Search

خطبے

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 9-1] Utangulizi Kwa Sura ya 9 

Injili ya Maji na Roho Kwa Waisraeli na kwa Wamataifa!
 
Kwa nini Paulo alisema kuwa anahuzuni sana na uchungu unaoendelea katika moyo wake kwa ajili ya watu wake? Ni kwa sababu Paulo alikuwa ana kitu anachokitaka kwa ajili ya ndugu zake, na ndio maana alikuwa radhi kulaaniwa na kukatwa toka katika Kristo kwa ajili yao. Kwa mujibu wa mwili wake, Paulo alipenda sana kwamba watu wake waweze kuokolewa. 
Katika kipindi hiki, tunapendezwa sana na kuihubiri injili ya maji na Roho katika ulimwengu mzima. Kuueneza ukweli huu wa injili ni kitu ambacho ni muhimu sana kwa Mungu na kwa wakati huo huo ni lengo kuu kwa waamini waliozaliwa tena upya. Kitu kingine ambacho kinatufanya tuwe makini ni kwamba Waisraeli wataipokea au hawataipokea injili ya maji na Roho katika siku za mwisho. Ni lazima tuendelee kuwombea Waisraeli ili kwamba waweze kuokolewa, kwa kuwa watakapo ipokea injili tutajua kwa hakika kuwa kuja kwa Bwana wetu mara ya pili kunakaribia. 
Mada yangu ya maombi kwa mwaka huu ni kuomba kwa ajili ya uinjilisti katika ulimwengu mzima na kupokelewa kwa injili ya kweli na Waisraeli. Pia ninaomba kuwa Waisraeli wawapate watumishi wa Mungu kwa ajili ya Waisareli wenzao. Wakati fulani Mungu aliwapatia Waisraeli Sheria na pia aliwafanya kuwa ufalme wa makuhani mbele ya macho yake. Kristo mwenyewe alikuja kwa jinsi ya mwili toka kwa Waisraeli, lakini walikataa kumwamini yeye, na bado wapo kinyume na Mungu kwa kuendelea kugeuka kinyume na mapenzi yake. 
 

Bwana Alituambia Kuwa Itakuwa Vigumu Kuipata Imani Wakati Atakapokuja Tena
 
Baada ya kuwa injili imeanzia Yerusalem ni mapenzi ya Mungu kwamba injili hii ienezwe katika ulimwengu mzima. Hata hivyo, siku hizi mioyo ya watu imefanywa kuwa migumu. Watu wengi wamepotea mbali na kuacha kuutafuta ukweli. 
Hivi karibuni katika filamu iliyokuwa imepewa jina la “Jaribu la Mwisho la Kristo” ambayo ilimwonyesha Yesu kuwa ni kama mtoto asiye wa haki ilitolewa hapa Korea. Ilikuwa imejawa na dhihaka na ujumbe wake mkuu ulikuwa ukisema kuwa Yesu si Mungu na hakuwahi kuwa Mungu bali alikuwa ni mwanadamu wa kawaida, kama alivyokuwa Mwana wa Mfalme Siddharta wa India ambaye alikuja baadaye kujulikana kama Buddha. Filamu hii inaukanyaga ukweli kuwa Yesu ni Mungu na Mwokozi wetu. Hii ndiyo sababu Mungu alisema, “Walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?” (Luka 18:8). 
Yesu Kristo ambaye tunamwamini ni Mungu, na yuko juu kuliko viumbe vyake vyote na anapaswa kuabudiwa na kutukuzwa milele. Hali akiwa amezaliwa kati ya Waisraeli, Yesu alizichukua dhambi zetu zote kwa kubatizwa na Yohana, aliimwaga damu yake na kufa Msalabani, siku ya tatu akafufuka tena toka kwa wafu na amefanyika kuwa Mwokozi wa wale wote wanaomwamini yeye. Bwana, ambaye alifanyika kuwa haki ya Mungu alitukomboa sisi toka katika dhambi zetu zote kwa kuwahesabia haki wote wanaomwamini yeye. 
Paulo alituambia sisi kuwa bila kujalisha kuwa Waisaeli ni wengi kiasi gani, wazawa wa Ibrahimu, yaani wale wanaoweza kufanyika watoto wa Mungu ni wale tu wanaomwamini Yesu. 
