2-4. Bila shaka Roho Mtakatifu hunena na sisi kila siku. Hata wakati wa kanisa la mwanzo, mitume wa Yesu waliweza kufanya miujiza mingi. Bila shaka pia Roho Mtakatifu aliyetenda kazi nyakati hizo bado ndiye yeye atendaye hata sasa kwa njia ile ile. Kwa hiyo basi watu wengi wa Mungu hufanya miujiza katika jina la Yesu kwa mfano kukemea pepo au kuponya magaonjwa na mambo mengine yote katika kuwarejesha watu kwa Yesu. Natumaini kazi hizi kufanywa kwa kupitia Roho Mtakatifu, ikiwa ndivyo ilivyo, nini basi tofauti kati ya Roho Mtakatifu ambaye kwa uweza mkuu alitenda miujiza katika nyakati za kanisa la mwanzo na huyu atendaye miujiza kwa sasa? Je, Mungu si yule yule jana leo na hata sikuzote?
Ama kwa hakika hakuna tofauti kati ya yule atendaye miujiza nyakati za kanisa la mwanzo na huyu atendaye kazi leo hii. Tofauti pekee iliyopo ni ikiwa watu watendao miujiza katika nyakati hizi endapo wameamini injili ya maji na Roho ama la. Sababu ya hili ni kwamba ingawa Roho wa Mungu nyakati zote ni yule yule pasipo kujali muda au vipindi, tofauti huja endapo mtu anao ufahamu halisi wa Injia halali ya kumpokea Roho Mtakatifu. Watu wengi nyakati hizi hutenda miujiza pasipo kuwa na ufahamu wa kibiblia ulio hakika katika kumpokea Roho Mtakatifu. Biblia inatuonyesha katika Matendo 2:38, Yohana 5:2-8 na 1Petro 3:21 kwamba njia pekee ya kumpokea Roho Mtakatifu ni kuamini injili ya maji na Roho. “Mfano wa mambo haya ni ubatizo unao waokoa ninyi pia siku hizi.” Bila shaka Roho Mtakatifu alitenda mambo kama vile kuponya magonjwa na kukemea pepo pale Roho Mtakatifu alipo weka makazi ndani ya mitume katika nyakati hizo za kanisa la mwanzo. Hata hivyo hawakutoza fedha au kutoa sauti kali wakati walipokuwa wakitumia vipawa vya kiroho kama tuonavyo shuhudia nyakati hizi baadhi ya watu wafanyavyo. Mitume walidhihirisha uweza uliomo ndani yao kuwa ni mojawapo tu ya njia ya kufikisha ujumbe wa injili. Zaidi ya yote kuponya magonjwa na kukemea pepo hazikuwa kazi pekee za Roho Mtakatifu katika nyakati hizo za kanisa la mwanzo. Hii ilikuwa ni sehemu ndogo kati ya ile kazi kuu. Kwa jinsi hiyo basi ni hatari sana kudhani kwamba miujiza na maajabu yote kama vile kuponya magonjwa kukemea pepo na kunena kwa lugha katika ukristo wanyakati hizi ni hakika ya kazi za Roho Mtakatifu. Yatupasa kuamini ya kwamba aina zote za matukio yasiyo ya kawaida tunayo ya shuhudia kwa macho yetu katika ukristo wa nyakati hizi hayatokani na nguvu za Roho Mtakatifu. Bali yatupasa tuweze kung’amua watumishi wa kweli wa Mungu walio na uwepo wa Roho Mtakatifu, dhidi ya wale wasio naye ambao ama kwa hakika wamejawa na mapepo ndani yao. Hata ikiwa mtu ataweza kukemea pepo, kuponya magonjwa na hata kunena kwa lugha ikiwa bado anadhambi moyoni na huku haiamini injili ya maji na Roho, hakika huyo amejawa na pepo wachafu. Yesu pia alisema katika Mathayo 7:20-23 “Ndipo kwa matunda yao mtawatambua si kila mtu aniambiaye Bwana Bwana, atakaye ingia katika Ufalme wa Mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako na kwa jina lako kutoa pepo na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia, Amini sikuwajua ninyi kamwe endokeni kwangu ninyi mtendao maovu.” Tusifikiri ya kwamba kutenda miujiza pekee kwa mtu ndiko kunaonyesha kwamba anafanya kwa kupitia kazi za Roho Mtakatifu. Badala yake imetupasa kuchunguza kwa kina endapo mtu huyo anaihubiri injili ya maji na Roho au ikiwa yeye ni mwenye haki kwa kupokea msamaha wa dhambi zake zote. Roho Mtakatifu kamwe hatoweza kuweka makazi ndani ya mtu aliye na dhambi moyoni. Roho Mtakatifu hachangamani na dhambi. Msamaha wa dhambi katika nyakati za mwanzo ndiyo ulikuwa ukithibitishwa kwa kushuka kwa Roho Mtakatifu. Na ndiyo ilikuwa ni zawadi au kipawa cha Mungu kwa wale wote walio pata ondoleo la dhambi zao zote. Ingawa watu wengi bado wanadhani ya kwamba kuponya magonjwa kunena kwa lugha na kukemea pepo kwa jina la Yesu bila shaka ni kazi za Roho Mtakatifu. Hili ni kosa na ni imani ya hatari. Yatupasa tuweze kueleza endapo watu hawa wana tenda miujiza ya kweli hata ikiwa mtu anauwezo wa kutenda miujiza mingi kwa jina la Yesu. Lakini ikiwa hajui au hata kuamini injili ya kweli ya maji na Roho, ndipo basi ataweza kuwa mwalimu mwongo. Watu aina hii huangamiza nafsi za watu wengi na kudai fedha ili kutosheleza tamaa zao za kidunia. Hivyo kazi za mtu aliye na dhambi moyoni si kazi kweli za Roho Mtakatifu bali ni za pepo wa uovu. Roho Mtakatifu aliye tenda kazi nyakati za kanisa la mwanzo na huyu atendaye sasa ni mmoja. Hata hivyo ipo tofauti ya wazi kati ya kazi za Roho Mtakatifu zinazoonekana kwa walio mpokea Roho Mtakatifu na zapepo waovu wanao onekana kwa kupitia manabii wa uongo.