Search

Mahubiri

Somo la 11: Maskani

[11-11] Sisi Hatumo Miongoni Mwao Wanaosita na Kupotea kwa Sababu ya Dhambi Zetu (Yohana 13:1-11)

Sisi Hatumo Miongoni Mwao Wanaosita na Kupotea kwa Sababu ya Dhambi Zetu
(Yohana 13:1-11)
“Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo. Hata wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simon Iskariote, moyo wa kumsaliti; Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu, aliondoka chakulani; akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa akajifunga kiunoni. Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga. Hivyo yuaja kwa Simon Petro. Huyu akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi? Yesu akajibu, akamwambia, nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye. Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, kama nisipokutawadha huna shirika nami. Simon Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hata na mikono yangu na kichwa changu pia. Yesu akamwambia, Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote. Kwa maana alimjua yeye atakaye msaliti; ndio maana alisema Si nyote mlio safi. Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea? Ninyi mwaniita, Mwalimu, na Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo ilivyo.”
 

Neno lote la Biblia ni fumbo kwa walimu wa uongo ambao hawajazaliwa tena upya. Kwa hiyo wanajaribu kulifafanua Neno la Mungu kwa namna yao wenyewe kwa mawazo yaliyoundwa na mwanadamu. Hata hivyo, wao wenyewe hawashawishiki kuamini kile wanachokifundisha. Kama matokeo ya hali hiyo, hata miongoni mwa wale wanaoamini katika Yesu, kuna wachache sana wenye uhakika wa wokovu wao.
Kwa nini hali iko hivi? Ni kwa sababu wanasema kuwa wanaamini katika Yesu hata pale ambapo hawaifahamu injili ya maji na Roho. Wakristo wa jinsi hiyo wanafikiria kuwa hawataharibiwa kwa sababu wanaamini katika Yesu. Lakini wanatakiwa kutambua kuwa jambo hili likitazamwa toka katika mtazamo wa kibiblia, ni ukweli ambao haujakamilika kwao kuwa wanastahili kuharibiwa la sivyo wazaliwe upya tena kwa maji na kwa Roho.
Ni imani ya kijumla inayoshikiliwa na watu kufikiri kuwa ingawa hawaufahamu ukweli, na kwa sababu wanaamini katika Yesu kwa upofu, basi angalau hawataweza kuharibiwa. Hata hivyo, kama vile ambavyo hawawezi kulifahamu Neno kiusahihi, basi kwa kweli hawawezi kutambua toka katika Neno kwamba wanaamini kimakosa hata pale wanapokuwa bado hawajaokolewa kikamilifu. 
Hivyo, ikiwa watu wanalifafanua Neno la Biblia kimaandiko na kisha wakatoka na mafundisho yao yenye msingi katika mawazo yao binafsi, basi watu wa jinsi hiyo, hata kama walimwamini Yesu Kristo, hawawezi kupokea ondoleo la dhambi na kwa hakika wataishia kuzimu kwa sababu ya dhambi zao. Kwa hiyo, Biblia si kitu ambacho tunapaswa kukifumbua kwa njia zetu binafsi, bali ni lazima tumngojee Mungu atupatie ufahamu kwa kupitia watakatifu wake waliozaliwa tena upya kwa Neno la kweli. Ni lazima pia tutambue kuwa Neno lote la Mungu linaelezewa ndani ya Injili ya maji na Roho. 
Yesu alisema, “Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu” (Yohana 3:5). Wale wanaofahamu na kukiamini kifungu hiki kiusahihi kwa hakika wanaweza kukombolewa toka katika dhambi zote na kisha kuungia Ufalme wa Mbinguni. Yesu alisema kwamba ni wale tu ambao mioyo yao imesafishwa toka katika dhambi kwa kuiamini injili ya maji na Roho ndio wanaoweza kuingia Mbinguni. Lakini ikiwa watu wanaamini pasipo kuifahamu injili ya maji na Roho iliyotolewa na Bwana—ambayo ni ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa za Hema Takatifu la Kukutania—basi wataharibiwa kwa sababu ya dhambi zao. 
Ikiwa tutaharibiwa kwa sababu ya dhambi zetu hata pale tunapomwamini Yesu, Je, halitakuwa ni jambo la kukatisha tamaa hilo? Kwa kweli inanisikitisha sana mimi kwa undani kufikiri kwamba ingawa kuna watu wengi sana katika ulimwengu huu wanaoamini katika Yesu kuwa ni Mwokozi wao, wengi wao hawawezi kujibu kwa kujiamini pale wanapoulizwa ikiwa wana hakika kuwa wameokolewa toka katika dhambi zao zote. Hakuna kosa kusema kwamba wenye dhambi wote bila kujalisha kuwa wanamkiri Yesu au la, wataharibiwa kwa sababu ya dhambi zao. Je, ni watu wangapi ambao kweli wataharibiwa hata pale wanapoamini katika Yesu? 
Mathayo 7 inatueleza sisi kuwa ingawa wengi wanaoamini katika Bwana watamwambia Yesu kwamba walitabiri, walifukuza mapepo, na kwamba walifanya vitu vingi vya kushangaza kwa jina lake, bado Yesu atawaacha. Yesu alisema kwamba atawaambia watu hao, “Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu!” (Mathayo 7:23). Bwana wetu alisema kuwa si kila mtu anayeliita jina lake ataingia Mbinguni. Vivyo hivyo, Bwana atawakemea wale ambao wameielewa vibaya injili ya maji na Roho. 
Pamoja na hayo watu wengi hawatambui kuwa wameelewa na kuamini vibaya katika Yesu, hali ambayo ni ya kuhuzunisha sana kwa Bwana wetu. Ukiachilia kuwa kuna watu ambao Bwana wetu anawakemea kwa kuwa na imani yao potofu, bado kuna watu wengi ambao wanaelekea katika maangamizi yao binafsi. 
Hii ndiyo sababu mioyo yetu inaomboleza kwa ajili ya Wakristo wa sasa wa mazoea. Wanamwamini Yesu kiholela hali wakiwa hawawezi kuifahamu maana ya kweli ya injili ya maji na Roho jinsi ilivyo kibiblia. Hii ndiyo sababu ni muhimu sana kwetu kuihubiri injili ya maji na Roho kwa watu wote wa jinsi hiyo. 
Ni muhimu sana kwetu sote kufahamu na kuamini katika injili ya maji na Roho. Je, tunawezaje basi kuufahamu ukweli wa injili ya maji na Roho? Kwa kweli ni kwa kuyasikia mafundisho juu ya injili ya maji na Roho yaliyomo katika Neno la Mungu. Kwa kweli ni lazima tuufahamu na kuuamini ukweli wa injili ili tuweze kuitwa na Mungu kuwa ni watakatifu wake. Ni kwa kufanya hivyo ndipo tunapoweza kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa imani, kupokea ondoleo la dhambi kwa imani, na kisha kufanyika wana wa Mungu kwa imani. 
Hii ndiyo sababu Ukristo unalenga katika wokovu unaopokelewa kwa imani. Dini za ulimwengu zinasifia matendo ya mtu binafsi. Lakini ukweli halisi unatuambia sisi kuwa wokovu ni karama ya Mungu, na si kwa matendo ya mwanadamu, mtu awaye yote asije akajisifu (Waefeso 2:8-9). Ukristo wa Kweli unaionyesha njia ya kuweza kuokolewa toka katika dhambi na kuingia Mbinguni kwa kufahamu na kuamini katika injili ya maji na Roho tu. 
Kifungu kikuu cha leo toka katika injili ya Yohana kinahusu injili ya maji na Roho. Hali akijua kuwa saa yake imefika ya yeye kufa Msalabani, Yesu alifikiria kuiosha miguu ya wanafunzi wake. Na hii ilikuwa ni mara kabla ya Sikukuu ya Pasaka. Sikukuu ya Pasaka ni ya muhimu sana kwa Wayahaudi. Kwa kuwa ilikuwa ni siku ambayo watu wa Israeli walipotoroka toka Misri na wakaokolewa toka katika utumwa wao, siku hii imefanyika kuwa ni siku kubwa sana kwa Wayahudi. Kwa hiyo watu wa Israeli waliikumbuka Sikukuu ya Pasaka ya Agano la Kale na waliishikilia kwa kuifanyia kumbukumbu kwa kufanya taratibu za kidini za Pasaka pamoja. 
Wakati wa chakula cha jioni, Yesu aliwakusanya wanafunzi wake pamoja na akaamua kuwaeleza wanafunzi wake kitu ambacho kinabeba umuhimu mkubwa sana. Kwa kuiosha miguu ya wanafunzi kabla yeye mwenyewe hajafariki Msalabani, Yesu alitaka kuwafundisha wanafunzi wake kuhusu ukweli ambao umeziosha dhambi zao halisi. Kwa kuja kwa Sikukuu ya Pasaka, Yesu alifahamu kuwa atakamatwa kama Mwanakondoo wa Pasaka, na kuwa atasulubiwa, kufa, na kisha kufufuka tena toka kwa wafu. Kwa hiyo Yesu alitaka kuwafundisha wanafunzi wake kwamba kama Mwanakondoo wa sadaka ya kuteketezwa, amezioshelea mbali hata dhambi zao halisi. Tukiliweka jambo hili katika sura nyingine, Yesu aliiosha miguu ya wanafunzi wake ili aweze kuwapatia fundisho muhimu sana kabla ya kufa Msalabani.
 