Waisraeli watakutana na majaribu mengi na mapigo hapo baadaye. Mapenzi ya Mungu ni kwamba baadhi yao hapo mwishoni wafikie hatua ya kumwamini Bwana wetu kuwa ni Mwokozi wao. Pamoja na kuwa Bwana wetu amezichukua dhambi zote za ulimwengu zikiwamo dhambi za Waisraeli bado Waisraeli wanakataa kumwamini Yesu kuwa ni Mwokozi wao. 
Je, wewe ni dhaifu? Baadhi yetu tunaweza kuwa wadhaifu zaidi au tukawa na nguvu zaidi kuliko wengine. Lakini mbele za Mungu sisi sote tumejawa na mapungufu. Tunaweza kufanyika watoto wa Mungu walio huru toka katika dhambi kwa kuamini kuwa Bwana wetu alikuja hapa duniani akazichukua dhambi zetu zote katika mwili wake kwa ubatizo wake, na akahukumiwa na kuadhibiwa badala yetu kwa kufa Msalabani. Ni lazima tuzisifu na kuamini katika nguvu za Mungu ambazo zimetufanya sisi kuwa watu wake walio huru toka katika dhambi. Kwa kweli Bwana wetu ni mkuu sana. 
Baadhi ya watu wanafikiria kuwa kila kitu kipo kwa sababu ya wanaume. Kwa mfano, wanafikiri kuwa sheria zinatungwa na kupitishwa na wanaume. Hata hivyo, ni lazima tutambue kuwa si kila kitu kinatokana na wanaume; vitu vyote vinafanywa viwezekana kwa mapenzi ya Mungu tu. Mungu aliiumba dunia hii na ulimwengu mzima. Hata zile sheria zilizoundwa na wanadamu zinazotutawala kwa asili yake zimejengwa kutokana na mapenzi ya Mungu. 
Kwa kuwa Mungu anafanya kazi katika kila kitu na kila kitu kinafanyika kwa mapenzi yake, basi sisi ni lazima tuigundue haki yake katika mambo yote. Wakati tulipokuwa tungali wadhaifu, tulipokuwa tukitenda dhambi kinyume na Mungu, na tulipokuwa tumekatwa kutoka kwake kwa sababu ya dhambi zetu, Mungu aliahidi kumtuma Yesu Kristo kwa ajili yetu. Yesu alizitimiza ahadi za Mungu kwa kufanyika mwili na kwa ubatizo ambao kwa huo ametukomboa toka katika dhambi za ulimwengu. 
Sasa, wakati injili ya maji na Roho inaenea katika kila kona ya ulimwengu, basi mpango wa Mungu wa asili utakamilika. Tunapoangalia jinsi matukio mbalimbali ulimwenguni yanavyotokea, tunaweza kuona kuwa Marekani na Israeli zipo katikati. Ninaamini kuwa pasipo msaada wa Mungu vita nyingine ya dunia inawezekana kutokea. 
Wakati Kitu cha Biashara Ulimwenguni kilipoanguka, matokeo yake yaliweza kuonekana katika ulimwengu mzima. Katika wakati huu ikiwa ulimwengu utakuwa umegubikwa na vita tena ni kitu gani kitatokea kwetu? Kwa hakika tunaweza tusiweza kupona na kurudi katika hali ya kawaida toka katika vita nyingine ya dunia. Hata hali ya mazingira ya asili yanaweza pia yasipone kutokana na uharibu utakaokuwa umefanyika. Nina amini kuwa ninyi nyote mtaomba ili kwamba tuweze kuhubiri injili ya maji na Roho katika ulimwengu mzima kwa amani. Wasiwasi wetu ni kuwa pasipo amani duniani tunaweza tusifanikiwe kufanya hivyo. Sisi sote ni lazima tuombe kwa ajili ya amani na tujitahidi kuondoa vita na ugaidi. 
