Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 3: Ufunuo

3-5. Ufalme wa Milenia Utaanza Lini? (Je, ni Ufalme Kabla ya Dhiki au Baada ya Dhiki?)

Watu wengi wanaamini kwamba watakatifu watanyakuliwa kabla ya ujio wa Dhiki Kuu ya miaka saba, na kwamba wakati wa Dhiki Kuu watakuwa tayari wapo katika Ufalme wa Kristo wa Milenia, badala ya hapa duniani. Hata hivyo, tunapoithibitisha imani hii kwa Neno la Mungu, basi tunaweza kuona kwa urahisi kwamba imani hii si sahihi. 
Bwana Mungu wetu anautoa Ufalme wa Kristo kwa watakatifu wake kwa miaka elfu moja kama thawabu kwa ajili ya kufanya kazi na kuutoa uhai wao kwa ajili ya injili. Kama vile Ufunuo 20:4 inavyotueleza, “Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.”
Kifungu hicho hapo juu kinatuelezea sisi ambao tutaweza kuingia katika Ufalme wa Milenia. Hawa ndio wale ambao pamoja na Dhiki Kuu, walipigana dhidi ya Mpinga Kristo, wakauawa ili kuilinda imani yao, wala hawakuipokea chapa ya Mnyama wala kuiabudu sanamu yake. Ili kutenganisha kati ya ngano na makapi, Mungu amewaruhusu wanadamu kuwa na chaguo la kuipokea au kutoipokea alama ya Mnyama. Mungu anataka kutenganisha ngano na makapi kwa kuwanyakua watakatifu na kisha kuwapa thawabu ya Ufalme wa Kristo kwa sababu ya imani na ushindi wao dhidi ya Shetani. 
Kwa kuwa watu wa Mungu watakuwa ndio kikwazo kikuu kwa Mpinga Kristo ili asisimame kinyume na Mungu, na kujifanyia sanamu yake, na ili asiweze kuwafanya watu kuipokea alama yake. Basi, Mpinga Kristo atazitoa juhudi zake zote ili kuwaondolea mbali. Lakini watakatifu hawatasalimu amri kwa yule Mnyama, watapambana naye kwa imani, watayapokea mauaji ya kuwa wafia-dini, na kwa sababu hiyo watamtukuza Mungu. Idadi kubwa ya watakatifu, huku wakiangalia zaidi juu ya maisha yao baada ya kifo, wayapokea kwa hiari mauaji ya kuwa wafia-dini ili kuilinda imani yao katika Mungu. Kwa kuwa Mpinga Kristo ataleta mateso mengi kiasi hicho kwa watakatifu katika kipindi cha Dhiki Kuu, basi ndio maana Mungu amemwandalia Mpinga Kristo na wafuasi wake mapigo ya mabakuli saba na adhabu ya kuzimu ambako wataungua milele. 
Kwa hiyo, ulimwengu huu utaangamizwa kikamilifu na utavunjwavunjwa kwa mapigo ya mabakuli saba, kwa tetemeko kuu, kwa kiasi ambacho hakijawahi kuonekana. Kama matokeo, ulimwengu wa kwanza utatoweka bila hata kuacha alama yake. Kisha Mungu atawaamuru malaika zake kumkamata Mnyama na kisha kumfunga katika shimo la kuzimu lisilo na mwisho kwa miaka elfu moja, Bwana wetu atamfunga kwanza Mnyama katika shimo la kuzimu kabla ya kuwaruhusu watakatifu wake kuishi katika Ufalme wa Kristo wa Milenia. 
Kwa kuwa shetani hatakuwepo katika Ufalme wa Milenia mahali ambapo watakatifu watatawala pamoja na Kristo, basi huko hakuna waongo wala laana tena. Isaya 35:8-10 inaelezea juu ya Ufalme wa Kristo ambao utawajia watakatifu walioshiriki katika ufufuo wa kwanza kama ifuatavyo: “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo. Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo. Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.”
Ufalme wa Kristo, utakaodumu kwa miaka elfu moja kama hapo juu, utakuja baada ya dunia kupitia Dhiki Kuu ya miaka saba na baada ya kupita na kuangamizwa kwa ulimwengu unaoongozwa na Shetani na Mpinga Kristo. Hivyo, ufalme huu, ni zawadi ambayo Bwana wetu atawapatia watakatifu wake kwa kuteswa na kuwa wafia-dini ili kuilinda imani yao katika injili ya maji na Roho, na kwa kufanya kazi ili kuihubiri injili hii.