Sababu Iliyomfanya Yesu Kuiosha Miguu ya Petro

 
Hebu tuangalie jinsi Yesu alivyosema alipoamua kuwaosha wanafunzi miguu yao na kisha Petro akakataa: “Kama nisipokutawadha, huna shirika nami” (Yohana 13:8). Msemo huu ni wa muhimu na wakutisha kiasi gani? Hata hivyo, Yesu alitaka hasa kuwafundisha wanafunzi wake kuwa ni aina ipi ya imani iliyotumika kuzioshelea mbali dhambi zao halisi, na jinsi ilivyokuwa muhimu kwa wanafunzi wake wote na Yeye mwenyewe kwamba alipaswa kuwaosha miguu yao kabla ya kufa Msalabani. 
Hivyo, Yesu aliondoka chakulani akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa akajifunga kiunoni, kisha akatia maji katika bakuli akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu. Kisha ikafuata zamu ya Simon Petro, lakini Petro aliendelea kukataa. Alimwambia Yesu, “Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi?” Petro alipigwa na mshangao kwamba Yesu anataka kuiosha miguu yake. Kwa sababu alimwamini Yesu na alimtumikia kama Mwana wa Mungu, ilikuwa ni vigumu kwake kulipokea jambo kama hilo ambalo kwake halikuwa na maana. Na hii ndiyo sababu Petro aliuliza inawezekanaje kwa Bwana kutaka kuiosha miguu yake, akidhani kuwa kama ingelikuwa ni suala la kuoshana miguu, basi ni yeye Petro ndiye alipaswa kuiosha miguu ya Bwana, na pia aliona wazi kuwa haikuwa sahihi kwa yeye kumruhusu Bwana kuiosha miguu yake. Basi, hali akiwa ameshtushwa na jambo hili, Petro alisema, “Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi?” kisha akakataa kuoshwa miguu. 
Kisha Yesu akasema katika aya ya 7, “Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.” Hii ilimaanisha kuwa, “Kwa sasa wewe hufahamu kwa nini ninafanya hivi. Lakini baada ya kufa Msalabani, kufufuka toka kwa wafu na kisha kupaa Mbinguni, ndipo utakapoitambua sababu kuwa ni kwa nini niliiosha miguu yako.” Kisha Yesu akasema katika hali ya kulazimisha, “Kama nisipokutawadha, huna shirika nami.” Pasipo Yesu kuiosha miguu ya Petro, basi Petro na Yesu wasingekuwa na lolote la kuhusiana kati yao. Kutokuwa na shirika na Yesu maana yake ni kutokuwa na uhusiano na na yeye, hivyo Petro hakuwa na chaguo zaidi ya kuiweka miguu yake mbele ya Yesu. Kisha Yesu akaiweka miguu ya Petro katika beseni, akaiosha, kisha akaifuta miguu yake kwa taulo. 
Wakati Bwana aliposema kwa Petro, “Kama nisipokutawadha, huna shirika nami,” Petro alisitushwa na kauli hii, ndipo akasema, “Basi nioshe zaidi ili kwamba niwe na shirika nawe. Nioshe miguu yangu, kichwa changu, na mwili wangu wote!” Baada ya kusikia haya Yesu alisema, “Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote.”
Mara nyingi Yesu alitamka yale ambayo yaliwafanya watu kutekewa na kuchanganyikiwa kwa muda. Hali wakishindwa kufahamu yale ambavyo Yesu aliyasema, watu walijifanya kuyafahamu vibaya, kutoamini, na kufanya vitu vya kipuuzi. Wale ambao hawajapokea ondoleo la dhambi kwa kutoamini katika injili ya maji na Roho hawawezi kufahamu kiusahihi kile ambacho Yesu alikiongea kwa Petro katika kifungu hiki. Kwa nini? Kwa sababu wale ambao hawana Roho Mtakatifu hawawezi kuifahamu maana sahihi ya Neno la Mungu. 
Si kila mtu anaweza kuutambua ukweli uliofunuliwa katika Biblia, hata kama yeye ni mwenye akili na vipawa kiasi gani vya kidunia. Watu wa jinsi hiyo wanayafahamu maandiko vizuri katika hali yake ya kiuandishi, lakini ikiwa hawaufahamu ukweli wa maji na Roho, hawawezi kuyaunganisha mafumbo yote vizuri na hawawezi kuipata aina ya imani inayoweza kuziosha dhambi zao hata kama wangejitahidi kiasi gani. 
Bwana alisema, “Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote.” (Yohana 13:10). Kifungu hiki cha maandiko ni kifungu kigumu sana kukielewa kwa Wakristo wengi wa siku hizi, kwa kuwa hawawezi kujihakikishia wao wenyewe ikiwa wamekwisha wekwa huru toka katika dhambi zao halisi au la. Kwa kweli wanakishikilia kifungu hiki kuwa ni msingi wa mafundisho ya maombi ya toba, fundisho hili linapatikana sana katika mafundisho ya kiorthodoksi katika Ukristo. 
Wao wanakifafanua kifungu hiki kama ifuatavyo: “Mara tunapoamini katika Yesu kuwa ni Mwokozi wetu, basi tunasamehewa dhambi zetu zote ikiwamo dhambi ya asili. Lakini kwa sababu sisi si wakamilifu na kwamba hatuwezi kujizuia kufanya dhambi kila siku, basi tunajikuta tena kuwa ni wenye dhambi, basi inatupasa kuomba msamaha wa Mungu ili tuweze kuwekwa huru toka katika dhambi zetu hizi halisi. Kwa kufanya hivyo basi tunaweza kusafishwa dhambi zetu, na kisha kuurudisha uhusiano wetu na Mungu tena.”
Huo ni upuuzi! Je, ni kweli kuwa unaweza kusafishwa dhambi zako halisi kwa kutoa maombi ya toba? Je, itakuwaje kuhusu zile dhambi ambazo unaweza ukasahau kuziombea toba kutoka na kutokuwa makini? Je, dhambi hizi zinawezaje kusamehewa? 
Kanisa, ambalo ni mwili wa Kristo, kwa kweli ni kusanyiko la wale wote wanaoamini katika injili ya maji na Roho iliyotolewa na Bwana wetu. Kwa hiyo Yesu aliposema kuwa mwili wote ni safi kabisa, na kwamba sio wanafunzi wote ambao ni safi, alilisema hili akimaanisha Yuda ambaye hakumwamini. Ni kwa sababu alifahamu kuwa Yuda alikuwa hajamwamini na ndio maana alisema “lakini si nyote.”
Ni lazima tuamini kuwa Bwana wetu ameziosha dhambi zetu mara moja na kwa ajili ya wote kwa injili ya maji na Roho, ambao ni ukweli wa msingi wa Biblia. Hivyo ikiwa tutashindwa kufahamu dondoo muhimu za Neno na kisha tukajitahidi kulifahamu Neno la Mungu katika njia zetu wenyewe, basi tunaweza kuangukia katika dhana ambayo si ya kweli. Hata sasa, kuna watu wengi ambao wameangukia katika dhana hiyo potofu, na wanaishia kuvitoa vitu vyao vyote na wengine hata kuuawa kwa ajili ya imani yao hata pale ambapo hawamfahamu Yesu kiusahihi, lakini mwisho wao ni kuwa wataharibiwa kwa sababu ya dhambi zao. 
 


