Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 3: Ufunuo

3-3. Mwanamke Katika Sura ya 12 Ni Nani?

Mwanamke katika sura ya 12 ana maanisha ni Kanisa la Mungu katikati ya Dhiki Kuu. Kwa kupitia mwanamke anayeteswa na Mnyama, sura ya 12 inatuonyesha kwamba Kanisa la Mungu litadhuriwa sana na Shetani nyakati za mwisho zitakapowadia. Hata hivyo, kwa kupitia ulinzi maalumu wa Mungu, Kanisa la Mungu litamshinda Shetani na Mpinga Kristo kwa imani yake, kisha litapokea utukufu wa kuvikwa baraka kuu za Mungu. 
Kwa kuwa watakatifu wanaodumu katika Kanisa la Mungu watapokea maboresho ya imani hata katika nyakati za Dhiki, basi watamshinda Mpinga Kristo kwa kuyapokea mauaji ya kuwa wafia-dini kwa imani katika injili ya maji na Roho. Mungu anatueleza ukweli huu kwa kupitia lugha ya picha ya mwanamke katika sura ya 12. 
Ufunuo 12:13-17 inatueleza kwamba, “Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume. Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo. Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule. Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake. Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.”
Shetani, ambaye mara nyingi katika Biblia anatajwa kuwa ni Mnyama, kwa asili yake alikuwa ni malaika aliyefukuzwa toka Mbinguni kwa kutaka kuchukua nafasi ya Mungu. Kwa kuwa kama matokeo ya uasi huo, Ibilisi, pamoja na malaika wengine waliomfuata walitupwa toka Mbinguni, na huku akifahamu kuwa hivi karibuni atafungwa katika shimo la kuzimu lisilo na mwisho, basi alikuja hapa duniani na kisha kulitesa Kanisa la Mungu na watakatifu wa Mungu. 
Ingawa Shetani alijaribu kumzuia Yesu Kristo asikifanye kile ambacho alikuja kukifanya hapa duniani—yaani kuwaokoa wanadamu toka katika dhambi—hata hivyo Kristo alizichukua dhambi za ulimwengu kwa ubatizo wake, akaimwaga damu yake Msalabani, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa sababu hiyo amewaokoa wanadamu toka katiak dhambi zao zote. Hivyo, Yesu aliyatimiza mapenzi ya Baba. Pamoja na Shetani kujaribu kuingilia kazi ya Yesu ya kuyatenda mapenzi ya Mungu ili kuwaokoa wanadamu toka katika dhambi, Kristo alizishinda vurugu za Ibilisi na akayatimiza mapenzi yote ya Baba. 
Hata hivyo, kwa kuwadanganya watu wengi na kuwafanya kuwa washirika wake, Shetani amewafanya wasimame kinyume na Yesu Kristo na kinyume na watakatifu. Hali akijua kuwa siku zake zinahesabika, anawashawishi watu wa hapa duniani kusimama kinyume na Mungu na anawatesa watakatifu. Kwa kuhakikisha kwamba ulimwengu unajawa na dhambi, Shetani amemfanya kila mtu kukimbilia dhambi na ameifanya mioyo yao kuwa migumu ili kusimama kinyume na Mungu kwa sababu ya maovu yao. 
Shetani anawashambulia watakatifu wapendwa wa Mungu kwa dhambi bila kikomo, kwa kuwa anafahamu kuwa ana muda mchache. Shetani amemfanya kila mtu katika ulimwengu huu kuikimbilia dhambi na ameifanya mioyo yao kuwa migumu ili kusimama kinyumena Mungu na watakatifu wa Mungu kwa dhambi zao. Kwa hiyo, nyakati za mwisho zitakapowadia, watakatifu ni lazima wailinde imani yao kwa kupambana na kumshinda Shetani. 
Lakini Mungu ameihifadhi baraka maalumu kwa ajili ya watakatifu wake, hii ni kwa sababu anawapenda watakatifu wanaodumu ndani ya Kanisa lake. Baraka hii ni kwamba atawatunza watakatifu kwa kuwajenga kiimani katika Kanisa la Mungu katika ile miaka mitatu na nusu ya kwanza katika ile miaka ya Dhiki, yaani kabla Mpinga Kristo hajatokea hapa ulimwenguni, na kisha kuwadanganya watu na kuwafanya kuwa watumishi wake ili kusimama kinyume na Mungu na watumishi wa Mungu. Kwa nini? Kwa sababu wakati wa dhambi nyingi utakapowadia na wakati Mpinga Kristo atakapotokea, basi ni lazima watakatifu watauawa na kuwa wafia-dini. Ili kufanya hivyo, Mungu atawatunza watakatifu wake kwa kupitia Kanisa lake na atawawezesha kuwa wafia-dini kwa imani yao kwa mika mitatu na nusu—yaani, “kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati” (Ufunuo 12:14).