Hakuna dini iliyoundwa na wanadamu inayoweza kuondoa dhambi za mwanadamu. Ni Yesu Kristo tu na ni yeye tu anayeweza kutukomboa toka katika dhambi zetu. Dhambi zetu zinaweza kutoweshewa mbali na kuhukumiwa kwa kupitia ubatizo wake tu toka kwa Yohana na damu yake Msalabani. Baraka hii inatolewa kwa wale wanaoamini katika haki ya Mungu. Njia pekee inayoweza kutufanya sisi tukombolewe toka katika dhambi zetu ni kwa kuamini katika ubatizo na damu ya Yesu. Hakuna njia nyingine. Sisi hatupatanishwi dhambi zetu kwa maombi ya toba kama ambavyo watu wengi wa dini wanavvyopendelea kufanya. Bali njia pekee ya kutufanya tupatanishwe na Mungu kutokana na dhambi zetu ni kwa kuamini katika haki ya Mungu ambayo imetukomboa toka katika dhambi zetu zote kwa ukamilifu kwa kupitia kufanyika mwili kwa Yesu ambaye alizichukulia mbali dhambi zetu zote kwa ubatizo wake na damu yake Msalabani. 
 

Tunaokolewa Toka Katika Dhambi Zetu Zote Kwa Kuamini Katika Ukweli wa Injili ya Maji na Roho 
 
Ukweli huu ni lazima uhubiriwe katika kila kona ya ulimwengu. Ni lazima tutambue kuwa kutoamini katika ukweli huu ni dhambi ya Waisraeli na Wamataifa pia. Kila mtu ni lazima aamini katika injili ya maji na Roho. 
Mataifa yote, Waisraeli na Wamataifa wote hawawezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kutenda dhambi wakati wanapoishi hapa ulimwengu. Lakini Bwana wetu alizishughulikia dhambi hizi zote mara moja na kwa wote kwa ubatizo wake. Je, kunaweza kuwa na ukweli rahisi na wa wazi kuliko ukweli huu wa ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani? Kwa nini Yohana alimbatiza Yesu? Yesu alibatizwa na Yohana na alisulubiwa ili kwamba aweze kuzichukua dhambi zetu zote mara moja na kwa wote. Watu wataelekea katika maangamizi yao kwa sababu ya dhambi ikiwa hawataupokea na kuuamini ukweli huu. 
Ubatizo ambao Yesu aliupokea “kwa kuwa” (Mathayo 3:15) unaitimiza haki yote. Neno ‘kwa kuwa’ kwa Kiyunani ni ‘hoo’-tos gar’, lina maanisha ni ‘kwa namna hii,’ ‘ndivyo ipasavyo,’ au ‘hakuna njia nyingine zaidi ya hii.’ Neno hili linaonyesha kuwa Yesu alizichukua dhambi za mwanadamu katika mwili wake kwa kupitia ubatizo alioupokea toka kwa Yohana. Kwa kuwa Yesu alizichukua dhambi zetu zote za ulimwengu katika mwili wake kwa kubatizwa na Yohana, basi ndio maana Yesu aliweza kuubeba Msalaba na kuimwaga damu yake juu yake kwa niaba yetu. Ni lazima tutambue kuwa huu ni ukweli wa upatanisho ambao kwa huo ulimwengu mzima unaweza kukombolewa. 
Bwana wetu alituambia kuwa, “Ninyi mkikaa katika Neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli. Nanyi mtaifahamu kweli, na hiyo kweli itawaweka huru.” (Yohana 8:31-32) Ubatizo wa Yesu na damu yake ndio kweli ya Mungu ambayo imetukomboa toka katika dhambi zetu na imejengwa katika Neno la Mungu lililoandikwa. Ukweli wa upatanisho utadumu pamoja na injili ya maji na Roho hadi milele. Mungu Baba aliamua kwa mapenzi yake kuwa wenye dhambi wapatanishwe na ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani. Tunapoamini katika ubatizo wake na damu yake kwa ajili ya ukombozi wetu basi tunakuwa tunaamini kile ambacho Mungu amekiweka kwa ajili yetu. Dhambi zetu zinapatanishwa wakati tunapoamini katika ukweli wa injili ya maji na Roho. 