Sababu Inayomfanya Yesu Kuiosha Miguu Yetu

 
Je, ni kwanini Petro angekuwa na shirika na Yesu ati kwa sababu tu ya Yesu kuiosha miguu yake? Ni kwa sababu Yesu angalifanyika kuwa Mwokozi wa kweli wa Petro pale tu ambapo angezitoweshea mbali dhambi zote katika maisha yote ya Petro. Yesu alikuja hapa duniani, alizichukua dhambi zote za mwanadamu kwa kupitia ubatizo wake alioupokea toka kwa Yohana, alikufa Msalabani, akafufuka toka kwa wafu, na kwa hiyo alizioshelea mbali dhambi za Petro na dhambi zote za wanafunzi wake mara moja na kwa ajili ya wote. Yesu alitaka kuuandika ukweli huu katika fikra zao. Lakini kwa sababu wanafunzi wake walilifikiria tendo hili la Yesu la kuwaosha kuwa ni suala la kimaadili, hawakufahamu sababu kuwa ni kwa nini Yesu aliwaosha miguu. 
Walipaswa kutambua kuwa sio dhambi zao za sasa tu bali hata dhambi zao za baadaye ambazo watakuja kuzifanya zitatishia kuwaua kiroho. Hivyo walipaswa kutambua kwamba hata zile dhambi ambazo watakuja kuzifanya wakati ujao zilikwishapitishwa zote kwa Yesu kwa imani. Na hii ndiyo sababu Petro asingekuwa na shirika na Yesu hadi pale alipooshwa miguu, Petro alipaswa kutambua fundisho kuu la Yesu la kuiosha miguu yake na miguu ya wanafunzi wengine. Yesu alimfundisha Petro ukweli kuwa kwa kubatizwa, Yesu amekwishaiosha “kila dhambi” ambayo Petro aliifanya kutokana na kutokuwa mkamilifu na mdhaifu. Hii ndiyo sababu Yesu alipaswa kuiosha miguu ya Petro, na ndiyo sababu iliyomfanya Petro akubali kuoshwa miguu yake na Yesu. Petro angaliweza kuwa mshirika wa Yesu ikiwa tu aliamini kuwa dhambi zote alizozifanya katika kipindi chake cha maisha kutokana na udhaifu na kutokuwa mkamilifu zilikwisha oshwa mbali mara moja na kwa ajili ya wote wakati Yesu alipobatizwa na Yohana. 
Tunaweza kuufahamu ukweli wa maji na Roho kwa kulisikia Neno la Mungu. Ni kwa kulifahamu na kuamini katika Neno la injili ya maji na Roho ambalo limezitowesha dhambi zetu zote ndipo tunapoweza kusafishwa toka katika dhambi zetu zote halisi. Yesu alisema, “Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu.” Kwa sababu Yesu amekwisha kuzioshelea mbali dhambi zetu zote na ametufanya sisi kuwa safi, wale wanaoamini katika ukweli huu ndio wale ambao dhambi zao zote zimeondolewa. 
Kwa kweli Yesu Kristo ameziosha dhambi zote kwa kubatizwa katika Mto Yordani na kwa kuzichukua dhambi zetu zote katika mwili wake. Na kwa kwenda Msalabani, kusulibiwa, kumwaga damu yake, kufa, na kisha kufufuka tena toka kwa wafu, Yesu amefanyika kuwa Mwokozi wetu wa milele. Kwa ubatizo ambao aliupokea na kwa damu ya Msalaba, Bwana amefanyika kuwa Mwokozi wetu mkamilifu. Vivyo hivyo, kwa kupitia injili ya maji na Roho, Bwana wetu amewawezesha wote wanaoamini katika yeye kuoshwa dhambi zao zote mara moja na kwa wote kwa njia ya imani. 
Wale wanaoufahamu ukweli huu na kisha kuuamini wanaweza kabisa kuondolewa dhambi zao halisi. Ikitazamwa toka katika mtazamo wa Mungu, ni kweli kuwa wanadamu wote wameoshwa dhambi zao kwa matendo ya haki ya Yesu. Tunachotakiwa kukifanya ili dhambi zetu zote ziweze kuoshwa ni kuipokea neema hii bure kwa kuwa na imani katika injili ya maji na Roho. Je, hii ndiyo hali halisi? Kwa kweli ndivyo ilivyo! Kwa imani yetu inayoamini katika ukweli huu, tumefanyika kuwa wale ambao wamekwisha oshwa. 
Yesu alisema kuwa wale ambao wamekwisha oshwa wanahitaji kutawadha tu miguu yao, kwa sababu ingawa kwa sehemu tunatenda dhambi kila siku, Yesu alikwisha zichukua dhambi zote katika mwili wake pale alipobatizwa, Yesu amezioshelea mbali dhambi zetu zote katika kipindi chetu chote cha maisha, ni kwa kuuthibitisha ukweli huu kila siku ndipo tunapoweza kutatuliwa suala la dhambi zetu halisi. 
Hivi ndivyo kifungu hiki kinavyotueleza. Ukweli ni kuwa wale ambao wamepokea ondoleo la dhambi kwa kuamini katika injili ya maji na Roho—ambayo ni, Yesu alizipokea dhambi zote kwa kupitia ubatizo ambao aliupokea toka kwa Yohana, alikufa Msalabani hali akiwa amebeba dhambi za ulimwengu, na akafufuka tena toka kwa wafu—bado wanaishi maisha yao hali wakiendelea kutenda dhambi, kwa kuwa hata wao wana miili. Hata hivyo, Mungu alikwishazichukua katika mwili wake dhambi zote ambazo watu wanazifanya katika maisha yao ya kila siku baada ya kuwa wamemwamini Yesu, kuwa kuwa Yesu ni mkuu. 
Hali akivuka nyakati, toka enzi hadi enzi, Mungu amekwisha itimiza kazi yake mara moja ambayo imezitoweshea mbali dhambi zote za mwanadamu. Kama hivyo, Yesu alizipokea dhambi zote za nyakati zetu zote tulizoishi kwa kupitia Yohana baada ya kubatizwa, alikufa Msalabani hali akiwa amezibeba dhambi hizo zote, kisha akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo amezioshelea mbali dhambi zetu zote. Lakini, pamoja na jambo hili sisi tunaaminije? Pamoja na kuuamini ukweli huu, bado tunasumbuliwa na dhambi kila siku ambazo tunazitenda katika maisha yetu kwa kutokuwa wakamilifu. 
Hii ndiyo sababu kuwa kila siku inatupasa kuuthibitisha ukweli huu, kwa imani yetu, ukweli kwamba Yesu alizichukua dhambi hizi zote katika mwili wake, dhambi ambazo tunazitenda katika kipindi chote cha maisha yetu tunapoishi na kutembea hapa duniani. Kwa kubatizwa, Yesu amezioshelea mbali dhambi za ulimwengu mara moja na kwa ajili ya wote, lakini ni lazima tuuthibitshe ukweli huu kwa imani yetu siku hadi siku, nyakati baada ya nyakati. 
Kama ilivyokuwa kwa Petro, ili abakie mwenye kuunganishwa na Yesu kwa imani, alipaswa kukumbuka kuwa Yesu aliiosha miguu yake, ili sisi tuweze kuishi katika wokovu wake, sisi nasi inatupasa kuuthibitisha ukweli huo kila siku kuwa Yesu amekwisha ziondolea mbali dhambi zetu zote kwa ubatizo wake na damu ya Msalaba. Lakini wale ambao hawaamini katika ukweli huu hawawezi kuzioshelea mbali dhambi zao milele. Wale ambao hawajaziosha dhambi zao zote kwa kutokuamini katika injili ya maji na Roho ndio wale ambao wasio na ushirika na Yesu. Ingawa kila siku wanajaribu bila kukoma kuzioshelea mbali dhambi zao, dhambi zao hazioshwi, kwa kuwa dhambi wanazojaribu kuziosha kwa kutoa sala za toba si dhambi nyepesi kiasi hicho. Kila dhambi inafuatiwa na hukumu ya Mungu ya kutisha. 
Kwa hiyo, wale wanaojaribu kuzioshelea mbali dhambi zao kwa maombi yao ya toba, badala ya kuzioshelea mbali kwa kuamini katika injili ya maji na Roho, watakuja kutambua kuwa hakuna hata sehemu ndogo ya dhambi zao iliyooshwa. Je, tunaweza kuzioshelea mbali dhambi zetu kwa kutoa sala za toba za jinsi hiyo kila siku? Hata kama sisi wenyewe tutaamini kuwa tumeoshwa dhambi zetu zote kwa maombi yetu ya toba, ukweli ni kuwa dhambi hizi zitakuwa bado zimebakia zote kama zilivyokuwa.
Ni wale tu walioiosha miili yao yote kwa kuamini katika injili ya maji na Roho ndio wanaostahili kuiosha miguu yao kadri wanavyoishi katika maisha yao, na ndio hao tu waliofunikwa katika neema inayowawezesha kuzioshelea mbali dhambi zao kwa imani kila siku na hivyo kuutunza usafi wao milele. 
Kwa kubatizwa, Yesu alizichukua katika mwili wake dhambi zetu zote halisi mara moja na kwa ajili ya wote. Hivyo tunaamini kuwa kwa ubatizo wake Yesu pia alizichukua dhambi zetu zote ambazo tunazozifanya kutokana na kutokuwa wakamilifu kadri tunavyoishi katika maisha yetu, na kwamba Yesu aliibeba pia adhabu yote ya dhambi hizo. Kwa maneno mengine, Yesu alituambia sisi kuwa hakutakiwi kuwa na kitu kama kujikwaa au kufa kutokana na kuanguka katika udhaifu wetu wenyewe.
Baada ya Yesu kuiosha miguu ya wanafunzi wake, alichokuwa amekibakiza ilikuwa ni kufa Msalabani, kufufuka tena toka kwa wafu, na kisha kupaa Mbinguni. Yesu asingeliendelea kuwa na wanafunzi wake, bali kama ilivyoandikwa katika Neno, atakuwa katika mkono wa kuume wa Mungu Baba. Na kisha atakuja tena.
Lakini ikiwa Yesu angalikufa Msalabani pasipo kuwafundisha wanafunzi wake kuhusu jambo hili, wangeliwezaje kubakia katika ulimwengu huu na kuieneza injili ya maji na Roho? Wanafunzi wa Yesu wangaliendelea kuishi hali wakitenda dhambi halisi, kwa kuwa walikuwa ni wadhaifu na wasio wakamilifu, na wasingelifahamu kitu cha kufanya pale walipotenda dhambi ya wivu, uchoyo au chuki, wasingeliweza kuishi kwa imani. Je, wangaliwezaje basi kuieneza injili kwa watu wengine? Wasingeliweza kufanya hivyo. Hii ndiyo maana Yesu alihitaji kwa hakika kuwaeleza wanafunzi wake kuwa amekwishazioshelea mbali hata dhambi hizi, na hii ndiyo sababu Yesu aliiosha miguu yao. 
 


