Search

Поширені запитання щодо Християнської Віри

Запитання 2: Святий Дух

2-7. Je wafuasi wa Yesu walimpokea Roho tofauti katika vipindi pasipo kuhusika na msamaha wa dhambi?

Swala la kumpokea Roho Mtakatifu si tukio lenye kupishana kwa muda na ukombozi. Twaweza kuona katika Biblia kwamba wafuasi wa Yesu walikuwa tayari wamekwisha mwamini Yesu kwamba alikwisha beba dhambi zote za ulimwengu kwa njia ya ubatizo wa Yohana hata kabla ya kumpokea Roho Mtakatifu (1 Petro 3:21 Mfano wa mambo haya ni ubatizo unaowaokoa ninyi pia siku hizi).
Msamaha wa dhambi maana yake ni wokovu wa dhambi. Kwa maneno mengine ni kutakaswa dhambi zetu zote mioyoni. Siku hizi wakristo wengi wamechanganyikiwa juu ya maana ya msamaha wa dhami ambao Yesu alitupatia. Watu hawafahamu vile namna ya kupata msamaha wa dhambi. Hudhani ya kwamba tayari wamekwisha pokea ukombozi kwa dhambi zao. Kwa wale walio kwisha pokea msamaha wa dhambi zao wanashuhuda ndani yao. Hata hivyo ikiwa mtu hana ushuhuda wa neno la ukombozi ndani yake basi hakika bado hajampokea Roho Mtakatifu na pia hata msamaha wa dhambi zake zote.
Ikiwa anahisia za kimwili katika kujazwa Roho, hii ni matokeo ya kupotoshwa na hisia zako tu. Shetani hujigeuza na kuwa kama malaika wa nuru (2 Wakorintho 11:14-15, Wagalatia 1:7-9) akimlaghai mtu huyo na kumpotosha toka katika ukweli (Mathayo 7:21-23).
Wale walio kwisha samehewa dhambi zao wanaushuhuda ndani yao kwa sababu wanaamini Injili ya maji na Roho. Katika 1 Yohana 5:4-12 Mungu anamshuhudia Yesu Kristo aliyekuja kwa maji na damu. Zaidi ya yote anasema ikiwa mtu atakubali juu ya Roho fofauti au Injili tofauti (2 Wakorinto 11:4) basi mtu huyo haja pata msamaha wa dhambi au hata Roho Mtakatifu. Watu wataweza kupokea msamaha wa dhambi ikiwa tu watamwamini Yesu Kristo aliyekuja kwa Injili ya maji na Roho Mtakatifu. Ni muhimu katika kupata msamaha wa dhambi. Msamaha wa dhambi ni muhimu kwa ajili ya uwepo wa Roho Mtakatifu.