpokea Roho Mtakatifu. Mungu aliziondoa dhambi zetu zote kwa ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Amefanikisha katika kumpokea Roho Mtakatifu ili kwamba watu wote waweze kujua hili. Pia utakuja kugundua kwamba uwepo wa Roho Mtakatifu huja kwa kuiamini injili njema. 
Kulingana na kile kilichoandikwa katika biblia, hatutaweza kupokea Roho Mtakatifu kwa njia ya maombi na kutubu. Watu hudhani ya kwamba Roho Mtakatifu ni kitu kitolewacho pale unapofanya aina nyingi za maombi. Lakini kwa kifupi hivyo sivyo ilivyo. Roho Mtakatifu hutolewa kwa wale wanao amini injili njema na hatimaye kufanywa kuwa watoto wa Mungu. Uwepo wa Roho Mtakatifu ni uthibitisho kwamba mtu amekuwa ni mwana wa Mungu. Mungu huwapa Roho Mtakaifu wale wote wenye kuamini injili njema kama uthibitisho wake.
Ikiwa watu watamwamini Yesu lakini huku hawajui au kuamini injili hii hakika kamwe hatoweza kuwa na uhakika kama kweli dhambi zao zote zilitwika juu yake. Hivyo watu wote ni lazima waijue na kuiamini injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani ambayo ndiyo injili njema iliyo futa dhambi zetu zote. 
Ni nani anayeshuhudia kwamba Yesu alichukua dhambi zote za ulimwengu? Yohana mbatizaji ndiye ashuhudiaye. Kwa kuwa alimbatiza na Yohana na kubeba dhambi zote za ulimwengu hivi ndivyo Mungu Baba yetu alivyo panga (Warumi 4:13-21, 16:1-30). Ni nani aliyetekeleza mpango huu? Yesu ndiye aliye tekeleza. Ni nani anayeleta uhakika wa kutimizwa kwa mpango huu mwishoni? Roho Mtakatifu ndiye aletaye. Mungu ni Utatu Mtakatifu utimizao ondoleo la dhambi kwa ubatizo na damu ya msalabani na hivyo kutufanya kuwa watoto wake. Roho Mtakatifu huweka makazi ndani yetu na kutupa uhakika yakwamba tumekwisha okolewa toka dhambini pale Yesu alipo timiza mpango wa Mungu.
Je mambo ya ulimwengu huonekana kuwa ni magumu na yakuchanganya? Na ni kwakiasi gani mawazo yako yamechanganyikiwa? Mtu hawezi kuamini injili hii njema ikiwa hatoachana na fikra zake binafsi za mafundisho ya Ukristo wa nyakati hizi ambayo wengi huamini ni yale yasemayo “dhambi za asili zimefutwa lakini zile za kila siku husamehewa pale mtu anapoomba toba”. Hata hivyo hili ni mbali kabisa na ukweli kamili; kwa hakika ni injili ya ulaghai. Ikiwa unaamini hili hutoweza kamwe kuielewa biblia toka mwanzo hadi mwisho, na kwa kadiri muda utakavyo kwenda utakumbana na ugumu zaidi katika maisha ya kumfuata Yesu. Na ndiyo maana katikati ya wakristo wapo wale wenyekuamini injili tofauti na Mungu tofauti.
Baadhi yao husema kwamba, wamepokea uwepo wa Roho Mtakatifu kwa “maombi”. Inawezekana ikaonekana kuwa ni ukweli, lakini biblia inaelezea kwamba Roho Mtakatifu alitua juu ya Yesu kama huwa pale alipobatizwa na kutoka majini. Hii ndiyo injili ya kweli ambapo Roho mtakatifu huja juu ya wale wote wanao iamini injili.
Kwa nyongeza baadhi ya watu husema kwamba wamepokea Roho Mtakatifu kwa kufanya sala za toba. Je, Roho Mtakatifu hutolewa pale watu wanapofanya sala za toba tu? Mungu ni wa haki. Roho Mtakatifu haji kwasababu yeye kaona huruma kwao. Haijalishi ikiwa watu watalia au kusali kwa bidii, Roho Mtakatifu kamwe hawezi kuja juu yao. Yeye hushuka juu ya wale wote walio amini ya kwamba, Mungu alikwisha timiza mpango wake wa kuwaokoa. Yakupasa uwe makini, nakwamba hutoweza kumpokea Roho Mtakatifu hata kama utakaa kwa muda mrefu na kusali mbele za Mungu. Roho Mtakatifu yuko nje ya mapenzi ya mtu.