Kama Ondoleo la Dhambi Lililodhihirishwa Katika Hema Takatifu la Kukutania

 
Tunapofungua na kuingia katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania, kwanza tutaiona madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na birika la kunawia la shaba. Fundisho la kwanza ambalo Hema Takatifu la Kukutania linatupatia sisi katika maisha yetu ya imani ni kwamba ikiwa tumefanya dhambi mbele za Mungu, basi hukumu ya Mungu inatusubiri. Kimsingi, maisha yetu ya imani, kama yanavyoelekezwa na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, yanaanza na adhabu ya dhambi na kifo. Tunapaswa kuadhibiwa mbele za Mungu kwa ajili ya dhambi zetu, lakini Bwana alikuja hapa duniani ili kuzichukua dhambi zetu katika mwili wake. 
Kama ambavyo sadaka ya kuteketezwa ya Agano la Kale ilivyoyapokea maovu ya wenye dhambi kwa kuwekewa mikono juu yake, na kisha kumwaga damu yake na kufa, na kisha nyama yake kuwekwa katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kuchomwa na moto, mnyama huyo alihukumiwa kwa haki kwa ajili ya makosa ya wenye dhambi kwa kuibeba hukumu ya moto, basi hivyo ndivyo ambavyo Yesu alifanya kwa ajili yetu. Badala ya sisi kufa, Yesu alilipokea tendo la kuwekewa mikono toka kwa Yohana, aliimwaga damu yake na kufa Msalabani, na hivyo alilipa mshahara wa dhambi zetu kwa kifo chake mwenyewe. 
Tunafanya dhambi kila siku, na tutaendelea kufanya dhambi hadi siku ile tutakapokufa. Wewe na mimi ndio wale ambao tusingeweza kujiokoa bali kustahili kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Lakini, ili kutuokoa watu kama sisi toka katika dhambi zetu na hukumu ya adhabu, Bwana aliacha kiti cha enzi cha utukufu Mbinguni kisha akaja hapa duniani, alizichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa kuupokea ubatizo toka kwa Yohana, aliutoa mwili wake Msalabani, alisulubiwa, na akamwaga damu yake ya thamani, alifufuka toka kwa wafu, na hivyo amefanyika kuwa Mwokozi wetu wa kweli. Kutambua na kuifahamu sheria ya kifo, kwamba tunastahili kuhukumiwa na kufa kwa sababu ya dhambi zetu, hiyo ndiyo sehemu ya kuanzia katika imani. 
Ni wale tu wanaofahamu na kuamini kuwa ni lazima wafe kwa ajili ya dhambi zao ndio wanaoweza kufanyika wale wanaoweza kupokea kuoshwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi kwa kuzipitisha dhambi zao zote kwa Yesu kwa imani. Imani ya kweli inaanza toka katika imani ya jinsi hiyo. Sisi tulianza katika imani hii tumefanyika wakamilifu kwa kuithibitisha imani yetu kuwa Yesu Kristo amezitoweshea mbali dhambi zote tunazozifanya kila siku na amezioshelea mbali hata dhambi zile ambazo tutakuja kuzifanya hapo baadaye. 
Hata Kuhani Mkuu na wanawe wanaoonyeshwa katika Hema Takatifu la Kukutania walitoa sadaka zao za kuteketezwa kila asubuhi na jioni. Walileta sadaka zao za kuteketezwa kila mara, waliilaza mikono yao juu ya kichwa cha mwanasadaka, waliikinga damu yake, kisha wakaitoa kwa Mungu. Na hii ndiyo sababu hakukuwa na kiti katika Hema Takatifu la Kukutania. Kwa maneno mengine, waliendelea kutoa sadaka wakati wote kiasi kuwa hakukuwa na muda wa wao kukaa na kupumzika. Vivyo hivyo, sisi tulikuwa ni watu ambao tulikuwa tukifanya dhambi pasipo kukoma na hivyo tusingeweza kuikwepa hukumu ya Mungu kwa ajili ya dhambi tulizozitenda, lakini Yesu Kristo ametuokoa sisi kikamilifu toka katika dhambi zetu zote kwa ubatizo alioupokea na kwa damu yake aliyoimwaga. 
Ni lazima tuianze imani yetu kwa kuamini kwamba hatuwezi kukwepa zaidi ya kufa kwa sababu ya dhambi zetu. Kwa watu kama sisi, Yesu alikuja hapa duniani na alizichukua dhambi zetu katika mwili wake mara moja na kwa ajili ya wote kwa kubatizwa. Baada ya kuzichukua dhambi zetu kwa ubatizo wake, Yesu Kristo alizibeba dhambi hizo zote Msalabani na kisha akalipa mshahara wa dhambi hizi kwa kuimwaga damu yake na kuyatoa maisha yake mwenyewe. Na kwa kufufuka tena toka kwa wafu, Yesu amefanyika kuwa Mwokozi wetu wa kudumu. 
Warumi 6:23 inasema, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.” Kwa kweli sisi ni wale ambao tulipaswa kufa kwa sababu ya dhambi zetu, lakini Yesu Kristo ametuokoa sisi kikamilifu. Kwa maneno mengine, kwa kubatizwa, kwa kufa Msalabani, na kwa kufufuka tena toka kwa watu, Bwana wetu ametupatia ondoleo la dhambi na uzima wa milele. Je, unaamini hivyo? Hapa ndipo imani inapoanzia. 
Kwa namna yoyote ile, je, hufikirii kuwa, “Siwezi kumfuta Yesu tena kwa sababu mimi si mkamilifu vya kutosha”? Je, pengine unafikiri kwamba wewe ni takataka na mwenye mwili mdhaifu kwa ngono, na kwamba hata pale unapoiamini injili ya maji na Roho ni vigumu sana kwako kuendelea mbele? Hii ndiyo imani inayorudi nyuma katika toba.
Hebu tuangalie Waebrania 10:36-39: “Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiishi kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi. Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia. Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.” Imesemwa kuwa sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea. Wale wanaoamini katika ukweli huu wanateswa sana, wanadharauliwa, na wanakutana na magumu mengi. Lakini urithi wa Mbinguni, ambao haupungui wala kurudi nyuma daima, unatusubiri. Vitu vyote vilivyo mbinguni vinatusubiri sisi wamiliki wake. 
Waebrania 10:34-35 inasema, “Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang’anywa mali zenu, mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo. Basi msiutupe ujasiri wenu kwa kuwa una thawabu kuu.” Hiyo ni sahihi. Kwa kuwa wewe na mimi tunaoamini katika injili ya maji na Roho, urithi udumuo wa Mbinguni unatusubiri. Mungu ametoa Mbingu kuwa ni zawadi ya urithi kwa wale ambao wamepokea ondoleo la dhambi. 
Hii ndio maana Mungu ametueleza sisi kutouacha ujasiri wetu katika kuingojea ahadi yake. Hali tukifahamu kuwa tutakuja kupokea thawabu kuu kwa sababu ya imani yetu, basi sisi hatupotei, bali tunapaswa kuifanya imani yetu kuwa imara zaidi na kutopoteza ujasiri wetu. Ni lazima tuwe na imani inayoamini katika injili ya maji na Roho, ukweli halisi, tuvipige vita vyetu vya kiroho hadi mwisho, tuokoe nafsi za watu na hatimaye kushinda. 