Ikiwa unaamini kwa wakati huu katika ubatizo wa Kristo na damu yake Msalabani, ambayo ni ukweli wa upatanisho kwa ajili ya ukombozi wako basi kwa hakika utahesabiwa haki. Kwa upande mwingine, ikiwa huamini basi ujue ya kuwa wewe ni mwenye dhambi. “Wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu,” (Warumi3:23) Tunaweza kuokolewa toka katika dhambi zetu zote na kufanyika watoto wa Mungu kwa kumwamini Yesu Kristo kuwa ni Mwokozi wetu. Hakuna sababu inayomfanya mtu asiamini katika ukweli wa injili ya maji na Roho. Hakuna hata mmoja asiyeihitaji injili hii kwa ajili ya ukombozi. Kila mtu anaihitaji injili hii. Kwa nini mtu hapendi kuiamini injili hii wakati ukweli wa injili ya maji na Roho upo wazi mbele zake? 
Watu wengi katika ulimwengu mzima wameipokea injili ya maji na Roho na wanaihubiri injili hiyo zaidi na zaidi. Baadhi yao wameomba kwa kujitolea kuwa wasambazaji wa vitabu vyetu. Ikiwa utakuwa umekombolewa toka katika dhambi zako kwa kuamini katika damu ya Yesu Msalabani tu basi kila mtu katika ulimwengu angekuwa amehesabiwa haki na kuwa huru mbali na dhambi. Ikiwa mtu anaamini tu katika damu ya Yesu Msalabani, basi mtu huo ataendelea kutenda dhambi hata kama atakuwa anazirudia sala za toba kila siku. Kwa kuwa sala hizo ni sehemu ya utaratibu wao hali zikihusisha hisia na utekelezaji wa mambo ya kidini. 
Ikiwa unajaribu kuziosha dhambi zako kwa kutoa sala za toba, basi kwa hakika unatenda dhambi kubwa dhidi ya Mungu, kwa kuwa matendo yako yanaishushia heshima haki ya Mungu ambayo inaweza kutimizwa si kwa juhudi zako binafsi bali kwa ubatizo wa Yesu na sadaka yake Msalabani ambayo kwa hiyo Yesu alizichukua dhambi zako zote na akaadhibiwa kwa ajili yako. 
Ikiwa utamkubali Yesu kuwa ni Mwokozi wako, basi amini kuwa upatanisho wako wa dhambi ni kuwa kupitia ubatizo wa Yesu na kifo chake Msalabani. Yesu aliahidi kuwakomboa wenye dhambi toka katika dhambi zao, na aliishi akiitunza ahadi yake kwa kubatizwa na Yohana katika Mto Yordani na kwa kuimwaga damu yake Msalabani ili kuitimiza haki ya Mungu. Kuna sababu gani ya kutufanya tusiuamini ukweli huu? Ni lazima uamini katika ubatizo wa Yesu na damu yake aliyoimwaga Msalabani kwa ajili ya ukombozi wako. 
Ukweli kuwa Yesu alizichukua dhambi zote za ulimwegu katika mwili wake wakati alipobatizwa unapatikana katika Mathayo 3:13-17. Ni wale tu ambao hawapendi kusamehewa dhambi zao zote ndio wanaoweza kukataa kuuamini ukweli huu. Unaweza kufanyika mtoto wa Mungu na kupokea uzima wa milele kwa kuamini katika ukweli wa injili ya maji na Roho tu—hakuna kitu kingine kinachoweza kukuomboa toka katika dhambi zako. Hakuna kitu kizuri kama kuamini katika ukweli huu, hakuna kitu chochote ambacho ni zawadi nzuri toka wa Mungu zaidi ya msamaha wake. Miongoni mwa karama nyingi ambazo Mungu ametupatia, upatanisho wa dhambi ndiyo karama nzuri kuliko zote. 
Karama ya pili kwa uzuri ambayo Mungu ametupatia ni ule Ufalme wa Milenia unaokuja ambapo tutatawala pamoja naye, na karama ya tatu ni kwamba baada ya utawala huo tutaishi katika Ufalme wa Mbinguni na kutawala pamoja na Mungu milele. Mungu ameuruhusu ukweli huu wa ukombozi katika nyakati hizi za mwisho kufunuliwa kwa Waisareli na Wamataifa. 
Kama ilivyotabiriwa katika Maandiko, watumishi wawili wa Mungu watainuka kati ya Waisraeli na Mungu atafanya miujiza ya kushangaza ya injili kwa kupitia watumishi hao. Kisha Waisraeli wataisikia injili ya maji na Roho kwa kupitia watumishi hao wawili ambao Mungu atawainua toka kati yao, na wengi watamwamini Yesu kuwa ni Masihi wao. Sisi tunaisubiri siku hiyo kama Yohana alivyosubiri kwa kusema, “Na uje Bwana Yesu!” (Ufunuo 22:20). 
