Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 3: Ufunuo

3-4. Je, Babeli ni Nini?

Neno Babeli linatumika katika Biblia kuumanisha ulimwengu huu ambao umeachana na Mungu. Habari kuhusu “Mnara wa Babeli” inapatikana katika Agano la Kale. Kadri watu walivyoziunganisha pamoja nguvu zao ili kuujenga Mnara wa Babeli ili kumwacha Mungu, Mungu aliwazuia ili wasiujenge mnara, aliharibu kazi yao kwa kuivuruga lugha yao, kisha akawatawanya. 
Vivyo hivyo, ulimwengu huu ni kama wakati wa Mnara wa Babeli. Wafalme wa nchi wamefanya ukahaba na wameishi kwa starehe kwa vitu hapa ulimwenguni, na wafanyabiashara wote wamemdharau Mungu katika maisha yao, wametingwa kwa kuuza na kununua vitu vyote ambavyo Mungu amewapatia. Kwa kutumia dini, manabii wa uongo wameishi maisha yao huku wakiongea kwa sauti, na kujibadilisha kuwa wafanya biashara wanaozifanyia biashara roho za watu, huku wakijirundia baraka ya utajiri wa mali na vitu vya ulimwengu huu. Wameupenda ulimwengu, huku wakisema hakuna ulimwengu uliojengwa na mwanadamu ambao umekuwa bora zaidi kuliko huu wa sasa. 
Vivyo hivyo, nyakati za mwisho zitakapowadia, ulimwengu huu utakuwa mchafu sana mbele za Mungu na dhambi itakuwa imeenea sana ndani yake kiasi kuwa Mungu hatakuwa na la kufanya zaidi ya kuuharibu ulimwengu huu ambao yeye mwenyewe aliuumba. Huku wakiupenda mno ulimwnegu, watu wa ulimwengu huu wameuhesabu ulimwengu huu kuwa ndio Mungu wao, huku wakiamini na kuufuata. Hivyo, ulimwengu huu umefanyika kuwa kitanda cha dhambi, watu wanaoishi katika kitanda hiki cha dhambi wamelewa kwa aina mbalimbali za dhambi, na hivyo dhambi hizi zimesababisha anguko la ulimwengu. Hivyo hatimaye ulimwengu utakabiliana na mwisho wake utakaoletwa na mapigo ya mabakuli saba ya Mungu. 
Sababu nyingine itakayofanya ulimwengu huu ukabiliane na mapigo ya mabakuli saba toka kwa Mungu ni kwa sababu, watu wake kwa vile wanavyoupenda ulimwengu, wamegeuka na kuwa watumishi wa Shetani na wa Mpinga Kristo, na huku wakiziunganisha juhudi zao na Mpinga Kristo, wamewaua watakatifu waliozaliwa tena upya wanaoamini katika injili ya maji na Roho iliyotolewa na Bwana. 
Nyakati za mwisho zitakapowadia, watu watasalimu amri kwa Mpinga Kristo, wataipokea alama ya Shetani itakayotolewa na Mpinga Kristo, na hivyo watageuka na kuwa watumishi wa huyo mwovu. Kwa kuwa watu wa ulimwengu huu, wakiwa wamefanya uhaini pamoja na Mpinga Kristo, watakuwa wamesimama kinyume na Mungu na kuwaua wataktifu wa Mungu, basi Mungu atawalipa sawasawa na walivyowaletea mateso, dhiki, na vifo kwa watakatifu.