Hata maamuzi ya kihistoria ya mwanadamu katika dunia hii huweza kubadilika, lakini injili njema na sheria ya uwepo wa Roho Mtakatifu havibadiliki; hivyo haviwezi kufutika. Ikiwa watu hawaelewi juu ya injili njema ni vigumu kwao kurudi katika matendo ya imani ya kweli. Ni kwasababu hiyo basi watu wengi hawawezi kumpokea Roho Mtakatifu. Utajisikiaje kuangushwa ikiwa umemwamini Yesu lakini hatimaye ukaangamia kwasababu tu hukuwa unaijua injili njema? Biblia inasema kwamba kwa baaadhi ya watu injili njema ya Yesu ni kikwazo kwao na mwamba uangushao.
Ikiwa umekwisha elewa juu ya maajabu ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana basi hakika utaweza kusamehewa dhambi zako na kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu. Yeye ndiye aliye okoa watu wote kwa kubatizwa kwake, kufa kwake msalabani na kufufuka kwake. Ukombozi Yesu aliouleta kwetu ulikuwa ndiyo njia ya haki ya wokovu. Amekuwa mwokozi wa kweli wa wenye dhambi wote na kutuhitimishia kwa uwepo wa Roho Mtakatifu.
 

Nipale tu, utakapo amini!

Imeandikwa katika biblia Agano la Kale, yakwamba, pale makuhani walipo zamisha miguu yao katika mto Yordani, ndipo mto ulipo kauka. Ni maajabu tosha kwa maji kusimama, lakini miujiza mingi ilifuatia. Cha ajabu zaidi ni mto kugeuka kuwa ardhi kavu. Tukio hili lilithibitsha uhakika wa wokovu wa Mungu aliopelekea ondoleao la dhambi kwa njia ya ubatizo wa Yesu na damu yake masalabani. Ardhi kavu inawakilisha vile dhabi zote za ulimwengu vile zingekuja kusemeahewa kwa shukrani ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Dhambi zote zilianzia toka kwa Adamu hadi wanadamu wote lakini laana iliisha kwa ubatizo wa Yesu. Hivyo kile tunacho paswa kufanyani kusamehewa dhambi zetu zote kwa kuwa na imani na hivyo kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu. Je unaamini ukweli huu mzuri ambao Yesu alizibeba dhambi zetu zote kwa njia ya ubatizo wake pale mto Yordani?
Inakubidi uamini kwamba Yesu Kristo alibatizwa ili aweze kubeba dhambi za ulimwengu. Kwa nyongeza, inakupasa pia kujua, kuelewa na kuamini kwa jinsi gani umuhimu wa ubatizo wake ulivyo kuwa. Ikiwa makuhani wasingeli ingia Yordani, watu wa Israeli wasingeliweza kuingia kwa urahisi katika nchi ya Kanani. Hatua moja muhimu ya kwanza katika kuingia Kanani ilikuwa ni kuvuka mto Yordani. Hivyo ikiwa tutavuka mto Yordani na sanduku la Agano, ndipo basi tutaweza kuingia nchi ya Kanani. Hii inatufundisha kwamba mtu aweza kusamehewa dhambi zake kwa kuamini injili ya maji na Roho.
Biblia inasema kwamba ubatizo wa Yesu ilikuwa ni kazi ya Mungu. Hili pia lilitokaea kwa kulinganisha na makuhani. Kama vile maji ya mto Yordani yalivyo simama pale makuhani walipo tumbukiza miguu yao katika maji, nao watu wa ulimwengu wataweza kuokolewa kwa dhambi zao kwa kuamini injili hii.
Uwepo wa Roho Mtakatifu hutunukiwa kwa msingi wa imani ya injili hii njema ya ubatio wa Yesu na damu yake msalabani. Injili hii itakuongoza katika kupokea msamaha wa dhambi na Roho Mtakatifu. Injili hii njema ya maji na Roho ni jambo lisilowekwa kando katika kujipatia uwepo wa Roho Mtakatifu.