Wakati utakapowadia wa Bwana wetu kuja tena ndipo utakapotambua jinsi ilivyokuwa muhimu kwako wewe kuuamini ukweli huu ambao kwa uhuo ulisamehewa na kuokolewa. Ni shauku yangu kuu toka moyoni kwamba ukombolewe toka katika dhambi zako zote kwa kuamini katika ukweli wa injili ya maji na Roho. Ulimwengu unaweza kubadilika, lakini injili ya maji na Roho ambayo kwa hiyo Mungu ametuokoa sisi toka katika dhambi zetu ni ukweli usiobadilika kamwe na wa milele. Ni lazima tuuamini ukweli huu ili tuweze kupokea wokovu usiobadilika wa upatanisho. Ukombozi wa Mungu na uwe nawe. 
 

Mungu Ametukomboa Sisi Kwa Kutufanya Kuwa Vyombo vya Rehema
 
Warumi sura ya 9 inasema kuwa Mungu alimwokoa Yakobo kwa sababu alikuwa amependwa sana kuliko Esau. Kwa hiyo, Yakobo alifanywa kuwa ni chombo cha rehema wakati Esau alifanywa kuwa chombo cha ghadhabu. Hii inaleta swali la kwa nini? Swali hilo ni kuwa je, Mungu alimpendelea Yakobo halafu akamchukia Esau? Bila shaka kutakuwa na watu wengi ambao wanaweza kutoa hoja kuwa “Kwa kuwa Mungu aliamua na kumchagua mmoja na kumpenda hali akimchukia mwingine bila sababu, basi kwa hakika uchaguzi wake tangu asili si sahihi.” 
Tunapouangalia ulimwengu ulioumbwa na Mungu tunaweza kuona jinsi ulivyo mzuri na jinsi uumbaji ulivyokuwa safi. Mimea, wanyama, na vitu vingine vyote ambavyo viliumbwa na Mungu vinaonekana kuwa ni vikamilifu sana. Sasa inawezekanaje basi Mungu akampenda mtu mmoja wakati anamchukia mwingine? Lakini jambo hili haliko hivyo. 
Kwa sababu ya utovu wa nidhamu wa Adamu na Hawa, dhambi iliingia duniani, na kwa sababu ya dhambi hizi, wale wote waliokuja baada yao walipangiwa kuendelea katika dhambi na hawakuweza kufanya lolote zaidi ya kustahili kuadhibiwa kwenda kuzimu. Kwa kuwa Mungu alimkomboa Yakobo toka katika dhambi na hakumkomboa Esau haimaanishi kuwa alitenda jambo baya. Mbele za macho yake Mungu alikuwa na kila sababu ya kufanya hivyo.
Tunaweza kuwaona watu wengi ambao wana tabia kama ya Esau katika jamii ya Kikristo. Kwa kawaida mtu wa jinsi hiyo hawezi kukosa kwenye ibada bila kujalisha kuwa ibada hiyo inafanyika lini na wapi, hata kama ni kuanzia mapema asubuhi hadi jioni. Baadhi yao wanaweza hata kutumia muda mwingi kanisa kuliko hata nyumbani, wakitoka kazini kwenda kanisani na si nyumbani. Watu wa jinsi hiyo tunaweza kuwaita kuwa ni ‘wanariadha wa kidini’. Hata hivyo, kuna wengi miongoni mwao ambao haichukulii haki ya Mungu kwa umakini. Hii ni kwa sababu wanajaribu kuijenga haki yao wenyewe, na wanapofanya hivyo wanajikuta wakiidharau haki ya Mungu. 
Hata wale ambao wanaidharau haki ya Mungu bado wanapenda kwenda mbinguni na wanapenda dhambi zao zisamehewe. Lakini juhudi zao zinalenga katika kujaribu kuimarisha haki yao binafsi mbele za Mungu na watu wengine, na si kuokolewa toka katika dhambi zao. Mungu alisema kwa wale ambao hawaamini katika haki yake kuwa imani katika haki ya Mungu si ya kila mtu. 
