1-30. Ikiwa ufahamu wako juu ya maji na Roho ulikuwa sahihi, hivyo wokovu ingekuwa rahisi kwa yule mwovu aliyesulubiwa na Yesu. Ikiwa mwovu huyo angelichukuliwa kuwa ni msamaha kulingana na sheria, basi Mungu asingekuwa mwenye haki, kwa sababu angevunja sheria yake mwenyewe ya kuingia ufalme wa Mbinguni. Je, waweza vipi kulielezea hili juu ya wokovu wa huyu mwovu pale msalabani?
Katika wakati huo, Wayahudi wote walikuwa wakisubiri kuja kwa Masia. Hivyo, walijua fika juu ya “sheria na mpangilio wa kutoa zabihu ambao Mungu alikwisha wapa kwa kupitia Musa, kuliko watu wengine wowote waliamini kwamba Masia angekuja kulingana na sheria ya Mungu katika upatanisho, na ungewaweka huru tokana na dhambi zao zote.
Ingawa hawakuamini ubatizo wa Yesu uliotoka kwa Mungu kupitia Yohana Mbatizaji ambao ungemtwika dhambi zote za ulimwengu Yesu (Marko 11:27-33) lakini walimchukulia Yesu kama aliye wapotosha watu hivyo wakmsulubisha.
Kwa kuwa Warumi walilindwa na sheria ya kuteswa au kusulibiwa kulingana na sheria ya Kirumi (Matendo 22:25-29, 23:27) twajua basi wale waovu pale msalabani hawakuwa Warumi bali ni Wayahudi. Na pia tunajua kuwa waovu hawa walikuwa ni Wayahudi waliomwogopa Mungu kutokana na maneno yake aliyasema “Bwana unikumbuke utakapofika katika Ufalme wako” (Luka 23:42). Yule muovu wa Kiyahudi tayari alikuwa akielewa sheria na mpangilio wa utoaji wa dhabihu ambao Mungu alimpa Musa. Hivyo aliamini kwamba Masi angelikuja kulingana na sheria ya Mungu ya Mungu katika msamaha.
Wale wajao kwa Mungu yawapasa kukiri kwamba ni wenye dhambi,walio wekewa mwisho wa jehanamu kwa dhambi zao. Mwovu yule alikiri dhambi zake kwa kusema “nayo ni haki kwetu sisi kwa kuwa tunapokea malipo tiliyostahili kwa matendo yetu” (Luka 23:41). Tuweza pia kujua kwamba mwovu huyu alikuwa na hofu ya Mungu na tumaini lake lilikuwa ni kuingia katika Ufalme wa Mbinguni kutokana na maneno yake aliyosema “Bwana unikumbuke utakapofika katika Ufalme wako” (Luka 23:42).
Alisema “lakini huyu mtu hakutenda lolote baya” (Luka 23:41). Alijua vipi juu ya matendo ya Yesu? Aliamini kwamba Yesu alitungwa katika mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu alizaliwa na Bikira Mariam,alibatizwa na Yohana Mbatizaji mwakilishi wa wanadamu wote. Alibeba dhambi za ulimwengu na kusulubiwa. Alikuwa ni Myahudi aliyeamini kile Yesu alichofanya kwa watu wote, pamoja na yeye ingawa alikuwa akisulibiwa kwa sababu ya kupokea ujira wa matendo hapa duniani.
Wale wote wenye kutubu dhambi zao kwa kupitia ubatizo wa Yohana huitambua haki ya Mungu pale wanaposikia kwamba dhambi zao zote zilikwisha bebwa na Yesu kwa ubatizo wake.Ili haki kwa wale wasio upokea ubatizo huo wa toba kukataa mapenzi ya Mingu kwa sababu hawakuamini ubatizo wa Yesu (Luka 7:28-30).
Kinyume chake yule mwovu aliyeokoka alikiri kila kitu Yesu alichofanya kilikuwa ni sahihi hali kwa yule Myahudi mwingine hakufanya hivyo. Yawezakana akawa ni mojawapo ya wayahudi ambao waliosikia habari hizo zote ambazo zilikwisha timia kati yao (Luka 1:1). Angeweza hata kusema kwamba Yesu alikuwa ni mwenye haki na Masia aliyetabiriwa kuja kwa sababu mwishowe alikuja kuamini pale msalabani kwamba Yesu alizibeba dhambi zake zote kwa kupitia ubatzi wake. Kwa hilo aliweza kuokolewa. Alikuwa pia ameokolewa kwa kuamini Injili ya ubatizo wa maji Roho kwa sababu Mungu ni haki hutoa haki kwa wale waaminio ubatizo wa Yesu na msalaba wake kutokana na sheria yake ya Roho wa Uzima.