Search

שאלות נפוצות על האמונה הנוצרית

נושא 2: רוח הקודש

2-10. Niliwahi kuishi kwa muda mrefu na huzuni baada ya tabibu kunifanyia uchunguzi na kugundua kwamba tatizo langu la tumbo lilikuwa ni saratani. Siku moja rafiki yangu Mkristo alinitembelea na kuaniambia ya kwamba kila atakaye hudhuria mkutano wa hadhara katika kanisa lao ataponywa magonjwa ya aina zote. Kwangu mimi niliyekuwa sina imani na Mungu, kwa wakati huo kuponywa kwa ugonjwa kwa nguvu za Mungu ingelikuwa ni jambo zuri na laukweli. Katika siku ya mwisho wa mkutano huo, kila mtu alimjia mtumishi huyo ili kupokea tendo la kuwekewa mikono yake. Aliponiwekea mikono juu yangu aliniambia niseme maneno nisiyo yaelewa na kuniuliza ikiwa na mwamni Yesu Kristo kwa uponyaji wa nguvu zake. Ingawa kusema kweli sikuwa namwamini moyoni nilifedheheka na kujibu ndiyo. Na papo hapo nilihisi kitu kama joto la umeme likipita ndani yangu. Niliweza kuhisi mwilini kuwa saratani emeponywa. Nikaamua kumwamini Bwana muda huo huo na baadaye furaha kuu na amani ilinijia moyoni na nikaanza maisha mapya. Nilianza pia kujitolea kueneza injili. Nadhani huyo alikuwa ni Roho Mtakatifu aliye sababisha yote haya na naamini ya kwamba ameweka makazi ndani ya moyo wangu. Je wewe nawe hudhani kuwa ni hivyo?

Ama kwa hakika ulipatwa na jambo la ajabu. Nimekwisha sikia shuhuda nyingi za aina hii toka kwa watu walio jitolea maisha yao kuishi kwa ajili ya Bwana baada ya matukio ya majibu ya sala zao kwa Mungu. Hata hivyo, ningelipenda kukuuliza ikiwa muujiza huo wako usio kwa kawaida utaweza kuwa bila shaka ni uthibitisho wa kwamba umempokea Roho Mtakatifu.
Kwa jambo la hakika, wakristo wengi nyakat hizi wataweza kujibu “Ndiyo” kwa swali hili. Wakati fulani Ukristo wa Magharibi ulikuwa ukianguka katika kipindi cha watu kupenda ya dunia. Kwa kipindi hicho kukaja wakati ulio kuwa ikiitwa “Vugu vugu la Karama za Kipentekoste” (Pentecostal-Charsmatic Movement) uliochipuka na Ukristo ukaonekana kuamka ajabu, na hasa katika nchi zisizo endelea na zilizoendelea.
Matokeo yake wakristo wengi waliangukia katika tabia hii ya uamsho ambayo ilitilia mkazo zaidi umuhimu wa matendo ya miujiza isiyo ya kawaida. Wale waliokuwa wakiongoza mikutano hii ya uamsho mara nyingine walipata umaarufu mkubwa wakiwa wainjilisti wa uamsho. Zaidi ya yote kwa kuwa walikua na shuhuda za ajabu zikiwa zao binafsi na kuelezea imani yao kwa njia yao.
Hata hivyo Biblia inasema “Hapana” kwa swali hilo hapo juu. Bila shaka Roho Mtakatifu anao uwezo kweli wa kutenda miujiza isiyo ya kawaida. Ingawa kwa kuwa yeye ni Roho wa kweli (Yohana 15:26) tutaweza kupokea Roho Mtakatifu ikiwa tu kwa njia ya neno la kweli.
Petro alimpokea Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste na kwa kifua mbele aliweza kuihubiri injili akisema “Mungu umemfanya Yesu huyo mliye msulubisha kuwa Bwana na Kristo”. Ndipo wayahudi walio kuwa wakimsikiliza Petro na Mitume wengine wakajibu wakisema “Tutendeje ndugu zetu?” (Matendo 2:36-37) na akawajibu. “Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kua ahadi hii ni kwa ajili yenu na kwa watoto wenu na kwa watu wote walio mbali na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie” (Matendo 2:38-39).
Kwa maneno mengine Mungu alisema bayana kwamba atamleta Roho Mtakatifu kama zawadi kwa wenye haki walio pokea ondoleo la dhambi kwa kuamini injili ya Yesu Kristo. Uthibitisho wa pekee wa Roho Mtakatifu kuweka makazi ndani ya moyo wa mtu ni lile neno la kweli.
Je umekwisha pokea ondoleo la dhambi kwa njia ya injili ya maji na Roho? Ikiwa ndiyo basi utaweza kuwa na uhakika kuwa Roho Mtakatifu umekwisha weka makazi ndani ya moyo wako.
Hata hivyo haijalishi ni tukio gani la ajabu unaloweza kuanalo hapo awali au jambo linalo kushangaza ambalo ulilitenda, lakini bila shaka bado hujaweza kumpokea Roho Mtakatifu ikiwa bado unadhambi moyoni mwako. Sababu ni kwamba huna ushuhuda wa ondoleo la dhambi litokanalo na msingi wa neno la kweli. Kama ilivyo giza kutoweza kuwa na nuru, ndivyo hata Roho Mtakatifu hatoweza kuja ndani ya mwenye dhambi au hata kuweka makazi.
Nilikwisha pokea maswali ya aina mbali mbali yahusuyo jambo hili na utaweza kupata majibu yote kwa njia ya wewe kuamini juu ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani. Sasa kila anayeamini juu ya Yesu ataweza kumpokea Roho Mtakatifu ambaye Mungu aliahidi kumwaga katika nyakati hizi za mwisho. Tunamshukuru Bwana Mungu. Haleluyah!
Kitabu hiki kimejaa habari muhimu juu ya Roho Mtakatifu kitaweza kukusaidia kujibu maswali yako ikiwa ungehitaji kujua zaidi juu ya injili ya maja na Roho. Tafadhali pitia vitabu vya mwanzo vya mwandishi vilivyo katika mlolongo wa vitabu vyako vya Kikristo.
Je, umezaliwa kweli kwa maji na kwa Roho? 
Seoul: Hephizabah (toleo la Kiswahili)
Rudi katika Injili ya maji na Roho
Seoul: Hephzibah (toleo la Kiswahili)
Mungu anakuhitaji wewe uweze kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu na hatimaye umsubiri Bwana kuja kwake. Ikiwa unaamini maneno ya Mungu pamoja na mwandishi basi utapokea uwepo wa Roho Mtakatifu na hatimaye kumrudishia Bwana utukufu.