Kwa hakika, sisi watakatifu ni lazima tuiweke imani hii inayoamini katika injili ya maji na Roho. Ni lazima tuwe na imani hii, kwamba hata kama sisi si wakamilifu na wenye mapungufu na kwamba tunatenda dhambi kila siku kadri tunavyoishi hapa duniani, bado ukweli unabakia kuwa Bwana ametuokoa sisi kikamilifu kwa kubatizwa na Yohana na kwa kuimwaga damu yake Msalabani kwa ajili yetu. Ni kwa imani hii ndipo tunaweza kuwa na ujasiri mkuu na kisha kuishi maisha yetu katika usahihi hadi mwisho wa ulimwengu. Ni lazima twende mbele za Mungu kwa imani, tukimbie mbio za imani hali tukiwa na injili hii ya kweli, tuieneze injili, na kisha tuishi maisha yetu kwa kuitumikia injili. Hii ndio sababu Biblia inatueleza sisi, “Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiishi kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi.” (Waebrania 10:36).
“Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.” (Waebrania 10:38-39). Sisi tunaoishi kwa imani katika injili ya maji na Roho, ndio wale ambao wanaweza kuwaokoa wengine toka katika dhambi zote. Hali inapokuwa hivi, pamoja na kuwa na imani inayoweza kuwaokoa wengine, inawezekanaje sisi tukasita na kupotea? Ikiwa hatutaendelea kuiangalia injili ya maji na Roho, basi imani yetu itapungua na tutaishia kuanguka katika dimbwi la kifo ili kufa moja kwa moja. Baada ya kupokea ondoleo la dhambi, jukumu letu sasa ni kuendelea kukimbia hali tukiwa na imani yetu hali tukifuata mapenzi ya Mungu, na si kuangukia katika udhaifu wetu wenyewe, kisha tukabaki katika anguko hilo na kuishia kufa. 
Sisi tunaoamini katika injili ya maji na Roho hatumo miongoni mwao wanaopotea. Sisi ndio wale ambao tuna aina ya imani inayoweza kuokoa nafsi za wangu wengine pia. Tunapokuwa watu wa jinsi hiyo, inawezekanaje tena tukajikunja na kufa kwa sababu ya udhaifu wetu? Kamwe hatuwezi kufanya hivyo. Wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho hawamo kamwe miongoni mwao wanaosita na kupotea. Haijalishi ni kwa kiasi gani wewe na mimi tunaweza kuwa wadhaifu na wenye mapungufu, sisi ni wenye haki ambao tunaishi maisha yetu ya imani hali tukiwa na uthibitibisho mkuu katika injili ya maji na Roho. 
Wewe na mimi ni lazima tufikirie pale ambapo imani yetu ilianza, toka katika kusitasita na kupotea na kisha uishi kwa imani. Kimsingi, sisi tulikuwa ni watu ambao tusingekwepa bali kufa kwa ajili ya dhambi zetu, lakini kwa kuamini katika injili ya maji na Roho, injili ambayo kwa hiyo Bwana wetu ametuokoa wewe na mimi toka katika dhambi zote, kwa hiyo tumepokea wokovu wetu wa milele. 
Kwa maneno mengine, kwa kuwa tuliianza imani yetu kwa kukiri kikamilifu juu ya udhaifu wetu, mapungufu, uwezo mdogo, na uovu kwa asilimia 100, basi baada ya kuwa tumepokea ondoleo la dhambi, basi tunapoishi na kutembea hapa duniani hali tukifanya dhambi, hatutaweza kushinda mpaka pale tutakapozipitisha dhambi zetu zote kwa Yesu Kristo kwa kuiamini injili ya maji na Roho na kisha kuzioshelea mbali dhambi hizo kwa imani katika ubatizo wa Yesu. Hii ndio sababu kwamba kwa hakika tunapaswa kutambua kuwa sisi si miongoni mwao wanaosita na kupotea, na kwamba kwa kweli sisi tunayaishi maisha yetu kwa imani. 
Kwa baadhi ya nyakati, hali tukiwa tumefungwa na matukio na hali mbalimbali, tunaweza kuangukia katika magumu na majaribu mbalimbali, na kwa jinsi tulivyo wadhaifu, maisha yetu ya imani yanaweza pia kuanguka tusiweze kusonga mbele. Lakini hatutakufa. Ili kumfundisha Petro jambo hili ndio maana Yesu alimwambia, “Kama nisipokutawadha, huna shirika nami.” Yesu alizifuta dhambi zote za Petro. Kama ambavyo Bwana alibatizwa na kuzichukua katika mwili wake dhambi zote alizozifanya Petro katika maisha yake yote, kisha akafa Msalabani, akafufuka tena toka kwa wafu, na hivyo akawa amemwokoa Petro, basi vivyo hivyo, Bwana ametuokoa wewe na mimi toka katika dhambi zetu zote na adhabu ya dhambi. 
Ni mpaka pale Yesu atakapokuwa amefanya hivyo, na kama sivyo wewe na mimi tungewezaje kuwa na ushirika na Yesu? Na kama isingekuwa injili ya maji na Roho, tungewezaje kuokolewa toka katika dhambi zetu zote na kuwaongoza wengine ili nao waweze kuokolewa pia? Ikiwa isingekuwa ni injili ya maji na Roho tusingeweza kufanya mambo kama haya. Huu ndio ukweli ambao Yesu alitaka kumfundisha Petro. 
Wewe na mimi tumeyasikia na kuyaelewa mafundisho haya, lakini je tuko vipi hasa? Je, hatujisikii kuwa tuna huzuni katika roho kutokana na mapungufu yetu? Je, baada ya hapo hatuangukii katika udhaifu wetu? Kwa sababu tunajiona kuwa tuna mapungufu na wadhaifu, tunajikuta tukianguakia katika dharau binafsi kwa urahisi. Unaweza hata kuongea mwenyewe kwa nafsi yako, “Je, ninawezaje kumfuata Yesu hadi mwisho? Ninaona ni afadhali niache kumfuata wakati huu! Ninahakika kuwa hata Bwana anafikiria kuwa ni bora kwangu mimi kuliacha Kanisa.” Kama isingekuwa injili ya ubatizo ambayo Yesu aliipokea, kwa kweli tungeishia kuangukia katika upotevu wa milele. 
Amini katika ukweli kwamba, hata pale ambapo wewe na mimi hatukuwa na chaguo zaidi ya kufa kwa sababu ya dhambi zetu, Bwana wetu amekwisha tukomboa toka katika dhambi zetu na adhabu. Hata kama mwili wetu ni mdhaifu sana na kwamba hatuwezi kujizuia zaidi ya kuendelea kutenda dhambi tena hata baada ya kuwa tumepokea ondoleo la dhambi, bado ni lazima tukiri wokovu mkamilifu na sahihi wa Yesu uliokamilishwa na ubatizo ambao Yesu aliupokea na damu yake aliyoimwaga. 
Wewe na mimi ni lazima tuikiri imani yetu, “Tukiongea kimsingi, siwezi zaidi ya kufa kwa sababu ya dhambi zangu. Hiyo ni sawa. Lakini, Bwana hakuja hapa duniani kwa ajili yangu na akazichukua dhambi zangu zote katika mwili wake kwa kubatizwa? Je, Yesu hakuzipokea dhambi zangu zote zilizopitishwa kwake kwa kupitia ubatizo wake? Na je, Yesu hakufa Msalabani? Je, Yesu hakufufuka tena toka kwa wafu, na kwamba hadi sasa yuko hai? Kwa kuwa dhambi zangu zilipitishwa kwa Yesu Kristo, haijalishi jinsi nilivyo na mapungufu, na haijalishi jinsi mapungufu yangu yanavyofunuliwa, bado mimi ninabakia kuwa nisiye na dhambi. Hivyo mimi si miongoni mwao wanaosita na kupotea na kisha kufa.” Hivyo, kwa kuamini katika njia hii, ni lazima tuachilie mbali udhaifu wetu. 
Hata kama tutakuwa na mapungufu tena kesho, kwa kuamini katika ubatizo ambao Yesu aliupokea katika injili ya maji na Roho, basi tunaweza kuundoa uovu wetu mara zote. Kwa kutumia imani, ni lazima tuondolee mbali kifo cha kiroho na laana zinazotutembelea kutokana na udhaifu wetu. 
Ni lazima tuutafakari ukweli huu mara nyingi kadri tutakavyoweza, hali tukisema, “Bwana ameniokoa mimi. Kwa kuwa dhambi zangu zote zilipitishwa kwa Bwana, Je, nina dhambi au la? Kwa kweli sina dhambi!” Kwa kuamini hivyo, tunaweza kuuondolea mbali udhaifu na dhambi zetu, ithibitishe injili ya maji na Roho mara nyingine tena, na halalisha ukweli kuwa tumeokolewa kikamilifu kwa imani. Hivi ndivyo tunavyoweza kumkimbilia Mungu kila siku.
 