Je, ni aina ipi ya watu ambao wanaweza kuamini katika haki ya Mungu? Hawa ni watu ambao wanazitambua dhambi zao, ambao kwa mawazo yao wanatambua kuwa wao si kitu chochote. Hao ni aina ya watu ambao mara baada ya kuigundua haki ya Mungu kwa kupitia upatanisho wake uliodhihirishwa katika injili ya maji na Roho, basi huamini mara moja na kuanza kumpa Mungu utukufu. Ile hali yetu ya kuiamini haki ya Mungu na kwamba tumeokolewa maana yake ni kuwa sisi ni watu tunaostahili kuonewa huruma na tunaohitaji haki ya Mungu. Vinginevyo tungelipaswa kuishi katika dhambi katika maisha yetu yote yaliyosalia. 
Lakini wale ambao wanaitafuta haki yao binafsi mbele za Mungu ndio wale walio na majivuno. Mtu wa jinsi hiyo anaweza kusema, “Bwana, nilikutolea fungu la kumi, nilikesha usiku kucha nikiomba, sijawahi kukosa hata siku moja sala ya asubuhi kwa miaka kumi iliyopita, na nimefanya matendo mema kwa ajili yako.” 
Hata hivyo, Mungu angelifurahishwa zaidi ikiwa mtu huyo angetambua kuwa yeye hana haki yoyote ile, na kwamba alipaswa kuamini katika haki ya Mungu kwa kupitia upatanisho wa maji na Roho badala ya kujaribu kuthibitisha juhudi zake binafsi ambazo hawezi kuwa nazo. 
Hata sasa, katika jamii ya Wakristo kuna watu wengi ambao wanafanya mambo ya aina nyingi ili kujaribu kuionyesha haki yao binafsi. Baadhi yao wanaigiza hata maneno yao kuwa ya uaminifu. Lakini kwa kuwa hawaamini katika haki ya Mungu iliyodhihirishwa kwa kupitia injili ya maji na Roho, dhambi zao hazijaoshelewa mbali kikamilifu. Mungu ataamua juu ya mwisho wao. Sisi sote tunatarajia kuwa watafanyika kuwa watoto wa Mungu kwa kupitia ondoleo la dhambi kwa imani katika ubatizo wa Bwana wetu na damu yake kama ukweli wa upatanisho. 
Kuhusiana na vyombo vya wokovu, Mtume Paulo alisema kuwa Mungu ana rehema kwa yeyote aliyemrehemu, na ana huruma kwa yeyote anayemuone huruma. Je, ni akina basi ambao wanaokea rehema za Mungu? Wanadamu wote hawawezi kuishi kwa kulishika Neno la Mungu ingawa wanapenda kufanya hivyo. Pamoja na nia yao njema ya kuamini na kuishi kwa kulifuata Neno lake bado wanadamu wanajikwaa mara kwa mara. Wanaishia wakijiona kuwa wamemkosea Mungu na wanafikiria kuwa wanastahili kwenda kuzimu na kuadhibiwa huko. Hivyo wanamwomba Mungu ili awarehemu hali wakitambua kuwa wanastahili kuonewa huruma hapa duniani na katika Ufalme wa Mungu. Kwa kuwa wanatambua kuwa hawawezi kuokolewa hadi pale Mungu atakapowarehemu na kwa sababu hiyo wanamwomba Mungu kwa juhudi ili awarehemu. 
Kwa maneno mengine, ukombozi toka katika dhambi unapatikana kwa wale ambao Mungu anawahurumia, na kwa wale ambao anawarehemu. Mungu aliwapatia watu wa jinsi hii injili ya maji na Roho kwa kumfanya Mwanawe pekee kuzichukua dhambi zote katika mwili wake kwa ubatizo wake na kufa Msalabani na kwa kufufuka toka katika wafu—ili kuwakomboa toka katika maangamizi yao ya uhakika. Mungu wetu ana huruma kwa wale ambao wanastahili kuonewa huruma. 
Lakini inaonekana kuwa katika ulimwengu huu kuna watu wengi ambao Mungu ana ghadhabu juu yao kuliko wale ambao anaowaonea huruma. Mungu anatueleza kuwa katika jamii ya sasa ya Kikristo kuna wengi ambao ni vyombo vya rehema na wale ambao ni vyombo vya ghadhabu. Kwa maneno mengine, kuna watu ambao wanapendwa na Mungu na watu ambao hawapendwi na Mungu. 
