Search

שאלות נפוצות על האמונה הנוצרית

נושא 2: רוח הקודש

2-6. Je, kunena kwa lugha si ushahidi wa kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu? Ni kwavipi basi tutaweza kujua yumo ndani yetu?

Hatutoweza kuwa na uhakika endapo mtu anaweza kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yake kwakuwa tu ananena kwa lugha. Hata watu walio pagawa na pepo wachafu hunena kwa lugha. Yakupasa uelewe ya kwamba shetani aweza kufanya mtu anene kwa lugha ngeni kwa jina la Yesu Kristo.
Ikiwa tutasema ya kwamba kunena kwa lugha ni ushuhuda wa Roho Mtakatifu kuweka makazi ndani ya mtu, basi hakika hili si sahihi kulingana na uhalisi wa kibiblia na hivyo kupeleka katika dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu. (1Wakorintho 12:30) inasema “wote wana karama za kuponya wagonjwa? wotewanena kwa lugha? wote wafasiri?” Kwakuwa Roho Mtakatifu ni Roho wa Mungu yeye hawezi kuwa na dhambi ndani yake wala kamwe hawezi kuweka makazi ndani ya mtu mwenye dhambi moyoni.
Imetupasa kutoamini kwamba mtu amempokea Roho Mtakatifu kwasababu tu ameweza kunena kwa lugha, bali yatupasa awali tuchunguze ikiwa mtu huyo amekwisha pokea msamaha wa dhambi kwa kuamini injili ya maji na Roho. Ikiwa mtu fulani atadhani ya kwamba amekwisha mpokea Roho Mtakatifu kwa sababu tu ana aina fulani ya matukio yasiyo ya kawaida, kama vile kunena kwa lugha, basi upo uwezekano mkubwa kwamba amepotoka katika udanganyifu wa shetani (2 Wathesalonike 2:10). Roho Mtakatifu ni karama ambayo hutolewa na Mungu kwa watu wote walio kwisha kupata msamaha wa dhambi kwa kupitia maneno yake Mungu.
Kwa kukujibu swali lako la pili, Roho Mtakatifu ni Mungu halisi na ni Roho wa kweli. Hivyo yeye hutenda kazi pamoja na injili ya maji na Roho. Yeye hafanyi kazi kulingana na mapenzi ya mwanadamu. Huwaongoza wenye dhambi katika kuiamini injili ya maji na Roho, akiwafundisha ukweli wenye haki, na pia akifundisha kwa upole juu ya injili ambayo ndiyo mapenzi ya Mungu pamoja nao. Haji juu ya watu kwa hisia za moto au kutetemesha miili. Mungu amewapa Roho Mtakatifu wale wote wenye haki ambao dhambi zao zimefutwa kwa njia ya utii wao wa injili ya maji na Roho. Amewafundisha kwamba wao wamekuwa watoto wa Mungu. Roho Mtakatifu hushuhudia ndani ya mioyo ya wenye haki kwamba wamekuwa ni watu wasiyo na dhambi na wenye haki kamili kupitia injili ya maji na Roho.
Hivyo ikiwa mtu atanena kwa lugha huku akiwa bado anadhambi moyoni Roho huyo aliye ndani yake hakika si yule Roho Mtakatifu bali ni roho wa shetani. Ikiwa unataka Roho Mtakatifu aweke makazi ndani ya moyo amini injili ya maji na Roho na ndipo basi Bwana atakubariki na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yako.