Dhambi Zote Zilitoweka Wakati Yesu Alipobatizwa

 
Akina Kaka na akina dada, Neno hili aliloliongea Yesu kwa Petro na wanafunzi wake lina umuhimu kiasi gani? Yesu aliwaosha miguu wanafunzi wake ili waweze kusimama imara katika injili ya maji na Roho hata baada ya kifo chake, hasa pale ambao watakuja kuanguka katika udhaifu wao. Kama Yesu asingeliiosha miguu ya Petro na wanafunzi wengine, je, nini kingetokea baada ya Yesu Msalabani, kufufuka tena toka kwa wafu baada ya siku tatu, na kisha kupaa katika Ufalme wa Mungu? Je, wanafunzi wake wangewezaje kutatua tatizo la udhaifu wao baada ya udhaifu huo kufunuliwa? Walipaswa kutatua udhaifu huo kwa imani inayoamini katika ubatizo ambao Yesu aliupokea, na kama wasingeliamini hivyo, basi ingekuwa ni vigumu kwao kutatua udhaifu wao. 
Ni lazima tutatue tatizo la udhaifu wetu na dhambi halisi kwa imani inayofahamu na kuamini katika ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, ambazo ni huduma za Yesu. Ikiwa Yesu asingeliwafundisha wanafunzi wake juu ya nguvu ya ubatizo ambayo aliipokea, basi wanafunzi wake wangefadhaika na hatimaye kufa kiroho. Wasingeliweza kuwa na nguvu ya kuwa na imani ya kuweza kuutoa muda wote wa maisha yao katika injili, kuyatoa maisha yao ili kuokoa nafsi za wengine, na mwishoni hata kuuawa, na kwa kweli kwa hakika wangeliweza kushindwa kuilinda imani yao na kuishia kufadhaika. 
Lakini kwa mujibu wa masimulizi ya kidesturi yaliyokabidhiwa kwetu, inasemekana kuwa wanafunzi wote kumi na mbili wa Yesu waliihubiri injili na wote waliuawa kwa ajili ya imani. Miongoni mwa wanafunzi kumi na mbili wa Yesu, jina la mwanafunzi ambaye alikuwa na mashaka zaidi ni Tomaso. Lakini hata huyu Tomaso alienda kuhubiri India na aliuawa huko kwa ajili ya imani yake. 
Je, imani hii iliyowawezesha wanafunzi hawa wa Yesu kuuawa kwa ajili ya imani yao ilikuwa wapi? Imani hii ilijazwa na ujasiri, kwamba Yesu alizichukua katika mwili wake dhambi zao zote katika muda wote wa maisha yao kwa kubatizwa, na kwamba walifanyika kuwa wasafi kikamilifu kwa kuwa dhambi zao zote zilipitishwa kwa Yesu, na kwamba walifanyika kikamilifu kuwa wana wa Mungu mwenyewe na kwamba wataurithi Ufalme—ilikuwa ni sahihi kwa sababu walikuwa na imani hii na ndio maana waliweza kuieneza injili ya maji na Roho katika ulimwengu huu na kisha kwenda Mbinguni ambako Mungu aliwaita. Kwa maneno mengine, sisi sote, tunaweza kuuawa kwa ajili ya imani hii pale ambapo Mungu akipenda. 
Wakati Petro alipomkana Yesu mara tatu nje ya ua wa Pilato, ndipo alipokuja kutambua kwa hakika kile ambacho Yesu alikimaanisha pale alipomwambia, “Kama nisipokutawadha, huna shirika nami.” Baaba ya Yesu kupaa Mbinguni, Petro na wanafunzi wengine wa Yesu walitambua ni kwa nini Yesu aliwatawadha miguu yao, nao wakaamini na kuihubiri injili ya maji na Roho kwa mkazo mkuu. 
Wakristo wa leo, ikiwa hawaufahamu ukweli huu uliopo katika ubatizo wa Yesu, basi wataona ni vigumu sana kuishi maisha yao ya imani na mwishowe wataacha kumwamini Yesu. Ikiwa tumefungwa kwa udhaifu wetu wenyewe, dhamiri zetu zitashtakiwa na kuvurugika kutokana na kutokuwa na uweza wa kulitatua tatizo hili, na kwa sababu ya dhamiri zetu zilizovurugika, basi hatutaweza tena kujitokeza Kanisani. Na hii ni kweli kwa kila mwanachama wa Kanisa la Kristo, na pia ukweli huu unawahusu hata watoto wetu. 
Kaka zangu na dada zangu, ikiwa ulizaliwa na dhambi, je utaweza kumwabudu Mungu? Leo hii, hata wale ambao hawajazaliwa upya wanaenda Kanisani, wanatoa sala zao za toba kwa ajili ya dhambi zao, na wanamwabudu Mungu, na wanafanya hivyo kwa sababu wao wanamwamini Yesu kama sehemu ya dini tu. 
Lakini kwa wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho, ikiwa wanahisi kuwa nafsi zao zina dhambi kwa sababu ya udhaifu wao na kwa sababu ya kufungwa na udhaifu huo, basi hawawezi kuja mbele za Mungu na kumwabudu. Kwa wakati kama huu, ni lazima tuzisafishe nafsi zetu kwa kuamini katika nguvu ya ubatizo ambao Yesu aliupokea, kwa kuamini kwamba Yesu alizipokea dhambi zetu zote kwa kupitia ubatizo wake. 
Wakristo hao wa mazoea ambao hawaufahmu ukweli wa injili ya maji na Roho hawaifahamu njia ya imani, hivyo wanajaribu kwa upofu kuondolewa dhambi zao kwa kutumia sala za toba. Kama ilivyo kwa wengine wanaozifuata dini za ulimwengu kwa upofu wanaomba kwa unyenyekevu kwa miungu yao hali wakisihi, “Ninakuomba, tafadhali samehe dhambi zangu na unibariki mimi na familia yangu. Nitafanya chochote kile, nitakupatia sadaka zaidi, nitatenda matendo mema; tafadhali nisamehe dhambi zangu,” Wakristo wa mazoea wa jinsi hiyo wanafuata dini waliyojifanyia wao wenyewe. 
Yesu alimwambia Petro, “Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye. Kama nisipokutawadha huna shirika nami.” Ikiwa wanafunzi wa Yesu wasingeliutambua ukweli uliofichika katika Neno hili hata baada ya hapa, wasingeliweza kuzaliwa upya katika injili hii ya maji na Roho iliyotolewa na Yesu na kufanya kazi ambazo zimewaokoa watu wengine toka katika dhambi. Ikiwa Yesu alipokuwa akiitawadha miguu ya Petro asingelipandikiza ndani yake uhakika wa wokovu mkamilifu kwa kupitia nguvu ya ubatizo alioupokea, basi Petro asingeliweza kuuawa na kulitimiza jukumu lake kama kiongozi wa Kanisa la Mungu. 
Kama isingekuwa ukweli wa injili ya maji na Roho, basi hata sisi tusingeliweza kuja mbele za Mungu na kumpatia ibada ya imani kwa sababu ya dhambi zetu, hii ni kwa sababu ya dhambi ambazo tunaendelea kuzifanya. Wale ambao wamesafishwa dhambi zao kwa kuamini katika injili ya maji na Roho ndio wanaoweza kuja katika Kanisa la Mungu. Na watu hao wanaweza kuzioshelea mbali dhambi zao kwa imani mahali popote wanapokuwapo. Kama ambavyo Bwana alisema kuwa wale ambao miili yao ni safi hawahitaji kuoga bali kutawadha tu miguu yao, kila tunapotenda dhambi kutokana na udhaifu wetu, basi ni lazima tukumbuke na kuamini kuwa dhambi zetu hizo zilikwishapitishwa kwa Yesu wakati alipobatizwa. 
Dhambi zetu zilipitishwa kwa Yesu wakati Yesu alipobatizwa (Mathayo 3:15). Ikiwa dhambi zilizokuwamo katika mioyo yetu zilipitishwa kwa Yesu, je, tuna dhambi au hatuna dhambi? Ukweli ni kuwa sisi hatuna dhambi. Kwa sababu dhambi zetu zilipitishwa kwa Yesu mara moja na kwa wote kwa kupitia ubatizo wake, sisi tumefanyika kuwa wasafi kwa kuwa dhambi zetu zilitoweshewa mbali kwa imani, na kwa sababu tupo safi, haijalishi ni kwa kiasi gani tunaweza kuwa na mapungufu, bado sisi ni makuhani mbele za Mungu. Hii ndio sababu wale wanaoamini katika injili ya ukweli ya maji na Roho wanaweza kutoka kiulaini katika madhaifu yao na kisha wakamwendea Mungu kwa imani, wakaifanya kazi yake kwa imani, wakamshukuru kwa ajili ya wokovu ambao amewapatia, wakampatia sifa zinazomtukuza Mungu, na kisha wakaieneza injili ya maji na Roho kwa wengine pia. 
“Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.” Je, uliufahamu ukweli huu mara ya kwanza ulipopokea ondoleo la dhambi? Inawezekana ikawa hujafahamu. Hata hivyo, sisi sote tumeshalisikia fundisho hili na tunalifahamu. Pamoja na kuwa wewe na mimi tunatenda dhambi kila siku na mapungufu yetu yanafunuliwa, kama ambavyo Yesu aliitawadha miguu ya Petro, basi vivyo hivyo Yesu ameitawadha miguu yetu kila siku. 