Warumi 9:17 inatueleza kuwa, “Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote.” Mungu aliwaruhusu watu kama Farao kuinuka ili kwamba nguvu zake ziweze kujulikana. Hata hivyo, Mungu alionyesha rehema zake kwa vyombo vya rehema ilikwamba jina lake liweze kutangazwa katika ulimwengu mzima. Sisi sote tulikuwa tumepangiwa kwenda kuzimu kwa sababu ya dhambi zetu na ghadhabu ya Mungu. Lakini tuliokolewa toka katika dhambi zetu zote kwa kuwa Mungu alitupatia upendo wa haki yake, kwa kuwa alikuwa na rehema kwetu sisi ambao tulimwamini Yeye. 
Wale wasioamini katika haki ya Mungu na wanaopendezwa katika kuifuta haki yao binafsi watu hao wapo kinyume na Mungu. Hawa ni wale watu ambao Mungu amewaacha kwa ajili ya ghadhabu yake; kwa kuwa ili ghadhabu yake kuu iweze kuonekana ni lazima kuwe na wale ambao wanabakia kusimama kinyuma naye, na kwa kupitia hili hukumu ya Mungu ya haki itaonekana. 
Watu kama Farao ndio wale ambao wameukataa upendo wa haki ya Mungu. Mungu alimpatia Farao mapigo kumi na mwisho likiwa ni kifo. Kwa wale ambao wamemkataa Mungu wanasubiriwa na ziwa la moto usiokwisha. Hii ndiyo nguvu ya ghadhabu ya Mungu. Kuna watu wengi wenye nguvu katika ulimwengu huu na kuna wengi wanaomkana Mungu, lakini hatimaye Mungu atashusha chini ili kuitangaza nguvu ya ghadhabu yake. Hii ndio sababu Mungu anaiacha mioyo migumu ya wale ambao wanamkana peke yake. 
Jambo la muhimu kwetu ni jinsi tunavyoweza kuwa vyombo vya rehema, kwa sababu kwa kufanyika vyombo vya rehema tunaweza kuamini katika upendo wa haki ya Mungu. Hatuna kitu cha kukionyesha mbele za Mungu; bali tulizaliwa ili tuweze kuuamini upendo wake wa haki. Biblia inatueleza hadithi kuhusu mtoza ushuru na Farisayo waliokuwa wakiomba mbele za Mungu. Mungu alimrehemu yule mtoza ushuru na hakumrehemu Farisayo. Watu walio kama mtoza ushuru ni wale ambao wanajitambua mbele za Mungu kuwa hawajafanya jambo lolote lililo jema na kwamba wanapungukiwa na utukufu wa Mungu na kwa sababu hiyo wanamwomba Mungu ili awarehemu. 
Kuna aina ya watu ambao wanaweza kufunikwa katika upendo wa haki ya Mungu. Lakini watu walio kama Farisayo mara nyingi wanajivunia mambo ambayo wameyafanya kwa ajili ya Mungu—kwamba walitoa fungu la kumi, kwamba walifunga mara mbili kwa wiki, kwamba waliomba, na kwamba walikuwa wamejitoa sana katika dini. Tunaweza kuvikwa upendo wa haki ya Mungu au tukastahilishwa adhabu na ghadhabu ya Mungu kutegemeana na mahali ambapo tumesimama mbele za Mungu. Ikiwa tutaifanya mioyo yetu kuwa migumu basi dhambi zetu zitabaki milele na hazitasamehewa. Pasipo msamaha wa Mungu basi hatima yetu itakuwa ni kuzimu. 
Injili ya maji na Roho imekuwa ikihubiriwa katika ulimwengu mzima. Wale ambao bado hawajaokolewa wanabakia kuwa hawajaokolewa kwa sababu wameifanya mioyo yao kuwa migumu. Hakuna kitu cha haki ndani ya wanadamu, na ni kwa imani tu ndipo tunapoweza kuvikwa katika upendo wa haki ya Mungu. Hata kama Mungu aliwaumba, Mungu anawachukia wale ambao hawataki kuitambua haki yake. Lakini wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho ambayo ni haki ya Mungu watapendwa na Mungu na watapokea uzima wa milele. 
