Kwa sababu ya Changamoto ya COVID-19 na usumbufu kwa huduma ya utumaji barua kimataifa, tumesimamisha kwa muda huduma yetu ya 'Utumaji wa Vitabu vya Bure viyilivyo chapishwa.
Kwa kuzingatia hali hii hatuwezi kukutumia vitabu hivi kwa wakati huu.
Omba kwamba janga hili litamalizika hivi karibuni na kuanza tena kwa huduma ya posta.
Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho
1-3. Sheria zipi zilizoletwa na Mungu?
Mungu ni wa mipango, ndiye Mungu wa kweli na hakika ndiye aliye hai. Hivyo, aliweka sheria ulimwenguni kwa sababu zifuatazo: ① Aliwapa wenye dhambi Sheria na Amri ili waokolewe kwa dhambi zao “kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria” (Warumi 3:20). ② Sheria ya pili ni Sheria ya Imani iokoayo wenye dhambi. “Sheria ya Roho wa uzima” (Warumi 8:2) inayotoa njia ya wokovu kupitia imani katika Yesu Kristo mwokozi wetu (Warumi 5:1-2). Yesu alishuka ulimwenguni kuitimiza hii sheria. Alibatizwa akatoa damu yake Msalabani na akafufuka. Yesu aliweka sheria ya wokovu ili kuokoa wale wote wenye dhambi ulimwenguni. Mungu aliweka Sheria ya Imani kwa wale tu wenye kuamini wokovu utokanao kwa maji na Roho. Yeyote atakaye okolewa na kuwa mwana wa Mungu yampasa kwanza kuamini Sheria hii ya Imani ambayo Mungu ameitoa. Ndiyo pekee njia ya kuokoka. Kwa haya, ameruhusu njia ya kwenda mbinguni kwa wale wenye kuamini kuzaliwa kiroho katika kweli tokana na sheria hii.