Search

关于基督教信仰的常见问题解答

话题2:圣灵

2-8. Nini maana ya kupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu?

Yatupasa kuelewa sababu ya ubatizo wa Yesu. Paulo alihubiri Injili ya ubatizo wa Yesu kwa baadhi ya Waefeso alipo sikia ya kwamba walikuwa wamebatizwa kwa “ubatizo wa Yohana tu”. Waliweza batizwa katika jina la Yesu Kristo na kupokea Roho Mtakatifu mioyoni mwao kwa kuamini kile Paulo alichosema juu ya ubatizo wa Yesu. Asili ya ubatizo wa Yesu alio upokea toka kwa Yohana na ubatizo huo wa Yohana wa toba ilikuwa ni tofauti. Ubatizo wa Yesu ulikuwa ni kutakasa dhambi ambao ni moja kwa moja unauhusiano na kupokea Roho Mtakatifu.
Sasa basi nini asili ya ubatizo wa Yohana? Alipaza sauti “tubuni enyi wazao wa nyoka! Acheni miungu yenu ya kigeni mnayo itumikia na kumrudia Mungu wa kweli”. Ubatizo wa Yohana ulikuwa ni watoba ambao uliwafanya watu wa mrudie Mungu. Hata hivyo ubatizo wa Yesu alio upata toka kwa Yohana ulikuwa ni kwa nia ya kumtwika dhambi za ulimwengu. Hii ndiyo tofauti kati ya ubatizo wa Yohana na ule wa Yesu kwa Yohana. Ubatizo wa Yesu ulitimiza haki yote.
Sasa basi ubatizo gani ulio timiza haki yote? Ni ubatizo ambao kwa kupitia Yesu ndiyo uliobeba dhambi zote za wanadamu tokea Adamu hadi mtu wa mwisho kuishi ulimwenguni. Kwa maneno mengine, ubatizo wa Yesu kwa Yohana ulikamilisha haki yote.
Kutimiza haki yote maana yake Mungu alimleta Mwana wake abatizwe na Yohana ili kubeba dhambi kwa ajili hiyo kwa kuhukumiwa msalabani Mungu alimfufua Yesu toka kifoni hivyo kutakasa wale wote wenye kumwamini.
Hili lilifanywa kwa ajili ya watu wote. Ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani ulituletea wokovu wa milele, msamaha wa dhambi zetu zote na nafasi ya kuishi na Mungu milele. Hii ndiyo haki ya Mungu upendo na wokovu wa wanadamu wote. Hapa tunaweza kuthibitisha ubatizo wa Roho Mtakatifu ulikamilishwa kwa kupitia ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani.
Ili kubatizwa katika jina la Yesu Kristo yatupasa tuwe na ushuhuda wa kuamini kwamba dhambi zetu zote ulimwenguni zilitwikwa juu ya Yesu kwa njia ya ubatizo wake. Kila aliye pokea msamaha wa dhambi kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani itampasa abatizwe katika jina la Yesu Kristo.
Hivyo tunabatizwa ikiwa ni uthibitisho wa imani yetu katika ubatizo wa Yesu na kutumiza ile amri ya Yesu iliyo sema “Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi mkwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu” (Mathayo 28:19). Yesi alibatizwa na Yohana ili kwamba aweze kubeba dhambi zote za ulimwengu na kwa kuwa huu ndiyo ukweli uongozao watu katika kumpokea Roho mtakatifu, hivyo basi utaweza kuitwa pia ni ubatizo wa Roho Mtakatifu.