Wakristo wengi katika ulimwengu huu kwa sasa wanaishi kama vyombo vya ghadhabu mbele za Mungu. Hii ndio sababu tunahitaji kujifunza toka katika kitabu cha Warumi juu ya haki ya Mungu ilivyo. Sababu inayomfanya Mungu awapende baadhi na kuwachukia wengine ni kwa sababu baadhi yao wanaamini katika haki ya Mungu wakati wengine hawaamini katika haki hiyo. Huu ndio ukweli ambao ninapenda kuuzungumzia. Kile ambacho Mungu alikifanya kwa Yakobo na Esau ni sahihi. Kati ya wale wanaomwamini Yesu kuna wengi ambao wanapenda wapendwe na Mungu pasipo kuiamini injili ya maji na Roho. Watu hawa ni kama Esau na Mungu atawahukumu kulingana na dhambi zao. 
Mungu alimtuma Mwanawe ili abatizwe na Yohana ili kuchukulia mbali dhambi zote ulimwenguni mara moja na kwa wote. Je, unaamini katika ukweli huu? Je, unauamini ukweli huu kwa kina katika moyo wako? Kwa wakati fulani sisi sote tutakombolewa toka katika dhambi zetu zote mara tutakapoamini katika ukweli wa injili ya maji na Roho ambao kwa hiyo haki ya Mungu imefunuliwa. Yesu alizichukulia mbali dhambi zote za ulimwengu huu na akaziweka mabegani mwake, akafa Msalabani kwa ajili ya wote mara moja ili kwamba sisi pia tuweze kuwekwa huru toka katika dhambi zetu zote. 
Lakini ikiwa tunajaribu kupatanishwa pasipo kuamini katika haki ya Mungu tutakuwa tukitenda dhambi dhidi yake. Ikiwa hatuiamini haki yake, basi itamaanisha kuwa Yesu Kristo atapaswa kubatizwa na kufa kila siku kwa ajili ya dhambi zetu. Je, unafikiri Mungu katika hekima yake anaweza kuchagua njia kama hiyo? Ili kutukomboa sisi toka katika dhambi zetu zote Mungu alimtuma Mwanawe pekee mara moja ili abatizwe, asulubiwe na kufa na kufufuka kwa ajili ya dhambi zetu zote ili aweze kutuokoa kikamilifu mara moja na kwa wote. 
Mungu wetu ni Mungu mwenye haki. Mungu alipanga ondoleo la dhambi zetu ndani ya haki yake. Mungu hazitoweshei mbali dhambi zetu ati kwa sababu tunauomba msamaha wake kila tunapofanya dhambi. Badala yake, Mungu alizitoweshea mbali dhambi zote za wale ambao waliwahi kukombolewa kwa kuiamini haki ya Mungu. 
Sasa inakuwaje kwa zile dhambi ambazo tunazitenda kila siku? Dhambi hizi zinashughulikiwa wakati tunapokuwa tukimwabudu Mungu kwa shukrani kwa ajili ya haki yake na tunapomrudishia Mungu utukufu. Kwa mujibu wa mtazamo wa Mungu, Yesu alizichukua katika mwili wake dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo wake, akaimwaga damu Msalabani na akahukumiwa badala yetu, na kwa hiyo alizichukua dhambi zetu mara moja kwa ajili ya wokovu wetu mkamilifu. Upendo wa haki ya Mungu umekamilishwa toka katika mpango wake ili kuziondoa dhambi zote za ulimwengu mara moja. 
Warumi 9:25 inasema, “Ni kama vile alivyosema katika Hosea: Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu.” Ndiyo, Mungu alisema kuwa atawaita watu wake wale ambao hawakuwa watu wake. Kwa hakika sisi tumekombolewa toka katika dhambi zetu zote kwa kuamini katika haki yake kwa kuwa haki ya Mungu tunayoiamini si nadharia. Kwa kuwa ni hakika, wale ambao wanaidharau haki yake watachukiwa na kuhukumiwa kama Esau. Hakuna hata mmoja anayeweza kujivunia haki yake mbele za Mungu. 
Mungu alituokoa kwa haki yake ili kutukomboa toka katika dhambi zetu zote. Tunawezaje basi kutomshukuru na kumsifu Mungu? Sisi hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kuieneza injili ya haki ya Mungu kwa shukrani na imani.