Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 3: Ufunuo

3-11. Unasema kwamba Yesu atakuja ili kuwanyakua watakatifu wake, na kwamba atashuka hapa duniani ili kupigana vita ya Harmagedoni. Je, una maanisha kwamba Bwana atakuja hapa duniani mara mbili? Je, tofauti ya mambo hayo mawili ni ipi?

Kushuka kwa Yesu toka Mbinguni ili kuwanyakua watakatifu wake na kurudi kwake duniani ili kumhukumu Ibilisi kwa kupitia vita ya Harmagedoni ni mambo mawili tofauti. 
Baaba ya ile miaka mitatu na nusu ya kwanza katika ile Dhiki Kuu kuisha, na mara baada ya mauaji wa watakatifu kutoka kwa Mpinga Kristo, basi Bwana atashuka toka Mbingunini. Wakati huu, watakatifu ambao watakuwa wamelala katika makaburi yao na watakatifu ambao watakuwa wamestahimili katika kipindi cha Dhiki pasipo kuipokea alama ya Mnyama na hivyo kuilinda imani yao watafufuliwa na kuinuliwa angani na kisha kuonana na Bwana angani. Kuanzia wakati huo na kuendelea, watakatifu watakuwa wakati wote pamoja na Bwana. Wakati huu, Bwana hatashuka hapa duniani. Kwa nini? Kwa sababu mapigo ya mabakuli saba ambayo yatamhukumu Shetani na Mpinga Kristo yatakuwa bado hayajamiminwa hapa duniani. 
Hivyo, Mtume Paulo katika 1 Wathesalonike 4:17 alitueleza kwamba, “Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.” Watakatifu waliopambana na Mpinga Kristo na kisha kuuawa kama wafia-dini ili kuilinda imani yao watashiriki katika ufufuo wa kwanza, kisha watakutana na Bwana angani na wala si hapa duniani, kisha wataingia katika karamu ya harusi ya Mwana-kondoo huko Mbinguni pamoja na Yesu Kristo, ambaye amefanyika kuwa Bwana-harusi wao. 
Baada ya hili, Mungu atawaamuru malaika wake kuyamimina mapigo ya mabakuli saba yaliyojazwa ghadhabu ya Mungu, mapigo ambayo alikuwa ameyahifadhi kwa uvumilivu tangu wakati wa uumbaji, kwa ajili ya Mpinga Kristo na wafuasi wake, na wenye dhambi wote wa ulimwengu huu watakaokuwa wapo duniani. Hivyo, ulimwengu utakabiliana na mapigo makubwa sana ambayo hakuna mfano wake uliowahi kuonekana hapo kabla. Watakatifu watakaokutana na Bwana angani watakuwa wakimsifu Bwana angani kwa ajili ya mapigo ya mabakuli saba yatakayokuwa yakimiminwa hapa duniani. 
Baada ya kuwa wameshiriki katika ufufuo na unyakuo kupitia Bwana, basi watasimama katika bahari ya kioo iliyochangamana na moto ili kuisifu hukumu ya haki ambayo Mungu anaileta duniani. Hivo, watakatifu ambao waliuawa na kuwa wafia-dini na walioshiriki katika ufufuo na unyakuo wao kwa kupitia nguvu za Bwana watamsifu Bwana bila kukoma, watamsifu kwa ajili ya wokovu ambao amewapatia, na kwa hukumu yake kwa Mpinga Kristo na watumishi wake kutokana na nguvu zake kuu na zisizo na kikomo. 
Kila mtu hapa ulimwenguni atateseka sana wakati malaika watakapokuwa wakiyamimina mapigo yao, yaani kuanzia pigo la vidonda na majipu, pigo la bahari kugeuka na kuwa damu; pigo la bahari kugeuka na kuwa damu; pigo la maji kugeuka na kuwa damu; pigo la kuunguzwa na joto kali la jua; na pigo la giza na maumivu. Wakati malaika wa sita atakapolimimina bakuli lake katika ule mkubwa wa Frati, maji yake yatakauka, ili kuiandaa njia ya wafalme toka mashariki. Kutokana na pigo hili kutakuwa na njaa kubwa sana itakayoikumba dunia, njaa ambayo italeta mateso makubwa kwa wanadamu. Mapepo yatakuwa mengi sana, huku yakishawishi roho za watu kupitia Mpinga Kristo na nabii wa uongo. 
Kisha, roho za mashetani zitawashawishi wafalme wa duniani kwa ajili ya vita na kuwakusanya mahali panapoitwa Harmagedoni ili kupigana na Mungu Mwenyezi. Hapa ndipo mahali ambapo vita ya mwisho kati ya Shetani na Mungu itapiganwa. Lakini kwa kuwa Yesu ni Mungu Mwenyezi, atashuka toka angani akiwa ameketi katika farasi mweupe pamoja na jeshi lake, atamshinda shetani, na kisha kumtupa Mnyama katika ziwa liwakalo kwa moto na kibiriti (Ufunuo 19:11-21). Kwa kuwa hivi sasa Yesu Kristo ana nguvu kamili kama Bwana anayekuja mara ya pili, basi ataonekana hapa duniani ili kuuhukumu ulimwengu na kumwangamiza Mnyama. 
Kwa hiyo, tunapaswa kutambua kwamba wakati Yesu Kristo atakaposhuka toka Mbinguni wakati wa unyakuo wa watakatifu, hatashuka hadi hapa duniani, bali atakuja angani na kuwachukua watakatifu kwenda mahali alipo, atawaruhusu kukutana nao angani na kuwaingiza katika karamu ya harusi Mbinguni. Wakati Bwana atakaporudi hapa duniani, atafanya hivyo ili kumshinda Shetani na jeshi lake wanaosimama kinyume na Mungu, atawashinda kwa Neno lake lenye nguvu katika Vita ya Harmagedoni, atafanya hivyo ili kumtupa Ibilisi katika ziwa la moto na kibiriti, na kisha kuwaua wafuasi wake wote watakaokuwa wamesalia. Huu ndio ujio wa Bwana wa mara ya pili. Tunapaswa kuwa na ufahamu na imani sahihi ambayo inaweza kutofautisha kati ya kushuka kwa Bwana angani na ujio wake wa mara ya pili hapa duniani. 
Hata hivyo kuna watu wengi wanaofikiri kwamba Bwana atashuka moja kwa moja hapa duniani wakati unyakuo utakapotokea. Kwa kweli hiyo si sahihi. Unyakuo utakapotokea, Bwana hatakuja hapa duniani, bali atakuwepo angani. Kwa maneno mengine, atawainua na kuwapokea watakatifu angani. 
Kwa hiyo, unapaswa kuondokana na fikra kwamba Bwana atakuja tena hapa duniani wakati wa unyakuo, na badala yake unapaswa kwa kuzingatia Neno lililoandikwa, uanapswa kufahamu kwamba unyakuo wa watakatifu utatokea wakati malaika wa saba atakapolipiga tarumbeta lake.