Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-24. Nini maana ya ubatizo wa toba alio leta Yohana?

Yohana Mbatizaji alikuwa ni mtumishi wa Mungu, aliye zaliwa miezi sita kabla ya Yesu, na alitabiriwa kuja kwake katika Malaki, awe nabii wa mwisho katika Agano la Kale.
“Ikumbuke torati ya Mungu, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu, Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana” (Malaki 4:4-6).
Wakati Yesu alipozaliwa, watu wa Israeli waliyaacha maneno ya magano ya Mungu na kuabudu miungu ya kigeni. Walitolea wanyama walio vipofu na wasio safi kama sadaka, na kufanya hekalu ya Mungu kuwa sehemu ya biashara, Yesu Kristo, pia alitabiriwa kuja kwake katika Sheria ya Musa na Manabii. Sheria humpa mwanadamu ufahamu wa dhambi, kwa kumuonyesha jinsi ile alivyo mwovu (Warumi 3:20). Ni dhambi kutofuata hata amri mojawapo iliyoandikwa katika kitabu cha Sheria.
Katika Agano la kale, mwenye dhambi asiye heshimu vipengele vya sheria alileta sadaka ya dhambi mbele ya madhabau, kwa kuweka mikono yake juu ya kichwa cha yule mnyama ili kumtwika dhambi juu yake, na kumchinja mnyama huyo kama sadaka ya dhambi ili aweze kusamehewa dhambi zake na kuunganishwa tena na Mungu Ndipo pia kuhani huchukua kiasi cha damu na kuweka katika pembe zilizo katika altare ya sadaka ya kuteketezwa na kumwagia ilibaki juu ya sinia la altare.
Hivyo, watu wa Israeli hawakuweza kukombolewa toka dhambini, ukiachilia zile sadaka zisizo na idadi zilizotolewa kila siku. Hivyo, Mungu akafanya azimio la kudumu kwao, siku ya upatanisho. Ilikuwa katika kipindi hicho Mungu angeweza kusamehe dhambi za mwaka katika siku ya kumi ya mwezi wa saba. Katika siku hiyo Haruni, Kuhani Mkuu, aliwachukua mbuzi wawili na kupiga gura juu yao; mmoja wa Bwana na mwingine wa Azazeli ndipo alipowekea mikono yake juu ya kichwa cha yule wa Bwana ili kumtwika dhambi za mwaka za wana wa Israeli juu yake. Haruni alimchinja na kuichukua damu kwa kunyunyizia mara saba juu ya uso wa kiti cha rehema.
Alipo maliza kupatanisha kwa ajili ya Hekalu takatifu, alimtoa mnyama mwingine. Alimwekea mikono yake juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai na kutubu juu yake dhambi zote za mwaka za wana waisraeli. Kwa njia hii, dhambi zote za mwaka zili wekewa juu yake, na kupelekwa kwa kutelekezwa jangwani katika mikono ya mtua liye tayari. Waisraeli walikombolewa kwa dhambi zao kwa namna hii.
Ingawa sadaka ilitolewa kulingana na sheria ya Agano la Kale haikuweza kuwafanya wale wote waliotolea sadaka ya mwaka kwa mwaka kuwa safi. Ilikuwa ni jinsi ya kivuli au mfano wa mambo mema yatarajiwayo (tendo la haki kwa Masia) mbeleni (Waebrania 10:1). Watu wa Israeli hawakumngojea Yesu Kristo, Mwokozi badala yake waliabudu miungu ya ugenini katika ulimwengu wa uovu waliacha maneno ya unabii wa Agano la kale. 
Kwa haya Mungu akasema kabla kwamba atamtuma Yohana Mbatizaji ili kurudisha mioyo ya Waisraeli, kurudia kwwa Mungu na kutayarisha mioyo hiyo pia kumpokea Yesu Kristo. Kabla Yohana Mbatizaji kumbatiza YESU, alitoa ubatizo wa toba kwa waisraeli jangwani Yedea.
Dhumuni lake kubatiza kwa maji lilikuwa kuwaongoza katika kusubiri na kumwamini Yesu aliwafundisha kwamba Mwokozi atabatizwa naye kwa njia ya kuwekewa mikono ili kubeba dhambi zote za ulimwengu na kusulubiwa ili kuwaokoa toka dhambini. Alisema kwamba Yesu atakuja na kuiondolea mbali sadaka ile isiyo kamilika ya kale na kutoa sadaka ya milele kwa mwili wake; yeye atabeba dhambi zote kwa ubatizo wake, kama ilivyo wana wa Israeli walipo kombolewa kwa kuleta sadaka ya dhambi isiyo na doa, kwa kuwekea mikono juu yake, na kuchinjwa kulingana na utaratibu wa kutoa sadaka katika Agano la kale.
Waisraeli wengi walikiri dhambi, kutubu na kubatizwa naye. “Tubuni” maana yake “kumrudia kwa moyo Bwana.” Kwa kukumbuka sheria ya Agano la kale, walimjia Yohana na kukiri kwamba walikuwa hawana tumaini wenye dhambi, ambao wasingeweza kujizuia kutenda dhambi hadi kifoni. Walikiri pia kwamba hawatoweza kuingia katika ufalme wa Mbinguni kwa matendo yao mema ya sheria na kumrudia kwa moyo Yesu Kristo ambaye angefuta dhambi zao zote mara moja na kwa wote, na kuwafungulia malango ya ufalme wa Mbinguni.
Ubatizo ambao Yohana Mbatizaji alio utoa kwa Waisraeli ulikuwa ni katika mfululizo wa matukio. Aliwaongoza kukiri juu ya dhambi zao maishani, kutubu na kumgeukia Yesu Christo, ambaye naye atakuja kubatizwa kwake, yeye (Yohana) akiwa Kuhani Mkuu na mwakilishi wa wanadamu, na hatimaye kusulubiwa ili kuwaokoa kwa dhambi zao zote, punde atakapo wabatizwa. Hii ndiyo toba ya kweli kibiblia.
Hivyo, Yohana aliwaambia makutano waliokusanyika “kwali mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto” (Mathayo 3:11).
Yohana Mbatizaji aligeuza nia za watu kwa Yesu, kwa kuwashuhudia kwamba Yesu atakuja kubeba dhambi zote za ulimwengu (Yohana 1:29) na kufa kwa ajili yao kwa kujitolea. Kwa haya, Yesu binafsi alibeba ushuhuda ya Yohana aliyekuja kutuonyesha njia ya haki (Mathayo 21:32).