Mwanzoni, tulifurahia pale tulipoamini kwa mara ya kwanza kuwa dhambi zilizokuwamo katika mioyo tangu muda mrefu na dhambi ambazo tulikuwa tumezifanya hivi karibuni zote zilipitishwa kwa Yesu, lakini tumeona jinsi mapungufu yetu yanavyofunuliwa na jinsi ambavyo tunafungwa na udhaifu wetu hata baada ya kupokea ondoleo la dhambi. Katika nyakati kama hizo, ni kwa kufahamu na kuamini kuwa Yesu alichukua katika mwili wake dhambi hizo kwa kupitia ubatizo wake na kwamba tunaweza kwa hakika kuzipitisha dhambi zetu kwake dhambi zote ambazo tutazifanya wakati ujao. 
Je, kwa hiyo wenye haki wanafanya dhambi kwa uhuru kwa sababu ya fundisho hili? Kwa kweli hawafanyi hivyo kamwe. Warumi 1:17 inasema, “Mwenye haki ataishi kwa imani”. Baadhi ya watu walisimama kinyume na injili ya maji na Roho hali wakisema kwa ujinga, “Na tufanye mabaya, ili yaje mema” (Warumi 3:8). Je, wale waliozaliwa upya wanaweza kutenda dhambi zaidi na kwa uhuru baada ya kuwa wamepokea ondoleo la dhambi? Kwa kweli ni hapana!
Kaka zangu na dada zangu, tunapofikiria na kuamini katika injili ya maji na Roho, je, tunazo dhambi au la? Kwa kweli hatuna dhambi! Pia, hata kama tuna mapungufu, je sisi ni wakamilifu au si wakamilifu kwa imani? Jibu ni kuwa sisi ni wakamilifu. Yesu alipotuambia sisi kuwa miili yetu ni safi alimaanisha kuwa kwa kupitia ubatizo wake, damu, na ufufuo, ametufanya sisi kuwa wasafi kikamilifu. 
Sisi pia tumekuja kuifahamu nguvu ya injili ya maji na Roho baada ya kuamini katika Yesu. Kwa hiyo, ni lazima tuitumie hii nguvu ya injili ya maji na Roho katika maisha yetu ya kila siku. Kadri tunavyoitumia imani hii kila siku, pengine tunaweza kujikuta baadaye tumeichoka, tukishangaa kuwa ni kwa muda gani tutaendelea kufanya hivi. Lakini, kwa wakati kama huu, ni wapi tena ambapo ni lazima turudi kwa mara nyingine tena? Ni lazima turudi kwa Bwana kwa kuamini kwamba ingawa kimsingi tulipaswa kufa kwa sababu ya dhambi zetu, Bwana ametuokoa sisi toka katika dhambi zote kwa kuzichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa kupitia ubatizo, kufa Msalabani, na kisha kufufuka tena toka kwa wafu. 
Kumbuka kuwa makuhani walitakiwa kutoa sadaka ya kuteketezwa katika ua wa Hema Takatifu la Kukutania kila siku na kisha kuiosha mikono yao na miguu katika birika la shaba la kila wakati walipolipitia. Kama wao walivyofanya, ni lazima kwanza tuufikirie upendo wa Bwana na kisha tuutafakari kwa imani. Kimsingi, tusingeweza kufanya lolote zaidi ya kufa kwa sababu ya dhambi zetu, lakini Bwana alizichukua dhambi zetu katika mwili wake na kisha alizioshelea mbali dhambi hizo, na kwa kuadhibiwa kwa sababu ya dhambi zetu Msalabani, basi Yesu ameifanya adhabu ya dhambi kufikia ukomo wake. Kwa njia hii, na kwa kutumia ubatizo na damu ya Bwana, Yesu ametuokoa sisi kikamilifu toka katika dhambi zetu zote na adhabu. 
Kila siku, ni lazima tuuandike upendo huu wa Yesu katika mioyo yetu, upendo ambao umetuokoa sisi ambao tusingeweza kufanya lolote zaidi ya kufa kwa sababu ya dhambi, upendo ambao unaturuhusu kuja mbele za Mungu kwa imani inayoamini katika fundisho hili. Hatukuwa na chaguo zaidi ya kufa, lakini kwa sababu ya Bwana, tumeokolewa kikamilifu na tumefanyika wana wa Mungu wenye haki. Bwana anapokuwa ametupatia imani ya jinsi hiyo, je, haitupasi sisi kuwa na imani ya jinsi hiyo wakati wote? 
Sisi ni wasafiri tunaoishi katika dunia hii kwa muda tu na kisha tunaondoka. Neno ‘wasafiri’ lina maanisha ni watu waliomo safarini. Wasafiri maana yake ni wale wanaosafiri toka mahali pamoja hadi mahali pengine. Sisi ni wasafiri tunaokaa mahali pamoja kwa muda mfupi na kisha kuondoka na kwenda mahali pengine baada ya kukamilisha huduma yetu pale. Sisi ni wasafiri ambao tunapaswa kurudi katika Ufalme wa Mungu baada ya kuwa tumeishi hapa duniani kwa kitambo tu. Kadri tunavyoishi maisha yetu kama wasafiri tukipita katika ulimwengu huu na kwenda katika Ufalme wa Mbinguni, kunakuwepo na nyakati ambapo tunatamani kuiacha safari na kuanguka ardhini. Kutakuwepo na nyakati ambapo hata wewe pia utataka kuanguka chini kimwili na kiroho. Nyakati kama hizi ni lazima zije kwa sababu wakati wewe unapokuwa mkamilifu, mazingira yanayokuzunguka hayako hivyo, au mazingira yanapokuwa sawa, basi mawazo mabaya ya mwili wako yanaendelea kuinuka. 
Kwa sisi ambao tupo kama hivyo, Bwana wetu ametupatia Neno ambalo ni muhimu sana kwetu. “Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.” Ni kweli, sasa tunafahamu. Kadri tunavyoishi maisha kama wasafiri, basi kila wakati mapungufu yetu yanapofunuliwa, na kila tunapokuwa tumefungwa kwa sababu ya madhaifu yetu na kunaswa na mambo mbalimbali, ni lazima tukumbuke kwamba tumepokea ondoleo la dhambi kikamilifu kwa kuamini katika ubatizo wa Yesu ambaye ametoweshea mbali hata mambo haya, na katika damu ya Msalaba. Kwa kuamini katika injili ya maji na Roho, sisi tumepokea ondoleo la dhambi kikamilifu. 
Tunapolitazama Hema Takatifu la Kukutania, ndipo tunagundua jinsi lilivyo na maelezo ya kina. Kama inavyodhihirishwa pia katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, ni kweli kuwa mshahara wa dhambi ni mauti. Kwa sababu tunatenda dhambi kila siku, basi tulipaswa kuadhibiwa na kuuawa kila siku kutokana na dhambi zetu hizi. Katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa unadhihirishwa ukweli kuwa Yesu Kristo alikuja kama mwanakondoo wa kutolewa sadaka, alipokea kule kuwekewa mikono na kisha alikufa kwa niaba yetu. Tukiipita madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, ndipo tunaliona birika la shaba la kunawia, hapo ndipo tunapotafakari juu ya injili ya maji na Roho kuzioshelea mbali dhambi zetu tunazozifanya kila siku. Injili hii ya maji na Roho ni ukweli mkamilifu uliotuokoa sisi toka katika dhambi ya asili na dhambi halisi. 
Je, karama ya Mungu iliyo ndani ya Yesu Kristo Bwana wetu ni ipi? Je, si ondoleo la dhambi na uzima milele? Bwana wetu ametuokoa sisi kikamilifu. Ametuokoa sisi kikamilifu, sisi ambao tulipaswa kufa kwa ajili ya dhambi zetu wakati wowote. Dhambi zote tunazozifanya katika kipindi chote cha maisha yetu zimesafishwa mbali kwa imani yetu katika maji na damu, na kwa Neno, kwamba Bwana ameitawadha hata miguu yetu. Kwa sababu Bwana alizichukua dhambi zetu zote katika mwili wake pale alipobatizwa na kwamba dhambi zote tunazozifanya katika kipindi chote cha maisha yetu zilipitishwa kwake, Yesu Kristo hali akiwa amebeba dhambi zetu, alihukumiwa Msalabani kwa sababu ya dhambi hizo na kisha alikufa, akafufuka toka kwa wafu, na kwa hiyo amefanyika kuwa Mwokozi mkamilifu. Ni pale tunapomwamini huyu Yesu Kristo ndipo tunapofanyika kuwa wakamilifu. Na pamoja na kuwa miili yetu inaweza kuwa na mapungufu, basi kwa kuwa tuna imani sahihi na kamilifu, basi sisi tutaishi maisha ya kiroho yaliyobarikiwa na kisha kuingia katika Ufalme wa Mungu.
 

Je, Wewe Si Kama Petro kwa Sasa?
 
Kama ambavyo Yesu aliiosha miguu ya Petro, je, huyo Yesu hajakuosha miguu yako? Ni sahihi kusema kuwa Yesu ametuosha miguu yetu kila siku. Hii ndio sababu Yesu alizichukua dhambi zetu zote katika mwili wake kwa kubatizwa, na kisha akafa Msalabani kwa ajili ya dhambi hizi kwa niaba yetu. Kisha akafufuka tena toka kwa wafu baada ya siku tatu. Vivyo hivyo, kwa kupitia ubatizo wake, damu yake Msalabani, na ufufuko wake, Yesu amefanyika kuwa Mwokozi mkamilifu. Sisi tunamwamini huyu Yesu Kristo kikamilifu.
Ni kwa imani ndio maana tunamwabudu Mungu kikamilifu, na ni kwa imani ndipo tunazifanya kazi zake kikamilifu. Matendo yetu hayawezi kuwa makamilifu. Ni imani yetu ndiyo inayotufanya sisi kuwa wakamilifu. Hii ndio maana tunapaswa kuishi kama wanafunzi wa Yesu kwa kuamini katika injili ya maji na Roho. Sisi hatumo miongoni mwao wanaosita na kupotea katika imani. Ingawa tunaweza kuwa na mapungufu, bado tunaweza kukimbia kwa imani, na kwa kweli ni lazima tukimbie zaidi na zaidi kwa imani. “Mwenye haki ataishi kwa imani.” “Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake.” Kutokana na ukweli kuwa tumefanyika kuwa wakamilifu kwa imani, na kuwa watu tunaoweza kuziokoa nafsi za watu wengine, ikiwa hatutajitoa sisi wenyewe katika huduma ya Mungu ya kuwaokoa wengine, basi tutakuja kuanguakia katika dimbwi la kusitasita na kusononeka, na hatimaye kufa katika dhambi zetu.
Wale wasio na dhambi wanafurahia wakati wanapozifanya kazi zake za haki. Wanafurahia kuieneza injili ya Mungu inayookoa nafsi nyingine. Lakini wenye dhambi hawafurahii kufanya yaliyo ya haki. Kwa kuwa wale waliokwisha kupokea ondoleo la dhambi, kufanya yaliyo ya haki unakuwa ndio mkate wao wa kiroho. Kuieneza injili ulimwenguni mwote ndio jambo sahihi la kulifanya linaloziokoa nafsi za watu wengine, lakini kwa wakati huohuo ndio mkate wetu wa kila siku wa maisha. Kutokana na kutenda yaliyo sahihi, mioyo yetu inajazwa na Roho na kisha nguvu mpya inachipua ndani yetu. Kadri roho zetu zinavyokua na kukomaa, ndivyo tunavyozidi kufanyika mashujaa. Kwa hiyo, ili tuweze kuishi kama Ibrahimu, na ili tuweze kubarikiwa na Mungu na kisha kuwashirikisha wengine baraka hizi, basi ni lazima tupende haki, tupende yaliyo mema, na kisha tupende kuieneza injili. Hata kama sisi ni wadhaifu, ili nafsi zetu zisife, basi tunapaswa kuendelea kuyatenda matendo haya mema. Kwa hakika sisi wenye haki tunaweza kufa kiroho ikiwa tutaacha kutenda kazi kwa ajili ya utume wake mwema. Hii ndio sababu Yesu alisema, “Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa” (Mathayo 5:6).
Pia Yesu alisema, “Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu” (Mathayo 5:8). Wale waliopokea ondoleo la dhambi na wanaoamini kuwa Bwana alimezioshelea mbali dhambi zetu zote basi hao watakuja kumwona Mungu. Kisha watakuja kumwamini Mungu, kumfuata, na kisha kuzieneza baraka za mbinguni katika ulimwengu mzima. 
Sisi tumefanyika kuwa wakamilifu kwa imani. Kwa kuwa tusingeweza kufanya chochote zaidi ya kufa kutokana na dhambi zetu, lakini Bwana alikuja hapa duniani, alibatizwa, akafa Msalabani kwa ajili yetu, na kwa hiyo ametuokoa sisi kikamilifu. Huu ndio ukweli, na ndio njia ya kwenda katika Ufalme wa Mbinguni. Kuutambua ukweli huo ni kuitambua njia ya imani. Hakuna njia nyingine zaidi ya hii. Hatuwezi kuingia Mbinguni kwa matendo yetu mema. Bali ni kwa kutambua na kuamini katika kile ambacho Bwana wetu amekifanya kwa ajili yetu ndipo tunapoweza kuingia Mbinguni. 
Kwa sehemu kubwa, ikiwa tungewagawa watu katika makundi ya aina mbili, basi tungeona kuwa kuna wale ambao wameyazoelea yaliyo mema na wale walioyazoelea mabaya. Wale walioyazoelea mabaya ni wale ambao hawajapokea kikamilifu ondoleo la dhambi. Kwa kuamini katika kila ambacho Bwana amekifanya kwa ajili yetu, sisi tumefanyika kuwa vifaa au vyombo vya haki, lakini wale ambao hawajapokea ondoleo la dhambi bado hawawezi kufanya lolote zaidi ya kubakia kuwa ni vifaa au vyombo vya Mwovu bila kujalisha nia zao.
Kwa wakati huu, ninakueleza wewe kwa ujasiri kuwa Mungu ametupatia sisi wokovu wake mkamilifu, imani kamilifu, na ondoleo la dhambi kamilifu. Je, matendo yako yana mapungufu hata pale unapoendelea kuiamini injili hii, na je, kwa namna yoyote ile moyo wako unajaribiwa kurudi nyuma kutokana na hali hii? Huhitaji kuwa hivyo, kwa kuwa wenye haki wataishi kwa imani. Je, si kwamba Bwana, ambaye anafahamu madhaifu na mapungufu yetu, alikwisha yachukua mambo haya yote kwa ubatizo wake?
Hebu nikupatie mfano wa kila siku unaoonyesha jinsi ambavyo tulivyo na mapungufu. Mara kadhaa tunacheza soka pamoja. Ilipotokea kuwa timu yangu ipo katika shida, hali mpira ukija kwa nguvu kuelekea katika goli letu, mara nyingi nilijikuta nikiupiga kwenda nje au hata kuudaka kwa mikono yangu. Je, mimi nilikuwa ni golikipa? Kwa kweli mimi si golikipa. Ni kwamba nilipenda tu kushinda. Katika mazingira kama hayo, sisi sote, wahudumu, watakatifu, na watumishi wa Mungu kwa pamoja tunafanya kila kiwezekanacho kujaribu kushinda. Unaweza ukajisahau kuwa unajirahisisha; lengo lako ni kushinda, kiasi kuwa unafanya kila aina ya makosa kimchezo. Mchezo unashindaniwa kwa nguvu sana na kila mtu anafanya kila liwezekanalo ili kushinda, kiasi kuwa hakuna mchezo unaoweza kuufunua utupu na ubinafsi wa tabia ya mwanadamu kama ilivyo kwa mchezo wa soka. Ikiwa timu yetu ipo katika shida, tunajikuta hatusiti kucheza rafu, kuibia, na kusisitizia upande wetu tu.
Mambo haya ya kujivutia katika mchezo yanakuwa ni ruhusa kwa upande wetu, lakini ikiwa timu pinzani imefanya makosa hayo hayo tunamlilia mwamuzi kutoa kadi ya njano, na mara nyingi hata maamuzi ya mwamuzi hayatarajiwi kufanya kazi kabisa. Hivi ndivyo hasa tulivyo. Mara nyingi tunapenda kile chenye faida kwa upande wetu, kwa timu yetu, na kwetu binafsi, na mara nyingi tunapenda kile kinachotupatia faida tu. Pamoja na hayo Mungu ametuokoa sisi tulio watu wa jinsi hiyo. Pamoja na kuwa tumejawa na mawaa, mapungufu, na ukosefu wa sheria, lakini kwa mujibu wa imani yetu, sisi tumefanyika kuwa wale waliozaliwa upya pasipo mawaa.
Bwana ametuokoa sisi kikamilifu toka katika dhambi zetu zote. Na hii ndiyo sababu tunamwita Bwana kuwa ni Mungu wa wokovu, na Mungu wa wokovu kuwa ni Bwana. Bwana ni Mungu wetu wa wokovu. Petro alikiri kuwa, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai” (Mathayo 16:16). Na Mungu aliithibitisha imani yake kuwa ni ile itokayo kwa Mungu. Neno Kristo hapa lina maanisha kuwa ni Yule aliyezichukua dhambi zetu katika mwili wake na kisha akazitoweshea mbali. Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu aliye hai. Kama Mwana wa Mungu na Mwokozi wetu, Yesu ametuokoa sisi kikamilifu. Hivyo, iweni na ujasiri katika mioyo yenu hata kama mtajihisi kuwa mna mapungufu na madhaifu katika kuihudumia injili.
Nafsi zenu, mioyo yenu, na miili yenu isirudishwe nyuma na kusimamishwa; bali, jikazeni kwa imani na muwe na ujasiri, watu wakuu wenye haki ambao mnaieneza imani ya Mungu iliyotolewa kwa mapana na kwa umbali. Niangalie mimi. Sina kitu cha kujionyesha katika mwili wangu, lakini je, siienezi injili katika ulimwengu wote? Je, wewe si kama mimi nilivyo? Usifikirie kuwa wale wanaoonekana kuwa hawana mapungufu ndivyo walivyo au wako huru kabisa toka katika mapungufu yoyote. Wenye dhambi ni wanafiki tu. Wanafiki pia ni wanadamu kama wewe ulivyo, na kwa hiyo inawezekanaje miili yao ikawa myema, yenye heshima, na safi kiasi hicho? Kitu ambacho mara nyingi kina mapungufu ni miili ya wanadamu. Unapaswa kutambua kuwa wale wanaoonyesha wema au ubora wao, hasa katika jamii za Kikristo, kwa kweli wanaionyesha tu ile asili ya unafiki wao. 
Mungu wetu ametuokoa sisi kikamilifu. Kwa hiyo, tunaweza kuihudumia injili ya maji na Roho kwa imani zetu ambazo zimetufanya sisi kuwa wakamilifu, hali tukitiwa nguvu na ukamilifu wa haki wa Mungu. Tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha sisi kuokolewa kwa imani kwa kupitia ukweli wa wokovu kwamba Mungu alipanga hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Dhambi zako zote zilikwisha oshelewa mbali wakati Yesu alipobatizwa na kuimwaga damu yake Msalabani. Ninaamini kuwa ninyi nyote mtaamini katika ukweli huu.